Zaburi 112

Baraka za Mwenye Haki

1 MsifuniBwana.

Heri mtu yule amchayeBwana,

mtu yule apendezwaye sana na amri zake.

2 Watoto wake watakuwa wenye uwezo katika nchi,

kizazi cha watu waadilifu kitabarikiwa.

3 Nyumbani mwake kuna mali na utajiri,

haki yake hudumu milele.

4 Hata gizani nuru humzukia mtu mwadilifu,

yule mwenye rehema, huruma na haki.

5 Mema yatamjia mtu yule aliye mkarimu na mwenye kukopesha bila riba,

anayefanya mambo yake kwa haki.

6 Hakika hatatikisika kamwe,

mtu mwenye haki atakumbukwa milele.

7 Hataogopa habari mbaya,

moyo wake ni thabiti, ukimtegemeaBwana.

8 Moyo wake ni salama, hatakuwa na hofu,

mwishoni ataona ushindi dhidi ya adui zake.

9 Ametawanya vipawa vyake kwa ukarimu akawapa maskini,

haki yake yadumu milele,

pembea yake itatukuzwa kwa heshima.

10 Mtu mwovu ataona na kuchukizwa,

atasaga meno yake na kutoweka,

kutamani kwa mtu mwovu kutaishia patupu.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/112-9a9d1bf374d655d84427efbeb9eed1f0.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

5 − two =