Kuomba Msamaha (Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Daudi Baada Ya Kukemewa Na Nabii Nathani Kwa Kuzini Na Bathsheba) 1 Ee Mungu, unihurumie, kwa kadiri ya upendo wako usiokoma, kwa kadiri ya huruma yako kuu uyafute makosa yangu. 2 Unioshe na uovu wangu wote na unitakase dhambi yangu. 3 Kwa maana ninajua makosa yangu, na dhambi yangu […]
Category Archives: Zaburi
Zaburi 52
Hukumu Ya Mungu (Kwa Mwimbishaji: Utenzi Wa Daudi Baada Ya Doegi, Mwedomu, Kumwendea Sauli Na Kumjulisha Kuwa Daudi Amekwenda Nyumbani Kwa Abimeleki) 1 Ewe jitu, mbona unajivunia ubaya? Kwa nini unajivuna mchana kutwa, wewe ambaye ni fedheha mbele za Mungu? 2 Ulimi wako hupanga mashauri mabaya ya maangamizi, ni kama wembe mkali, ninyi mfanyao hila. […]
Zaburi 53
Uovu Wa Wanadamu (Kwa Mwimbishaji: Mtindo Wa Mahalathi. Utenzi Wa Daudi) 1 Mpumbavu anasema moyoni mwake, “Hakuna Mungu.” Wameharibika, na njia zao ni za uovu kabisa, hakuna hata mmoja atendaye mema. 2 Mungu huwachungulia wanadamu chini kutoka mbinguni aone kama wako wenye akili, wo wote wanaomtafuta Mungu. 3 Kila mmoja amegeukia mbali, wameharibika wote pamoja, […]
Zaburi 54
Kuomba Ulinzi Wa Mungu Kutokana Na Adui (Kwa Mwimbishaji Na Ala Za Nyuzi Za Uimbaji. Utenzi Wa Daudi Wakati Mtu Mmoja Wa Zifu Alipomwendea Sauli Na Kumjulisha Kuwa Daudi Amejificha Kwao) 1 Ee Mungu uniokoe kwa jina lako, unifanyie hukumu kwa uwezo wako. 2 Ee Mungu, sikia maombi yangu, usikilize maneno ya kinywa changu. 3 […]
Zaburi 55
Maombi Ya Mtu Aliyesalitiwa Na Rafiki (Kwa Mwimbishaji: Na Ala Za Uimbaji. Utenzi Wa Daudi) 1 Ee Mungu, sikiliza maombi yangu, wala usidharau hoja yangu, 2 nisikie na unijibu. Mawazo yangu yananisumbua na nimehangaishwa 3 kwa sauti ya adui, kwa kukaziwa macho na waovu, kwa sababu wananiletea mateso juu yangu na kunitukana kwa hasira zao. […]
Zaburi 56
Kumtumaini Mungu (Kwa Mwimbishaji: Mtindo Wa Njiwa Mkimya Wa Mbali. Utenzi Wa Daudi Baada Ya Kukamatwa Na Wafilisti Huko Gathi) 1 Ee Mungu unihurumie, maana watu wananifuatia vikali; mchana kutwa wanazidisha mashambulizi yao. 2 Wasingiziaji wangu wananifuatia mchana kutwa, wengi wananishambulia kwa kiburi chao. 3 Wakati ninapoogopa, nitakutumaini wewe. 4 Katika Mungu, ambaye neno lake […]
Zaburi 57
Kuomba Msaada (Kwa Mwimbishaji: Mtindo Wa Usiharibu! Utenzi Wa Daudi Baada Ya Kumponyoka Sauli Pangoni) 1 Unihurumie, Ee Mungu, unihurumie, kwa maana nafsi yangu inakukimbilia. Chini ya uvuli wa mbawa zako nitakimbilia mpaka maafa yapite. 2 Namlilia Mungu Aliye Juu Sana, Mungu atimizaye makusudi yake kwangu. 3 Hutuma kutoka mbinguni na kuniokoa, akiwakemea wale wanaonifuatilia […]
Zaburi 58
Mungu Kuwaadhibu Waovu (Kwa Mwimbishaji: Mtindo Wa Usiharibu! Utenzi Wa Daudi) 1 Enyi watawala, Je, kweli mwanena kwa haki? Je, mnahukumu kwa unyofu miongoni mwa watu? 2 La, mioyoni mwenu mnatunga udhalimu, na mikono yenu hupima jeuri duniani. 3 Waovu ni wapotovu hata tangu kuzaliwa kwao, toka tumboni mwa mama zao ni wakaidi na husema […]
Zaburi 59
Kuomba Ulinzi Wa Mungu (Kwa Mwimbishaji: Mtindo Wa Usiharibu. Utenzi Wa Daudi Wakati Sauli Alipotuma Wapelelezi Wamwue) 1 Ee Mungu, uniokoe na adui zangu, unilinde kutokana na hao wanaoinuka dhidi yangu. 2 Uniponye na watu watendao mabaya, uniokoe kutokana na wamwagao damu. 3 Tazama wanavyonivizia! Watu wakali wanajiunga pamoja kwa ubaya dhidi yangu, EeBwana, mimi […]
Zaburi 60
Kuomba Kuokolewa (Kwa Mwimbishaji: Mtindo Wa Shushani Eduthi. Utenzi Wa Daudi Wa Kufundisha Wakati Alipopigana Na Waaramu Kutoka Aramu-Naharaimu Na Aramu-Soba, Yoabu Aliporudi Nyuma Na Kuwaua Waedomu 12,000 Katika Bonde La Chumvi) 1 Ee Mungu, umetukataa na kutokea ghafula juu yetu, umekasirika, sasa uturejeshe upya! 2 Umetetemesha nchi na kuipasua; uiponye na kutengeneza mavunjiko yake, […]