Kumbukumbu La Torati 19

Miji Ya Makimbilio

1 WakatiBwanaMungu wenu atakapokuwa amewaangamiza mataifa ambayo nchi yao anawapa ninyi, wakati mtakapokuwa mmewafukuza na kuishi katika miji yao na nyumba zao,

2 ndipo mtenge miji mitatu iliyopo katikati ya nchi kwa ajili yenu, katika nchi ambayoBwanaMungu wenu anawapa kuimiliki.

3 Jengeni barabara katika miji hiyo na kuigawa mara tatu, nchi anayowapaBwanaMungu wenu kama urithi, ili kwamba ye yote amuuaye mtu aweze kukimbilia humo.

4 Hii ndiyo kanuni kuhusu mtu amuuaye mwingine na kukimbilia humo kuokoa maisha yake, yaani, yeye amuuaye jirani yake bila kukusudia, wala hakumchukia kabla ya hapo.

5 Kwa mfano, mtu aweza kwenda msituni na jirani yake kukata miti, naye anapozungusha shoka kuangusha mti, shoka linaweza kuchomoka kutoka kwenye mpini na kumpiga jirani yake na kumwua. Yule mtu anaweza kukimbilia katika mmojawapo ya miji hii na kuokoa maisha yake.

6 Kama sivyo, mlipiza kisasi cha damu anaweza kumfuatilia kwa hasira kali, naye akamkamata na kumwua kama umbali ni mrefu sana hata ingawa hastahili kifo, kwa sababu amemwua jirani yake bila kukusudia.

7 Hii ndiyo sababu nimewaagiza ninyi kutenga miji mitatu ya makimbilio kwa ajili yenu.

8 KamaBwanaMungu wenu akipanua nchi yenu, kama alivyoahidi kwa kiapo kwa baba zenu na kuwapa nchi yote aliyowaahidi,

9 kwa sababu mmefuata kwa uangalifu sheria zote ninazowaamuru leo, kumpendaBwanaMungu wenu na kuenenda siku zote katika njia zake, ndipo mtenge miji mingine, mitatu zaidi.

10 Fanyeni hivi ili damu isiyo na hatia isimwagwe katika nchi yenu, ambayoBwanaMungu wenu anawapa kama urithi wenu, ili kwamba msije mkawa na hatia ya kumwaga damu.

11 Lakini kama mtu anamchukia ndugu yake, akamvizia, akamshambulia na kumwua, kisha akakimbilia katika mmojawapo ya miji hii,

12 wazee wa mji wake watatuma ujumbe kwake, kumleta kutoka mji ule na kumkabidhi mlipiza kisasi cha damu kumwua.

13 Msimwonee huruma. Lazima mwondoe katika Israeli hatia ya umwagaji damu isiyo na hatia ili kwamba mpate kufanikiwa.

14 Usisogeze jiwe la mpaka wa jirani yako ambao uliwekwa na wale waliokutangulia katika urithi upokeao katika nchiBwanaMungu wako anayowapa kuimiliki.

Mashahidi

15 Shahidi mmoja hatoshi kumtia hatiani mtu kwa uhalifu au kosa lo lote ambalo anaweza kuwa amelitenda. Lazima shauri lithibitishwe kwa ushuhuda wa mashahidi wawili au watatu.

16 Kama shahidi mwenye nia ya kumdhuru mwingine akisimama kumshtaki mtu kwa uhalifu,

17 watu wawili wanaohusika katika mabishano lazima wasimame mbele zaBwanana mbele ya makuhani na waamuzi ambao wako kazini wakati huo.

18 Waamuzi lazima wafanye uchunguzi kwa makini na shahidi akionekana kuwa ni mwongo, akitoa ushuhuda wa uongo dhidi ya ndugu yake,

19 basi mtende kama alivyotaka kumtendea ndugu yake. Ni lazima mwuondoe uovu miongoni mwenu.

20 Watu watakaosalia watasikia hili na kuogopa, uovu kama huo kamwe hautatendeka tena miongoni mwenu.

21 Msionyeshe huruma, uhai kwa uhai, jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/DEU/19-17631560fea3017c87fda7a33e32af0f.mp3?version_id=1627—

Kumbukumbu La Torati 20

Kwenda Vitani

1 Mtakapokwenda vitani kupigana na adui zenu na mkaona farasi na magari ya vita na jeshi kubwa kuliko lenu, msiwaogope, kwa sababuBwanaMungu wenu aliyewatoa kutoka Misri, atakuwa pamoja nanyi.

2 Wakati mtakapokaribia kwenda vitani, kuhani atakuja mbele na kuhutubia jeshi.

3 Atasema: “Sikia, Ee Israeli, leo unakwenda vitani kupigana na adui zako. Usife moyo wala usiogope, usitishwe wala usitiwe hofu mbele yao.

4 Kwa kuwaBwanaMungu wenu ndiye huenda pamoja nanyi kuwapigania dhidi ya adui zenu na kuwapatia ushindi.”

5 Maafisa wataliambia jeshi: “Je, kuna ye yote aliyejenga nyumba mpya ambayo haijawekwa wakfu? Yeye na arudi nyumbani, ama sivyo anaweza kufa vitani na mtu mwingine akaiweka wakfu.

6 Je, kuna ye yote aliyepanda shamba la mizabibu na hajaanza kulifurahia? Yeye na arudi nyumbani, au sivyo anaweza kufa vitani na mtu mwingine akalifurahia.

7 Je, kuna ye yote aliyeposa mwanamke na hajamwoa? Yeye na arudi nyumbani, ama sivyo anaweza kufa vitani na mtu mwingine akamwoa.”

8 Kisha maafisa wataongeza haya, “Je, kuna mtu anayeogopa ama kufa moyo? Yeye na arudi nyumbani ili ndugu zake nao wasije wakafa moyo pia.”

9 Wakati maafisa watakapomaliza kuzungumza na jeshi, watawateua wakuu wa vikosi.

10 Wakati mtakapokwenda kushambulia mji, wapeni watu wake masharti ya amani.

11 Wakikubali na kuwafungulia malango yao, watu wake wote watawatumikia kwa kufanya kazi ngumu na watawatumikia.

12 Ikiwa watakataa kufanya mapatano ya amani na wakiwaingiza katika vita, basi mtauzunguka mji huo kwa vita.

13 WakatiBwanaMungu wenu atakapouweka mji huo mkononi mwenu, waueni kwa upanga wanaume wote waliomo ndani yake.

14 Kwa upande wa wanawake, watoto, mifugo na kila kitu kingine cho chote ndani ya huo mji, mnaweza kuvichukua kama nyara kwa ajili yenu. Nanyi mnaweza kuzitumia hizo nyara ambazoBwanaMungu wenu amewapa kutoka kwa adui zenu.

