Yeremia 48

Ujumbe Kuhusu Moabu

1 Kuhusu Moabu:

Hili ndiloBwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo:

“Ole wa Nebo, kwa maana utaharibiwa.

Kiriathaimu utaaibishwa na kutekwa;

Misgabu itaaibishwa na kuvunjwa vunjwa.

2 Moabu haitasifiwa tena;

huko Heshboni watu watafanya shauri baya la anguko lake:

‘Njoni na tuangamize taifa lile.’

Wewe nawe, Ee Madmeni, utanyamazishwa;

upanga utakufuatia.

3 Sikiliza kilio kutoka Horonaimu,

kilio cha maangamizi makuu na uharibifu.

4 Moabu utavunjwa,

wadogo wake watapiga kelele.

5 Wanapanda kwenda njia ya kuelekea Luhithi,

wakilia kwa uchungu wanapotembea,

kwenye njia inayoshuka kwenda Horonaimu

kilio cha uchungu kwa ajili ya uharibifu kinasikika.

6 Kimbieni! Okoeni maisha yenu,

iweni kama kichaka jangwani.

7 Kwa kuwa mmetumainia matendo yenu na mali zenu,

ninyi pia mtachukuliwa mateka,

# naye Kemoshiatakwenda uhamishoni,

pamoja na makuhani wake na maafisa wake.

8 Mharabu atakuja dhidi ya kila mji,

wala hakuna mji utakaookoka.

Bonde litaangamizwa na uwanda utaharibiwa,

kwa sababuBwanaamesema.

9 Wekeni chumvi kwa ajili ya Moabu,

kwa kuwa ataangamizwa;

miji yake itakuwa ukiwa,

pasipo kuwa na mtu atakayeishi ndani yake.

10 “Alaaniwe yeye afanyaye kazi yaBwanakwa hila!

Alaaniwe yeye auzuiaye upanga wake usimwage damu!

11 “Moabu amestarehe tangu ujana wake,

kama divai iliyoachwa kwenye machujo yake,

haikumiminwa kutoka chombo kimoja hadi kingine,

hajaenda uhamishoni.

Kwa hiyo ana ladha ile ile kama aliyokuwa nayo,

nayo harufu yake haijabadilika.

12 Lakini siku zinakuja,”

asemaBwana,

“nitakapotuma watu wamiminao kutoka kwenye magudulia,

nao watammimina;

wataacha magudulia yake yakiwa matupu

na kuvunja mitungi yake.

13 Kisha Moabu atamwonea aibu mungu wao Kemoshi,

kama vile nyumba ya Israeli walivyoona aibu

# wakati walipotegemea mungu wa Betheli.

14 “Mwawezaje kusema, ‘Sisi ni mashujaa,

watu jasiri katika vita’?

15 Moabu ataangamizwa na miji yake itavamiwa,

vijana wake waume walio bora sana watachinjwa,”

asema Mfalme, ambaye jina lake

niBwanaMungu Mwenye Nguvu Zote.

16 “Kuanguka kwa Moabu kumekaribia,

janga kubwa litamjia kwa haraka.

17 Ombolezeni kwa ajili yake, ninyi nyote mnaoishi kumzunguka,

ninyi nyote mnaojua sifa zake,

semeni, ‘Tazama jinsi ilivyovunjika fimbo ya kifalme yenye nguvu,

tazama jinsi ilivyovunjika fimbo iliyotukuka!’

18 “Shuka kutoka katika fahari yako

na uketi katika ardhi iliyokauka,

Enyi wenyeji wa Binti wa Diboni,

kwa maana yeye aangamizaye Moabu atakuja dhidi yako

na kuangamiza miji yako

iliyozungushiwa maboma.

19 Simama kando ya barabara na utazame,

wewe ambaye unaishi Aroeri.

Mwulize mwanaume anayekimbia

na mwanamke anayetoroka,

waulize, ‘Kumetokea nini?’

20 Moabu amefedheheshwa, kwa kuwa amevunjwavunjwa.

Lieni kwa huzuni na kupiga kelele!

Tangazeni kando ya Arnoni

kwamba Moabu ameangamizwa.

21 Hukumu imefika kwenye uwanda wa juu:

katika Holoni, Yasa na Mefaathi,

22 katika Diboni, Nebo

na Beth-Diblathaimu,

23 katika Kiriathaimu, Beth-Gamuli

na Beth-Meoni,

24 katika Keriothi na Bosra;

kwa miji yote ya Moabu,

iliyoko mbali na karibu.

25 Pembeya Moabu imekatwa,

mkono wake umevunjwa,”

asemaBwana.

26 “Mlevye,

kwa kuwa amemdharauBwana.

Moabu na agaegae katika matapishi yake,

yeye na awe kitu cha dhihaka.

