Zaburi 80

Maombi Kwa Ajili Ya Kuponywa Kwa Taifa

(Kwa Mwimbishaji: Mtindo Wa Yungiyungi. Zaburi Ya Asafu)

1 Ee Mchungaji wa Israeli tusikie,

wewe umwongozaye Yosefu kama kundi;

wewe uketiye katika kiti cha enzi

katikati ya makerubi, angaza

2 mbele ya Efraimu, Benyamini na Manase.

Uamshe nguvu zako,

uje utuokoe.

3 Ee Mungu, uturejeshe,

utuangazie uso wako,

ili tuweze kuokolewa.

4 EeBwanaMungu Mwenye Nguvu Zote,

hata lini hasira yako itawaka na kufoka moshi

dhidi ya maombi ya watu wako?

5 Umewalisha kwa mkate wa machozi,

umewafanya wanywe machozi bakuli tele.

6 Tumekuwa chanzo cha ugomvi kwa jirani zetu,

na adui zetu wanatudhihaki.

7 Ee Mungu Mwenye Nguvu Zote, uturejeshe;

utuangazie uso wako,

nasi tuweze kuokolewa.

8 Ulileta mzabibu kutoka Misri,

ukawafukuza mataifa ukaupanda.

9 Uliandaa shamba kwa ajili yake,

mizizi ikawa imara, ukajaza nchi.

10 Milima ilifunikwa kwa kivuli chake,

matawi yake yakafunika mierezi mikubwa.

11 Matawi yake yalienea mpaka Baharini,

# machipukizi yake mpaka kwenye Mto.

12 Mbona umebomoa kuta zake

ili kwamba wote wapitao karibu

wazichume zabibu zake?

13 Nguruwe mwitu wanauharibu

na wanyama wa kondeni hujilisha humo.

14 Turudie, Ee Mungu Mwenye Nguvu Zote!

Tazama chini kutoka mbinguni na uone!

Linda mzabibu huu,

15 mche ulioupanda

kwa mkono wako wa kuume,

mwana uliyemlea

kwa ajili yako mwenyewe.

16 Mzabibu wako umekatwa, umechomwa moto,

kwa kuwakemea watu wako huangamia.

17 Mkono wako na utulie juu ya mtu aliyeko mkono wako wa kuume,

mwana wa mtu uliyemlea

kwa ajili yako mwenyewe.

18 Ndipo hatutakuacha tena,

utuhuishe nasi tutaliitia jina lako.

19 EeBwanaMungu Mwenye Nguvu Zote, uturejeshe;

utuangazie uso wako,

ili tuweze kuokolewa.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/80-e66411dc1eba208e8eb0c3030a5e0c2d.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

seven + 5 =