Zaburi 72

Maombi Kwa Ajili Ya Mfalme

(Zaburi Ya Solomoni)

1 Ee Mungu, mjalie mfalme aamue kwa haki yako,

mwana wa kifalme kwa haki yako.

2 Atawaamua watu wako kwa haki,

watu wako walioonewa kwa haki.

3 Milima italeta mafanikio kwa watu,

vilima tunda la haki.

4 Atawatetea walioonewa miongoni mwa watu

na atawaokoa watoto wa wahitaji,

ataponda mdhalimu.

5 Atadumu kama jua, kama mwezi,

vizazi vyote.

6 Atakuwa kama mvua inyeshayo

juu ya shamba lililofyekwa,

kama manyunyu yanyeshayo ardhi.

7 Katika siku zake wenye haki watastawi;

mafanikio yatakuwepo

mpaka mwezi utakapokoma.

8 Atatawala kutoka bahari hadi bahari

# na kutoka Mtompaka miisho ya dunia.

9 Makabila ya jangwani watamsujudia,

na adui zake wataramba mavumbi.

10 Wafalme wa Tarshishi na wa pwani za mbali

watamletea kodi;

wafalme wa Sheba na Seba

watampa zawadi.

11 Wafalme wote watamsujudia

na mataifa yote yatamtumikia.

12 Kwa maana atamwokoa mhitaji anayemlilia,

aliyeonewa asiye na wa kumsaidia.

13 Atawahurumia wanyonge na wahitaji

na kuwaokoa wahitaji kutoka mauti.

14 Atawaokoa kutoka uonevu na ukatili,

kwani damu yao ni ya thamani machoni pake.

15 Aishi maisha marefu!

Dhahabu ya Sheba na apewe.

Watu na wamwombee daima

na kumbariki mchana kutwa.

16 Nafaka ijae tele katika nchi yote,

juu ya vilele vya vilima na istawi.

Tunda lake na listawi kama Lebanoni,

listawi kama majani ya kondeni.

17 Jina lake na lidumu milele,

na lidumu kama jua.

Mataifa yote yatabarikiwa kupitia yeye,

nao watamwita mbarikiwa.

18 BwanaMungu, Mungu wa Israeli, apewe sifa,

yeye ambaye peke yake hutenda mambo ya ajabu.

19 Jina lake tukufu lisifiwe milele,

ulimwengu wote ujae utukufu wake.

Amen na Amen.

20 Huu ndio mwisho wa maombi ya Daudi mwana wa Yese.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/72-abe08fca07014b184f67512ba27e742f.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

two × two =