Kumbukumbu La Torati 9

Si Kwa Sababu Ya Haki Ya Waisraeli

1 Sikiliza, Ee Israeli. Sasa mnakaribia kuvuka Yordani mwingie na kuwafukuza mataifa makubwa na yenye nguvu kuliko ninyi pamoja na miji mikubwa yenye kuta zilizofika juu angani.

2 Watu ni wenye nguvu na warefu, ni wana wa Waanaki! Mnafahamu habari zao na mmesikia inavyosemekana: “Ni nani awezaye kusimama dhidi ya Waanaki?”

3 Iweni na hakika leo kwambaBwanaMungu wenu ndiye atakayetangulia kuvuka mbele yenu kama moto uteketezao. Atawaangamiza; atawatiisha mbele yenu. Nanyi mtawafukuza na kuwaangamiza mara moja, kamaBwanaalivyowaahidi.

4 Baada yaBwanaMungu wenu kuwafukuza mbele yenu, msiseme mioyoni mwenu, “Bwanaametuleta hapa kuimiliki nchi hii kwa sababu ya haki yetu.” La, ni kwa sababu ya uovu wa mataifa haya kwambaBwanaanawafukuza mbele yenu.

5 Si kwa sababu ya haki yenu wala uadilifu wenu kwamba mtaimiliki nchi yao; lakini kwa sababu ya uovu wa mataifa haya,BwanaMungu wenu atawafukuza mbele yenu, ili kutimiza lile alilowaapia baba zenu Abrahamu, Isaki na Yakobo.

6 Basi mjue, si kwa sababu ya haki yenuBwanaMungu wenu anawapa nchi hii nzuri kuimiliki, kwa kuwa ninyi ni taifa lenye shingo ngumu.

Ndama Ya Dhahabu

7 Kumbukeni hili, kamwe msisahau jinsi mlivyomkasirishaBwanaMungu wenu kwa hasira huko jangwani. Tangu siku mlipotoka Misri mpaka mlipofika hapa, mmekuwa waasi dhidi yaBwana.

8 Kule Horebu mliamsha ghadhabu yaBwana, kwa hiyo alikasirika vya kutosha hata akataka kuwaangamiza.

9 Nilipopanda mlimani kupokea mbao za mawe, mbao za Agano lileBwanaalilofanya nanyi, nilikaa mlimani siku arobaini mchana na usiku, sikula mkate wala sikunywa maji.

10 Bwanaalinipa mbao mbili za mawe zilizoandikwa kwa kidole cha Mungu. Juu ya mbao hizo kulikuwapo amri zote ambazoBwanaaliwatangazieni kule mlimani kwa njia ya moto, siku ya kusanyiko.

11 Mwisho wa siku arobaini mchana na usiku,Bwanaalinipa mbao mbili za mawe, mbao za Agano.

12 KishaBwanaakaniambia, “Shuka chini mara moja, kwa sababu watu wako ambao umewatoa katika nchi ya Misri wamepotoka. Wamegeukia mbali haraka kutoka lile nililowaagiza, wamejitengenezea sanamu ya kusubu.”

13 NayeBwanaakaniambia, “Nimewaona watu hawa nao ni watu wenye shingo ngumu sana!

14 Niache, ili nipate kuwaangamiza na kufuta jina lao kutoka chini ya mbingu. Nami nitakufanya kuwa taifa lenye nguvu zaidi na kuwa wengi kuliko wao.”

15 Kwa hiyo niligeuka na kutelemka kutoka mlimani kwani mlima ulikuwa ukiwaka moto. Pia vibao vile viwili vya Agano vilikuwa mikononi mwangu.

16 Nilipotazama, niliona kuwa mmefanya dhambi dhidi yaBwanaMungu wenu; mmejifanyia sanamu ya kusubu katika umbo la ndama. Mmegeuka upesi kutoka njia ileBwanaaliyowaagiza.

17 Kwa hiyo nilichukua vibao vile viwili nikavitupa na kuvipasua vipande vipande mbele ya macho yenu.

18 Ndipo tena nikasujudu mbele zaBwanakwa siku arobaini mchana na usiku. Sikula mkate wala sikunywa maji, kwa sababu ya dhambi yote mliyoifanya, mkifanya lile lililo ovu mbele zaBwanana kumkasirisha.

19 Niliogopa hasira na ghadhabu yaBwana, kwa kuwa aliwakasirikia vya kutosha na kutaka kuwaangamiza. LakiniBwanaalinisikiliza tena.

20 Bali yeye alimkasirikia Aroni kiasi cha kutaka kumwangamiza, nami wakati huo nilimwombea Aroni pia.

21 Kisha nikachukua ile sanamu ya ndama mliyoitengeneza na kuichoma kwenye moto. Nikaiponda na kuisaga ikawa unga laini kama vumbi, nikatupa lile vumbi kwenye kijito kilichotiririka toka mlimani.

22 Pia mlimkasirishaBwanahuko Tebera, Masa na Kibroth-Hataava.

23 Vile vile wakatiBwanaalipowatuma kutoka Kadesh-Barnea, alisema, “Kweeni, mkaimiliki nchi ambayo nimekwisha wapa.” Lakini mliasi dhidi ya agizo laBwanaMungu wenu. Hamkumtegemea wala kumtii.

24 Mmekuwa waasi dhidi yaBwanatangu nilipowajua ninyi.

25 Nilianguka kifudifudi mbele zaBwanakwa zile siku arobaini mchana na usiku kwa sababuBwanaalikuwa amesema angewaangamiza ninyi.

26 NilimwombaBwanana kusema, “EeBwanaMwenyezi, usiangamize watu wako, urithi wako mwenyewe ule ulioukomboa kwa uweza wako mkuu na kuwatoa katika nchi ya Misri kwa mkono wenye nguvu.

27 Wakumbuke watumishi wako Abrahamu, Isaki na Yakobo. Usiangalie ukaidi wa watu hawa, uovu wao wala dhambi yao.

28 Watu wa nchi ile uliyotutoa sisi wasije wakasema, ‘Ni kwa sababuBwanahakuweza kuwachukua mpaka nchi aliyokuwa amewaahidia, kwa sababu aliwachukia, akawaleta ili aje kuwaua jangwani.’

