Yoshua 13

Sehemu Za Kanaani Ambazo Hazijatwaliwa

1 Yoshua alipokuwa mzee na umri wake ukiwa umesogea sana,Bwanaakamwambia, “Wewe ni mzee sana, na bado kumesalia sehemu kubwa sana za nchi ambazo ni za kutwaliwa.

2 “Haya ndiyo maeneo ambayo bado hayajatekwa: maeneo yote ya Wafilisti na Wageshuri:

3 Eneo hili linaanzia Mto Shihori ulioko mashariki mwa Misri, kuelekea kaskazini kwenye mpaka wa Ekroni, ambayo yote ilihesabiwa kuwa ya Wakanaani (ambako kuna miji mitano ya watawala wa Kifilisti, ambayo ni Gaza, Ashdodi, Ashkeloni, Gathi na Ekroni: ndiyo nchi ya Waavi);

4 kuanzia upande wa kusini, eneo lote la Wakanaani, kuanzia Ara ambayo ni ya Wasidoni, ikienea hadi Afeki, na nchi ya Waamori,

5 eneo la Wagebali; na sehemu yote ya Lebanoni kuelekea mashariki, kuanzia Baal-Gadi chini ya Mlima Hermoni hadi Lebo-Hamathi.

6 “Nayo nchi yote ya vilima kuanzia Lebanoni hadi Misrefoth-Maimu, pamoja na eneo lote la Wasidoni, mimi mwenyewe nitawafukuza watoke mbele ya Waisraeli, hakikisha umeligawa eneo hili kwa Israeli kuwa urithi, kama nilivyokuamuru,

7 sasa basi, ligawanye eneo hili kwa yale makabila tisa na ile nusu ya kabila la Manase kuwa urithi.”

Mgawanyo Wa Nchi Mashariki Ya Yordani

8 Ile nusu nyingine ya kabila la Manase, Wareubeni na Wagadi, wao walishapokea urithi Mose aliokuwa amewapa mashariki ya Yordani, sawasawa na mtumishi waBwanaalivyowagawia.

9 Eneo lao lilienea toka Aroeri, iliyoko ukingoni mwa Bonde la Arnoni kuanzia mji ulio katikati ya bonde, ikijumuisha nchi ya uwanda wa juu wote wa Medeba mpaka Diboni,

10 nayo miji yote ya Sihoni mfalme wa Waamori, aliyetawala Heshboni, hadi mpakani mwa Waamori.

11 Vile vile ilijumuisha Gileadi, nchi ya Wageshuri na Wamaaka, mlima wote wa Hermoni na Bashani yote hadi Saleka,

12 yaani ufalme wote wa Ogu katika Bashani, waliokuwa wametawala katika Ashtarothi na Edrei ambao ndio mabaki ya Warefai. Mose alikuwa amewashinda na kuteka nchi yao.

13 Lakini Waisraeli hawakuwafukuza watu wa Geshuri na wa Maaka, kwa hiyo wanaendelea kuishi miongoni mwa Waisraeli mpaka leo hii.

14 Lakini kabila la Lawi, Mose hakuwapa urithi, kwa kuwa sadaka za kuteketezwa kwa moto zilizotolewa kwaBwana, Mungu wa Israeli, ndizo zilizokuwa urithi wao, kama alivyowaahidi.

15 Haya ndiyo maeneo ambayo Mose alikuwa amewapa kabila la Reubeni ukoo kwa ukoo:

16 Kuanzia nchi ya Aroeri iliyo ukingoni mwa Bonde la Aroni, na kuanzia mji ulio katikati ya bonde, pia uwanda wote wa juu kupita Madeba

17 mpaka Heshboni na miji yake yote kwenye uwanda wa juu, ikiwa ni pamoja na Diboni, Bamoth-Baali, Beth-Baal-Meoni,

18 Yahasa, Kedemothi, Mefaathi,

19 Kiriathaimu, Sibma, Sereth-Shahari juu ya kilima kilicho katika bonde,

20 Beth-Peori, matelemko ya Pisga na Beth-Yeshimothi:

21 miji yote ya uwanda wa juu na eneo lote la utawala wa Sihoni mfalme wa Waamori, aliyetawala Heshboni. Mose alikuwa amemshinda Sihoni, pia watawala wakuu wa Wamidiani, ambao ni Evi, Rekemu, Suri, Huri na Reba, waliokuwa wameungana na Sihoni, ambao waliishi katika nchi ile.

22 Pamoja na wale waliouawa katika vita, Waisraeli walikuwa wamemwua kwa upanga Balaamu mwana wa Beori aliyekuwa nabii.

23 Mpaka wa Wareubeni ulikuwa ni ukingo wa Mto Yordani. Miji hii ndiyo iliyokuwa urithi wa Wareubeni ukoo kwa ukoo.

24 Haya ndiyo maeneo ambayo Mose alikuwa amewagawia kabila la Gadi, ukoo kwa ukoo:

25 Nchi ya Yazeri, miji yote ya Gileadi na nusu ya nchi ya Amoni mpaka Aroeri, karibu na Raba;

26 kuanzia Heshboni mpaka Ramath-Mizpa na Betonimu, tena kutoka Mahanaimu hadi nchi ya Debiri;

27 tena katika bonde, Beth-Haramu, Beth-Nimra, Sukothi na Safoni na sehemu iliyobaki ya eneo la utawala wa Sihoni mfalme wa Heshboni (upande wa mashariki wa Mto Yordani, nchi inayoishia kwenye Bahari ya Kinerethi).

28 Miji hii na vijiji vyake vilikuwa urithi wa kabila la Gadi ukoo kwa ukoo.

29 Haya ndiyo maeneo ambayo Mose alikuwa amewapa hiyo nusu ya kabila la Manase, yaani kwa nusu ya jamaa ya uzao wa Manase, ukoo kwa ukoo:

30 Nchi iliyoenea kuanzia Mahanaimu, pamoja na Bashani yote, ufalme wote wa Ogu mfalme wa Bashani, makazi yote ya Yairi huko Bashani, miji sitini,

31 nusu ya Gileadi, Ashtarothi na Edrei (miji ya kifalme ya Ogu katika Bashani). Hii ilikuwa kwa ajili ya wazao wa Makiri mwana wa Manase, kwa ajili ya nusu ya wana wa Makiri, ukoo kwa ukoo.

32 Huu ndio urithi alioutoa Mose wakati alipokuwa katika tambarare za Moabu, ng’ambo ya Yordani mashariki ya Yeriko.

33 Lakini kwa kabila la Walawi, Mose hakuwapa urithi;BwanaMungu, Mungu wa Israeli ndiye urithi wao, kama alivyowaahidi.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOS/13-b8e513113b2dafec03164a2e19db157f.mp3?version_id=1627—

Yoshua 14

Mgawanyo Wa Nchi Magharibi Mwa Yordani

1 Basi haya ndiyo maeneo Waisraeli waliyopokea kama urithi katika nchi ya Kanaani, ambayo kuhani Eleazari, Yoshua mwana wa Nuni na viongozi wa koo za kabila za Israeli waliwagawia.

