Kuomba Msaada: Kuokolewa Kutokana Na Maadui
(Zaburi Ya Daudi)
1 EeBwana, pingana na wale wanaopingana nami,
upigane na hao wanaopigana nami.
2 Uchukue ngao na kigao,
inuka unisaidie.
3 Inua mkuki wako na fumolako
dhidi ya hao wanaonifuatia.
Uiambie nafsi yangu,
“Mimi ni wokovu wako.”
4 Wafedheheshwe na waaibishwe
wale wanaotafuta uhai wangu,
wanaofanya shauri kuniangamiza
warudishwe nyuma kwa hofu.
5 Wawe kama makapi yapeperushwayo na upepo,
malaika waBwanaakiwafukuza;
6 njia yao na iwe giza na ya utelezi,
malaika waBwanaakiwafuatilia.
7 Kwa vile walinifichia wavu wao bila sababu,
na bila sababu wamenichimbia shimo,
8 maafa na yawapate ghafula:
wavu walionifichia na uwatege wenyewe,
na waanguke katika shimo hilo,
kwa maangamizo yao.
9 Ndipo nafsi yangu itashangilia katikaBwana
na kuufurahia wokovu wake.
10 Nitapaza sauti yangu nikisema,
“Ni nani aliye kama wewe, EeBwana?
Huwaokoa maskini kutokana na watu
walio na nguvu kuliko wao,
maskini na mhitaji kutokana
na wanaowanyang’anya!”
11 Mashahidi wakatili wanainuka,
wananiuliza kwa mambo nisiyoyajua.
12 Wananilipa baya kwa jema
na kuiacha nafsi yangu ukiwa.
13 Lakini walipokuwa wagonjwa,
nilivaa nguo ya gunia
na nikajinyenyekesha kwa kufunga.
Maombi yangu yaliponirudia bila kujibiwa,
14 niliendelea kuomboleza
kama vile wao ni rafiki au ndugu.
Niliinamisha kichwa chini kwa huzuni
kama vile ninayemwombolezea mama yangu.
15 Lakini nilipojikwaa,
walikusanyika kwa shangwe;
washambuliaji walijikusanya dhidi yangu
bila mimi kujua.
Walinisingizia pasipo kukoma.
16 Kama watu wasiomcha Mungu wamedhihaki,
wamenisagia meno.
17 EeBwana, utatazama mpaka lini?
Niokoe maisha yangu na maangamizi yao,
uhai wangu wa thamani
kutokana na simba hawa.
18 Nami nitakushukuru mbele ya kusanyiko kubwa,
nitakusifu katikati ya watu wengi.
19 Usiwaache wale wanaonisimanga,
wale ambao ni adui zangu bila sababu;
usiwaache wale ambao ni adui zangu bila sababu
wakonyeze jicho kwa hila.
20 Hawazungumzi kwa amani,
bali wanatunga mashtaka ya uongo
dhidi ya wale wanaoishi kwa utulivu katika nchi.
21 Hunifumbulia vinywa vyao wakisema,
“Aha! Aha! Kwa macho yetu wenyewe tumeliona.”
22 EeBwana, umeona hili, usiwe kimya.
Usiwe mbali nami, EeBwana.
23 Amka, inuka unitetee!
Unipiganie Mungu wangu na Bwana wangu.
24 Nihukumu kwa haki yako, EeBwanaMungu wangu,
sawasawa na haki yako;
usiwaache wakusimange.
25 Usiwaache wafikiri, “Aha, hili ndilo tulilotaka!”
Au waseme, “Tumemmeza.”
26 Wote wanaofurahia dhiki yangu
na waaibishwe na wachanganyikiwe;
hao wanaojiinua dhidi yangu
na wavikwe aibu na dharau.
27 Wale wanaofurahia hukumu yangu ya haki
na wapige kelele za shangwe na furaha;
hebu waseme siku zote,
“Bwanaatukuzwe,
ambaye amefurahia
mafanikio ya mtumishi wake.”
28 Ulimi wangu utanena haki yako
na sifa zako mchana kutwa.
—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/35-55cb7add9158b71d13574b9940749697.mp3?version_id=1627—