Zaburi 48

Sayuni, Mji Wa Mungu

(Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Wana Wa Kora)

1 Bwanani mkuu na anayestahili kusifiwa sana,

katika mji wa Mungu wetu,

mlima wake mtakatifu.

2 Ni mzuri katika kuinuka kwake juu sana,

furaha ya dunia yote.

# Kama vilele vya juu sana vya Safonini Mlima Sayuni,

mji wa Mfalme Mkuu.

3 Mungu yuko katika ngome zake;

amejionyesha mwenyewe kuwa ngome yake.

4 Wakati wafalme walipounganisha nguvu,

waliposonga mbele pamoja,

5 Danwalimwona nao wakashangaa,

wakakimbia kwa hofu.

6 Kutetemeka kuliwashika huko,

maumivu kama ya mwanamke

mwenye utungu wa kuzaa.

7 Uliwaangamiza kama meli za Tarshishi

zilizovunjwa na upepo wa mashariki.

8 Kama tulivyokuwa tumesikia,

ndivyo tulivyoona

katika mji waBwanaMwenye Nguvu Zote,

katika mji wa Mungu wetu:

Mungu ataufanya uwe salama milele.

9 Ee Mungu, hekaluni mwako

tunatafakari upendo wako usiokoma.

10 Ee Mungu, kama jina lako lilivyo,

sifa zako zinafika hadi miisho ya dunia,

Mkono wako wa kuume umejazwa na haki.

11 Mlima Sayuni unashangilia,

vijiji vya Yuda vinafurahi

kwa sababu ya hukumu zako.

12 Tembeeni katika Sayuni,

uzungukeni mji,

hesabuni minara yake.

13 Yatafakarini vyema maboma yake,

angalieni ngome zake,

ili mpate kusimulia habari zake

kwa kizazi kijacho.

14 Kwa kuwa huyu Mungu ni Mungu wetu

milele na milele;

atakuwa kiongozi wetu hata mwisho.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/48-e221b6e7706605fa6c85745014786c40.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

nineteen − four =