Zaburi 101

Ahadi Ya Kuishi Kwa Uadilifu Na Kwa Haki (Zaburi Ya Daudi) 1 Nitaimba juu ya upendo wako na haki yako; kwako wewe, EeBwana, nitaimba sifa. 2 Nitazingatia kuishi maisha yasiyo na lawama: utakuja kwangu lini? Nitatembea nyumbani mwangu kwa moyo usio na lawama. 3 Sitaweka mbele ya macho yangu kitu kiovu. Ninayachukia matendo ya watu […]

Zaburi 102

Maombi Ya Mtu Mwenye Taabu (Maombi Ya Mtu Aliyechoka, Anayeteseka, Anayemimina Malalamiko Kwa Bwana ) 1 EeBwana, usikie maombi yangu, kilio changu cha kuomba msaada kikufikie. 2 Usinifiche uso wako ninapokuwa katika shida. Unitegee sikio lako, ninapoita, unijibu kwa upesi. 3 Kwa kuwa siku zangu zinatoweka kama moshi, mifupa yangu inaungua kama kaa la moto. […]

Zaburi 103

Upendo Wa Mungu (Zaburi Ya Daudi) 1 Ee nafsi yangu, umhimidiBwana, vyote vilivyomo ndani yangu vilihimidi jina lake takatifu. 2 Ee nafsi yangu, umhimidiBwana, wala usisahau wema wake wote, 3 akusamehe dhambi zako zote, akuponya magonjwa yako yote, 4 aukomboa uhai wako na kaburi, akuvika taji ya upendo na huruma, 5 atosheleza mahitaji yako kwa […]

Zaburi 104

Katika Kumsifu Muumba 1 Ee nafsi yangu, umhimidiBwana. EeBwanaMungu wangu, wewe ni mkuu sana, umejivika utukufu na enzi. 2 Amejifunika katika nuru kama vile kwa vazi, amezitandaza mbingu kama hema 3 na kuziweka nguzo za orofa yake juu ya maji. Huyafanya mawingu kuwa gari lake kubwa zuri, na hupanda kwenye mbawa za upepo. 4 Hufanya […]

Zaburi 105

Uaminifu Wa Mungu Kwa Israeli 1 MshukuruniBwana, liitieni jina lake, wajulisheni mataifa yale aliyoyatenda. 2 Mwimbieni yeye, mwimbieni yeye sifa, waambieni matendo yake yote ya ajabu. 3 Utukufu kwa jina lake takatifu, mioyo ya wale wamtafutaoBwanana ifurahi. 4 MtafuteniBwanana nguvu zake, utafuteni uso wake siku zote. 5 Kumbuka matendo ya ajabu aliyoyafanya, miujiza yake na […]

Zaburi 106

Wema Wa Bwana Kwa Watu Wake 1 MsifuniBwana. MshukuruniBwana, kwa kuwa ni mwema; upendo wake wadumu milele. 2 Ni nani awezaye kusimulia matendo makuu yaBwana au kutangaza kikamilifu sifa zake? 3 Heri wale wanaodumisha haki, ambao daima wanafanya yaliyo mema. 4 EeBwana, unikumbuke unapowatendea mema watu wako, uwe msaada wangu unapowaokoa, 5 ili niweze kufurahia […]

Zaburi 107

Kumsifu Mungu Kwa Wema Wake 1 MshukuruniBwana, kwa kuwa yeye ni mwema, upendo wake wadumu milele. 2 Waliokombolewa waBwanana waseme hivi, wale aliowaokoa kutoka katika mkono wa adui, 3 wale aliowakusanya kutoka nchi mbalimbali, kutoka mashariki na magharibi, kutoka kaskazini na kusini. 4 Baadhi yao walitangatanga jangwani, hawakuona njia ya kuwafikisha katika mji ambao wangeweza […]

Zaburi 108

Kuomba Msaada Dhidi Ya Adui (Zaburi Ya Daudi. Wimbo) 1 Ee Mungu, moyo wangu ni thabiti, nitaimba na kusifu kwa moyo wangu wote. 2 Amka, kinubi na zeze! Nitayaamsha mapambazuko. 3 EeBwana, nitakusifu katikati ya mataifa, nitaimba sifa zako katikati ya mataifa. 4 Kwa maana upendo wako ni mkuu, juu kuliko mbingu, uaminifu wako hufika […]

Zaburi 109

Lalamiko La Mtu Aliyeko Kwenye Shida (Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Daudi) 1 Ee Mungu, ambaye ninakusifu, usiwe kimya, 2 kwa maana watu waovu na wadanganyifu wamefungua vinywa vyao dhidi yangu; wasema dhidi yangu kwa ndimi za udanganyifu. 3 Wamenizunguka kwa maneno ya chuki, wananishambulia bila sababu. 4 Wanachonilipa badala ya urafiki wangu ni kunishtaki, lakini […]

Zaburi 110

Bwana Na Mfalme Wake Mteule (Zaburi Ya Daudi) 1 Bwanaamwambia Bwana wangu: “Keti mkono wangu wa kuume, mpaka nitakapowafanya adui zako kuwa mahali pa kuweka miguu yako.” 2 Bwanaataeneza fimbo yako ya utawala yenye nguvu kutoka Sayuni; utatawala katikati ya adui zako. 3 Askari wako watajitolea kwa moyo katika siku yako ya vita. Ukiwa umevikwa […]