Mambo ya Walawi 9

Makuhani Waanza Huduma Yao

1 Katika siku ya nane Mose akawaita Aroni na wanawe na wazee wa Israeli.

2 Akamwambia Aroni, “Chukua ndama dume kwa ajili ya sadaka yako ya dhambi na kondoo dume kwa sadaka yako ya kuteketezwa, wote wawili wasiwe na dosari, nao uwalete mbele zaBwana.

3 Kisha waambie Waisraeli: ‘Chukueni mbuzi dume kwa ajili ya sadaka ya dhambi, ndama na mwana-kondoo, wote wawili wawe wa umri wa mwaka mmoja, wasio na dosari, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa

4 na maksai na kondoo dume kwa ajili ya sadaka ya amani, ili kutoa dhabihu mbele zaBwana, pamoja na sadaka ya nafaka iliyochanganywa na mafuta. Kwa kuwa leoBwanaatawatokea.’ ”

5 Wakavileta vile vitu Mose alivyowaagiza mbele ya Hema la Kukutania, nalo kusanyiko lote likakaribia na kusimama mbele zaBwana.

6 Ndipo Mose akasema, “Hili ndiloBwanaalilowaagiza mlifanye, ili utukufu waBwanaupate kuonekana kwenu.”

7 Mose akamwambia Aroni, “Njoo madhabahuni ili utoe dhabihu yako ya sadaka ya dhambi na sadaka yako ya kuteketezwa, ufanye upatanisho kwa ajili yako mwenyewe na kwa ajili ya watu; kisha utoe sadaka ya upatanisho kwa ajili ya watu, kama vileBwanaalivyoagiza.”

8 Hivyo Aroni akaja madhabahuni na kumchinja yule ndama kuwa sadaka ya dhambi kwa ajili yake mwenyewe.

9 Wanawe wakamletea damu, na akachovya kidole chake katika hiyo damu, akaitia kwenye pembe za madhabahu, damu iliyobaki akaimwaga chini ya madhabahu.

10 Juu ya madhabahu akateketeza mafuta, figo na mafuta yanayofunika ini kutoka kwenye hiyo sadaka ya dhambi, kamaBwanaalivyomwagiza Mose,

11 nyama na ngozi akaviteketeza nje ya kambi.

12 Kisha Aroni akachinja sadaka ya kuteketezwa. Wanawe wakamletea damu naye akainyunyiza pande zote za madhabahu.

13 Wakamletea sadaka ya kuteketezwa kipande kwa kipande, pamoja na kichwa, naye akaviteketeza juu ya madhabahu.

14 Akasafisha sehemu za ndani na miguu na kuviteketeza juu ya sadaka ya kuteketezwa juu ya madhabahu.

15 Kisha Aroni akaleta sadaka ile iliyokuwa kwa ajili ya watu. Akachukua yule mbuzi wa sadaka ya dhambi kwa ajili ya watu, akamchinja na kumtoa kwa ajili ya sadaka ya dhambi, kama alivyofanya kwa ile ya kwanza.

16 Aroni akaleta sadaka ya kuteketezwa na kuitoa kama ilivyoelekezwa.

17 Pia akaleta sadaka ya nafaka, akachukua konzi moja na kuiteketeza juu ya madhabahu pamoja na sadaka ya kuteketezwa ya asubuhi.

18 Akachinja maksai na kondoo dume kama sadaka ya amani kwa ajili ya watu. Wanawe wakampa ile damu, naye akainyunyiza kwenye madhabahu pande zote.

19 Lakini sehemu zile za mafuta ya yule maksai na kondoo dume, yaani mafuta ya mkia, mafuta yaliyofunika tumbo, ya figo na yaliyofunika ini,

20 hivi vyote wakaviweka juu ya vidari, kisha Aroni akayateketeza hayo mafuta ya wanyama juu ya madhabahu.

21 Aroni akaviinua vile vidari na paja la kulia mbele zaBwanakuwa sadaka ya kuinuliwa, kama Mose alivyoagiza.

22 Kisha Aroni akainua mikono yake kuwaelekea watu na kuwabariki. Naye baada ya kutoa dhabihu ya sadaka ya dhambi, sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya amani, akashuka chini.

23 Kisha Mose na Aroni wakaingia kwenye Hema la Kukutania. Walipotoka nje wakawabariki watu; nao utukufu waBwanaukawatokea watu wote.

24 Moto ukaja kutoka katika uwepo waBwana, ukairamba ile sadaka ya kuteketezwa, pamoja na sehemu ya mafuta yaliyokuwa juu ya madhabahu. Watu wote walipoona jambo hili, wakapiga kelele kwa furaha na kusujudu.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/LEV/9-f65bac37e3efd4719446c215302c6523.mp3?version_id=1627—

Mambo ya Walawi 10

Kifo Cha Nadabu Na Abihu

1 Nadabu na Abihu wana wa Aroni wakachukua vyetezo vyao, wakaweka moto ndani yake na kuongeza uvumba; kisha wakamtoleaBwanamoto usio halali, kinyume na agizo la Mungu.

2 Hivyo moto ukaja kutoka katika uwepo waBwanana kuwaramba, nao wakafa mbele zaBwana.

3 Kisha Mose akamwambia Aroni, “Hili ndilo alilonenaBwanawakati aliposema:

“ ‘Miongoni mwa wale watakaonikaribia

nitajionyesha kuwa mtakatifu;

machoni pa watu wote

nitaheshimiwa.’ ”

Aroni akanyamaza.

4 Mose akawaita Mishaeli na Elisafani, wana wa Uzieli mjomba wake Aroni, akawaambia, “Njoni hapa; itoeni miili ya binamu zenu nje ya kambi mbali na mahali patakatifu.”

5 Hivyo wakaja na kuwaondoa, wakiwa wamevalia makoti yao ya ibada, wakawapeleka nje ya kambi, kama Mose alivyoamuru.

6 Ndipo Mose akamwambia Aroni pamoja na wanawe, Eleazari na Ithamari, “Msifunue vichwa vyenu wala msirarue mavazi yenu, la sivyo mtakufa naBwanaataikasirikia jumuiya nzima. Lakini ndugu zenu, nyumba yote ya Israeli wanaweza kuwaombolezea wale ambaoBwanaamewaangamiza kwa moto.

7 Msitoke nje ya ingilio la Hema la Kukutania la sivyo mtakufa, kwa sababu mafuta yaBwanaya upako yako juu yenu.” Kwa hiyo wakafanya kama vile Mose alivyosema.

8 KishaBwanaakamwambia Aroni,

9 “Wewe na wanao msinywe mvinyo wala kinywaji kingine kilichochachuka wakati mwingiapo katika Hema la Kukutania, la sivyo mtakufa. Hili litakuwa Agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo.

10 Ni lazima mtenganishe kilicho kitakatifu na kile kilicho cha kawaida, kati ya yaliyo najisi na yaliyo safi,

11 na lazima mwafundishe Waisraeli amri zote ambazoBwanaaliwapa kupitia Mose.”

12 Mose akamwambia Aroni pamoja na wanawe waliosalia, Eleazari na Ithamari, “Chukueni sadaka ya nafaka iliyobaki kutoka katika sadaka zilizotolewa kwaBwanakwa moto, muile hapo kando ya madhabahu ikiwa imeandaliwa bila chachu, kwa sababu ni takatifu sana.

13 Mtaila katika mahali patakatifu kwa sababu ni fungu lenu na fungu la wana wenu la sadaka zilizotolewa kwaBwanakwa moto, kwa maana hivyo ndivyo nilivyoamuriwa.

14 Lakini wewe na wanao na binti zako mwaweza kula kidari kile kilichoinuliwa na paja lile lililotolewa. Mtavila mahali safi pa kawaida ya ibada; mmepewa wewe na watoto wako kuwa fungu lenu la sadaka za amani za Waisraeli.

