Isaya 38

Kuugua Kwa Mfalme Hezekia

1 Katika siku hizo Hezekia akaugua naye akawa karibu na kufa. Nabii Isaya mwana wa Amozi akamwendea na kumwambia, “Hili ndilo asemaloBwana: Tengeneza mambo ya nyumba yako, kwa sababu utakufa, hutapona.”

2 Hezekia akageuza uso wake kuelekea ukutani na kumwombaBwana,

3 “EeBwana, kumbuka, jinsi nilivyotembea mbele zako kwa uaminifu na kujitoa kwa moyo wote nami nimefanya lile lililo jema machoni pako.” Naye Hezekia akalia sana sana.

4 Ndipo neno laBwanalikamjia Isaya:

5 “Nenda ukamwambie Hezekia, ‘Hili ndilo asemaloBwana, Mungu wa baba yako Daudi: Nimesikia maombi yako na nimeona machozi yako, nitaiongeza miaka kumi na mitano katika maisha yako.

6 Nami nitakuokoa wewe pamoja na mji huu kutoka katika mkono wa mfalme wa Ashuru. Nitaulinda mji huu.

7 “ ‘Hii ndiyo ishara yaBwanakwako ya kwambaBwanaatafanya kile alichoahidi:

8 Nitafanya kivuli cha jua kwenye ngazi iliyojengwa na Ahazi kirudi nyuma madaraja kumi.’ ” Hivyo jua likarudi nyuma madaraja kumi ambayo lilikuwa limeshuka.

9 Maandiko ya Hezekia mfalme wa Yuda baada ya kuugua kwake na kupona:

10 Nilisema, “Katika ustawi wa maisha yangu

# je, ni lazima nipite katika malango ya mauti

na kupokonywa miaka yangu iliyobaki?”

11 Nilisema, “Sitamwona tenaBwana,

Bwanakatika nchi ya walio hai,

wala sitamtazama tena mwanadamu,

wala kuwa na wale ambao sasa wanakaa katika ulimwengu huu.

12 Kama hema la mchunga mifugo,

nyumba yangu imebomolewa na kutwaliwa kutoka kwangu.

Kama mfumaji nimevingirisha maisha yangu,

naye amenikatilia mbali kutoka kitanda cha mfumi,

mchana na usiku uliyakomesha maisha yangu.

13 Nilingoja kwa uvumilivu hadi mapambazuko,

lakini kama simba alivunja mifupa yangu yote,

mchana na usiku uliyakomesha maisha yangu.

14 Nililia kama mbayuwayu au korongo,

niliomboleza kama hua aombolezaye.

Macho yangu yalififia nilipotazama mbinguni.

Ee Bwana, ninataabika, njoo unisaidie!”

15 Lakini niseme nini?

Amesema nami,

naye yeye mwenyewe amelitenda hili.

Nitatembea kwa unyenyekevu

katika miaka yangu yote

kwa sababu ya haya maumivu makali

ya nafsi yangu.

16 Bwana, kwa mambo kama haya watu huishi,

nayo roho yangu hupata uzima katika hayo pia.

Uliniponya

na kuniacha niishi.

17 Hakika ilikuwa kwa ajili ya faida yangu ndiyo maana nikapata maumivu makali.

Katika upendo wako ukaniokoa

kutoka katika shimo la uharibifu;

umeziweka dhambi zangu zote

nyuma yako.

18 Kwa maana kaburihaliwezi kukusifu,

mauti haiwezi kuimba sifa zako;

wale washukao chini shimoni

hawawezi kuutarajia uaminifu wako.

19 Walio hai, walio hai, wanakusifu,

kama ninavyofanya leo;

baba huwaambia watoto wao

habari za uaminifu wako.

20 Bwanaataniokoa,

nasi tutaimba kwa vyombo vya nyuzi

siku zote za maisha yetu

katika Hekalu laBwana.

21 Isaya alikuwa amesema, “Uandae mkate wa tini uubandike juu ya jipu, naye atapona.”

22 Hezekia alikuwa ameuliza, “Ni ishara ipi kwamba nitapanda kwenda hekaluni mwaBwana?”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ISA/38-e25042c08218db7f0aab76070ad3053b.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

nine + two =