29 Bali wao ni watu wako, urithi wako ule ulioutoa Misri kwa uweza wako mkuu na kwa mkono wako ulionyooka.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/DEU/9-f6f1a5dcfb89326722970806253438ff.mp3?version_id=1627—

Kumbukumbu La Torati 10

Vibao Vingine Vya Amri Kumi

1 Wakati uleBwanaaliniambia, “Chonga vibao viwili vya mawe kama vile vya kwanza uje kwangu juu mlimani. Pia utengeneze Sanduku la mbao.

2 Nitaandika juu ya vibao maneno yaliyokuwa katika vile vibao vya kwanza, ambavyo ulivivunja. Kisha utaviweka ndani ya Sanduku.”

3 Hivyo nikatengeneza Sanduku kwa mti wa mshita, nikachonga pia vibao vya mawe kama vile vya kwanza, kisha nikakwea mlimani nikiwa na vibao viwili mikononi mwangu.

4 Bwanaakaandika juu ya hivi vibao kile alichokuwa amekiandika kabla, Amri Kumi alizokuwa amewatangazia juu mlimani, kutoka kwenye moto siku ile ya kusanyiko.Bwanaakanikabidhi.

5 Kisha nikashuka kutoka mlimani na kuweka vibao ndani ya Sanduku nililokuwa nimelitengeneza, kamaBwanaalivyoniagiza, navyo viko huko sasa.

6 (Waisraeli walisafiri kutoka visima vya Yaakani hadi Mosera. Huko Aroni alifariki na kuzikwa, naye Eliezeri mwanawe akachukua nafasi yake kama kuhani.

7 Kutoka pale, walisafiri hadi Gudgoda wakaendelea mpaka Yotbatha, nchi yenye vijito vya maji.

8 Wakati huoBwanaaliteua kabila la Lawi kulibeba Sanduku la Agano laBwana, kusimama mbele zaBwanaili kutoa huduma, na kutangaza baraka kwa Jina lake, kama wanavyofanya mpaka leo.

9 Hiyo ndiyo sababu ya Walawi kutokuwa na sehemu wala urithi miongoni mwa ndugu zao;Bwanandiye urithi wao, kamaBwanaMungu wao alivyowaambia.)

10 Basi nilikaa mlimani kwa siku arobaini mchana na usiku, kama nilivyofanya mara ya kwanza, piaBwanaalinisikiliza hata wakati huu. Haikuwa nia yake kuwaangamiza.

11 Bwanaakaniambia, “Nenda, ukawaongoze watu katika njia yao ili kwamba waweze kuingia na kuimiliki nchi ile niliyowaapia baba zao kuwapa.”

Mche Bwana

12 Na sasa, Ee Israeli,BwanaMungu wako anataka nini kwako ila kumchaBwanaMungu wako, kwenda katika njia zake, kumpenda na kumtumikiaBwanaMungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote,

13 na kuyashika maagizo yaBwanana amri zake ninazokupa leo kwa mafanikio yako mwenyewe?

14 Mbingu, hata mbingu za juu sana, dunia na kila kitu kilichomo ndani yake, ni mali yaBwanaMungu wako.

15 Hata hivyoBwanaalikuwa na shauku na baba zako, akawapenda na akawachagua ninyi, wazao wao, kuliko mataifa yote, kama ilivyo leo.

16 Kwa hiyo tahirini mioyo yenu, na msiwe na shingo ngumu tena.

17 Kwa kuwaBwanaMungu wenu ni Mungu wa miungu na Bwana wa mabwana, Mungu mkuu, mwenye uweza na wa kutisha, ambaye hana upendeleo na hapokei rushwa.

18 Huwapigania yatima na wajane, humpenda mgeni, akimpa chakula na mavazi.

19 Nanyi wapendeni wageni, kwa kuwa ninyi wenyewe mlikuwa wageni huko Misri.

20 McheBwanaMungu wako na umtumikie yeye. Shikamana naye kwa uthabiti na kuapa kwa jina lake.

21 Yeye ni sifa yako; yeye ni Mungu wako, ambaye alikutendea yale maajabu makubwa na ya kutisha uliyoyaona kwa macho yako mwenyewe.

22 Baba zako walioshuka kwenda Misri jumla yao walikuwa sabini, na sasaBwanaMungu wako amekufanya wengi kama nyota za angani.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/DEU/10-ef0829b15dd02672c90a099b6e3f50fb.mp3?version_id=1627—

Kumbukumbu La Torati 11

Mpende Na Umtii Bwana

1 MpendeBwanaMungu wako na kushika masharti yake, amri zake, sheria zake na maagizo yake siku zote.

2 Kumbuka hivi leo kwamba sio watoto wako walioona na kujua marudi yaBwanaMungu wako: utukufu wake, mkono wake wenye nguvu, mkono wake ulionyooshwa;

3 ishara alizozifanya na mambo aliyoyafanya katikati ya Misri, kwa Farao mfalme wa Misri na kwa nchi yake yote;

4 lile alilolifanyia jeshi la Wamisri, farasi na magari yake, jinsi alivyowafurikisha na maji ya Bahari ya Shamu walipokuwa wakiwafuatilia ninyi na jinsiBwanaalivyowaletea angamizo la kudumu juu yao.

5 Haikuwa ni watoto wenu walioona lile Mungu alilowafanyia huko jangwani mpaka mkafika mahali hapa,

6 wala lile Mungu alilowafanyia Dathani na Abiramu, wana wa Eliabu wa kabila la Reubeni, wakati ardhi ilipofungua kinywa chake katikati ya Israeli yote, ikawameza pamoja na wa nyumbani mwao, hema zao na kila kitu kilichokuwa hai ambacho kilikuwa mali yao.

7 Bali ilikuwa ni macho yenu wenyewe ambayo yaliona mambo haya yote makuuBwanaaliyoyatenda.

8 Kwa hiyo fuateni maagizo yote ninayowapa leo, ili mpate kuwa na nguvu za kuingia na kuiteka nchi ile ambayo mnavuka Yordani kuimiliki,

9 ili mpate kuishi siku nyingi katika nchi ile ambayoBwanaaliapa kuwapa baba zenu na wazao wao, nchi itiririkayo maziwa na asali.

10 Nchi mnayoiingia kuimiliki haifanani na nchi ya Misri mlikotoka ambako mlipanda mbegu yenu na kuinywesha, kama bustani ya mboga.