15 Hivi ndivyo mtakavyofanya kwa miji yote ambayo iko mbali nanyi, ambayo haimilikiwi na mataifa ya karibu.

16 Hata hivyo, katika miji ya mataifa ambayoBwanaMungu wenu anawapa kama urithi, msiache kitu cho chote hai kinachopumua.

17 Waangamizeni kabisa Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi, kamaBwanaMungu wenu alivyowaamuru.

18 La sivyo, watawafundisha kufuata mambo yote ya machukizo wanayofanya wakiabudu miungu yao, nanyi mtatenda dhambi dhidi yaBwanaMungu wenu.

19 Wakati mtakapouzunguka mji kwa vita kwa muda mrefu, mkipigana dhidi yake ili kuuteka, msiharibu miti yake kwa kuikata kwa shoka, kwa sababu mtaweza kula matunda yake. Hivyo msiikate. Je, miti hiyo ya mashambani ni watu, hata muizingire?

20 Hata hivyo, mnaweza kuikata miti ambayo sio miti ya matunda na kuitumia kujenga ngome, mpaka mji ulio katika vita na ninyi utakapoanguka.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/DEU/20-3a4de4468fde17501e21364fee187822.mp3?version_id=1627—

Kumbukumbu La Torati 21

Upatanisho Kuhusu Mauaji

1 Kama mtu akikutwa ameuawa, naye amelala kwenye shamba katika nchi ambayoBwanaMungu wenu anawapa kuimiliki, wala haijulikani ni nani aliyemwua,

2 wazee wenu na waamuzi watatoka na kupima umbali kutoka maiti alipolala mpaka kwenye miji ya jirani.

3 Kisha wazee wa ule mji uliokaribu zaidi na yule maiti watamchukua mtamba ambaye hajapata kufanyishwa kazi na ambaye hajafungwa nira,

4 na kumpeleka kwenye bonde ambalo halijapata kulimwa au kupandwa mazao na ambapo kuna chemchemi itiririkayo. Huko kwenye hilo bonde watamvunja yule mtamba shingo.

5 Makuhani, hao wana wa Lawi, watasogea mbele, kwa kuwaBwanaMungu wenu, amewachagua kuhudumu na kutoa baraka katika jina laBwana, na kuamua mashauri yote ya mabishano na mashambulio.

6 Ndipo wazee wote wa mji ulio karibu zaidi na huyo maiti watanawa mikono yao juu ya huyo mtamba ambaye shingo yake imevunjwa huko kwenye bonde,

7 nao watatangaza: “Mikono yetu haikumwaga damu hii, wala macho yetu hayakuona likifanyika.

8 EeBwana, ukubali upatanisho kwa watu wako Israeli, ambao umewakomboa, wala usiwahesabie watu wako hatia ya damu ya mtu asiyekuwa na hatia.” Nayo damu iliyomwagika itakuwa imefanyiwa upatanisho.

9 Hivyo mtakuwa mmejitakasa wenyewe kutoka hatia ya kumwaga damu isiyokuwa na hatia, kwa kuwa mmefanya lile lililo sawa mbele za macho yaBwana.

Kuoa Mwanamke Mateka

10 Mkienda vitani kupigana na adui zenu nayeBwanaMungu wenu akawatia adui mikononi mwenu, nanyi mkachukua mateka,

11 kama ukiona miongoni mwa mateka mwanamke mzuri wa sura nawe wavutwa naye, waweza kumwoa akawa mke wako.

12 Mlete nyumbani mwako, anyoe nywele na kukata kucha zake,

13 avue nguo alizokuwa amevaa alipotekwa. Baada ya kuishi nyumbani mwako na kumwombolezea baba yake na mama yake kwa mwezi mzima, ndipo utakapoweza kumwendea na kuwa mume wake naye atakuwa mke wako.

14 Lakini kama hutaendelea kupendezwa naye, mwache aende po pote anapotaka. Kamwe huwezi kumuuza au kumtendea kama mtumwa, kwa sababu utakuwa umemvunjia heshima.

Haki Ya Mzaliwa Wa Kwanza

15 Kama mwanaume ana wake wawili, naye anampenda mmoja na mwingine hampendi na wote wawili wamemzalia wana wa kiume, lakini mwana mzaliwa wa kwanza ni wa yule mke asiyempenda,

16 wakati anapotoa wosia wa mali yake kwa wanawe, kamwe asitoe haki za mzaliwa wa kwanza kwa mwana wa mke ampendaye kwa upendeleo, badala ya mzaliwa hasa wa kwanza, ambaye ni mwana wa mke ambaye hampendi.

17 Ni lazima amkubali mwana wa mke asiyempenda kama mzaliwa wa kwanza kwa kumpa sehemu ya vile vyote alivyonavyo maradufu. Mwana huyo ni ishara ya kwanza ya nguvu za baba yake. Haki ya mzaliwa wa kwanza ni yake yeye.

Mwana Mwasi

18 Kama mtu ana mwana mkaidi na mwasi ambaye hamtii baba yake na mama yake, na hasikii wazazi wanapomrudi,

19 baba yake na mama yake watamleta kwa wazee kwenye lango la mji wake.

20 Watawaambia wazee, “Huyu mwanetu ni mkaidi na mwasi. Hatutii sisi, yeye ni mpotovu na mlevi.”

21 Kisha wanaume wote wa mjini mwake watampiga kwa mawe mpaka afe. Ndivyo imewapasa kuondoa maovu kati yenu. Israeli yote itasikia hili na kuogopa.