2 Urithi wao uligawanywa kwa kura kwa yale makabila tisa na nusu, kamaBwanaalivyomwagiza Mose.

3 Mose alikuwa amewapa yale makabila mawili na nusu urithi wao upande wa mashariki ya Yordani, lakini Walawi hawakupewa urithi miongoni mwa hao wengine,

4 kwa kuwa wana wa Yosefu walikuwa makabila mawili, Manase na Efraimu. Walawi hawakupata mgawo wa ardhi, bali walipewa miji tu kwa ajili ya kuishi, pamoja na maeneo ya malisho kwa ajili ya makundi yao ya kondoo, mbuzi na ng’ombe.

5 Kwa hiyo Waisraeli wakagawana ile nchi, kama vileBwanaalivyomwagiza Mose.

Kalebu Anapewa Mji Wa Hebroni

6 Kisha watu wa Yuda wakamwendea Yoshua huko Gilgali, naye Kalebu mwana wa Yefune, Mkenizi, akawaambia, “Unajua jambo ambaloBwanaalimwambia Mose mtu wa Mungu huko Kadesh-Barnea kukuhusu wewe na mimi.

7 Nilikuwa na umri wa miaka arobaini, wakati Mose mtumishi waBwana, aliponituma kutoka Kadesh-Barnea kuipeleleza hiyo nchi. Nami nikamletea taarifa kama kulingana na nilivyosadiki moyoni.

8 Lakini wenzangu tuliopanda nao waliifanya mioyo ya watu iyeyuke kwa hofu. Bali mimi, nilimfuataBwanaMungu wangu kwa moyo wote.

9 Hivyo siku ile Mose akaniapia, ‘Nchi ambayo umeikanyaga kwa miguu yako itakuwa urithi wako na wa watoto wako milele, kwa sababu umemfuataBwanaMungu wangu kwa moyo wote.’

10 “Sasa basi, kama vileBwanaalivyoahidi, ameniweka hai kwa miaka arobaini na mitano tangu wakati alipomwambia Mose jambo hili, wakati Waisraeli wakiwa wanazunguka jangwani. Hivyo mimi hapa leo, nina umri wa miaka themanini na mitano!

11 Bado ninazo nguvu kama siku ile Mose aliponituma. Bado ninazo nguvu za kwenda vitani sasa kama vile nilivyokuwa wakati ule.

12 Basi nipe nchi hii ya kilima, ambayoBwanaaliniahidi siku ile. Wewe mwenyewe ulisikia wakati ule kwamba Waanaki walikuwako huko na miji yao ilikuwa mikubwa na yenye maboma, lakini, kwa msaada waBwana, nitawafukuza watoke huko kama vile alivyonena.”

13 Ndipo Yoshua akambariki Kalebu mwana wa Yefune, naye akampa Hebroni kuwa urithi wake.

14 Hivyo Hebroni ikawa mali ya Kalebu mwana wa Yefune, Mkenizi tangu wakati ule, kwa sababu alimwandamaBwana, Mungu wa Israeli, kwa moyo wote.

15 (Hebroni uliitwa Kiriath-Arba hapo mwanzo, kutokana na huyo Arba ambaye alikuwa mtu mkuu kupita wote miongoni mwa Waanaki.)

Kisha nchi ikawa na amani bila vita.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOS/14-5c30e7dda61437aa5e4ce45651021cfa.mp3?version_id=1627—

Yoshua 15

Mgawo Kwa Yuda

1 Mgawo kwa kabila la Yuda, ukoo kwa ukoo, ulishuka kufikia nchi ya Edomu, hadi Jangwa la Sini mwisho kabisa upande wa kusini.

2 Mpaka wao wa kusini ulianzia kwenye ghuba iliyoko kwenye ncha ya kusini mwa Bahari ya Chumvi,

3 ukakatiza kusini mwa Akrabimu, ukaendelea hadi Sini ukaenda hadi kusini mwa Kadesh-Barnea. Tena ukapitia Hesroni ukapanda hadi Adari na ukapinda hadi Karka.

4 Kisha ukaendelea mpaka Azmoni na kuunganika na Mto wa Misri, na kuishia baharini. Huu ndio mpaka wao wa upande wa kusini.

5 Mpaka wa upande wa mashariki ni Bahari ya Chumvi hadi mahali Mto Yordani unapoingilia.

Mpaka wa kaskazini ulianzia penye ghuba ya bahari mahali Mto Yordani unapoingilia,

6 ukapanda hadi Beth-Hogla, na kuendelea kaskazini mwa Beth-Araba hadi kwenye jiwe la Bohani mwana wa Reubeni.

7 Kisha mpaka ulipanda hadi Debiri kutoka Bonde la Ahori na kugeuka kaskazini hadi Gilgali inayotazamana na matelemko ya Adumimu, kusini mwa bonde. Ukaendelea hadi maji ya En-Shemeshi na kutokeza huko En-Rogeli.

8 Kisha ukapanda kwa kufuata Bonde la Ben-Hinomu sambamba na mtelemko wa kusini wa mji wa Wayebusi (yaani Yerusalemu). Kutoka hapo ukapanda juu ya kilima magharibi ya Bonde la Hinomu mwisho wa ncha ya kaskazini ya Bonde la Warefai.

9 Kutoka juu ya kilima mpaka ukaendelea hadi kwenye chemchemi ya maji ya Neftoa, ukatokea kwenye miji ya Mlima Efroni na kutelemka kuelekea Baala (yaani Kiriath-Yearimu).

10 Kisha ukapinda upande wa magharibi kutoka Baala hadi Mlima Seiri ukafuatia mtelemko wa kaskazini wa Mlima Yearimu (yaani Kesaloni), ukaendelea chini hadi Beth-Shemeshi na kukatiza hadi Timna.

11 Ukaelekea hadi kwenye mtelemko wa kaskazini wa Ekroni, ukageuka kuelekea Shikeroni, ukapita hadi Mlima Baala na kufika Yabneeli. Mpaka ukaishia baharini.

12 Mpaka wa magharibi ni pwani ya Bahari Kuu.

Hii ndiyo iliyokuwa mipaka ya watu wa Yuda kwa koo zao.

Nchi Aliyopewa Kalebu

13 Kwa kufuata maagizo yaBwanakwake, Yoshua alimpa Kalebu mwana wa Yefune sehemu katika Yuda: Kiriath-Arba, yaani Hebroni (Arba alikuwa baba wa Anaki).

