Hesabu 5

Utakaso Wa Kambi

1 Bwanaakamwambia Mose,

2 “Waamuru Waisraeli kumtoa nje ya kambi mtu ye yote ambaye ana ugonjwa wa ngozi uambukizao, au anayetokwa na majimaji ya aina yo yote, au ambaye ni najisi kwa utaratibu wa ibada kwa sababu ya maiti.

3 Hii itakuwa ni kwa wote, yaani, wanaume na wanawake; watoeni nje ya kambi ili wasije wakanajisi kambi yao, ambamo ninaishi miongoni mwao.”

4 Waisraeli wakafanya hivyo; wakawatoa nje ya kambi. Wakafanya kama vileBwanaalivyokuwa amemwelekeza Mose.

Malipo Kwa Ajili Ya Makosa

5 Bwanaakamwambia Mose,

6 “Waambie Waisraeli, ‘Wakati mwanaume au mwanamke akimkosea mwenzake kwa njia yo yote, na kwa hivyo akawa si mwaminifu kwaBwana, mtu huyo ana hatia,

7 na ni lazima atubu dhambi aliyoifanya. Ni lazima atoe malipo kamili kwa ajili ya kosa lake, aongeze sehemu ya tano juu ya malipo hayo na kutoa yote kwa mtu aliyemkosea.

8 Lakini ikiwa mtu huyo hana jamaa ya karibu ambaye malipo yanaweza kufanywa kwa ajili ya kosa, malipo yatakuwa mali yaBwana, nayo ni lazima apewe kuhani, pamoja na kondoo dume ambaye anatumika kufanyia upatanisho kwa ajili yake.

9 Matoleo yote matakatifu ya Waisraeli wanayoleta kwa kuhani yatakuwa yake.

10 Kila kitu cha mtu kilichowekwa wakfu ni chake mwenyewe, lakini kile atoacho kwa kuhani kitakuwa cha kuhani.’ ”

Jaribio Kwa Ajili Ya Mke Asiye Mwaminifu

11 KishaBwanaakamwambia Mose,

12 “Nena na Waisraeli uwaambie: ‘Ikiwa mke wa mtu amepotoka na si mwaminifu kwa mumewe,

13 kwa kukutana kimwili na mwanaume mwingine, tendo hili likafichika kwa mumewe na unajisi wake usigundulike (kwa kuwa hakuna ushahidi dhidi yake, naye hakukamatwa katika tendo hilo),

14 nazo hisia za wivu zikamjia mumewe na kumshuku mkewe, naye mke yule ni najisi, au mumewe ana wivu na akamshuku ingawa si najisi,

15 basi atampeleka mkewe kwa kuhani. Huyo mume itampasa apeleke pia sadaka ya unga wa shayiri kiasi cha sehemu ya kumi ya efakwa niaba ya mkewe. Huyo mwanaume kamwe asimimine mafuta juu ya huo unga wala asiweke uvumba juu yake, kwa sababu ni sadaka ya nafaka kwa ajili ya wivu, sadaka ya ukumbusho ili kukumbushia uovu.

16 “ ‘Kuhani atamleta huyo mwanamke na kumsimamisha mbele zaBwana.

17 Kisha kuhani atachukua sehemu ya maji matakatifu ndani ya gudulia la udongo na kuchanganya na baadhi ya vumbi kutoka katika sakafu ya Maskani.

18 Baada ya kuhani kumsimamisha huyo mwanamke mbele zaBwana, atazifungua nywele za huyo mwanamke na kuweka sadaka ya ukumbusho mikononi mwake, ile sadaka ya nafaka kwa ajili ya wivu, huku kuhani mwenyewe akishikilia yale maji machungu yaletayo laana.

19 Kisha kuhani atamwapiza huyo mwanamke, akimwambia, “Ikiwa hakuna mwanaume mwingine aliyekutana kimwili nawe, wala hujapotoka na kuwa najisi wakati ukiwa umeolewa na mumeo, maji haya machungu yaletayo laana na yasikudhuru.

20 Lakini ikiwa umepotoka wakati ukiwa umeolewa na mume wako na umejinajisi mwenyewe kwa kukutana kimwili na mwanaume mwingine asiyekuwa mumeo”;

21 hapa kuhani atamweka huyo mwanamke chini ya laana ya kiapo akisema: “Bwanana awafanye watu wako wakulaani na kukukataa, wakatiBwanaatakapolifanya paja lako kupooza na tumbo lako kuvimba.

22 Maji haya yaletayo laana na yaingie ndani ya mwili wako ili tumbo lako livimbe na paja lako lipooze.”

“ ‘Kisha mwanamke atasema, “Amen. Iwe hivyo.”

23 “ ‘Kuhani ataandika laana hizi kwenye kitabu, kisha atazioshea laana hizo kwenye yale maji machungu.

24 Kuhani atamnywesha yule mwanamke yale maji machungu yaletayo laana, nayo maji haya yatamwingia na kumsababishia maumivu makali.

25 Kuhani atachukua sadaka ya nafaka kwa ajili ya wivu kutoka mikononi mwa huyo mwanamke, naye ataipunga mbele zaBwanana kuileta madhabahuni.

26 Kisha kuhani atachota sadaka ya nafaka mkono uliojaa kama sadaka ya ukumbusho na kuiteketeza juu ya madhabahu, baada ya hayo, atamtaka huyo mwanamke anywe yale maji.

27 Kama amejitia unajisi na kukosa uaminifu kwa mumewe, wakati anapotakiwa anywe maji yale yaletayo laana, yatamwingia na kusababisha maumivu makali; tumbo lake litavimba na paja lake litapooza, naye atakuwa amelaaniwa miongoni mwa watu wake.

28 Hata hivyo, ikiwa huyo mwanamke hakujitia unajisi, naye ni safi, atasafishwa hatia na ataweza kuzaa watoto.

29 “ ‘Basi, hii ndiyo sheria ya wivu mwanamke anapopotoka na kujitia unajisi wakati akiwa ameolewa na mumewe,

30 au hisia za wivu zinapomjia mwanaume kwa sababu ya kumshuku mkewe. Kuhani atamfanya huyo mwanamke kusimama mbele zaBwanana atatumia sheria hii yote kwa huyo mwanamke.

31 Mume atakuwa hana hatia ya kosa lo lote, bali mwanamke atayachukua matokeo ya dhambi yake.’ ”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/NUM/5-67c5a126272d4a1a35b1946bc2c3f693.mp3?version_id=1627—

Hesabu 6

Mnadhiri

1 Bwanaakamwambia Mose,

2 “Sema na Waisraeli na uwaambie: ‘Ikiwa mwanaume au mwanamke anataka kuweka nadhiri maalum, nadhiri ya kutengwa kwa ajili yaBwanakama Mnadhiri,

3 ni lazima ajitenge na mvinyo na kinywaji kingine cho chote chenye chachu, na kamwe asinywe siki itokanayo na mvinyo au itokanayo na kinywaji kingine chenye chachu. Kamwe asinywe maji ya zabibu wala kula zabibu mbichi au kavu.

