Hesabu 35

Miji Kwa Ajili Ya Walawi

1 Bwanaakamwambia Mose katika nchi tambarare ya Moabu, kando ya Mto Yordani kuvukia Yeriko,

2 “Waagize Waisraeli kuwapa Walawi miji ya kuishi kutoka urithi ambao Waisraeli wataumiliki. Wape maeneo ya malisho kuzunguka hiyo miji.

3 Kisha watakuwa na miji ya kuishi na maeneo ya malisho kwa ajili ya ng’ombe zao, mbuzi, kondoo na mifugo yao mingine yote.

4 “Maeneo ya malisho kuzunguka miji hiyo ambayo mtawapa Walawi yataenea mita 450 kutoka kwenye ukuta wa miji.

5 Nje ya mji, pima mita 900 upande wa mashariki, upande wa kusini mita 900, upande wa magharibi mita 900, na upande wa kaskazini mita 900, na mji utakuwa katikati. Eneo hili litakuwa lao kwa ajili ya malisho.

Miji Ya Makimbilio

6 “Miji sita mtakayowapa Walawi itakuwa ya makimbilio, ambayo mtu anayemwua mwenzake aweza kukimbilia humo. Nyongeza ya hiyo, wapeni miji mingine arobaini na miwili.

7 Kwa jumla inawapasa kuwapa Walawi miji arobaini na minane, pamoja na maeneo ya malisho yao.

8 Miji ambayo mtawapa Walawi kutoka nchi ambayo Waisraeli wanamiliki itatolewa kwa uwiano wa urithi wa kila kabila. Chukua miji mingi kutoka lile kabila lenye miji mingi, lakini uchukue miji michache kutoka kwa kabila lile lenye miji michache.”

9 KishaBwanaakamwambia Mose:

10 “Sema na Waisraeli, uwaambie: ‘Wakati mtakapovuka Yordani kuingia Kanaani,

11 chagueni baadhi ya miji iwe miji yenu ya makimbilio, ambayo mtu ambaye amemua mwenzake bila kukusudia aweza kukimbilia humo.

12 Itakuwa mahali pa kukimbilia kutoka mlipiza kisasi, ili kwamba mtu aliyeshitakiwa kwa mauaji asife kabla ya kujitetea mbele ya mkutano.

13 Miji hii sita mtakayoitoa itakuwa miji yenu ya makimbilio.

14 Mtatoa miji mitatu ng’ambo hii ya Yordani na miji mingine mitatu upande wa Kanaani kama miji ya makimbilio.

15 Miji hii sita itakuwa mahali pa makimbilio kwa ajili ya Waisraeli, wageni na watu wengine wo wote wanaoishi katikati yenu, ili kwamba mtu ye yote ambaye ameua mtu mwingine pasipo kukusudia aweze kukimbilia humo.

16 “ ‘Kama mtu akimpiga mwenzake kwa chuma naye mtu huyo akafa, mtu huyo ni mwuaji; mwuaji sharti atauawa.

17 Au kama mtu analo jiwe mkononi mwake ambalo laweza kuua, naye akampiga mwenzake akafa, yeye ni mwuaji; mwuaji huyo sharti atauawa.

18 Au kama mtu ana chombo cha mti mkononi mwake ambacho chaweza kuua, naye akampiga mwenzake akafa, yeye ni mwuaji; mwuaji huyo sharti atauawa.

19 Mlipiza kisasi cha damu atamwua mwuaji; wakati akikutana naye, atamwua.

20 Ikiwa mtu ana chuki ya siku nyingi na mwenzake akamsukuma au akamtupia kitu kwa kukusudia naye akafa,

21 au ikiwa katika uadui akampiga ngumi naye akafa, mtu yule sharti atauawa; yeye ni mwuaji. Mlipiza kisasi cha damu atamwua mwuaji atakapokutana naye.

22 “ ‘Lakini kama mtu akimsukuma mwenziwe ghafula pasipo chuki, au kumtupia kitu pasipo kukusudia,

23 au, pasipo kumwona, akimwangushia jiwe ambalo laweza kumwua naye akafa, basi kwa kuwa hakuwa adui yake naye hakukusudia kumumiza,

24 kusanyiko lazima liamue kati yake na mlipiza kisasi wa damu kufuatana na sheria hizi.

25 Kusanyiko ni lazima limlinde yule anayeshtakiwa kuua kutoka kwa mlipiza kisasi wa damu, na kumrudisha katika mji wa makimbilio alikokuwa amekimbilia. Lazima akae humo mpaka atakapokufa Kuhani Mkuu ambaye alikuwa amepakwa mafuta matakatifu.

26 “ ‘Lakini kama mshtakiwa atatoka nje ya mipaka ya mji wa makimbilio ambao amekimbilia,

27 na mlipiza kisasi wa damu akamkuta nje ya mji, mlipiza kisasi wa damu anaweza kumwua mshtakiwa huyo bila kuwa na hatia ya kuua.

28 Mshtakiwa lazima akae katika mji wake wa makimbilio mpaka atakapokufa Kuhani Mkuu; atarudi tu kwenye mali yake baada ya kifo cha Kuhani Mkuu.

29 “ ‘Hizi ndizo kanuni za sheria zitakazohitajiwa kwenu na katika vizazi vyenu vijavyo, po pote mtakapoishi.

30 “ ‘Ye yote anayeua mtu atauawa kama mwuaji ikiwa tu kuna ushuhuda wa mashahidi. Lakini hakuna mtu atakayeuawa kwa ushuhuda wa shahidi mmoja tu.

31 “ ‘Usikubali fidia yo yote ya kuokoa uhai wa mwuaji ambaye anastahili kufa. Mtu huyo hakika lazima auawe.

32 “ ‘Usikubali fidia ya mtu ye yote ambaye amekimbilia katika mji wa makimbilio na kumruhusu kurudi kuishi katika nchi yake kabla ya kifo cha Kuhani Mkuu.

33 “ ‘Msiinajisi nchi mnayoishi. Umwagaji damu hunajisi nchi, na upatanisho hauwezekani kufanyika katika nchi ambayo damu imemwagwa, isipokuwa tu kwa damu ya yule aliyeimwaga damu.

