Kumbukumbu La Torati 29

Kufanya Upya Agano

1 Haya ndiyo maneno ya AganoBwanaaliyomwagiza Mose kufanya na Waisraeli huko Moabu, kuwa nyongeza ya Agano alilofanya nao huko Horebu.

2 Mose akawaita Waisraeli wote akawaambia:

Macho yenu yameona yale yoteBwanaaliyofanya kwa Mfalme Farao huko Misri, kwa maafisa wake wote na kwa nchi yake yote.

3 Kwa macho yenu wenyewe mliona yale majaribu makubwa, ishara zile za miujiza na maajabu makubwa.

4 Lakini mpaka leoBwanahajawapa akili ya kuelewa au macho yanayoona au masikio yanayosikia.

5 Kwa muda wa miaka arobaini niliyowaongoza jangwani, nguo zenu hazikuchakaa, wala viatu miguuni mwenu.

6 Hamkula mkate na hamkunywa divai wala kileo cho chote. Nilifanya hivi ili mpate kujua kuwa mimi ndimiBwanaMungu wenu.

7 Wakati mlipofika mahali hapa, Sihoni mfalme wa Heshboni na Ogu mfalme wa Bashani walikuja kupigana dhidi yetu, lakini tuliwashinda.

8 Tuliichukua nchi yao na kuwapa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase kama urithi wao.

9 Fuateni kwa bidii masharti ya Agano hili, ili kwamba mweze kustawi katika kila kitu mnachofanya.

10 Ninyi nyote leo mnasimama mbele zaBwanaMungu wenu; mkiwa viongozi na wakuu wenu, wazee na maafisa wenu, na wanaume wengine wote wa Israeli,

11 pamoja na watoto wenu, wake zenu na pia wageni waishio katika kambi zenu wanaowapasulia kuni na kuwachotea maji.

12 Mnasimama hapa ili kufanya Agano naBwanaMungu wenu, Agano ambalo Mungu analifanya nanyi siku hii ya leo na kulitia muhuri kwa kiapo,

13 kuwathibitisha ninyi siku hii ya leo kama taifa lake, ili aweze kuwa Mungu wenu kama alivyowaahidi na kama alivyowaapia baba zenu Abrahamu, Isaki na Yakobo.

14 Ninafanya Agano hili pamoja na kiapo chake, sio na ninyi tu

15 mnaosimama hapa na sisi leo mbele zaBwanaMungu wetu, bali pia pamoja na wale ambao hawapo hapa leo.

16 Ninyi wenyewe mnajua jinsi tulivyoishi nchini Misri na jinsi tulivyopita katikati ya nchi mpaka tukafika hapa.

17 Mliona miongoni mwao vinyago vyao vya kuchukiza na sanamu za miti na mawe, za fedha na dhahabu.

18 Hakikisheni kwamba hakuna mwanaume au mwanamke, ukoo au kabila miongoni mwenu leo ambalo moyo wake utamwachaBwanaMungu wetu, kwenda kuabudu miungu ya mataifa hayo. Hakikisheni hakuna mzizi miongoni mwenu unaotoa sumu chungu ya namna hii.

19 Wakati mtu wa namna hii asikiapo maneno ya kiapo hiki, hujibariki mwenyewe na kisha hufikiri, “Nitakuwa salama, hata kama nikiendelea kuifuata njia yangu mwenyewe.” Hili litaleta maafa juu ya nchi iliyonyeshewa sawasawa na nchi kame.

20 Bwanakamwe hatakuwa radhi kumsamehe, ghadhabu na wivu wa Mungu vitawaka dhidi ya mtu huyo. Laana zote zilizoandikwa katika kitabu hiki zitamwangukia naBwanaatafuta jina lake chini ya mbingu.

21 Bwanaatamtwaa peke yake kutoka makabila ya Israeli kwa maangamizo, kulingana na laana zote za Agano zilizoandikwa kwenye Kitabu hiki cha Sheria.

22 Watoto wako watakaofuata baada yako katika vizazi vya baadaye na wageni ambao watakuja kutoka nchi za mbali, wataona maafa, yaliyoipata nchi na magonjwa ambayoBwanaaliyaleta juu yake.

23 Nchi yote itakuwa jaa linaloungua la chumvi na kiberiti: hakutakuwa kilichopandwa, hakutakuwa kinachochipua, wala hakutakuwa mimea inayoota juu yake. Itakuwa kama maangamizo ya Sodoma na Gomora, Adma na Seboimu, ambazoBwanaaliangamiza kwa hasira kali.

24 Mataifa yote yatauliza: “Kwa niniBwanaamefanya hivi juu ya nchi hii? Kwa nini hasira hii kali ikawaka?”

25 Na jibu litakuwa: “Ni kwa sababu watu hawa waliacha Agano laBwana, Mungu wa baba zao, Agano alilofanya nao wakati alipowatoa katika nchi ya Misri.

26 Walienda zao na kuabudu miungu mingine na kuisujudia, miungu wasioijua, miungu ambayo Mungu hakuwapa.

27 Kwa hiyo hasira yaBwanaikawaka dhidi ya nchi hii, hivyo Mungu akaleta juu yake laana zote zilizoandikwa katika kitabu hiki.

28 Katika hasira kali na katika ghadhabu kuuBwanaaliwang’oa kutoka katika nchi yao na kuwasukumia katika nchi nyingine, kama ilivyo sasa.”

29 Mambo ya siri ni yaBwanaMungu wetu, bali yaliyofunuliwa ni yetu na watoto wetu milele, ili tuweze kuyafanya maneno yote ya sheria hii.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/DEU/29-641d211a50d6b7fe9da4756f972f2499.mp3?version_id=1627—

Kumbukumbu La Torati 30

Mafanikio Baada Ya Kumgeukia Bwana

1 Wakati baraka hizi zote pamoja na laana nilizoziweka mbele yako zitakapokujia, nawe ukazitafakari moyoni popoteBwanaMungu wako atakapokutawanya miongoni mwa mataifa,

2 hapo wewe na watoto wako mtakapomrudiaBwanaMungu wako, na kumtii kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote kulingana na kila kitu ninachokuamuru leo,

3 ndipoBwanaMungu wako atakapokurudisha kutoka utumwani na kukuhurumia, naye atakukusanya tena kutoka katika mataifa yote kule alikokutawanya wewe.

4 Hata kama umefukuziwa katika nchi ya mbali kiasi gani chini ya mbingu, kutoka hukoBwanaMungu wako atakukusanya na kukurudisha.

5 Atakurudisha katika nchi iliyokuwa mali ya baba zako, nawe utaimiliki. Atakufanya ufanikiwe sana na kukuzidisha kwa idadi kuliko baba zako.

6 BwanaMungu wako ataitairi mioyo yenu na mioyo ya wazao wenu ili mweze kumpenda kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote ukaishi.

7 BwanaMungu wako ataweka laana hizi zote juu ya adui zako ambao wanakuchukia na kukutesa.

8 Utamtii tenaBwanana kuzishika amri zake zote ninazokupa leo.

9 NdipoBwanaMungu wako atakapokufanikisha sana katika kazi zote za mikono yako na katika uzao wa tumbo lako, wadogo wa mifugo yako na mazao ya nchi yako.Bwanaatakufurahia tena na kukufanikisha, kama alivyowafurahia baba zako,

10 kama ukimtiiBwanaMungu wako, na kuzishika amri zake na maagizo yake ambayo yameandikwa katika Kitabu hiki cha Sheria, na kumgeukiaBwanaMungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote.