Sheria Mbalimbali

22 Kama mtu ana hatia ya kosa linalompasa kuuawa naye akauawa, mwili wake utaangikwa mtini,

23 kamwe msiuache mwili wake mtini usiku kucha. Hakikisheni mnauzika mwili wake siku ile ile, kwa sababu kila mtu anayeangikwa mtini yupo chini ya laana ya Mungu. Msiinajisi nchi ambayoBwanaMungu wenu anawapa kama urithi wenu.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/DEU/21-c7d6cd2392c23cd0f166dbea026bbcb9.mp3?version_id=1627—

Kumbukumbu La Torati 22

1 Kama ukimwona ng’ombe au kondoo wa ndugu yako anapotea, usipuuze, bali uhakikishe unamrudisha kwa mwenyewe.

2 Ikiwa huyo ndugu haishi karibu nawe au kama hufahamu yeye ni nani, mchukue nyumbani kwako huyo mnyama umweke mpaka mwenyewe aje kumtafuta. Ndipo umrudishie.

3 Fanya vivyo hivyo ukimkuta punda wa nduguyo au joho lake au cho chote alichopoteza. Usipuuze jambo hilo.

4 Kama ukimwona punda wa nduguyo au ng’ombe wake ameanguka barabarani, usipuuze jambo hilo. Msaidie asimame kwa miguu yake.

5 Haimpasi mwanamke kuvaa nguo za kiume wala mwanaume kuvaa nguo za kike, kwa maanaBwanaMungu wenu anachukia ye yote ambaye hufanya hivi.

6 Kama ukikuta kiota cha ndege kando ya barabara, iwe juu ya mti au chini, naye ndege amelala juu ya makinda au mayai, usimchukue huyo ndege pamoja na makinda yake.

7 Waweza kuchukua makinda, lakini uwe na hakika ya kumwacha huyo ndege, ili upate kufanikiwa na uweze kuishi maisha marefu.

8 Wakati unapojenga nyumba mpya, fanya ukuta wa kuzuia kandokando ya dari ili usijiletee hatia ya kumwaga damu juu ya nyumba yako ikiwa ye yote ataanguka kutoka humo.

9 Usipande aina mbili za mbegu katika shamba lako la mizabibu; ikiwa utafanya hivyo, si mazao utakayopanda tu yatakuwa najisi, bali nayo matunda ya shamba la mizabibu pia.

10 Usilime kwa maksai aliyefungwa nira pamoja na punda.

11 Usivae nguo za sufu na kitani zilizofumwa pamoja.

12 Fanya vishada kwenye pembe nne za joho unalovaa.

Kukiuka Taratibu Za Ndoa

13 Ikiwa mtu atamwoa mke na, baada ya kufanya naye tendo la ndoa, akamchukia,

14 akimsingizia na kumwita jina baya, akisema, “Nilimwoa mwanamke huyu, lakini nilipomkaribia sikupata uthibitisho wa ubikira wake”

15 ndipo baba na mama wa msichana wataleta uthibitisho kwamba alikuwa bikira kwa wazee wa mji kwenye lango.

16 Baba wa msichana atawaambia wazee, “Nilimwoza binti yangu kwa huyu mwanaume, lakini hampendi.

17 Sasa amemsingizia na kusema, ‘Sikumkuta huyu binti akiwa bikira.’ Lakini hapa kuna uthibitisho wa ubikira wa binti yangu.” Kisha wazazi wake wataonyesha nguo zake kwa wazee wa mji,

18 nao wazee watamchukua huyo mwanaume na kumwadhibu.

19 Watamtoza shekeli mia mojaza fedha na kupewa wazazi wa msichana, kwa sababu mwanaume huyu amempa bikira wa Kiisraeli jina baya. Ataendelea kuwa mke wake; kamwe hawezi kumpa talaka siku zote za maisha yake.

20 Hata hivyo, kama shtaka ni la kweli na hakuna uthibitisho juu ya ubikira wa huyo msichana ulioweza kupatikana,

21 huyo msichana ataletwa kwenye mlango wa nyumba ya baba yake, na hapo watu wa mji wake watampiga kwa mawe hadi afe. Amefanya kitu cha aibu katika Israeli kwa kutokuwa na utaratibu wakati akiwa nyumbani kwa babaye. Lazima mwondoe uovu katikati yenu.

22 Ikiwa mwanaume atakutwa akizini na mke wa mtu mwingine, wote wawili, mwanaume na mwanamke aliyezini naye, lazima wauawe. Lazima mwondoe uovu katika Israeli.

23 Ikiwa mwanaume atakutana na bikira mjini ambaye ameposwa na mtu akazini naye,

24 utawachukua wote wawili kwenye lango la mji na kuwapiga kwa mawe mpaka wafe; yule msichana kwa kuwa alikuwa mjini na hakupiga kelele kuomba msaada, na yule mwanaume kwa sababu amemtenda jeuri mke wa mtu mwingine. Lazima mwondoe uovu katikati yenu.

25 Lakini ikiwa itatokea mwanaume akakutana na msichana aliyeposwa huko mashambani, akambaka, mwanaume aliyefanya hivi peke yake ndiye atakayeuawa.

26 Usimtendee msichana yule jambo lo lote; hajafanya dhambi inayostahili kifo. Shauri hili ni kama lile la ye yote ambaye anamshambulia na kumwua kwa makusudi jirani yake,

27 kwa maana mwanaume huyo alimkuta msichana huko mashambani, na ingawa msichana aliyeposwa alipiga kelele, hapakuwa na mtu wa kumwokoa.

28 Ikiwa itatokea mwanaume akutane na bikira ambaye hajaposwa na kumbaka nao wakakutwa,

29 mwanaume atamlipa baba wa msichana shekeli hamsiniza fedha. Ni lazima amwoe huyo msichana, kwa maana amemfanyia jeuri. Kamwe hawezi kumpa talaka siku zote za maisha yake.

30 Mwanaume asimwoe mke wa baba yake; kamwe asidhalilishe kitanda cha baba yake.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/DEU/22-a5dbdccab002c86593a6a6accc4bd6b4.mp3?version_id=1627—

Kumbukumbu La Torati 23

Kutengwa Na Mkutano

1 Asiingie mtu ye yote aliyehasiwa kwa kupondwa makende au kwa kukatwa uume wake katika kusanyiko laBwana.

2 Mtu ye yote ambaye amezaliwa kwenye ndoa isiyo halali au wazao wake wasiingie kwenye kusanyiko laBwana, hata mpaka kizazi cha kumi.

3 Hapatakuwa na Mwamori au Mmoabi au ye yote wa wazao wao atakayeruhusiwa kuingia katika kusanyiko laBwana, hata mpaka kizazi cha kumi.