34 Msiinajisi nchi mnayoishi, ambayo nami ninakaa, kwa kuwa Mimi,Bwana, ninakaa katikati ya Waisraeli.’ ”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/NUM/35-6325f346d85f830fac09ac893a1b97e7.mp3?version_id=1627—

Hesabu 36

Urithi Wa Binti Za Selofehadi

1 Viongozi wa jamaa ya ukoo wa Gileadi mwana wa Makiri, mwana wa Manase, ambao walikuwa wametoka katika koo za wazao wa Yosefu, walikuja na kuzungumza mbele ya Mose na viongozi, wakuu wa jamaa ya Waisraeli.

2 Wakasema, “WakatiBwanaalipomwamuru bwana wangu kuwapa Waisraeli nchi kama urithi kwa kura, alikuamuru kutoa urithi wa ndugu yetu Selofehadi kwa binti zake.

3 Sasa ikiwa wataolewa na watu wa makabila mengine ya Kiisraeli, itakuwa kwamba urithi wao utaondolewa kutoka urithi wa mababu zetu na kuongezwa katika urithi wa kabila ambalo dada hao wameolewa. Kwa hiyo sehemu ya urithi tuliyogawiwa itachukuliwa kutoka kwetu.

4 Wakati mwaka wa Yubile kwa Waisraeli utakapofika, urithi wao utaongezwa kwa lile kabila ambalo wameolewa, na mali yao itaondolewa kutoka urithi wa kabila la mababu zetu.”

5 Ndipo kwa agizo laBwanaMose akatoa amri ifuatayo kwa Waisraeli: “Kile wazao wa kabila la Yosefu wanachosema ni kweli.

6 Hivi ndivyoBwanaanavyoamuru kwa binti za Selofehadi: Wanaweza kuolewa na mtu ye yote wampendaye, mradi tu waolewe miongoni mwa koo za kabila za baba yao.

7 Hakuna urithi katika Israeli utakaohamishwa kutoka kabila moja kwenda kabila jingine, kwa kuwa kila Mwisraeli atatunza ardhi ya kabila lake aliyoirithi kutoka kwa baba zake.

8 Kila binti atakayerithi ardhi katika kabila lo lote la Israeli ni lazima aolewe na mtu kutoka kabila na ukoo wa baba yake, ili kila Mwisraeli amiliki urithi wa baba zake.

9 Hakuna urithi uwezao kuhamishwa kutoka kabila moja kwenda kabila jingine, kwa kuwa kila kabila la Israeli litatunza nchi linayorithi.”

10 Kwa hiyo binti za Selofehadi wakafanya kamaBwanaalivyomwamuru Mose.

11 Binti za Selofehadi, ambao ni Mala, Tirsa, Hogla, Milka na Noa, wakaolewa na waume, wana wa ndugu za baba yao.

12 Waliolewa ndani ya koo za wazao wa Manase mwana wa Yosefu, na urithi wao ukabaki katika ukoo na kabila la baba yao.

13 Haya ndiyo maagizo na masharti ambayoBwanaaliwapa Waisraeli kupitia Mose katika tambarare za Moabu, karibu na Yordani ng’ambo ya Yeriko.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/NUM/36-97526d7e64ebf4cf2fca720d17228cb7.mp3?version_id=1627—

Mambo ya Walawi 1

Sadaka Ya Kuteketezwa

1 Bwanaakamwita Mose na kusema naye kutoka kwenye Hema la Kukutania, akamwambia,

2 “Sema na Waisraeli na uwaambie, ‘Ye yote miongoni mwenu aletapo sadaka ya mnyama kwaBwana, alete mnyama kama sadaka yake kutoka kundi lake la ng’ombe au la kondoo na mbuzi.

3 “ ‘Kama sadaka hiyo ni ya kuteketezwa kutoka kwenye kundi la ng’ombe, atamtoa ng’ombe dume asiye na dosari. Ni lazima amlete kwenye ingilio la Hema la Kukutania ili aweze kukubalika kwaBwana.

4 Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha sadaka ya kuteketezwa, nayo itakubaliwa kwa niaba yake ili kufanya upatanisho kwa ajili yake.

5 Atamchinja yule fahali mchanga mbele zaBwana, kisha wana wa Aroni kuhani wataleta damu na kuinyunyiza pande zote za madhabahu iliyoko penye ingilio la Hema la Kukutania.

6 Ataichuna hiyo sadaka ya kuteketezwa na kuikata vipande vipande.

7 Wana wa Aroni kuhani wataweka moto juu ya madhabahu na kupanga kuni juu ya huo moto.

8 Kisha wana wa Aroni kuhani watapanga vile vipande vya nyama, pamoja na kichwa na mafuta ya huyo mnyama juu ya zile kuni zinazowaka juu ya madhabahu.

9 Ataziosha sehemu za ndani na miguu yake kwa maji, naye kuhani atavichoma vyote juu ya madhabahu. Hii ni sadaka ya kuteketezwa, sadaka iliyotolewa kwa moto, yenye harufu nzuri ya kumpendezaBwana.

10 “ ‘Kama sadaka ni ya kuteketezwa kutoka kwenye kundi la kondoo au mbuzi, atamtoa mnyama dume asiye na dosari.

11 Atamchinja upande wa kaskazini wa madhabahu mbele zaBwana, nao wana wa Aroni kuhani watanyunyizia damu yake pande zote za madhabahu.

12 Atamkata vipande vipande, naye kuhani atavipanga, pamoja na kichwa na mafuta ya mnyama juu ya zile kuni zinazowaka juu ya madhabahu.

13 Ataosha sehemu za ndani na miguu kwa maji, naye kuhani atavileta vyote na kuvichoma juu ya madhabahu. Hii ni sadaka ya kuteketezwa, sadaka iliyotolewa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendezaBwana.

14 “ ‘Kama sadaka ya kuteketezwa inayotolewa kwaBwanani ndege, atamtoa hua au kinda la njiwa.

15 Kuhani atamleta kwenye madhabahu, naye atamvunja shingo na kumnyofoa kichwa na kumchoma juu ya madhabahu, damu yake itachuruzishwa ubavuni mwa madhabahu.

16 Ataondoa kifuko cha chakula pamoja na uchafu wake na kuvitupa upande wa mashariki wa madhabahu, mahali pale penye majivu.