Uzima Na Mauti

11 Ninachokuagiza leo sio kigumu sana kwako au usichokiweza.

12 Hakiko juu mbinguni, ili uulize, “Ni nani atakayepanda kwenda mbinguni kukileta na kututangazia ili tuweze kutii?”

13 Wala hakiko ng’ambo ya bahari, ili uulize, “Ni nani atakayevuka bahari kwenda kukichukua na kututangazia ili tupate kutii?”

14 La hasha! Lile neno liko karibu sana nawe; liko kinywani mwako na ndani ya moyo wako ili uweze kulitii.

15 Tazama, naweka mbele yako leo uzima na mafanikio, mauti na maangamizo.

16 Ninakuamuru leo kwamba umpendeBwanaMungu wako, utembee katika njia zake, na kutunza maagizo yake, amri na sheria zake; ndipo utakapoishi na kuongezeka, nayeBwanaMungu wako atakubariki katika nchi unayoiingia kuimiliki.

17 Lakini kama moyo wako ukigeukia mbali ukawa huna utii, kama umevutwa kuisujudia miungu mingine na kuiabudu,

18 nakutangazia leo hii kwamba hakika utaangamizwa. Hutaishi maisha marefu katika nchi unayovuka Yordani kuiingia na kuimiliki.

19 Leo ninaziita mbingu na nchi kama mashahidi dhidi yako kwamba nimeweka mbele yako uzima na mauti, baraka na laana. Basi sasa chagueni uzima, ili wewe na watoto wako mpate kuishi,

20 na ili upate kumpendaBwanaMungu wako, uisikilize sauti yake na kuambatana naye. Kwa kuwaBwanandiye uzima wako, na atakupa wingi wa siku ili upate kuishi katika nchi aliyoapa kuwapa baba zako Abrahamu, Isaki na Yakobo.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/DEU/30-7e4558bdab08c84d5d0739a04ab37b77.mp3?version_id=1627—

Kumbukumbu La Torati 31

Yoshua Kutawala Baada Ya Mose

1 Kisha Mose akaenda akasema maneno haya kwa Waisraeli wote:

2 “Sasa nina miaka mia moja na ishirini nami siwezi tena kuwaongoza.Bwanaameniambia, ‘Hutavuka Yordani.’

3 BwanaMungu wenu, yeye mwenyewe atavuka mbele yenu. Ataangamiza mataifa haya mbele yenu, nanyi mtaimiliki nchi yao. Pia Yoshua atavuka mbele yenu, kamaBwanaalivyosema.

4 NayeBwanaatawafanyia watu hao kile alichowafanyia Sihoni na Ogu, wafalme wa Waamori, ambao aliwaangamiza pamoja na nchi yao.

5 Bwanaatawakabidhi kwenu, nanyi lazima mwatendee yale yote niliyowaamuru.

6 Iweni imara na moyo wa ushujaa. Msiogope wala msifadhaike kwa sababu yao, kwa kuwaBwanaMungu wenu anakwenda pamoja nanyi; kamwe hatawaacha wala hatawatupa ninyi.”

7 Kisha Mose akamwita Yoshua na akamwambia mbele ya Israeli wote, “Uwe imara na moyo wa ushujaa, kwa kuwa ni lazima uende na watu hawa katika nchi ileBwanaaliyowaapia baba zao kuwapa, nawe ni lazima uwagawie kama urithi wao.

8 Bwanamwenyewe atakutangulia naye atakuwa pamoja nawe; kamwe hatakuacha wala hatakutupa. Usiogope, wala usifadhaike.”

Kusoma Sheria

9 Kwa hiyo Mose akaandika sheria hii na kuwapa makuhani, wana wa Lawi, waliochukua Sanduku la Agano laBwanana wazee wote wa Israeli.

10 Kisha Mose akawaamuru, akasema: “Mwishoni mwa kila miaka saba, katika mwaka wa kufuta madeni, wakati wa Sikukuu ya Vibanda,

11 Waisraeli wote wanapokuja mbele zaBwanaMungu wenu mahali atakapopachagua, utasoma sheria hii mbele yao masikioni mwao.

12 Kusanya watu wote, wanaume, wanawake, watoto na wageni wanaoishi katika miji yenu, ili waweze kusikia na kujifunza kumchaBwanaMungu wenu na kufuata kwa bidii maneno yote ya sheria hii.

13 Watoto wao, ambao hawaijui sheria hii, lazima waisikie na kujifunza kumchaBwanaMungu wenu kwa muda mtakaoishi katika nchi mnayovuka Yordani kuimiliki.”

Kuasi Kwa Waisraeli Kunatabiriwa

14 Bwanaakamwambia Mose, “Sasa siku ya kifo chako imekaribia. Mwite Yoshua, mkajihudhurishe katika Hema la Kukutania, mahali nitakapompa maagizo ya kazi.” Kwa hiyo Mose na Yoshua wakaja na kujihudhurisha kwenye Hema la Kukutania.

15 KishaBwanaakatokea katika Hema katika nguzo ya wingu, nalo wingu likasimama juu ya ingilio la Hema.

16 KishaBwanaakamwambia Mose: “Unakwenda kupumzika na baba zako, nao watu hawa hivi karibuni watazini na miungu migeni ya nchi wanayoingia. Wataniacha na kuvunja Agano nililofanya nao.

17 Siku hiyo nitawakasirikia na kuwaacha; nitawaficha uso wangu, nao wataangamizwa. Maafa mengi na shida nyingi zitakuja juu yao, nao siku hiyo watauliza, ‘Je, maafa haya hayakuja juu yetu kwa sababu Mungu wetu hayuko pamoja nasi?’

18 Nami hakika nitauficha uso wangu siku hiyo kwa sababu ya maovu yao yote kwa kugeukia miungu mingine.

19 “Sasa ujiandikie wimbo huu, uwafundishe Waisraeli na uwaamuru wauimbe, ili upate kuwa ushahidi wangu dhidi yao.

20 Nitakapokwisha kuwaingiza katika nchi itiririkayo maziwa na asali, nchi niliyowaahidi baba zao kwa kiapo, nao watakapokula wakashiba na kufanikiwa, watageukia miungu mingine na kuiabudu, wakinikataa mimi na kuvunja Agano langu.

21 Maafa na shida zitakapokuja juu yao, wimbo huu utashuhudia dhidi yao, kwa sababu hautasahauliwa na wazao wao. Ninajua lile wanaloandaa kufanya, hata kabla sijawaingiza katika nchi niliyowaahidi kwa kiapo.”

22 Hivyo Mose akaandika wimbo huu siku ile na akawafundisha Waisraeli.

23 Bwanaakampa Yoshua mwana wa Nuni agizo hili: “Uwe hodari na shujaa, kwa kuwa utawaleta Waisraeli katika nchi niliyowaahidi kwa kiapo, nami mwenyewe nitakuwa pamoja nawe.”

24 Baada ya Mose kumaliza kuandika kwenye kitabu maneno ya sheria hii kutoka mwanzo hadi mwisho,

25 akawapa Walawi wale waliolibeba Sanduku la Agano laBwanaagizo hili, akawaambia:

26 “Chukueni Kitabu hiki cha Sheria mkakiweke kando ya Sanduku la Agano laBwanaMungu wenu. Hapo ndipo kitakapokaa kama shahidi dhidi yenu.

27 Kwa kuwa ninajua jinsi mlivyo waasi na mlivyo na shingo ngumu. Kama mmekuwa mkiasi dhidi yaBwananikiwa bado niko hai na nikiwa pamoja nanyi, mtaasi mara ngapi baada ya kufa kwangu!

