Hesabu 25

Moabu Yashawishi Israeli

1 Wakati Israeli alipokuwa akikaa Shitimu, wanaume wa Israeli walianza kuzini na wanawake wa Kimoabu,

2 ambao waliwaalika kushiriki katika kutoa kafara kwa miungu yao. Watu wakala na kusujudu mbele ya miungu hii.

3 Kwa hiyo Israeli akaungana katika kumwabudu Baali wa Peori. Hasira yaBwanaikawaka dhidi yao.

4 Bwanaakamwambia Mose, “Uwachukue viongozi wote wa watu hawa, uwaue na uwaweke hadharani mchana peupe mbele zaBwana, ili hasira kali yaBwanaiweze kuondoka kwa Israeli.”

5 Kwa hiyo Mose akawaambia waamuzi wa Israeli, “Kila mmoja wenu lazima awaue wale wanaume wenu, walioshiriki katika kumwabudu Baali wa Peori.”

6 Ndipo mwanaume wa Kiisraeli akamleta mwanamke wa Kimidiani katika jamaa yake pale pale mbele ya Mose na mkutano wote wa Israeli walipokuwa wakilia kwenye lango la Hema la Kukutania.

7 Finehasi mwana wa Eleazari, mwana wa kuhani Aroni, alipoona jambo hili, akaondoka kwenye kusanyiko, akachukua mkuki mkononi mwake,

8 akamfuata yule Mwisraeli ndani ya hema. Akawachoma mkuki wote wawili kwa pamoja, ukapenya kwenye mwili wa yule Mwisraeli na mwili wa yule mwanamke. Ndipo tauni iliyokuwepo dhidi ya Waisraeli ikakoma.

9 Lakini wale waliokufa kwa hiyo tauni walikuwa watu 24,000.

10 Bwanaakamwambia Mose,

11 “Finehasi mwana wa Eleazari, mwana wa kuhani Aroni, amegeuza hasira yangu mbali na Waisraeli, kwa sababu alikuwa na wivu kama nilio nao kwa heshima yangu miongoni mwao, hata kwamba kwa wivu wangu sikuwaangamiza.

12 Kwa hiyo mwambie Finehasi ninafanya Agano langu la amani naye.

13 Yeye pamoja na wazao wake watakuwa na Agano la ukuhani milele, kwa sababu alikuwa na wivu kwa ajili ya heshima ya Mungu wake, na akafanya upatanisho kwa Waisraeli.”

14 Jina la Mwisraeli ambaye aliuawa pamoja na mwanamke wa Kimidiani ni Zimri mwana wa Salu, kiongozi wa jamaa ya Simeoni.

15 Jina la mwanamke wa Kimidiani aliyeuawa ni Kozbi binti wa Suri, aliyekuwa mkuu wa kabila la jamaa ya Wamidiani.

16 Bwanaakamwambia Mose,

17 “Watendeeni Wamidiani kama adui na muwaue,

18 kwa sababu wao waliwatendea kama adui wakati walipowadanganya katika tukio la Peori na dada yao Kozbi, binti wa kiongozi wa Kimidiani, mwanamke ambaye aliuawa wakati tauni ilipokuja kama matokeo ya tukio la Peori.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/NUM/25-bd2332b34b9c96b44a543da63c15ad04.mp3?version_id=1627—

Hesabu 26

Kuhesabiwa Watu Mara Ya Pili

1 Baada ya hiyo tauni,Bwanaakamwambia Mose na Eleazari mwana wa kuhani Aroni,

2 “Hesabu jumuiya yote ya Kiisraeli kwa jamaa zao, wale wote wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, ambao wanaweza kutumika katika jeshi la Israeli.”

3 Hivyo Mose na kuhani Eleazari wakazungumza na watu kwenye nchi tambarare ya Moabu, ng’ambo ya Yordani kutokea Yeriko, wakasema,

4 “Hesabuni wanaume wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, kamaBwanaalivyomwagiza Mose.”

Hawa ndio Waisraeli waliotoka Misri:

5 Wazao wa Reubeni, mwana mzaliwa wa kwanza wa Israeli, walikuwa:

kutoka kwa Hanoki, ukoo wa Wahanoki;

kutoka kwa Palu, ukoo wa Wapalu;

6 kutoka kwa Hesroni, ukoo wa Wahezroni;

kutoka kwa Karmi, ukoo wa Wakarmi.

7 Hizi zilikuwa ndizo koo za Reubeni; wale waliohesabiwa walikuwa 43,730.

8 Mwana wa Palu alikuwa Eliabu,

9 nao wana wa Eliabu walikuwa Nemueli, Dathani na Abiramu. Hawa wawili Dathani na Abiramu ndio walikuwa maafisa wa jumuiya ambao walimwasi Mose na Aroni, na walikuwa miongoni mwa wafuasi wa Kora wakati walipomwasiBwana.

10 Ardhi ilifunua kinywa chake na kuwameza pamoja na Kora, ambaye wafuasi wake walikufa wakati moto ulipowateketeza wanaume 250. Nao walikuwa kama alama ya onyo.

11 Pamoja na hayo, hao ukoo wa Kora hawakufa.

12 Wazao wa Simeoni kwa koo zao walikuwa:

kutoka kwa Nemueli, ukoo wa Wanemueli;

kutoka kwa Yamini, ukoo wa Wayamini;

13 kutoka kwa Sohari, ukoo wa Wasohari;

kutoka kwa Shauli, ukoo wa Washauli.

14 Hizi ndizo koo za Simeoni; walikuwa 22,200.

15 Wazao wa Gadi kwa koo zao walikuwa:

kutoka kwa Sifoni, ukoo wa Wasifoni;

kutoka kwa Hagi, ukoo wa Wahagi;

kutoka kwa Shuni, ukoo wa Washuni;

16 kutoka kwa Ozni, ukoo wa Waozni;

kutoka kwa Eri, ukoo wa Waeri;

17 kutoka kwa Arodi, ukoo wa Waarodi;

kutoka kwa Areli, ukoo wa Waareli.

18 Hizi ndizo zilizokuwa koo za Gadi; wale waliohesabiwa walikuwa 40,500.

19 Eri na Onani walikuwa wana wa Yuda, lakini walifia huko Kanaani.

20 Wazao wa Yuda kwa koo zao walikuwa:

kutoka kwa Shela, ukoo wa Washela;

kutoka kwa Peresi, ukoo wa Waperesi;

kutoka kwa Zera, ukoo wa Wazera.

21 Wazao wa Peresi walikuwa:

kutoka kwa Hesroni, ukoo wa Wahezroni;

kutoka kwa Hamuli, ukoo wa Wahamuli.

22 Hizi ndizo zilizokuwa koo za Yuda; wale waliohesabiwa walikuwa 76,500.

23 Wazao wa Isakari kwa koo zao walikuwa:

kutoka kwa Tola, ukoo wa Watola;

kutoka kwa Pua, ukoo wa Wapua;

24 kutoka kwa Yashubu, ukoo wa Wayashubu;

kutoka kwa Shimroni, ukoo wa Washimroni.

25 Hizi ndizo zilizokuwa koo za Isakari; wale waliohesabiwa walikuwa 64,300.

26 Wazao wa Zabuloni kwa koo zao walikuwa:

kutoka kwa Seredi, ukoo wa Waseredi;

kutoka kwa Eloni, ukoo wa Waeloni;

kutoka kwa Yahleeli, ukoo wa Wayaleeli.

