Zaburi 89

Wimbo Wakati Wa Taabu Ya Kitaifa

(Utenzi Wa Ethani Wa Jamii Ya Ezra)

1 Nitaimba juu ya upendo mkuu waBwanamilele;

kwa kinywa changu nitajulisha uaminifu wako

ujulikane kwa vizazi vyote.

2 Nitatangaza kuwa upendo wako unasimama imara milele

na uaminifu wako umeuthibitisha mbinguni.

3 Ulisema, “Nimefanya Agano na mteule wangu,

nimemwapia mtumishi wangu Daudi,

4 ‘Nitaimarisha uzao wako milele

na kudumisha ufalme wako kwa vizazi vyote.’ ”

5 EeBwana, mbingu zinayasifu maajabu yako,

uaminifu wako pia, katika kusanyiko la watakatifu.

6 Kwa kuwa ni nani katika mbingu juu

anayeweza kulinganishwa naBwana?

Ni nani miongoni mwa viumbe vya mbinguni

aliye kamaBwana?

7 Katika kusanyiko la watakatifu Mungu huogopwa sana,

anahofiwa kuliko wote wanaomzunguka.

8 EeBwanaMwenye Nguvu Zote,

ni nani aliye kama wewe?

EeBwana, wewe ni mwenye nguvu,

na uaminifu wako unakuzunguka.

9 Wewe unatawala bahari yenye msukosuko;

wakati mawimbi yake yanapoinuka, wewe unayatuliza.

10 Wewe ulimponda Rahabu

kama mmojawapo wa waliochinjwa;

kwa mkono wako wenye nguvu,

uliwatawanya adui zako.

11 Mbingu ni zako, nayo nchi pia ni yako,

uliuwekea ulimwengu msingi

pamoja na vyote vilivyomo.

12 Uliumba kaskazini na kusini;

Tabori na Hermoni

wanaliimbia jina lako kwa furaha.

13 Mkono wako umejaa uwezo;

mkono wako una nguvu,

mkono wako wa kuume umetukuzwa.

14 Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chako cha enzi;

upendo na uaminifu vinakutangulia.

15 Heri ni wale ambao wamejifunza kukusifu kwa shangwe,

wanaotembea katika mwanga

wa uwepo wako, EeBwana.

16 Wanashangilia katika jina lako mchana kutwa,

wanafurahi katika haki yako.

17 Kwa kuwa wewe ni utukufu na nguvu yao,

# kwa wema wako unatukuza pembeyetu.

18 Naam, ngao yetu ni mali yaBwana,

aliye Mtakatifu Pekee wa Israeli ni mfalme wetu.

19 Ulizungumza wakati fulani katika maono,

kwa watu wako waaminifu ukasema:

“Nimeweka nguvu kwa shujaa,

nimemwinua kijana miongoni mwa watu.

20 Nimempata Daudi mtumishi wangu,

nimemtia mafuta yangu matakatifu.

21 Kitanga changu kitamtegemeza,

hakika mkono wangu utamtia nguvu.

22 Hakuna adui atakayemtoza ushuru,

hakuna mtu mwovu atakayemwonea.

23 Nitawaponda adui zake mbele zake

na kuwaangamiza watesi wake.

24 Upendo wangu mkamilifu utakuwa pamoja naye,

kwa Jina langu pembe yake itatukuzwa.

25 Nitauweka mkono wake juu ya bahari,

mkono wake wa kuume juu ya mito.

26 Naye ataniita kwa sauti, ‘Wewe ni Baba yangu,

Mungu wangu, Mwamba na Mwokozi wangu.’

27 Nitamteua pia awe mzaliwa wangu wa kwanza,

aliyetukuka kuliko wafalme wote wa dunia.

28 Nitadumisha upendo wangu kwake milele,

na Agano langu naye litakuwa imara.

29 Nitaudumisha uzao wake milele,

kiti chake cha enzi kama mbingu zinavyodumu.

30 “Kama wanae wataacha amri yangu

na wasifuate sheria zangu,

31 kama wakihalifu maagizo yangu

na kutoshika amri zangu,

32 nitaadhibu dhambi yao kwa fimbo,

uovu wao kwa kuwapiga,

33 lakini sitauondoa upendo wangu kwake,

wala sitausaliti uaminifu wangu kamwe.

34 Mimi sitavunja Agano langu

wala sitabadili

lile ambalo midomo yangu imelitamka.

35 Mara moja na kwa milele,

nimeapa kwa utakatifu wangu,

nami sitamdanganya Daudi:

36 kwamba uzao wake utaendelea milele

na kiti chake cha enzi

kitadumu mbele zangu kama jua;

37 kitaimarishwa milele kama mwezi,

shahidi mwaminifu angani.”

38 Lakini wewe umemkataa, umemdharau,

umemkasirikia sana mpakwa mafuta wako.

39 Umelikana Agano lako na mtumishi wako

na umeinajisi taji yake mavumbini.

40 Umebomoa kuta zake zote

na ngome zake zote umezifanya kuwa magofu.

41 Wote wapitao karibu wamemnyang’anya mali zake;

amekuwa dharau kwa jirani zake.

42 Umeutukuza mkono wa kuume wa adui zake,

umewafanya watesi wake wote washangilie.

43 Umegeuza makali ya upanga wake

na hukumpa msaada katika vita.

44 Umeikomesha fahari yake,

na kukiangusha kiti chake cha enzi.

45 Umezifupisha siku za ujana wake,

umemfunika kwa vazi la aibu.

46 Hata lini, EeBwana? Utajificha milele?

Ghadhabu yako itawaka kama moto hata lini?

47 Kumbuka jinsi maisha yangu yanavyopita haraka.

Ni ubatili kiasi gani umemuumba mwanadamu!

48 Ni mtu gani awezaye kuishi na asione kifo,

# au kujiokoa mwenyewe kutoka nguvu za kaburi?

49 EeBwana, uko wapi upendo wako mkuu wa mwanzoni,

ambao katika uaminifu wako ulimwapia Daudi?

50 Bwana kumbuka jinsi mtumishi wako amesimangwa,

jinsi ninavyovumilia moyoni mwangu

dhihaka za mataifa yote,

51 dhihaka ambazo kwazo adui zako

wamenisimanga, EeBwana,

ambazo kwazo wamesimanga

kila hatua ya mpakwa mafuta wako.

52 MsifuniBwanamilele!

Amen na Amen.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/89-837c39996f28e55d2ddacbac4029ab64.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

3 × four =