4 Kwa kuwa hawakuja kuwalaki wakiwa na mkate na maji mlipokuwa njiani mlipotoka Misri, tena walimwajiri Balaamu mwana wa Beori kutoka Pethori iliyoko Aramu-Naharaimuili kuwalaani ninyi.

5 Hata hivyo,BwanaMungu wenu hakumsikiliza Balaamu bali aligeuza laana kuwa baraka kwenu kwa sababuBwanaMungu wenu anawapenda.

6 Msitafute mapatano ya urafiki nao maisha yenu yote.

7 Usimchukie Mwedomu, kwa kuwa yeye ni ndugu yako. Usimchukie Mmisri, kwa sababu uliishi kama mgeni katika nchi yake.

8 Kizazi cha tatu cha watoto watakaozaliwa nao wanaweza kuingia katika kusanyiko laBwana.

Unajisi Katika Kambi

9 Unapokuwa umepiga kambi dhidi ya adui zako, jitenge na kitu cho chote kisicho safi.

10 Ikiwa mtu amechafuka kwa sababu ya kutokwa na shahawa usiku, inampasa atoke nje ya kambi na kukaa huko.

11 Lakini jioni ikikaribia ataoga, na baada ya jua kuzama ataingia tena kambini.

12 Tengeni mahali nje ya kambi ambapo mnaweza kwenda kujisaidia.

13 Kama sehemu ya vifaa vyenu iweni na kitu cha kulimia, nanyi mnapojisaidia, chimba shimo na kisha funika kile kikutokacho.

14 Kwa kuwaBwanaMungu wenu hutembea katika kambi yenu ili kuwalinda na kuwaweka adui zenu mikononi mwenu. Kambi yenu ni lazima iwe takatifu, ili asione kitu cho chote miongoni mwenu kilicho kichafu akageuka na kuwaacha.

Sheria Mbalimbali

15 Ikiwa mtumwa amekimbilia kwako, usimrudishe kwa bwana wake.

16 Mwache aishi miongoni mwenu mahali po pote anapopapenda na katika mji wo wote anaochagua. Usimwonee.

17 Asiwepo Mwisraeli mwanamke kahaba au mwanaume hanithi wa mahali pa kuabudia miungu.

18 Kamwe usilete mapato ya ukahaba ikiwa ni ya mwanamke au ni ya mwanaume katika nyumba yaBwanaMungu wako kwa ajili ya nadhiri yo yote, kwa sababuBwanaMungu wako anachukizwa na yote mawili.

19 Usimtoze ndugu yako riba, iwe ni fedha ama chakula ama kitu kingine cho chote ambacho waweza kupata riba juu yake.

20 Unaweza kumtoza mgeni riba, lakini siyo nduguyo Mwisraeli, ili kwambaBwanaMungu wako akubariki katika kila kitu unachoweka mkono katika nchi unayoiingia kuimiliki.

21 Ukiweka nadhiri kwaBwanaMungu wako, usichelewe kuitimiza, kwa kuwaBwanaMungu wako atakudai, nawe utakuwa na hatia ya dhambi.

22 Lakini ukijizuia kuweka nadhiri, hutakuwa na hatia.

23 Cho chote kitakachotamkwa kwa midomo yako ni lazima uhakikishe umekifanya, kwa sababu uliweka nadhiri yako kwa hiari mbele zaBwanaMungu wako kwa kinywa chako mwenyewe.

24 Kama ukiingia katika shamba la mizabibu la jirani yako, unaweza kula zabibu kadiri utakavyo, lakini usiweke cho chote kwenye kikapu chako.

25 Kama ukiingia katika shamba la nafaka la jirani yako, unaweza kukwanyua kwa mikono yako, lakini usikate kwa mundu nafaka iliyosimama.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/DEU/23-53383c563ac1f5e66e79b39871b3173e.mp3?version_id=1627—

Kumbukumbu La Torati 24

Sheria Kuhusu Ndoa Na Talaka

1 Ikiwa mtu atamwoa mke na akamchukia kwa sababu ya kukosa adabu, akamwandikia hati ya talaka, akampa na kumfukuza kutoka nyumbani kwake,

2 ikiwa baada ya kuondoka nyumbani kwake atakuwa mke wa mtu mwingine,

3 ikiwa mume wake wa pili atachukizwa naye akamwandikia hati ya talaka, akampa na kumfukuza kutoka nyumbani kwake, au kama akifa,

4 basi yule mume wake wa kwanza, ambaye alimpa talaka, haruhusiwi kumwoa tena baada ya mwanamke huyo kuwa najisi. Hayo yatakuwa machukizo machoni paBwana. Usilete dhambi juu ya nchi ambayoBwanaMungu wako anakupa kama urithi.

5 Kama mtu ameoa karibuni, kamwe asipelekwe vitani au kupewa wajibu mwingine wo wote. Kwa mwaka mmoja atakuwa huru kubaki nyumbani ili amfurahishe mke aliyemwoa.

6 Usitoe jozi ya mawe ya kusagia, hata ikiwa lile la juu, kuweka rehani kwa ajili ya deni, kwa sababu itakuwa ni kuweka uhai wa mtu kama dhamana.

7 Kama mtu akikamatwa akiiba ye yote miongoni mwa ndugu zake wa Waisraeli na kumtenda kama mtumwa au akimwuza, mwizi huyo ni lazima auawe. Nawe utaondoa uovu kutoka miongoni mwenu.

8 Pakitokea magonjwa ya ngozi ya kuambukiza, mwe waangalifu sana kufanya sawasawa na maagizo ya makuhani, ambao ni Walawi. Ni lazima mfuate kwa uangalifu yale niliyowaamuru.

9 Kumbukeni kileBwanaMungu wenu alichomfanyia Miriamu njiani baada ya ninyi kutoka Misri.

10 Unapomkopesha jirani yako cho chote, usiingie nyumbani kwake kutwaa kile anachokitoa kama rehani.

11 Ukae nje na umwache huyo mtu uliyemkopesha akuletee hiyo rehani.

12 Ikiwa mtu huyo ni maskini, usiende kulala ukiwa na hiyo rehani yake katika milki yako.

13 Rudisha vazi lake kabla ya machweo ya jua ili apate kulilalia. Kisha atakushukuru na kitaonekana kama kitendo cha haki mbele zaBwanaMungu wako.

14 Usimwonee mtu maskini na mhitaji ambaye umemwajiri, akiwa ni nduguyo Mwisraeli au mgeni anayeishi katika mojawapo ya miji yenu.