14 Kutoka Hebroni Kalebu alifukuza hao wana watatu wa Anaki, nao ni Sheshai, Ahimani na Talmai, wazao wa Anaki.

15 Kutoka hapo akaondoka kupigana dhidi ya watu waishio Debiri (jina la Debiri hapo kwanza iliitwa Kiriath-Seferi).

16 Kalebu akasema, “Nitamwoza binti yangu Aksa kwa mtu atakayeweza kupigana na kuteka Kiriath-Seferi.”

17 Basi Othnieli mwana wa Kenazi, ndugu yake Kalebu, akauteka; hivyo Kalebu akamtoa Aksa binti yake aolewe naye.

18 Siku moja baada ya yule mwanamke kuolewa na Othnieli, alimsihi amwombe Kalebu baba yake shamba. Aliposhuka kutoka juu ya punda wake, Kalebu akamwuliza, “Wataka nikufanyie nini?”

19 Akamjibu, “Nifanyie jambo moja la hisani. Kwa kuwa umenipa shamba lililoko huko Negebu, nipe pia chemchemi za maji.” Basi Kalebu akampa Aksa binti yake chemchemi za juu na za chini.

Miji Ya Yuda

20 Huu ndio urithi wa kabila la Yuda, ukoo kwa ukoo:

21 Miji ya kusini kabisa ya kabila la Yuda katika Negebu kuelekea mpaka wa Edomu ilikuwa:

Kabseeli, Ederi, Yaguri,

22 Kina, Dimona, Adada,

23 Kedeshi, Hazori, Ithnani,

24 Zifu, Telemu, Bealothi,

25 Hazor-Hadata, Kerioth-Hesroni (yaani Hazori),

26 Amamu, Shema, Molada,

27 Hasar-Gada, Heshmoni, Beth-Peleti,

28 Hasar-Shuali, Beer-Sheba, Biziothia,

29 Baala, Iyimu, Esemu,

30 Eltoladi, Kesili, Horma,

31 Siklagi, Madmana, Sansana,

32 Lebaothi, Shilhimu, Aini na Rimoni; hiyo yote ni miji ishirini na tisa, pamoja na vijiji vyake.

33 Upande wa magharibi chini ya vilima:

Eshtaoli, Sora, Ashna,

34 Zanoa, En-Ganimu, Tapua, Enamu,

35 Yarmuthi, Adulamu, Soko, Azeka,

36 Shaaraimu, Adithaimu na Gedera (au Gederothaimu); yote ni miji kumi na minne, pamoja na vijiji vyake.

37 Senani, Hadasha, Migdal-Gadi,

38 Dileani, Mispa, Yoktheeli,

39 Lakishi, Boskathi, Egloni,

40 Kaboni, Lahmasi, Kitlishi,

41 Gederothi, Beth-Dagoni, Naama na Makeda; yote ni miji kumi na sita pamoja na vijiji vyake.

42 Libna, Etheri, Ashani,

43 Yifta, Ashna, Nesibu,

44 Keila, Akzibu na Maresha; yote ni miji tisa pamoja na vijiji vyake.

45 Ekroni, pamoja na viunga vyake na vijiji vyake;

46 magharibi ya Ekroni, maeneo yote yaliyokuwa karibu na Ashdodi, pamoja na vijiji vyake;

47 Ashdodi, miji yake na vijiji vyake na Gaza viunga vyake na vijiji vyake, hadi kufikia Mto wa Misri na Pwani ya Bahari Kuu.

48 Katika nchi ya vilima:

Shamiri, Yatiri, Soko,

49 Dana, Kiriath-Sana (yaani Debiri),

50 Anabu, Eshtamoa, Animu,

51 Gosheni, Holoni na Gilo; miji kumi na mmoja pamoja na vijiji vyake.

52 Arabu, Duma, Ashani,

53 Yanimu, Beth-Tapua, Afeka,

54 Humta, Kiriath-Arba (yaani Hebroni), na Siori; miji tisa pamoja na vijiji vyake.

55 Maoni, Karmeli, Zifu, Yuta,

56 Yezreeli, Yokdeamu, Zanoa,

57 Kaini, Gibea na Timna; miji kumi pamoja na vijiji vyake.

58 Halhuli, Beth-Zuri, Gedori,

59 Maarathi, Beth-Anothi na Eltekoni; miji sita pamoja na vijiji vyake.

60 Kiriath-Baali (yaani Kiriath-Yearimu) na Raba; miji miwili pamoja na vijiji vyake.

61 Huko jangwani:

Beth-Araba, Midini, Sekaka,

62 Nibshani, Mji wa Chumvi, na En-Gedi; miji sita pamoja na vijiji vyake.

63 Yuda hakuweza kuwafukuza Wayebusi, ambao walikuwa wakiishi Yerusalemu; hadi leo Wayebusi huishi huko pamoja na watu wa Yuda.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOS/15-fbac4cf1d47ad803a8f9eb62b5644fee.mp3?version_id=1627—

Yoshua 16

Mgawo Kwa Ajili Ya Efraimu Na Manase

1 Mgawanyo wa Yosefu ulianzia Yordani ya Yeriko, mashariki mwa miji ya Yeriko na kutoka hapo ulipanda kupitia jangwani na kuingia katika nchi ya vilima ya Betheli.

2 Ukaendelea kutoka Betheli (ndiyo Luzu), ukavuka kuingia nchi ya Waariki huko Atarothi,

3 ukatelemkia kuelekea magharibi hadi nchi ya Wayafleti mpaka sehemu ya Beth-Horoni ya Chini hadi Gezeri, ukiishia baharini.

4 Kwa hiyo Manase na Efraimu, wazao wa Yosefu, walipokea urithi wao.

5 Hii ndiyo iliyokuwa nchi ya Efraimu, ukoo kwa ukoo:

Mpaka wa urithi wao ulianzia Atarothi Adari upande wa mashariki hadi Beth-Horoni ya Juu,

6 na kuendelea mpaka baharini. Kutoka Mikmethathi upande wa kaskazini ulipinda kuelekea mashariki mpaka Taanath-Shilo, ukipitia Yanoa upande wa mashariki.

7 Kisha ulitelemkia kutoka Yanoa hadi Atarothi na Naara, ukagusa Yeriko na kutokea katika Mto Yordani.

8 Kutoka Tapua mpaka ulikwenda magharibi hadi Kijito cha Kana na kuishia baharini. Huu ulikuwa ndio urithi wa kabila la Waefraimu, ukoo kwa ukoo.

9 Pia ulijumuisha miji yote na vijiji vyake ambavyo vilitengwa kwa ajili ya Waefraimu ndani ya urithi wa kabila la Manase.

10 Hawakuwafukuza Wakanaani waishio Gezeri; mpaka leo Wakanaani wanaishi miongoni mwa watu wa Efraimu lakini wanatakiwa kufanya kazi ngumu za kulazimishwa.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOS/16-706763d0d49207b997fa5a4ed8490565.mp3?version_id=1627—

Yoshua 17

Mgawo Wa Nusu Nyingine Ya Manase Upande Wa Magharibi

1 Huu ndio mgawo wa kabila la Manase kama mzaliwa wa kwanza wa Yosefu, yaani kwa ajili ya Makiri, mzaliwa wa kwanza wa Manase. Makiri alikuwa baba wa Wagileadi, ambao walipokea Gileadi na Bashani kwa sababu Wamakiri walikuwa askari wakuu.