17 Atampasua na kumweka wazi katika mabawa yake lakini asimwachanishe kabisa, kisha kuhani ataichoma juu ya zile kuni zinazowaka juu ya madhabahu. Hii ni sadaka ya kuteketezwa, sadaka iliyotolewa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendezaBwana.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/LEV/1-deabb07d229dcc822e31e854512bd8bc.mp3?version_id=1627—

Mambo ya Walawi 2

Sadaka Ya Nafaka

1 “ ‘Mtu ye yote aletapo sadaka ya nafaka kwaBwana, sadaka yake itakuwa ya unga laini. Atamimina mafuta juu yake, aweke uvumba juu yake

2 naye atapeleka kwa makuhani wana wa Aroni. Kuhani atachukua konzi moja iliyojaa unga laini na mafuta, pamoja na uvumba wote na kuuteketeza kama sehemu ya kumbukumbu juu ya madhabahu, sadaka iliyotolewa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendezaBwana.

3 Sadaka ya nafaka iliyobaki ni ya Aroni na wanawe, ni sehemu ya sadaka iliyo takatifu sana iliyotolewa kwaBwanakwa moto.

4 “ ‘Kama utaleta sadaka ya nafaka iliyookwa jikoni, itakuwa ya unga laini: maandazi yaliyotengenezwa bila kutiwa chachu, yaliyochanganywa na mafuta, au mikate myembamba iliyotengenezwa bila kutiwa chachu na iliyopakwa mafuta.

5 Iwapo sadaka yako ya nafaka imeandaliwa kwenye kikaango, itakuwa ni ya unga laini uliochanganywa na mafuta na bila chachu.

6 Ukande na kumimina mafuta juu yake; hii ni sadaka ya nafaka.

7 Kama sadaka yako ya nafaka imepikwa kwenye sufuria, itatengenezwa kwa unga laini na mafuta.

8 Ilete hiyo sadaka ya nafaka iliyotengenezwa kwa vitu hivi kwaBwana; mkabidhi kuhani ambaye ataipeleka madhabahuni.

9 Naye atatoa ile sehemu ya kumbukumbu kutoka kwenye hiyo sadaka ya nafaka na kuiteketeza juu ya madhabahu kuwa sadaka iliyotolewa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendezaBwana.

10 Sadaka ya nafaka iliyobaki ni ya Aroni na wanawe; ni sehemu ya sadaka iliyo takatifu sana ya sadaka iliyotolewa kwaBwanakwa moto.

11 “ ‘Kila sadaka ya nafaka unayoleta kwaBwanani lazima ifanywe bila kutiwa chachu, kwa kuwa huna ruhusa kuchoma chachu yo yote au asali katika sadaka itolewayo kwaBwanakwa moto.

12 Unaweza kuzileta kwaBwanakama sadaka ya malimbuko, lakini haziwezi kutolewa juu ya madhabahu kama harufu nzuri ya kupendeza.

13 Koleza sadaka zako zote za nafaka kwa chumvi. Usiache kuweka chumvi ya Agano la Mungu wako katika sadaka zako za nafaka; weka chumvi kwenye sadaka zako zote.

14 “ ‘Kama ukileta malimbuko ya sadaka ya nafaka kwaBwana, utatoa masuke yaliyopondwa ya nafaka mpya iliyookwa kwa moto.

15 Weka mafuta na uvumba juu yake; ni sadaka ya nafaka.

16 Kuhani atateketeza ile sehemu ya kumbukumbu kutoka kwenye hiyo sadaka ya nafaka iliyopondwa kwa mafuta, pamoja na uvumba wote, kama sadaka iliyotolewa kwaBwanakwa moto.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/LEV/2-24e32029302d8f3709ba31dc1ce6c159.mp3?version_id=1627—

Mambo ya Walawi 3

Sadaka Ya Amani

1 “ ‘Kama sadaka ya mtu ni sadaka ya amani, naye akatoa ng’ombe kutoka katika kundi, akiwa dume au jike, atamleta huyo mbele zaBwanamnyama asiye na dosari.

2 Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha hiyo sadaka yake na kumchinja penye ingilio la Hema la Kukutania. Ndipo makuhani wana wa Aroni watanyunyiza damu yake pande zote za madhabahu.

3 Kutoka kwenye hiyo sadaka ya amani ataleta sadaka iliyotolewa kwaBwanakwa moto: mafuta yote ya mnyama yafunikayo sehemu za ndani, ama yanayoungana na hizo sehemu za ndani,

4 figo zote pamoja na mafuta yote yanayozizunguka karibu na kiuno na yale yanayofunika ini, ambayo atayaondoa pamoja na figo.

5 Kisha wana wa Aroni wataiteketeza juu ya madhabahu, juu ya ile sadaka ya kuteketezwa iliyoko juu ya kuni zinazowaka, kama sadaka ya kuteketezwa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendezaBwana.

6 “ ‘Kama akitoa kondoo au mbuzi kutoka katika kundi kama sadaka ya amani kwaBwana, atamtoa dume au jike asiye na dosari.

7 Kama akimtoa mwana-kondoo, atamleta mbele zaBwana.

8 Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha sadaka yake naye atamchinja mbele ya Hema la Kukutania. Kisha wana wa Aroni watanyunyiza damu yake kwenye madhabahu pande zote.

9 Kutoka kwenye hiyo sadaka ya amani ataleta dhabihu iliyotolewa kwaBwanakwa moto: mafuta yake, mafuta yote ya mkia uliokatwa karibu na uti wa mgongo, mafuta yote yanayofunika sehemu za ndani au yale yanayounganika nazo,

10 figo mbili pamoja na mafuta yanayozizunguka yaliyo karibu na kiuno na yale yanayofunika ini, ambayo atayatoa pamoja na figo.

11 Kuhani ataviteketeza juu ya madhabahu kama chakula, sadaka iliyotolewa kwaBwanakwa moto.

12 “ ‘Kama sadaka yake ni mbuzi, ataileta mbele zaBwana.

13 Ataweka mkono wake juu ya kichwa chake na kumchinja mbele ya Hema la Kukutania. Kisha wana wa Aroni watanyunyiza damu yake kwenye madhabahu pande zote.

14 Kutokana na ile sadaka anayotoa, atatoa sadaka hii kwaBwanakwa moto: mafuta yote yanayofunika sehemu za ndani na yale yanayoungana nazo,

15 figo zote mbili pamoja na mafuta yaliyo juu yake karibu na kiuno na yanayofunika ini, ambayo atayaondoa pamoja na figo.

16 Kuhani ataviteketeza juu ya madhabahu kama chakula, sadaka iliyotolewa kwa moto, harufu nzuri. Mafuta yote ya mnyama ni yaBwana.