15 Mlipe ujira wake kila siku kabla ya jua kutua, kwa sababu yeye ni maskini na anautegemea ujira huo. La sivyo, anaweza kumliliaBwanadhidi yako, nawe ukapata hatia ya dhambi.

16 Baba wasiuawe kwa ajili ya watoto wao, wala watoto wasiuawe kwa ajili ya baba zao; kila mmoja atakufa kwa ajili ya dhambi yake mwenyewe.

17 Usipotoshe hukumu ya mgeni au yatima, au kuchukua vazi la mjane kama rehani.

18 Kumbukeni kwamba mlikuwa watumwa huko Misri, nayeBwanaMungu wenu akawakomboa kutoka huko. Hii ndiyo sababu ninawaamuru kutenda hili.

19 Unapovuna shamba lako na ukasahau mganda, usirudi kuuchukua. Acha kwa ajili ya mgeni, yatima na mjane, iliBwanaMungu wako aweze kukubariki wewe katika kazi zote za mikono yako.

20 Unapovuna zeituni kutoka katika miti yako, usirudie matawi mara ya pili. Acha kilichobaki kwa ajili ya mgeni, yatima na mjane.

21 Unapochuma zabibu katika shamba lako la mizabibu usirudie tena. Acha zinazobaki kwa ajili ya mgeni, yatima na mjane.

22 Kumbuka kwamba mlikuwa watumwa katika nchi ya Misri. Ndiyo sababu ninawaamuru kufanya hili.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/DEU/24-bae5375b07ac98e1f0ea5c5d90ebfdea.mp3?version_id=1627—

Kumbukumbu La Torati 25

1 Watu wanapokuwa na ugomvi, wapeleke mahakamani na waamuzi wataamua shauri hilo; watawaachia wasio na kosa na kuwahukumu wenye hatia.

2 Kama mtu mwenye hatia anastahili kuchapwa, mwamuzi atamwamuru alale chini ili achapwe mbele yake idadi ya viboko kulingana na kosa lake,

3 lakini kamwe asichapwe zaidi ya viboko arobaini. Ikiwa atachapwa zaidi ya viboko arobaini, nduguyo atadhalilika machoni pako.

4 Usimfunge maksai kinywa anapopura nafaka.

5 Ikiwa ndugu wanaishi pamoja na mmoja wao akafa bila kuacha mwana, kamwe mjane wake asiolewe nje ya jamaa hiyo. Ndugu wa mumewe atamchukua amwoe na kutimiza wajibu wa shemeji kwake.

6 Mwana wa kwanza atakayemzaa atapewa jina la ndugu aliyekufa ili jina lake lisifutike katika Israeli.

7 Hata hivyo, ikiwa ndugu huyo wa mume hataki kuoa huyo mke wa nduguye, mjane atawaendea wazee kwenye lango la mji na kusema, “Ndugu wa mume wangu anakataa kuendeleza jina la nduguye katika Israeli. Hataki kutimiza wajibu wa shemeji kwangu.”

8 Ndipo wazee wa mji wake watamwita na kuzungumza naye. Kama atashikilia kukataa akisema, “Sitaki kumwoa,”

9 mjane wa nduguye atamwendea mbele ya wazee, atamvua kiatu kimoja na kumtemea mate usoni, na kusema, “Hivi ndivyo ambavyo hufanywa kwa mtu ambaye atakataa kuendeleza jamaa ya ndugu yake.”

10 Jamaa ya mtu huyo itafahamika katika Israeli kama Jamaa ya Aliyevuliwa Kiatu.

11 Ikiwa watu wawili wanapigana na mke wa mmoja wao akaja kumwokoa mumewe na yule anayemshambulia, naye mke huyo akifika na kumkamata sehemu za siri,

12 huyo mwanamke utamkata mkono wake. Usimhurumie.

13 Usiwe na mawe ya kupimia ya aina mbili katika mkoba wako, moja zito na jingine jepesi.

14 Usiwe na vipimo viwili tofauti katika nyumba yako, kimoja kikubwa, kingine kidogo.

15 Ni lazima uwe na uzito na vipimo sahihi na vya haki, ili upate kuishi maisha marefu katika nchi anayokupaBwanaMungu wako.

16 Kwa maanaBwanaMungu wako humchukia ye yote ambaye hufanya mambo kama haya, ye yote anayetenda kwa udanganyifu.

17 Kumbuka kile Waamaleki walichowatendea mlipokuwa njiani mkitoka Misri.

18 Wakati mlipokuwa mmechoka na kuishiwa nguvu kwa safari yenu, wakawapiga wale wote waliokuja nyuma. Waamaleki hawakumwogopa Mungu.

19 BwanaMungu wako atakapokupa pumziko mbali na adui zako wote wanaokuzunguka katika nchi akupayo kuimiliki kuwa urithi, utafutilia mbali kumbukumbu lote la Waamaleki chini ya mbingu. Usisahau!

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/DEU/25-a69a9ede5b6c28f1d8fb30b623580e89.mp3?version_id=1627—

Kumbukumbu La Torati 26

Malimbuko Na Zaka

1 Mtakapokuwa mmeingia nchi ile ambayoBwanaMungu wenu anawapa kama urithi na mtakapokuwa mmeimiliki na kukaa ndani yake,

2 chukueni baadhi ya mavuno ya kwanza ya yale yote mtakayozalisha kutoka udongo wa nchi ambayoBwanaMungu wenu anawapa na mweke kwenye kapu. Kisha uende mahali ambapoBwanaMungu wako atapachagua kuwa makao kwa ajili ya Jina lake

3 na umwambie kuhani atakayekuwapo kwa wakati huo, “Ninatangaza leo kwaBwanaMungu wako kwamba nimekuja katika nchi ambayoBwanaaliwaapia baba zetu kwamba atatupa.”

4 Kuhani atapokea lile kapu mikononi mwako na kuliweka chini mbele ya madhabahu yaBwanaMungu wako.

5 Kisha utatangaza mbele zaBwanaMungu wako: “Baba yangu alikuwa Mwarami aliyekuwa anatangatanga, akaenda Misri pamoja na watu wachache akaishi huko akawa taifa kubwa, lenye nguvu na watu wengi.

