Kuomba Ulinzi (Kwa Mwimbishaji: Kwa Ala Za Nyuzi Za Uimbaji. Zaburi Ya Daudi) 1 Ee Mungu, sikia kilio changu, usikilize maombi yangu. 2 Kutoka miisho ya dunia ninakuita, ninaita huku moyo wangu unadhoofika; uniongoze kwenye mwamba ule ulio juu kuliko mimi. 3 Kwa kuwa umekuwa kimbilio langu, ngome imara dhidi ya adui. 4 Natamani kukaa […]
Category Archives: Zaburi
Zaburi 62
Mungu Kimbilio La Pekee (Kwa Mwimbishaji: Mtindo Wa Yeduthuni. Zaburi Ya Daudi) 1 Kwa Mungu peke yake nafsi yangu inapata pumziko; wokovu wangu watoka kwake. 2 Yeye peke yake ndiye mwamba wangu na wokovu wangu; yeye ni ngome yangu, sitatikisika kamwe. 3 Mtamshambulia mtu hata lini? Je, ninyi nyote mtamtupa chini, ukuta huu ulioinama na […]
Zaburi 63
Shauku Kwa Ajili Ya Uwepo Wa Mungu (Zaburi Ya Daudi Wakati Alipokuwa Katika Jangwa La Yuda) 1 Ee Mungu, wewe ni Mungu wangu, nakutafuta kwa moyo wote; nafsi yangu inakuonea kiu, mwili wangu unakuonea wewe shauku, katika nchi kame na iliyochoka mahali ambapo hapana maji. 2 Nimekuona katika mahali patakatifu na kuuona uwezo wako na […]
Zaburi 64
Kuomba Ulinzi Dhidi Ya Maadui (Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Daudi) 1 Ee Mungu, unisikie, ninapoeleza lalamiko langu, uyahifadhi maisha yangu kutokana na vitisho vya adui. 2 Unifiche kutokana na shauri la siri la waovu, kutokana na zile kelele za kundi la watenda mabaya. 3 Wanaonoa ndimi zao kama panga na kuelekeza maneno yao kama mishale […]
Zaburi 65
Kusifu Na Kushukuru (Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Daudi. Wimbo) 1 Ee Mungu, sifa zakungojea katika Sayuni; kwako wewe nadhiri zetu zitatimizwa. 2 Ee wewe usikiaye maombi, kwako wewe watu wote watakuja. 3 Tulipokuwa tumefunikwa kabisa na dhambi, wewe ulisamehe makosa yetu. 4 Heri wale uliowachagua na kuwaleta karibu ili waishi katika nyua zako! Tunashibishwa kwa […]
Zaburi 66
Kusifu Mungu Kwa Ajili Ya Wema Wake (Kwa Mwimbishaji: Wimbo. Zaburi) 1 Mpigieni Mungu kelele za shangwe, dunia yote! 2 Imbeni utukufu wa jina lake; mpeni sifa zake kwa utukufu! 3 Mwambieni Mungu, “Jinsi gani yalivyo ya kutisha matendo yako! Uwezo wako ni mkuu mno kiasi kwamba adui wananyenyekea mbele zako. 4 Dunia yote yakusujudia, […]
Zaburi 67
Mataifa Yahimizwa Kumsifu Mungu (Kwa Mwimbishaji: Na Ala Za Nyuzi Za Muziki. Zaburi. Wimbo) 1 Mungu uturehemu na kutubariki, na kutuangazia nuru za uso wako, 2 ili njia zako zijulikane duniani, wokovu wako katikati ya mataifa yote. 3 Ee Mungu, mataifa na wakusifu, mataifa yote na wakusifu. 4 Mataifa yote na wafurahi na kuimba kwa […]
Zaburi 68
Wimbo Wa Taifa Wa Shangwe Kwa Ushindi (Kwa Mwimbishaji: Zaburi ya Daudi. Wimbo) 1 Mungu na ainuke, watesi wake na watawanyike, adui zake na wakimbie mbele zake. 2 Kama vile moshi upeperushwavyo na upepo, vivyo hivyo uwapeperushe mbali, kama vile nta iyeyukavyo kwenye moto, vivyo hivyo waovu na waangamie mbele za Mungu. 3 Bali wenye […]
Zaburi 69
Kilio Cha Kuomba Msaada Wakati Wa Dhiki (Kwa Mwimbishaji: Mtindo wa Yungiyungi. Zaburi ya Daudi) 1 Ee Mungu, uniokoe, kwa maana maji yamenifika shingoni. 2 Ninazama kwenye vilindi vya matope, pasipo mahali pa kukanyaga; nimefika kwenye maji makuu, mafuriko yamenigharikisha. 3 Nimechoka kwa kuomba msaada, koo langu limekauka. Macho yangu yanafifia, nikimtafuta Mungu wangu. 4 […]
Zaburi 70
Kuomba Msaada (Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Daudi. Maombolezo) 1 Ee Mungu, ufanye haraka kuniokoa, EeBwana, njoo hima unisaidie. 2 Waaibike na kufedheheshwa wale wanaotafuta uhai wangu; wale wanaotamani kuangamizwa kwangu warudishwe nyuma kwa aibu. 3 Wale waniambiao, “Aha! Aha!” warudi nyuma kwa sababu ya aibu yao. 4 Lakini wote wakutafutao na washangilie na kukufurahia, wale […]