28 Kusanyeni mbele yangu wazee wote wa makabila yenu na maafisa wenu wote, ili nipate kusema maneno haya masikioni mwao na kuziita mbingu na nchi ili kushuhudia dhidi yao.

29 Kwa kuwa ninajua baada ya kifo changu hakika mtakuwa waovu kabisa na kugeuka kutoka njia niliyowaamuru ninyi. Katika siku zijazo, maafa yatawapata kwa sababu mtafanya maovu mbele ya macho yaBwana, na kuchochea hasira yake kwa yale mikono yenu itakayokuwa imefanya.”

Wimbo Wa Mose

30 Mose akayasoma maneno ya wimbo huu kutoka mwanzo hadi mwisho katika masikio ya kusanyiko lote la Israeli:

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/DEU/31-352d8c8e6fa80c4366c1ca104f0630c5.mp3?version_id=1627—

Kumbukumbu La Torati 32

1 Sikilizeni, enyi mbingu, nami nitasema;

sikia, ee nchi, maneno ya kinywa changu.

2 Mafundisho yangu na yanyeshe kama mvua,

na maneno yangu na yashuke kama umande,

kama manyunyu juu ya majani mabichi,

kama mvua tele juu ya mimea myororo.

3 Nitalitangaza jina laBwana.

Naam, sifuni ukuu wa Mungu wetu!

4 Yeye ni Mwamba, kazi zake ni kamilifu,

njia zake zote ni haki.

Mungu mwaminifu ambaye hakosei,

yeye ni mnyofu na mwenye haki.

5 Wamefanya mambo ya upotovu mbele zake;

kwa aibu yao, wao si watoto wake tena,

lakini ni kizazi kilicho kiovu na kilichopotoka.

6 Je, hii ndiyo njia ya kumlipaBwana,

enyi watu wajinga na wasio na busara?

Je, yeye siye Baba yenu, Muumba wenu,

aliyewafanya ninyi na kuwaumba?

7 Kumbuka siku za kale;

tafakari vizazi vya zamani vilivyopita.

Uliza baba yako, naye atakuambia,

wazee wako, nao watakueleza.

8 Aliye Juu Sana alipowapa mataifa urithi wao,

alipogawanya wanadamu wote,

aliweka mipaka kwa ajili ya mataifa

sawasawa na hesabu ya wana wa Israeli.

9 Kwa kuwa fungu laBwanani watu wake,

Yakobo kura yake ya urithi.

10 Katika nchi ya jangwa alimkuta,

katika nyika tupu ivumayo upepo.

Alimhifadhi na kumtunza;

akamlinda kama mboni ya jicho lake,

11 kama tai avurugaye kiota chake,

na kurukaruka juu ya makinda yake,

ambaye hutanda mabawa yake kuwadaka,

na huwachukua kwenye mbawa zake.

12 Bwanapeke yake alimwongoza;

hakuwepo mungu mgeni pamoja naye.

13 Akamfanya apande sehemu zilizoinuka za nchi,

akamlisha kwa mavuno ya mashamba.

Akamlea kwa asali toka mwambani,

na kwa mafuta kutoka mwamba mgumu,

14 kwa jibini na maziwa kutoka makundi ya ng’ombe

na kutoka makundi ya mbuzi,

kwa mafuta ya wana-kondoo na mbuzi,

kwa kondoo waume wazuri wa Bashani,

na kwa ngano nzuri.

Ukanywa damu ya zabibu inayotoa povu.

15 Yeshurunialinenepa na kupiga teke;

alikuwa na chakula tele,

akawa mzito na akapendeza sana.

Akamwacha Mungu aliyemwumba,

na kumkataa Mwamba Mwokozi wake.

16 Wakamfanya Mungu kuwa na wivu kwa miungu yao migeni,

na kumkasirisha kwa sanamu zao

za machukizo.

17 Wakatoa dhabihu kwa pepo, ambao si Mungu:

miungu wasiyoijua,

miungu iliyojitokeza siku za karibuni,

miungu ambayo baba zenu hawakuiogopa.

18 Mkamwacha Mwamba, aliyewazaa ninyi;

mkamsahau Mungu aliyewazaa.

19 Bwanaakaona hili, akawakataa,

kwa sababu alikasirishwa

na wanawe na binti zake.

20 Akasema, “Nitawaficha uso wangu,

nami nione mwisho wao utakuwa nini,

kwa kuwa wao ni kizazi kilichopotoka,

watoto ambao si waaminifu.

21 Wamenifanya niwe na wivu

kwa kile ambacho si mungu,

na kunikasirisha kwa sanamu zao

zisizokuwa na thamani.

Nitawafanya wawaonee wivu wale ambao si taifa,

nitawafanya wakasirishwe na taifa

lile lisilo na ufahamu.

22 Kwa maana moto umewashwa kwa hasira yangu,

ule uwakao hadi kwenye vina vya mauti.

Utateketeza dunia pamoja na mazao yake,

na kuwasha moto katika misingi ya milima.

23 “Nitalundika majanga juu yao

na kutumia mishale yangu dhidi yao.

24 Nitatuma njaa kali dhidi yao maradhi mabaya,

yateketezayo na tauni ya kufisha;

nitawapelekea meno makali ya wanyama mwitu,

na sumu ya nyoka wale watambaao mavumbini.

25 Barabarani upanga utawakosesha watoto;

nyumbani mwao hofu itatawala.

Vijana wao wa kiume na wa kike wataangamia,

pia watoto wachanga na wazee wenye mvi.

26 Nilisema ningewatawanya

na kufuta kumbukumbu lao

katika mwanadamu.

27 Lakini nilihofia dhihaka za adui,

adui asije akashindwa kuelewa,

na kusema, ‘Mikono yetu imeshinda;

Bwanahakufanya yote haya.’ ”

28 Wao ni taifa lisilo na akili,

hakuna busara ndani yao.

29 Laiti wangekuwa na hekima wangefahamu hili,

na kutambua mwisho wao utakuwa aje!

30 Mtu mmoja angewezaje kufukuza elfu moja,

au wawili kufukuza elfu kumi,

kama si kwamba Mwamba wao amewauza,

kama si kwambaBwanaamewaacha?

31 Kwa kuwa mwamba wao si kama Mwamba wetu,

sawasawa na vile adui zetu wanavyokiri.

32 Mzabibu wao unatoka kwenye mzabibu wa Sodoma,

na kutoka kwenye mashamba ya Gomora.

Zabibu zake zimejaa sumu,

na vishada vyake vimejaa uchungu.

33 Mvinyo wao ni sumu ya nyoka,

sumu yenye kufisha ya swila.

34 “Je, hili sikuliweka akiba

na kulifungia kwenye vyumba vyangu vya hazina?

35 Ni juu yangu kulipiza kisasi; nitalipiza.

Wakati utakapowadia mguu wao utateleza;

siku yao ya maafa ni karibu,

na maangamizo yao yanawajia haraka.”

36 Bwanaatahukumu watu wake,

na kuwahurumia watumishi wake

anapoona nguvu zao zimekwisha,

wala hakuna ye yote aliyebaki,

mtumwa au aliye huru.

37 Atasema: “Sasa iko wapi miungu yao,

mwamba walioukimbilia,

38 miungu wale waliokula mafuta ya dhabihu zao

na kunywa mvinyo wa sadaka zao za vinywaji?

Wainuke basi, wawasaidie!

Wawapeni basi ulinzi!

39 “Tazama basi, Mimi mwenyewe, Mimi Ndiye!

Hakuna mungu mwingine ila Mimi.

Mimi ninaua na Mimi ninafufua,

Mimi nimejeruhi na Mimi nitaponya,

wala hakuna awezaye kuokoa kutoka mkononi mwangu.