15 Paja lile lililotolewa na kidari kile kilichoinuliwa lazima viletwe pamoja na sehemu za mafuta ya sadaka za kuteketezwa kwa moto, ili kuinuliwa mbele zaBwanakama sadaka ya kuinuliwa. Hili litakuwa fungu lako la kawaida na wanao, kamaBwanaalivyoagiza.”

16 Mose alipouliza kuhusu mbuzi atolewaye kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na kukuta kwamba ameteketezwa, aliwakasirikia Eleazari na Ithamari, wana wa Aroni waliobaki, akawauliza,

17 “Kwa nini hamkula sadaka ya dhambi katika eneo la mahali patakatifu? Ni takatifu sana, mlipewa ninyi ili kuondoa hatia ya jumuiya kwa ajili ya kuwafanyia upatanisho mbele zaBwana.

18 Kwa kuwa damu yake haikuletwa ndani ya Mahali Patakatifu, mngemla mbuzi huyo ndani ya mahali patakatifu kama nilivyoagiza.”

19 Aroni akamjibu Mose, “Leo wanangu wametoa sadaka zao za dhambi na sadaka zao za kuteketezwa mbele zaBwana, lakini mambo kama haya yamenitokea mimi. Je,Bwanaangependezwa kama ningekuwa nimekula sadaka ya dhambi leo?”

20 Mose aliposikia haya, akaridhika.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/LEV/10-8a6f20c18b66629902eb1ed084ce8489.mp3?version_id=1627—

Mambo ya Walawi 11

Vyakula Najisi Na Visivyo Najisi

1 Bwanaakawaambia Mose na Aroni,

2 “Waambie Waisraeli: ‘Kati ya wanyama wote waishio juu ya nchi, hawa ndio mtakaowala:

3 Mwaweza kula mnyama ye yote mwenye kwato zilizogawanyika sehemu mbili na ambaye hucheua.

4 “ ‘Kuna wanyama wengine ambao hucheua tu au wenye kwato zilizogawanyika tu, lakini hao kamwe msiwale. Ngamia, ingawa hucheua hana kwato zilizogawanyika; kwa kawaida ya ibada hiyo ni najisi kwenu.

5 Pelele, ingawa hucheua, lakini hana kwato zilizogawanyika; huyo ni najisi kwenu.

6 Sungura, ingawa hucheua lakini hana kwato zilizogawanyika; ni najisi kwenu.

7 Naye nguruwe ingawa anazo kwato zilizogawanyika sehemu mbili, lakini hacheui; ni najisi kwenu.

8 Kamwe msile nyama yao wala kugusa mizoga yao; wao ni najisi kwenu.

9 “ ‘Kuhusu viumbe vyote vinavyoishi ndani ya maji ya bahari na vijito, mtakula wale wote wenye mapezi na magamba.

10 Lakini viumbe vyote ndani ya bahari au vijito visivyo na mapezi na magamba, vikiwa miongoni mwa makundi au viumbe vyote ndani ya maji, hivyo ni machukizo kwenu.

11 Navyo vitakuwa machukizo kwenu. Msile nyama yao, nayo mizoga yao itakuwa machukizo.

12 Cho chote kinachoishi ndani ya maji ambacho hakina mapezi na magamba kitakuwa chukizo kwenu.

13 “ ‘Wafuatao ndio ndege watakaokuwa machukizo kwenu, hivyo msiwale kwa sababu ni chukizo: tai, furukombe, kipungu,

14 mwewe mwekundu, aina zote za mwewe mweusi,

15 aina zote za kunguru,

16 mbuni, kirukanjia, dudumizi, kipanga, shakwe, aina zote za mwewe,

17 bundi, mnandi, bundi mkubwa,

18 mumbi, mwari, mderi,

19 korongo, aina zote za koikoi, hudihudi na popo.

20 “ ‘Wadudu wote warukao wale watembeao kwa miguu minne watakuwa chukizo kwenu.

21 Lakini, wako viumbe wenye mabawa ambao hutembea kwa miguu minne mtakaowala: wale wenye vifundo katika miguu yao ya kurukaruka juu ya ardhi.

22 Miongoni mwa hawa, mtakula nzige wa aina zote, senene, parare au panzi.

23 Lakini viumbe wengine wote wenye mabawa na wenye miguu minne ni machukizo kwenu.

Wanyama Ambao Ni Najisi

24 “ ‘Wanyama hawa watawanajisi ninyi. Ye yote agusaye mizoga yao atakuwa najisi mpaka jioni.

25 Ye yote atakayebeba mizoga ya viumbe hawa ni lazima afue nguo zake naye atakuwa najisi mpaka jioni.

26 “ ‘Kila mnyama mwenye ukwato ulioachana lakini haukugawanyika kabisa au yule asiyecheua ni najisi kwenu; ye yote atakayegusa mzoga wo wote wa hao atakuwa najisi.

27 Miongoni mwa wanyama wote watembeao kwa miguu minne, wale watembeao kwa vitanga vyao ni najisi kwenu; ye yote atakayegusa mizoga yao atakuwa najisi mpaka jioni.

28 Ye yote atakayebeba mizoga yao ni lazima afue nguo zake na atakuwa najisi mpaka jioni. Wanyama hawa ni najisi kwenu.

29 “ ‘Kuhusu wanyama watambaao juu ya ardhi, hawa ni najisi kwenu: kicheche, panya, aina yo yote ya mijusi mikubwa,

30 guruguru, kenge, mijusi ya ukutani, goromoe na kinyonga.

31 Hao wote watambaao juu ya ardhi ni najisi kwenu. Ye yote atakayegusa mizoga yao atakuwa najisi mpaka jioni.

32 Ikiwa mmoja wao atakufa na kuangukia juu ya kitu fulani, chombo hicho, hata kikiwa cha matumizi gani, kitakuwa najisi, kiwe kimetengenezwa kwa mti, nguo, ngozi au gunia. Kiweke ndani ya maji; kitakuwa najisi mpaka jioni, kisha kitakuwa safi tena.

33 Ikiwa mmoja wa wanyama aliyekufa ataangukia ndani ya chungu, kila kilichomo katika chungu hicho kitakuwa najisi, nawe ni lazima uvunje chungu hicho.

34 Chakula cho chote ambacho chaweza kuliwa lakini kikawa kimeingia maji kutoka kwenye chungu hicho ni najisi na kitu cho chote cha majimaji ambacho chaweza kunyweka kutoka kwenye chungu hicho ni najisi.

35 Cho chote ambacho mzoga wa mmojawapo utaangukia kitakuwa najisi, jiko au chungu cha kupikia ni lazima kivunjwe. Ni najisi, nawe ni lazima uvihesabu kuwa najisi.

36 Lakini chemchemi au kisima, mahali pa kuchota maji, patakuwa safi, lakini ye yote atakayegusa moja ya mizoga hii ni najisi.

37 Kama mzoga ukianguka juu ya mbegu zo zote ambazo ni za kupanda, zinabaki safi.

38 Lakini kama mbegu imetiwa maji na mzoga ukaanguka juu yake, hiyo mbegu ni najisi kwenu.

39 “ ‘Kama mnyama ambaye mnaruhusiwa kumla akifa, ye yote atakayeugusa mzoga wake atakuwa najisi mpaka jioni.

40 Ye yote atakayekula sehemu ya mzoga huo ni lazima afue nguo zake, naye atakuwa najisi mpaka jioni. Ye yote atakayebeba mzoga huo ni lazima afue nguo zake, naye atakuwa najisi mpaka jioni.

41 “ ‘Kila kiumbe kitambaacho juu ya ardhi ni chukizo; kisiliwe.

42 Msile kiumbe cho chote kitambaacho juu ya ardhi, kiwe kitambaacho kwa tumbo lake au kitambaacho kwa miguu minne au kwa miguu mingi; ni chukizo.

