Thawabu Ya Kumtii Bwana
(Wimbo Wa Kwenda Juu)
1 Heri ni wale wote wamchaoBwana,
waendao katika njia zake.
2 Utakula matunda ya kazi yako;
baraka na mafanikio vitakuwa vyako.
3 Mke wako atakuwa kama mzabibu uzaao
katika nyumba yako;
wana wako watakuwa kama machipukizi ya mizeituni
kuizunguka meza yako.
4 Hivyo ndivyo atakavyobarikiwa
mtu amchayeBwana.
5 Bwanana akubariki kutoka Sayuni
siku zote za maisha yako,
na uone mafanikio ya Yerusalemu,
6 nawe ujaliwe kuishi
uone watoto wa watoto wako.
Amani iwe juu ya Israeli.
—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/128-42322bf991cd46273a32779b87cfd157.mp3?version_id=1627—