4 Kwa muda wote atakaokuwa Mnadhiri, kamwe hatakula cho chote kitokanacho na mzabibu, sio mbegu wala maganda.

5 “ ‘Kwa muda wote wa nadhiri yake ya kujitenga kwa ajili yaBwana, wembe hautapita kichwani mwake. Ni lazima awe mtakatifu mpaka kipindi cha kujitenga kwake kwa ajili yaBwanakiishe; ni lazima aache nywele za kichwa chake zirefuke.

6 Kwa kipindi cho chote cha kujitenga kwa ajili yaBwanahatakaribia maiti.

7 Hata kama baba yake mwenyewe au mama au kaka au dada akifa, hatajinajisi mwenyewe kwa taratibu za ibada kwa ajili yao, kwa sababu ishara ya kujiweka wakfu kwake kwa Mungu ipo katika kichwa chake.

8 Kwa kipindi chote cha kujitenga kwake yeye ni wakfu kwaBwana.

9 “ ‘Kama mtu ye yote akifa ghafula karibu naye, atakuwa ametiwa unajisi nywele zake alizoziweka wakfu, hivyo ni lazima anyoe nywele zake siku ya utakaso wake, yaani siku ya saba.

10 Kisha siku ya nane ni lazima alete hua wawili au makinda mawili ya njiwa kwa kuhani katika mlango wa Hema la Kukutania.

11 Kuhani atatoa mmoja kama sadaka ya dhambi, na mwingine kama sadaka ya kuteketezwa ili kufanya upatanisho kwa ajili yake kwa sababu ametenda dhambi kwa kuwepo mbele ya maiti. Siku iyo hiyo atakiweka wakfu kichwa chake.

12 Ni lazima ajitoe kabisa kwaBwanakwa kipindi cha kujitenga kwake, na ni lazima atoe mwana-kondoo wa mwaka mmoja kama sadaka ya hatia. Siku zilizopita hazitahesabiwa kwa sababu alijitia unajisi katika siku zake za kujitenga.

13 “ ‘Basi hii ndiyo sheria kwa ajili ya Mnadhiri baada ya kipindi chake cha kujitenga kupita. Ataletwa kwenye ingilio la Hema la Kukutania.

14 Hapo atatoa sadaka zake kwaBwana: yaani, mwana-kondoo wa mwaka mmoja asiye na waa kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, kondoo mke wa mwaka mmoja asiye na waa kwa ajili ya sadaka ya dhambi, kondoo dume asiye na waa kwa ajili ya sadaka ya amani,

15 pamoja na sadaka zake za nafaka na za vinywaji, na kikapu cha mikate isiyotiwa chachu, yaani maandazi yaliyotengenezwa kwa unga laini uliochanganywa na mafuta, na mikate myembamba iliyopakwa mafuta.

16 “ ‘Kuhani atavileta vitu hivyo mbele zaBwanana kufanya sadaka ya dhambi na sadaka ya kuteketezwa.

17 Ataleta pia kikapu cha mikate isiyotiwa chachu, na atatoa dhabihu kondoo dume kama sadaka ya amani kwaBwana, pamoja na sadaka yake ya nafaka na sadaka ya kinywaji.

18 “ ‘Kisha kwenye ingilio la Hema la Kukutania, Mnadhiri ni lazima anyoe nywele zake ambazo alikuwa ameziweka wakfu. Atazichukua hizo nywele na kuziweka ndani ya moto ulio chini ya dhabihu ya sadaka ya amani.

19 “ ‘Baada ya Mnadhiri kunyoa hizo nywele zake za kujitenga kwake, kuhani atampa mikononi mwake bega la kondoo dume lililochemshwa, na pia andazi na mkate mwembamba kutoka kwenye kikapu, vyote vikiwa vimetengenezwa bila kuwekwa chachu.

20 Kisha kuhani atavipunga mbele zaBwanakama sadaka ya kupunga; ni vitakatifu na ni mali ya kuhani, pamoja na kile kidari kilichopungwa na lile paja lililotolewa. Baada ya hayo, Mnadhiri anaweza kunywa divai.

21 “ ‘Hii ndiyo sheria ya Mnadhiri ambaye anaweka nadhiri kwa matoleo yake kwaBwanakufuatana na kujitenga kwake, zaidi ya cho chote kile anachoweza kupata. Ni lazima atimize nadhiri aliyoiweka kufuatana na sheria ya Mnadhiri.’ ”

Baraka Ya Kikuhani

22 Bwanaakamwambia Mose,

23 “Mwambie Aroni na wanawe, ‘Hivi ndivyo mtakavyowabariki Waisraeli. Waambieni:

24 “ ‘ “Bwanaakubariki

na kukulinda;

25 Bwanaakuangazie nuru ya uso wake

na kukufadhili;

26 Bwanaakugeuzie uso wake

na kukupa amani.” ’

27 “Hivyo wataliweka Jina langu juu ya Waisraeli, nami nitawabariki.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/NUM/6-9851c137e30f5a4ecb9302071f22f373.mp3?version_id=1627—

Hesabu 7

Sadaka Wakati Wa Kuweka Wakfu Maskani Ya Bwana

1 Mose alipomaliza kuisimamisha Maskani, aliitia mafuta na kuiweka wakfu pamoja na samani zake zote. Pia alitia madhabahu mafuta na kuweka wakfu pamoja na vyombo vyake vyote.

2 Ndipo viongozi wa Israeli, wale wakuu wa jamaa waliokuwa viongozi wa kabila wasimamizi wa wale waliohesabiwa, wakatoa sadaka.

3 Walizileta kama matoleo yao mbele zaBwana: magari sita ya kukokotwa yaliyofunikwa, pamoja na maksai kumi na wawili; yaani maksai mmoja kutoka kwa kila kiongozi, na gari moja la kukokotwa kutoka kwa kila viongozi wawili. Haya waliyaleta mbele ya Maskani.

4 Bwanaakamwambia Mose,

5 “Vikubali vitu hivi kutoka kwao, ili viweze kutumika katika kazi kwenye Hema la Kukutania. Wapatie Walawi kama kazi ya kila mtu itakavyohitaji.”

6 Hivyo Mose akachukua yale magari ya kukokotwa pamoja na maksai, na kuwapa Walawi.

7 Aliwapa Wagerishoni magari mawili ya kukokotwa na maksai wanne, kama walivyohitaji kwa kazi yao,

8 na pia aliwapa Wamerari magari manne ya kukokotwa na maksai wanane, kama kazi yao ilivyohitaji. Wote walikuwa chini ya maelekezo ya Ithamari mwana wa kuhani, Aroni.

9 Lakini Mose hakuwapa Wakohathi cho chote kati ya hivyo, kwa sababu walitakiwa kubeba vitu vitakatifu mabegani mwao, vile walikuwa wanawajibika.

10 Wakati madhabahu ilipotiwa mafuta, viongozi walileta sadaka zao kwa ajili ya kule kuwekwa wakfu kwake na kuziweka mbele ya madhabahu.

11 Kwa maanaBwanaalikuwa amemwambia Mose, “Kila siku kiongozi mmoja ataleta sadaka yake ili kuwekwa wakfu madhabahu.”

12 Yule ambaye alileta sadaka yake siku ya kwanza alikuwa Nashoni, mwana wa Aminadabu, wa kabila la Yuda.

13 Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka;

14 sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba;

15 fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;

16 mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;

17 maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Nashoni mwana wa Aminadabu.