40 Ninainua mkono wangu kuelekea mbinguni na kusema:

Hakika kama niishivyo milele,

41 wakati ninapounoa upanga wangu unaometameta

na mkono wangu unapoushika ili kutoa hukumu,

nitalipiza kisasi juu ya adui zangu

na kuwalipiza wale wanaonichukia.

42 Nitailevya mishale yangu kwa damu,

wakati upanga wangu ukitafuna nyama:

damu ya waliochinjwa pamoja na mateka,

vichwa vya viongozi wa adui.”

43 Furahini, Enyi mataifa, pamoja na watu wake,

kwa kuwa atailipiza damu ya watumishi wake,

atalipiza kisasi juu ya adui zake

na kufanya upatanisho

kwa ajili ya nchi na watu wake.

44 Mose na Yoshuamwana wa Nuni wakaja, wakanena maneno yote ya wimbo watu wakiwa wanasikia.

45 Mose alipomaliza kuyasoma maneno haya yote kwa Israeli wote,

46 akawaambia, “Yawekeni moyoni maneno yote ambayo nimewatangazia kwa makini siku hii ya leo, ili kwamba mpate kuwaagiza watoto wenu wayatii kwa bidii maneno yote ya sheria hii.

47 Siyo maneno matupu tu kwenu, bali ni uzima wenu. Kwa hayo mtaishi maisha marefu katika nchi mnayovuka Yordani kuimiliki.”

Mose Kufia Juu Ya Mlima Nebo

48 Siku hiyo hiyoBwanaakamwambia Mose,

49 “Kwea katika mapangano ya Mlima Abarimu hadi kilima cha Nebo kilichoko Moabu, ng’ambo ya Yeriko, na uitazame Kanaani, nchi ninayowapa Waisraeli kama milki yao wenyewe.

50 Utafia kwenye mlima huo unaokwea na kukusanyika pamoja na watu wako, kama ndugu yako Aroni alivyokufa juu ya Mlima Hori naye akakusanyika kwa watu wake.

51 Hii ni kwa sababu ninyi wawili mlivunja uaminifu nami mbele ya Waisraeli kwenye maji ya Meriba-Kadeshi katika Jangwa la Sini, na kwa sababu hamkuuinua utakatifu wangu miongoni mwa Waisraeli.

52 Kwa hiyo, utaiona tu nchi kwa mbali; wewe hutaiingia nchi ninayowapa watu wa Israeli.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/DEU/32-58ef675860feeb6b511494e672a545f8.mp3?version_id=1627—

Kumbukumbu La Torati 33

Mose Anayabariki Makabila

1 Hii ndiyo baraka Mose mtu wa Mungu aliyotamka kwa Waisraeli kabla ya kifo chake.

2 Alisema:

“Bwanaalikuja kutoka Mlima Sinai,

akachomoza kama jua juu yao

kutoka Mlima Seiri,

akaangaza kutoka Mlima Parani.

Alikuja pamoja na watakatifu makumi elfu

kutoka kusini,

kutoka matelemko ya mlima wake.

3 Hakika ni wewe ambaye huwapenda watu,

watakatifu wako wote wamo mkononi mwako.

Miguuni pako wote wanasujudu

na kutoka kwako wanapokea mafundisho,

4 sheria ile Mose aliyotupa sisi,

tulio milki ya kusanyiko la Yakobo.

5 Alikuwa mfalme juu ya Yeshuruni

wakati viongozi wa watu walipokusanyika,

pamoja na makabila ya Israeli.

6 “Reubeni na aishi, asife,

wala watu wake wasiwe wachache.”

7 Akasema hili kuhusu Yuda:

“EeBwana, sikia kilio cha Yuda,

mlete kwa watu wake.

Kwa mikono yake mwenyewe hujitetea.

Naam, uwe msaada wake

dhidi ya adui zake!”

8 Kuhusu Lawi alisema:

# “Thumimu yako na Urimuyako ulimpa,

mtu yule aliyewaminifu kwako.

Ulimjaribu huko Masa

na kushindana naye

kwenye maji ya Meriba.

9 Alinena hivi kuhusu baba yake na mama yake,

‘Mimi siwahitaji kamwe.’

Akawasahau jamaa zake,

asiwatambue hata watoto wake,

lakini akaliangalia neno lako

na kulilinda Agano lako.

10 Humfundisha Yakobo mausia yako

na Israeli sheria yako.

Hufukiza uvumba mbele zako

na sadaka nzima za kuteketezwa

juu ya madhabahu yako.

11 EeBwana, bariki ustadi wake wote,

nawe upendezwe na kazi ya mikono yake.

Vipige viuno vya wale wainukao dhidi yake;

wapige adui zake hata wasiinuke tena.”

12 Kuhusu Benyamini akasema:

“Mwache mpenzi waBwana

apumzike salama kwake,

kwa maana humkinga mchana kutwa,

na yuleBwanaampendaye

hupumzika kati ya mabega yake.”

13 Kuhusu Yosefu akasema:

“Bwanana aibariki nchi yake

kwa umande wa thamani

kutoka mbinguni juu,

na vilindi vya maji

vilivyotulia chini;

14 pamoja na vitu vilivyo bora sana

viletwavyo na jua,

na vitu vizuri sana vinavyoweza

kutolewa na mwezi;

15 pamoja na zawadi bora sana

za milima ya zamani

na kwa wingi wa baraka

za vilima vya milele;

16 pamoja na baraka nzuri mno

za ardhi na ukamilifu wake,

na upendeleo wake yeye

aliyeishi kwenye kichaka

kilichokuwa kinawaka moto.

Hivi vyote na vikae juu ya kichwa cha Yosefu,

juu ya paji la uso la aliye mkuu

miongoni mwa ndugu zake.

17 Katika fahari yeye ni kama fahali mzaliwa wa kwanza;

pembe zake ni pembe za nyati,

na kwa pembe hizo atapiga mataifa,

hata yaliyo miisho ya dunia.

Hivyo ndivyo yalivyo makumi elfu ya Efraimu;

hivyo ndivyo yalivyo maelfu ya Manase.”

18 Kuhusu Zabuloni akasema:

“Shangilia, Zabuloni, wakati wa kutoka nje,

nawe Isakari, katika mahema yako.

19 Watawaita mataifa kwenye mlima,

na huko mtatoa dhabihu za haki;

watajifurahisha kwa wingi uliojaza bahari,

kwa hazina zilizofichwa mchangani.”

20 Kuhusu Gadi akasema:

“Atabarikiwa yeye aongezaye milki ya Gadi!

Gadi huishi huko kama simba,

akirarua kwenye mkono au kichwa.

21 Alijichagulia nchi nzuri kuliko zote

kwa ajili yake mwenyewe;

fungu la kiongozi lilikuwa limehifadhiwa

kwa ajili yake.

Viongozi wa watu walipokusanyika,

alitimiza haki ya mapenzi yaBwana,

na hukumu zake kuhusu Israeli.”

22 Kuhusu Dani akasema:

“Dani ni mwana simba,

akiruka kutoka Bashani.”

23 Kuhusu Naftali akasema:

“Naftali amejaa tele upendeleo waBwana,

naye amejaa baraka yake;

atarithi magharibi na kusini.”

24 Kuhusu Asheri akasema:

“Mbarikiwa zaidi sana katika wana ni Asheri;

yeye na apate upendeleo kwa ndugu zake,

yeye na anawe miguu yake kwenye mafuta.

25 Makomeo ya malango yako yawe chuma na shaba,

nazo nguvu zako zitakuwa sawa na siku zako.