27 Hizi ndizo zilizokuwa koo za Zabuloni, wale waliohesabiwa walikuwa 60,500.

28 Wazao wa Yosefu kwa koo zao kutoka kwa Manase na kwa Efraimu walikuwa:

29 Wazao wa Manase:

kutoka kwa Makiri, ukoo wa Wamakiri (Makiri alikuwa baba wa Gileadi);

kutoka kwa Gileadi, ukoo wa Wagileadi.

30 Hawa ndio waliokuwa wazao wa Gileadi:

kutoka kwa Iezeri, ukoo wa Waiezeri;

kutoka kwa Heleki, ukoo wa Waheleki;

31 kutoka kwa Asrieli, ukoo wa Waasrieli;

kutoka kwa Shekemu, ukoo wa Washekemu;

32 kutoka kwa Shemida, ukoo wa Washemida;

kutoka kwa Heferi, ukoo wa Waheferi.

33 (Selofehadi mwana wa Heferi hakuzaa wana, bali alikuwa na watoto wa kike tu, ambao majina yao yalikuwa Mahla, Noa, Hogla, Milka na Tirsa.)

34 Hizi ndizo zilizokuwa koo za Manase; wale waliohesabiwa walikuwa 52,700.

35 Hawa walikuwa wazao wa Efraimu kwa koo zao:

kutoka kwa Shuthela, ukoo wa Washuthela;

kutoka kwa Bekeri, ukoo wa Wabekeri;

kutoka kwa Tahani, ukoo wa Watahani;

36 Hawa ndio walikuwa wazao wa Shuthela:

kutoka kwa Erani, ukoo wa Waerani.

37 Hizi ndizo zilizokuwa koo za Efraimu; wale waliohesabiwa walikuwa 32,500.

Hawa ndio waliokuwa wazao wa Yosefu kwa koo zao.

38 Wazao wa Benyamini kwa koo zao walikuwa:

kutoka kwa Bela, ukoo wa Wabela;

kutoka kwa Ashbeli, ukoo wa Waashbeli;

kutoka kwa Ahiramu, ukoo wa Waahiramu;

39 kutoka kwa Shufamu, ukoo wa Washufamu;

kutoka kwa Hufamu, ukoo wa Wahufamu.

40 Wazao wa Bela kutoka kwa Ardi na Naamani walikuwa:

kutoka kwa Ardi, ukoo wa Waardi;

kutoka kwa Naamani, ukoo wa Wanaamani.

41 Hizi ndizo zilizokuwa koo za Benyamini; wale waliohesabiwa walikuwa 45,600.

42 Hawa ndio waliokuwa wazao wa Dani kwa koo zao:

kutoka kwa Shuhamu, ukoo wa Washuhamu.

Hizi ndizo zilizokuwa koo za Dani:

43 Wote walikuwa koo za Washuhamu; wale waliohesabiwa walikuwa 64,400.

44 Wazao wa Asheri kwa koo zao walikuwa:

kutoka kwa Imna, ukoo wa Waimna;

kutoka kwa Ishvi, ukoo wa Waishvi;

kutoka kwa Beria, ukoo wa Waberia;

45 kutoka kwa wazao wa Beria:

kutoka kwa Heberi, ukoo wa Waheberi;

kutoka kwa Malkieli, ukoo wa Wamalkieli.

46 (Asheri alikuwa na binti aliyeitwa Sera.)

47 Hizi ndizo zilizokuwa koo za Asheri; wale waliohesabiwa walikuwa 53,400.

48 Wazao wa Naftali kwa koo zao walikuwa:

kutoka kwa Yahseeli, ukoo wa Wayaseeli;

kutoka kwa Guni, ukoo wa Waguni;

49 kutoka kwa Yeseri, ukoo wa Wayeseri;

kutoka kwa Shilemu, ukoo wa Washilemu.

50 Hizi ndizo zilizokuwa koo za Naftali; wale waliohesabiwa walikuwa 45,400.

51 Jumla ya hesabu ya wanaume wa Israeli ilikuwa 601,730.

52 Bwanaakamwambia Mose,

53 “Watagawiwa nchi kama urithi kwa kulingana na hesabu ya majina.

54 Kundi kubwa zaidi lipe urithi mkubwa zaidi, na kundi dogo zaidi lipewe urithi mdogo zaidi; kila kundi litapokea urithi wake kulingana na hesabu ya wale walioorodheshwa.

55 Hakikisha kuwa nchi inagawanywa kwa kura. Kile kitakachorithiwa na kila kikundi kitakuwa kwa kulingana na majina ya kabila la babu yao.

56 Kila urithi utagawanywa kwa kura miongoni mwa makundi makubwa na madogo.”

57 Hawa walikuwa Walawi ambao walihesabiwa kwa koo zao:

kutoka kwa Gershoni, ukoo wa Wagerishoni;

kutoka kwa Kohathi, ukoo wa Wakohathi;

kutoka kwa Merari, ukoo wa Wamerari.

58 Hizi pia zilikuwa koo za Walawi:

ukoo wa Walibni;

ukoo wa Wahebroni;

ukoo wa Wamatili;

ukoo wa Wamushi;

ukoo wa Wakora.

(Kohathi alikuwa baba aliyemzaa Amramu;

59 jina la mke wa Amramu ni Yokobedi, naye pia alikuwa mzao wa Lawi, ambaye alizaliwa kwa Walawi nchini Misri. Alimzalia Amramu: Aroni, Mose na dada yao Miriamu.

60 Aroni alikuwa baba yake Nadabu na Abihu, Eleazari na Ithamari.

61 Lakini Nadabu na Abihu walikufa wakati walipotoa sadaka mbele zaBwanakwa moto usioruhusiwa.)

62 Wanaume wote wa Walawi wa umri wa mwezi mmoja na zaidi walikuwa 23,000. Wao hawakuhesabiwa pamoja na Waisraeli wengine kwa sababu hawakupokea urithi miongoni mwao.

63 Hawa ndio walioorodheshwa na Mose na kuhani Eleazari wakati walipowahesabu Waisraeli kwenye nchi tambarare ya Moabu, kando ya Yordani ng’ambo ya Yeriko.

64 Hakuna hata mmoja wao aliyekuwa miongoni mwa wale waliohesabiwa na Mose na kuhani Aroni wakati walipowahesabu Waisraeli katika Jangwa la Sinai.

65 Kwa maanaBwanaalikwishawaambia hao Waisraeli hakika wangekufa huko jangwani, wala hakuna mmoja wao aliyeachwa, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune na Yoshua mwana wa Nuni.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/NUM/26-c783ac4c556bd1e9e1e21a144754f30c.mp3?version_id=1627—

Hesabu 27

Binti Wa Selofehadi

1 Binti za Selofehadi mwana wa Heferi, mwana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase, walikuwa wa koo za Manase mwana wa Yosefu. Majina ya hao binti yalikuwa Mahla, Noa, Hogla, Milka na Tirsa. Walikaribia

2 ingilio la Hema la Kukutania na kusimama mbele ya Mose, kuhani Eleazari, viongozi na kusanyiko lote, wakasema,

3 “Baba yetu alikufa jangwani. Hakuwa miongoni mwa wafuasi wa Kora, ambao walifungamana pamoja dhidi yaBwana, lakini alikufa kwa ajili ya dhambi yake mwenyewe na hakuacha wana.

4 Kwa nini jina la baba yetu lifutike kutoka katika ukoo wake kwa sababu hakuwa na mwana? Tupatie milki miongoni mwa ndugu za baba yetu.”

5 Kwa hiyo Mose akalileta shauri lao mbele zaBwana,

6 nayeBwanaakamwambia,

7 “Wanachosema binti za Selofehadi ni sawa, ni lazima kwa hakika uwape milki kama urithi miongoni mwa ndugu za baba yao, na kubadili urithi wa baba yao uwe wao.

