Zaburi 104

Katika Kumsifu Muumba

1 Ee nafsi yangu, umhimidiBwana.

EeBwanaMungu wangu, wewe ni mkuu sana,

umejivika utukufu na enzi.

2 Amejifunika katika nuru kama vile kwa vazi,

amezitandaza mbingu kama hema

3 na kuziweka nguzo za orofa yake

juu ya maji.

Huyafanya mawingu kuwa gari lake kubwa zuri,

na hupanda kwenye mbawa za upepo.

4 Hufanya pepo kuwa wajumbewake,

miali ya moto watumishi wake.

5 Ameiweka dunia kwenye misingi yake,

hawezi kamwe kuondoshwa.

6 Uliifunika kwa kilindi kama kwa vazi,

maji yalisimama juu ya milima.

7 Lakini kwa kukemea kwako maji yalikimbia,

kwa sauti ya radi yako yalikimbia,

8 yakapanda milima, yakatelemka mabondeni,

mpaka mahali pale ulipoyakusudia.

9 Uliyawekea mpaka ambao hayawezi kuuvuka,

kamwe hayataifunika dunia tena.

10 Hufanya chemchemi zimwage maji mabondeni,

hutiririka kati ya milima.

11 Huwapa maji wanyama wote wa kondeni,

punda mwitu huzima kiu yao.

12 Ndege wa angani hufanya viota kando ya maji,

huimba katikati ya matawi.

13 Huinyeshea milima kutoka orofa zake,

dunia inatoshelezwa kwa matunda ya kazi yake.

14 Huyafanya majani ya mifugo yaote,

na mimea kwa ajili ya watu kupanda,

wajipatie chakula kutoka ardhini:

15 divai ya kuufurahisha moyo wa mwanadamu,

mafuta kwa ajili ya kung’arisha uso wake

na mkate wa kutia mwili nguvu.

16 Miti yaBwanainanyeshewa vizuri,

mierezi ya Lebanoni aliyoipanda.

17 Humo ndege hufanya viota vyao,

korongo ana nyumba yake

kwenye msunobari.

18 Milima mirefu ni makao ya mbuzi-mwitu,

majabali ni kimbilio la pelele.

19 Mwezi hugawanya majira,

na jua hutambua wakati wake wa kutua.

20 Unaleta giza, kunakuwa usiku,

wanyama wote wa mwituni

huzungukazunguka.

21 Simba hunguruma kwa mawindo yao,

na kutafuta chakula chao kutoka kwa Mungu.

22 Jua huchomoza, nao huondoka kwa kunyata,

hurudi na kulala katika mapango yao.

23 Kisha mwanadamu hutoka nje

na kwenda kazini kwake,

katika kazi yake mpaka jioni.

24 EeBwana, jinsi gani zilivyo nyingi kazi zako!

Kwa hekima ulizifanya zote,

dunia imejaa viumbe vyako.

25 Pale iko bahari, kubwa na yenye nafasi tele,

imejaa viumbe visivyo na idadi,

vitu vyenye uhai vikubwa na vidogo.

26 Huko meli huenda na kurudi,

# pia Lewiathani, uliyemwumba

acheze ndani yake.

27 Hawa wote wanakutazama wewe,

uwape chakula chao kwa wakati wake.

28 Wakati unapowapa,

wanakikusanya,

unapofumbua mkono wako,

wao wanashibishwa mema.

29 Unapoficha uso wako,

wanapata hofu,

unapoondoa pumzi yao,

wanakufa na kurudi mavumbini.

30 Unapopeleka Roho wako,

wanaumbwa,

nawe huufanya upya uso wa dunia.

31 Utukufu waBwanana udumu milele,

Bwanana azifurahie kazi zake,

32 yeye aitazamaye dunia, nayo ikatetemeka,

aigusaye milima nayo ikatoa moshi.

33 NitamwimbiaBwanamaisha yangu yote;

nitaimba sifa kwa Mungu wangu

muda wote ninaoishi.

34 Kutafakari kwangu na kumpendeze yeye,

ninapofurahi katikaBwana.

35 Lakini wenye dhambi na watoweke katika dunia

na waovu wasiwepo tena.

# Ee nafsi yangu, MsifuBwana.

MhimidiniBwana.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/104-e585def5ed27db73babc7cf5c5653b5a.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

sixteen + sixteen =