26 “Hakuna mwingine kama Mungu wa Yeshuruni,

ambaye hupanda juu ya mbingu ili akusaidie,

na juu ya mawingu katika utukufu wake.

27 Mungu wa milele ni kimbilio lako,

na chini kuna mikono ya milele.

Atamfukuza adui yako mbele yako,

akisema, ‘Mwangamize yeye!’

28 Hivyo Israeli ataishi salama peke yake.

Mzao wa Yakobo ni salama

katika nchi ya nafaka na divai mpya,

mahali ambapo mbingu

hudondosha umande.

29 Ee Israeli, wewe umebarikiwa!

Ni nani kama wewe,

taifa lililookolewa naBwana?

Yeye ni ngao yako na msaada wako,

na upanga wako uliotukuka.

Adui zako watatetemeka mbele yako,

nawe utapakanyaga

# mahali pao pa juu.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/DEU/33-a6c4e364662300629ffa031e84f19aaf.mp3?version_id=1627—

Kumbukumbu La Torati 34

Kifo Cha Mose

1 Kisha Mose akaupanda mlima Nebo kutoka tambarare za Moabu mpaka kilele cha Pisga, ng’ambo ya Yeriko. HukoBwanaakamwonyesha nchi yote: kutoka Gileadi mpaka Dani,

2 Naftali yote, nchi ya Efraimu na Manase, nchi yote ya Yuda mpaka bahari ya magharibi,

3 Negebu na nchi yote kuanzia Bonde la Yeriko, Mji wa Mitende, hadi Soari.

4 KishaBwanaakamwambia, “Hii ndiyo nchi niliyomwahidi Abrahamu na Isaki na Yakobo kwa kiapo niliposema, ‘Nitawapa wazao wako.’ Nimekuruhusu uione kwa macho yako, lakini hutavuka kuingia.”

5 Naye Mose mtumishi waBwanaakafa huko Moabu, kamaBwanaalivyokuwa amesema.

6 Mungu akamzika huko Moabu, katika bonde mkabala na Beth-Peori, lakini hakuna ajuaye kaburi lake lilipo mpaka leo.

7 Mose alikuwa na umri wa miaka mia moja na ishirini alipofariki; hata hivyo nguvu ya macho yake haikufifia wala mwili wake haukudhoofika.

8 Waisraeli wakaomboleza kwa ajili ya Mose kwenye tambarare za Moabu kwa siku thelathini, mpaka wakati wa kulia na kuomboleza ulipopita.

9 Basi Yoshua mwana wa Nuni alijazwa roho ya hekima kwa sababu Mose alikuwa ameweka mikono yake juu yake. Kwa hiyo Waisraeli wakamsikiliza na wakafanya yale ambayoBwanaalikuwa amemwagiza Mose.

10 Tangu wakati huo, katika Israeli hajainuka nabii mwingine kama Mose, ambayeBwanaalimjua uso kwa uso,

11 aliyetenda ishara zote zile za miujiza na maajabu ambayoBwanaalimtuma kuyatenda huko Misri, yaani kwa Farao na maafisa wake wote na nchi yake yote.

12 Kwa kuwa hakuna mtu ye yote aliyewahi kuonyesha nguvu nyingi ama kutenda matendo ya kutisha ambayo Mose aliwahi kuyafanya mbele ya Israeli yote.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/DEU/34-e0154b8f805c9e884caee9fc493f73d2.mp3?version_id=1627—

Hesabu 1

Watu Wahesabiwa Kwa Mara Ya Kwanza

1 Bwanaalisema na Mose katika Jangwa la Sinai, katika Hema la Kukutania, siku ya kwanza ya mwezi wa pili, katika mwaka wa pili baada ya Waisraeli kutoka nchi ya Misri. Akamwambia,

2 “Hesabu watu wa jumuiya yote ya Waisraeli kwa kufuata koo zao na jamaa zao, ukiorodhesha kila mwanaume kwa jina lake, mmoja mmoja.

3 Wewe na Aroni mtawahesabu kwa migawanyo yao wanaume wote katika Israeli wenye miaka ishirini na kuendelea ambao wanaweza kutumika katika jeshi.

4 Mwanaume mmoja kutoka kila kabila, kila aliye kiongozi wa jamaa yake, atawasaidia.

5 Haya ndiyo majina ya wanaume watakaowasaidia:

“kutoka Reubeni, ni Elisuri mwana wa Shedeuri;

6 kutoka Simeoni, ni Shelumieli mwana wa Surishadai;

7 kutoka Yuda, ni Nashoni mwana wa Aminadabu;

8 kutoka Isakari, ni Nethaneli mwana wa Suari;

9 kutoka Zabuloni, ni Eliabu mwana wa Heloni;

10 kutoka wana wa Yosefu:

kutoka Efraimu, ni Elishama mwana wa Amihudi;

kutoka Manase, ni Gamalieli mwana wa Pedasuri;

11 kutoka Benyamini, ni Abidani mwana wa Gideoni;

12 kutoka Dani, ni Ahiezeri mwana wa Amishadai;

13 kutoka Asheri, ni Pagieli mwana wa Okrani;

14 kutoka Gadi, ni Eliasafu mwana wa Deueli;

15 kutoka Naftali, ni Ahira mwana wa Enani.”

16 Hawa walikuwa wanaume walioteuliwa kutoka jumuiya, viongozi wa makabila ya baba zao. Walikuwa wakuu wa koo za Israeli.

17 Mose na Aroni wakawachukuwa wanaume hao ambao walikuwa wamepewa majina yao,

18 wakaita jumuiya yote pamoja katika siku ya kwanza ya mwezi wa pili. Watu wakaonyesha nasaba zao kwa koo zao na jamaa zao, nao wanaume waliokuwa na miaka ishirini au zaidi walioorodheshwa kwa majina, mmoja mmoja,

19 kamaBwanaalivyomwagiza Mose. Hivyo aliwahesabu katika Jangwa la Sinai:

20 Kutoka wazao wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa kiume wa Israeli:

Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, mmoja mmoja, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.

21 Idadi kutoka kabila la Reubeni ilikuwa watu 46,500.

22 Kutoka wazao wa Simeoni:

Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi walihesabiwa na kuorodheshwa kwa majina, mmoja mmoja, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.

23 Idadi kutoka kabila la Simeoni walikuwa watu 59,300.

24 Kutoka wazao wa Gadi:

Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.

25 Idadi kutoka kabila la Gadi walikuwa watu 45,650.

26 Kutoka wazao wa Yuda:

Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.

27 Idadi kutoka kabila la Yuda walikuwa watu 74,600.

28 Kutoka wazao wa Isakari:

Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.

29 Idadi kutoka kabila la Isakari walikuwa watu 54,400.

30 Kutoka wazao wa Zabuloni:

Waume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.

31 Idadi kutoka kabila la Zabuloni walikuwa watu 57,400.

32 Kutoka wana wa Yosefu:

Kutoka wazao wa Efraimu:

Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.

33 Idadi kutoka kabila la Efraimu walikuwa watu 40,500.

34 Kutoka wazao wa Manase:

Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.

35 Idadi kutoka kabila la Manase walikuwa watu 32,200.

36 Kutoka wazao wa Benyamini:

Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.

37 Idadi kutoka kabila la Benyamini walikuwa watu 35,400.

38 Kutoka wazao wa Dani:

Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.

39 Idadi kutoka kabila la Dani walikuwa watu 62,700.

40 Kutoka wazao wa Asheri:

Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.

41 Idadi kutoka kabila la Asheri walikuwa watu 41,500.

42 Kutoka wazao wa Naftali:

Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.