11 Lakini nchi mnayovuka Yordani kuimiliki ni nchi ya milima na mabonde inywayo mvua kutoka mbinguni.

12 Ni nchi ambayoBwanaMungu wenu anaitunza; macho yaBwanaMungu wenu yanaitazama daima kutoka mwanzo wa mwaka hadi mwisho wa mwaka.

13 Hivyo kama mkiyatii maagizo yangu ninayowapa leo kwa uaminifu, yaani kwa kumpendaBwanaMungu wenu, na kumtumikia kwa moyo wako wote na kwa roho yenu yote,

14 ndipo atawanyweshea mvua katika nchi yenu kwa majira yake, mvua ya masika na ya vuli, ili mpate kuvuna nafaka zenu, divai mpya na mafuta.

15 Nitawapa majani kwa ajili ya ng’ombe wenu, nanyi mtakula na kushiba.

16 Jihadharini, la sivyo mtashawishika kugeuka na kuabudu miungu mingine na kuisujudia.

17 Ndipo hasira yaBwanaitawaka dhidi yenu, naye atafunga mbingu ili mvua isinyeshe nayo ardhi haitatoa mazao, nanyi mtaangamia mara katika nchi nzuri ambayoBwanaanawapa.

18 Yawekeni haya maneno yangu katika mioyo yenu na akili zenu, yafungeni kama alama juu ya mikono yenu na kwenye paji za nyuso zenu.

19 Wafundisheni watoto wenu, yazungumzeni wakati mketipo nyumbani na wakati mtembeapo njiani, wakati mlalapo na wakati mwamkapo.

20 Yaandikeni juu ya miimo ya nyumba zenu na juu ya malango yenu,

21 ili kwamba siku zenu na siku za watoto wenu zipate kuwa nyingi katika nchi ileBwanaaliyoapa kuwapa baba zenu, kama zilivyo nyingi siku za mbingu juu ya nchi.

22 Kama mkishika kwa makini maagizo haya yote ninayowapa kuyafuata, ya kumpendaBwanaMungu wenu, kuenenda katika njia zake zote na kushikamana naye kwa uthabiti,

23 ndipoBwanaatawafukuza mataifa haya yote mbele yako, nawe utawafukuza mataifa yaliyo makubwa na yenye nguvu kuliko wewe.

24 Kila mahali mtakapoweka mguu wenu patakuwa penu: Nchi yenu itaenea kutoka jangwa la Lebanoni, na kutoka mto wa Eufrati hadi bahari ya magharibi.

25 Hapatakuwa na mtu atakayeweza kusimama dhidi yenu.BwanaMungu wenu, kama alivyoahidi, ataweka juu ya nchi yote utisho na hofu kwa ajili yenu po pote mwendako.

26 Tazama, leo ninaweka mbele yenu baraka na laana:

27 baraka kama mtatii maagizo yaBwanaMungu wenu, ambayo ninawapa leo;

28 laana kama hamtatii maagizo yaBwanaMungu wenu na kuacha njia ambayo ninawaamuru leo kwa kufuata miungu mingine, ambayo hamkuijua.

29 WakatiBwanaMungu wenu atakapokuwa amewaleta katika nchi mnayoiingia kuimiliki, mtatangaza baraka kutoka Mlima Gerizimu, na kutangaza laana kutoka Mlima Ebali.

30 Kama mnavyofahamu, milima hii ipo ng’ambo ya Yordani, magharibi ya barabara, kuelekea machweo ya jua, karibu na miti mikubwa ya More, katika nchi ya wale Wakanaani wanaoishi Araba, jirani na Gilgali.

31 Karibu mvuke ng’ambo ya Yordani kuingia na kuimiliki nchi ambayoBwanaMungu wenu anawapa. Wakati mtakapokuwa mmeichukua na mnaishi humo,

32 hakikisheni kwamba mnatii amri na sheria zote ninazoziweka mbele yenu leo.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/DEU/11-0c440b75a351e17e19fce5f90e126964.mp3?version_id=1627—

Kumbukumbu La Torati 12

Mahali Pekee Pa Kuabudia

1 Hizi ndizo amri na sheria ambazo ni lazima mwe waangalifu kuzifuata katika nchi ambayoBwana, Mungu wa baba zenu, amewapa kumiliki, kwa muda wote mtakaoishi katika nchi.

2 Haribuni kabisa kila mahali pao pa kuabudia kwenye milima mirefu, vilima na chini ya kila mti mkubwa ambamo mataifa haya mnayokwenda kuchukua ardhi yao huabudia miungu yao.

3 Bomoeni madhabahu zao, vunjeni yale mawe wanayoabudu, chomeni moto nguzo zao za Ashera; katilieni mbali sanamu za miungu yao na mfute majina yao mahali hapo.

4 Kamwe msimwabuduBwanaMungu wenu kama wanavyoabudu wao.

5 Bali mtatafuta mahaliBwanaMungu wenu atakapopachagua katika makabila yenu yote ili aliweke jina lake huko kuwa makao yake. Mahali hapo ndipo iwapasapo kwenda;

6 hapo ndipo mtakapoleta sadaka zenu za kuteketezwa na dhabihu, zaka zenu na changizo zenu, kile ulichoweka nadhiri kutoa, sadaka zenu za hiari na malimbuko ya makundi yenu ya ng’ombe pamoja na mbuzi na kondoo.

7 Hapo, katika uwepo waBwanaMungu wenu, ninyi pamoja na jamaa zenu, mtakula na kufurahia kila kitu ambacho mmegusa kwa mikono yenu, kwa sababuBwanaMungu wenu amewabariki.

8 Msifanye kama tunavyofanya hapa leo, kila mtu anavyopenda mwenyewe,

9 kwa kuwa bado hamjafikia mahali pa mapumziko na urithi ambaoBwanaMungu wenu anawapa.

10 Lakini mtavuka Yordani na kuishi katika nchiBwanaMungu wenu anayowapa kama urithi, naye atawapa pumziko kutokana na adui zenu wote wanaowazunguka ili ninyi mpate kuishi kwa salama.

