Mungu Mmoja Wa Kweli
1 Sio kwetu sisi, EeBwana, sio kwetu sisi
bali utukufu ni kwa jina lako,
kwa sababu ya upendo
na uaminifu wako.
2 Kwa nini mataifa waseme,
“Yuko wapi Mungu wao?”
3 Mungu wetu yuko mbinguni,
naye hufanya lo lote limpendezalo.
4 Lakini sanamu zao ni za fedha na dhahabu,
zilizotengenezwa kwa mikono ya wanadamu.
5 Zina vinywa, lakini haziwezi kusema,
zina macho, lakini haziwezi kuona;
6 zina masikio, lakini haziwezi kusikia,
zina pua, lakini haziwezi kunusa;
7 zina mikono, lakini haziwezi kupapasa,
zina miguu, lakini haziwezi kutembea;
wala koo zao haziwezi kutoa sauti.
8 Wale wanaozitengeneza watafanana nazo,
vivyo hivyo wale wote wanaozitumainia.
9 Ee nyumba ya Israeli, mtumaininiBwana,
yeye ni msaada na ngao yako.
10 Ee nyumba ya Aroni, mtumaininiBwana,
yeye ni msaada na ngao yako.
11 Ninyi mnaomcha, mtumaininiBwana,
yeye ni msaada na ngao yenu.
12 Bwanaanatukumbuka na atatubariki:
ataibariki nyumba ya Israeli,
ataibariki nyumba ya Aroni,
13 atawabariki wale wanaomchaBwana,
wadogo kwa wakubwa.
14 Bwanana awawezeshe kuongezeka,
ninyi na watoto wenu.
15 Mbarikiwe naBwana
Muumba wa mbingu na dunia.
16 Mbingu zilizo juu sana ni mali yaBwana,
lakini dunia amempa mwanadamu.
17 Sio wafu wanaomsifuBwana,
# wale washukao mahali pa kimya,
18 bali ni sisi tunaomtukuzaBwana,
sasa na hata milele.
# MsifuniBwana.
—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/115-0d3279443497f8791dd5f7b28dc7850f.mp3?version_id=1627—