18 Siku ya pili yake Nethaneli mwana wa Suari, kiongozi wa kabila la Isakari, alileta sadaka yake.

19 Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka;

20 sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba;

21 fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;

22 mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;

23 maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Nethaneli mwana wa Suari.

24 Siku ya tatu Eliabu mwana wa Heloni, kiongozi wa kabila la Zabuloni, alileta sadaka yake.

25 Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka;

26 sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba;

27 fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;

28 mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;

29 maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Eliabu mwana wa Heloni.

30 Siku ya nne Elisuri mwana wa Shedeuri, kiongozi wa kabila la Reubeni, alileta sadaka yake.

31 Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka;

32 sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba;

33 fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;

34 mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;

35 maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Elisuri mwana wa Shedeuri.

36 Siku ya tano Shelumieli mwana wa Surishadai, kiongozi wa watu wa Simeoni, alileta sadaka yake.

37 Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka;

38 sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba;

39 fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;

40 mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;

41 maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Shelumieli mwana wa Surishadai.

42 Siku ya sita Eliasafu mwana wa Deueli, kiongozi wa watu wa Gadi, alileta sadaka yake.

43 Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka;

44 sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba;

45 fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;

46 mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;

47 maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Eliasafu mwana wa Deueli.

48 Siku ya saba Elishama mwana wa Amihudi, kiongozi wa watu wa Efraimu, alileta sadaka yake.

49 Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka;

50 sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba;

51 fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;

52 mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;

53 maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Elishama mwana wa Amihudi.

54 Siku ya nane Gamalieli mwana wa Pedasuri, kiongozi wa watu wa Manase, alileta sadaka yake.

55 Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka;

56 sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba;

57 fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;

58 mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;

59 maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Gamalieli mwana wa Pedasuri.

60 Siku ya tisa Abidani mwana wa Gideoni, kiongozi wa watu wa Benyamini, alileta sadaka yake.

61 Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka;

62 sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba;

63 fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;

64 mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;

65 maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Abidani mwana wa Gideoni.

66 Siku ya kumi Ahiezeri mwana wa Amishadai, kiongozi wa watu wa Dani, alileta sadaka yake.

67 Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka;

68 sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba;

69 fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;

70 mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;

71 maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Ahiezeri mwana wa Amishadai.

72 Siku ya kumi na moja Pagieli mwana wa Okrani, kiongozi wa watu wa Asheri, alileta sadaka yake.

73 Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka;

74 sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba;

75 fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;

76 mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;

77 maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Pagieli mwana wa Okrani.

78 Siku ya kumi na mbili Ahira mwana wa Enani, kiongozi wa watu wa Naftali, alileta sadaka yake.

79 Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka;

80 sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba;

81 fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;

82 mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;

83 maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Ahira mwana wa Enani.

84 Hizi zilikuwa ndizo sadaka za viongozi wa Israeli madhabahu ilipowekwa wakfu wakati ilipotiwa mafuta: sahani kumi na mbili za fedha, bakuli kumi na mbili za fedha za kunyunyizia, na masinia kumi na mawili ya dhahabu.

85 Kila sahani ya fedha ilikuwa na uzito wa shekeli 130, na kila bakuli la fedha la kunyunyizia lilikuwa na uzito wa shekeli sabini. Masinia yote kumi na mawili yalikuwa na uzito wa shekeli 2,400kulingana na shekeli ya mahali patakatifu.

86 Sahani kumi na mbili za dhahabu zilizojazwa uvumba zilikuwa na uzito wa shekeli kumi kila moja, kulingana na shekeli ya mahali patakatifu. Kwa jumla, sahani za dhahabu zilikuwa na uzito wa shekeli 120.

87 Jumla ya wanyama waliotolewa kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa walikuwa fahali kumi na wawili wachanga, kondoo waume kumi na wawili na wana-kondoo waume kumi na wawili wa mwaka mmoja, pamoja na sadaka zao za nafaka. Mbuzi waume kumi na wawili walitolewa kwa ajili ya sadaka za dhambi.

88 Jumla ya wanyama kwa ajili ya dhabihu ya sadaka ya amani walikuwa maksai ishirini na wanne, kondoo waume sitini, mbuzi waume wa mwaka mmoja sitini na wana-kondoo waume wa mwaka mmoja sitini. Hizi zilikuwa ndizo sadaka zilizoletwa kwa ajili ya kuwekwa wakfu kwa madhabahu baada ya kutiwa mafuta.

89 Mose alipoingia kwenye Hema la Kukutania kuzungumza naBwana, alisikia sauti ikisema naye kutoka kati ya wale makerubi wawili waliokuwa juu ya kile kiti cha rehema, juu ya Sanduku la Ushuhuda. Mose akazungumza naye.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/NUM/7-ed01d157c4698a513d1d7d46ca969b24.mp3?version_id=1627—

Hesabu 8

Kuwekwa Kwa Taa

1 Bwanaakamwambia Mose,

2 “Sema na Aroni umwambie, ‘Wakati utakapoziweka zile taa saba, zinatakiwa kuangaza eneo lililo mbele ya kinara cha taa.’ ”

3 Aroni akafanya hivyo; akaziweka zile taa ili zielekee mbele kwenye kinara cha taa, kama vileBwanaalivyomwamuru Mose.

4 Hivi ndivyo kinara cha taa kilivyotengenezwa: Kilitengenezwa kwa dhahabu iliyofuliwa, kuanzia kwenye kitako chake hadi kwenye maua yake. Kinara cha taa kilitengenezwa sawasawa kabisa na kielelezo ambachoBwanaalikuwa amemwonyesha Mose.

Kutengwa Kwa Walawi Kwa Ajili Ya Bwana

5 Bwanaakamwambia Mose:

6 “Watwae Walawi kutoka miongoni mwa Waisraeli wengine na uwatakase kwa kawaida ya ibada.

7 Ili kuwatakasa fanya hivi: Nyunyizia maji ya utakaso juu yao; kisha uwaambie wanyoe nywele kwenye mwili mzima, wafue nguo zao na hivyo wajitakase wenyewe.

8 Waambie wamchukue fahali mchanga pamoja na sadaka yake ya nafaka ya unga laini uliochanganywa na mafuta; kisha utamchukua fahali mchanga wa pili kwa ajili ya sadaka ya dhambi.

9 Walete Walawi mbele ya Hema la Kukutania na ukusanye jumuiya yote ya Waisraeli.

10 Utawaleta Walawi mbele zaBwana, na Waisraeli wataweka mikono yao juu ya Walawi.

11 Aroni atawaweka Walawi mbele zaBwanakama sadaka ya kupunga kutoka kwa Waisraeli, ili kwamba wawe tayari kuifanya kazi yaBwana.

12 “Baada ya Walawi kuweka mikono yao juu ya vichwa vya hao mafahali wawili, tumia mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi kwaBwana, na mwingine kuwa sadaka ya kuteketezwa, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya Walawi.

13 Waambie hao Walawi wasimame mbele ya Aroni na wanawe, kisha wawatoe kama sadaka ya kupunga kwaBwana.

14 Kwa njia hii utakuwa umewatenga Walawi kutoka Waisraeli wengine, nao Walawi watakuwa wangu.

15 “Utakapokuwa umekwisha kuwatakasa Walawi na kuwatoa kama sadaka ya kupunga, watakuja kufanya kazi yao katika Hema la Kukutania.