17 “ ‘Hii ni kanuni ya kudumu kwa vizazi vijavyo, po pote muishipo: Msile mafuta yo yote ya mnyama wala damu.’ ”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/LEV/3-30e0dd081a734a80fdd3be46a67ad9f9.mp3?version_id=1627—

Mambo ya Walawi 4

Sadaka Ya Dhambi

1 Bwanaakamwambia Mose,

2 “Waambie Waisraeli: ‘Mtu ye yote afanyapo dhambi bila kukusudia na akatenda lile lililokatazwa katika amri yo yote yaBwana:

3 “ ‘Ikiwa kuhani aliyetiwa mafuta amefanya dhambi na kuwaletea watu hatia, lazima alete kwaBwanafahali mchanga asiye na dosari, kuwa sadaka ya dhambi kwa ajili ya dhambi aliyotenda.

4 Atamkabidhi huyo fahali kwenye ingilio la Hema la Kukutania mbele zaBwana. Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha huyo fahali na kumchinja mbele zaBwana.

5 Kisha kuhani huyo aliyetiwa mafuta atachukua sehemu ya damu ya huyo fahali na kuileta katika Hema la Kukutania.

6 Atachovya kidole chake katika hiyo damu na kuinyunyiza sehemu yake mara saba mbele zaBwanambele ya pazia la mahali patakatifu.

7 Kisha kuhani atatia sehemu ya hiyo damu juu ya pembe za madhabahu ya kufukizia uvumba wenye harufu nzuri iliyoko mbele zaBwanakatika Hema la Kukutania. Damu iliyobaki ya huyo fahali ataimwaga chini ya hiyo madhabahu ya kuteketezea sadaka kwenye ingilio la Hema la Kukutania.

8 Atayaondoa mafuta yote ya fahali huyo wa sadaka ya dhambi, mafuta yale yanayofunika sehemu za ndani au zile zinazounganika nazo,

9 figo zote mbili na mafuta yaliyo juu yake karibu na kiuno na yale yanayofunika ini ambayo atayaondoa pamoja na figo zote,

10 kama vile mafuta yanayoondolewa kutoka kwenye maksai aliyetolewa sadaka ya amani. Kisha kuhani ataviteketeza juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa.

11 Lakini ngozi ya huyo fahali na nyama zake zote, pamoja na kichwa na miguu yake, sehemu za ndani na matumbo,

12 yaani sehemu nyingine zote zilizobaki za huyo fahali, lazima azitoe nje ya kambi mpaka mahali palipo safi kiibada, ambapo majivu hutupwa, naye atamchoma kwa moto juu ya kuni zilizoko juu ya lundo la majivu.

13 “ ‘Ikiwa jumuiya yote ya Israeli watatenda dhambi pasipo kukusudia na kufanya lile lililokatazwa katika amri yo yote yaBwana, hata kama jumuiya haifahamu juu ya jambo hilo, wana hatia.

14 Wanapotambua juu ya dhambi waliyoitenda, lazima kusanyiko lilete fahali mchanga kuwa sadaka ya dhambi na kuikabidhi mbele ya Hema la Kukutania.

15 Wazee wa jumuiya wataweka mikono yao juu ya kichwa cha huyo fahali aliye mbele zaBwana, naye fahali atachinjwa mbele zaBwana.

16 Kisha kuhani aliyetiwa mafuta ataiingiza sehemu ya damu ya huyo fahali ndani ya Hema la Kukutania.

17 Atachovya kidole chake kwenye damu na kuinyunyiza mara saba mbele zaBwanambele ya hilo pazia.

18 Atatia sehemu ya hiyo damu juu ya pembe za ile madhabahu iliyo mbele zaBwanakatika Hema la Kukutania. Damu iliyobaki ataimwaga chini ya madhabahu ya kuteketezea sadaka, penye ingilio la Hema la Kukutania.

19 Atayaondoa mafuta yote ya yule fahali na kuyateketeza juu ya madhabahu,

20 naye atamfanyia fahali huyu kama alivyomfanyia yule fahali mwingine wa sadaka ya dhambi. Kwa njia hii kuhani atawafanyia watu upatanisho, nao watasamehewa.

21 Kisha atamchukua yule fahali nje ya kambi na kumteketeza kama alivyomteketeza yule wa kwanza. Hii ni sadaka ya dhambi kwa ajili ya jumuiya.

22 “ ‘Wakati kiongozi ametenda dhambi bila kukusudia na kufanya yaliyokataliwa katika amri yo yote yaBwanaMungu wake, ana hatia.

23 Atakapofahamishwa dhambi aliyotenda, ni lazima alete mbuzi dume asiye na dosari kama sadaka yake.

24 Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha yule mbuzi na kumchinja mahali pale ambapo sadaka za kuteketezwa huchinjwa mbele zaBwana. Hii ni sadaka ya dhambi.

25 Kisha kuhani atachukua sehemu ya damu ya sadaka ya dhambi kwa kidole chake na kuitia kwenye pembe za madhabahu ya sadaka ya kuteketeza na kuimwaga damu iliyobaki chini ya madhabahu.

26 Atayateketeza mafuta yote juu ya madhabahu kama alivyoteketeza mafuta ya sadaka ya amani. Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho wa dhambi kwa ajili ya yule mtu, naye atasamehewa.

27 “ ‘Kama mtu katika jumuiya ametenda dhambi pasipo kukusudia na kufanya lile lililokatazwa katika amri yo yote yaBwana, yeye ana hatia.

28 Atakapofahamishwa dhambi yake aliyoitenda, ni lazima alete mbuzi jike asiye na dosari kama sadaka yake kwa ajili ya dhambi aliyotenda.

29 Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha sadaka ya dhambi na kumchinjia mahali pa kuteketezea sadaka.

30 Kisha kuhani atachukua sehemu ya ile damu kwa kidole chake na kuitia kwenye pembe za madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na kuimwaga damu iliyobaki chini ya madhabahu.

31 Atayaondoa mafuta yote, kama vile mafuta yaondolewavyo kwenye sadaka ya amani, naye kuhani atayateketeza juu ya madhabahu kama harufu nzuri ya kumpendezaBwana. Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake, naye atasamehewa.

32 “ ‘Ikiwa ataleta mwana-kondoo kama sadaka yake ya dhambi, atamleta jike asiye na dosari.

33 Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha huyo mwana-kondoo na kumchinja kwa ajili ya sadaka ya dhambi mahali sadaka ya kuteketezwa ichinjiwapo.

34 Kisha kuhani atachukua sehemu ya damu ya sadaka ya dhambi kwa kidole chake na kuitia juu ya pembe za madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na ile damu iliyobaki ataimwaga chini ya madhabahu.

