Zaburi 140

Kuomba Ulinzi Wa Mungu

(Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Daudi)

1 EeBwana, niokoe, kutoka kwa watu waovu;

nilinde na watu wenye jeuri,

2 ambao hupanga mipango mibaya mioyoni mwao

na kuchochea vita siku zote.

3 Wao hufanya ndimi zao kali kama za nyoka,

sumu ya nyoka imo midomoni mwao.

4 EeBwana, niepushe na mikono ya waovu;

nilinde na watu wenye jeuri

wanaopanga kunikwaza miguu yangu.

5 Wenye kiburi wameficha mtego wa kuninasa,

wametandaza kamba za wavu wao,

wametega mitego kwenye njia yangu.

6 EeBwana, ninakuambia,

“Wewe ni Mungu wangu.”

EeBwana, usikie kilio changu

na kunihurumia.

7 EeBwanaMwenyezi,

Mwokozi wangu mwenye nguvu,

unikingaye kichwa changu siku ya vita:

8 EeBwana, usiwape waovu matakwa yao,

usiache mipango yao ikafanikiwa,

wasije wakajisifu.

9 Vichwa vya wanaonizunguka na vifunikwe

na shida zinazosababishwa na midomo yao.

10 Makaa ya mawe ya moto na yawaangukie!

Na watupwe motoni,

katika mashimo ya matope,

wasiinuke tena kamwe.

11 Wasingiziaji na wasifanikiwe katika nchi;

maafa na yawawinde watu wenye jeuri.

12 Najua kwambaBwanahuwapatia maskini haki,

na kuitegemeza njia ya mhitaji.

13 Hakika wenye haki watalisifu jina lako,

na waadilifu wataishi mbele zako.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/140-c7abfd880fe0c293fccb9cebb7d5d1a7.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

17 − 8 =