2 Kwa hiyo mgawo huu ulikuwa kwa ajili ya watu wa Manase waliokuwa wamebaki, ambao ni koo za Abiezeri, Heleki, Asrieli, Shekemu, Heferi na Shemida. Hawa ndio wanaume wengine wa uzao wa Manase mwana wa Yosefu kwa koo zao.

3 Basi Selofehadi mwana wa Heferi, mwana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase hakuwa na wana waume ila binti tu, ambao majina yao ni Mala, Noa, Hogla, Milka na Tirsa.

4 Wakawaendea kuhani Eleazari, Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi, wakasema: “Bwanaalimwagiza Mose atupatie urithi miongoni mwa ndugu zetu.” Kwa hiyo Yoshua akawapa urithi pamoja na ndugu wa baba yao, kufuatana na agizo laBwana.

5 Fungu la Manase lilikuwa na sehemu kumi za nchi, licha ya Gileadi na Bashani mashariki mwa Yordani,

6 kwa sababu wale binti za kabila la Manase walipokea urithi miongoni mwa ndugu zao. Nchi ya Gileadi ilikuwa mali ya wale wazao wengine wa Manase waliobaki.

7 Nchi ya Manase ilienea kuanzia Asheri hadi Mikmeta mashariki mwa Shekemu. Mpaka ulielekea upande wa kusini kutoka pale ukajumuisha watu wanaoishi En-Tapua.

8 (Nchi ya Tapua ilikuwa mali ya Manase, lakini Tapua yenyewe iliyo mpakani mwa nchi ya Manase ilikuwa ya Waefraimu.)

9 Kisha mpaka uliendelea kuelekea kusini hadi Kijito cha Kana. Kulikuwepo miji ya Efraimu iliyokuwa miongoni mwa miji ya Manase, lakini mpaka wa Manase ulikuwa upande wa kaskazini wa kile kijito na kuishia kwenye baharia.

10 Nchi ya kusini mwa kile kijito ilikuwa ya Efraimu, na ile iliyokuwa upande wa kaskazini mwa kile kijito ilikuwa ya Manase. Nchi ya Manase ilienea hadi baharini na ikapakana na Asheri upande wa kaskazini, na kupakana na nchi ya Isakari upande wa mashariki.

11 Miji ifuatayo katika nchi ya Isakari na Asheri ilipewa Manase: Beth-Shani, Ibleamu na watu wa Dori, Endori, Taanaki na Megido, pamoja na vijiji vyote vinavyohusika na miji hiyo.

12 Lakini Wamanase hawakuweza kuimiliki miji hii, kwa kuwa Wakanaani waliendelea kuishi katika maeneo hayo.

13 Hata hivyo, Waisraeli walivyoendelea kupata nguvu waliwatumikisha Wakanaani na kuwatia katika kazi ngumu za kulazimisha, lakini hawakuwafukuza kutoka katika ile nchi.

Kabila La Yosefu Lakataa

14 Kabila la Yosefu wakamwambia Yoshua, “Kwa nini umetupa sisi mgawo mmoja tu na sehemu moja tu kuwa urithi? Sisi tu watu wengi sana, nayeBwanaametubariki kwa wingi.”

15 Yoshua akajibu, “Kama ninyi ni wengi sana, na kama nchi ya vilima ya Efraimu ni ndogo sana kwenu, pandeni msituni mkafyeke eneo kwa ajili yenu huko kwenye nchi ya Waperizi na Warefai.”

16 Kabila la Yosefu wakajibu, “Hiyo nchi ya vilima haitutoshi, nao Wakanaani wote wanaoishi katika tambarare wanayo magari ya chuma, wote wa Beth-Shani na miji yake, na wale walio katika Bonde la Yezreeli.”

17 Lakini Yoshua akanena na nyumba ya Yosefu, yaani Efraimu na Manase: “Ninyi ni wengi sana na wenye nguvu sana. Hamtakuwa na mgawo mmoja tu,

18 bali pia nchi hii ya kilima yenye msitu. Ifyekeni, nayo mipaka yake itakuwa yenu umbali mtakaoweza kufika. Ingawa Wakanaani wana magari ya chuma, nao wana nguvu, mwaweza kuwafukuza humo.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOS/17-08fd184471b7bfdaf688e5db5159549f.mp3?version_id=1627—

Yoshua 18

Mgawanyo Wa Nchi Iliyobaki

1 Kusanyiko lote la Waisraeli likakusanyika huko Shilo na kusimamisha Hema ya Mkutano. Nchi ikawa chini ya utawala wao,

2 lakini palikuwa bado makabila saba ya Israeli ambayo yalikuwa hayajapokea urithi wao.

3 Hivyo Yoshua akawaambia Waisraeli, “Je, mtasubiri hata lini ili kuingia kumiliki nchi ambayoBwana, Mungu wa baba zenu, amewapa?

4 Chagueni watu watatu kutoka kwenye kila kabila. Nitawatuma hao watu kukagua hiyo nchi ambayo bado haijatekwa, nao watanirudia wakiwa na taarifa ya mapendekezo ya mgawanyo wa urithi wa kila kabila.

5 Mtaigawanya hiyo nchi sehemu saba. Yuda atabaki katika nchi yake upande wa kusini na nyumba ya Yosefu katika nchi yake upande wa kaskazini.

6 Baada ya kuandika maelezo ya hizo sehemu saba za nchi, myalete kwangu, nami nitawagawia kwa kura mbele zaBwanaMungu wetu.

7 Hata hivyo, Walawi hawatakuwa na sehemu miongoni mwenu, maana huduma ya ukuhani kwaBwanandio urithi wao. Nao Gadi, Reubeni na nusu ya kabila la Manase wameshapata urithi wao upande wa mashariki mwa Yordani, ambako Mose mtumishi waBwanaaliwapa.”

8 Hivyo hao watu walipokuwa wanaondoka kwenda kuandika vizuri kuhusu hiyo nchi, Yoshua akawaagiza, “Nendeni mkakague hiyo nchi na mwandike maelezo yake. Kisha mrudi kwangu, nami nitawapigia kura hapa Shilo mbele zaBwana.”

9 Ndipo hao watu walipoondoka na kupita katika ile nchi yote. Wakaandika maelezo yake, mji kwa mji, katika sehemu saba kwenye kitabu na kurudisha taarifa kwa Yoshua huko kambini Shilo.

10 Basi Yoshua akapiga kura kwa ajili yao huko Shilo mbele zaBwana, akagawanya nchi kwa Waisraeli kwa kufuatana na mgawanyo wa kabila zao.

Mgawo Kwa Benyamini

11 Kura iliangukia kabila la Benyamini, ukoo kwa ukoo. Nchi yao waliyogawiwa ilikuwa kati ya kabila la Yuda na la Yosefu.