8 “Waambie Waisraeli, ‘Ikiwa mtu atakufa naye hakuacha mwana, utampa binti yake urithi wake.

9 Ikiwa hana binti, wape ndugu zake wa kiume urithi wake.

10 Ikiwa hana ndugu wa kiume toa urithi wake kwa ndugu za baba yake.

11 Ikiwa baba yake hakuwa na ndugu wa kiume, toa urithi wake kwa ndugu wa karibu katika ukoo wake, ili aumiliki. Hili litakuwa dai la sheria kwa Waisraeli, kamaBwanaalivyomwamuru Mose.’ ”

Yoshua Kuchukua Nafasi Ya Mose

12 KishaBwanaakamwambia Mose, “Panda juu ya mlima huu katika kilele cha Abarimu uione nchi ambayo nimewapa Waisraeli.

13 Baada ya kuiona, wewe pia utakusanywa pamoja na watu wako kama ndugu yako Aroni alivyokusanywa,

14 kwa kuwa jumuiya ilipoasi amri yangu kwenye maji katika Jangwa la Sini, wakati jumuiya ilipogombana nami, nyote wawili mliacha kuitii amri yangu ya kuniheshimu kama mtakatifu mbele ya macho yao.” (Haya yalikuwa maji ya Meriba huko Kadeshi, katika Jangwa la Sini.)

15 Mose akamwambiaBwana,

16 “Bwana, Mungu wa roho zote za wanadamu, na amteue mtu juu ya jumuiya hii

17 ili atoke na kuingia mbele yao, atakayewaongoza katika kutoka kwao na kuingia kwao, ili watu waBwanawasiwe kama kondoo wasio na mchungaji.”

18 Kwa hiyoBwanaakamwambia Mose, “Mchukue Yoshua mwana wa Nuni, mtu ambaye Roho yuko ndani yake, uweke mkono juu yake.

19 Msimamishe mbele ya kuhani Eleazari pamoja na kusanyiko lote, umpe maagizo mbele yao.

20 Mpe sehemu ya mamlaka yako ili jumuiya yote ya Waisraeli ipate kumtii.

21 Atasimama mbele ya kuhani Eleazari, ambaye atapokea maamuzi kwa ajili yake, kwa kuuliza mbele zaBwanakwa ile Urimu. Kwa amri yake, yeye na jumuiya yote ya Waisraeli watatoka, na kwa amri yake, wataingia.”

22 Mose akafanya kamaBwanaalivyomwagiza. Akamtwaa Yoshua na kumsimamisha mbele ya kuhani Eleazari na kusanyiko lote.

23 Kisha akaweka mikono yake juu ya kichwa cha Yoshua na kumpa maagizo, kama vileBwanaalivyoelekeza kupitia kwa Mose.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/NUM/27-24eba0022fa5a222294381f74ed8d63a.mp3?version_id=1627—

Hesabu 28

Sadaka Za Kila Siku

1 Bwanaakamwambia Mose,

2 “Wape Waisraeli agizo hili na uwaambie: ‘Hakikisheni kwamba mnaniletea mimi kwa wakati uliowekwa chakula kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa kwa moto, kama harufu nzuri ya kupendeza.’

3 Waambie: ‘Hii ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto mnayomtoleaBwana: wana kondoo wawili wa mwaka mmoja wasio na dosari, kama sadaka ya kawaida ya kuteketezwa kila siku.

4 Andaa mwana-kondoo mmoja asubuhi na mwingine jioni,

5 kila mmoja atolewe pamoja na sadaka ya nafaka sehemu ya kumi ya efaya unga laini uliochanganywa pamoja na robo ya hiniya mafuta ya zeituni.

6 Hii ni sadaka ya kawaida ya kuteketezwa iliyoanzishwa katika Mlima Sinai kama harufu nzuri ya kupendeza, sadaka iliyotolewa kwaBwanakwa moto.

7 Sadaka ya kinywaji itakayotolewa pamoja na kila mwana-kondoo ni robo ya hini ya kinywaji kilichochachuka. Mimina sadaka ya kinywaji kwaBwanamahali patakatifu.

8 Andaa yule mwana-kondoo wa pili jioni, pamoja na sadaka ya nafaka na sadaka ya kinywaji kama ulivyofanya kwa ile sadaka nyingine ya asubuhi. Hii ni sadaka iliyotolewa kwa kuteketezwa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendezaBwana.

Sadaka Za Sabato

9 “ ‘Siku ya Sabato, utatoa sadaka ya wana-kondoo wawili wa mwaka mmoja wasiokuwa na dosari pamoja na sadaka yake ya kinywaji na sadaka ya nafaka yenye uzito wa sehemu mbili za kumi za efaza unga laini uliochanganywa na mafuta.

10 Hii ni sadaka ya kuteketezwa itakayotolewa kwa ajili ya kila Sabato, pamoja na sadaka ya kawaida ya kuteketezwa na sadaka yake ya kinywaji.

Sadaka Za Kila Mwezi

11 “ ‘Siku ya kwanza ya kila mwezi, mtamleteaBwanasadaka ya kuteketezwa ya fahali wawili wachanga, kondoo dume mmoja na wana-kondoo saba wa mwaka mmoja, wote wasiokuwa na dosari.

12 Pamoja na kila fahali kutakuwa na sadaka ya nafaka ya unga laini sehemu tatu za kumi za efauliochanganywa na mafuta, pamoja na kondoo dume mmoja, sadaka ya nafaka ya unga laini uliochanganywa na mafuta;

13 pamoja na kila mwana-kondoo, sadaka ya nafaka yenye uzito wa sehemu ya kumi ya efa ya unga laini uliochanganywa na mafuta. Hii ni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, harufu nzuri, sadaka ya kuteketezwa iliyotolewa kwa moto kwaBwana.

14 Pamoja na kila fahali kutakuwa na sadaka ya kinywaji nusu ya hiniya divai; pamoja na kila kondoo dume, theluthi moja ya hini; na pamoja na kila mwana-kondoo robo hini. Hii ni sadaka ya kuteketezwa ya kila mwezi itakayotolewa kila mwandamo wa mwezi kwa mwaka.

15 Zaidi ya sadaka ya kawaida ya kuteketezwa pamoja na sadaka yake ya kinywaji, mbuzi mmoja dume atatolewa kwaBwanakama sadaka ya dhambi.

Pasaka

16 “ ‘Katika siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza itafanyika Pasaka yaBwana.

17 Katika siku ya kumi na tano ya mwezi huo itakuwa sikukuu; kwa siku saba mtakula mkate usiotiwa chachu.

18 Katika siku ya kwanza mwe na kusanyiko takatifu, msifanye kazi za kawaida.

19 Leteni mbele zaBwanasadaka ya kuteketezwa, sadaka ya kuteketezwa ya mafahali wawili wachanga, kondoo dume mmoja na wana-kondoo waume saba wenye umri wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari.

20 Pamoja na kila fahali andaa sadaka ya nafaka sehemu tatu za kumi za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta; pamoja na kondoo dume, andaa sehemu mbili za kumi za efa;

21 pia pamoja na kila mmoja wa wale wana-kondoo saba, andaa sehemu ya kumi ya efa.

22 Pia mtoe beberu mmoja kama sadaka ya dhambi ambaye atafanya upatanisho kwa ajili yenu.

23 Andaa hizi licha ya zile sadaka za kawaida za kuteketezwa za kila asubuhi.

24 Kwa njia hii andaa chakula cha sadaka ya kuteketezwa kila siku, kwa siku saba kama harufu nzuri impendezayoBwana. Hii itaandaliwa licha ya ile sadaka ya kawaida ya kuteketezwa ya kila siku pamoja na sadaka yake ya kinywaji.