35 Ataondoa mafuta yote, kama vile mafuta yaondolewavyo kutoka kwenye mwana-kondoo wa sadaka ya amani, naye kuhani atayateketeza juu ya madhabahu juu ya zile sadaka zilizotolewa kwaBwanakwa moto. Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake kwa dhambi aliyoitenda, naye atasamehewa.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/LEV/4-027b8315a75173eaadcd1d4ab22d837f.mp3?version_id=1627—

Mambo ya Walawi 5

Sadaka Nyingine Za Kuondoa Dhambi

1 “ ‘Ikiwa mtu atakuwa ametenda dhambi kwa sababu hakusema alipotakiwa kutoa ushahidi hadharani kuhusu jambo aliloona au kujua habari zake, yeye anastahili adhabu.

2 “ ‘Au kama mtu akigusa kitu cho chote ambacho si safi kwa kawaida ya ibada, kama ni mizoga ya wanyama pori walio najisi, au ya wanyama wafugwao walio najisi, au ya viumbe vitambaavyo ardhini, hata kama hana habari, amekuwa najisi na mwenye hatia.

3 “ ‘Au kama akigusa kitu kilicho kichafu kinachotokana na binadamu, kitu cho chote kile kinachoweza kumfanya awe najisi, hata ikiwa hana habari juu yake, atakapojua atakuwa ana hatia.

4 “ ‘Au kama mtu ameapa kufanya kitu cho chote bila kufikiri kikiwa chema au kibaya, kwa vyo vyote mtu aweza kuapa kwa uzembe akiwa hana habari juu yake, hata kama hatambui juu yake kwa vyo vyote, atakapofahamu atakuwa na hatia.

5 “ ‘Wakati mtu ye yote atakapokuwa na hatia katika mojawapo ya haya, lazima akiri kuwa ni kwa njia gani ametenda dhambi,

6 na kwa ajili ya adhabu ya dhambi aliyoitenda lazima alete kwaBwanakondoo jike au mbuzi kutoka kwenye kundi lake kama sadaka ya dhambi; naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake kwa dhambi yake.

7 “ ‘Lakini huyo mtu kama hataweza kumtoa mwana-kondoo, ataleta hua wawili au makinda mawili ya njiwa kwaBwanakuwa adhabu kwa ajili ya dhambi yake, mmoja wa hao ndege kwa ajili ya sadaka ya dhambi na wa pili kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa.

8 Atawaleta kwa kuhani, ambaye atamtoa kwanza huyo mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi. Atamvunja shingo yake na kuacha kichwa chake kikining’inia,

9 naye atanyunyiza sehemu ya hiyo damu ya sadaka ya dhambi kwenye pembe za madhabahu, damu iliyobaki lazima ichuruzwe chini ya madhabahu. Hii ni sadaka ya dhambi.

10 Kisha kuhani atamtoa yule wa pili kama sadaka ya kuteketezwa kwa kufuata utaratibu uliowekwa na kufanya upatanisho kwa ajili yake kwa dhambi aliyoitenda, naye atasamehewa.

11 “ ‘Ikiwa basi, hawezi kupata hua wawili au makinda mawili ya njiwa, ataleta sehemu ya kumi ya efaya unga laini kwa ajili ya sadaka ya dhambi. Kamwe asiweke mafuta wala uvumba juu yake kwa sababu ni sadaka ya dhambi.

12 Atauleta kwa kuhani, naye atauchukua unga huo konzi moja kama sehemu ya kumbukumbu na atauteketeza kwenye madhabahu juu ya sadaka zilizotolewa kwaBwanakwa moto. Hii ni sadaka ya dhambi.

13 Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake kwa dhambi mojawapo ya hizo alizotenda, naye atasamehewa. Sadaka iliyobaki itakuwa ya kuhani, kama ilivyokuwa ile sadaka ya nafaka.’ ”

Sadaka Ya Hatia

14 Bwanaakamwambia Mose:

15 “Mtu anapokiuka na kutenda dhambi pasipo kukusudia kuhusu mojawapo ya mambo matakatifu yaBwana, huyo mtu ataleta kwaBwanakama adhabu, kondoo dume mmoja kutoka katika kundi lake, asiye na dosari na mwenye thamani halisi kifedha, kulingana na shekeli ya mahali patakatifu. Hii ni sadaka ya hatia.

16 Ni lazima alipe kwa yale aliyoshindwa kufanya kuhusu vitu vitakatifu, kwa kuongeza sehemu ya tano ya thamani ile na kuitoa yote kwa kuhani, ambaye atamfanyia upatanisho kwa huyo kondoo dume kama sadaka ya dhambi, naye atasemehewa.

17 “Kama mtu akifanya dhambi na kufanya yale yaliyokatazwa katika mojawapo ya amri zaBwana, hata ikiwa hajui, yeye ana hatia na anastahili adhabu.

18 Atamletea kuhani kama sadaka ya hatia kondoo dume kutoka kundi lake, kondoo asiye na dosari na mwenye thamani halisi kifedha. Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake kwa kosa alilotenda bila kukusudia, naye atasamehewa.

19 Hii ni sadaka ya hatia; amekuwa na hatia kwa kufanya kosa dhidi yaBwana.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/LEV/5-af066fdeecbc995d0f06de7814e528c1.mp3?version_id=1627—

Mambo ya Walawi 6

Kurudisha Kilichochukuliwa

1 Bwanaakamwambia Mose:

2 “Kama mtu ye yote akitenda dhambi naye si mwaminifu kwaBwanakwa kumdanganya jirani yake kuhusu kitu fulani alichokabidhiwa au kimeachwa chini ya utunzaji wake au kimeibwa, au kama akimdanganya,

3 au akiokota mali iliyopotea na akadanganya au kuapa kwa uongo, au kama akitenda dhambi yo yote ambayo watu waweza kuitenda;

4 wakati akitenda dhambi hizo na kuwa mwenye hatia, ni lazima arudishe kile alichokuwa amekiiba au amekichukua kwa dhuluma, au alichokuwa amekabidhiwa, au mali iliyokuwa imepotea akaipata,

5 au cho chote alichokuwa amekiapia kwa uongo. Lazima akirudishe kikamilifu, aongeze sehemu ya tano ya thamani yake na kumpa vyote mwenye mali siku ile anapopeleka sadaka yake ya hatia.

6 Kisha kama adhabu lazima amletee kuhani, yaani kwaBwana, sadaka yake ya hatia, kondoo dume kutoka katika kundi asiye na dosari na mwenye thamani kamili.