6 Lakini Wamisri walituonea na kututaabisha, wakitufanyisha kazi ngumu.

7 Kisha tulimliliaBwana, Mungu wa baba zetu, nayeBwanaakasikia sauti yetu na akaona huzuni yetu, taabu yetu na mateso yetu.

8 Kwa hiyoBwanaakatutoa nchi ya Misri kwa mkono wenye nguvu na ulionyooshwa, pamoja na utisho mkuu, ishara za miujiza na maajabu.

9 Akatuleta mahali hapa akatupa nchi hii, nchi inayotiririka maziwa na asali;

10 nami sasa ninaleta malimbuko ya ardhi ambayo wewe, EeBwana, umenipa.” Weka kapu mbele zaBwanaMungu wako na usujudu mbele zake.

11 Kisha wewe pamoja na Walawi na wageni wote walioko miongoni mwenu mtafurahi katika vitu vyote vizuri ambavyoBwanaMungu wenu amewapa pamoja na wa nyumbani mwenu.

12 Wakati utakapokuwa umeshatoa zaka zote za mazao yako katika mwaka wa tatu, ambao ni mwaka wa zaka, utampa Mlawi, mgeni, yatima na mjane, ili waweze kula katika miji yenu na kushiba.

13 Kisha umwambieBwanaMungu wako: “Nimeondoa katika nyumba yangu ile sehemu iliyowekwa wakfu na nimempa Mlawi, mgeni, yatima na mjane, kulingana na yote uliyoamuru. Sijazihalifu amri zako wala kusahau hata mojawapo.

14 Sijala sehemu iliyowekwa wakfu wakati nilipokuwa nikiomboleza, wala sijaondoa mojawapo wakati nilipokuwa najisi, wala sijatoa sehemu yake yo yote kwa wafu. NimemtiiBwanaMungu wangu; nimefanya kila kitu ulichoniamuru.

15 Angalia chini kutoka mbinguni, maskani yako matakatifu, uwabariki watu wako Israeli pamoja na nchi uliyotupa kama ulivyoahidi kwa kiapo kwa baba zetu, nchi inayotiririka maziwa na asali.”

Fuata Maagizo Ya Bwana

16 BwanaMungu wako anakuagiza leo kufuata amri hizi na sheria; zishike kwa bidii kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote.

17 Umetangaza leo kwambaBwanandiye Mungu wako na kwamba utafuata njia zake, kwamba utayashika maagizo yake, amri zake na sheria zake nawe utamtii.

18 NayeBwanaametangaza leo kwamba ninyi ni taifa lake, hazina yake ya thamani kama alivyoahidi, ili kwamba mpate kuyashika maagizo yake yote.

19 Ametangaza kwamba atawaweka juu kuliko mataifa mengine aliyoyafanya katika sifa, kuwa fahari na heshima, na kwamba mtakuwa taifa takatifu kwaBwanaMungu wenu, kama alivyoahidi.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/DEU/26-beb6ce991e82a641bc01c2e5844202a8.mp3?version_id=1627—

Kumbukumbu La Torati 27

Madhabahu Katika Mlima Ebali

1 Mose na wazee wa Israeli wakawaagiza watu: “Yashikeni maagizo haya yote ninayowaagiza leo.

2 Mtakapokuwa mmevuka Mto Yordani na kuingia katika nchi awapayoBwanaMungu wenu, msimamishe mawe makubwa na mkayatie lipu.

3 Andikeni juu yake maneno yote ya sheria hii wakati mtakapokuwa mmevuka na kuingia katika nchi awapayoBwanaMungu wenu, nchi itiririkayo maziwa na asali, kama vileBwana, Mungu wa baba zenu, alivyowaahidi.

4 Mtakapokuwa mmevuka Yordani, simamisheni mawe haya juu ya Mlima Ebali, kama ninavyowaagiza leo, mkayatie lipu.

5 Huko mjengeeniBwanaMungu wenu madhabahu, madhabahu ya mawe. Msitumie kifaa cho chote cha chuma juu yake.

6 Jengeni madhabahu yaBwanaMungu wenu kwa mawe ya shambani, na mtoe sadaka za kuteketezwa juu yake kwaBwanaMungu wenu.

7 Toeni sadaka za amani juu yake, mkizila na kufurahia mbele zaBwanaMungu wenu.

8 Nanyi mtaandika maneno yote ya sheria hii kwa wazi sana juu ya mawe haya ambayo mmesimamisha.”

Laana Kutoka Mlima Ebali

9 Kisha Mose na makuhani, ambao ni Walawi, wakawaambia Israeli wote, “Nyamaza Ee Israeli, sikiliza! Sasa umekuwa taifa laBwanaMungu wako.

10 MtiiBwanaMungu wako, na kufuata amri zake na maagizo ninayokupa leo.”

11 Siku ile ile Mose akawaagiza watu:

12 Mtakapovuka Mto Yordani, makabila haya yatasimama juu ya Mlima Gerizimu kubariki watu: Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari, Yosefu na Benyamini.

13 Makabila haya yatasimama juu ya Mlima Ebali kwa kutamka laana: Reubeni, Gadi, Asheri, Zabuloni, Dani na Naftali.

14 Nao Walawi watawasomea watu wote wa Israeli kwa sauti kubwa:

15 “Alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga au mwenye kusubu sanamu, kitu ambacho ni chukizo kwaBwana, kazi ya mikono ya fundi stadi, na kuisimamisha kwa siri.”

Kisha watu wote watasema, “Amen!”

16 “Alaaniwe mtu amdharauye baba yake na mama yake.”

Kisha watu wote watasema, “Amen!”

17 “Alaaniwe mtu asogezaye jiwe la mpaka wa jirani yake.”

Kisha watu wote watasema, “Amen!”

18 “Alaaniwe mtu ampotoshaye kipofu njiani.”

Kisha watu wote watasema, “Amen!”

19 “Alaaniwe mtu apotoshaye haki ya mgeni, yatima au mjane.”

Kisha watu wote watasema, “Amen!”

20 “Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na mke wa baba yake, kwa maana anadharau malazi ya baba yake.”

Kisha watu wote watasema, “Amen!”

21 “Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na mnyama ye yote.”

Kisha watu wote watasema, “Amen!”

22 “Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na dada yake, binti wa baba yake au binti wa mama yake.”

Kisha watu wote watasema, “Amen!”

23 “Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na mama mkwe wake.”

Kisha watu wote watasema, “Amen!”