27 Je, Israeli hakuwa kitu chako cha kudhihakiwa?

Je, alikamatwa miongoni mwa wezi,

kiasi cha kutikisa kichwa chako kwa dharau

kila mara unapozungumza juu yake?

28 Ondokeni kwenye miji yenu na mkaishi katikati ya miamba,

enyi mnaoishi Moabu.

Iweni kama huwa ambaye hutengeneza kiota

chake kwenye mdomo wa pango.

29 “Tumesikia juu ya kiburi cha Moabu:

kutakabari kwake kwa kiburi na majivuno,

kiburi chake na ufidhuli wake,

na kujivuna kwa moyo wake.

30 Ninaujua ujeuri wake lakini ni bure,”

asemaBwana,

“nako kujisifu kwake hakumsaidii cho chote.

31 Kwa hiyo namlilia Moabu,

kwa ajili ya Moabu yote ninalia,

ninaomboleza kwa ajili

ya watu wa Kir-Haresethi.

32 Ninalia machozi kwa ajili yenu,

kama Yazeri aliavyo,

Enyi mizabibu ya Sibma.

Matawi yako yameenea mpaka baharini;

yamefika mpaka Bahari ya Yazeri.

Mwarabu ameanguka juu ya matunda yako

yaliyoiva na mizabibu.

33 Shangwe na furaha vimetoweka

kutoka kwenye bustani na mashamba ya Moabu.

Nimekomesha kutiririka kwa divai kutoka katika mashinikizo;

hakuna hata mmoja ayakanyagaye

kwa kelele za shangwe.

Ingawa kuna kelele,

sio za shangwe.

34 “Sauti ya kilio chao inapanda

kutoka Heshboni mpaka Eleale na Yahazi,

kutoka Soari mpaka Horonaimu na Eglath-Shelishiya,

kwa kuwa hata maji ya Nimrimu yamekauka.

35 Katika Moabu nitakomesha wale wote watoao sadaka

mahali pa juu pa kuabudia miungu,

na kufukiza uvumba kwa miungu yao,”

asemaBwana.

36 “Kwa hiyo moyo wangu unaomboleza kwa ajili ya Moabu kama filimbi;

unaomboleza kama filimbi

kwa ajili ya watu wa Kir-Haresethi.

Utajiri waliojipatia umetoweka.

37 Kila kichwa kimenyolewa

na kila mwenye ndevu zimekatwa;

kila mkono umekatwa na kila kiuno kimefunikwa

kwa nguo ya gunia.

38 Juu ya mapaa yote katika Moabu

na katika viwanja

hakuna kitu cho chote isipokuwa maombolezo,

kwa kuwa nimemvunja Moabu

kama gudulia ambalo hakuna mtu ye yote anayelitaka,”

asemaBwana.

39 “Tazama jinsi alivyovunjikavunjika!

Jinsi wanavyolia kwa huzuni!

Tazama jinsi Moabu anavyogeuka kwa aibu!

Moabu amekuwa kitu cha kudhihakiwa,

kitu cha kutisha kwa wale wote

wanaomzunguka.”

40 Hili ndilo asemaloBwana:

“Tazama! Tai anashuka chini,

akitanda mbawa zake juu ya Moabu.

41 Miji itatekwa na ngome zake

zitatwaliwa.

Katika siku hiyo, mioyo ya mashujaa wa Moabu

itakuwa kama moyo wa mwanamke

aliye katika utungu wa kuzaa.

42 Moabu ataangamizwa kama taifa

kwa sababu amemdharauBwana.

43 Hofu kuu, shimo na mtego unawangojea,

Enyi watu wa Moabu,”

asemaBwana.

44 “Ye yote atakayeikimbia hiyo hofu kuu

ataanguka ndani ya shimo,

ye yote atakayepanda kutoka shimoni,

atanaswa katika mtego,

kwa sababu nitaleta juu ya Moabu

mwaka wa adhabu yake,”

asemaBwana.

45 “Katika kivuli cha Heshboni,

wakimbizi wamesimama pasipo msaada,

kwa kuwa moto umezimika huko Heshboni,

mwali wa moto kutoka katikati ya Sihoni;

unaunguza vipaji vya nyuso za Moabu,

mafuvu yao wenye kujivuna kwa kelele.

46 Ole wako, Ee Moabu!

Watu wa Kemoshi wameangamizwa;

wana wako wamepelekwa uhamishoni

na binti zako wamechukuliwa mateka.

47 “Lakini nitarudisha mateka wa Moabu,

katika siku zijazo,”

asemaBwana.

Huu ndio mwisho wa hukumu juu ya Moabu.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JER/48-f4cb2d105b31349f0d5963d492217cd1.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

eight + 16 =