Yeremia 45

Ujumbe Kwa Baruki

1 Hili ndilo nabii Yeremia alilomwambia Baruki mwana wa Neria katika mwaka wa nne wa kutawala kwake Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, baada ya Baruki kuandika katika kitabu maneno ambayo yalitoka kinywani mwa Yeremia wakati ule:

2 “Hili ndiloBwana, Mungu wa Israeli, akuambialo wewe Baruki:

3 Ulisema, ‘Ole wangu!Bwanaameongeza huzuni juu ya maumivu yangu, nimechoka kwa kulia kwa uchungu wala sipati pumziko.’ ”

4 Bwanaakasema, “Mwambie hivi: ‘Hili ndilo asemaloBwana: Nitakibomoa kile nilichokijenga na kung’oa kile nilichokipanda, katika nchi yote.

5 Je, utajitafutia mambo makubwa kwa ajili yako mwenyewe? Usiyatafute hayo. Kwa kuwa nitaleta maangamizi juu ya watu wote, asemaBwana, lakini po pote utakapokwenda nitayaokoa maisha yako.’ ”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JER/45-ec89824bdbfc3cb8636fd7a64eb5df53.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

4 × 4 =