Isaya 40

Faraja Kwa Watu Wa Mungu

1 Wafarijini, wafarijini watu wangu,

asema Mungu wenu.

2 Sema na Yerusalemu kwa upole,

umtangazie

kwamba kazi yake ngumu imekamilika,

kwamba dhambi yake imefanyiwa fidia,

kwamba amepokea kutoka mkononi mwaBwana

maradufu kwa ajili ya dhambi zake zote.

3 Sauti ya mtu aliaye:

“Itengenezeni jangwani njia yaBwana,

nyosheni njia kuu nyikani

kwa ajili ya Mungu wetu.

4 Kila bonde litainuliwa,

kila mlima na kilima kitashushwa;

ardhi yenye mabonde patasawazishwa,

mahali palipoparuza patanyooshwa.

5 Utukufu waBwanautafunuliwa,

nao wanadamu wote kwa pamoja watauona.

Kwa maana kinywa chaBwanakimenena.”

6 Sauti husema, “Piga kelele.”

Nami nikasema, “Nipige kelele gani?”

“Wanadamu wote ni kama majani,

nao utukufu wao wote

ni kama maua ya kondeni.

7 Majani hunyauka na maua huanguka,

kwa sababu pumzi yaBwanahuyapuliza.

Hakika wanadamu ni majani.

8 Majani hunyauka na maua huanguka,

lakini neno la Mungu wetu lasimama milele.”

9 Wewe uletaye habari njema Sayuni,

panda juu ya mlima mrefu.

Wewe uletaye habari njema Yerusalemu,

inua sauti yako kwa kupiga kelele,

inua sauti, usiogope;

iambie miji ya Yuda,

“Yuko hapa Mungu wenu!”

10 Tazameni,BwanaMwenyezi anakuja na nguvu,

nao mkono wake ndio utawalao kwa ajili yake.

Tazameni, ujira wake u pamoja naye,

nayo malipo yake yanafuatana naye.

11 Huchunga kundi lake kama mchungaji wa mifugo:

Hukusanya wana-kondoo katika mikono yake

na kuwachukua karibu na moyo wake,

huwaongoza taratibu wale wanyonyeshao.

12 Ni nani aliyepima maji ya bahari

kwenye konzi ya mkono wake,

# au kuzipima mbingu kwa shibiriyake?

Ni nani aliyeyashika mavumbi ya dunia katika kikapu,

au kupima milima kwenye kipimio

na vilima kwenye mizani?

13 Ni nani aliyeyafahamu mawazo yaBwana,

au kumfundisha kama mshauri wake?

14 Ni nani ambayeBwanaametaka shauri kwake ili kumwelimisha,

naye ni nani aliyemfundisha njia iliyo sawa?

Ni nani aliyemfundisha maarifa

au kumwonyesha mapito ya ufahamu?

15 Hakika mataifa ni kama tone ndani ya ndoo,

ni kama vumbi jembamba juu ya mizani,

huvipima visiwa kana kwamba vilikuwa vumbi laini.

16 Lebanoni hautoshi kwa moto wa madhabahuni,

wala wanyama wake hawatoshi kwa sadaka za kuteketezwa.

17 Mbele yake mataifa yote ni kama si kitu,

yanaonekana yasio na thamani

na zaidi ya bure kabisa.

18 Basi, utamlinganisha Mungu na nani?

Utamlinganisha na kitu gani?

19 Kwa habari ya sanamu, fundi huisubu,

naye mfua dhahabu huifunika kwa dhahabu

na kuitengenezea mikufu ya fedha.

20 Mtu aliye maskini sana asiyeweza kuleta sadaka kama hii

huuchagua mti usiooza.

Humtafuta fundi stadi

wa kusimamisha sanamu ambayo haitatikisika.

21 Je, hujui?

Je, hujasikia?

Je, hujaambiwa tangu mwanzo?

Je, hujafahamu tangu kuumbwa kwa dunia?

22 Anakaa kwenye kiti cha enzi juu ya duara ya dunia,

nao watu wakaao ndani yake ni kama panzi.

Huzitandaza mbingu kama chandarua

na kuzitandaza kama hema la kuishi.

23 Huwafanya wakuu kuwa si kitu

na kuwashusha watawala wa dunia hii kuwa kitu bure.

24 Mara baada ya kupandwa,

mara baada ya kutiwa ardhini

mara baada ya kutoa mizizi yao ardhini,

ndipo huwapulizia nao wakanyauka,

nao upepo wa kisulisuli

huwapeperusha kama makapi.

25 “Utanilinganisha mimi na nani?

Au ni nani anayelingana nami?”

Asema yeye Aliye Mtakatifu.

26 Inueni macho yenu mtazame mbinguni:

Ni nani aliyeumba hivi vyote?

Yeye aletaye nje jeshi la nyota moja baada ya nyingine

na kuziita kila moja kwa jina lake?

Kwa sababu ya uweza wake mkuu na nguvu zake kuu,

hakuna hata mojawapo inayokosekana.

27 Kwa nini unasema, Ee Yakobo,

nanyi Ee Israeli, kulalamika,

“Njia yangu imefichwaBwanaasiione,

Mungu wangu hajali shauri langu?”

28 Je wewe, hufahamu?

Je wewe, hujasikia?

Bwanani Mungu wa milele,

Muumba wa miisho ya dunia.

Hatachoka wala kulegea,

wala hakuna hata mmoja

awezaye kuupima ufahamu wake.

29 Huwapa nguvu waliolegea

na huongeza nguvu za wadhaifu.

30 Hata vijana huchoka na kulegea,

nao vijana wanaume kujikwaa na kuanguka,

31 bali wale wamtumainioBwana

atafanya upya nguvu zao.

Watapaa juu kwa mbawa kama tai;

watapiga mbio wala hawatachoka,

watatembea kwa miguu wala hawatazimia.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ISA/40-3461f7e73668810625cba05ce7394d8c.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

three × 2 =