11 Kisha kuhusu mahaliBwanaMungu wenu atakapopachagua kuwa mahali pa makao ya Jina lake, hapo ndipo inapowapasa kuleta kila kitu ninachowaamuru: sadaka zenu za kuteketezwa na dhabihu, zaka zenu na changizo, pamoja na vitu vyote vyenye thamani ambavyo mmeweka nadhiri kumtoleaBwana.

12 Hapo furahini mbele zaBwanaMungu wenu, ninyi, wana wenu na binti zenu, watumishi wenu wa kiume na wa kike, pamoja na Walawi kutoka katika miji yenu ambao hawana mgawo wala urithi wao wenyewe.

13 Iweni waangalifu, msitoe dhabihu zenu za kuteketezwa mahali po pote mnapopapenda.

14 Mtazitoa tu mahali pale ambapoBwanaatachagua katika mojawapo ya makabila yenu, nanyi hapo zingatieni kila jambo ninalowaamuru.

15 Hata hivyo, mnaweza kuwachinja wanyama wenu katika miji yenu yo yote ile na kula nyama nyingi mpendavyo kama vile mmemchinja paa au kulungu, kulingana na baraka mtakazojaliwa naBwanaMungu wenu. Watu walio najisi au walio safi wanaweza kula.

16 Lakini kamwe usinywe damu; imwage juu ya ardhi kama maji.

17 Hamruhusiwi kula katika miji yenu zaka yenu ya nafaka, ya divai mpya na ya mafuta, au mzaliwa wa kwanza wa makundi yenu ya ng’ombe na makundi yenu ya mbuzi na kondoo, wala cho chote ambacho mmeweka nadhiri kukitoa, au sadaka zako za hiari, wala matoleo maalum.

18 Badala yake, mtakula vitu hivyo katika uwepo waBwanaMungu wenu mahali ambapoBwanaMungu wenu atapachagua: wewe, wana wako na binti zako, watumishi wako wa kiume na wa kike, na Walawi kutoka miji yenu. Mnatakiwa mfurahi mbele zaBwanaMungu wenu kwa kula kitu mtakachoweka mikono yenu.

19 Mwe waangalifu msiwapuuze Walawi kwa muda wote mnaoishi katika nchi yenu.

20 BwanaMungu wenu atakapokuwa ameongeza nchi yenu kama alivyowaahidi, nanyi mkitamani nyama na mkisema, “Ningependa nyama,” hapo unaweza kula nyingi upendavyo.

21 Kama mahali ambapoBwanaMungu wenu atapachagua kuweka Jina lake ni mbali sana kutoka kwenu, unaweza kuchinja wanyama kutoka makundi yenu ya ng’ombe, ya mbuzi na ya kondoo ambayoBwanaamewapa, kama nilivyokuamuru, na mkiwa katika miji yenu wenyewe mnaweza kula nyingi mtakavyo.

22 Mle kama vile mngekula paa na kulungu. Wote walio najisi kiibada na walio safi mwaweza kula.

23 Lakini hakikisheni kwamba hamkunywa damu, kwa sababu damu ni uhai, kamwe msile uhai pamoja na nyama.

24 Hamruhusiwi kamwe kunywa damu; imwageni juu ya ardhi kama maji.

25 Msinywe damu, ili mweze kufanikiwa ninyi pamoja na watoto wenu baada yenu, kwa sababu mtakuwa mkifanya lililo haki machoni paBwana.

26 Lakini vichukueni vitu vyenu vilivyowekwa wakfu pamoja na vile mlivyoweka nadhiri, mwende mahali paleBwanaatakapopachagua.

27 Leteni sadaka zenu za kuteketezwa juu ya madhabahu yaBwanaMungu wenu, vyote nyama na damu. Damu ya dhabihu zenu lazima imiminwe kando ya madhabahu yaBwanaMungu wenu, lakini nyama mnaweza kula.

28 Mwe waangalifu kutii masharti haya yote ninayowapa, ili kwamba siku zote mweze kufanikiwa, ninyi pamoja na watoto wenu baada yenu, kwa sababu mtakuwa mkifanya lililo jema na sahihi mbele za macho yaBwanaMungu wenu.

29 BwanaMungu wenu atayakatilia mbali mbele yenu mataifa ambayo punde kidogo mtayavamia na kuyaondoa. Lakini mtakapokuwa mmeyafukuza na kuishi katika nchi yao,

30 na baada ya kuangamizwa mbele yenu, mwe waangalifu msijiingize katika tanzi kwa kuuliza habari za miungu yao, mkisema, “Je, mataifa haya hutumikiaje miungu yao? Nasi tutafanya vivyo hivyo.”

31 Kamwe msimwabuduBwanaMungu wenu kwa njia wanayoabudu miungu yao, kwa sababu katika kuabudu miungu yao, wanafanya aina zote za machukizo anayoyachukiaBwana. Hata huwateketeza wana wao na binti zao kwa moto kama kafara kwa miungu yao.

32 Angalieni kwamba mnafanya yote niliyowaamuru; msiongeze kitu wala msipunguze kitu.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/DEU/12-d19b23d00de47ca8635847849612199c.mp3?version_id=1627—

Kumbukumbu La Torati 13

Kuabudu Miungu Mingine

1 Kama nabii, au yule anayetabiri kwa njia ya ndoto, akijitokeza miongoni mwenu na akawatangazia ishara ya miujiza na ajabu,

2 ikiwa ishara au ajabu ya aliyozungumza ikatokea, naye akasema, “Na tufuate miungu mingine” (miungu ambayo hamjaifahamu) “na tuiabudu,”

3 kamwe msiyasikilize maneno ya nabii wala mwota ndoto huyo.BwanaMungu wenu anawajaribu kuangalia kama mnampenda kwa moyo wenu wote na kwa roho yenu yote.

4 NiBwanaMungu wenu ambaye mnapaswa kumfuata tena ni yeye mnapaswa kumheshimu. Shikeni maagizo yake na kumtii, mtumikieni na kushikamana naye.

5 Huyo nabii au mwota ndoto lazima auawe, kwa sababu amehubiri uasi dhidi yaBwanaMungu wenu, ambaye aliwatoa kutoka nchi ya Misri na kuwakomboa kutoka nchi ya utumwa; amejaribu kuwageuza kutoka njia ambayoBwanaMungu wenu aliwaagiza mfuate. Ni lazima mwondoe uovu miongoni mwenu.