12 Upande wa kaskazini mpaka wao ulianzia Yordani, kupitia kaskazini ya mtelemko wa Yeriko na kuendelea magharibi kuingia katika nchi ya vilima, ukitokea kwenye jangwa la Beth-Aveni.

13 Kutoka hapo ulikatiza kwenye mtelemko wa kusini wa Luzu (yaani Betheli) na kushuka hadi Ataroth-Adari katika kilima kusini mwa Beth-Horoni ya chini.

14 Kutoka kilima kinachotazamana na Beth-Horoni upande wa kusini mpaka ulizunguka kusini kufuatia upande wa magharibi, ukatokezea Kiriath-Baali (yaani Kiriath-Yearimu), mji wa watu wa Yuda. Huu ndio uliokuwa upande wa magharibi.

15 Upande wa kusini mpaka ulianzia kwenye viunga vya Kiriath-Yearimu kwa upande wa magharibi, nao ukatokeza kwenye chemchemi ya maji ya Neftoa.

16 Mpaka ukatelemka hadi kwenye mwanzo wa mlima unaotazamana na Bonde la Ben-Hinomu, kaskazini ya Bonde la Warefai. Ukaendelea chini kwenye Bonde la Hinomu na kupitia mtelemko wa kusini wa mji wa Wayebusi na kisha hadi En-Rogeli.

17 Kisha ukapinda kuelekea kaskazini, ukaenda hadi En-Shemeshi na kuendelea mpaka Gelilothi, inayotazamana na Njia ya Adumimu, ukatelemka hadi kwenye Jiwe la Bohani mwana wa Reubeni.

18 Ukaendelea upande wa mtelemko wa kaskazini wa Beth-Araba ukatelemka hadi Araba.

19 Kisha ukaendelea mpaka kwenye mtelemko wa kaskazini wa Beth-Hogla na kujitokeza kwenye ghuba ya kaskazini ya Bahari ya Chumvi, kwenye maingilio ya Mto Yordani upande wa kusini. Huo ndio uliokuwa mpaka wa kusini.

20 Mto Yordani ulikuwa ndio mpaka wa upande wa mashariki.

Hii ilikuwa ndiyo mipaka iliyoonyesha urithi wa koo za Benyamini pande zote.

21 Kabila za Benyamini, ukoo kwa ukoo, zilikuwa na miji ifuatayo:

Yeriko, Beth-Hogla, Emeki-Kesisi,

22 Beth-Araba, Semaraimu, Betheli,

23 Avimu, Para na Ofra,

24 Kefar-Amoni, Ofni, na Geba; miji kumi na miwili pamoja na vijiji vyake.

25 Gibeoni, Rama na Beerothi,

26 Mispa, Kefira, Moza,

27 Rekemu, Irpeeli, Tarala,

28 Zela, Elefu, mji wa Wayebusi (yaani Yerusalemu), Gibea na Kiriathi; miji kumi na minne pamoja na vijiji vyake.

Huu ndio uliokuwa urithi wa Benyamini kwa ajili ya koo zake.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOS/18-ea1dcbd53a72ff19fa7387ac9f8880e1.mp3?version_id=1627—

Yoshua 19

Mgawo Kwa Simeoni

1 Kura ya pili ikaangukia kabila la Simeoni, ukoo kwa ukoo. Urithi wao ulikuwa ndani ya nchi ya Yuda.

2 Ulijumuisha:

Beer-Sheba (au Sheba), Molada,

3 Hasar-Shuali, Bala na Esemu,

4 Eltoladi, Bethuli, Horma,

5 Siklagi, Beth-Markabothi, Hazar-Susa,

6 Beth-Lebaothi na Sharuheni; hii ilikuwa miji kumi na mitatu pamoja na vijiji vyake.

7 Pia Aini, Rimoni, Etheri, na Ashani, hii ilikuwa miji minne na vijiji vyake,

8 pamoja na vijiji vyote vinavyoizunguka miji hii mpaka Baalath-Beeri (ambayo ndiyo Rama iliyo katika Negebu).

Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Simeoni ukoo kwa ukoo.

9 Urithi wa Wasimeoni ulitolewa kutoka katika fungu la Yuda, kwa kuwa fungu la Yuda lilikuwa kubwa kuliko walivyohitaji. Hivyo kabila la Simeoni lilipewa urithi wao ndani ya nchi ya Yuda.

Mgawo Kwa Wazabuloni

10 Nayo kura ya tatu ikaangukia kabila la Zabuloni, ukoo kwa ukoo:

Mpaka wa urithi wao uliendelea hadi Saridi.

11 Kuelekea upande wa magharibi ukafika Marala, ukagusa Dabeshethi, na kuendelea mpaka kijito cha maji karibu na Yokneamu.

12 Ukageuka mashariki kuanzia Saridi kuelekea maawio ya jua hadi kwenye nchi ya Kisiloth-Tabori na kwenda hadi Daberathi kupanda Jafia.

13 Kisha ukaendelea mashariki hadi Gath-Heferi na kufika Eth-Kasini, ukatokea Rimoni na kugeuka kuelekea Nea.

14 Huko mpaka ukazungukia upande wa kaskazini hadi Hanathoni na kuishia katika Bonde la Ifta-Eli.

15 Miji mingine ni Katathi, Nahalali, Shimroni, Idala na Bethlehemu. Kulikuwa na miji kumi na miwili pamoja na vijiji vyake.

16 Miji hii na vijiji vyake vilikuwa ndio urithi wa Zabuloni, ukoo kwa ukoo.

Mgawo Kwa Isakari

17 Kura ya nne ikamwangukia Isakari, ukoo kwa ukoo.

18 Nchi yao ilijumuisha:

Yezreeli, Kesulothi, Shunemu,

19 Hafaraimu, Shioni, Anaharathi,

20 Rabithi, Kishioni, Ebesi,

21 Remethi, En-Ganimu, En-Hada na Beth-Pasesi.

22 Mpaka ukagusa Tabori, Shahasuma na Beth-Shemeshi, na ukaishia kwenye Mto Yordani. Hii ilikuwa miji kumi na sita, pamoja na vijiji vyake.

23 Miji hii pamoja na vijiji vyake ilikuwa urithi wa kabila la Isakari, ukoo kwa ukoo.

Mgawo Kwa Asheri

24 Kura ya tano iliangukia kabila la Asheri, ukoo kwa ukoo.

25 Nchi yao ilijumuisha:

Miji ya Helkathi, Hali, Beteni, Akishafu,

26 Alameleki, Amadi na Mishali. Upande wa magharibi mpaka uligusa Karmeli na Shihor-Libnathi.

27 Tena ukageuka mashariki kuelekea Beth-Dagoni, ukagusa Zabuloni na Bonde la Ifta-Eli, ukaenda upande wa kaskazini hadi Beth-Emeki na Neyeli, ukipitia Kabul upande wa kushoto.