7 Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele zaBwana, naye atasamehewa kwa kosa lo lote katika mambo hayo aliyoyatenda yaliyomfanya kuwa na hatia.”

Sadaka Ya Kuteketezwa

8 Bwanaakamwambia Mose:

9 “Mpe Aroni na wanawe agizo hili: ‘Haya ndiyo masharti kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa: Sadaka ya kuteketezwa itabaki kwenye moto juu ya madhabahu usiku kucha, mpaka asubuhi, nao moto lazima uwe unaendelea kuwaka juu ya madhabahu.

10 Kisha kuhani atavaa mavazi yake ya kitani, pamoja na nguo za kitani za ndani, kisha ataondoa majivu ya sadaka ya kuteketezwa ambayo moto umeteketeza juu ya madhabahu na kuyaweka kando ya madhabahu.

11 Kisha atayavua mavazi haya na kuvaa mengine, atachukua yale majivu nje ya kambi na kupeleka mahali palipo safi kwa kawaida ya ibada.

12 Moto ulio juu ya madhabahu lazima uwe unaendelea kuwaka, kamwe usizimike. Kila asubuhi kuhani ataongeza kuni na kupanga sadaka ya kuteketezwa juu ya moto na kuteketeza mafuta ya sadaka za amani juu yake.

13 Moto lazima uendelee kuwaka juu ya madhabahu mfululizo, kamwe usizimike.

Sadaka Ya Nafaka

14 “ ‘Haya ndiyo masharti ya sadaka ya nafaka: Wana wa Aroni wataileta mbele zaBwana, mbele za madhabahu.

15 Kuhani atachukua konzi ya unga laini na mafuta, pamoja na uvumba wote juu ya sadaka ya nafaka na kuteketeza sehemu ya kumbukumbu juu ya madhabahu kama harufu nzuri ya kumpendezaBwana.

16 Aroni na wanawe watakula sehemu iliyobaki, lakini italiwa bila kutiwa chachu mahali patakatifu, wataila kwenye ua wa Hema la Kukutania.

17 Kamwe haitaokwa na chachu; nimewapa kama fungu lao la sadaka iliyotolewa kwangu kwa moto. Ni takatifu sana kama vile ilivyo sadaka ya dhambi na ya hatia.

18 Kila mwanaume mzao wa Aroni aweza kuila. Ni fungu lake la kawaida la sadaka zilizotolewa kwaBwanakwa moto kwa vizazi vijavyo. Cho chote kinachozigusa kitakuwa kitakatifu.’ ”

19 TenaBwanaakamwambia Mose,

20 “Hii ni sadaka ambayo Aroni na wanawe wanapaswa kuleta kwaBwanasiku atakapotiwa mafuta: sehemu ya kumi ya efaya unga laini kama sadaka ya kawaida ya nafaka, nusu yake ataitoa asubuhi na nusu nyingine jioni.

21 Iandae kwa mafuta kwenye kikaango; ilete ikiwa imechanganywa vizuri na utoe hiyo sadaka ya nafaka ikiwa imevunjwa vipande vipande kuwa harufu nzuri ya kumpendezaBwana.

22 Mtoto atakayeingia mahali pake kama kuhani aliyetiwa mafuta ndiye atakayeiandaa. Ni fungu la kawaida laBwana, nalo litateketezwa kabisa.

23 Kila sadaka ya nafaka ya kuhani itateketezwa kabisa; kamwe haitaliwa.”

Sadaka Ya Dhambi

24 Bwanaakamwambia Mose,

25 “Mwambie Aroni na wanawe: ‘Haya ndiyo masharti kwa ajili ya sadaka ya dhambi: Sadaka ya dhambi itachinjwa mbele zaBwanamahali sadaka ya kuteketezwa ichinjiwapo, ni takatifu sana.

26 Kuhani anayeitoa ndiye atakayeila, italiwa mahali patakatifu, katika ua wa Hema la Kukutania.

27 Cho chote kitakachogusa nyama yo yote ya hiyo sadaka kitakuwa kitakatifu na kama hiyo damu itadondokea juu ya vazi, lazima uifulie mahali patakatifu.

28 Chungu cha udongo kitakachopikiwa nyama lazima kivunjwe, lakini kama imepikiwa kwenye chombo cha shaba, chombo hicho kitasuguliwa na kusuuzwa kwa maji.

29 Kila mwanaume katika familia ya kuhani aweza kula nyama hiyo, ni takatifu sana.

30 Lakini kila sadaka ya dhambi ambayo damu yake imeletwa ndani ya Hema la Kukutania kufanya upatanisho katika Mahali Patakatifu kamwe haitaliwa; lazima iteketezwe.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/LEV/6-f56f7289a76a7ea82f9450ac76acc376.mp3?version_id=1627—

Mambo ya Walawi 7

Sadaka Ya Hatia

1 “ ‘Haya ndiyo masharti kwa ajili ya sadaka ya hatia, ambayo ni takatifu sana:

2 Sadaka ya hatia itachinjiwa mahali pale ambapo sadaka ya kuteketezwa huchinjiwa, damu yake itanyunyizwa pande zote za madhabahu.

3 Mafuta yake yote yatatolewa sadaka: mafuta ya mkia na mafuta yale yanayofunika sehemu za ndani,

4 figo zote mbili pamoja na mafuta yanayozizunguka yaliyo karibu na kiuno na yale yanayofunika ini, ambayo yataondolewa pamoja na hizo figo.

5 Kuhani atayateketeza juu ya madhabahu kuwa sadaka iliyotolewa kwaBwanakwa moto. Hii ni sadaka ya hatia.

6 Mwanaume ye yote katika jamaa ya kuhani aweza kuila, lakini lazima iliwe mahali patakatifu, ni takatifu sana.

7 “ ‘Sheria hii ya sadaka ya hatia ni sawa sawa na ile ya sadaka ya dhambi: Nyama ya yule mnyama aliyetolewa sadaka ni ya yule kuhani anayesimamia ibada ya upatanisho.

8 Kuhani anayetoa sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya ye yote anaweza kuichukua ile ngozi ya mnyama yule aliyetolewa iwe yake.

9 Kila sadaka ya nafaka iliyookwa jikoni au kupikwa katika sufuria au katika kikaangio itakuwa ya kuhani anayeitoa

10 na kila sadaka ya nafaka, ikiwa imechanganywa na mafuta au kavu, itakuwa ya wana wa Aroni, nayo itagawanywa sawa.