6 Kama ndugu yako hasa, au mwanao au binti yako, au mke umpendaye, au rafiki yako wa karibu sana akikushawishi kwa siri, akisema, “Na twende tukaabudu miungu mingine” (miungu ambayo ninyi wala baba zenu hamkuifahamu,

7 miungu ya watu wanaowazunguka, ikiwa karibu au mbali, kutoka mwisho mmoja wa nchi mpaka mwingine),

8 usikubali wala usimsikilize. Usimhurumie! Usimwache wala usimkinge.

9 Hakika ni lazima auawe. Ni lazima mkono wako uwe wa kwanza katika kumwua kisha mikono ya watu wengine wote.

10 Mpigeni kwa mawe mpaka afe, kwa sababu alijaribu kuwageuza mtoke kwaBwanaMungu wenu ambaye aliwatoa Misri, kutoka nchi ya utumwa.

11 Kisha Israeli wote watasikia na kuogopa, wala hakuna mmoja miongoni mwenu atakayefanya uovu tena.

12 Kama mkisikia ikisemwa kwamba moja ya miji ambayoBwanaMungu wenu anawapa mkae ndani yake

13 kuna wanaume waovu wameinuka miongoni mwenu na wamewapotosha watu wa mji, wakisema, “Twendeni tukaabudu miungu mingine” (miungu ambayo hamkuifahamu),

14 ndipo itakubidi kuuliza, kupima na kuchunguza kwa makini. Kama ni kweli, tena ikihakikishwa kwamba jambo hili lichukizalo limefanyika miongoni mwenu,

15 kwa hakika ni lazima muwaue kwa upanga wale wote wanoishi katika mji ule. Uharibuni kabisa, pamoja na watu wake na mifugo yake.

16 Kusanyeni nyara zote za mji katika uwanja wa wazi na kuuchoma mji kabisa pamoja na nyara zake zote kama sadaka ya kuteketezwa kwaBwanaMungu wenu. Utabaki kuwa magofu milele na hautajengwa tena.

17 Hakuna kimoja kati ya vitu vilivyolaaniwa kitakachokutwa mikononi mwenu, iliBwanaageuze hasira yake kali. Atawahurumia na kuwa na rehema kwenu pia kuongeza idadi yenu, kama alivyowaahidi baba zenu,

18 kwa sababu mnamtiiBwanaMungu wenu, mkizishika amri zake zote zile ninazowapa leo na kufanya lile lililo jema machoni pake.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/DEU/13-aa3d692f62a1ad31f67c25e05d49d35b.mp3?version_id=1627—

Kumbukumbu La Torati 14

Vyakula Vilivyo Najisi Na Vilivyo Safi

1 Ninyi ni watoto waBwanaMungu wenu. Msijichanje ama kujinyoa upara kwenye paji la uso kwa ajili ya aliyekufa,

2 kwa maana ninyi ni taifa takatifu kwaBwanaMungu wenu.Bwanaamewachagua ninyi kuwa taifa la kipekee kutoka mataifa yote juu ya uso wa dunia, mwe tunu yake.

3 Msile kitu cho chote ambacho ni machukizo.

4 Hawa ndio wanyama mtakaokula: ng’ombe, kondoo, mbuzi,

5 kulungu, paa, kongoni, paa mweupe, mbuzi-mwitu, pofu na kondoo wa mlimani.

6 Mnaweza kumla mnyama ye yote mwenye kwato zilizogawanyika mara mbili, pia yule anayecheua.

7 Hata hivyo, miongoni mwa wale wanaocheua au wale walio na kwato zilizogawanyika kamwe msile ngamia, sungura na pelele. Iwapo wanacheua, lakini hawana kwato zilizogawanyika; ni najisi kwenu kwa taratibu za kiibada.

8 Nguruwe pia ni najisi; ingawa ana kwato zilizogawanyika, hacheui. Msile nyama yake wala kugusa mzoga wake.

9 Katika viumbe hai vyote viishivyo kwenye maji, mnaweza kula ye yote aliye na mapezi pamoja na magamba.

10 Lakini cho chote kisicho na mapezi na magamba msile; kwenu ni najisi.

11 Mnaweza kula ndege ye yote aliye safi.

12 Lakini wafuatao msiwale: tai, kipungu, kipungu mweusi,

13 kengewa mwekundu, kengewa mweusi, mwewe wa aina yo yote,

14 kunguru wa aina yo yote,

15 mbuni, kirukanjia, dudumizi, kipanga wa aina yo yote

16 bundi, muvurila, bundi mkubwa,

17 mwari, nderi, ndezi, mnandi,

18 membe, koikoi wa aina yo yote, hudihudi na popo.

19 Wadudu wote warukao kwa makundi ni najisi kwenu, msiwale.

20 Lakini viumbe vyote vyenye mabawa vilivyo safi mwaweza kula.

21 Msile kitu cho chote mtakachokuta kimekufa. Mnaweza kumpa mgeni ye yote anayeishi katika mojawapo ya miji yenu, naye anaweza kula au mnaweza kumuuzia mtu wa nchi nyingine. Lakini ninyi ni watu watakatifu kwaBwanaMungu wenu.

Msitokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake.

Zaka

22 Hakikisheni mmetenga sehemu ya kumi ya mazao yote ya mashamba yenu kila mwaka.

23 Mtakula zaka za nafaka yenu, divai mpya, mafuta na wazaliwa wa kwanza wa makundi yenu ya ng’ombe na ya kondoo na mbuzi mbele zaBwanaMungu wenu pale mahali atakapopachagua kama maskani kwa ajili ya Jina lake, ili kwamba mpate kujifunza kumheshimuBwanaMungu wenu daima.

24 Lakini ikiwa mahali pale ni mbali sana nanyi mmebarikiwa naBwanaMungu wenu na hamwezi kubeba zaka yenu (kwa sababu mahali paleBwanaatakapopachagua kuliweka Jina lake ni mbali sana),

25 basi badilisheni zaka yenu kuwa fedha, mkaichukue hiyo fedha mwende nayo mahaliBwanaMungu wenu atakapopachagua.

26 Tumieni hiyo fedha kununua cho chote ukitakacho: ng’ombe, kondoo, divai au kinywaji cho chote chenye chachu au cho chote mnachotaka. Kisha ninyi na wa nyumbani mwenu mtaila mbele zaBwanaMungu wenu na kufurahi.