28 Ukaendelea hadi Abdoni, Rehobu, Hamoni na Kana, na kufika Sidoni Kuu.

29 Mpaka huo ukageukia nyuma kuelekea Rama na kwenda hadi kwenye mji wenye ngome wa Tiro, ukageuka kuelekea Hosa na kutokeza baharini katika nchi ya Akzibu,

30 Uma, Afeki na Rehobu. Ilikuwepo miji ishirini na miwili, pamoja na vijiji vyake.

31 Miji hii pamoja na vijiji vyake ilikuwa ndio urithi wa kabila la Asheri, ukoo kwa ukoo.

Mgawo Kwa Naftali

32 Kura ya sita iliangukia kabila la Naftali, ukoo kwa ukoo:

33 Mpaka wao uliendelea kutoka Helefi na kwenye mti mkubwa ulio katika Sananimu, ukipitia Adami-Nekebu na Yabineeli hadi Lakumu na kuishia katika Mto Yordani.

34 Mpaka ukaendelea magharibi kupitia Aznoth-Tabori na kutokea Hukoki. Ukagusa Zabuloni upande wa kusini, Asheri upande wa magharibi, na Yordani upande wa mashariki.

35 Miji yenye ngome ilikuwa Sidimu, Seri, Hamathi, Rakathi, Kinerethi,

36 Adama, Rama, Hazori,

37 Kedeshi, Edrei, na En-Hasori,

38 Ironi, Migdal-Eli, Horemu, Beth-Anathi na Beth-Shemeshi. Kulikuwa na miji kumi na tisa na vijiji vyake.

39 Miji hiyo pamoja na vijiji vyake ndio iliyokuwa urithi wa kabila la Naftali, ukoo kwa ukoo.

Mgawo Kwa Dani

40 Kura ya saba iliangukia kabila la Dani, ukoo kwa ukoo.

41 Nchi ya urithi wao ilijumuisha:

Sora, Eshtaoli, Ir-Shemeshi,

42 Shaalabini, Aiyaloni, Ithla,

43 Eloni, Timna, Ekroni,

44 Elteke, Gibethoni, Baalathi,

45 Yehudi, Bene-Beraki, Gath-Rimoni,

46 Me-Yarkoni na Rakoni, pamoja na eneo linalotazamana na Yafa.

47 (Lakini Wadani walipata shida kuimiliki nchi yao, kwa hiyo walipanda kuishambulia Leshemu, wakaitwaa, wakawaua watu wake kwa upanga na kuukalia. Walikaa Leshemu na kuuita Dani kufuatana na jina la baba yao.)

48 Miji hii na vijiji vyake ndio iliyokuwa urithi wa kabila la Dani, ukoo kwa ukoo.

Mgawo Kwa Yoshua

49 Walipomaliza kugawanya nchi katika migawo kulingana na sehemu zao zilizowaangukia, Waisraeli wakampa Yoshua mwana wa Nuni urithi katikati yao,

50 kama vileBwanaalivyokuwa ameamuru. Walimpa mji alioutaka, ambao ni Timnath-Seraulio katika nchi ya vilima ya Efraimu. Naye akajenga mji, akakaa huko.

51 Hizo ndizo nchi ambazo Eleazari kuhani, Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa koo za kabila za Israeli walizigawanya kwa kura huko Shilo mbele zaBwanapenye ingilio la Hema la Kukutania. Nao wakamaliza kazi ya kuigawanya hiyo nchi.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOS/19-a382a1f74d5d00631596cca7fbf30244.mp3?version_id=1627—

Yoshua 20

Miji Ya Makimbilio

1 NdipoBwanaakamwambia Yoshua,

2 “Waambie Waisraeli, watenge miji ya kukimbilia, kama nilivyokuamuru kupitia Mose,

3 ili mtu ye yote atakayemwua mtu kwa bahati mbaya na pasipokukusudia aweze kukimbilia huko na kujiepusha na mlipiza kisasi cha damu.

4 “Anapokimbilia mojawapo ya miji hii, atasimama kwenye maingilio ya lango la mji na kueleza wazee wa mji kuhusu shauri lake. Kisha watampokea katika mji wao na kumpa mahali pa kuishi nao.

5 Kama mlipiza kisasi cha damu akimfuatilia, wazee wa mji kamwe wasimkabidhi yule mshtakiwa, kwa sababu alimwua jirani yake bila kukusudia, na bila kuwa na nia ya kudhuru.

6 Huyu aliyeua atakaa kwenye mji huo mpaka awe amesimama kukabili mashtaka yake mbele ya kusanyiko na mpaka Kuhani Mkuu anayehudumu kwa wakati huo atakapokufa. Ndipo atakapoweza kurudi nyumbani kwake katika mji ambao aliukimbia.”

7 Basi wakatenga Kedeshi katika Galilaya kwenye nchi ya vilima ya Naftali, Shekemu katika nchi ya vilima ya Efraimu, na Kiriath-Arba (yaani Hebroni) kwenye nchi ya vilima ya Yuda.

8 Katika upande wa mashariki ya Yordani ya Yeriko wakatenga Bezeri katika jangwa katika uwanda wa juu katika kabila la Reubeni, Ramoth katika Gileadi katika kabila la Gadi, na Golani huko Bashani katika kabila la Manase.

9 Mwisraeli ye yote au mgeni ye yote aishiye miongoni mwao aliyemwua mtu kwa bahati mbaya, angeweza kukimbilia katika miji hiyo iliyotengwa na asiuawe na mwenye kulipiza kisasi cha damu kabla hajasimama kukabili mashtaka mbele ya kusanyiko.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOS/20-c7cceb20f5e46f9c32b9499b2e677e89.mp3?version_id=1627—

Yoshua 21

Miji Kwa Ajili Ya Walawi

1 Basi viongozi wa jamaa ya Walawi, wakamwendea kuhani Eleazari, Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa jamaa nyingine za makabila ya Israeli

2 huko Shilo katika Kanaani na kuwaambia, “Bwanaaliagiza kupitia Mose kuwa mtupe miji ya kuishi yenye sehemu za malisho kwa ajili ya mifugo yetu.”

3 Hivyo kama vileBwanaalivyoagiza, Waisraeli wakawapa Walawi miji ifuatayo pamoja na sehemu zake za malisho kutoka katika urithi wao wenyewe.

4 Kura ya kwanza ikatoka kwa ajili ya Wakohathi, ukoo kwa ukoo. Walawi waliokuwa wazao wa kuhani Aroni walipewa miji kumi na mitatu kutoka katika makabila ya Yuda, Simeoni na Benyamini.

5 Wazao wengine waliobaki wa Wakohathi walipewa miji kumi kutoka katika koo za makabila ya Efraimu, Dani na nusu ya Manase.

6 Wazao wa Gershoni walipewa kwa kura miji kumi na mitatu kutoka katika koo za makabila ya Isakari, Asheri, Naftali na nusu ya Manase huko Bashani.