24 “Alaaniwe mtu amuuaye jirani yake kwa siri.”

Kisha watu wote watasema, “Amen!”

25 “Alaaniwe mtu apokeaye rushwa ili kumwua mtu asiye na hatia.”

Kisha watu wote watasema, “Amen!”

26 “Alaaniwe mtu ambaye hatashika maneno haya ya sheria hii kwa kuyafanya.”

Kisha watu wote watasema, “Amen!”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/DEU/27-39b6836bc29112f6af7d77339696ec95.mp3?version_id=1627—

Kumbukumbu La Torati 28

Baraka Kwa Ajili Ya Utii

1 Kama ukimtiiBwanaMungu wako kwa bidii na kufuata amri zake zote ninazokupa leo kwa bidii,BwanaMungu wako atakuweka juu ya mataifa yote katika dunia.

2 Baraka hizi zote zitakuja juu yako na kukupata, kama ukimtiiBwanaMungu wako:

3 Utabarikiwa mjini na utabarikiwa mashambani.

4 Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na mazao ya nchi yako na wanyama wako wachanga wa kufugwa, yaani ndama wa makundi yako ya ng’ombe, na wana-kondoo wa makundi yako.

5 Kapu lako na vyombo vyako vya kukandia vitabarikiwa.

6 Utabarikiwa uingiapo na utabarikiwa utokapo.

7 Bwanaatasababisha adui wainukao dhidi yako kushindwa mbele yako. Watakujia kwa njia moja lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba.

8 Bwanaataagiza baraka juu ya ghala zako na juu ya kila kitu utakachogusa kwa mkono wako.BwanaMungu wako atakubariki katika nchi anayokupa.

9 Bwanaatakufanya kuwa taifa lake takatifu, kama alivyokuahidi kwa kiapo, kama ukishika maagizo yaBwanaMungu wako na kwenda katika njia zake.

10 Kisha mataifa yote ya dunia wataona kuwa unaitwa kwa jina laBwana, nao watakuogopa.

11 Bwanaatakupa kustawi kwa wingi, katika tunda la uzao wa tumbo lako, katika wanyama wachanga wa mifugo yako na katika mazao ya ardhi yako, katika nchi aliyowaapia baba zako kuwapa.

12 Bwanaatafungua mbingu, ghala zake za baraka, kukupa mvua kwa majira yake na kubariki kazi zako zote za mikono yako. Utakopesha mataifa mengi lakini hutakopa kwa ye yote.

13 Bwanaatakufanya kichwa, wala si mkia. Kama utazingatia maagizo yaBwanaMungu wako ninayokupa siku hii ya leo na kuyafuata kwa bidii, daima utakuwa juu, kamwe hutakuwa chini.

14 Usihalifu amri zangu zo zote ninazokupa leo, kwa kwenda kuume au kushoto, kwa kufuata miungu mingine na kuitumikia.

Laana Kwa Kutokutii

15 Hata hivyo, kama hutamtiiBwanaMungu wako na kuzishika kwa bidii amri zake zote na maagizo ninayokupa leo, laana hizi zote zitakuja juu yako na kukupata:

16 Utalaaniwa mjini na utalaaniwa mashambani.

17 Kapu lako na chombo chako cha kukandia kitalaaniwa.

18 Uzao wa tumbo lako utalaaniwa, mazao ya ardhi yako, ndama wa makundi yako ya ng’ombe na wana-kondoo wa makundi yako.

19 Utalaaniwa uingiapo na utokapo.

20 Bwanaataleta laana juu yako, fadhaa na kukaripiwa katika kila kitu unachokigusa kwa mkono wako, mpaka uwe umeharibiwa na kuangamizwa ghafula kwa ajili ya maovu uliyoyafanya kwa kumwacha yeye.

21 Bwanaatakupiga kwa magonjwa mpaka akuangamize kutoka katika nchi unayoiingia kuimiliki.

22 Bwanaatakupiga kwa magonjwa ya kudhoofisha, kwa homa na kuwashwa, hari na kwa ukame, kutu na kuwa na uchungu ambavyo vitakupiga mpaka uangamie.

23 Anga juu yako itakuwa shaba, na ardhi chini yako itakuwa chuma.

24 Bwanaatafanya mvua ya nchi yako kuwa mavumbi na mchanga; vitakujia kutoka angani mpaka uangamie.

25 Bwanaatakufanya ushindwe mbele ya adui zako. Utawajia kwa njia moja lakini utawakimbia mbele yao kwa njia saba, nawe utakuwa kitu cha kuchukiza kwa falme zote za dunia.

26 Mizoga yenu itakuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wa nchi, wala hapatakuwepo mtu ye yote wa kuwafukuza.

27 Bwanaatakupiga kwa majipu ya Misri na kwa vidonda vitokavyo usaha na kuwashwa, ambako huwezi kuponywa.

28 Bwanaatakupiga kwa wazimu, upofu na kuchanganyikiwa kwa akili.

29 Wakati wa adhuhuri utapapasapapasa huko na huko kama mtu kipofu katika giza. Hutafanikiwa katika lo lote ufanyalo; siku baada ya siku utaonewa na kunyang’anywa, wala hakuna ye yote atakayekuokoa.

30 Utaposa mke, lakini mtu mwingine atakutana naye kimwili. Utajenga nyumba, lakini hutaishi ndani yake. Utapanda shamba la mizabibu, lakini hutakula matunda yake.

31 Ng’ombe wako atachinjwa mbele ya macho yako lakini hutakula nyama yake. Punda wako atachukuliwa kwa nguvu kutoka kwako wala hatarudishwa. Kondoo wako watapewa adui zako, wala hakuna mtu ye yote wa kuwaokoa.

32 Wanao na binti zako watatolewa kwa mataifa mengine, nawe utayachosha macho yako ukiwatazamia siku baada ya siku, hutakuwa na nguvu kuinua mkono.

33 Taifa usilolijua watakula mazao ya nchi yako na taabu ya kazi yako, hutakuwa na cho chote, bali kuonewa kikatili siku zako zote.

34 Vitu utakavyoviona kwa macho yako vitakufanya wazimu.

35 Bwanaatayapiga magoti yako na miguu yako kwa majipu yenye maumivu makali yasiyoponyeka, yakienea kutoka nyayo za miguu yako hadi utosini.