16 Wao ndio Waisraeli ambao watatolewa kabisa kwangu. Nimewatwaa kama mali yangu mwenyewe badala ya mzaliwa wa kwanza, mzaliwa wa kwanza wa kiume kutoka kwa kila mwanamke wa Kiisraeli.

17 Kila mzaliwa wa kwanza wa kiume katika Israeli, awe wa mwanadamu au mnyama, ni wangu. Wakati nilipowaua wazaliwa wote wa kwanza huko Misri, niliwatenga kwa ajili yangu mwenyewe.

18 Nami nimewatwaa Walawi badala ya wazaliwa wote wa kwanza wa kiume katika Israeli.

19 Kati ya Waisraeli wote, nimempa Aroni na wanawe Walawi kama zawadi ili wafanye kazi katika Hema la Kukutania kwa niaba ya Waisraeli, na kufanya upatanisho kwa ajili yao ili pasiwepo na pigo lo lote litakalowapata Waisraeli wakati watakapokaribia mahali patakatifu.”

20 Mose, Aroni na jumuiya yote ya Waisraeli wakawafanyia Walawi kamaBwanaalivyomwamuru Mose.

21 Walawi wakajitakasa wenyewe na wakafua nguo zao. Kisha Aroni akawasogeza mbele zaBwanakuwa sadaka ya kupunga, na kufanya upatanisho kwa ajili yao ili kuwatakasa.

22 Baada ya hayo, Walawi walikuja kufanya kazi yao katika Hema la Kukutania chini ya usimamizi wa Aroni na wanawe. Waliwafanyia Walawi kama vileBwanaalivyomwamuru Mose.

23 Bwanaakamwambia Mose,

24 “Hili linawahusu Walawi: Wanaume wenye umri wa miaka ishirini na mitano au zaidi watakuja kushiriki katika kazi kwenye Hema la Kukutania,

25 lakini watakapofika umri wa miaka hamsini, ni lazima waache kazi zao za kawaida wala wasiendelee.

26 Wanaweza kuwasaidia ndugu zao kufanya wajibu wao katika Hema la Kukutania, lakini wao wenyewe kamwe hawatafanya hiyo kazi. Basi, hivi ndivyo utakavyogawa wajibu kwa Walawi.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/NUM/8-9c3b2beda352a25ba9fadd06a50575b1.mp3?version_id=1627—

Hesabu 9

Pasaka Huko Sinai

1 Bwanaakasema na Mose katika Jangwa la Sinai katika mwezi wa kwanza wa mwaka wa pili baada ya Waisraeli kutoka Misri. Akasema,

2 “Waamuru Waisraeli waadhimishe Pasaka katika wakati ulioamuriwa.

3 Adhimisheni wakati ulioamuriwa, yaani wakati wa kuzama jua siku ya kumi na nne ya mwezi huu, kufuatana na desturi zake zote na masharti yake.”

4 Hivyo Mose akawaambia Waisraeli waiadhimishe Pasaka,

5 nao wakafanya hivyo kwenye Jangwa la Sinai wakati wa kuzama jua siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza. Waisraeli wakafanya kila kitu kama vileBwanaalivyomwamuru Mose.

6 Lakini baadhi yao hawakuweza kuadhimisha Pasaka siku ile kwa sababu walikuwa najisi kwa taratibu za kiibada kwa ajili ya kugusa maiti. Kwa hiyo wakamwendea Mose na Aroni siku ile ile,

7 wakamwambia Mose, “Tumekuwa najisi kwa sababu tumegusa maiti, lakini kwa nini tuzuiliwe kumtoleaBwanasadaka yake pamoja na Waisraeli wengine katika wakati ulioamuriwa?”

8 Mose akawajibu, “Ngojeni mpaka nitafute kileBwanaanachoagiza kuwahusu ninyi.”

9 NdipoBwanaakamwambia Mose,

10 “Waambie Waisraeli: ‘Wakati mmoja wenu au wazao wenu wanapokuwa najisi kwa sababu ya maiti au wakiwa safarini, hata hivyo wanaweza kuadhimisha Pasaka yaBwana.

11 Wataiadhimisha wakati wa kuzama jua siku ya kumi na nne ya mwezi wa pili. Watamla mwana-kondoo, pamoja na mkate usiotiwa chachu, na mboga chungu.

12 Wasibakize cho chote hadi asubuhi wala wasivunje mifupa ya mwana-kondoo. Wakati wanapoadhimisha Pasaka, hawana budi kufuata masharti yote.

13 Lakini kama mtu ni safi kwa taratibu za kiibada naye hayuko safarini asipoadhimisha Pasaka, mtu huyo hana budi kukatiliwa mbali na watu wake kwa sababu hakutoa sadaka yaBwanakwa wakati ulioamuriwa. Mtu huyo atawajibika kubeba matokeo ya dhambi yake.

14 “ ‘Mgeni anayeishi miongoni mwenu ambaye anataka kuadhimisha Pasaka yaBwana, lazima afanye hivyo kwa kufuata desturi na masharti. Lazima masharti yawe sawasawa kwa mgeni na mzawa.’ ”

Wingu La Moto Juu Ya Maskani

15 Katika siku hiyo ambayo Maskani, Hema la Ushuhuda, liliposimamishwa, wingu liliifunika. Kuanzia jioni mpaka asubuhi wingu lililokuwa juu ya maskani lilionekana kama moto.

16 Hivyo ndivyo lilivyoendelea kuwa; wingu liliifunika wakati wa mchana, na usiku lilionekana kama moto.

17 Wakati wo wote wingu lilipoinuka kutoka juu ya Hema, nao Waisraeli waliondoka; mahali po pote wingu liliposimama, Waisraeli walipiga kambi.

18 Kwa amri yaBwanaWaisraeli waliondoka, na kwa amri yake walipiga kambi. Kwa muda wote wingu liliposimama juu ya Maskani, Waisraeli walibaki wamepiga kambi.

19 Wakati wingu lilipobaki juu ya Maskani kwa muda mrefu, Waisraeli walitii amri yaBwananao hawakuondoka.

20 Wakati mwingine wingu lilikuwa juu ya Maskani kwa siku chache tu; kwa amri yaBwanawangelipiga kambi na kisha kwa amri yake wangeliondoka.

21 Wakati mwingine wingu lilikuwapo kuanzia jioni mpaka asubuhi tu, na lilipoinuka asubuhi, nao waliondoka. Ikiwa ni mchana au usiku, wakati wo wote wingu lilipoinuka, waliondoka.

22 Ikiwa wingu lilikaa juu ya Maskani kwa siku mbili au mwezi au mwaka, Waisraeli wangebaki wamepiga kambi na hawakuondoka; lakini lilipoinuka, wangeondoka.

23 Kwa amri yaBwanawalipiga kambi, na kwa amri yaBwanawaliondoka. Walitii amri yaBwana, kufuatana na agizo lake kupitia Mose.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/NUM/9-befe803cce6de1a5d4676487a0b545ea.mp3?version_id=1627—

Hesabu 10

Tarumbeta Za Fedha

1 Bwanaakamwambia Mose:

2 “Tengeneza tarumbeta mbili za fedha ya kufua, uzitumie kwa kuita jumuiya pamoja na wakati wa kuvunja makambi ili kuondoka.