25 Siku ya saba muwe na kusanyiko takatifu na msifanye kazi zenu za kaiwada.

Sikukuu Ya Majuma

26 “ ‘Siku ya malimbuko, mnapomleteaBwanasadaka ya nafaka mpya wakati wa Sikukuu ya Majuma, mwe na kusanyiko takatifu na msifanye kazi za kawaida.

27 Mlete sadaka ya kuteketezwa ya mafahali wawili wachanga, kondoo dume mmoja, na pia wana-kondoo saba wenye umri wa mwaka mmoja, kama harufu nzuri ya kumpendezaBwana.

28 Pamoja na kila fahali itatolewa sadaka ya nafaka ya unga laini sehemu tatu za kumi za efa uliochanganywa na mafuta; pamoja na kondoo dume, andaa sehemu mbili za kumi za efa za unga laini;

29 na sehemu ya kumi ya efa ya unga laini kwa kila mmoja wa wana-kondoo saba.

30 Ongeza Beberu mmoja kwa kufanya upatanisho kwa ajili yenu.

31 Andaa hizi sadaka pamoja na sadaka zake za vinywaji, kuwa nyongeza ya sadaka za kawaida za kuteketezwa, pamoja na sadaka yake ya nafaka. Hakikisha kuwa wanyama hao hawana dosari.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/NUM/28-c47f33263bb0d321271ec9fcdcc0debe.mp3?version_id=1627—

Hesabu 29

Sikukuu Ya Tarumbeta

1 “ ‘Katika siku ya kwanza ya mwezi wa saba mtakuwa na kusanyiko takatifu na msifanye kazi ya kawaida. Ni siku kwa ajili yenu ya kupiga tarumbeta.

2 Mtatayarisha sadaka ya kuteketezwa kama harufu nzuri impendezayoBwanaya fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja, na wana-kondoo saba wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari.

3 Pamoja na fahali andaeni sadaka ya nafaka sehemu ya kumi tatu za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta; kwa kondoo dume, andaa unga sehemu ya kumi mbili za efa;

4 na pamoja na wana-kondoo saba kila mmoja aandaliwe na sehemu ya kumi ya efa ya unga.

5 Ongeza beberu mmoja kama sadaka ya dhambi kufanya upatanisho kwa ajili yenu.

6 Hivi ni nyongeza ya sadaka za kuteketezwa kila mwezi na kila siku pamoja na sadaka zake za nafaka na sadaka za vinywaji kama ilivyoainishwa. Ni sadaka zinazotolewa kwaBwanakwa moto, harufu inayopendeza.

Siku Ya Upatanisho

7 “ ‘Kwenye siku ya kumi ya mwezi huu wa saba mtakuwa na kusanyiko takatifu. Mtajikana wenyewe na msifanye kazi.

8 Toeni sadaka ya kuteketezwa ya fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja, na wana-kondoo saba wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari, kama harufu nzuri inayompendezaBwana.

9 Pamoja na fahali andaeni sadaka ya nafaka sehemu ya kumi tatu za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta; pamoja na kondoo dume, sehemu ya kumi mbili za efa za unga laini;

10 na kwa kila mmoja wa wana-kondoo saba andaa sehemu ya kumi ya unga laini kwa kila mmoja.

11 Ongeza beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, katika nyongeza ya sadaka ya dhambi kwa ajili ya upatanisho, na sadaka ya kawaida ya kuteketezwa pamoja na sadaka yake ya nafaka, na sadaka zake za vinywaji.

Sikukuu Ya Vibanda

12 “ ‘Katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, mtakuwa na kusanyiko takatifu, na hamtafanya kazi za kawaida. Adhimisheni sikukuu kwaBwanakwa siku saba.

13 Toeni sadaka ya kuteketezwa mafahali wachanga kumi na watatu, kondoo waume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari, kama harufu nzuri inayompendezaBwana.

14 Pamoja na hao mafahali kumi na watatu, kila mmoja aandaliwe na sadaka ya nafaka sehemu ya kumi tatu za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta; kwa kondoo waume wawili, kila mmoja aandaliwe sehemu ya kumi mbili za efa za unga laini;

15 na kwa wana-kondoo kumi na wanne, kila mmoja aandaliwe sehemu ya kumi ya efa ya unga laini.

16 Ongeza beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, kwa nyongeza ya sadaka ya kawaida ya kuteketezwa, na sadaka yake ya nafaka, pamoja na sadaka ya vinywaji.

17 “ ‘Katika siku ya pili andaeni mafahali wachanga kumi na wawili, kondoo waume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari.

18 Pamoja na mafahali, kondoo waume, na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka na sadaka za vinywaji, kulingana na idadi iliyoainishwa.

19 Weka beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, kwa nyongeza ya kawaida ya sadaka ya kuteketezwa, na sadaka yake ya nafaka, pamoja na sadaka zao za vinywaji.

20 “ ‘Katika siku ya tatu andaeni mafahali wachanga kumi na wawili, kondoo waume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari.

21 Pamoja na mafahali, kondoo waume, na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka na sadaka za vinywaji, kulingana na idadi iliyoainishwa.

22 Weka beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, kwa nyongeza ya kawaida ya sadaka ya kuteketezwa, na sadaka yake ya nafaka, pamoja na sadaka zao za vinywaji.

23 “ ‘Katika siku ya nne andaeni mafahali wachanga kumi na wawili, kondoo waume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari.

24 Pamoja na mafahali, kondoo waume, na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka na sadaka za vinywaji, kulingana na idadi iliyoainishwa.

25 Weka beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, kwa nyongeza ya kawaida ya sadaka ya kuteketezwa, na sadaka yake ya nafaka, pamoja na sadaka zao za vinywaji.

26 “ ‘Katika siku ya tano andaeni mafahali tisa, kondoo waume wawili na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari.

27 Pamoja na mafahali, kondoo waume na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka na sadaka za kinywaji kulingana na idadi iliyoainishwa.

28 Ongeza beberu mmoja kama sadaka ya dhambi katika nyongeza ya sadaka ya kawaida ya kuteketezwa na sadaka yake ya nafaka pamoja na sadaka ya kinywaji.

29 “ ‘Katika siku ya sita andaeni mafahali wachanga kumi na wawili, kondoo waume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari.

30 Pamoja na mafahali, kondoo waume, na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka na sadaka za vinywaji, kulingana na idadi iliyoainishwa.

31 Weka beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, kwa nyongeza ya kawaida ya sadaka ya kuteketezwa, na sadaka yake ya nafaka, pamoja na sadaka zao za vinywaji.

32 “ ‘Katika siku ya saba andaeni mafahali wachanga kumi na wawili, kondoo waume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari.

33 Pamoja na mafahali, kondoo waume, na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka na sadaka za vinywaji, kulingana na idadi iliyoainishwa.

34 Weka beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, kwa nyongeza ya kawaida ya sadaka ya kuteketezwa, na sadaka yake ya nafaka, pamoja na sadaka zao za vinywaji.

35 “ ‘Katika siku ya nane mtakuwa na kusanyiko, na msifanye kazi ya kawaida.

36 Toeni sadaka ya kuteketezwa kama harufu nzuri inayompendezaBwana, sadaka ya kuteketezwa ya fahali mmoja, kondoo dume mmoja, na wana-kondoo waume saba wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari.