43 Idadi kutoka kabila la Naftali walikuwa watu 53,400.

44 Hawa walikuwa wanaume waliohesabiwa na Mose, Aroni na viongozi kumi na wawili wa Israeli, kila mmoja akiwakilisha jamaa yake.

45 Wanaume wote Waisraeli waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi la Israeli, walihesabiwa kufuatana na jamaa zao.

46 Jumla ya hesabu yao ilikuwa watu 603,550.

47 Hata hivyo jamaa ya kabila la Lawi hawakuhesabiwa pamoja na wengine.

48 Bwanaalikuwa amemwambia Mose:

49 “Kamwe usihesabu kabila la Lawi wala kuwaweka pamoja katika hesabu ya Waisraeli wengine.

50 Badala yake, waweke Walawi kuwa viongozi wa Maskani ya Ushuhuda, juu ya samani zake na kila kitu kilichomo ndani yake. Wao watabeba Maskani na samani zake zote; wataitunza na kupiga kambi kuizunguka.

51 Wakati wo wote Maskani inapohamishwa, Walawi wataifungua, na wakati wo wote maskani inapotakiwa kusimamishwa, Walawi watafanya kazi hiyo. Mtu ye yote mwingine ambaye atasogea karibu nayo atauawa.

52 Waisraeli watapiga mahema yao kwa makundi makundi, kila mwanaume katika kambi yake mwenyewe chini ya bendera yake.

53 Hata hivyo, Walawi watapiga mahema yao kuzunguka Maskani ya Ushuhuda ili ghadhabu isiipate jumuiya ya Waisraeli. Walawi watawajibika kwa utunzaji wa Maskani ya Ushuhuda.”

54 Waisraeli walifanya yote haya sawasawa kamaBwanaalivyomwamuru Mose.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/NUM/1-4dd2702063645dbc088512caaee4e489.mp3?version_id=1627—

Hesabu 2

Mpangilio Wa Kambi Za Makabila

1 Bwanaaliwaambia Mose na Aroni:

2 “Waisraeli watapiga kambi zao kuzunguka Hema la Kukutania kwa umbali fulani kutoka kwenye hema, kila mwanaume chini ya alama yake pamoja na bendera ya jamaa yake.”

3 Kwa upande wa mashariki kuelekea maawio ya jua, kambi ya makundi ya Yuda watapiga kambi chini ya alama yao. Kiongozi wa watu wa Yuda ni Nashoni mwana wa Aminadabu.

4 Kundi lake lina watu 74,600.

5 Kabila la Isakari watapiga kambi karibu na Yuda. Kiongozi wa watu wa Isakari ni Nethaneli mwana wa Suari.

6 Kundi lake lina watu 54,400.

7 Kabila la Zabuloni litafuata. Kiongozi wa watu wa Zabuloni ni Eliabu mwana wa Heloni.

8 Kundi lake lina watu 57,400.

9 Wanaume wote walio katika kambi ya Yuda, kufuatana na makundi yao, ni 186,400. Wao watatangulia kwanza kuondoka.

10 Kwa upande wa kusini kutakuwa kambi ya makundi ya Reubeni chini ya alama yao. Kiongozi wa watu wa Reubeni ni Elisuri mwana wa Shedeuri.

11 Kundi lake lina watu 46,500.

12 Kabila la Simeoni watapiga kambi karibu na Reubeni. Kiongozi wa watu wa Simeoni ni Shelumieli mwana wa Surishadai.

13 Kundi lake lina watu 59,300.

14 Kabila la Gadi litafuata. Kiongozi wa watu wa Gadi ni Eliasafu mwana wa Deueli.

15 Kundi lake lina watu 45,650.

16 Wanaume wote walio katika kambi ya Reubeni, kufuatana na makundi yao, ni 151,450. Nao watakuwa nafasi ya pili kuondoka.

17 Kisha Hema la Kukutania na kambi ya Walawi vitakuwa katikati ya kambi zote. Wao watasafiri kwa utaratibu ule ule kama walivyopiga kambi, kila mmoja mahali pake mwenyewe chini ya alama yake.

18 Upande wa magharibi kutakuwepo na kambi ya makundi ya Efraimu chini ya alama yao. Kiongozi wa watu wa Efraimu ni Elishama mwana wa Amihudi.

19 Kundi lake lina watu 40,500.

20 Kabila la Manase litafuata baada ya Efraimu. Kiongozi wa watu wa Manase ni Gamalieli mwana wa Pedasuri.

21 Kundi lake lina watu 32,200.

22 Kabila la Benyamini litafuata baada ya Manase. Kiongozi wa watu wa Benyamini ni Abidani mwana wa Gideoni.

23 Kundi lake lina watu 35,400.

24 Wanaume wote walio katika kambi ya Efraimu kufuatana na makundi yao ni 108,100. Nao watakuwa nafasi ya tatu kuondoka.

25 Upande wa kaskazini kutakuwa na makundi ya kambi ya Dani, chini ya alama yao. Kiongozi wa watu wa Dani ni Ahiezeri mwana wa Amishadai.

26 Kundi lake lina watu 62,700.

27 Kabila la Asheri watapiga kambi karibu na Dani. Kiongozi wa watu wa Asheri ni Pagieli mwana wa Okrani.

28 Kundi lake lina watu 41,500.

29 Kabila la Naftali litafuata. Kiongozi wa watu wa Naftali ni Ahira mwana wa Enani.

30 Kundi lake lina watu 53,400.

31 Wanaume wote walio katika kambi ya Dani ni 157,600. Wao watakuwa wa mwisho kuondoka chini ya alama yao.

32 Hawa ndio Waisraeli, wakiwa wamehesabiwa kufuatana na jamaa zao. Wote wale walio kambini kwa makundi yao ni watu 603,550.

33 Hata hivyo, Walawi hawakuhesabiwa pamoja na Waisraeli wengine, kamaBwanaalivyomwagiza Mose.

34 Kwa hiyo Waisraeli wakafanya kila kituBwanaalichomwamuru Mose. Hivyo ndivyo walivyopiga kambi chini ya alama zao, pia hivyo ndivyo walivyoondoka, kila mmoja akiwa na ukoo wake na jamaa yake.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/NUM/2-9826c94294424bf79a970f89ee9a4019.mp3?version_id=1627—

Hesabu 3

Walawi

1 Hii ni hesabu ya jamaa ya Aroni na Mose kwa wakati uleBwanaalipozungumza na Mose, katika Mlima Sinai.

2 Majina ya wana wa Aroni yalikuwa: Nadabu mzaliwa wa kwanza na Abihu, Eleazari na Ithamari.

3 Hayo yalikuwa majina ya wana wa Aroni, makuhani wapakwa mafuta, ambao walikuwa wamesimikwa kuhudumu kama makuhani.

4 Hata hivyo Nadabu na Abihu walikufa mbele zaBwanawakati walipotoa sadaka kwa moto usioruhusiwa mbele zake katika Jangwa la Sinai. Hawakuwa na wana; kwa hiyo Eleazari na Ithamari peke yao walihudumu kama makuhani wakati wote wa maisha ya Aroni baba yao.

5 Bwanaakamwambia Mose,

6 “Walete watu wa kabila la Lawi mbele ya Aroni kuhani ili wamsaidie.

7 Watafanya huduma kwa ajili yake na kwa jumuiya yote katika Hema la Kukutania kwa kufanya kazi za Maskani.

8 Watatunza samani zote za Hema la Kukutania, wakitimiza wajibu wa kuhudumia Waisraeli kwa kufanya kazi ya Maskani.

9 Wakabidhi Walawi kwa Aroni na wanawe; hao ndio Waisraeli ambao wanakabidhiwa kabisa kwake.

10 Waweke Aroni na wanawe kuhudumu kama makuhani; mtu mwingine ye yote atakayesogelea mahali patakatifu ni lazima auawe.”