7 Wazao wa Merari, ukoo kwa ukoo, walipewa miji kumi na miwili kutoka katika makabila ya Reubeni, Gadi na Zabuloni.

8 Kwa hiyo Waisraeli wakawapa Walawi miji hii pamoja na sehemu zake za malisho, kama vileBwanaalivyokuwa ameagiza kupitia kwa Mose.

9 Kutoka katika makabila ya Yuda na Simeoni waligawa miji ifuatayo kwa majina

10 (miji hii walipewa wazao wa Aroni ambao walitokana na koo za Wakohathi za Walawi, kwa sababu fungu la kwanza liliwaangukia):

11 Waliwapa Kiriath-Arba (yaani Hebroni), pamoja na sehemu zake za malisho zilizoizunguka, katika nchi ya vilima ya Yuda. (Arba alikuwa baba wa Anaki.)

12 Lakini mashamba na vijiji vilivyozunguka mji walikuwa wamempa Kalebu mwana wa Yefune kuwa milki yake.

13 Kwa hiyo wazao wa kuhani Aroni wakapewa Hebroni (mji wa makimbilio kwa ajili ya ye yote aliyeshtakiwa kwa mauaji), Libna,

14 Yatiri, Eshtemoa,

15 Holoni, Debiri,

16 Aini, Yuta na Beth-Shemeshi; kwa jumla ilikuwa miji tisa pamoja na sehemu zake za malisho kutoka kwa makabila haya mawili.

17 Kutoka katika kabila la Benyamini wakawapa Gibeoni, Geba,

18 Anathothi na Almoni; miji yote minne pamoja na sehemu zake za malisho.

19 Miji yote waliyopewa makuhani, wazao wa Aroni, ilikuwa jumla kumi na mitatu, pamoja na sehemu zake za malisho.

20 Koo nyingine za Wakohathi, ambao pia ni Walawi, walipewa miji kutoka katika kabila la Efraimu:

21 Katika nchi ya vilima ya Efraimu walipewa Shekemu (mji wa makimbilio kwa ajili ya ye yote anayeshtakiwa kwa mauaji) na Gezeri,

22 Kibsaimu na Beth-Horoni, pamoja na sehemu zake za malisho; yote ilikuwa miji minne.

23 Pia kutoka kabila la Dani wakapokea Elteke, Gibethoni,

24 Aiyaloni na Gath-Rimoni; yote miji minne pamoja na sehemu zake za malisho.

25 Kutoka katika nusu ya kabila la Manase, wakapokea Taanaki na Gath-Rimoni; yote miji miwili pamoja na sehemu zake za malisho.

26 Miji yote hii kumi pamoja na sehemu zake za malisho ilipewa koo za Wakohathi zilizobaki.

27 Koo za Walawi za Wagerishoni walipewa:

kutoka katika nusu ya Manase,

Golani katika Bashani (mji wa makimbilio kwa ye yote aliyeshtakiwa kwa mauaji) na Beeshtera, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji miwili;

28 kutoka katika kabila la Isakari walipewa,

Kishioni, Daberathi,

29 Yermuthi na En-Ganimu, yote miji minne pamoja na sehemu zake za malisho;

30 kutoka kabila la Asheri walipewa,

Mishali, Abdoni,

31 Helkathi na Rehobu, yote miji minne pamoja na sehemu zake za malisho;

32 Kutoka katika kabila la Naftali walipewa,

Kedeshi katika Galilaya (mji wa makimbilio kwa ajili ya ye yote anayeshtakiwa kwa mauaji), Hamoth-Dori na Kartani, yote miji mitano pamoja na sehemu zake za malisho.

33 Jumla yote ya miji ya koo za Wagerishoni ilikuwa kumi na mitatu, pamoja na sehemu zake za malisho.

34 Koo za Wamerari (waliobaki wa Walawi) walipewa:

kutoka katika kabila la Zabuloni,

Yokneamu, Karta,

35 Dimna na Nahalali, miji minne pamoja na sehemu zake za malisho;

36 kutoka katika kabila la Reubeni walipewa,

Bezeri, Yahazi,

37 Kedemothi na Mefaathi, miji minne pamoja na sehemu zake za malisho;

38 kutoka katika kabila la Gadi walipewa,

Ramoth katika Gileadi (mji wa makimbilio kwa ajili ya ye yote anayeshtakiwa kwa ajili ya mauaji), Mahanaimu,

39 Heshboni na Yazeri, miji minne pamoja na sehemu zake za malisho.

40 Miji yote waliyopewa koo za Wamerari, ambao walikuwa mabaki ya Walawi, jumla ni kumi na miwili.

41 Miji yote ya Walawi katika nchi iliyoshikwa na Waisraeli ilikuwa arobaini na minane, pamoja na sehemu zake za malisho.

42 Kila mmoja wa miji hii ulikuwa na sehemu ya malisho kuuzunguka; ndivyo ilivyokuwa kwa miji hii yote.

43 Kwa hiyoBwanaakawapa Israeli nchi yote aliyokuwa ameapa kuwapa baba zao, nao wakaimiliki na kukaa humo.

44 Bwanaakawapa raha kila upande, kama vile alivyokuwa amewaapia baba zao, hakuna hata mmoja wa adui zao aliyeweza kusimama mbele yao,Bwanaakawatia adui zao wote mikononi mwao.

45 Hakuna hata mojawapo ya ahadi nzuri zaBwanakwa ajili ya nyumba ya Israeli ambayo haikutimia; kila moja ilitimia.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOS/21-3289d313f3c32f8264ff0432930a553c.mp3?version_id=1627—

Yoshua 22

Makabila Ya Mashariki Yarudi Nyumbani

1 Ndipo Yoshua akawaita Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase,

2 naye akawaambia, “Mmeshafanya yale yote Mose mtumishi waBwanaaliyowaamuru, nanyi mmenitii kwa kila jambo nililowaamuru.

3 Kwa muda mrefu sasa, hadi siku hii ya leo, hamkuwaacha ndugu zenu, bali ninyi mmetimiza ile kaziBwanaMungu wenu aliyowapa.

4 Sasa kwa kuwaBwanaMungu wenu amewapa ndugu zenu raha kama alivyoahidi, rudini nyumbani mwenu katika nchi ile ambayo Mose mtumishi waBwanaaliwapa ng’ambo ya pili ya Yordani.

5 Lakini mwe waangalifu sana kushika amri na sheria zile Mose mtumishi waBwanaalizowapa: yaani kumpendaBwanaMungu wenu na kuenenda katika njia zake zote, kutii amri zake, kushikamana naye kwa uthabiti na kumtumikia kwa moyo wenu wote na roho yenu yote.”