37 Pamoja na fahali, kondoo dume na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka, na sadaka za vinywaji, kulingana na idadi iliyoainishwa.

38 Ongeza beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, katika nyongeza ya sadaka ya kawaida ya kuteketezwa, na sadaka yake ya nafaka pamoja na sadaka ya kinywaji.

39 “ ‘Zaidi ya kile unachoweka nadhiri na sadaka zenu za hiari, andaeni hizi kwa ajili yaBwanakwenye sikukuu zenu zilizoamuriwa: sadaka zenu za kuteketezwa, sadaka za nafaka, sadaka za vinywaji, pamoja na sadaka zenu za amani.’ ”

40 Mose akawaambia Waisraeli yale yoteBwanaaliyomwagiza.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/NUM/29-d3ae3ab60847480027a5403b20baff68.mp3?version_id=1627—

Hesabu 30

Nadhiri

1 Mose akawaambia viongozi wa makabila ya Israeli: “Hili ndiloBwanaanaloagiza:

2 Wakati mwanaume awekapo nadhiri kwaBwana, au anapoapa kujifunga kwa ahadi, kamwe asitangue neno lake, bali ni lazima afanye kila kitu alichosema.

3 “Wakati mwanamwali anayeishi bado nyumbani kwa baba yake atakapoweka nadhiri kwaBwana, ama amejifunga mwenyewe kwa ahadi,

4 na baba yake akasikia kuhusu nadhiri au ahadi yake lakini asimwambie lo lote, ndipo nadhiri zake zote na kila ahadi aliyoiweka na kujifunga kwayo itathibitika.

5 Lakini kama baba yake akimkataza wakati anapoisikia, hakuna nadhiri wala ahadi yake ye yote aliyojifunga kwayo itakayosimama;Bwanaatamwacha huru huyo mwanamwali kwa sababu baba yake amemkataza.

6 “Ikiwa ataolewa baada ya kuweka nadhiri au baada ya midomo yake kutamka ahadi fulani bila kufikiri akawa amejifunga hivyo,

7 na mume wake akasikia habari hiyo asimwambie neno lo lote, ndipo nadhiri zake ama ahadi zake ambazo alikuwa amejifunga nazo zitathibitika.

8 Lakini ikiwa mume wake atamkataza atakaposikia kuhusu hilo, atakuwa ametangua nadhiri ambazo zilikuwa zimemfunga mkewe, ama ahadi aliyotamka pasipo kufikiri ambayo amejifunga kwayo, nayeBwanaatamwacha huru yule mwanamke.

9 “Nadhiri yo yote ama patano ambalo limefanywa na mjane ama mwanamke aliyeachika vitakuwa vimemfunga.

10 “Ikiwa mwanamke anayeishi na mumewe ataweka nadhiri ama kujifunga mwenyewe kwa ahadi chini ya kiapo,

11 na mumewe akasikia kuhusu jambo hili lakini asimwambie lo lote wala hakumkataza, ndipo viapo vyake vyote au ahadi zinazomfunga zitakapothibitika.

12 Lakini ikiwa mumewe atabatilisha nadhiri hizo baada ya kuzisikia, basi hakuna nadhiri au ahadi zo zote alizoziweka kwa midomo yake zitakazothibitika. Mumewe atakuwa amezibatilisha, naBwanaatamweka huru yule mwanamke.

13 Mumewe anaweza kuthibitisha au kutangua nadhiri ye yote anayoweka, au ahadi ye yote aliyoweka kwa kuapa ili kujikana mwenyewe.

14 Lakini ikiwa mumewe hasemi lo lote kwake kuhusu jambo hilo siku baada ya siku, basi mumewe atakuwa amethibitisha nadhiri zote, na ahadi zote zinazomfunga mkewe. Anavithibitisha kwa kutokusema lo lote kwa mkewe anapoyasikia hayo.

15 Hata hivyo, ikiwa mumewe atavibatilisha baada ya kusikia hayo, basi atawajibika kwa hatia ya mkewe.”

16 Haya ndiyo masharti ambayoBwanaalimpa Mose kuhusu mahusiano kati ya mtu na mkewe, na kati ya baba na binti yake ambaye bado anaishi nyumbani kwa baba yake.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/NUM/30-7e5cf57541a5082412b8624462d26a62.mp3?version_id=1627—

Hesabu 31

Kulipiza Kisasi Juu Ya Wamidiani

1 Bwanaakamwambia Mose,

2 “Uwalipize kisasi Wamidiani kwa ajili ya Waisraeli. Halafu baada ya hayo, utakufa.”

3 Kwa hiyo Mose akawaambia watu, “Waandaeni baadhi ya wanaume wenu waende vitani kupigana na Wamidiani ili wawalipize kisasi chaBwana.

4 Peleka wanaume 1,000 vitani kutoka kila kabila la Israeli.”

5 Kwa hiyo waliandaliwa wanaume 12,000 kwa vita, wanaume 1,000 kutoka kila kabila, walitolewa kutoka koo za Israeli.

6 Mose aliwatuma vitani, watu 1,000 kutoka kila kabila, pamoja na Finehasi mwana wa kuhani Eleazari, ambaye alichukua vyombo vya mahali patakatifu na tarumbeta za kuashiria.

7 Walipigana dhidi ya Wamidiani, kamaBwanaalivyomwagiza Mose, nao waliua kila mwanaume.

8 Miongoni mwa watu waliouawa walikuwepo wafalme watano wa Midiani, nao ni Evi, Rekemu, Suri, Huri na Reba. Vile vile walimwua Balaamu mwana wa Beori kwa upanga.

9 Waisraeli waliwateka wanawake wa Kimidiani pamoja na watoto wao na walichukua makundi ya ng’ombe, kondoo na mali zao kama nyara.

10 Walichoma moto miji yote ambayo Wamidiani walikuwa wanaishi, pamoja na kambi zao zote.

11 Walichukua nyara zote na mateka, pamoja na watu na wanyama,

12 nao waliwaleta wafungwa mateka na nyara kwa Mose na kwa kuhani Eleazari, nao Waisraeli walikusanyika kwenye kambi zao katika tambarare za nchi ya Moabu, kando ya Yordani ng’ambo ya Yeriko.

13 Mose, kuhani Eleazari na viongozi wote wa jumuiya wakatoka kuwalaki nje ya kambi.

14 Mose aliwakasirikia maafisa wa jeshi, yaani hao wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia, ambao walirudi kutoka vitani.

15 Mose akawauliza, “Je, mmewaacha wanawake wote hai?”

16 “Wanawake hao ndio waliofuata ushauri wa Balaamu, nao ndio waliowasababisha Waisraeli wamwasiBwanakwa kile kilichotokea kule Peori, na kwa hiyo pigo liliwapata watu waBwana.

17 Sasa waue wavulana wote. Pia umuue kila mwanamke ambaye alikwisha fanya tendo la ndoa,

18 lakini mwacheni hai kwa ajili yenu kila msichana ambaye kamwe hajawahi kuzini na mwanaume.

19 “Ninyi nyote ambao mmeua mtu ye yote au kumgusa mtu ye yote ambaye ameuawa, lazima mkae nje ya kambi kwa muda wa siku saba. Katika siku ya tatu na ya saba lazima mjitakase wenyewe pamoja na wafungwa wenu.