43 Msijitie unajisi kwa cho chote katika viumbe hivi. Msijitie unajisi kwa viumbe hivyo na hivyo ninyi wenyewe kuwa najisi.

44 Mimi ndimiBwanaMungu wenu; jitakaseni mwe watakatifu, kwa sababu mimi ni mtakatifu. Msijitie unajisi wenyewe kwa kiumbe cho chote kile kiendacho juu ya ardhi.

45 Mimi ndimiBwananiliyewapandisha mtoke Misri ili niwe Mungu wenu; kwa hiyo iweni watakatifu kwa sababu Mimi ni mtakatifu.

46 “ ‘Haya ndiyo masharti kuhusu wanyama, ndege, kila kiumbe hai kiendacho ndani ya maji na kila kiumbe kiendacho juu ya ardhi.

47 Ni lazima mpambanue kati ya kilicho najisi na kilicho safi, kati ya viumbe hai vinavyoweza kuliwa na vile visivyoweza kuliwa.’ ”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/LEV/11-3c8148bc0ab79bd23a4d822cf8c495bf.mp3?version_id=1627—

Mambo ya Walawi 12

Utakaso Baada Ya Kuzaa Mtoto

1 Bwanaakamwambia Mose,

2 “Waambie Waisraeli: ‘Mwanamke ambaye atapata mimba na kuzaa mtoto wa kiume atakuwa najisi kwa kawaida ya ibada kwa siku saba, kama anavyokuwa najisi wakati wa siku zake za hedhi.

3 Mvulana atatahiriwa siku ya nane.

4 Kisha ni lazima huyo mwanamke asubiri kwa siku thelathini na tatu ndipo atakaswe kutoka damu kwake. Hataruhusiwa kugusa kitu cho chote kilicho kitakatifu au kuingia mahali patakatifu mpaka siku za kutakaswa kwake zimetimia.

5 Kama akimzaa mtoto wa kike, mwanamke huyo atakuwa najisi kwa majuma mawili, kama wakati wake wa hedhi. Kisha atasubiri kwa siku sitini na sita ndipo atatakaswa kutoka damu kwake.

6 “ ‘Siku zake za utakaso kwa ajili ya mwana au binti, zitakapotimia, mwanamke huyo atamletea kuhani kwenye ingilio la Hema la Kukutania mwana-kondoo mwenye umri wa mwaka mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa na kinda la njiwa au hua kwa ajili ya sadaka ya dhambi.

7 Atavitoa mbele zaBwanaili kufanya upatanisho kwa ajili yake, na kisha atakuwa safi kwa desturi ya ibada kutokana na kutokwa damu kwake.

“ ‘Haya ndiyo masharti kwa ajili ya mwanamke atakayezaa mtoto wa kiume au wa kike.

8 Kama huyo mwanamke hana uwezo wa kumpata mwana-kondoo, ataleta hua wawili au makinda mawili ya njiwa, moja kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa na mwingine kwa ajili ya sadaka ya dhambi. Kwa njia hii, kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake, naye atakuwa safi.’ ”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/LEV/12-eef421abdea28ae9b3ba4027fcfbf034.mp3?version_id=1627—

Mambo ya Walawi 13

Masharti Kuhusu Magonjwa Ya Ngozi Yaambukizayo

1 Bwanaakawaambia Mose na Aroni,

2 “Iwapo mtu ye yote atakuwa na uvimbe au upele au alama nyeupe juu ya ngozi yake ambayo yaweza kuwa ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza, ni lazima aletwe kwa Aroni kuhani ama kwa wanawe, kuhani mmojawapo.

3 Kuhani atachunguza hicho kidonda kilichopo juu ya ngozi yake na kama nywele za mahali palipo na kidonda zimebadilika kuwa nyeupe na ikiwa kidonda kimeingia ndani ya ngozi, basi ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza yaani ukoma. Kuhani atakapomchunguza, atamtangaza mtu huyo kuwa ni najisi kwa kawaida ya ibada.

4 Kama alama juu ya ngozi yake ni nyeupe lakini haionekani kuwa imeingia ndani zaidi ya ngozi na nywele kwenye alama hiyo hazijageuka kuwa nyeupe, kuhani atamtenga mtu huyo mahali pa pekee kwa siku saba.

5 Siku ya saba, kuhani atamchunguza na kama hakuona badiliko kwenye kile kidonda na hakijaenea juu ya ngozi, atamtenga kwa siku nyingine saba.

6 Siku ya saba kuhani atamchunguza tena, na kama kidonda kimepungua na hakijaenea juu ya ngozi, kuhani atamtangaza mtu huyo kuwa ni safi, ni upele tu. Ni lazima mtu huyo afue mavazi yake, naye atakuwa safi.

7 Lakini ikiwa ule upele utaenea juu ya ngozi yake baada ya yeye kujionyesha kwa kuhani na kutangazwa kuwa safi, ni lazima aende tena kwa kuhani.

8 Kuhani atamchunguza na kama upele umeenea kwenye ngozi, atamtangaza kuwa najisi, kwani ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza yaani ukoma.

9 “Wakati mtu ye yote ana ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza, ni lazima aletwe kwa kuhani.

10 Kuhani atamchunguza na kama kuna uvimbe mweupe juu ya ngozi ambao umefanya nywele kuwa nyeupe na kama kuna nyama mbichi ndani ya uvimbe,

11 ni ugonjwa sugu wa ngozi na kuhani atamtangaza kuwa najisi. Hatamtenga tena kwa sababu ni najisi tayari.

12 “Ikiwa ugonjwa utakuwa umeenea kwenye ngozi yake yote kwa kadiri kuhani atakavyoweza kuona, kwamba umeenea kwenye ngozi yote ya huyo mgonjwa kutoka kichwani mpaka wayo,

13 kuhani atamchunguza, na kama ugonjwa umeenea mwili mzima, atamtangaza huyo mtu kuwa safi. Kwa kuwa mwili wote umekuwa mweupe, yeye ni safi.

14 Lakini itokeapo nyama mbichi kwenye ngozi yake atakuwa najisi.

15 Kuhani atakapoiona hiyo nyama mbichi atamtangaza mtu huyo kuwa najisi. Hiyo nyama mbichi ni najisi, ana ugonjwa wa kuambukiza.

16 Hiyo nyama mbichi ikigeuka na kuwa nyeupe, ni lazima amwendee kuhani.

17 Kuhani atamchunguza, kama vidonda vimekuwa vyeupe, kuhani atamtangaza mgonjwa huyo kuwa safi; kisha atakuwa safi.

18 “Wakati mtu ana jipu juu ya ngozi yake nalo likapona,

19 napo mahali palipokuwa na jipu, pakatokea uvimbe mweupe au alama yenye wekundu na weupe, ni lazima akajionyeshe kwa kuhani.

20 Kuhani atapachunguza, na kama uvimbe umezama ndani ya ngozi na nywele zimegeuka kuwa nyeupe, kuhani atamtangaza mtu huyo kuwa najisi. Ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza uliojitokeza pale jipu lilipokuwa.

21 Lakini ikiwa wakati kuhani anapopachunguza pakawa hapana nywele nyeupe ndani yake wala hakuna shimo, bali pamepungua, basi kuhani atamtenga mtu huyo kwa siku saba.

22 Kama unaenea kwenye ngozi, kuhani atamtangaza kuwa najisi; ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza.

23 Lakini ikiwa ile alama haijabadilika wala kuenea, ni kovu tu kutokana na jipu, kuhani atamtangaza kuwa safi.

24 “Wakati mtu ameungua kwenye ngozi yake pakatokea alama yenye wekundu na weupe, au alama nyeupe ikaonekana penye nyama mbichi pale palipoungua,

25 kuhani ataichunguza ile alama, na kama nywele zilizoko juu yake zimegeuka kuwa nyeupe, napo pametokea shimo, basi huo ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza ambao umetokea juu ya jeraha la moto. Kuhani atamtangaza kuwa najisi; ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza.

