Kuomba Msaada
(Maombi Ya Daudi)
1 EeBwana, sikia na unijibu,
kwa maana mimi ni maskini na mhitaji.
2 Linda maisha yangu, kwa maana nimejiweka kwako,
wewe ni Mungu wangu,
mwokoe mtumishi wako anayekutumaini.
3 EeBwana, nihurumie mimi,
kwa maana ninakuita mchana kutwa.
4 Mpe mtumishi wako furaha,
kwa kuwa kwako wewe, EeBwana,
ninainua nafsi yangu.
5 EeBwana, wewe ni mwema na mwenye kusamehe,
umejaa upendo kwa wote wakuitao.
6 EeBwana, sikia maombi yangu,
sikiliza kilio changu unihurumie.
7 Katika siku ya shida yangu nitakuita,
kwa maana wewe utanijibu.
8 EeBwana, katikati ya miungu hakuna kama wewe,
hakuna matendo ya kulinganishwa na yako.
9 EeBwana, mataifa yote uliyoyafanya
yatakuja na kuabudu mbele zako;
wataliletea utukufu jina lako.
10 Kwa maana wewe ni mkuu
na unafanya mambo ya ajabu;
wewe peke yako ndiwe Mungu.
11 EeBwana, nifundishe njia yako,
nami nitakwenda katika kweli yako;
nipe moyo usiositasita,
ili niweze kulicha jina lako.
12 EeBwana, wangu, nitakusifu kwa moyo wote;
nitaliadhimisha jina lako milele.
13 Kwa maana upendo wako ni mkuu kwangu;
# umeniokoa kutoka kwenye vilindi vya kaburi.
14 Ee Mungu, wenye majivuno wananishambulia;
kundi la watu wakatili linatafuta uhai wangu:
watu wasiokuheshimu wewe.
15 Lakini wewe, EeBwana, ni Mungu wa huruma na neema,
si mwepesi wa hasira,
bali ni mwingi wa upendo na uaminifu.
16 Nigeukie na unihurumie;
mpe mtumishi wako nguvu zako,
# mwokoe mwana wa mtumishi wako wa kike.
17 Nipe ishara ya wema wako,
ili adui zangu waione nao waaibishwe,
kwa kuwa wewe, EeBwana,
umenisaidia na kunifariji.
—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/86-374bffae46feebf1d5ca5d4a064fa2db.mp3?version_id=1627—