20 Takaseni kila vazi pamoja na kila kitu kilichotengenezwa kwa ngozi, kwa singa za mbuzi au kwa mti.”

21 Kisha kuhani Eleazari aliwaambia askari ambao walikuwa wamekwenda vitani, “Haya ndiyo matakwa ya sheria ambayoBwanaalimpa Mose:

22 Dhahabu, fedha, shaba, chuma, bati, risasi,

23 na kitu kingine cho chote ambacho kinaweza kuhimili moto lazima mkipitishe kwenye moto, kisha kitakuwa safi. Lakini ni lazima pia kitakaswe kwa maji ya utakaso. Kitu cho chote kisichoweza kuhimili moto lazima kipitishwe kwenye yale maji ya utakaso.

24 Katika siku ya saba fueni nguo zenu, nanyi mtakuwa safi. Kisha mtaweza kuingia kambini.”

Kugawanya Mateka

25 Bwanaakamwambia Mose,

26 “Wewe na kuhani Eleazari pamoja na viongozi wa jamaa ya jumuiya mtahesabu watu wote na wanyama ambao walitekwa.

27 Gawanyeni hizo nyara kati ya askari ambao walishiriki katika vita na kwa jumuiya.

28 Kutoka katika fungu la wale waliokwenda kupigana vitani, tenga kama ushuru kwa ajili yaBwanakitu kimoja kati ya kila mia tano, ikiwa ni wanadamu, ng’ombe, punda, kondoo au mbuzi.

29 Chukua ushuru huu kutoka katika fungu lao, umpe kuhani Eleazari kama sehemu yaBwana.

30 Kutoka katika fungu la Waisraeli, chukua kitu kimoja kati ya kila hamsini, ikiwa ni wanadamu, ng’ombe, punda, kondoo, mbuzi au wanyama wengine. Hivyo uwape Walawi, ambao wanawajibika kutunza Maskani yaBwana.”

31 Kwa hiyo Mose na kuhani Eleazari wakafanya kamaBwanaalivyomwagiza Mose.

32 Nyara zilizobaki kutoka katika mateka ambayo askari walichukua ni kondoo 675,000,

33 ng’ombe 72,000,

34 punda 61,000,

35 na wanawake 32,000 ambao hawakumjua mume kwa kufanya tendo la ndoa.

36 Nusu ya fungu la wale waliokwenda kupigana vitani lilikuwa:

Kondoo 337,500

37 ambayo ushuru kwa ajili yaBwanailikuwa kondoo 675;

38 ng’ombe 36,000 ambao ushuru kwa ajili yaBwanaulikuwa ng’ombe 72;

39 punda 30,500 ambao ushuru kwa ajili yaBwanaulikuwa punda 61;

40 Watu 16,000 ambao ushuru kwa ajili yaBwanaulikuwa watu 32.

41 Mose alimpa kuhani Eleazari ushuru kama sehemu yaBwana, kamaBwanaalivyomwagiza Mose.

42 Ile nusu iliyokuwa ya Waisraeli, ambayo Mose aliitenga kutoka kwa ile ya watu waliokwenda vitani,

43 nusu iliyokuwa ya jumuiya, ilikuwa kondoo 337,500,

44 ng’ombe 36,000,

45 punda 30,500,

46 na wanadamu 16,000.

47 Kutoka hiyo nusu iliyokuwa ya Waisraeli, Mose alichagua moja kati ya kila hamsini ya wanadamu na wanyama, kamaBwanaalivyomwagiza, naye aliwapa Walawi, ambao waliwajibika kutunza Maskani yaBwana.

48 Kisha maafisa ambao walikuwa juu ya vikosi vya jeshi, wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia, walimwendea Mose

49 na kumwambia, “Watumishi wako wamehesabu askari walio chini ya amri yetu na hakuna hata mmoja aliyekosekana.

50 Kwa hiyo tumeleta kama sadaka kwaBwanavyombo vya dhahabu kila mmoja wetu alivyopata, yaani vikuku, bangili, pete za muhuri, vipuli na mikufu, ili kufanya upatanisho kwa ajili yetu mbele zaBwana.”

51 Mose na kuhani Eleazari wakapokea kutoka kwao dhahabu, yaani vyombo vyote vilivyonakishiwa.

52 Dhahabu yote kutoka kwa wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia ambavyo Mose na kuhani Eleazari walimleteaBwanakama zawadi ilikuwa shekeli 16,750.

53 Kila askari alikuwa amejichukulia nyara zake binafsi.

54 Mose na kuhani Eleazari walipokea dhahabu kutoka kwa wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia, wakazileta katika Hema la Kukutania kama ukumbusho kwa Waisraeli mbele zaBwana.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/NUM/31-eadb759677f6f7a0016d2908c1fe3554.mp3?version_id=1627—

Hesabu 32

Makabila Ng’ambo Ya Yordani

1 Kabila la Wareubeni na Wagadi, ambao walikuwa na makundi makubwa ya ng’ombe, kondoo na mbuzi, waliona kuwa nchi ya Yazeri na nchi ya Gileadi ni nzuri kwa mifugo.

2 Hivyo walimjia Mose, na kuhani Eleazari na viongozi wa jumuiya, na kuwaambia,

3 “Atarothi, Diboni, Yazeri, Nimra, Heshboni, Eleale, Sebamu, Nebo na Beoni,

4 nchi ambayoBwanaameishinda mbele ya wana wa Israeli inafaa kwa mifugo, nao watumishi wako wana mifugo.

5 Kama tumepata kibali mbele ya macho yako, nchi hii na ipewe watumishi wako kama miliki yetu. Usitufanye tuvuke Yordani.”

6 Mose akawaambia Wagadi na Wareubeni, “Je, watu wa nchi yenu watakwenda vitani wakati ninyi mmeketi hapa?

7 Kwa nini mmewakatisha Waisraeli tamaa wasivuke katika nchi ambayoBwanaamewapa?

8 Hivi ndivyo baba zenu walivyofanya wakati nilipowatuma kutoka Kadesh-Barnea kuipeleleza nchi.

9 Baada ya kufika kwenye Bonde la Eshkoli na kuitazama nchi, waliwakatisha tamaa Waisraeli wasiingie katika nchi ambayoBwanaalikuwa amewapa.

10 Siku ile hasira yaBwanailiwaka naye akaapa kiapo hiki:

11 ‘Kwa kuwa hawakunifuata kwa moyo wote, hakuna mtu ye yote mwenye miaka ishirini au zaidi ambaye alikuja kutoka Misri atakayeona nchi niliyoahidi kwa kiapo kwa Abrahamu, Isaki na Yakobo;

12 hakuna hata mmoja isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, Mkenizi, na Yoshua mwana wa Nuni, kwa sababu walimfuataBwanakwa moyo wote.’

13 Hasira yaBwanailiwaka dhidi ya Waisraeli na akawafanya watangetange katika jangwa kwa miaka arobaini, mpaka kizazi chote cha wale waliofanya maovu mbele yake kimeangamia.

14 “Nanyi mko hapa, uzao wa wenye dhambi, mkisimamia mahali pa baba zenu na mkimfanyaBwanakuwakasirikia Waisraeli hata zaidi.

15 Kama mkigeuka na mkiacha kumfuata, atawaacha tena watu hawa wote jangwani, na mtakuwa sababu ya maangamizi yao.”

16 Ndipo wakamjia Mose na kumwambia, “Tungalitaka kujenga mazizi hapa kwa ajili ya mifugo yetu na miji kwa ajili ya wanawake wetu na watoto.

17 Lakini sisi tuko tayari kuchukua silaha zetu na kutangulia mbele ya Waisraeli mpaka tutakapowaleta mahali pao. Wakati huo wanawake wetu na watoto wataishi katika miji yenye ngome, kwa ajili ya ulinzi dhidi ya wenyeji wa nchi.