11 Bwanaakamwambia Mose,

12 “Nimewatwaa Walawi kutoka miongoni mwa Waisraeli badala ya mzaliwa wa kwanza wa kiume wa kila mwanamke wa Mwisraeli. Walawi ni wangu,

13 kwa kuwa wazaliwa wote wa kwanza ni wangu. Nilipowaua wazaliwa wa kwanza huko Misri, nilimtenga kila mzaliwa wa kwanza katika Israeli awe wangu, akiwa mwanadamu au mnyama. Watakuwa wangu. Mimi ndimiBwana.”

14 Bwanaakamwambia Mose katika Jangwa la Sinai,

15 “Wahesabu Walawi kwa jamaa zao na koo zao. Mhesabu kila mwanaume mwenye umri wa mwezi mmoja au zaidi.”

16 Kwa hiyo Mose akawahesabu, kama alivyoamriwa na neno laBwana.

17 Haya yalikuwa majina ya wana wa Lawi:

Gershoni, Kohathi na Merari.

18 Haya ndiyo yaliyokuwa majina ya koo za Wagerishoni:

Libni na Shimei.

19 Koo za Wakohathi zilikuwa ni:

Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.

20 Koo za Wamerari zilikuwa ni:

Mahli na Mushi.

Hizi ndizo zilizokuwa koo za Walawi, kufuatana na jamaa zao.

21 Kulikuwa na koo za Walibni na Washimei kwa Gershoni; hizi ndizo zilizokuwa koo za Wagerishoni.

22 Idadi ya waume wote waliokuwa na mwezi mmoja au zaidi waliohesabiwa walikuwa 7,500.

23 Ukoo wa Wagerishoni walitakiwa kuweka kambi zao upande wa magharibi, nyuma ya Maskani.

24 Kiongozi wa jamaa za Wagerishoni alikuwa Eliasafu mwana wa Laeli.

25 Katika Hema la Kukutania, Wagerishoni walikuwa na wajibu wa kutunza Maskani na hema, vifuniko vyake, pazia katika mlango wa kuingilia ndani ya Hema la Kukutania,

26 mapazia ya ua unaozunguka Maskani na madhabahu, pamoja na kamba, na kila kinachohusika kwa matumizi yake.

27 Kwa Kohathi kulikuwepo koo za Waamrami, Waishari, Wahebroni na Wauzieli; hizi ndizo zilizokuwa koo za Wakohathi.

28 Hesabu ya wanaume wote wenye mwezi mmoja au zaidi ilikuwa watu 8,600. Wakohathi waliwajibika kutunza mahali patakatifu.

29 Koo za Wakohathi zilitakiwa kuweka kambi zao upande wa kusini wa Maskani.

30 Kiongozi wa jamaa za koo za Wakohathi alikuwa Elisafani mwana wa Uzieli.

31 Waliwajibika kutunza Sanduku la Agano, meza, kinara cha taa, madhabahu, na vile vyombo vya mahali patakatifu vinavyotumika kuhudumu, pazia, na kila kitu kinachohusika na matumizi yake.

32 Kiongozi mkuu wa Walawi alikuwa Eleazari mwana wa kuhani, Aroni. Aliwekwa juu ya wale waliowajibika kutunza mahali patakatifu.

33 Kwa Merari kulikuwa na koo za Wamahli na Wamushi; hizi zilikuwa koo za Merari.

34 Hesabu ya waume wote wenye umri wa mwaka mmoja au zaidi waliohesabiwa walikuwa 6,200.

35 Kiongozi wa jamaa za koo za Wamerari alikuwa Surieli mwana wa Abihaili; hawa walitakiwa kuweka kambi zao upande wa kaskazini mwa Maskani.

36 Wamerari waliwekwa kutunza miimo ya Maskani, mataruma yake, nguzo, vitako na vifaa vyake vyote na kila kitu kilichohusika na matumizi yake,

37 na pia nguzo za ua unaozunguka pamoja na vitako vyake, vigingi vya hema na kamba zake.

38 Mose, na Aroni na wanawe walitakiwa kuweka kambi zao mashariki mwa Maskani, kuelekea maawio ya jua, mbele ya Hema la Kukutania. Wao walihusika na utunzaji wa mahali patakatifu kwa niaba ya Waisraeli. Mtu mwingine ye yote aliyepasogelea mahali patakatifu angeuawa.

39 Jumla ya hesabu ya Walawi waliohesabiwa na Mose na Aroni kwa amri yaBwana, kufuatana na koo, pamoja na kila mwanaume mwenye mwezi mmoja au zaidi walikuwa 22,000.

40 Bwanaakamwambia Mose, “Wahesabu wazaliwa wa kwanza wa kiume wote wa Waisraeli wenye umri wa mwezi mmoja au zaidi na uorodheshe majina yao.

41 Nitwalie Walawi badala ya wazaliwa wa kwanza wa Waisraeli, nayo mifugo ya Walawi badala ya wazaliwa wa mifugo ya Waisraeli. Mimi ndimiBwana.”

42 Hivyo Mose akawahesabu wazaliwa wa kwanza wote wa Waisraeli, kamaBwanaalivyomwamuru.

43 Jumla ya hesabu ya wazaliwa wa kwanza waume wenye umri wa mwezi mmoja au zaidi, walioorodheshwa kwa majina walikuwa 22,273.

44 Bwanaakamwambia Mose,

45 “Watwae Walawi badala ya wazaliwa wa kwanza wote wa Israeli, nayo mifugo ya Walawi badala ya mifugo yao. Walawi watakuwa wangu. Mimi ndimiBwana.

46 Ili kukomboa wazao wa kwanza 273 wa Waisraeli ambao wamezidi hesabu ya Walawi,

47 kusanya shekeli tanokwa kila mmoja, kufuatana na shekeli ya mahali patakatifu, ambayo ina uzito wa gera ishirini.

48 Mpe Aroni na wanawe hizo fedha kwa ajili ya ukombozi wa idadi ya Waisraeli waliozidi.”

49 Kwa hiyo Mose akakusanya fedha za ukombozi kutoka kwa wale ambao hesabu yao ilizidi wale waliokombolewa na Walawi.

50 Kutokana na wazaliwa wa kwanza wa Waisraeli alikusanya fedha yenye uzito wa shekeli 1,365kufuatana na shekeli ya mahali patakatifu.

51 Mose akampa Aroni na wanawe ile fedha ya ukombozi, kama alivyoamuriwa na neno laBwana.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/NUM/3-e86f3cb2b11f7d6ad28c7b04ad5715bb.mp3?version_id=1627—

Hesabu 4

Wakohathi

1 Bwanaakawaambia Mose na Aroni,

2 “Wahesabu Wakohathi walio sehemu ya Walawi kwa koo zao na jamaa zao.

3 Wahesabu wanaume wote wenye umri wa miaka thelathini hadi hamsini wanaokuja kutumika katika kazi ya Hema la Kukutania.

4 “Hii ndiyo kazi ya Wakohathi katika Hema la Kukutania: Watatunza vitu vilivyo vitakatifu sana.

5 Wakati kambi inapohamishwa, Aroni na wanawe wataingia ndani na kushusha lile pazia la kuzuilia na kufunika nalo Sanduku la Ushuhuda.

6 Kisha watafunika juu yake na ngozi ya mnyama, na kutandaza juu yake kitambaa cha rangi ya buluu iliyokolea na kuingiza mipiko mahali pake.