3 Tarumbeta zote mbili zikipigwa, jumuiya yote itakusanyika mbele yako katika ingilio la Hema la Kukutania.

4 Kama tarumbeta moja tu ikipigwa, viongozi, yaani wakuu wa koo za Israeli, ndio watakaokusanyika mbele yako.

5 Wakati mlio wa kujulisha hatari ukipigwa, makabila yaliyo na makambi upande wa mashariki yataondoka.

6 Ukisikika mlio wa pili wa jinsi hiyo, walioko kwenye makambi ya kusini wataondoka. Mlio huo wa kujulisha hatari utakuwa ishara ya kuondoka.

7 Ili kukusanya kusanyiko, piga tarumbeta zote, lakini siyo kwa mlio wa kujulisha hatari.

8 “Wana wa Aroni, makuhani, ndio watakaopiga hizo tarumbeta. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa ajili yenu na kwa vizazi vijavyo.

9 Wakati mtakapopigana vita katika nchi yenu wenyewe dhidi ya adui anayewaonea, piga tarumbeta kwa mlio wa kujulisha hatari. Ndipo utakumbukwa naBwanaMungu wenu na kuokolewa kutoka kwa adui zenu.

10 Pia nyakati za furaha yenu, yaani sikukuu zenu zilizoamriwa na sikukuu za Mwezi Mwandamo, mtapiga tarumbeta juu ya sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka zenu za amani, nazo zitakuwa ukumbusho kwa ajili yenu mbele za Mungu wenu. Mimi ndimiBwana, Mungu wenu.”

Waisraeli Waondoka Sinai

11 Katika siku ya ishirini ya mwezi wa pili wa mwaka wa pili, wingu liliinuka kutoka juu ya maskani ya Ushuhuda.

12 Ndipo Waisraeli wakaondoka kutoka Jangwa la Sinai wakasafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine mpaka wingu lilipotua katika Jangwa la Parani.

13 Waliondoka kwa mara ya kwanza kwa agizo la Mungu kupitia kwa Mose.

14 Vikosi vya kambi ya Yuda vilitangulia kwanza chini ya alama yao. Nahshoni mwana wa Aminadabu alikuwa kiongozi wao.

15 Nethaneli mwana wa Suari alikuwa kiongozi wa kabila la Isakari,

16 naye Eliabu mwana wa Heloni alikuwa kiongozi wa kabila la Zabuloni.

17 Ndipo Maskani iliposhushwa, nao wana wa Gershoni na wana wa Merari ambao waliibeba wakaondoka.

18 Vikosi vya kambi ya Reubeni vilifuata, chini ya alama yao. Elisuri mwana wa Shedeuri alikuwa kiongozi wao.

19 Shelumieli mwana wa Surishadai aliongoza kikosi cha kabila la Simeoni,

20 naye Eliasafu mwana wa Deueli aliongoza kikosi cha kabila la Gadi.

21 Kisha Wakohathi wakaondoka, wakichukua vitu vitakatifu. Maskani ilikuwa isimamishwe kabla wao hawajafika.

22 Vikosi vya kambi ya Efraimu vilifuata, chini ya alama yao. Elishama mwana wa Amihudi alikuwa kiongozi wao.

23 Gamalieli mwana wa Pedasuri aliongoza kikosi cha kabila la Manase,

24 naye Abidani mwana wa Gideoni alikuwa kiongozi wa kikosi cha kabila la Benyamini.

25 Mwishowe, kama kikosi cha nyuma cha ulinzi wa vikosi vyote, vikosi vya kambi ya Dani viliondoka chini ya alama yao. Ahiezeri mwana wa Amishadai alikuwa kiongozi wao.

26 Pagieli mwana wa Okrani aliongoza kikosi cha kabila la Asheri,

27 naye Ahira mwana wa Enani aliongoza kikosi cha kabila la Naftali.

28 Huu ulikuwa ndio utaratibu wa kuondoka wa vikosi vya Waisraeli walipokuwa wanaondoka.

29 Basi Mose akamwambia Hobabu mwana wa Reueli, Mmidiani, mkwewe Mose, “Tunaondoka kwenda mahali ambapoBwanaamesema ‘Nitawapa ninyi mahali hapo.’ Twende pamoja nasi tutakutendea mema, kwa maanaBwanaameahidi mambo mema kwa Israeli.”

30 Akajibu, “Hapana, sitakwenda; nitarudi kwenye nchi yangu mwenyewe na watu wangu mwenyewe.”

31 Lakini Mose akasema, “Tafadhali usituache. Wewe unajua mahali ambapo yatupasa kupiga kambi jangwani, nawe unaweza kuwa macho yetu.

32 Ikiwa utafuatana nasi, tutashirikiana nawe mema yo yote tutakayopewa naBwana.”

33 Hivyo waliondoka kutoka mlima waBwana, nao wakasafiri kwa siku tatu. Sanduku la Agano laBwanaliliwatangulia kwa zile siku tatu ili kuwatafutia mahali pa kupumzika.

34 Wingu laBwanalilikuwa juu yao wakati wa mchana walipoondoka kambini.

35 Wakati wo wote Sanduku lilipoondoka, Mose alisema,

“EeBwana, inuka!

Watesi wako na watawanyike;

adui zako na wakimbie mbele zako.”

36 Wakati wo wote Sanduku liliposimama, alisema,

“EeBwana, rudi,

kwa maelfu ya Waisraeli wasiohesabika.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/NUM/10-d7a0b35e516f26690d4d8c62f3451e7b.mp3?version_id=1627—

Hesabu 11

Moto Kutoka Kwa Bwana

1 Basi watu wakalalamika kwa habari ya taabu zao masikioni mwaBwana, naye alipowasikia, hasira yake ikawaka. Ndipo moto kutoka kwaBwanaukawaka miongoni mwao na kuteketeza baadhi ya viunga vya kambi.

2 Watu walipomlilia Mose, akamwombaBwana, nao moto ukazimika.

3 Hivyo mahali pale pakaitwa Tabera, kwa sababu moto kutoka kwaBwanauliwaka miongoni mwao.

Kware Kutoka Kwa Bwana

4 Umati wa watu wenye zogo waliokuwa miongoni mwao walitamani sana chakula kingine, Waisraeli wakaanza kulia tena na kusema, “Laiti tungekuwa na nyama tule!

5 Tunakumbuka wale samaki tuliokula huko Misri bila gharama, pia yale matango, matikitimaji, mboga, vitunguu, na vitunguu saumu.

6 Lakini sasa tumepoteza hamu ya chakula; hatuoni kitu kingine cho chote isipokuwa hii mana!”

7 Mana ilifanana kama mbegu za giligilani, nayo ilikuwa na rangi ya manjano iliyopauka.

8 Hao watu walikwenda kukusanya, kisha waliisaga kwa mawe ya kusagia ya mkono au kuitwanga kwenye vinu. Waliipika vyunguni au kutengeneza maandazi. Ladha yake ilikuwa kama kitu kilichotengenezwa kwa mafuta ya zeituni.