6 Ndipo Yoshua akawabariki na kuwaaga waende zao, nao wakaenda nyumbani mwao.

7 (Kwa nusu ya kabila la Manase Mose alikuwa amewapa eneo katika Bashani na ile nusu nyingine Yoshua aliwapa eneo upande wa magharibi ya Yordani pamoja na ndugu zao.) Yoshua alipowapeleka waende zao nyumbani mwao, aliwabariki,

8 akisema, “Rudini ninyi nyumbani mwenu na utajiri wenu, yaani makundi makubwa ya mifugo, mkiwa na fedha, dhahabu, shaba na chuma, pia wingi wa nguo, nanyi mkagawane na ndugu zenu hizo nyara zilizotoka kwa adui zenu.”

9 Kwa hiyo Wareubeni, Wagadi na hiyo nusu ya kabila la Manase wakawaacha Waisraeli huko Shilo katika nchi ya Kanaani ili kurudi Gileadi, nchi yao wenyewe waliyoipata sawasawa na agizo laBwanakupitia Mose.

10 Walipofika Gelilothi karibu na Yordani, katika nchi ya Kanaani, Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase wakajenga madhabahu ya fahari kubwa huko kando ya Yordani.

11 Wale Waisraeli wengine waliposikia kwamba Wareubeni, Wagadi na ile nusu ya kabila la Manase walikuwa wamejenga madhabahu upande wa magharibi mwa Yordani kwenye mpaka wa Kanaani huko Gelilothi,

12 kusanyiko lote la Israeli wakakusanyika huko Shilo ili wakapigane vita dhidi yao.

13 Kwa hiyo hao Waisraeli wengine wakamtuma Finehasi mwana wa kuhani Eleazari katika nchi ya Gileadi, aende kwa Wareubeni, Wagadi na hiyo nusu ya kabila la Manase.

14 Wakatuma pamoja naye watu kumi ambao ni viongozi, mmoja kwa ajili ya kila kabila la Israeli, kila mmoja aliye kiongozi katika mgawanyiko wa jamaa miongoni mwa koo za Israeli.

15 Walipofika katika nchi ya Gileadi, kwa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase, wakawaambia:

16 “Kusanyiko lote laBwanalasema: ‘Je, mmewezaje kuacha kumwamini Mungu wa Israeli kwa kufanya jambo kama hili? Mmewezaje kumwachaBwanana sasa kujijengea madhabahu dhidi yake na kumwasi?

17 Je, dhambi ya Peori ilikuwa ndogo sana kwetu? Mpaka leo hatujatakasika kutokana na dhambi hiyo, hata ingawa kulikuja tauni juu ya kusanyiko laBwana!

18 Je, sasa ndiyo mnamwachaBwana?

“ ‘Kama mkimwasiBwanaleo, kesho atalikasirikia kusanyiko lote la Israeli.

19 Kama nchi mnayomiliki imenajisika, vukeni mje katika nchi yaBwana, mahali Maskani yaBwanailipo, nanyi mkajitwalie sehemu miongoni mwetu, lakini msije mkaasi dhidi yaBwanawala dhidi yetu sisi kwa kujijengea madhabahu nyingine kwa ajili yenu, zaidi ya madhabahu yaBwanaMungu wetu.

20 Wakati Akani mwana wa Zera alipokosa uaminifu kwa vitu vilivyowekwa wakfu, je, ghadhabu ya Mungu haikulipata kusanyiko lote la Israeli? Wala hakuwa yeye peke yake aliyekufa kwa ajili ya hiyo dhambi yake.’ ”

21 Ndipo Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase walipowajibu viongozi wa koo za Israeli, wakisema:

22 “Yeye Mwenye Nguvu, Mungu,Bwana! Yeye Mwenye Nguvu, Mungu,Bwana! Yeye anajua! Israeli na wajue! Kama hili limekuwa ni kuasi au kukosa utii kwaBwana, asituache hai siku hii ya leo.

23 Kama tumejijengea madhabahu yetu wenyewe ili kumwachaBwanana kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za nafaka, au kutoa sadaka za amani juu yake,Bwanamwenyewe na atupatilize leo.

24 “Sivyo! Tulifanya hivyo kwa hofu kwamba siku zijazo wazao wenu wanaweza wakawaambia wazao wetu, ‘Mna uhusiano gani naBwana, Mungu wa Israeli?

25 Bwanaameifanya Yordani kuwa mpaka kati yetu na ninyi, ninyi Wareubeni na Wagadi! Hamna fungu kwaBwana.’ Kwa hiyo wazao wenu wanaweza wakawasababisha wazao wetu wakaacha kumchaBwana.

26 “Hii ndiyo sababu tulisema, ‘Tujiweke tayari na tujenge madhabahu, lakini si kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa au dhabihu.’

27 Badala yake, itakuwa ni ushahidi kati yetu na ninyi na vizazi vijavyo, kwamba tutamwabuduBwanakatika mahali patakatifu pake pamoja na sadaka zetu za kuteketezwa, dhabihu na sadaka za amani. Ndipo siku zijazo wazao wenu hawataweza kuwaambia wazao wetu, ‘Ninyi hamna fungu katikaBwana.’

28 “Nasi tulisema, ‘Ikiwa wakati wo wote watatuambia hilo, au kuwaambia uzao wetu, tutawajibu hivi: Angalieni nakala hii ya madhabahu yaBwana, ambayo baba zetu waliijenga, si kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa na dhabihu, bali kama ushahidi kati yetu sisi na ninyi.’

29 “Hili jambo la kumwasiBwanana kumwacha siku hii ya leo kwa kujenga madhabahu kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, sadaka za nafaka na dhabihu, zaidi ya madhabahu yaBwanaMungu wetu iliyo mbele ya maskani yake na liwe mbali nasi.”

30 Wakati kuhani Finehasi na viongozi wa kusanyiko, wakuu wa koo za Israeli, waliposikia hayo waliyosema hao Wareubeni, Wagadi na hiyo nusu ya kabila la Manase, wakaridhika.

31 Naye Finehasi mwana wa kuhani Eleazari, akawaambia hao Wareubeni, Wagadi na hiyo nusu ya kabila la Manase, “Leo tunajua kwambaBwanayuko pamoja nasi, kwa sababu hamkukosa uaminifu kwaBwanakatika jambo hili. Sasa mmewaokoa Waisraeli na mkono waBwana.”

32 Ndipo Finehasi, mwana wa kuhani Eleazari na viongozi wakarudi Kanaani kutoka kwenye kukutana kwao na Wareubeni na Wagadi huko Gileadi nao wakatoa taarifa kwa Waisraeli.

33 Walifurahi kusikia taarifa hiyo, nao wakamhimidi Mungu. Wala hawakuzungumza tena habari za kupigana vita dhidi yao kuharibu nchi ambayo Wareubeni na Wagadi waliishi.

34 Nao Wareubeni na Wagadi wakaiita ile madhabahu Edi, yaani Shahidi: kwa kuwa itakuwa shahidi kati yetu na ninyi kwambaBwanandiye Mungu.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOS/22-28b4efe4dc43b505ff70d12f79c11a8d.mp3?version_id=1627—