18 Hatutarudi nyumbani mwetu mpaka kila Mwisraeli amepokea urithi wake.

19 Hatutapokea urithi wo wote pamoja nao ng’ambo ya pili ya Yordani, kwa sababu urithi wetu umekuja kwetu upande wa mashariki ya Yordani.”

20 Kisha Mose akawaambia, “Kama mtafanya jambo hili, kama mtajivika silaha mbele zaBwanakwa ajili ya vita,

21 na kama ninyi nyote mtakwenda mmejivika silaha ng’ambo ya Yordani mbele zaBwanampaka awe amewafukuza adui zake mbele zake,

22 hadi wakati nchi itakapokuwa imeshindwa mbele zaBwana, ndipo mtaweza kurudi na kuwa huru kutoka masharti yenu kwaBwanana Israeli. Nayo nchi hii itakuwa milki yenu mbele zaBwana.

23 “Lakini mkishindwa kufanya hili, mtakuwa mnatenda dhambi dhidi yaBwana; nanyi iweni na hakika kuwa dhambi yenu itawapata.

24 Jengeni miji kwa ajili ya wanawake na watoto wenu, na mazizi kwa ajili ya mbuzi na kondoo zenu, lakini fanyeni yale mliyoahidi.”

25 Wagadi na Wareubeni wakamwambia Mose, “Sisi watumishi wako tutafanya kama bwana wetu anavyotuagiza.

26 Watoto na wake zetu, makundi ya mbuzi na kondoo, na makundi ya ng’ombe zetu, watabaki hapa katika miji ya Gileadi.

27 Lakini watumishi wenu, kila mwanaume aliyevaa silaha za vita, watavuka ng’ambo kupigana mbele zaBwana, sawa kama bwana wetu anavyosema.”

28 Kisha Mose akatoa amri kuhusu wao kwa kuhani Eleazari, na Yoshua mwana wa Nuni na viongozi wa jamaa za makabila ya Waisraeli.

29 Mose akawaambia, “Ikiwa Wagadi na Wareubeni, kila mwanaume aliyevaa silaha za vita, atavuka Yordani pamoja nanyi mbele zaBwana, basi wakati mtakapoishinda nchi iliyoko mbele yenu, wapeni nchi ya Gileadi kama milki yao.

30 Lakini kama hawatavuka pamoja nanyi wakiwa wamevaa silaha za vita, lazima wakubali kupokea milki yao pamoja nanyi katika nchi ya Kanaani.”

31 Wagadi na Wareubeni wakajibu, “Watumishi wako watafanya lileBwanaalilosema.

32 Tutavuka mbele zaBwanakuingia Kanaani tukiwa tumevaa silaha za vita, lakini mali tutakayoirithi itakuwa ng’ambo hii ya Yordani.”

33 Kisha Mose akawapa Wagadi, Wareubeni, na nusu ya kabila la Manase mwana wa Yosefu ufalme wa Sihoni mfalme wa Waamori, na ufalme wa Ogu mfalme wa Bashani, nchi yote pamoja na miji yake, na nchi inayowazunguka.

34 Wagadi wakajenga Diboni, Atarothi, Aroeri,

35 Atroth-Shofani, Yazeri, Yogbeha,

36 Beth-Nimra na Beth-Harani kama miji iliyozungushiwa ngome, tena wakajenga mazizi kwa ajili ya makundi yao ya mbuzi na kondoo.

37 Nao Wareubeni wakajenga upya miji ya Heshboni, Eleale na Kiriathaimu,

38 pia Nebo na Baal-Meoni (majina ya hiyo miji yalibadilishwa) na Sibma. Miji waliyoijenga upya waliipa majina.

39 Wazao wa Makiri mwana wa Manase walikwenda Gileadi, wakaiteka nchi na kuwafukuza Waamori ambao walikuwa huko.

40 Kwa hiyo Mose akawapa Wamakiri, wazao wa Manase, nchi ya Gileadi, nao wakakaa huko.

41 Yairi, mzao wa Manase, akateka makao yao, akayaita Hawoth-Yairi.

42 Naye Noba akateka Kenathi na makao yaliyoizunguka, akayaita Noba kwa jina lake.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/NUM/32-b0d63069369cd0d9cd5355dbd4b2c2b8.mp3?version_id=1627—

Hesabu 33

Vituo Katika Safari Ya Waisraeli

1 Hivi ndivyo vituo katika safari ya Waisraeli wakati walipotoka Misri kwa vikosi chini ya uongozi wa Mose na Aroni.

2 Kwa agizo laBwana, Mose aliweka kumbukumbu ya vituo katika safari yao. Hivi ndivyo vituo katika safari yao:

3 Waisraeli walisafiri kutoka Ramesesi katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa kwanza, siku iliyofuata Pasaka. Walitembea kwa ujasiri wazi mbele ya Wamisri wote,

4 ambao walikuwa wakizika wazaliwa wao wa kwanza wote, ambaoBwanaalikuwa amewaua katikati yao, kwa kuwaBwanaalikuwa ameleta hukumu juu ya miungu yao.

5 Waisraeli waliondoka Ramesesi na kupiga kambi huko Sukothi.

6 Wakaondoka Sukothi na kupiga kambi huko Ethamu, pembeni mwa jangwa.

7 Wakaondoka Ethamu, wakageuka wakarudi Pi-Hahirothi, hadi mashariki ya Baal-Sefoni, wakapiga kambi yao karibu na Migdoli.

8 Wakaondoka Pi-Hahirothi wakapita katikati ya bahari mpaka jangwani, na baada ya kusafiri kwa siku tatu katika Jangwa la Ethamu, walipiga kambi huko Mara.

9 Wakaondoka Mara wakaenda Elimu, mahali ambapo palikuwa na chemchemi kumi na mbili na mitende sabini, huko wakapiga kambi.

10 Wakaondoka Elimu na kupiga kambi kando ya Bahari ya Shamu.

11 Wakaondoka kando ya Bahari ya Shamu na kupiga kambi katika Jangwa la Sini.

12 Wakaondoka katika Jangwa la Sini, wakapiga kambi huko Dofka.

13 Wakaondoka Dofka, wakapiga kambi huko Alushi.

14 Wakaondoka Alushi, wakapiga kambi Refidimu, mahali ambapo hapakuwa na maji kwa ajili ya watu kunywa.

15 Wakaondoka Refidimu na kupiga kambi katika Jangwa la Sinai.

16 Wakaondoka katika Jangwa la Sinai na kupiga kambi huko Kibroth-Hataava.

17 Wakaondoka Kibroth-Hataava na kupiga kambi huko Haserothi.

18 Wakaondoka Haserothi na kupiga kambi huko Rithma.

19 Wakaondoka Rithma na kupiga kambi huko Rimon-Peresi.

20 Wakaondoka Rimon-Peresi na kupiga kambi huko Libna.

21 Wakaondoka Libna na kupiga kambi huko Risa.

22 Wakaondoka Risa na kupiga kambi huko Kehelatha.

23 Wakaondoka Kehelatha na kupiga kambi kwenye mlima Sheferi.

24 Wakaondoka kwenye mlima Sheferi na kupiga kambi huko Harada.

25 Wakaondoka Harada na kupiga kambi huko Makelothi.

26 Wakaondoka Makelothi na kupiga kambi huko Tahathi.

27 Wakaondoka Tahathi na kupiga kambi huko Tera.

28 Wakaondoka Tera na kupiga kambi huko Mithka.

29 Wakaondoka Mithka na kupiga kambi huko Hashmona.

30 Wakaondoka Hashmona na kupiga kambi Moserothi.

31 Wakaondoka Moserothi na kupiga kambi huko Bene-Yakani.

32 Wakaondoka Bene-Yakani na kupiga kambi huko Hor-Hagidgadi.

33 Wakaondoka Hor-Hagidgadi na kupiga kambi huko Yotbatha.

34 Wakaondoka Yotbatha na kupiga kambi uko Abrona.

35 Wakaondoka Abrona na kupiga kambi huko Esion-Geberi.

36 Wakaondoka Esion-Geberi na kupiga kambi huko Kadeshi katika Jangwa la Sini.

37 Wakaondoka Kadeshi na kupiga kambi kwenye Mlima Hori, mpakani mwa Edomu.

38 Kwa amri yaBwana, kuhani Aroni alipanda Mlima Hori, mahali alipofia katika siku ya kwanza ya mwezi wa tano, mwaka wa arobaini baada ya Waisraeli kutoka Misri.