26 Lakini kama kuhani akichunguza na kuona kwamba hakuna nywele nyeupe kwenye alama ile wala hakuna shimo napo pameanza kupungua, basi kuhani atamtenga kwa siku saba.

27 Siku ya saba kuhani atamchunguza tena na kama unaenea kwenye ngozi, kuhani atamtangaza kuwa najisi; ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza.

28 Lakini, kama alama ile haikubadilika na wala haijaenea kwenye ngozi napo pamepungua, ni uvimbe kutokana na jeraha la moto na kuhani atamtangaza kuwa safi; ni kovu tu kutokana na kuungua.

29 “Ikiwa mwanaume au mwanamke ana kidonda juu ya kichwa au juu ya kidevu,

30 kuhani atakichunguza kile kidonda na kama ataona kuwa kimeingia ndani na nywele zilizoko juu yake ni njano na nyembamba, kuhani atamtangaza mtu huyo kuwa najisi, kwani ni upele; ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza wa kichwa au kidevu.

31 Lakini kama kuhani akichunguza aina hii ya kidonda, kikionekana kuwa hakina shimo na hakuna nywele nyeusi juu yake, ndipo atakapomtenga mtu huyo kwa siku saba.

32 Siku ya saba kuhani atachunguza kidonda kile, kama upele haujaenea na hakuna nywele za manjano juu yake wala hakuna shimo lo lote,

33 mtu huyo ni lazima atanyolewa isipokuwa mahali palipo na ugonjwa, naye kuhani atamtenga kwa siku nyingine saba.

34 Siku ya saba kuhani atachunguza tena ule upele; ikiwa kwamba haujaenea kwenye ngozi na hakuna shimo mahali pale, kuhani atamtangaza kuwa safi. Lazima afue nguo zake naye atakuwa safi.

35 Lakini ikiwa upele utaenea juu ya ngozi baada ya kutangazwa kuwa safi,

36 kuhani atamchunguza, na kama upele umeenea kwenye ngozi, kuhani hana haja ya kutazama kama kuna nywele za manjano, mtu huyo ni najisi.

37 Lakini, hata hivyo, katika hukumu yake akiona hapajabadilika na nywele nyeusi zimeota juu yake, upele umepona. Yeye si najisi na kuhani atamtangaza kuwa safi.

38 “Ikiwa mwanaume au mwanamke ana alama nyeupe juu ya ngozi yake,

39 kuhani atawachunguza, kama alama hizo zina weupe uliofifia, ni vipele visivyo na madhara vilivyojitokeza kwenye ngozi; mtu huyo ni safi.

40 “Wakati mwanaume hana nywele naye ana upaa, yeye ni safi.

41 Ikiwa hana nywele kwenye ngozi ya kichwa chake na ana upaa tangu kwenye paji, ni safi.

42 Lakini kama ana kidonda chenye wekundu na weupe kwenye kichwa chake chenye upaa au kwenye paji la uso ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza unaojitokeza kichwani au kwenye paji lake la uso.

43 Kuhani atamchunguza na kama kidonda kilichovimba juu ya kichwa chake au kwenye paji la uso ni chekundu au cheupe kama ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza,

44 mtu huyo ni mgonjwa naye ni najisi. Kuhani atamtangaza kuwa najisi kwa sababu ya kidonda kwenye kichwa chake.

45 “Mtu mwenye ugonjwa kama huo wa kuambukiza ni lazima avae nguo zilizoraruka, asichane nywele zake, afunike sehemu ya chini ya uso wake na apige kelele, ‘Najisi! Najisi!’

46 Kwa muda wote atakaokuwa na ugonjwa huo wa kuambukiza atabaki kuwa najisi. Ni lazima aishi peke yake; ni lazima aishi nje ya kambi.

Masharti Kuhusu Upele

47 “Kama vazi lo lote lina maambukizo ya upele: likiwa ni vazi la sufu au kitani,

48 lo lote lililofumwa au kusokotwa likiwa la kitani au la sufu, ngozi yo yote au cho chote kilichotengenezwa kwa ngozi,

49 tena kama maambukizo kwenye vazi, au ngozi, au lililofumwa au kusokotwa, au kifaa cho chote cha ngozi, ni rangi ya kijani au nyekundu, huo ni upele unaoenea na ni lazima kuhani aonyeshwe.

50 Kuhani atachunguza upele huo na kukitenga kifaa hicho kwa siku saba.

51 Siku ya saba atakichunguza, na kama upele umeenea kwenye nguo, au kifaa kilichofumwa au kusokotwa, au ngozi, kwa vyo vyote vile itumikavyo, ni upele uangamizao, kifaa hicho ni najisi.

52 Ni lazima aichome hiyo nguo, ikiwa ni ya sufu ama kitani iliyofumwa ama kusokotwa, ama chombo cho chote cha ngozi chenye maambukizo, kwa kuwa ni upele unaoangamiza; chombo chote ni lazima kichomwe moto.

53 “Lakini wakati kuhani atakapokichunguza na kuona kuwa ule upele haujaenea kwenye nguo iliyofumwa au kusokotwa, au vifaa vya ngozi,

54 ataagiza kwamba kifaa chenye maambukizo kisafishwe. Kisha atakitenga kwa siku saba.

55 Baada ya kifaa chenye maambukizo kusafishwa, kuhani atakichunguza, na kama upele hujaonyesha badiliko lo lote, hata kama haujaenea, ni najisi. Choma kwa moto, kama upele umeenea upande mmoja au mwingine.

56 Kama kuhani ataona kuwa ile alama imefifia baada ya kuoshwa, basi atararua sehemu iliyo ambukizwa ya nguo au ngozi au kifaa kilichofumwa au kusokotwa.

57 Lakini kama ikijitokeza tena kwenye nguo au kitu kilichofumwa au kusokotwa, ama kifaa cha ngozi, kwamba ule upele unaenea, cho chote chenye upele ni lazima kichomwe kwa moto.

58 Nguo, au kitu kilichofumwa au kusokotwa, au kifaa cho chote cha ngozi ambacho kimesafishwa na kuondolewa upele, ni lazima kioshwe tena, nacho kitakuwa safi.”

59 Haya ni masharti kuhusu maambukizo ya upele kwenye mavazi ya sufu au kitani, yaliyofumwa ama kusokotwa, ama kifaa cho chote cha ngozi, kwa ajili ya kuvitangaza kuwa safi au najisi.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/LEV/13-1dd318d46d339f273f3cce8e3649c399.mp3?version_id=1627—

Mambo ya Walawi 14

Kutakasa Kutoka Maambukizo Ya Magonjwa Ya Ngozi

1 Bwanaakamwambia Mose,

2 “Haya ndiyo masharti yamhusuyo mtu mgonjwa wakati wa kufanyiwa ibada ya utakaso wakati aletwapo kwa kuhani:

3 Kuhani atakwenda kumchunguza nje ya kambi. Kama mtu huyo atakuwa amepona ugonjwa wake wa ngozi wa kuambukiza,

4 kuhani ataagiza vitu vifuatavyo viletwe kwa ajili ya mtu atakayetakaswa: ndege wawili safi walio hai, mti wa mwerezi, kitani nyekundu na hisopo.

5 Kisha kuhani ataagiza kwamba mmoja wa ndege wale achinjwe kwenye chungu chenye maji safi.

6 Kisha kuhani atamchukua ndege aliye hai na kumtumbukiza pamoja na mti wa mwerezi, kitani nyekundu na hisopo ndani ya damu ya yule ndege aliyechinjiwa kwenye maji safi.

7 Atamnyunyizia yule mwenye ugonjwa wa kuambukiza maji hayo mara saba na kumtangaza kuwa safi. Kisha atamwachia yule ndege aliye hai aende zake kwenye mashamba.