Sadaka Ya Amani

11 “ ‘Haya ndiyo masharti kwa ajili ya sadaka ya amani ambayo mtu aweza kuileta kwaBwana:

12 “ ‘Ikiwa mtu atatoa sadaka ya amani kwa ajili ya kuonyesha shukrani, ndipo pamoja na sadaka hii ya shukrani, atatoa maandazi yasiyotiwa chachu yaliyochanganywa na mafuta, mikate myembamba isiyotiwa chachu iliyopakwa mafuta, maandazi ya unga laini uliokandwa vizuri na kuchanganywa na mafuta.

13 Pamoja na sadaka hii ya amani ya shukrani ataleta sadaka ya maandazi yaliyotengenezwa kwa chachu.

14 Ataleta moja ya kila aina ya andazi kama sadaka, matoleo kwaBwana; hii ni ya kuhani anayenyunyiza damu ya sadaka ya amani.

15 Nyama ya sadaka ya amani kwa ajili ya shukrani lazima iliwe siku iyo hiyo inapotolewa; hutabakiza kitu cho chote mpaka asubuhi.

16 “ ‘Lakini kama sadaka yake ni kwa ajili ya nadhiri au ni sadaka ya hiari, sadaka hiyo italiwa siku hiyo inapotolewa, lakini cho chote kinachobakia kinaweza kuliwa kesho yake.

17 Nyama yo yote ya sadaka inayobaki mpaka siku ya tatu lazima iteketezwe kwa moto.

18 Kama nyama yo yote ya sadaka ya amani italiwa siku ya tatu,Bwanahataikubali. Haitahesabiwa kwake huyo aliyeitoa, kwa kuwa ni najisi, mtu atakayekula sehemu yake yo yote atakuwa na hatia kwa uovu huo.

19 “ ‘Nyama ile inayogusa cho chote ambacho ni najisi kwa kawaida ya ibada kamwe haitaliwa, ni lazima iteketezwe kwa moto. Kuhusu nyama nyingine, mtu ye yote aliye safi kwa kawaida ya ibada anaweza kuila.

20 Lakini kama mtu ye yote ni najisi akila nyama yo yote ya sadaka ya amani iliyotolewa kwaBwana, huyo mtu atakatiliwa mbali na watu wake.

21 Kama mtu ye yote akigusa kitu kilicho najisi, ikiwa ni uchafu wa mwanadamu, au mnyama najisi, au kitu cho chote kilicho najisi, kitu cha kuchukiza, kisha akala nyama yo yote ya sadaka ya amani iliyotolewa kwaBwana, mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali na watu wake.’ ”

Kula Mafuta Na Kunywa Damu Kwakatazwa

22 Bwanaakamwambia Mose,

23 “Waambie Waisraeli: ‘Msile mafuta yo yote ya ng’ombe, kondoo wala mbuzi.

24 Mafuta ya mnyama aliyekutwa amekufa au ameraruliwa na mnyama pori yanaweza kutumika kwa kazi nyingine yo yote, lakini kamwe msiyale.

25 Mtu ye yote alaye mafuta ya mnyama ambaye ametolewa sadaka kwaBwanakwa moto ni lazima akatiliwe mbali na watu wake.

26 Po pote mtakapoishi, kamwe msinywe damu ya ndege ye yote wala ya mnyama.

27 Ikiwa mtu ye yote atakunywa damu, mtu huyo lazima akatiliwe mbali na watu wake.’ ”

Fungu La Makuhani

28 Bwanaakamwambia Mose,

29 “Waambie Waisraeli: ‘Mtu ye yote aletaye sadaka ya amani kwaBwanaataleta sehemu ya sadaka hiyo kama dhabihu yake kwaBwana.

30 Kwa mikono yake mwenyewe ataileta sadaka iliyotolewa kwaBwanakwa moto; ataleta mafuta ya huyo mnyama pamoja na kidari, naye atainua hicho kidari mbele zaBwanakuwa sadaka ya kuinuliwa.

31 Kuhani atayateketeza hayo mafuta juu ya madhabahu, lakini kidari kitakuwa cha Aroni na wanawe.

32 Paja la kulia la sadaka zako za amani utampa kuhani kama matoleo.

33 Mwana wa Aroni atoaye damu na mafuta ya sadaka ya amani, ndiye atakayepewa paja hilo la kulia kuwa fungu lake.

34 Kutoka kwenye sadaka za amani za Waisraeli, mimi Mungu nimepokea kidari kile kilichoinuliwa pamoja na lile paja lililotolewa, nami nimevitoa kwa kuhani Aroni na wanawe kuwa fungu lao la kawaida kutoka kwa Waisraeli.’ ”

35 Hii ndiyo sehemu ya sadaka zilizotolewa kwaBwanakwa moto ambazo zilitengwa kwa ajili ya Aroni na wanawe siku ile walipowekwa wakfu kumtumikiaBwanakatika kazi ya ukuhani.

36 Siku ile walipotiwa mafuta,Bwanaaliagiza kwamba Waisraeli wawape hili kama fungu lao la kawaida kwa vizazi vijavyo.

37 Basi haya ndiyo masharti kuhusu sadaka ya kuteketezwa, sadaka ya nafaka, sadaka ya dhambi, sadaka ya hatia, sadaka ya kuwekwa wakfu na sadaka ya amani,

38 ambayoBwanaalimpa Mose juu ya mlima Sinai siku ile alipowaagiza Waisraeli walete sadaka zao kwaBwana, katika Jangwa la Sinai.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/LEV/7-8d8c1857e4f0a0108791ceceab4492b1.mp3?version_id=1627—

Mambo ya Walawi 8

Kuwekwa Wakfu Kwa Aroni Na Wanawe

1 Bwanaakamwambia Mose,

2 “Mletee Aroni na wanawe mavazi yao, mafuta ya upako, fahali kwa ajili ya sadaka ya dhambi, kondoo waume wawili na kikapu chenye mikate iliyotengenezwa bila chachu,

3 kisha kusanya mkutano wote kwenye ingilio la Hema la Kukutania.”

4 Mose akafanya kamaBwanaalivyomwagiza, mkutano ukakusanyika kwenye ingilio la Hema la Kukutania.

5 Mose akaliambia kusanyiko, “Hili ndiloBwanaaliloagiza lifanyike.”

6 Kisha Mose akamleta Aroni na wanawe mbele, akawaosha kwa maji.

7 Akamvika Aroni koti, akamfunga mshipi, akamvika joho na kumvalisha kisibau. Pia akafunga kisibau juu yake na kukifunga kiunoni mwake kwa mshipi wake uliosokotwa kwa ustadi.