9 Umande ulipoanguka kambini wakati wa usiku, pia mana ilianguka pamoja nao.

10 Mose akasikia watu wa kila jamaa wakilia, kila mmoja kwenye mlango wa hema lake.Bwanaakakasirika mno, naye Mose akafadhaika.

11 AkamwulizaBwana, “Kwa nini umeleta taabu hii juu ya mtumishi wako? Nimekufanyia nini cha kukuchukiza hata ukaweka mzigo huu wa watu hawa wote juu yangu?

12 Je, watu hawa wote mimi ndiye niliyewatungisha mimba? Je, ni mimi niliyewazaa? Kwa nini unaniambia niwachukue mikononi mwangu, kama vile mlezi abebavyo mtoto mchanga, hadi kwenye nchi uliyowaahidi baba zao?

13 Nitapata wapi nyama kwa ajili ya watu wote hawa? Wanaendelea kunililia wakisema, ‘Tupe nyama tule!’

14 Mimi siwezi kuwabeba watu hawa wote peke yangu, mzigo ni mzito sana kwangu.

15 Kama hivi ndivyo unavyonitendea, uniue sasa hivi, yaani kama nimepata kibali machoni pako, wala usiniache nione maangamizi yangu mwenyewe.”

16 Bwanaakamwambia Mose: “Niletee wazee sabini wa Israeli, unaowafahamu kama viongozi na maafisa miongoni mwa watu. Walete katika Hema la Kukutania, ili waweze kusimama huko pamoja nawe.

17 Nami nitashuka na kusema nawe huko. Nami nitachukua sehemu ya Roho ile iliyo juu yako na kuiweka hiyo Roho juu yao. Watakusaidia kubeba mzigo wa watu hao ili usije ukaubeba peke yako.

18 “Waambie hao watu: ‘Jiwekeni wakfu wenyewe kwa ajili ya kesho, wakati mtakapokula nyama.Bwanaaliwasikia mlipolia, mkisema, “Laiti tungekuwa na nyama tule! Tulikuwa na hali nzuri zaidi katika nchi ya Misri!” SasaBwanaatawapa nyama, nanyi mtaila.

19 Hamtaila kwa siku moja tu, au siku mbili, au tano, kumi au siku ishirini,

20 bali kwa mwezi mzima mpaka ziwatokee puani nanyi mtaichukia kabisa, kwa kuwa mmemkataaBwana, ambaye yupo miongoni mwenu, nanyi mmelia mbele zake, mkisema, “Hivi kwa nini tulitoka Misri?” ’ ”

21 Lakini Mose alisema, “Mimi niko hapa miongoni mwa watu 600,000 wanaotembea kwa miguu, nawe umesema, ‘Nitawapa nyama za kula kwa mwezi mzima!’

22 Je, wangeweza kupata nyama ya kuwatosha hata kama makundi ya kondoo na ya ng’ombe yangechinjwa kwa ajili yao? Je, wangetosheka hata kama samaki wote wa baharini wangevuliwa kwa ajili yao?”

23 Bwanaakamjibu Mose, “Je, mkono waBwanani mfupi sana? Sasa utaona kama jambo nililolisema halitatimizwa kwa ajili yako au la.”

24 Kwa hiyo Mose akatoka na kuwaambia watu lile ambaloBwanaalikuwa amesema. Akawakusanya wazee wao sabini, akawasimamisha kuzunguka Hema.

25 KishaBwanaakashuka katika wingu na kunena na Mose, naye akachukua sehemu ya Roho iliyokuwa juu ya Mose na kuiweka hiyo Roho juu ya wale wazee sabini. Roho aliposhuka juu yao, wakatoa unabii, lakini hawakufanya hivyo tena.

26 Lakini, watu wawili, ambao majina yao ni Eldadi na Medadi, walibaki kambini. Walikuwa wameorodheshwa miongoni mwa wale wazee sabini, lakini hawakutoka kwenda kwenye Hema. Lakini Roho pia alishuka juu yao, nao wakatabiri huko kambini.

27 Mwanaume mmoja kijana alikimbia na kumwambia Mose, “Eldadi na Medadi wanatoa unabii kambini.”

28 Yoshua mwana wa Nuni, ambaye alikuwa msaidizi wa Mose tangu ujana wake, akajibu akasema, “Mose bwana wangu, wanyamazishe!”

29 Lakini Mose akajibu, “Je, unaona wivu kwa ajili yangu? Ningetamani watu wote waBwanawangekuwa manabii na kwambaBwanaangeweka Roho yake juu yao!”

30 Ndipo Mose na wale wazee wa Israeli wakarudi kambini.

31 Kisha ukatokea upepo kutoka kwaBwana, nao ukawaletea kware kutoka baharini. Ukawaangusha kwenye eneo lote linalozunguka kambi na kujaa ardhini kimo cha mita moja hivi kutoka ardhini kwenye eneo la umbali wa mwendo wa siku moja kila upande.

32 Mchana kutwa na usiku kucha pamoja na siku nzima iliyofuata watu walitoka kwenda kuokota kware. Hakuna mtu ye yote aliyekusanya chini ya homeri kumi. Kisha wakazianika kuzunguka kambi yote.

33 Lakini wakati walipokuwa wakila nyama ingali bado kati ya meno yao na kabla hawajamaliza kula, hasira yaBwanaikawaka dhidi ya watu, naye akawapiga kwa tauni.

34 Kwa hiyo mahali hapo pakaitwa Kibroth-Hataava, kwa sababu huko ndiko walipowazika watu ambao walitamani sana chakula kingine.

35 Kutoka Kibroth-Hataava watu wakasafiri mpaka Haaserothi na kukaa huko.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/NUM/11-58a1d45624f44c87cc2c9f6eeef0d02d.mp3?version_id=1627—

Hesabu 12

Miriamu Na Aroni Wampinga Mose

1 Miriamu na Aroni walianza kuzungumza dhidi ya Mose kwa sababu ya mke wake Mkushi, kwa kuwa alikuwa ameoa Mkushi.

2 Waliuliza, “Je,Bwanaamesema kupitia Mose peke yake? Je, hajasema kutupitia sisi pia?” NayeBwanaakasikia hili.

3 (Basi Mose alikuwa mtu mnyenyekevu sana, mnyenyekevu kuliko mtu mwingine ye yote katika uso wa dunia.)

4 GhafulaBwanaakawaambia Mose, Aroni na Miriamu, “Njoni katika Hema la Kukutania, ninyi nyote watatu.” Kwa hiyo wote watatu wakaenda.

5 KishaBwanaakashuka katika nguzo ya wingu, akasimama kwenye ingilio la Hema, akawaita Aroni na Miriamu. Wakati wote wawili waliposogea mbele,

6 Bwanaakasema, “Sikilizeni maneno yangu:

“Akiwapo nabii waBwanamiongoni mwenu,

nitajifunua kwake kwa maono,

nitanena naye katika ndoto.

7 Lakini sivyo kwa mtumishi wangu Mose;

yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote.

8 Kwake nitanena naye uso kwa uso,

waziwazi wala si kwa mafumbo;

yeye ataona umbo laBwana.

Kwa nini basi ninyi hamkuogopa

kuzungumza kinyume cha mtumishi wangu Mose?”

