Zaburi 37

Mwisho Wa Mtu Mwovu

(Zaburi Ya Daudi)

1 Usisumbuke kwa ajili ya watendao maovu wala usiwaonee wivu watu watendao maovu,

2 kwa maana kama majani watanyauka mara,

kama mimea ya kijani watakufa mara.

3 MtumainiBwanana utende yaliyo mema,

ukae katika nchi ukafurahie malisho salama.

4 Jifurahishe katikaBwananaye atakupa

haja za moyo wako.

5 MkabidhiBwananjia yako,

mtumaini yeye naye atatenda hili:

6 yeye atafanya haki yako ing’ae

kama mapambazuko,

hukumu kama jua la adhuhuri.

7 Tulia mbele zaBwana

na umngojee kwa uvumilivu;

usisumbuke watu wanapofanikiwa katika njia zao,

wanapotekeleza mipango yao miovu.

8 Epuka hasira na uache ghadhabu,

usihangaike, itakuongoza tu kwenye ubaya.

9 Kwa maana waovu watakatiliwa mbali,

bali wale wanaomtumainiBwanawatairithi nchi.

10 Bado kitambo kidogo, waovu hawataonekana,

ingawa utawatafuta, hawataonekana.

11 Bali wanyenyekevu watairithi nchi

na watafurahia amani tele.

12 Waovu hula njama dhidi ya wenye haki

na kuwasagia meno,

13 bali Bwana huwacheka waovu,

kwa sababu anajua siku yao inakuja.

14 Waovu huchomoa upanga na kupinda upinde,

ili wawaangushe maskini na wahitaji,

kuwachinja wale ambao njia zao ni nyofu.

15 Lakini panga zao zitachoma mioyo yao wenyewe,

na pinde zao zitavunjwa.

16 Bora kidogo walichonacho wenye haki

kuliko wingi wa mali

walizo nazo waovu wengi;

17 kwa maana nguvu za waovu zitavunjwa,

lakiniBwanahumtegemeza mwenye haki.

18 Bwanaanazifahamu siku za wanyofu,

na urithi wao utadumu milele.

19 Siku za maafa hawatanyauka,

siku za njaa watafurahia kuwa na wingi wa vitu.

20 Lakini waovu wataangamia:

Adui zaBwanawatatoweka

kama uzuri wa mashamba,

watatoweka,

watatoweka kama moshi.

21 Waovu hukopa na hawalipi,

bali wenye haki hutoa kwa ukarimu,

22 wale wanaobarikiwa naBwanawatairithi nchi,

bali wale anaowalaani watakatiliwa mbali.

23 KamaBwanaakipendezwa na njia ya mtu,

huimarisha hatua zake,

24 ajapojikwaa, hataanguka,

kwa maanaBwana

humtegemeza kwa mkono wake.

25 Nilikuwa kijana na sasa ni mzee,

lakini sijaona kamwe wenye haki wameachwa

au watoto wao wakiomba omba chakula.

26 Wakati wote ni wakarimu hukopesha bila masharti,

watoto wao watabarikiwa.

27 Acha ubaya na utende wema,

nawe utaishi katika nchi milele.

28 Kwa kuwaBwanahuwapenda

wenye haki naye hatawaacha waaminifu wake.

Watalindwa milele,

lakini uzao wa waovu utakatiliwa mbali;

29 wenye haki watairithi nchi,

na kuishi humo milele.

30 Kinywa cha mwenye haki hutamka hekima,

nao ulimi wake huzungumza lililo haki.

31 Sheria ya Mungu wake imo moyoni mwake;

nyayo zake hazitelezi.

32 Watu waovu huvizia wenye haki,

wakitafuta kuwaua;

33 lakiniBwanahatawaacha mikononi mwao

wala hatawaacha wahukumiwe

kuwa wakosa wanaposhtakiwa.

34 UmngojeeBwana,

na uishike njia yake.

Naye atakutukuza uirithi nchi,

waovu watakapokatiliwa mbali,

utaliona hilo.

35 Nimemwona mtu mwovu na mkatili akistawi

kama mwerezi wa Lebanoni,

36 lakini alitoweka mara na hakuonekana,

ingawa nilimtafuta,

hakupatikana.

37 Watafakari watu wasio na hatia,

wachunguze watu wakamilifu,

kuna mafanikio kwa mtu apendaye amani.

38 Lakini watenda dhambi wote wataangamizwa,

mafanikio yao yatakatiliwa mbali.

39 Wokovu wa wenye haki hutoka kwaBwana,

yeye ni ngome yao wakati wa shida.

40 Bwanahuwasaidia na kuwaokoa,

huwaokoa kutoka kwa waovu na kuwahifadhi,

kwa maana wanamkimbilia.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/37-e0d9208b6fe305ab72a7084c51613c73.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

twenty + 19 =