8 Akaweka kifuko cha kifuani juu yake, na kuweka Urimu na Thumimukwenye hicho kifuko.

9 Kisha akamvika Aroni kilemba kichwani pake, akaweka lile bamba la dhahabu, ile taji takatifu, upande wa mbele wa kilemba, kamaBwanaalivyomwagiza Mose.

10 Ndipo Mose akachukua mafuta ya upako na kuipaka maskani na kila kitu kilichokuwamo ndani yake, kisha akaviweka wakfu.

11 Akanyunyiza baadhi ya mafuta juu ya madhabahu mara saba, akiipaka madhabahu mafuta na vyombo vyake vyote pamoja na sinia na kinara chake, ili kuviweka wakfu.

12 Akamimina sehemu ya hayo mafuta ya upako kichwani mwa Aroni, akamtia mafuta ili kumweka wakfu.

13 Kisha akawaleta wana wa Aroni mbele, akawavika makoti, akawafunga mishipi na kuwavika vilemba kamaBwanaalivyomwagiza Mose.

14 Kisha akamtoa fahali kwa ajili ya sadaka ya dhambi, nao Aroni na wanawe wakaweka mikono yao juu ya kichwa chake.

15 Mose akamchinja yule fahali na akachukua sehemu ya hiyo damu, kisha kwa kidole chake akaitia kwenye pembe zote za madhabahu ili kuitakasa madhabahu. Akaimwaga damu iliyobaki chini ya madhabahu, kwa hiyo akaiweka wakfu ili kufanya upatanisho kwa ajili ya hiyo madhabahu.

16 Pia Mose akachukua mafuta yote yanayozunguka sehemu za ndani, mafuta yanayofunika ini, figo zote mbili na mafuta yake na kuyateketeza juu ya madhabahu.

17 Lakini fahali pamoja na ngozi yake na nyama yake na sehemu zake za ndani na matumbo akayateketeza nje ya kambi, kamaBwanaalivyomwagiza Mose.

18 Kisha Mose akamleta kondoo dume kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, Aroni na wanawe wakaweka mikono yao juu ya kichwa chake.

19 Ndipo Mose akamchinja yule kondoo dume na kunyunyiza damu yake pande zote za ile madhabahu.

20 Akamkata yule kondoo dume vipande vipande na kukiteketeza kichwa, vile vipande na yale mafuta.

21 Kisha akamsafisha sehemu za ndani na miguu kwa maji na kumteketeza yule kondoo dume mzima juu ya madhabahu kuwa sadaka ya kuteketezwa, harufu nzuri ya kumpendeza, sadaka iliyotolewa kwaBwanakwa moto, kamaBwanaalivyomwagiza Mose.

22 Kisha akaleta kondoo dume mwingine, ndiye kondoo dume kwa ajili ya kuwaweka wakfu, Aroni na wanawe wakaweka mikono yao juu ya kichwa chake.

23 Mose akamchinja yule kondoo dume na kuichukua sehemu ya damu yake na kuipaka juu ya ncha ya sikio la kuume la Aroni na juu ya kidole gumba cha mkono wa kuume na juu ya kidole kikubwa cha mguu wa kuume.

24 Pia Mose akawaleta hao wana wa Aroni mbele na kuipaka sehemu ya hiyo damu kwenye ncha za masikio yao ya kuume, juu ya vidole gumba vya mikono ya kuume na juu ya vidole vikubwa vya miguu ya kuume. Kisha akanyunyiza damu pande zote za madhabahu.

25 Akachukua mafuta ya mnyama: mafuta ya mkia, mafuta yote yanayozunguka sehemu za ndani, mafuta yanayofunika ini, figo zote mbili pamoja na mafuta yake na paja la kulia.

26 Kisha kutoka kwenye kikapu cha mikate iliyotengenezwa bila chachu, kilichokuwa mbele zaBwana, akachukua andazi moja, na jingine lililotengenezwa kwa mafuta, na mkate mwembamba; akaviweka hivi vyote juu ya mafungu ya mafuta ya mnyama na juu ya lile paja la kulia.

27 Akaviweka hivi vyote mikononi mwa Aroni na wanawe, na kuviinua mbele zaBwanakuwa sadaka ya kuinuliwa.

28 Kisha Mose akavichukua kutoka mikononi mwao na kuviteketeza juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa kuwa sadaka ya kuwekwa wakfu, harufu nzuri ya kupendeza, sadaka iliyotolewa kwaBwanakwa moto.

29 Kisha akachukua kidari, kilicho fungu la Mose la kondoo dume kwa ajili ya kuwekwa wakfu, na kukiinua mbele zaBwanakama sadaka ya kuinuliwa, kamaBwanaalivyomwagiza Mose.

30 Kisha Mose akachukua sehemu ya mafuta ya upako, sehemu ya damu kutoka kwenye madhabahu na kuvinyunyiza juu ya Aroni na mavazi yake, na juu ya wanawe na mavazi yao. Kwa hiyo akamweka Aroni na mavazi yake wakfu, pamoja na wanawe na mavazi yao.

31 Kisha Mose akamwambia Aroni na wanawe, “Pika hiyo nyama kwenye ingilio la Hema la Kukutania na uile hapo pamoja na mkate kutoka kwenye kikapu cha sadaka ya kuweka wakfu, kama nilivyoagiza, nikisema, ‘Aroni na wanawe wataila.’

32 Kisha teketeza nyama na mikate iliyobaki.

33 Msitoke kwenye ingilio la Hema la Kukutania kwa muda wa siku saba, mpaka siku zenu za kuwekwa wakfu ziwe zimetimia, kwa kuwa muda wenu wa kuwekwa wakfu utakuwa siku saba.

34 Lile lililofanyika leo liliagizwa naBwanaili kufanya upatanisho kwa ajili yenu.

35 Lazima mkae kwenye ingilio la Hema la Kukutania mchana na usiku kwa siku saba, na kufanya lileBwanaanalolitaka, ili kwamba msife; kwa kuwa hilo ndilo nililoamriwa.”

36 Kwa hiyo Aroni na wanawe wakafanya kila kituBwanaalichoamuru kupitia Mose.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/LEV/8-dfe94cfec217c020cbfd845cb5da41d4.mp3?version_id=1627—