9 Hasira yaBwanaikawaka dhidi yao, akawaacha.

10 Wakati hilo wingu lilipoinuka kutoka juu ya Hema, Miriamu akawa tayari ana ukoma, mweupe kama theluji. Aroni akamgeukia akaona ana ukoma;

11 akamwambia Mose, “Tafadhali, bwana wangu, usituhesabie dhambi hii ambayo tumeifanya kwa upumbavu.

12 Usimwache awe kama mtoto mchanga aliyezaliwa akiwa mfu, ambaye nusu ya mwili wake imeharibika hapo atokapo katika tumbo la mama yake.”

13 Hivyo Mose akamliliaBwanaakisema, “Ee Mungu, nakuomba umponye!”

14 Bwanaakamjibu Mose, “Je, kama baba yake angemtemea usoni, asingeona aibu kwa siku saba? Mfungie nje ya kambi kwa siku saba; baada ya hapo anaweza kurudishwa kambini.”

15 Kwa hiyo Miriamu akafungiwa nje ya kambi kwa siku saba, nao watu hawakuendelea na safari mpaka aliporudishwa kambini.

16 Baada ya hayo, watu waliondoka Haserothi, wakapiga kambi katika Jangwa la Parani.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/NUM/12-ca41a1439e1a5ac5eca1313dc61c6e01.mp3?version_id=1627—

Hesabu 13

Kupeleleza Kanaani

1 Bwanaakamwambia Mose,

2 “Watume baadhi ya watu wakaipeleleze nchi ya Kanaani, ambayo ninawapa Waisraeli. Kutoka katika kila kabila la baba zao tuma mmoja wa viongozi wao.”

3 Hivyo kwa agizo laBwanaMose akawatuma kutoka Jangwa la Parani. Wote walikuwa viongozi wa Waisraeli.

4 Haya ndiyo majina yao:

kutoka kabila la Reubeni, Shamua mwana wa Zakuri;

5 kutoka kabila la Simeoni, Shafati mwana wa Hori;

6 kutoka kabila la Yuda, Kalebu mwana wa Yefune;

7 kutoka kabila la Isakari, Igali mwana wa Yosefu;

8 kutoka kabila la Efraimu, Hoshea mwana wa Nuni;

9 kutoka kabila la Benyamini, Palti mwana wa Rafu;

10 kutoka kabila la Zabuloni, Gadieli mwana wa Sodi,

11 kutoka kabila la Manase (kabila la Yosefu), Gadi mwana wa Susi;

12 kutoka kabila la Dani, Amieli mwana wa Gemali;

13 kutoka kabila la Asheri, Sethuri mwana wa Mikaeli;

14 kutoka kabila la Naftali, Nabi mwana wa Wofsi;

15 kutoka kabila la Gadi, Geueli mwana wa Maki.

16 Haya ndiyo majina ya watu ambao Mose aliwatuma kuipeleleza nchi. (Mose akampa Hoshea mwana wa Nuni jina la Yoshua.)

17 Mose alipowatuma wakaipeleleze Kanaani, alisema, “Pandeni kupitia Negebu, mwende mpaka nchi ya vilima.

18 Mwuone nchi ni ya namna gani, na kama watu waishio humo wana nguvu au ni dhaifu, iwapo ni wachache au wengi.

19 Wanaishi katika nchi ya namna gani? Je, ni nzuri au mbaya? Wanaishi katika miji ya namna gani? Je, haina kuta au ngome?

20 Ardhi ikoje? Ina rutuba au la? Je, kuna miti ndani yake au la? Jitahidini kadiri mwezavyo kuleta baadhi ya matunda ya nchi.” (Ulikuwa msimu wa kuiva zabibu za kwanza.)

21 Hivyo wakapanda na kuipeleleza nchi kutoka Jangwa la Sini hadi Rehobu, kuelekea Lebo-Hamathi.

22 Wakapanda kupitia Negebu hadi wakafika Hebroni, mahali ambapo Ahimani, Sheshai na Talmai, wazao wa Anaki, walipoishi. (Hebroni ulikuwa umejengwa miaka saba kabla ya mji wa Soani ulioko Misri.)

23 Walipofika katika Bonde la Eshkoli, walivunja tawi lililokuwa na kishada kimoja cha zabibu. Wawili wao wakalichukua lile tawi kwenye mti, pamoja na komamanga na tini.

24 Eneo lile likaitwa Bonde la Eshkoli kwa sababu ya kile kishada cha zabibu ambacho Waisraeli walikikata huko.

25 Mwishoni mwa siku arobaini wakarudi kutoka kuipeleleza nchi.

Taarifa Juu Ya Upelelezi

26 Wakarudi kwa Mose, Aroni na jumuiya yote ya Waisraeli huko Kadeshi kwenye Jangwa la Parani. Hapo ndipo walipotoa habari kwao na kwa kusanyiko lote na kuwaonyesha matunda ya hiyo nchi.

27 Wakampa Mose taarifa hii: “Tuliingia katika nchi uliyotutuma, nayo inatiririka maziwa na asali! Hili hapa tunda lake.

28 Lakini watu wanaoishi huko ni wenye nguvu, na miji yao ina ngome na ni mikubwa sana. Huko tuliona hata wazao wa Anaki.

29 Waamaleki wanaishi Negebu; Wahiti, Wayebusi na Waamori wanaishi katika nchi ya vilima; nao Wakanaani wanaishi karibu na bahari na kando ya Yordani.”

30 Kisha Kalebu akawanyamazisha watu mbele ya Mose na kusema, “Imetupasa kupanda na kuimiliki nchi, kwa maana hakika tunaweza kufanya hivyo.”

31 Lakini watu waliokuwa wamepanda pamoja naye wakasema, “Hatuwezi kuwashambulia wale watu; wana nguvu kuliko sisi.”

32 Wakaeneza taarifa mbaya miongoni mwa Waisraeli kuhusu nchi waliyoipeleleza. Wakasema, “Nchi tuliyoipeleleza hula watu waishio ndani yake. Watu wote tuliowaona huko ni majitu.

33 Tuliwaona Wanefili huko (wazao wa Anaki wanatokana na Wanefili.) Tulijiona kama panzi machoni petu wenyewe, nao ndivyo walivyotuona.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/NUM/13-08507c2a8a2cf8b620a0a47e1763ca28.mp3?version_id=1627—

Hesabu 14

Watu Wanaasi

1 Usiku ule watu wote wa jumuiya walipaza sauti zao na kulia kwa sauti kuu.

2 Waisraeli wote wakanung’unika dhidi ya Mose na Aroni, nalo kusanyiko lote wakawaambia, “Laiti tungekuwa tumefia humo nchi ya Misri! Au humu kwenye hili jangwa!

3 Kwa niniBwanaanatuleta katika nchi hii ili tufe kwa upanga? Wake zetu na watoto wetu watachukuliwa kama nyara. Je, isingekuwa bora kwetu kurudi Misri?”

4 Wakasemezana wao kwa wao, “Inatupasa kumchagua kiongozi na kurudi Misri.”

5 Ndipo Mose na Aroni wakaanguka kifudifudi mbele ya kusanyiko lote la Kiisraeli lililokusanyika hapo.

6 Yoshua mwana wa Nuni na Kalebu mwana wa Yefune, waliokuwa miongoni mwa watu wale waliokwenda kuipeleleza nchi, wakararua nguo zao,

7 wakasema na kusanyiko lote la Kiisraeli, wakawaambia, “Nchi tuliyopita katikati yake na kuipeleleza ni nzuri sana sana.

