Kuomba Msaada
(Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Daudi. Maombolezo)
1 Ee Mungu, ufanye haraka kuniokoa,
EeBwana, njoo hima unisaidie.
2 Waaibike na kufedheheshwa
wale wanaotafuta uhai wangu;
wale wanaotamani kuangamizwa kwangu
warudishwe nyuma kwa aibu.
3 Wale waniambiao, “Aha! Aha!”
warudi nyuma kwa sababu ya aibu yao.
4 Lakini wote wakutafutao
na washangilie na kukufurahia,
wale wapendao wokovu wako daima na waseme,
“Mungu na atukuzwe!”
5 Hata sasa mimi ni maskini na mhitaji;
Ee Mungu, unijie haraka.
Wewe ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu;
EeBwana, usikawie.
—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/70-098f2b592afdfeb0c290fdafa03c8c88.mp3?version_id=1627—