27 Msiache kuwajali Walawi waishio katika miji yenu, kwa kuwa hao hawana shamba wala urithi wao wenyewe.

28 Mwishoni mwa kila mwaka wa tatu, leteni zaka zote za mazao ya miaka ile na uyahifadhi kwenye miji yenu,

29 ili Walawi (ambao hawana mashamba wala urithi wao wenyewe) na wageni, yatima na wajane wanaoishi kwenye miji yenu wapate kuja kula na kushiba, iliBwanaMungu wenu apate kuwabariki ninyi katika kazi zote za mikono yenu.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/DEU/14-3ccbf53850fb3f6d71aa3430deb33540.mp3?version_id=1627—

Kumbukumbu La Torati 15

Mwaka Wa Kufuta Madeni

1 Kila mwisho wa miaka saba ni lazima mfute madeni.

2 Hivi ndivyo itakavyofanyika: Kila mkopeshaji atafuta mkopo aliomkopesha Mwisraeli mwenzake. Hatamtaka Mwisraeli mwenzake au ndugu yake amlipe hilo deni, kwa sababu wakati waBwanawa kufuta madeni umetangazwa.

3 Unaweza kudai malipo kwa mgeni, lakini lazima ufute kila deni ambalo ndugu yako anawiwa nawe.

4 Hata hivyo, hapatakuwepo maskini miongoni mwenu, kwa kuwa katika nchiBwanaMungu wenu anayowapa kuimiliki kama urithi wenu, atawabariki sana,

5 ikiwa tutamtiiBwanaMungu wenu kikamilifu na kuwa waangalifu kuyafuata maagizo haya yote ninayowapa leo.

6 Kwa kuwaBwanaMungu wenu atawabariki kama alivyoahidi, nanyi mtawakopesha mataifa mengi lakini hamtakopa kwa ye yote. Mtatawala mataifa mengi lakini hakuna taifa litakalowatawala ninyi.

7 Ikiwa kuna mtu maskini miongoni mwa ndugu zenu, katika mji wo wote wa hiyo nchi ambayoBwanaMungu wenu anawapa, msiwe na moyo mgumu wala usimfumbie mkono ndugu yako aliye maskini.

8 Afadhali fungua mikono yako na umkopeshe kwa hiari cho chote anachohitaji.

9 Jihadhari usijiwekee wazo hili ovu: “Mwaka wa saba, mwaka wa kufuta madeni umekaribia,” usije ukaonyesha nia mbaya kwa ndugu yako mhitaji na ukaacha kumpa cho chote. Anaweza kumlalamikiaBwanadhidi yako nawe utakuwa umepatikana na hatia ya dhambi.

10 Mpe kwa ukarimu na ufanye hivyo bila kinyongo moyoni, ndipo kwa sababu ya hiliBwanaMungu wenu atakubariki katika kazi zako zote na kwa kila kitu utakachokiwekea mkono wako.

11 Siku zote watakuwepo watu maskini katika nchi. Kwa hiyo ninawaamuru mwe na mikono iliyokunjuliwa kuwaelekea ndugu zenu, kuwaelekea maskini na wahitaji katika nchi yenu.

Kuwaacha Huru Watumishi

12 Kama Mwebrania mwenzako, mwanaume au mwanamke, akijiuza kwako na kukutumikia miaka sita, katika mwaka wa saba ni lazima umwache aende zake akiwa huru.

13 Nawe wakati utakapomwachia usimwache aende mikono mitupu.

14 Mpe kwa uhuru kutoka katika zizi lako la kondoo na mbuzi, kutoka katika sakafu yako ya kupuria nafaka na kutoka katika mashinikizo yako ya kukamulia divai. Mpe kama vile ambavyoBwanaMungu wako alivyokubariki.

15 Kumbukeni kuwa ninyi mlikuwa watumwa huko Misri nayeBwanaMungu wenu aliwakomboa. Ndiyo sababu nimewapa agizo hili leo.

16 Lakini mtumishi wako akikuambia, “Sitaki kukuacha,” kwa sababu anakupenda wewe na jamaa yako naye anaridhika nawe,

17 ndipo utachukua chuma ndogo utoboe sikio lake mpaka hiyo chuma iingie kwenye ubao wa mlango, naye atakuwa mtumishi wako wa maisha. Ufanye vivyo hivyo kwa mtumishi wa kike.

18 Usifikiri kuwa kuna ugumu kumwacha mtumishi wako huru, kwa sababu utumishi wake kwako kwa miaka hii sita umekuwa wa thamani mara mbili ya ujira wa mtumishi wa kuajiriwa. NayeBwanaMungu wenu atakubarikia kwa kila kitu utakachofanya.

Wazaliwa Wa Kwanza Wa Wanyama

19 Wekeni wakfu kwaBwanaMungu wenu kila mzaliwa wa kwanza wa kiume wa makundi yenu ya n’gombe na ya mbuzi na kondoo. Maksai walio wazaliwa wa kwanza msiwafanyize kazi, wala msinyoe manyoya ya wazaliwa wa kwanza wa kondoo.

20 Kila mwaka ninyi na jamaa zenu mtapaswa kuwala mbele zaBwanaMungu wenu pale mahali atakapopachagua.

21 Kama mnyama ana dosari, akiwa ni kilema au kipofu au kama ana kilema kibaya, kamwe usimtoe dhabihu kwaBwanaMungu wenu.

22 Itawapasa kumla ninyi wenyewe katika miji yenu. Wote wasio safi na walio safi kwa desturi za kiibada mwaweza kula kama vile mnavyokula paa au kulungu.

23 Lakini kamwe msinywe damu; imwageni ardhini kama maji.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/DEU/15-02e56bd2cdd9be518a80ccea690ec933.mp3?version_id=1627—

Kumbukumbu La Torati 16

Pasaka

1 Shikeni mwezi wa Abibu, na kuiadhimisha Pasaka yaBwanaMungu wenu, kwa sababu katika mwezi wa Abibu, Mungu aliwatoa Misri usiku.

2 Mtatoa dhabihu ya Pasaka ya mnyama kwaBwanaMungu wenu kutoka kundi lenu la mbuzi na kondoo au la ng’ombe, mahali pale ambapoBwanaatapachagua kama makao kwa ajili ya Jina lake.

