Zaburi 36

Uovu Wa Mwanadamu

(Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Daudi Mtumishi Wa Mungu)

1 Kuna neno moyoni mwangu

kuhusu hali ya dhambi ya mwovu.

Hakuna hofu ya Mungu

mbele ya macho yake.

2 Kwa kuwa machoni pake mwenyewe hujisifu mno

kiasi kwamba hawezi kugundua

au kuichukia dhambi yake.

3 Maneno ya kinywa chake ni maovu na ya udanganyifu,

ameacha kuwa mwenye hekima na kutenda mema.

4 Hata kitandani mwake hupanga hila mbaya,

hujitia katika njia ya dhambi

na hakatai lililo baya.

5 Upendo wako, EeBwana,

unafika hadi katika mbingu,

uaminifu wako hadi kwenye anga.

6 Haki yako ni kama milima mikubwa,

hukumu zako ni kama kilindi kirefu sana.

EeBwana, wewe huwahifadhi

mwanadamu na mnyama.

7 Upendo wako usiokoma

ni wa thamani mno!

Wale wa daraja ya juu na ya chini

miongoni mwa wanadamu

hupata kimbilio katika uvuli wa mbawa zako.

8 Watajifurahisha katika wingi wa vitu vya nyumbani mwako,

nawe utawanywesha

katika mto wa furaha zako.

9 Kuwa pamoja nawe ni kijito cha uzima,

katika nuru yako twaona nuru.

10 Dumisha upendo wako kwa wale wanaokujua wewe,

haki yako kwa wale walio wanyofu wa moyo.

11 Mguu wa mwenye kiburi na usije dhidi yangu,

wala mkono wa mwovu usinifukuze.

12 Angalia jinsi watenda mabaya walivyoanguka:

wametupwa chini, hawawezi kuinuka!

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/36-1a88171c243532a801b4f48713566e12.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

13 − 11 =