8 “Huyo mtu atakayetakaswa ni lazima afue nguo zake, anyoe nywele zake zote, na aoge kwa maji; ndipo atakapokuwa safi kwa desturi ya ibada. Baada ya hili anaweza kuingia kambini, lakini ni lazima akae nje ya hema lake kwa siku saba.

9 Siku ya saba ni lazima anyoe nywele zake zote; yaani anyoe nywele za kichwa, ndevu zake, kope zake na nywele nyingine zote. Ni lazima afue nguo zake, na aoge kwa maji, naye atakuwa safi.

10 “Siku ya nane, ni lazima alete kondoo dume wawili na kondoo jike mmoja, wote wa mwaka mmoja, na wasio na dosari, pamoja na sehemu tatu za kumi za efaza unga laini uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya sadaka ya nafaka, na logi mojaya mafuta.

11 Kuhani atakayemtangaza kuwa safi atahitaji kumkabidhi mgonjwa aliyepona pamoja na sadaka zake zote mbele zaBwanakatika ingilio la Hema la Kukutania.

12 “Kisha kuhani atamchukua mmoja wa wale kondoo dume na kumtoa kuwa sadaka ya hatia pamoja na ile logi moja ya mafuta; ataviinua mbele zaBwanakuwa sadaka ya kuinuliwa.

13 Atamchinja huyo kondoo katika mahali patakatifu ambapo sadaka ya dhambi na ile ya kuteketezwa huchinjwa. Kama ilivyo sadaka ya dhambi, sadaka ya hatia ni ya kuhani; nayo ni takatifu sana.

14 Kuhani atachukua sehemu ya damu ya sadaka ya hatia na kuitia kwenye ncha ya sikio la kuume la yule atakayetakaswa, kwenye kidole gumba cha mkono wa kuume, na kidole kikubwa cha mguu wa kuume.

15 Kuhani atachukua sehemu ya ile logi ya mafuta, atamimina kwenye kiganja cha mkono wake mwenyewe wa kushoto,

16 atachovya kidole chake cha mkono wa kuume kwenye mafuta yaliyoko kwenye kiganja chake, na kwa kidole hicho atamnyunyizia mtu yule anayetakaswa mara saba mbele zaBwana.

17 Kuhani atampaka sehemu ya mafuta yaliyobaki kiganjani kwenye ncha ya sikio la kuume la yule anayetakaswa, kwenye kidole gumba cha mkono wa kuume, na kidole kikubwa cha mguu wa kuume, mahali pale pale alipompaka damu ya sadaka ya kuondoa hatia.

18 Kuhani atayapaka mafuta yaliyobaki kwenye kiganja chake juu ya kichwa cha yule anayetakaswa na kufanya upatanisho kwa ajili yake mbele zaBwana.

19 “Kisha kuhani atatoa dhabihu ya sadaka ya dhambi na kufanya upatanisho kwa ajili ya yule atakayetakaswa kutoka unajisi wake. Baada ya hayo, kuhani atachinja sadaka ya kuteketezwa

20 na kuitoa juu ya madhabahu, pamoja na sadaka ya nafaka ili kumfanyia upatanisho, naye atakuwa safi.

21 “Hata hivyo, kama ni maskini na hawezi kupata vitu hivi, ni lazima achukue mwana-kondoo mmoja kama sadaka ya hatia ipate kuinuliwa ili kumfanyia upatanisho pamoja na sehemu ya kumi ya efaya unga laini uliochanganywa na logi moja ya mafuta kwa ajili ya sadaka ya nafaka,

22 na hua wawili au makinda mawili ya njiwa, kile atakachoweza kupata, mmoja kwa sadaka ya dhambi, na mwingine kwa sadaka ya kuteketezwa.

23 “Katika siku ya nane ni lazima avilete vitu hivyo kwa kuhani, kwa ajili ya kutakaswa kwake kwenye ingilio la Hema la Kukutania mbele zaBwana.

24 Kuhani atamchukua mwana-kondoo kwa ajili ya sadaka ya hatia pamoja na ile logi ya mafuta ya kuinuliwa mbele zaBwanakuwa sadaka ya kuinuliwa.

25 Atamchinja huyo mwana-kondoo kwa ajili ya sadaka ya hatia pia ataichukua sehemu ya damu yake na kuipaka kwenye ncha ya sikio la kuume la yule atakayetakaswa, ataipaka pia kwenye kidole gumba cha mkono wa kuume, na kidole kikubwa cha mguu wa kuume.

26 Kuhani atamiminia sehemu ya mafuta kwenye kiganja chake cha mkono wa kushoto,

27 na kwa kidole chake cha shahada cha mkono wa kuume, atamnyunyizia yule anayetakaswa yale mafuta yaliyo kwenye kiganja chake mara saba mbele zaBwana.

28 Atampaka mafuta yaliyobaki kwenye kiganja chake katika sehemu zote kama alivyompaka damu ya sadaka ya hatia: yaani, kwenye ncha ya sikio la kuume la yule anayetakaswa, kwenye kidole gumba cha mkono wake wa kuume, na kidole kikubwa cha mguu wa kuume.

29 Kuhani atayapaka mafuta yaliyobaki katika kiganja chake kwenye kichwa cha yule anayetakaswa na kufanya upatanisho kwa ajili yake mbele zaBwana.

30 Kisha atatoa dhabihu wale hua ama yale makinda ya njiwa, ambayo mtu ataweza kuwapata,

31 mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na mwingine kuwa sadaka ya kuteketezwa, pamoja na sadaka ya nafaka. Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho mbele zaBwanakwa ajili ya yule anayetakaswa.”

32 Haya ndiyo masharti kwa mtu ye yote mwenye ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza na ambaye hana uwezo wa kutoa sadaka za kawaida kwa ajili ya kutakaswa kwake.

Kutakaswa Upele

33 Bwanaakamwambia Mose na Aroni,

34 “Mtakapoingia katika nchi ya Kanaani ambayo ninawapa kuwa milki yenu, nami nikaweka upele ueneao kwenye nyumba katika nchi ile,

35 ni lazima mwenye nyumba hiyo akamwambie kuhani, ‘Nimeona kitu fulani kinachofanana na upele kwenye nyumba yangu.’

36 Kuhani ataagiza vitu vyote vitolewe ndani ya nyumba kabla hajaenda kuchunguza kama ina ugonjwa huo, ili kitu cho chote ndani ya nyumba kisitangazwe kuwa najisi. Baada ya hili kuhani ataingia ndani na kuikagua hiyo nyumba.

37 Atachunguza upele huo katika kuta za nyumba hiyo, nazo kama zina rangi ya kijani kibichi au wekundu na kuna mibonyeo ndani ya ukuta,

38 kuhani atatoka na kufunga mlango wa nyumba hiyo kwa siku saba.

39 Siku ya saba, kuhani atarudi kuikagua nyumba. Kama upele umeenea juu ya kuta,

40 ataagiza kwamba mawe yote yaliyoambukizwa yaondolewe na kutupwa katika eneo lililo najisi nje ya mji.

41 Kuta zote za ndani ya nyumba hiyo ni lazima zikwanguliwe na kifusi chake kitupwe mahali najisi nje ya mji.

42 Kisha watachukua mawe mengine na kujenga palipobomolewa kwa udongo mpya wa mfinyanzi na kuipiga nyumba hiyo lipu mpya.

43 “Ikiwa upele huo utatokea tena ndani ya ile nyumba baada ya mawe kuondolewa na nyumba kukwanguliwa na kuwekwa lipu mpya,

44 kuhani atakwenda kuikagua na kama upele umeenea ndani ya nyumba, basi ni upele uharibuo; nyumba hiyo ni najisi.

45 Ni lazima ibomolewe: mawe yake, mbao na lipu yake, vikatupwe nje ya mji mahali palipo najisi.

46 “Ye yote atakayeingia katika nyumba hiyo ikiwa imefungwa atakuwa najisi mpaka jioni.