3 Msile nyama hiyo pamoja na mikate iliyotiwa hamira, lakini kwa siku saba mtakula mikate isiyotiwa chachu, mikate ya kujitesa, kwa sababu mliondoka Misri kwa haraka, ili kwamba siku zote za maisha yenu mpate kukumbuka wakati wenu wa kuondoka Misri.

4 Hamira isionekane katika mali zenu katika nchi yenu yote kwa siku saba. Nyama yo yote ya dhabihu mtakayotoa jioni ya siku ya kwanza isibakizwe mpaka asubuhi.

5 Kamwe msitoe dhabihu ya Pasaka katika mji wo wote ambaoBwanaMungu wenu amewapa,

6 isipokuwa mahali atakapopachagua kama makao kwa ajili ya Jina lake. Hapo ndipo lazima mtoe dhabihu ya Pasaka jioni, jua litakapotua, iwe kumbukumbu yenu ya kutoka Misri.

7 Okeni na mle mahali pale ambapoBwanaMungu wenu atakapopachagua, kisha asubuhi mrudi kwenye mahema yenu.

8 Kwa siku sita mtakula mikate isiyotiwa chachu na siku ya saba fanyeni kusanyiko kwa ajili yaBwanaMungu wenu na msifanye kazi.

Sikukuu Ya Mavuno

9 Mhesabu majuma saba tangu wakati mnapoanza kuchukua mundu kuvuna nafaka.

10 Kisha msherehekee Sikukuu ya Majuma kwaBwanaMungu wenu kwa kutoa sadaka ya hiari kwa kadiri ya baraka ambayoBwanaMungu wenu amewapa.

11 Shangilieni mbele zaBwanaMungu wenu mahali atakapopachagua kama makao ya Jina lake, ninyi, wana wenu na binti zenu, watumishi wenu wa kiume na wa kike, Walawi walio katika miji yenu, na wageni, yatima na wajane waishio miongoni mwenu.

12 Kumbukeni kwamba mlikuwa watumwa kule Misri na mfuate amri hizi kwa uangalifu.

Sikukuu Ya Vibanda

13 Adhimisheni sikukuu ya vibanda kwa siku saba baada ya kukusanya mazao yenu ya nafaka na kukamua zabibu.

14 Mfurahie sikukuu yenu, ninyi, wana wenu, binti zenu, watumishi wenu wa kiume na wa kike, Walawi, wageni, yatima na wajane ambao wanaishi katika miji yenu.

15 Kwa siku saba mtaiadhimisha sikukuu yaBwanaMungu wenu katika mahali atakapopachaguaBwana. Kwa kuwaBwanaMungu wenu atawabariki katika mavuno yenu na katika kazi zote za mikono yenu na furaha yenu itakamilika.

16 Wanaume wenu wote lazima wajitokeze mara tatu kwa mwaka mbele zaBwanaMungu wenu mahali atakapopachagua: kwa ajili ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, Sikukuu ya Majuma, na Sikukuu ya Vibanda. Hakuna mtu atakayejitokeza mbele zaBwanamikono mitupu:

17 Kila mmoja wenu ni lazima alete zawadi kulingana na jinsi ambavyoBwanaMungu wenu alivyowabariki.

Waamuzi

18 Wateue waamuzi na maafisa kwa kila kabila lenu katika kila mji ambaoBwanaMungu wenu anawapa, nao watawaamua watu kwa usawa.

19 Msipotoshe haki wala msifanye upendeleo. Msikubali rushwa kwa sababu rushwa hupofusha macho ya wenye busara na kugeuza maneno ya wenye haki.

20 Mfuate haki na haki peke yake, ili mweze kuishi na kuimiliki nchi ambayoBwanaMungu wenu anawapa.

Kuabudu Miungu Mingine

21 Msisimamishe nguzo yo yote ya Ashera kando ya madhabahu mliyomjengeaBwanaMungu wenu,

22 wala msisimamishe jiwe la kuabudu, kwa maanaBwanaMungu wenu anavichukia vitu hivi.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/DEU/16-d4f6f98e5664fa92f4ef6cd7f524d45f.mp3?version_id=1627—

Kumbukumbu La Torati 17

1 MsimtoleeBwanaMungu wenu dhabihu ya maksai au kondoo ambaye ana dosari yo yote au hitilafu ndani yake, kwa kuwa hilo litakuwa chukizo kwake.

2 Ikiwa mwanaume au mwanamke anayeishi kati ya mojawapo ya miji akupayoBwana, anakutwa anafanya uovu mbele zaBwanaMungu wenu, kwa kuvunja Agano lake,

3 naye amekwenda kinyume na agizo langu kuabudu miungu mingine na kuisujudia, kama vile jua, mwezi au nyota za angani,

4 hili likiwa limeletwa mbele yenu, ni lazima kulichunguza kikamilifu. Ikiwa ni kweli na kuwa limehakikishwa kwamba hili ni chukizo lililofanyika katika Israeli,

5 mchukueni huyo mwanaume au mwanamke ambaye amelifanya tendo hili ovu kwenye lango la mji wenu na kumpiga mawe mtu huyo mpaka afe.

6 Kwa ushuhuda wa mashahidi wawili au watatu mtu huyo atauawa, bali hakuna mtu atakayeuawa kwa ushuhuda wa shahidi mmoja tu.

7 Ni lazima kwanza mikono ya mashahidi itangulie kumwua huyo mtu. Ni lazima mwondoe uovu miongoni mwenu.

Mahakama Za Sheria

8 Kama mashauri yanaletwa katika mahakama zenu ambayo ni magumu zaidi kwenu kuyaamua, ikiwa ni umwagaji wa damu, madai au mashambulio, yapelekeni mahali ambapoBwanaMungu wenu atapachagua.

9 Nendeni kwa makuhani, ambao ni Walawi, na kwa mwamuzi ambaye atakuwa kazini wakati huo. Ulizeni kwao nao watawapa maamuzi.

10 Ni lazima mtende sawasawa na maamuzi watakayowapa mahaliBwanaatakapopachagua. Iweni waangalifu kufanya kila kitu watakachowaongoza kufanya.

