Ujumbe Kuhusu Misri
1 Hili ni neno laBwanalililomjia nabii Yeremia kuhusu mataifa:
2 Kuhusu Misri:
Huu ni ujumbe dhidi ya jeshi la Farao Neko mfalme wa Misri, lililoshindwa huko Karkemishi kwenye Mto Eufrati na Nebukadneza mfalme wa Babeli katika mwaka wa nne wa kutawala kwake Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda:
3 “Wekeni tayari ngao zenu, kubwa na ndogo,
mtoke kwa ajili ya vita!
4 Fungieni farasi lijamu,
pandeni farasi!
Shikeni nafasi zenu
mkiwa mmevaa chapeo!
Isugueni mikuki yenu,
vaeni dirii vifuani!
5 Je, ninaona nini?
Wametiwa hofu,
wanarudi nyuma,
askari wao wameshindwa.
Wanakimbia kwa haraka
pasipo kutazama nyuma,
tena kuna hofu kuu kila upande,”
asemaBwana.
6 Walio wepesi na wenye mbio hawawezi kukimbia,
wala wenye nguvu hawawezi kutoroka.
Kaskazini, kando ya Mto Eufrati
wanajikwaa na kuanguka.
7 “Ni nani huyu ajiinuaye kama Mto Nile,
kama mito yenye maji yanayofanya mawimbi?
8 Misri hujiinua kama Mto Nile,
kama mito yenye maji yanayofanya mawimbi.
Husema, ‘Nitainuka na kufunika dunia,
nitaiangamiza miji na watu wake.’
9 Songeni mbele, Enyi farasi!
Endesheni kwa ukali, Enyi magari ya farasi,
Endeleeni mbele, Enyi mashujaa:
# watu wa Kushina Putuwachukuao ngao,
# watu wa Ludiwavutao upinde.
10 Lakini ile siku ni ya Bwana,BwanaMwenye Nguvu Zote,
siku ya kulipiza kisasi,
kisasi juu ya adui zake.
Upanga utakula mpaka utakapotosheka,
mpaka utakapozima kiu yake kwa damu.
Kwa maana Bwana,BwanaMwenye Nguvu Zote, atatoa dhabihu
kwenye nchi ya kaskazini,
kando ya Mto Eufrati.
11 “Panda mpaka Gileadi ukapate zeri,
Ee Bikira Binti wa Misri.
Lakini umetumia dawa nyingi bila mafanikio;
huwezi kupona.
12 Mataifa yatasikia juu ya aibu yako,
kilio chako kitaijaza dunia.
Shujaa mmoja atajikwaa juu ya mwingine,
nao wataanguka chini pamoja.”
13 Huu ndio ujumbeBwanaaliomwambia nabii Yeremia juu ya kuja kwa Nebukadneza mfalme wa Babeli ili kuishambulia Misri:
14 “Tangaza hili katika Misri, nawe ulihubiri katika Migdoli,
# hubiri pia katika Memfisina Tahpanhesi:
‘Shikeni nafasi zenu na mwe tayari,
kwa kuwa upanga unawala
wale wanaokuzunguka.’
15 Kwa nini mashujaa wakoa wamesombwa
na kupelekwa mbali?
Hawawezi kusimama, kwa maanaBwana
atawasukuma awaangushe chini.
16 Watajikwaa mara kwa mara,
wataangukiana wao kwa wao.
Watasema, ‘Amka, turudi
kwa watu wetu na nchi yetu,
mbali na upanga wa mtesi.’
17 Huko watasema,
‘Farao mfalme wa Misri ni makelele tu,
amekosa wasaa wake.’
18 “Kwa hakika kama niishivyo,” asema Mfalme,
ambaye jina lake niBwanaMwenye Nguvu Zote,
“mmoja atakuja ambaye ni kama Tabori
miongoni mwa milima,
kama Karmeli kando ya bahari.
19 Funga mizigo yako kwenda uhamishoni,
wewe ukaaye Misri,
kwa kuwa Memfisi utaangamizwa
na kuwa magofu pasipo mkazi.
20 “Misri ni mtamba mzuri wa ng’ombe,
lakini kipanga anakuja
dhidi yake kutoka kaskazini.
21 Askari wake waliokodiwa katika safu zake
wako kama ndama walionenepeshwa.
Wao pia watageuka na kukimbia pamoja,
hawataweza kuhimili vita,
kwa maana siku ya msiba inakuja juu yao,
wakati wao wa kuadhibiwa.
22 Misri atatoa sauti kama ya nyoka anayekimbia
kadiri adui anavyowasogelea na majeshi,
watakuja dhidi yake wakiwa na mashoka,
kama watu wakatao miti.
23 Wataufyeka msitu wake,”
asemaBwana,
“hata kama umesongamana kiasi gani.
Ni wengi kuliko nzige,
hawawezi kuhesabika.
24 Binti wa Misri ataaibishwa,
atatiwa mikononi mwa watu wa kaskazini.”
25 BwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asema: “Nakaribia kuleta adhabu juu ya Amoni mungu wa Thebesi, na juu ya Farao, Misri na miungu yake, wafalme wake pamoja na wale wanaomtegemea Farao.
26 Nitawatia mikononi mwa wale wanaotafuta uhai wao, yaani Nebukadneza mfalme wa Babeli na maafisa wake. Hatimaye, hata hivyo, Misri itakaliwa kama nyakati zilizopita,” asemaBwana.
27 “Usiogope, Ee Yakobo mtumishi wangu,
usifadhaike, Ee Israeli.
Hakika nitakuokoa toka katika nchi za mbali,
uzao wako toka nchi ya uhamisho wao.
Yakobo atakuwa tena na amani na salama,
wala hakuna hata mmoja atakayewatia hofu.
28 Usiogope, Ee Yakobo mtumishi wangu,
kwa maana mimi niko pamoja nawe,”
asemaBwana.
“Ingawa nitayaangamiza kabisa mataifa yote
ambayo miongoni mwake nimekutawanya,
sitakuangamiza wewe kabisa,
Nitakurudi lakini kwa haki tu,
wala sitakuacha kabisa bila kukuadhibu.”
—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JER/46-0482eba6ec303002e91d40b4bb6f9d80.mp3?version_id=1627—