47 Ye yote atakayelala au kula ndani ya nyumba hiyo ni lazima afue nguo zake.

48 “Lakini ikiwa kuhani atakuja kuikagua na kukuta kuwa upele haujaenea tena baada ya nyumba kupigwa lipu, ataitangaza nyumba ile kuwa safi, kwa sababu upele umekwisha.

49 Ili kuitakasa nyumba hiyo, mwenye nyumba ataleta ndege wawili, mti wa mwerezi, kitani nyekundu na hisopo.

50 Atamchinja mmoja wa wale ndege kwenye chungu chenye maji safi.

51 Kisha atachukua mti wa mwerezi, hisopo, kitani nyekundu na ndege aliye hai na kuvitumbukiza ndani ya damu ya ndege aliyechinjwa pamoja na maji safi na kuinyunyizia nyumba ile mara saba.

52 Ataitakasa nyumba kwa damu ya yule ndege, maji safi, ndege aliye hai, mti wa mwerezi, hisopo na kitani nyekundu.

53 Kisha atamwachia yule ndege aliye hai huru mashambani nje ya mji. Kwa njia hii atafanya upatanisho kwa ajili ya nyumba ile, nayo itakuwa safi.”

54 Haya ndiyo masharti kuhusu aina yo yote ya ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza, mwasho wo wote,

55 upele ndani ya nguo au ndani ya nyumba,

56 kwa uvimbe, vipele au kipaku king’aacho,

57 kupambanua wakati kitu fulani ni safi au najisi.

Haya ndiyo masharti kuhusu magonjwa ya ngozi ya kuambukiza na upele.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/LEV/14-351a09a6716335fa75a860e093bd21a8.mp3?version_id=1627—

Mambo ya Walawi 15

Kutokwa Na Umajimaji Usababishao Unajisi

1 Bwanaakawaambia Mose na Aroni,

2 “Semeni na Waisraeli na mkawaambie: ‘Wakati mtu ye yote anapotokwa na usaha mwilini, usaha huo ni najisi.

3 Iwe kwamba unaendelea kutiririka kutoka mwilini mwake au umeziba, utamfanya kuwa najisi. Hivi ndivyo usaha wake utakavyomletea unajisi:

4 “ ‘Kitanda cho chote atakacholala mtu mwenye kutokwa na usaha kitakuwa najisi, na cho chote atakachokalia kitakuwa najisi.

5 Ye yote atakayegusa kitanda chake ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi mpaka jioni.

6 Ye yote atakayeketi juu ya kitu cho chote alichokalia mwenye kutokwa na usaha, ni lazima afue nguo zake, na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi mpaka jioni.

7 “ ‘Ye yote atakayemgusa mtu mwenye kutokwa na usaha ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi mpaka jioni.

8 “ ‘Ikiwa mtu mwenye kutokwa na usaha atamtemea mate mtu ye yote ambaye ni safi, mtu huyo ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi mpaka jioni.

9 “ ‘Kila tandiko ambalo mtu huyo atalikalia wakati wa kupanda mnyama litakuwa najisi

10 na ye yote atakayegusa kitu cho chote alichokuwa amekalia atakuwa najisi mpaka jioni; ye yote atakayeinua vitu hivyo, ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi mpaka jioni.

11 “ ‘Ye yote atakayeguswa na mtu anayetokwa na usaha bila kunawa mikono yake kwa maji, ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi mpaka jioni.

12 “ ‘Chungu cha udongo kitakachoguswa na mtu huyo ni lazima kivunjwe, na kifaa cho chote cha mbao kitaoshwa kwa maji.

13 “ ‘Wakati mtu atakapotakasika kutokwa usaha kwake, anapaswa kuhesabu siku saba za kawaida ya ibada ya utakaso; ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji safi, naye atatakasika.

14 Siku ya nane, atachukua hua wawili au makinda mawili ya njiwa, aje mbele zaBwanakwenye ingilio la Hema la Kukutania na kumpa kuhani.

15 Kuhani atavitoa dhabihu, huyo mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi na huyo mwingine kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa. Kwa njia hii atafanya upatanisho mbele zaBwanakwa ajili ya huyo mtu kwa sababu ya kutokwa usaha kwake.

16 “ ‘Wakati mtu akitokwa na shahawa, ni lazima aoge mwili mzima kwa maji, na atakuwa najisi mpaka jioni.

17 Vazi lo lote ama ngozi yenye shahawa juu yake ni lazima ioshwe kwa maji, na itakuwa najisi mpaka jioni.

18 Ikiwa mtu atalala na mwanamke na kukawa na kutoka kwa shahawa, ni lazima wote waoge kwa maji, nao watakuwa najisi mpaka jioni.

19 “ ‘Ikiwa mwanamke atatokwa na damu ya kawaida ya mwezi, atakuwa najisi kwa siku saba, na ye yote atakayemgusa atakuwa najisi mpaka jioni.

20 “ ‘Cho chote atakacholalia wakati wake wa hedhi kitakuwa najisi, na cho chote atakachokikalia kitakuwa najisi.

21 Ye yote atakayegusa kitanda chake ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi mpaka jioni.

22 Ye yote atakayegusa cho chote atakachokalia ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi mpaka jioni.

23 Kiwe ni kitanda ama cho chote alichokuwa amekikalia, ikiwa mtu ye yote atakigusa, atakuwa najisi mpaka jioni.

24 “ ‘Ikiwa mwanaume atalala naye na ile damu ya mwezi ikamgusa, atakuwa najisi kwa siku saba; kitanda cho chote atakachokilalia huyo mwanaume kitakuwa najisi.

25 “ ‘Ikiwa mwanamke atatokwa na damu kwa siku nyingi zaidi ya siku zake za mwezi au amekuwa na damu inayoendelea zaidi ya kipindi chake, atakuwa najisi kwa kipindi chote cha shida hiyo, kama ilivyokuwa katika siku za hedhi yake.

26 Kitanda cho chote atakachokilalia huyo mwanamke wakati akiendelea kutokwa na damu kitakuwa najisi, kama kilivyokuwa kitanda chake wakati wa siku zake za hedhi, na cho chote atakachokalia kitakuwa najisi, kama wakati wake wa hedhi.

27 Ye yote agusaye vitu hivyo atakuwa najisi; ni lazima afue nguo zake na kuoga kwa maji, naye atakuwa najisi mpaka jioni.

28 “ ‘Wakati atakapotakasika kutoka hedhi yake, ni lazima ahesabu siku saba, na baada ya hapo atakuwa safi kwa kawaida ya ibada.

29 Siku ya nane ni lazima achukue hua wawili au makinda mawili ya njiwa na kuyaleta kwa kuhani kwenye mlango wa Hema la Kukutania.

30 Kuhani atatoa dhabihu, huyo mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi na huyo mwingine kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa. Kwa njia hii, atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele zaBwanakwa sababu ya unajisi wa kutokwa damu kwake.

31 “ ‘Ni lazima uwatenge Waisraeli kutokana na vitu ambavyo vinawafanya najisi, ili wasife katika unajisi wao kwa kunajisi makao yangu, ambayo yapo katikati yao.’ ”

32 Haya ni masharti kwa ajili ya mtu mwenye kutokwa na usaha, kwa ajili ya ye yote atakayetokwa na shahawa,

33 kwa ajili ya mwanamke katika siku zake za hedhi, kwa ajili ya mwanaume au mwanamke atokwaye na usaha, na kwa ajili ya mwanaume alalaye na mwanamke ambaye ni najisi kwa kawaida ya ibada.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/LEV/15-e0b1759006a404cd259c5b1906a3978a.mp3?version_id=1627—

Mambo ya Walawi 16

Siku Ya Upatanisho

1 Bwanaakasema na Mose baada ya kifo cha wana wawili wa Aroni waliokufa walipokaribia mbele zaBwana.

2 Bwanaakamwambia Mose: “Mwambie ndugu yako Aroni asije wakati wo wote atakavyo yeye ndani ya Patakatifu pa Patakatifu nyuma ya pazia mbele ya kiti cha rehema kile kilichoko juu ya Sanduku la Agano, la sivyo atakufa, kwa sababu huwa ninatokea ndani ya wingu juu ya kile kiti cha rehema.

