Zaburi 31

Maombi na Sifa Kwa Kuokolewa Kutoka Kwa Adui

(Zaburi Ya Daudi)

1 EeBwana, ninakukimbilia wewe,

usiache nikaaibika kamwe,

kwa haki yako uniokoe.

2 Nitegee sikio lako, uje uniokoe haraka,

uwe kwangu mwamba wa kimbilio,

ngome imara ya kuniokoa.

3 Kwa kuwa wewe ni mwamba wangu

na ngome yangu, uniongoze na kunilinda

kwa ajili ya jina lako.

4 Uniepushe na mtego niliotegewa,

maana wewe ndiwe kimbilio langu.

5 Ninaikabidhi roho yangu mikononi mwako,

EeBwanaunikomboe,

wewe uliye Mungu wa kweli.

6 Ninawachukia wale wanaong’ang’ania sanamu batili;

mimi ninamtumainiBwana.

7 Nitafurahia na kushangilia upendo wako,

kwa kuwa uliona mateso yangu

na ulijua maumivu ya nafsi yangu.

8 Hukunikabidhi kwa adui yangu

bali umeiweka miguu yangu

mahali penye nafasi.

9 EeBwanaunihurumie, kwa kuwa niko kwenye shida;

macho yangu yanafifia kwa huzuni,

nafsi yangu na mwili wangu kwa sikitiko.

10 Maisha yangu yamedhoofika kwa majonzi,

naam, miaka yangu kwa kulia kwa maumivu makali;

nguvu zangu zinaisha kwa ajili ya mateso,

na mifupa yangu inachakaa.

11 Kwa sababu ya adui zangu wote,

nimedharauliwa kabisa na jirani zangu,

hata rafiki zangu wananiogopa,

wale wanionao barabarani hunikimbia.

12 Nimesahaulika miongoni mwao kama mtu aliyekufa,

nimekuwa kama chombo cha mfinyanzi kilichovunjika.

13 Kwa maana nimesikia maneno

niliyosingiziwa na watu wengi;

vitisho viko pande zote;

kwa kuwa wamefanya mashauri ya pamoja dhidi yangu

na kula njama kuniua.

14 Lakini mimi ninakutumaini wewe peke yako, EeBwana;

nimesema, “Wewe ndiwe Mungu wangu.”

15 Siku za maisha yangu ziko mikononi mwako,

uniokoe mikononi mwa adui zangu

na wale wanifuatiao.

16 Mwangazie mtumishi wako uso wako,

uniokoe kwa ajili ya upendo wako usiokoma.

17 Usiniache niaibike, EeBwana,

kwa maana nimekulilia wewe,

bali waovu waaibishwe

na kunyamazishwa Kuzimu.

18 Midomo yao isemayo uongo na inyamazishwe,

kwa maana kwa kiburi na dharau husema

kwa majivuno dhidi ya wenye haki.

19 Tazama jinsi ulivyo mkuu wema wako,

uliowawekea akiba wakuchao,

ambao huwapa wale wakukimbiliao

machoni pa watu.

20 Unawahifadhi katika uvuli wa uwepo wako

kutokana na hila za wanadamu;

katika makao yako huwaweka salama

kutokana na ndimi za mashtaka.

21 AtukuzweBwana,

kwa kuwa amenionyesha upendo wake wa ajabu

nilipokuwa katika mji uliozingirwa.

22 Kwa haraka yangu nilisema,

“Nimekatiliwa mbali na macho yako!”

Hata hivyo ulisikia kilio changu

ukanihurumia nilipokuita unisaidie.

23 MpendeniBwananinyi watakatifu wake wote!

Bwanahuwahifadhi waaminifu,

lakini wenye kiburi huwalipiza kikamilifu.

24 Iweni hodari na mjipe moyo,

ninyi nyote mnaomtumainiBwana.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/31-5c2a77da4be1198712267b5c53c1fb47.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

19 − 8 =