Yoshua 1

Bwana Anamwagiza Yoshua

1 Baada ya kifo cha Mose mtumishi waBwana,Bwanaakamwambia Yoshua mwana wa Nuni, msaidizi wa Mose:

2 “Mtumishi wangu Mose amekufa. Sasa basi, wewe pamoja na watu wote hawa, jiandaeni kuvuka huu Mto Yordani kuingia nchi ambayo karibu nitawapa wana wa Israeli.

3 Kila mahali nyayo za miguu yenu zitakapokanyaga nimewapa, kama vile nilivyomwahidi Mose.

4 Nchi yenu itaenea kuanzia jangwa hili hadi Lebanoni, tena kuanzia mto huu mkubwa wa Eufrati, yaani nchi yote ya Wahiti, hadi Bahari ile Kubwailiyoko upande wa magharibi.

5 Hakuna mtu ye yote atakayeweza kushindana na wewe siku zote za maisha yako. Kama vile nilivyokuwa pamoja na Mose, ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe, sitakuacha wala sitakupungukia.

6 “Uwe hodari na moyo wa ushujaa, kwa sababu wewe ndiwe utakayewaongoza watu hawa kuirithi nchi niliyowaapia baba zao kuwapa.

7 Uwe hodari tu na ushujaa mwingi. Uwe na bidii kutii sheria zote alizokupa Mose mtumishi wangu, usiziache kwa kugeuka kuelekea kuume au kushoto, ili upate kufanikiwa po pote uendako.

8 Usiache Kitabu hiki cha Torati kiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, ili upate kuwa mwangalifu kufanya kila kitu sawasawa na yote yaliyoandikwa ndani yake. Ndipo utakapoifanikisha njia yako na kisha utastawi sana.

9 Je, si mimi niliyekuamuru? Uwe imara na hodari sana. Usiogope wala usivunjike moyo, kwa kuwaBwanaMungu wako atakuwa pamoja nawe ko kote uendako.”

10 Ndipo Yoshua akawaagiza viongozi wa watu akisema,

11 “Pitieni katika kambi yote mkawaambie watu, ‘Wekeni tayari mahitaji yenu. Siku tatu kuanzia sasa mtavuka hii Yordani ili kuingia na kuimiliki nchi ambayoBwanaMungu wenu anawapa iwe yenu wenyewe.’ ”

12 Lakini kwa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase, Yoshua akasema,

13 “Kumbukeni agizo lile Mose mtumishi waBwanaalilowapa: ‘BwanaMungu wenu anawapa ninyi raha, naye amewapa nchi hii.’

14 Wake zenu, watoto wenu na mifugo yenu watakaa katika nchi ile Mose aliyowapa mashariki ya Yordani, lakini mashujaa wenu wote, wakiwa wamevikwa silaha kikamilifu lazima wavuke mbele ya ndugu zenu. Imewapasa kuwasaidia ndugu zenu hadi

15 Bwanaawape nao raha, kama alivyokwisha kufanya kwa ajili yenu hadi wao nao watakapokuwa wamemiliki nchi ileBwanaMungu wenu anayowapa. Baada ya hilo, mwaweza kurudi na kukalia nchi yenu wenyewe, ambayo Mose mtumishi waBwanaaliwapa mashariki ya Yordani kuelekea linakochomoza jua.”

16 Ndipo wakamjibu Yoshua, “Cho chote ambacho umetuagiza tutafanya na po pote utakapotutuma tutakwenda.

17 Kama vile tulivyomtii Mose kikamilifu, ndivyo tutakavyokutii wewe.BwanaMungu wako na awe pamoja nawe tu kama vile alivyokuwa pamoja na Mose.

18 Ye yote atakayeasi neno lako na kuacha kuyatii maneno yako, au cho chote utakachowaamuru, atauawa. Uwe imara na hodari tu!”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOS/1-45db6e272443fb54fa0c3826e0d53e04.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ten − 8 =