11 Fanyeni sawasawa na sheria wanayowafundisha na maamuzi wanayowapa. Msigeuke mkono wa kuume au kushoto kuacha kufanya yale wanayowaambia.

12 Mwanaume atakayeonyesha dharau kwa mwamuzi au kwa kuhani ambaye amewekwa kumtumikiaBwanaMungu wenu lazima auawe. Lazima mwondoe uovu katika Israeli.

13 Watu wote watasikia na kuogopa, nao hawatakuwa wenye kudharau tena.

Mfalme

14 Wakati utakapoingia katika nchi anayowapaBwanaMungu wenu kuimiliki na kukaa humo, nanyi mkasema, “Na tumweke mfalme juu yetu kama mataifa yanayotuzunguka,”

15 iweni na uhakika wa kumweka mfalme juu yenu ambayeBwanaMungu wenu atamchagua. Ni lazima atoke miongoni mwa ndugu zenu wenyewe. Msimweke mgeni juu yenu ambaye si ndugu wa Kiisraeli.

16 Hata hivyo, kamwe mfalme asijipatie hesabu kubwa ya farasi kwa ajili yake mwenyewe, au kuwafanya watu warudi Misri ili kupata farasi zaidi, kwa maanaBwanaamekuambia, “Hamtairudia njia ile tena.”

17 Kamwe asioe wake wengi, la sivyo moyo wake utapotoka. Kamwe asijilimbikizie kiasi kikubwa cha fedha na dhahabu.

18 Atakapokuwa amekalia kiti cha ufalme wake, ajiandikie kwenye kitabu nakala ya sheria kwa ajili yake mwenyewe kutoka zile sheria za makuhani ambao ni Walawi.

19 Atakuwa na nakala hiyo, naye ataisoma siku zote za maisha yake ili kwamba ajifunze kumheshimuBwanaMungu wake na kufuata kwa uangalifu maneno yote ya sheria hii na amri hizi,

20 naye asijifikirie kuwa ni bora kuliko ndugu zake na kuipotosha sheria. Ndipo yeye na wazao wake watatawala katika ufalme wake kwa muda mrefu katika Israeli.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/DEU/17-f2aa0ced8133fbbedcb2219aab4b0e7d.mp3?version_id=1627—

Kumbukumbu La Torati 18

Sadaka Kwa Makuhani Na Walawi

1 Makuhani ambao ni Walawi, yaani kabila lote la Lawi, hawatakuwa na mgawo wala urithi pamoja na Israeli. Wataishi kwa sadaka zitolewazo kwa ajili yaBwanaza kuteketezwa kwa moto, kwa maana huo ndio urithi wao.

2 Hawatakuwa na urithi miongoni mwa ndugu zao;Bwanandiye urithi wao, kama alivyowaahidi.

3 Hili ndilo fungu la makuhani kutoka kwa watu watakaotoa dhabihu ya fahali au kondoo: mguu wa mbele, mataya na matumbo.

4 Mtawapa malimbuko ya nafaka zenu, divai mpya, mafuta na sufu ya kwanza kutoka manyoya ya kondoo zenu,

5 kwa kuwaBwanaMungu wenu amewachagua pamoja na wazao wao kutoka makabila yenu kusimama na kuhudumu katika jina laBwanasiku zote.

6 Ikiwa Mlawi atahama kutoka mmojawapo ya miji yenu popote katika Israeli ambapo anaishi, akaja kwa moyo wote mahali ambapoBwanaatapachagua,

7 anaweza akahudumu katika jina laBwanaMungu wake kama Walawi wenzake wote wanaohudumu hapo mbele zaBwana.

8 Atashiriki sawa katika mafao yao, hata kama amepokea fedha kutoka mauzo ya mali ya jamaa yake.

Matendo Ya Machukizo

9 Wakati mtakapoingia katika nchi ambayoBwanaMungu wenu anawapa, msijifunze kuiga njia za machukizo za mataifa ya huko.

10 Asionekane mtu ye yote miongoni mwenu ampitishaye mwanawe au binti yake katika moto, atakayefanya uaguzi, ulozi, anayetabiri nyakati, anayejishughulisha na uchawi,

11 wala alogaye kwa kupiga mafundo, wala apandishaye pepo, anayeabudu mizimu, wala awaombaye wafu.

12 Mtu ye yote afanyaye mambo haya ni chukizo kwaBwana, tena ni kwa sababu ya matendo haya ya kuchukiza wayafanyayo ndiyo maanaBwanaMungu wenu atayafukuza mataifa hayo mbele yenu.

13 Kamwe msilaumiwe mbele zaBwanaMungu wenu.

Nabii

14 Mataifa mtakayowafukuza husikiliza wale wafanyao ulozi na uaguzi. Lakini kwenu ninyi,BwanaMungu wenu hajawaruhusu kufanya hivyo.

15 BwanaMungu wenu atawainulia nabii kama mimi kutoka miongoni mwa ndugu zenu wenyewe. Lazima mumsikilize yeye.

16 Kwa kuwa hivi ndivyo mlivyomwombaBwanaMungu wenu kule Horebu siku ile ya kusanyiko, wakati mliposema, “Na tusiisikie sauti yaBwanaMungu wetu, wala kuuona moto huu mkubwa tena, ama sivyo tutakufa.”

17 Bwanaakaniambia: “Wanachosema ni vyema.

18 Nitawainulia nabii kama wewe kutoka miongoni mwa ndugu zao; nitaweka maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia kila kitu nitakachomwamuru.

19 Kama mtu ye yote hakusikiliza maneno yangu ambayo nabii atayasema kwa Jina langu, mimi mwenyewe nitamwajibisha.

20 Lakini nabii ambaye atathubutu kusema kwa Jina langu kitu cho chote ambacho sikumwamuru akiseme, au nabii ambaye husema kwa jina la miungu mingine ni lazima auawe.”

21 Mnaweza kuulizana wenyewe, “Tutawezaje kujua wakati ujumbe haukusemwa naBwana?”

22 Ikiwa kile nabii anachotangaza kwa jina laBwanahakikutokea au kutimia, huo ni ujumbe ambaoBwanahakusema. Nabii huyo amesema kwa ujuaji. Msimwogope huyo.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/DEU/18-c2b66949ba184d38da65476c92845154.mp3?version_id=1627—