Zaburi 135

Wimbo Wa Sifa Kwa Mungu

1 MsifuniBwana.

Lisifuni jina laBwana,

msifuni, enyi watumishi waBwana,

2 ninyi ambao mnatumika ndani ya nyumba yaBwana,

katika nyua za nyumba ya Mungu wetu.

3 MsifuniBwana, kwa kuwaBwanani mwema,

liimbieni sifa jina lake, kwa maana hilo lapendeza.

4 Kwa maanaBwanaamemchagua Yakobo

kuwa wake mwenyewe,

Israeli kuwa mali yake ya thamani.

5 Ninajua ya kuwaBwanani mkuu,

kwamba Bwana wetu ni mkuu zaidi

kuliko miungu yote.

6 Bwanahufanya lo lote apendalo,

mbinguni na duniani,

katika bahari na vilindi vyake vyote.

7 Hufanya mawingu kupanda kutoka miisho ya dunia;

hupeleka umeme wa radi pamoja na mvua

na huleta upepo kutoka ghala zake.

8 Alimwua mzaliwa wa kwanza wa Misri,

mzaliwa wa kwanza

wa wanadamu na wanyama.

9 Alipeleka ishara zake na maajabu

katikati yako, Ee Misri,

dhidi ya Farao na watumishi wake wote.

10 Aliyapiga mataifa mengi,

na akaua wafalme wenye nguvu:

11 Mfalme Sihoni na Waamori,

Ogu mfalme wa Bashani

na wafalme wote wa Kanaani;

12 akatoa nchi yao kuwa urithi,

urithi kwa watu wake Israeli.

13 EeBwana, jina lako ladumu milele,

kumbukumbu za fahari zako,

EeBwana, kwa vizazi vyote.

14 MaanaBwanaatawathibitisha watu wake

kuwa wenye haki,

na kuwahurumia watumishi wake.

15 Sanamu za mataifa ni fedha na dhahabu,

zilizotengenezwa kwa mikono ya wanadamu.

16 Zina vinywa, lakini haziwezi kusema,

zina macho, lakini haziwezi kuona,

17 zina masikio, lakini haziwezi kusikia,

wala hakuna pumzi katika vinywa vyao.

18 Wale wanaozitengeneza watafanana nazo,

vivyo hivyo wote wanaozitumainia.

19 Ee nyumba ya Israeli, msifuniBwana;

Ee nyumba ya Aroni, msifuniBwana;

20 Ee nyumba ya Lawi, msifuniBwana;

ninyi mnaomcha, msifuniBwana.

21 MsifuniBwanakutoka Sayuni,

msifuni yeye aishiye Yerusalemu.

MsifuniBwana.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/135-b3cc2ae163386368ef8435e6ed41db87.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

11 + 4 =