39 Aroni alikufa juu ya Mlima Hori akiwa na umri wa miaka 123.

40 Mfalme Mkanaani wa Aradi, ambaye aliishi huko Negebu ya Kanaani, akasikia kwamba Waisraeli wanakuja.

41 Wakaondoka kwenye mlima Hori na kupiga kambi huko Salmona.

42 Wakaondoka Salmona, wakapiga kambi huko Punoni.

43 Wakaondoka Punoni, wakapiga kambi huko Obothi.

44 Wakaondoka Obothi, wakapiga kambi huko Iye-Abarimu, mipakani mwa Moabu.

45 Wakaondoka Iye-Abarimu, wakapiga kambi huko Diboni-Gadi.

46 Wakaondoka Diboni-Gadi na kupiga kambi huko Almon-Diblathaimu.

47 Wakaondoka Almon-Diblathaimu na kupiga kambi katika milima ya Abarimu, karibu na Nebo.

48 Wakaondoka kwenye milima ya Abarimu na kupiga kambi kwenye tambarare ya Moabu, kando ya Yordani ng’ambo ya Yeriko.

49 Huko kwenye tambarare za Moabu walipiga kambi kandokando ya Mto Yordani, kuanzia Beth-Yeshimothi mpaka Abel-Shitimu.

50 Katika tambarare za Moabu kando ya Yordani kuvukia Yeriko,Bwanaakamwambia Mose,

51 “Sema na Waisraeli uwaambie: ‘Mtakapovuka Mto Yordani kuingia Kanaani,

52 wafukuzeni wakazi wote wa nchi iliyo mbele yenu. Haribuni sanamu zao zote za kuchongwa, na sanamu zilizotengenezwa kwa kuyeyusha chuma, na kupabomoa mahali pao pa ibada.

53 Mtaimiliki nchi hiyo na kukaa huko, kwa kuwa nimewapeni ninyi kuimiliki.

54 Mtaigawanya nchi hiyo kwa kupiga kura, kufuatana na koo zenu. Kwa kundi kubwa zaidi toa urithi mkubwa zaidi, na kwa kundi dogo zaidi urithi mdogo zaidi. Cho chote kinachowaangukia kwa kura kitakuwa chao. Mtaigawanya nchi kufuatana na makabila ya babu zenu.

55 “ ‘Lakini kama hamkuwafukuza wenyeji wakaao katika nchi hiyo, wale mtakaowaruhusu wabaki watakuwa kama miiba kwenye macho yenu na miiba kwenu kila upande. Watawasumbua katika nchi mtakayoishi.

56 Kisha nitawatenda ninyi kile ambacho nimepanga kuwatenda wao.’ ”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/NUM/33-dbbc214f858652d3e7b638193b45b9ad.mp3?version_id=1627—

Hesabu 34

Mipaka Ya Kanaani

1 Bwanaakamwambia Mose,

2 “Waamuru Waisraeli na uwaambie: ‘Mtakapoingia nchi ya Kanaani, nchi ambayo itagawanywa kwenu kama urithi itakuwa na mipaka ifuatayo:

3 “ ‘Upande wenu wa kusini utajumuisha sehemu ya Jangwa la Sini kufuata mpaka wa Edomu. Upande wa mashariki mpaka wenu wa kusini utaanzia mwisho wa Bahari ya Chumvi,

4 katiza kusini mwa Pito la Akrabimu, endelea mpaka Sini na kwenda kusini ya Kadesh-Barnea. Kisha mpaka huo utaenda hadi Hasar-Adari hadi Azmoni,

5 mahali ambapo utapinda, na kuunganika na mpaka wa Misri na kumalizikia kwenye Bahari ya Kati.

6 “ ‘Mpaka wenu wa magharibi utakuwa Bahari ya Kati. Huu utakuwa mpaka wenu upande wa magharibi.

7 “ ‘Kwa mpaka wenu wa kaskazini, wekeni alama kuanzia Bahari ya Kati hadi mlima Hori,

8 na kutoka mlima Hori hadi Pito la Hamathi. Kisha mpaka utaenda hadi Sedadi,

9 kuendelea hadi Zifroni, na kuishia Hazar-Enani. Huu utakuwa mpaka wenu upande wa kaskazini.

10 “ ‘Kwa mpaka wenu wa mashariki, wekeni alama kuanzia Hazar-Enani hadi Shefamu.

11 Mpaka utaelekea kusini kuanzia Shefamu hadi Ribla upande wa mashariki wa Aini, na kuendelea kwenye mitelemko mashariki mwa Bahari ya Kinerethi.

12 Kisha mpaka utashuka kuelekea Mto Yordani na kuishia katika Bahari ya Chumvi.

“ ‘Hii itakuwa nchi yenu, ikiwa na mipaka yake kila upande.’ ”

13 Mose akawaamuru Waisraeli: “Gawanyeni nchi hii kwa kura kama urithi.Bwanaameagiza kwamba itolewe kwa yale makabila tisa na nusu,

14 kwa sababu jamaa ya kabila la Reubeni, kabila la Gadi, na nusu ya kabila la Manase wamekwishapokea urithi wao.

15 Haya makabila mawili na nusu wamekwishapokea urithi wao upande wa mashariki wa Yordani ng’ambo ya Yeriko, kuelekea maawio ya jua.”

16 Bwanaakamwambia Mose,

17 “Haya ndiyo majina ya watu ambao watakusaidia kugawanya nchi kama urithi: Eleazari kuhani na Yoshua mwana wa Nuni.

18 Tena uteue kiongozi mmoja kutoka kila kabila kusaidia kuigawanya nchi.

19 Haya ndiyo majina yao:

“Kalebu mwana wa Yefune,

kutoka kabila la Yuda;

20 Shemueli mwana wa Amihudi,

kutoka kabila la Simeoni;

21 Elidadi mwana wa Kisloni,

kutoka kabila la Benyamini;

22 Buki mwana wa Yogli,

kiongozi kutoka kabila la Dani;

23 Hanieli mwana wa Efodi,

kiongozi kutoka kabila la Manase mwana wa Yosefu;

24 Kemueli mwana wa Shiftani,

kiongozi kutoka kabila la Efraimu mwana wa Yosefu;

25 Elisafani mwana wa Parnaki,

kiongozi kutoka kabila la Zabuloni;

26 Patieli mwana wa Azani,

kiongozi kutoka kabila la Isakari;

27 Ahihudi mwana wa Shelomi,

kiongozi kutoka kabila la Asheri;

28 Pedaheli mwana wa Amihudi,

kiongozi kutoka kabila la Naftali.”

29 Hawa ndio watu ambaoBwanaaliamuru kuwa wagawanye urithi kwa Waisraeli katika nchi ya Kanaani.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/NUM/34-7acd76436f7b19c89a484215882d0836.mp3?version_id=1627—