3 “Hivi ndivyo Aroni atakavyoingia katika mahali patakatifu: akiwa na fahali mchanga kwa ajili ya sadaka ya dhambi na kondoo dume kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa.

4 Atavaa koti takatifu la kitani, pamoja na nguo za ndani za kitani; atafunga mshipi wa kitani kiunoni, na kuvaa kilemba cha kitani. Haya ni mavazi matakatifu, kwa hiyo ni lazima aoge kwa maji kabla ya kuyavaa mavazi hayo.

5 Atachukua mbuzi dume wawili kutoka kwa jumuiya ya Kiisraeli kwa ajili ya sadaka ya dhambi na kondoo dume kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa.

6 “Aroni atamtoa huyo fahali kwa ajili ya sadaka yake ya dhambi ili afanye upatanisho kwa ajili yake mwenyewe na nyumba yake.

7 Kisha atawachukua wale mbuzi waume wawili na kuwaleta mbele zaBwanakwenye ingilio la Hema la Kukutania.

8 Atapiga kura kwa ajili ya hao mbuzi wawili, mmoja kwa ajili yaBwanana mwingine kwa ajili ya Azazeli.

9 Aroni atamleta yule mbuzi ambaye kura yaBwanaimemwangukia na kumtoa dhabihu kwa ajili ya sadaka ya dhambi.

10 Lakini mbuzi aliyechaguliwa kwa kura kuwa wa Azazeli atatolewa akiwa hai mbele zaBwanaatumike kwa kufanya upatanisho kwa kumwacha aende jangwani kama aliyebebeshwa dhambi.

11 “Aroni atamleta yule fahali kwa ajili ya sadaka ya dhambi yake mwenyewe ili kufanya upatanisho kwa ajili yake na nyumba yake, naye atamchinja huyo fahali kwa ajili ya sadaka ya dhambi yake mwenyewe.

12 Atachukua chetezo kilichojaa makaa yanayowaka kutoka madhabahuni mbele zaBwanana konzi mbili za uvumba laini uliosagwa vizuri wenye harufu na kuvipeleka nyuma ya pazia.

13 Ataweka uvumba juu ya moto mbele zaBwana, na moshi wa uvumba utafunika kile kiti cha rehema kilicho juu ya Ushuhuda, ili kwamba asife.

14 Atachukua sehemu ya damu ya fahali na kwa kidole chake atanyunyiza sehemu ya mbele ya kiti cha rehema; kisha atanyunyiza sehemu ya hiyo damu kwa kidole chake mara saba mbele ya kiti cha rehema.

15 “Kisha atamchinja mbuzi wa sadaka ya dhambi kwa ajili ya watu na kuichukua damu yake nyuma ya pazia aifanyie kama alivyofanya kwa damu ya fahali: Atanyunyiza juu ya kiti cha rehema na mbele yake.

16 Kwa njia hii atafanya upatanisho kwa ajili ya Patakatifu pa Patakatifu kwa sababu ya unajisi na uasi wa Waisraeli, kwa dhambi zao zo zote. Atafanya hivyo kwa ajili ya Hema la Kukutania ambalo liko miongoni mwao katikati ya unajisi wao.

17 Mtu ye yote haruhusiwi kuwa ndani ya Hema la Kukutania kuanzia wakati Aroni anapoingia kufanya upatanisho katika Patakatifu pa Patakatifu mpaka atakapotoka nje, baada ya kujifanyia upatanisho yeye mwenyewe, nyumba yake pamoja na jumuiya yote ya Israeli.

18 “Kisha atatoka kuja kwenye madhabahu ile iliyo mbele zaBwanana kufanya upatanisho kwa ajili yake. Atachukua sehemu ya damu ya fahali na sehemu ya damu ya mbuzi na kuiweka kwenye pembe za madhabahu.

19 Atanyunyiza baadhi ya hiyo damu juu ya madhabahu kwa kidole chake mara saba ili kuitakasa na kuiweka wakfu kutokana na unajisi wa Waisraeli.

20 “Aroni atakapokuwa amemaliza kufanya upatanisho kwa ajili ya Patakatifu pa Patakatifu, Hema la Kukutania na madhabahu, atamleta mbele yule mbuzi aliye hai.

21 Ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha mbuzi aliye hai na kuungama juu yake uovu wote na uasi wa Waisraeli, yaani dhambi zao zote, kisha kuziweka juu ya kichwa cha huyo mbuzi. Atamwachia huyo mbuzi akimbilie jangwani kwa uangalizi wa mtu aliyepewa wajibu huo.

22 Yule mbuzi atachukua juu yake dhambi zao zote mpaka mahali pasipo na watu; naye yule mtu atamwachia akimbilie jangwani.

23 “Kisha Aroni atakwenda ndani ya Hema la Kukutania na kuvua yale mavazi ya kitani aliyoyavaa kabla ya kuingia katika Patakatifu pa Patakatifu, naye atayaacha pale.

24 Ataoga kwa maji mahali patakatifu na kuvaa mavazi yake ya kawaida. Kisha atatoka na kutoa dhabihu ya sadaka ya kuteketezwa kwa ajili yake na sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya watu, ili kufanya upatanisho kwa ajili yake na kwa ajili ya watu.

25 Pia atachoma mafuta ya mnyama wa sadaka ya dhambi juu ya madhabahu.

26 “Yule mtu anayemwachia yule mbuzi wa Azazeli ni lazima afue nguo zake na kuoga kwa maji; baadaye anaweza kuingia kambini.

27 Yule fahali na mbuzi aliyetolewa kwa ajili ya sadaka za dhambi, ambao damu yao ilikuwa imeletwa Patakatifu pa Patakatifu kwa ajili ya kufanya upatanisho, ni lazima watolewe nje ya kambi; ngozi zao, nyama, na matumbo yake pamoja na mavi vitateketezwa kwa moto.

28 Mtu atakayevichoma ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji; baadaye ataweza kuingia kambini.

29 “Hili litakuwa agizo la kudumu kwa ajili yenu: Katika siku ya kumi ya mwezi wa saba ni lazima mfunge wala msifanye kazi yo yote akiwa mzaliwa au mgeni anayeishi miongoni mwenu,

30 kwa sababu siku hii upatanisho utafanyika kwa ajili yenu ili kuwatakasa. Kisha, mbele zaBwana, mtakuwa safi kutokana na dhambi zenu zote.

31 Ni Sabato ya mapumziko, ni lazima mfunge; ni agizo la kudumu.

32 Kuhani ambaye ametiwa mafuta na kuwekwa wakfu ili kuingia mahali pa baba yake kama Kuhani Mkuu atafanya upatanisho. Atavaa mavazi matakatifu ya kitani,

33 na kufanya upatanisho kwa ajili ya Patakatifu pa Patakatifu, Hema la Kukutania na madhabahu, pia kwa ajili ya makuhani pamoja na jumuiya yote ya watu.

34 “Hili litakuwa agizo la kudumu kwa ajili yenu: Upatanisho utafanywa mara moja tu kwa mwaka kwa ajili ya dhambi zote za Waisraeli.”

Ndivyo ilivyofanyika, kama vileBwanaalivyomwamuru Mose.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/LEV/16-92910585a8733c242150f6080019d6ce.mp3?version_id=1627—

Mambo ya Walawi 17

Kunywa Damu Kumekatazwa

1 Bwanaakamwambia Mose,

2 “Sema na Aroni na wanawe pamoja na Waisraeli wote uwaambie: ‘Hili ndiloBwanaaliloagiza:

3 Mwisraeli ye yote atakayetoa dhabihu ya maksai, mwana-kondoo au mbuzi ndani ya kambi au nje yake,

4 badala ya kuileta kwenye ingilio la Hema la Kukutania ili kuileta kama sadaka kwaBwanambele ya Maskani yaBwana, mtu huyo atahesabiwa kuwa na hatia ya kumwaga damu; ni lazima akatiliwe mbali na watu wake.

