Zaburi 91

Mungu Mlinzi Wetu

1 Yeye akaaye mahali pa salama pake Yeye Aliye Juu Sana,

# atadumu katika uvuli wake Mwenyezi.

2 Nitasema kuhusuBwana, “Yeye ndiye

kimbilio langu na ngome yangu,

Mungu wangu, ambaye ninamtumaini.”

3 Hakika yeye ataniokoa na mtego wa mwindaji

na maradhi ya kuambukiza ya kuua.

4 Atakufunika kwa manyoya yake,

chini ya mbawa zake utapata kimbilio,

uaminifu wake utakuwa ngao na kinga yako.

5 Hutaogopa vitisho vya usiku,

wala mshale urukao mchana,

6 wala maradhi ya kuambukiza

yanayonyemelea gizani,

wala tauni iharibuyo adhuhuri.

7 Ijapo watu elfu wataangukia kando yako,

kumi elfu mkono wako wa kuume,

lakini haitakukaribia wewe.

8 Utatazama tu kwa macho yako

na kuona adhabu ya waovu.

9 Kama ukimfanya Aliye Juu Sana kuwa makao yako:

naam,Bwanaambaye ni kimbilio langu;

10 basi hakuna madhara yatakayokupata wewe,

wala maafa hayataikaribia hema yako.

11 Kwa kuwa atawaagiza malaika zake kwa ajili yako,

wakulinde katika njia zako zote.

12 Mikononi mwao watakuinua,

ili usijikwae mguu wako kwenye jiwe.

13 Utawakanyaga simba na nyoka wakali,

simba mkubwa na nyoka utawaponda kwa miguu.

14 Bwanaasema, “Kwa kuwa ananipenda

nitamwokoa;

nitamlinda kwa kuwa amelikubali Jina langu.

15 Ataniita, nami nitamjibu;

nitakuwa pamoja naye katika taabu,

nitamwokoa na kumheshimu.

16 Kwa siku nyingi nitamshibisha

na kumwonyesha wokovu wangu.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/91-1e8eb4d06957f2222bb9adcc5be6fad7.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

19 − 9 =