Kurejeshwa Kutoka Utumwani
(Wimbo Wa Kwenda Juu)
1 Bwanaalipowarejeza mateka Sayuni,
tulikuwa kama watu walioota ndoto.
2 Vinywa vyetu vilijaa kicheko,
ndimi zetu zilijaa nyimbo za shangwe.
Ndipo iliposemwa miongoni mwa mataifa,
“Bwanaamewatendea mambo makuu.”
3 Bwanaametutendea mambo makuu,
nasi tumejaa furaha.
4 EeBwana, turejeshee watu wetu waliotekwa,
kama vijito katika Negebu.
5 Wapandao kwa machozi
watavuna kwa nyimbo za shangwe.
6 Yeye azichukuaye mbegu zake
kwenda kupanda,
huku akilia,
atarudi kwa nyimbo za shangwe,
akiwa ameyachukua
matita ya mavuno yake.
—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/126-911e1a86f635da446023b7d1d66d0b5f.mp3?version_id=1627—