Yeremia 47

Ujumbe Kuhusu Wafilisti

1 Hili ndilo neno laBwanalililomjia nabii Yeremia kuhusu Wafilisti, kabla Farao hajaishambulia Gaza:

2 Hili ndilo asemaloBwana:

“Tazama jinsi maji yanavyoinuka huko kaskazini,

yatakuwa mafuriko yenye nguvu sana.

Yataifurikia nchi na vitu vyote vilivyomo ndani yake,

miji na wale waishio ndani yake.

Watu watapiga kelele;

wote waishio katika nchi wataomboleza

3 kwa sauti ya kwato za farasi waendao mbio,

kwa sauti ya magari ya adui

na mngurumo wa magurudumu yake.

Baba hawatageuka kuwasaidia watoto wao,

mikono yao italegea.

4 Kwa maana siku imewadia

kuwaangamiza Wafilisti wote

na kuwakatilia mbali walionusurika wote

ambao wangeweza kuisaidia Tiro na Sidoni.

Bwanaanakaribia kuwaangamiza Wafilisti,

# mabaki toka pwani za Kaftori.

5 Gaza atanyoa kichwa chake katika kuomboleza,

Ashkeloni atanyamazishwa.

Enyi mabaki kwenye tambarare,

mtajikatakata wenyewe mpaka lini?

6 “Mnalia, ‘Aa, upanga waBwana,

utaendelea mpaka lini ndipo upumzike?

Rudi ndani ya ala yako;

acha na utulie.’

7 Lakini upanga utatuliaje

wakatiBwanaameuamuru,

wakati ameuagiza

kuishambulia Ashkeloni pamoja na pwani yake?”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JER/47-c3edb0f62bd1412519000f571c8e9abe.mp3?version_id=1627—