5 Hii ni ili kwamba Waisraeli wamleteeBwanadhabihu wanazozifanya sasa mahali pa wazi mashambani. Ni lazima wazilete kwa makuhani, yaani kwaBwana, katika ingilio la Hema la Kukutania na kutoa dhabihu kama sadaka za amani.

6 Kuhani atanyunyiza damu kwenye madhabahu yaBwanakatika ingilio la Hema la Kukutania na kuyateketeza mafuta ya hiyo dhabihu kuwa harufu nzuri ya kumpendezaBwana.

7 Hawatatoa kamwe dhabihu zao kwa sanamu za mbuzi ambazo wamekuwa wakijifanyia nazo ukahaba. Hili litakuwa agizo la kudumu kwao na kwa ajili ya vizazi vijavyo.’

8 “Waambie: ‘Mwisraeli ye yote au mgeni ye yote anayeishi miongoni mwao atakayetoa sadaka ya kuteketezwa au dhabihu

9 bila kuileta kwenye ingilio la Hema la Kukutania ili kutoa dhabihu kwaBwana, mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali na watu wake.

10 “ ‘Mwisraeli ye yote au mgeni anayeishi miongoni mwao ambaye hunywa damu yo yote, nitakuwa kinyume cha mtu huyo atakayekunywa damu na kumkatilia mbali na watu wake.

11 Kwa kuwa uhai wa kiumbe uko ndani ya damu, nami nimewapa hiyo damu ili mfanyie upatanisho kwa ajili yenu wenyewe juu ya madhabahu; damu ndiyo ifanyayo upatanisho kwa ajili ya maisha ya mtu.

12 Kwa hiyo, ninawaambia Waisraeli, “Hakuna hata mmoja wenu anayeruhusiwa kunywa damu, wala mgeni anayeishi miongoni mwenu haruhusiwi kunywa damu.”

13 “ ‘Mwisraeli ye yote au mgeni anayeishi miongoni mwenu ambaye atamwinda mnyama au ndege anayeruhusiwa kuliwa ni lazima aimwage damu na kuifunika kwa udongo,

14 kwa sababu uhai wa kila kiumbe ni katika damu yake. Ndiyo sababu nimewaambia Waisraeli, “Kamwe msinywe damu ya kiumbe cho chote, kwa sababu uhai wa kila kiumbe ni katika damu yake; ye yote atakayekunywa damu ni lazima akatiliwe mbali.”

15 “ ‘Mtu ye yote, awe mzaliwa au mgeni, ambaye atakula mzoga wa kitu cho chote ama kilichouawa na wanyama mwitu ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi kwa kawaida ya ibada mpaka jioni, kisha atakuwa safi.

16 Lakini kama hakufua nguo zake na kuoga, atakuwa na hatia kwa kosa hilo.’ ”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/LEV/17-aaca7b63fca635cd053bb6e26c56a0de.mp3?version_id=1627—

Mambo ya Walawi 18

Uhusiano Wa Kukutana Kimwili Kinyume Cha Sheria

1 Bwanaakamwambia Mose,

2 “Sema na Waisraeli uwaambie: ‘Mimi ndimiBwanaMungu wenu.

3 Msifanye kama wafanyavyo huko Misri, mahali mlipokuwa mnaishi, wala msifanye kama wanavyofanya katika nchi ya Kanaani, mahali ninapowapeleka. Msifuate matendo yao.

4 Ni lazima mzitii sheria zangu, nanyi iweni waangalifu kuzifuata amri zangu. Mimi ndimiBwanaMungu wenu.

5 Mzishike amri zangu na sheria zangu, kwa maana mtu anayezitii ataishi kwa hizo. Mimi ndimiBwana.

6 “ ‘Hakuna mtu awaye yote atakayemsogelea ndugu wa karibu ili kukutana naye kimwili. Mimi ndimiBwana.

7 “ ‘Usimvunjie heshima baba yako kwa kukutana kimwili na mama yako. Yeye ni mama yako; usiwe na mahusiano kama hayo naye.

8 “ ‘Usikutane kimwili na mke wa baba yako; hiyo itamvunjia heshima baba yako.

9 “ ‘Usikutane kimwili na dada yako, wala binti wa baba yako, au binti wa mama yako, awe amezaliwa katika nyumba hiyo au mahali pengine.

10 “ ‘Usikutane kimwili na binti wa mwanao ama binti wa binti yako; utajivunjia heshima.

11 “ ‘Usikutane kimwili na binti wa mke wa baba yako, aliyezaliwa na baba yako; huyo ni dada yako.

12 “ ‘Usikutane kimwili na dada wa baba yako; ni ndugu wa karibu wa baba yako.

13 “ ‘Usikutane kimwili na dada wa mama yako, kwa sababu ni ndugu wa mama yako wa karibu.

14 “ ‘Usimvunjie heshima ndugu wa baba yako, kwa kukutana kimwili na mke wake; yeye ni shangazi yako.

15 “ ‘Usikutane kimwili na mkwe wako, yeye ni mke wa mwanao; usiwe na mahusiano kama hayo naye.

16 “ ‘Usikutane kimwili na mke wa kaka yako; utamvunjia heshima kaka yako.

17 “ ‘Usikutane kimwili na mwanamke kisha na binti yake. Usikutane kimwili na binti wa mwanawe au binti wa binti yake; hao ni ndugu zake wa karibu. Huo ni uovu.

18 “ ‘Usimchukue dada wa mke wako kuwa mke mwenza na kukutana naye kimwili wakati bado mke wako anaishi.

19 “ ‘Usimsogelee mwanamke ili kukutana naye kimwili wakati wa unajisi wa siku zake za mwezi.

20 “ ‘Usikutane kimwili na mke wa jirani yako na kujitia naye unajisi.

21 “ ‘Usimtoe mtoto wako ye yote awe kafara kwa mungu Moleki, kamwe usilinajisi jina la Mungu wako. Mimi ndimiBwana.

22 “ ‘Usikutane kimwili na mwanaume kama mtu akutanaye na mwanamke; hilo ni chukizo.

23 “ ‘Usikutane kimwili na mnyama na kujitia unajisi kwake. Mwanamke asijipeleke kwa mnyama ili kukutana naye kimwili; huo ni upotovu.

24 “ ‘Msijitie unajisi kwa njia yo yote katika hizi, kwa sababu hivi ndivyo mataifa nitakayoyafukuza mbele yenu yalivyojitia unajisi.

25 Hata nchi ikatiwa unajisi, hivyo nikaiadhibu kwa dhambi zake nayo nchi ikawatapika wakazi wake.

26 Lakini ni lazima uzitunze amri zangu na sheria zangu. Mzaliwa na wageni waishio miongoni mwenu kamwe wasifanye mambo yo yote ya machukizo haya,

27 kwa kuwa mambo haya yote yalifanywa na watu walioishi katika nchi hii kabla yenu na nchi ikawa najisi.

28 Kama mkiinajisi nchi, itawatapika kama ilivyowatapika mataifa yaliyowatangulia.

29 “ ‘Kila mtu atakayefanya mojawapo ya machukizo haya, watu hao ni lazima wakatiliwe mbali na watu wao.

30 Shikeni maagizo yangu, wala msifuate desturi za machukizo yo yote yaliyofanywa kabla hamjafika katika nchi hii na kujitia unajisi kwa hayo. Mimi ndimiBwanaMungu wako.’ ”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/LEV/18-18c061a224df94a9ee842eafd6e6248e.mp3?version_id=1627—