Zaburi 40

Wimbo Wa Sifa

(Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Daudi)

1 NilimngojaBwanakwa saburi,

naye akaniinamia akasikia kilio changu.

2 Akanipandisha kutoka shimo la uharibifu,

kutoka katika matope na utelezi;

akaiweka miguu yangu juu ya mwamba

na kunipa mahali imara pa kusimama.

3 Akaweka wimbo mpya kinywani mwangu,

wimbo wa sifa kwa Mungu wetu.

Wengi wataona na kuogopa

na kuweka tumaini lao kwaBwana.

4 Heri mtu yule amfanyayeBwanakuwa tumaini lake,

asiyewategemea wenye kiburi,

wale wenye kugeukia miungu ya uongo.

5 EeBwanaMungu wangu,

umefanya mambo mengi ya ajabu.

Mambo uliyopanga kwa ajili yetu

hakuna awezaye kukuhesabia;

kama ningesema na kuyaelezea,

yangekuwa mengi mno kuyaelezea.

6 Dhabihu na sadaka hukuvitaka,

# lakini umefungua masikio yangu,

sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi

hukuzihitaji.

7 Ndipo niliposema, “Mimi hapa, nimekuja:

imeandikwa kuhusu mimi katika gombo.

8 Ee Mungu wangu,

natamani kufanya mapenzi yako;

sheria yako iko ndani ya moyo wangu.”

9 Nimehubiri haki katika kusanyiko kubwa,

sikufunga mdomo wangu,

EeBwana, kama ujuavyo.

10 Sikuficha haki yako moyoni mwangu;

ninasema juu ya uaminifu wako na wokovu wako.

Sikuficha upendo wako na kweli yako

mbele ya kusanyiko kubwa.

11 EeBwana, usizuilie huruma zako,

upendo wako na kweli yako daima vinilinde.

12 Kwa maana taabu zisizo na hesabu zimenizunguka,

dhambi zangu zimenikamata, hata nisiweze kuona.

Zimekuwa nyingi kuliko nywele za kichwa changu,

nao moyo unazimia ndani yangu.

13 EeBwana, uwe radhi kuniokoa,

EeBwana, njoo hima unisaidie.

14 Wote wanaotafuta kuuondoa uhai wangu

na waaibishwe na kufadhaishwa;

wote wanaotamani kuangamizwa kwangu

na warudishwe nyuma kwa aibu.

15 Wale waniambiao, “Aha!”

wafadhaishwe na iwe aibu yao.

16 Bali wote wakutafutao

washangilie na kukufurahia,

wale wapendao wokovu wako siku zote waseme,

“Bwanaatukuzwe!”

17 Lakini bado mimi ni maskini na mhitaji;

Bwana na anifikirie.

Wewe ni msaada wangu na Mwokozi wangu;

Ee Mungu wangu, usikawie.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/40-6e5c826ea55f00171622d693cfba7ef5.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

four × 1 =