36 Bwanaatakupeleka wewe na mfalme uliyemweka juu yako uende kwenye taifa ambalo hukulijua wewe wala baba zako. Huko utaabudu miungu mingine, miungu ya miti na mawe.

37 Utakuwa kitu cha kuchukiza, tena kitu cha kudharauliwa na kudhihakiwa kwa mataifa yote hukoBwanaatakakokupeleka.

38 Utapanda mbegu nyingi katika shamba lakini utavuna haba, kwa sababu nzige watazila.

39 Utapanda mashamba ya mizabibu na kuyapalilia, lakini hutakunywa divai yake wala hutakusanya zabibu, kwa sababu wadudu watazila.

40 Utakuwa na mizeituni katika nchi yako yote, lakini hutatumia hayo mafuta yake, kwa sababu zeituni zitapukutika.

41 Utakuwa na wana na binti lakini hawatakuwa nawe, kwa sababu watachukuliwa mateka.

42 Makundi ya nzige yatavamia miti yako yote na mazao ya nchi yako.

43 Mgeni anayeishi miongoni mwako atainuka juu zaidi na zaidi kuliko wewe, lakini wewe utashuka chini zaidi na zaidi.

44 Yeye atakukopesha, lakini wewe hutamkopesha. Yeye atakuwa kichwa, lakini wewe utakuwa mkia.

45 Laana hizi zote zitakuja juu yako. Zitakufuatia na kukupata mpaka uangamizwe, kwa sababu hukumtiiBwanaMungu wako, na kuzishika amri zake na maagizo yake aliyokupa.

46 Zitakuwa ishara na ajabu kwako na kwa wazao wako milele.

47 Kwa sababu hukumtumikiaBwanaMungu wako kwa furaha na kwa moyo wakati wa kufanikiwa kwako,

48 kwa hiyo katika njaa na kiu, katika uchi na umaskini wa kutisha, utawatumikia adui ambaoBwanaatawatuma dhidi yako. Yeye ataweka nira ya chuma shingoni mwako hadi amekwisha kukuangamiza.

49 Bwanaataleta taifa dhidi yako kutoka mbali, kutoka miisho ya dunia, kama tai ashukiavyo mawindo chini, taifa ambalo hutaijua lugha yake,

50 taifa lenye uso mkali lisilojali wazee wala kuwahurumia vijana.

51 Watakula wadogo wa mifugo yako na mazao ya nchi yako mpaka umeangamia. Hawatakuachia nafaka, divai mpya au mafuta, wala ndama wo wote wa kundi lako au wana-kondoo wa kundi lako mpaka umekuwa magofu.

52 Nao wataizingira miji yote katika nchi yako mpaka kuta ndefu za ngome ambazo unazitegemea zimeanguka. Watazingira miji yote katika nchi ambayoBwanaMungu wako anakupa.

53 Utakula uzao wa tumbo lako, nyama ya wana wako na binti zako ambaoBwanaMungu wako amekupa, kwa sababu ya mateso yale adui zako watakayokuletea wakati wa kukuzingira.

54 Hata yule mtu mwungwana sana na makini miongoni mwako hatakuwa na huruma kwa ndugu yake mwenyewe au kwa mke ampendaye au watoto wake waliosalia,

55 naye hatampa hata mmoja wao nyama ya watoto wake ambao anawala. Kwa kuwa hakuna kitu kingine kilichosalia kwake katika mazingiwa makali ambayo adui yako watakuletea kwa miji yako yote.

56 Mwanamke ambaye ni muungwana sana na makini miongoni mwako, yaani ambaye ni makini sana na muungwana kiasi kwamba asingethubutu kugusa ardhi kwa wayo wa mguu wake, yeye atakuwa mchoyo kwa mume ampendaye na mwanawe mwenyewe au binti yake,

57 kondoo la nyuma kutoka kwenye tumbo lake na watoto anaowazaa. Kwa kuwa anakusudia kuwala kwa siri wakati wa kuzingirwa na katika taabu zile ambazo adui yako atazileta juu yako na miji yako.

58 Kama hutafuata kwa bidii maneno yote ya sheria hii, ambayo yameandikwa katika kitabu hiki na kama hutalicha hili jina la fahari na la kutisha, yaani laBwanaMungu wako,

59 Bwanaataleta mapigo ya kutisha juu yako na kwa wazao wako, maafa makali na ya kudumu, magonjwa mazito na ya kudumu.

60 Atakuletea juu yako magonjwa yote ya Misri yale uliyoyaogopa, nayo yataambatana nawe.

61 PiaBwanaatakuletea kila aina ya ugonjwa na maafa ambayo hayakuandikwa humu katika kitabu hiki cha sheria, mpaka utakapokuwa umeangamizwa.

62 Ninyi ambao mlikuwa wengi kama nyota za angani mtaachwa wachache tu, kwa sababu hamkumtiiBwanaMungu wenu.

63 Kama ilivyompendezaBwanakuwafanya ninyi mstawi na kuongezeka kwa idadi, ndivyo itakavyompendeza kuwaharibu na kuwaangamiza ninyi. Mtang’olewa kutoka katika nchi mnayoiingia kuimiliki.

64 KishaBwanaatawatawanya miongoni mwa mataifa yote, kutoka mwisho mmoja wa dunia hadi mwingine. Huko mtaabudu miungu mingine, miungu ya miti na ya mawe, ambayo ninyi wala baba zenu hamkuijua.

65 Miongoni mwa mataifa hayo hamtapata raha wala mahali pa kupumzisha wayo wa mguu wenu. HukoBwanaatawapa mahangaiko ya mawazo, macho yaliyochoka kwa kungojea na moyo uliokata tamaa.

66 Utaishi katika mahangaiko siku zote, ukiwa umejaa hofu usiku na mchana, wala hutakuwa kamwe na uhakika wa maisha yako.

67 Wakati wa asubuhi utasema hivi, “Laiti ingekuwa jioni!” Jioni utasema, “Laiti ingekuwa asubuhi,” kwa sababu ya hofu ile itakayojaza moyo wako na vitu vile macho yako yatakavyoviona.

68 Bwanaatawarudisha tena Misri kwa meli, safari niliyosema kamwe hamngeenda tena. Huko mtajiuza ninyi wenyewe kwa adui zenu kama watumwa wa kiume na wa kike, lakini hakuna ye yote atakayewanunua.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/DEU/28-6fbea6aabb2e7d221f9ac2e45f31a268.mp3?version_id=1627—