8 IkiwaBwanaanapendezwa nasi, atatuongoza kuingia katika nchi ile, nchi itiririkayo maziwa na asali, naye atatupa nchi hiyo.

9 Ila tu msimwasiBwana. Wala msiwaogope watu wa nchi hiyo, kwa sababu tutawameza. Ulinzi wao umeondoka, lakiniBwanayupo pamoja nasi. Msiwaogope.”

10 Lakini kusanyiko lote likazungumza juu ya kuwapiga kwa mawe. Ndipo utukufu waBwanaukaonekana katika Hema la Kukutania kwa Waisraeli wote.

11 Bwanaakamwambia Mose, “Watu hawa watanidharau mpaka lini? Wataendelea kukataa kuniamini mimi mpaka lini, ingawa nimetenda ishara za miujiza miongoni mwao?

12 Nitawapiga kwa tauni na kuwaangamiza, lakini nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa lenye nguvu kuliko wao.”

13 Mose akamwambiaBwana, “Ndipo Wamisri watasikia juu ya jambo hili! Kwa uweza wako uliwapandisha watu hawa kutoka miongoni mwao.

14 Nao watawaambia wenyeji wa nchi hii jambo hili. Wao tayari wameshasikia kwamba wewe, EeBwana, upo pamoja na watu hawa, na kuwa wewe, EeBwana, umeonekana uso kwa uso, nalo wingu lako hukaa juu yao, tena wewe, unawatangulia kwa nguzo ya wingu mchana na kwa nguzo ya moto usiku.

15 Ikiwa utawaua watu hawa wote kwa mara moja, mataifa ambayo yamesikia taarifa hii kukuhusu wewe watasema,

16 ‘Bwanaalishindwa kuwaingiza watu hawa katika nchi aliyowaahidi kwa kiapo; hivyo akawaua jangwani.’

17 “Basi sasa nguvu za Bwana na zionekane, sawasawa na vile ulivyosema,

18 ‘Bwanasi mwepesi wa hasira, ni mwingi wa upendo na mwenye kusamehe dhambi na uasi. Lakini haachi kumwadhibu mwenye hatia, huadhibu watoto kwa ajili ya dhambi ya baba zao hata kizazi cha tatu na cha nne.’

19 Kwa kadiri ya upendo wako mkuu, usamehe dhambi ya watu hawa, kama vile ulivyowasamehe tangu wakati walipotoka Misri mpaka sasa.”

20 Bwanaakajibu, “Nimewasamehe kama ulivyoomba.

21 Hata hivyo, kwa hakika kama niishivyo, na kwa hakika kama utukufu waBwanauijazavyo dunia yote,

22 hakuna hata mmoja wa watu hawa ambao waliuona utukufu wangu na ishara za miujiza niliyotenda huko Misri na huko jangwani, lakini ambaye hakunitii na akanijaribu mara hizi kumi,

23 hakuna hata mmojawapo atakayeona nchi niliyowaahidi baba zao kwa kiapo. Hakuna hata mmoja ambaye amenidharau atakayeiona.

24 Lakini kwa sababu mtumishi wangu Kalebu ana roho ya tofauti na ananifuata kwa moyo wote, nitamwingiza katika nchi aliyoiendea, nao wazao wake watairithi.

25 Kwa kuwa Waamaleki na Wakanaani wanaishi katika mabonde, kesho geukeni mwelekee jangwani kwa kufuata njia iendayo Bahari ya Shamu.”

26 Bwanaakamwambia Mose na Aroni:

27 “Jumuiya hii ovu itanung’unika dhidi yangu hadi lini? Nimesikia malalamiko ya hawa Waisraeli wanaonung’unika.

28 Hivyo waambie, ‘Hakika kama niishivyo, asemaBwana, nitawafanyia vitu vile vile nilivyosikia mkisema:

29 Kila mmoja wenu mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi ambaye alihesabiwa na ambaye amenung’unika dhidi yangu, miili yenu itaanguka katika jangwa hili.

30 Hakuna hata mmoja wenu atakayeingia katika nchi niliyoapa kwa mkono ulioinuliwa kuwa makao yenu, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, na Yoshua mwana wa Nuni.

31 Lakini watoto wenu ambao mlisema watachukuliwa kama mateka, nitawaingiza humo ili waifurahie nchi ambayo ninyi mmeikataa.

32 Lakini ninyi, miili yenu itaanguka katika jangwa hili.

33 Watoto wenu watakuwa wachungaji wa mifugo hapa kwa miaka arobaini, wakiteseka kwa ajili ya kukosa uaminifu kwenu, hadi mwili wa mtu wenu wa mwisho ulale katika jangwa hili.

34 Kwa miaka arobaini, mwaka mmoja kwa kila siku katika zile siku arobaini mlizoipeleleza nchi, mtateseka kwa ajili ya dhambi zenu, na kujua jinsi ilivyo vibaya kunifanya mimi kuwa adui yenu.’

35 MimiBwananimesema, na hakika nitafanya mambo haya kwa jumuiya hii yote ovu, ambayo imefungamana pamoja dhidi yangu. Watakutana na mwisho wao katika jangwa hili; hapa ndipo watafia.”

36 Hivyo watu wale ambao Mose alikuwa amewatuma kuipeleleza nchi, waliorudi na kuifanya jumuiya nzima kunung’unika dhidi ya Mose kwa kueneza taarifa mbaya kuhusu hiyo nchi,

37 watu hawa waliohusika kueneza taarifa mbaya kuhusu hiyo nchi walipigwa na kuanguka kwa tauni mbele zaBwana.

38 Miongoni mwa watu waliokwenda kuipeleleza hiyo nchi, ni Yoshua mwana wa Nuni, na Kalebu mwana wa Yefune peke yao waliosalia.

39 Mose alipotoa taarifa hii kwa Waisraeli wote, waliomboleza kwa uchungu.

40 Mapema asubuhi siku iliyofuata walipanda juu kuelekea kwenye nchi ya vilima virefu, wakasema, “Tumetenda dhambi. Tutakwea mpaka mahaliBwanaalipotuahidi.”

41 Lakini Mose akasema, “Kwa nini hamtii amri yaBwana? Jambo hili halitafanikiwa!

42 Msipande juu, kwa kuwaBwanahayupo pamoja nanyi. Mtashindwa na adui zenu,

43 kwa kuwa Waamaleki na Wakanaani watapambana nanyi huko. Kwa sababu mmemwachaBwana, hatakuwa pamoja nanyi, ninyi mtaanguka kwa upanga.”

44 Hata hivyo, kwa kiburi chao walipanda juu kuelekea nchi ya vilima virefu, ijapokuwa Mose hakutoka kambini wala Sanduku la Agano laBwana.

45 Ndipo Waamaleki na Wakanaani walioishi katika hiyo nchi ya vilima wakatelemka na kuwashambulia, wakawapiga njia yote hadi Horma.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/NUM/14-63bb5135a58486d93ccd99ed8ecc6bce.mp3?version_id=1627—