Zaburi 74

Maombi Kwa Ajili Ya Taifa Kuokolewa

(Utenzi Wa Asafu)

1 Ee Mungu, mbona umetukataa milele?

Mbona hasira yako inawaka na kutoka moshi

juu ya kondoo wa malisho yako?

2 Kumbuka watu uliowanunua zamani,

kabila la urithi wako, ambao uliwakomboa:

Mlima Sayuni, ambamo uliishi.

3 Geuza hatua zako kuelekea magofu haya ya kudumu,

uharibifu wote huu ambao adui ameuleta

katika mahali patakatifu.

4 Adui zako wamenguruma pale ulipokutana nasi,

wanaweka bendera zao kama alama.

5 Walifanya kama watu wanaotumia mashoka

kukata kichaka chote cha miti.

6 Walivunjavunja milango yote iliyonakishiwa

kwa mashoka na vishoka vyao.

7 Waliteketeza kabisa mahali patakatifu,

wakayanajisi makao ya Jina lako.

8 Walisema mioyoni mwao,

“Tutawaponda kabisa!”

Walichoma kila mahali ambapo Mungu

aliabudiwa katika nchi.

9 Hatukupewa ishara za miujiza;

hakuna manabii waliobaki,

hakuna ye yote kati yetu ajuaye

kwamba hali hii itachukua muda gani.

10 Ee Mungu, mtesi atakudhihaki mpaka lini?

Je, adui watalitukana jina lako milele?

11 Kwa nini unazuia mkono wako,

mkono wako wa kuume?

Uutoe kutoka katika makunjo ya vazi lako

na uwaangamize!

12 Lakini wewe, Ee Mungu,

ni mfalme wangu tangu zamani,

unaleta wokovu duniani.

13 Ni wewe uliyeigawanya bahari kwa uweza wako;

ulivunja vichwa vya wanyama wakubwa wa kutisha katika maji.

14 Ni wewe uliyeponda vichwa vya Lewiathani

nawe ukamtoa kama chakula

cha viumbe vya jangwani.

15 Ni wewe uliyefungua chemchemi na vijito,

ulikausha mito ambayo ilikuwa ikitiririka daima.

16 Mchana ni wako, nao usiku ni wako pia,

uliweka jua na mwezi.

17 Ni wewe uliyeiweka mipaka yote ya dunia,

ulifanya kiangazi na masika.

18 EeBwana, kumbuka jinsi mtesi alivyokudhihaki,

jinsi watu wapumbavu walivyolitukana jina lako.

19 Usiukabidhi uhai wa njiwa wako

kwa wanyama wakali wa mwitu;

usisahau kabisa uhai wa watu wako

wanaoteseka milele.

20 Likumbuke agano lako,

maana mara kwa mara mambo ya jeuri

yamejaa katika sehemu za giza katika nchi.

21 Usiruhusu walioonewa warudi nyuma kwa aibu;

maskini na wahitaji na walisifu jina lako.

22 Inuka, Ee Mungu, ujitetee;

kumbuka jinsi wapumbavu

wanavyokudhihaki mchana kutwa.

23 Usipuuze makelele ya watesi wako,

ghasia za adui zako,

zinazoinuka mfululizo.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/74-ecd31c4f04e9b5de7d636b79495e0199.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

14 + two =