Zaburi 71

Kuomba Ulinzi Na Msaada Siku Zote Za Maisha 1 EeBwana, nimekukimbilia wewe, usiniache nikaaibika kamwe. 2 Kwa haki yako uniponye na kuniokoa, unitegee sikio lako uniokoe. 3 Uwe mwamba wa kimbilio langu, mahali nitakapokimbilia kila wakati; toa amri ya kuniokoa, kwa kuwa wewe ni mwamba wangu na ngome yangu. 4 Ee Mungu wangu uniokoe kutoka […]

Zaburi 72

Maombi Kwa Ajili Ya Mfalme (Zaburi Ya Solomoni) 1 Ee Mungu, mjalie mfalme aamue kwa haki yako, mwana wa kifalme kwa haki yako. 2 Atawaamua watu wako kwa haki, watu wako walioonewa kwa haki. 3 Milima italeta mafanikio kwa watu, vilima tunda la haki. 4 Atawatetea walioonewa miongoni mwa watu na atawaokoa watoto wa wahitaji, […]

Zaburi 73

Haki Ya Mungu (Zaburi Ya Asafu) 1 Hakika Mungu ni mwema kwa Israeli, kwa wale ambao mioyo yao ni safi. 2 Bali kwangu mimi, miguu yangu ilikuwa karibu kuteleza; nilikuwa karibu mguu wangu kuachia uliposimama. 3 Kwa maana niliwaonea wivu wenye kujivuna nilipoona kufanikiwa kwa waovu. 4 Wao hawana taabu, miili yao ina afya na […]

Zaburi 74

Maombi Kwa Ajili Ya Taifa Kuokolewa (Utenzi Wa Asafu) 1 Ee Mungu, mbona umetukataa milele? Mbona hasira yako inawaka na kutoka moshi juu ya kondoo wa malisho yako? 2 Kumbuka watu uliowanunua zamani, kabila la urithi wako, ambao uliwakomboa: Mlima Sayuni, ambamo uliishi. 3 Geuza hatua zako kuelekea magofu haya ya kudumu, uharibifu wote huu […]

Zaburi 75

Mungu Ni Mwamuzi (Kwa Mwimbishaji: Kwa Ala Za Uimbaji Za Nyuzi. Zaburi Ya Asafu. Wimbo) 1 Ee Mungu, tunakushukuru, tunakushukuru wewe, kwa kuwa jina lako li karibu; watu husimulia matendo yako ya ajabu. 2 Unasema, “Ninachagua wakati maalum; ni mimi nihukumuye kwa haki. 3 Wakati dunia na watu wake wote inapotetemeka, ni mimi ninayezishikilia nguzo […]

Zaburi 76

Mungu Wa Israeli Ni Mhukumu Wa Dunia Yote (Kwa Mwimbishaji: Kwa Ala Za Nyuzi Za Muziki. Zaburi Ya Asafu. Wimbo) 1 Katika Yuda Mungu anajulikana, jina lake ni kuu katika Israeli. 2 Hema lake liko Salemu, makao yake katika Sayuni. 3 Huko alivunja mishale imetametayo, ngao na panga, silaha za vita. 4 Wewe unang’aa kwa […]

Zaburi 77

Matendo Makuu Ya Mungu Yanakumbukwa (Kwa Mwimbishaji: Mtindo Wa Yeduthuni. Zaburi Ya Asafu) 1 Nilimlilia Mungu ili anisaidie, nilimlilia Mungu ili anisikie. 2 Nilipokuwa katika taabu, nilimtafuta Bwana, usiku nilinyosha mikono bila kuchoka na nafsi yangu ilikataa kufarijiwa. 3 Ee Mungu, nilikukumbuka wewe, nililia kwa huzuni; nikatafakari, roho yangu ikadhoofika. 4 Ulizuia macho yangu kufumba; […]

Zaburi 78

Mungu Na Watu Wake (Utenzi Wa Asafu) 1 Enyi watu wangu, sikieni mafundisho yangu, sikilizeni maneno ya kinywa changu. 2 Nitafumbua kinywa changu kwa mafumbo, nitazungumza mambo yaliyofichika, mambo ya kale: 3 yale ambayo tuliyasikia na kuyajua, yale ambayo baba zetu walituambia. 4 Hatutayaficha kwa watoto wao; tutakiambia kizazi kijacho matendo yastahiliyo sifa yaBwana, uweza […]

Zaburi 79

Maombi Kwa Ajili Ya Wokovu Wa Taifa (Zaburi Ya Asafu) 1 Ee Mungu, mataifa yameuvamia urithi wako, wamelinajisi Hekalu lako takatifu, wameifanya Yerusalemu kuwa magofu. 2 Wametoa maiti za watumishi kuwa chakula cha ndege wa angani na nyama ya watakatifu wako kwa wanyama wa nchi. 3 Wamemwaga damu kama maji kuzunguka Yerusalemu yote, wala hakuna […]

Zaburi 80

Maombi Kwa Ajili Ya Kuponywa Kwa Taifa (Kwa Mwimbishaji: Mtindo Wa Yungiyungi. Zaburi Ya Asafu) 1 Ee Mchungaji wa Israeli tusikie, wewe umwongozaye Yosefu kama kundi; wewe uketiye katika kiti cha enzi katikati ya makerubi, angaza 2 mbele ya Efraimu, Benyamini na Manase. Uamshe nguvu zako, uje utuokoe. 3 Ee Mungu, uturejeshe, utuangazie uso wako, […]