1 Amka, amka, Ee Sayuni,
jivike nguvu.
Vaa mavazi yako ya fahari,
Ee Yerusalemu, mji mtakatifu.
Asiyetahiriwa na aliye najisi
hataingia kwako tena.
2 Jikung’ute mavumbi yako,
inuka, uketi kwenye kiti cha enzi, Ee Yerusalemu.
Jifungue minyororo iliyo shingoni mwako.
Ee Binti Sayuni uliye mateka.
3 Kwa kuwa hili ndilo asemaloBwana:
“Mliuzwa pasipo malipo,
nanyi mtakombolewa bila fedha.”
4 Kwa maana hili ndilo asemaloBwanaMwenyezi:
“Hapo kwanza watu wangu walishuka Misri kuishi,
hatimaye, Ashuru wakawaonea.
5 “Basi sasa nina nini hapa?” asemaBwana.
“Kwa kuwa watu wangu wamechukuliwa pasipo malipo,
nao wale wanaowatawala wanawadhihaki,”
asemaBwana.
“Mchana kutwa
jina langu limetukanwa bila kikomo.
6 Kwa hiyo watu wangu watalijua Jina langu;
kwa hiyo katika siku ile watajua
kwamba ndimi niliyetangulia kulisema.
Naam, ni mimi.”
7 Tazama jinsi ilivyo mizuri juu ya milima
miguu yao wale waletao habari njema,
wale wanaotangaza amani,
wanaoleta habari njema,
wanaotangaza wokovu,
wauambiao Sayuni,
“Mungu wako anatawala!”
8 Sikiliza! Walinzi wako wanapaza sauti zao,
kwa pamoja wanapaza sauti zao kwa furaha.
WakatiBwanaatakaporejea Sayuni,
wataliona kwa macho yao wenyewe.
9 Pazeni sauti ya nyimbo za furaha kwa pamoja,
enyi magofu ya Yerusalemu,
kwa maanaBwanaamewafariji watu wake,
ameikomboa Yerusalemu.
10 Mkono mtakatifu waBwanaumefunuliwa
machoni pa mataifa yote,
nayo miisho yote ya dunia itaona
wokovu wa Mungu wetu.
11 Ondokeni, ondokeni, tokeni huko!
Msiguse kitu kilicho najisi!
Tokeni kati yake mwe safi,
ninyi mchukuao vyombo vyaBwana.
12 Lakini hamtaondoka kwa haraka,
wala hamtakwenda kwa kukimbia;
kwa maanaBwanaatatangulia mbele yenu,
Mungu wa Israeli atakuwa mlinzi nyuma yenu.
Mateso Na Utukufu Wa Mtumishi
13 Tazama, mtumishi wangu atatenda kwa hekima;
atatukuzwa na kuinuliwa juu na kukwezwa sana.
14 Kama ambavyo walikuweko wengi
walioshangazwa naye,
uso wake ulikuwa umeharibiwa sana
zaidi ya mtu ye yote
na umbo lake kuharibiwa
zaidi ya mfano wa mwanadamu:
15 hivyo atashangaza mataifa mengi,
nao wafalme watafunga vinywa vyao
kwa sababu yake.
Kwa kuwa yale ambayo hawakuambiwa, watayaona,
nayo yale wasiyoyasikia,
watayafahamu.
—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ISA/52-60ccd17162f8f971ccf3535f61e23995.mp3?version_id=1627—