7 “Juu ya meza ya mikate ya Wonyesho watatandaza kitambaa cha buluu na waweke sahani juu yake, masinia, bakuli na magudulia kwa ajili ya sadaka za kinywaji; mkate ule ambao upo hapa daima utabaki juu yake.

8 Juu ya hivyo vitu watatandaza kitambaa chekundu na kufunika kwa ngozi laini ya mnyama na kuweka mipiko yake mahali pake.

9 “Watachukua kitambaa cha buluu na kufunika kinara cha taa kilicho kwa ajili ya nuru, pamoja na taa zake, mikasi yake, sinia zake, magudulia yake yote yaliyotumika kuwekea mafuta.

10 Kisha watakisokotea pamoja na vifaa vyake vyote katika ngozi laini ya mnyama na kukiweka kwenye jukwaa lake.

11 “Juu ya madhabahu ya dhahabu watatandaza kitambaa cha buluu na kukifunika kwa ngozi laini ya mnyama na kuweka mipiko yake mahali pake.

12 “Watavichukua vyombo vyote vinavyotumika kuhudumia mahali patakatifu, watavisokotea kwenye kitambaa cha buluu na kufunika kwa ngozi laini ya mnyama, na kuviweka juu ya miti ya kuchukulia.

13 “Wataondoa majivu kutoka katika madhabahu ya shaba na kutandaza kitambaa cha zambarau juu yake.

14 Kisha wataweka vyombo vyote juu yake vinavyotumika kwa kuhudumia madhabahuni pamoja na vyombo vya kutolea moto, nyuma, miiko na mabakuli ya kunyunyizia. Juu yake watatandaza ngozi laini ya mnyama ya kufunika, na kuweka mipiko mahali pake.

15 “Baada ya Aroni na wanawe kumaliza kazi ya kufunika samani takatifu na vyombo vyake vyote, watu watakapokuwa tayari kung’oa kambi, Wakohathi watakuja kufanya kazi ya kubeba. Lakini wasije wakagusa vitu vitakatifu la sivyo watakufa. Wakohathi ndio watakaobeba vile vitu vilivyomo katika Hema la Kukutania.

16 “Eleazari mwana wa Aroni, kuhani, ndiye atakayesimamia mafuta kwa ajili ya taa, uvumba wenye harufu nzuri, sadaka za kila siku za nafaka na mafuta ya upako. Ndiye atakayekuwa msimamizi wa maskani yote yaBwanana kila kitu kilichomo ndani mwake pamoja na samani takatifu na vyombo vyake.”

17 Bwanaakawaambia Mose na Aroni,

18 “Hakikisheni kwamba koo za kabila la Wakohathi hawatengwi kutoka Walawi.

19 Ili wapate kuishi wala wasife wanapokaribia vitu vitakatifu sana, uwafanyie hivi: Aroni na wanawe watakwenda mahali patakatifu na kumgawia kila mtu kazi yake, na kwamba ni nini atakachochukua.

20 Lakini Wakohathi hawaruhusiwi kuingia ndani ili kuangalia vitu vitakatifu, hata kwa kitambo kidogo, la sivyo watakufa.”

Wagerishoni

21 Bwanaakamwambia Mose,

22 “Wahesabu pia Wagerishoni kwa jamaa zao na koo zao.

23 Wahesabu wanaume wote wenye umri wa miaka thelathini hadi hamsini ambao huja kutumika katika Hema la Kukutania.

24 “Hii ndiyo huduma ya koo za Wagerishoni wakati wanapofanya kazi na kubeba mizigo.

25 Watabeba mapazia ya maskani. Hema la Kukutania, kifuniko chake na kifuniko cha nje cha ngozi laini ya mnyama, mapazia ya maingilio ya Hema la Kukutania,

26 mapazia ya ua unaozunguka Maskani na madhabahu, pazia la maingilio, kamba na vifaa vyote vinavyotumika katika huduma yake. Wagerishoni watafanya yote yatakiwayo kufanyika na vitu hivi.

27 Utumishi wao wote ukiwa ni kuchukua au wa kufanya kazi nyingine, utafanyika chini ya maelekezo ya Aroni na wanawe. Mtawapangia kama wajibu wao yote watakayoyafanya.

28 Hii ndiyo huduma ya koo za Wagerishoni katika Hema la Kukutania. Wajibu wao utakuwa chini ya maelekezo ya Ithamari mwana wa kuhani Aroni.

Wamerari

29 “Wahesabu Wamerari kwa koo zao na jamaa zao.

30 Wahesabu wanaume wote kuanzia umri wa miaka thelathini hadi hamsini ambao watakuja kutumika katika Hema la Kukutania.

31 Huu ndio wajibu wao wanapofanya huduma katika Hema la Kukutania: kubeba miimo ya Maskani, mataruma yake, nguzo na vitako,

32 nguzo za ua unaozunguka pamoja na vitako vyake, vigingi vya hema, kamba, vifaa vyake vyote na kila kitu kinachohusiana na matumizi yake. Kila mtu mpangie vitu maalum vya kubeba.

33 Huu ndio utumishi wa koo za Merari kama watakavyofanya kazi katika Hema la Kukutania, chini ya maelekezo ya Ithamari mwana wa kuhani, Aroni.”

Kuhesabiwa Kwa Koo Za Walawi

34 Mose, Aroni na viongozi wa jumuiya wakawahesabu Wakohathi kwa koo zao na jamaa zao.

35 Wanaume wote kuanzia umri wa miaka thelathini hadi hamsini ambao walikuja kutumika katika Hema la Kukutania,

36 waliohesabiwa kwa koo zao, walikuwa 2,750.

37 Hii ilikuwa ndiyo jumla ya wote wale wa koo za Wakohathi ambao walitumika katika Hema la Kukutania. Mose na Aroni waliwahesabu kufuatana na amri yaBwanakupitia kwa Mose.

38 Wagerishoni walihesabiwa kwa koo zao na jamaa zao.

39 Watu wote kuanzia umri wa miaka thelathini hadi hamsini ambao walikuja kutumika katika Hema la Kukutania,

40 waliohesabiwa kwa koo zao na jamaa zao, walikuwa 2,630.

41 Hii ilikuwa ndiyo jumla ya wale wa koo za Gershoni ambao walitumika katika Hema la Kukutania. Mose na Aroni waliwahesabu kufuatana na amri yaBwana.

42 Wamerari walihesabiwa kwa koo zao na jamaa zao.

43 Wanaume wote kuanzia umri wa miaka thelathini hadi miaka hamsini ambao walikuja kutumika katika Hema la Kukutania,

44 waliohesabiwa kwa koo zao, walikuwa 3,200.

45 Hii ilikuwa ndiyo jumla ya wale wa koo za Wamerari. Mose na Aroni waliwahesabu kufuatana na amri yaBwanakupitia kwa Mose.

46 Hivyo Mose, Aroni na viongozi wa Israeli waliwahesabu Walawi wote kwa koo zao na jamaa zao.

47 Wanaume wote wenye umri kuanzia miaka thelathini hadi hamsini waliokuja kufanya kazi ya kuhudumu na kubeba Hema la Kukutania

48 walikuwa watu 8,580.

49 Kwa amri yaBwanakupitia Mose, kila mmoja aligawiwa kazi yake na kuambiwa kitu cha kubeba.

Hivyo ndivyo walivyohesabiwa kamaBwanaalivyomwamuru Mose.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/NUM/4-76d36a970fda3a08e0fb98d54ca1fdd7.mp3?version_id=1627—