Mambo ya Walawi 19

Sheria Mbalimbali

1 Bwanaakamwambia Mose,

2 “Sema na kusanyiko lote la Israeli na uwaambie: ‘Iweni watakatifu kwa sababu Mimi,BwanaMungu wenu, ni mtakatifu.

3 “ ‘Kila mmoja wenu ni lazima amheshimu mama yake na baba yake, na pia ni lazima kuzishika Sabato zangu. Mimi ndimiBwanaMungu wenu.

4 “ ‘Msiabudu sanamu, wala msijitengenezee miungu ya shaba. Mimi ndimiBwanaMungu wenu.

5 “ ‘Mnapotoa dhabihu ya sadaka ya amani kwaBwana, toeni kwa namna ambayo itakubaliwa kwa niaba yenu.

6 Sadaka hiyo italiwa siku iyo hiyo mnayoitoa au kesho yake; cho chote kitakachobaki hadi siku ya tatu lazima kiteketezwe kwa moto.

7 Kama sehemu yo yote ya sadaka hiyo italiwa siku ya tatu, itakuwa si safi nayo haitakubaliwa.

8 Ye yote atakayekula atawajibishwa, kwa sababu amenajisi kitu kilicho kitakatifu kwaBwana; mtu huyo lazima akatiliwe mbali na watu wake.

9 “ ‘Wakati uvunapo mavuno ya nchi yako, usivune hadi kwenye mipaka ya shamba lako, wala usikusanye mabaki ya mavuno yako.

10 Usirudi mara ya pili katika shamba lako la mizabibu, wala usiokote zabibu zilizoanguka chini. Ziache kwa ajili ya maskini na mgeni. Mimi ndimiBwanaMungu wako.

11 “ ‘Usiibe.

“ ‘Usiseme uongo.

“ ‘Msidanganyane.

12 “ ‘Usiape kwa uongo kwa Jina langu na hivyo kulinajisi jina la Mungu wako. Mimi ndimiBwana.

13 “ ‘Usimdhulumu wala kumwibia jirani yako.

“ ‘Usishikilie mshahara wa kibarua usiku kucha hadi asubuhi.

14 “ ‘Usimlaani kiziwi wala usiweke kikwazo mbele ya kipofu, lakini umche Mungu wako. Mimi ndimiBwana.

15 “ ‘Usipotoshe haki; usionyeshe kumpendelea maskini wala upendeleo kwa mwenye cheo, bali mwamulie jirani yako kwa haki.

16 “ ‘Usiende huko na huko ukieneza uchochezi miongoni mwa watu wako.

“ ‘Usifanye kitu cho chote kile kinachohatarisha maisha ya jirani yako. Mimi ndimiBwana.

17 “ ‘Usimchukie ndugu yako moyoni mwako. Karipia jirani yako kwa uwazi ili usishiriki hatia yake.

18 “ ‘Usijilipizie kisasi wala kuwa na kinyongo dhidi ya mmoja wa jamaa yako, lakini mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe. Mimi ndimiBwana.

19 “ ‘Mtazishika amri zangu.

“ ‘Usiwaache wanyama wako wa kufugwa wakazaana na wengine wa aina tofauti.

“ ‘Usipande mbegu za aina mbili katika shamba lako.

“ ‘Usivae nguo iliyofumwa kwa nyuzi za aina mbili tofauti.

20 “ ‘Kama mwanaume atakutana kimwili na mwanamke ambaye ni msichana mtumwa aliyeposwa na mwanaume mwingine, lakini ambaye hajakombolewa wala hajapewa uhuru, lazima iwepo adhabu. Hata hivyo hawatauawa, kwa sababu msichana alikuwa bado hajaachwa huru.

21 Hata hivyo huyo mtu lazima alete kondoo dume kwenye ingilio la Hema la Kukutania kwa ajili ya sadaka ya hatia kwaBwana.

22 Pamoja na kondoo dume wa sadaka ya hatia, kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele zaBwanakwa ajili ya dhambi aliyotenda, naye atasamehewa dhambi yake.

23 “ ‘Mtakapoingia katika hiyo nchi na kupanda aina yo yote ya mti wa matunda, hesabuni matunda yake kama yaliyokatazwa. Kwa miaka mitatu mtayahesabu kwamba yamekatazwa; hayaruhusiwi kuliwa.

24 Katika mwaka wa nne matunda yote ya mti huo yatakuwa matakatifu, sadaka ya sifa kwaBwana.

25 Bali katika mwaka wa tano mnaweza kula matunda ya mti huo. Kwa njia hii mavuno yenu yataongezwa. Mimi ndimiBwanaMungu wako.

26 “ ‘Msile nyama yo yote yenye damu ndani yake.

“ ‘Msifanye uaguzi wala uchawi.

27 “ ‘Nywele za kichwa zisikatwe denge wala kunyoa pembe za ndevu zenu.

28 “ ‘Msichanje chale miili yenu kwa ajili ya mfu, wala msijichore alama juu ya miili yenu. Mimi ndimiBwana.

29 “ ‘Usimdhalilishe binti yako kwa kumfanya kahaba, la sivyo nchi itageukia ukahaba na kujaa uovu.

30 “ ‘Shika Sabato zangu na kuheshimu mahali pangu patakatifu. Mimi ndimiBwana.

31 “ ‘Msiwaendee waaguzi, wala msitafute wapunga pepo, kwa maana watawanajisi. Mimi ndimiBwanaMungu wako.

32 “ ‘Uwapo mbele ya mzee usimame, kuonyesha heshima kwa wazee, nawe umche Mungu wako. Mimi ndimiBwana.

33 “ ‘Wakati mgeni anaishi pamoja nawe katika nchi yako, usimnyanyase.

34 Mgeni anayeishi pamoja nawe ni lazima umtendee kama mmoja wa wazawa wa nchi yako. Mpende kama unavyojipenda mwenyewe, kwa maana ulikuwa mgeni katika nchi ya Misri. Mimi ndimiBwanaMungu wako.

35 “ ‘Usitumie vipimo vya udanganyifu unapopima urefu, kupima uzito, wala kupima wingi.

36 Tumia mizani halali, mawe ya kupimia uzito halali, efahalali, na hinihalali. Mimi ndimiBwanaMungu wako, ambaye alikutoa katika nchi ya Misri.

37 “ ‘Shika amri zangu zote na sheria zangu zote, nawe uzifuate. Mimi ndimiBwana.’ ”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/LEV/19-db6d14733c06153bac2213d6d778dcdc.mp3?version_id=1627—

Mambo ya Walawi 20

Adhabu Kwa Ajili Ya Dhambi

1 Bwanaakamwambia Mose,

2 “Sema na wana wa Israeli: ‘Mwisraeli ye yote au mgeni anayeishi katika Israeli ambaye atamtoa ye yote miongoni mwa watoto wake kuwa sadaka kwa mungu Moleki, mtu huyo lazima auawe. Watu wa jumuiya hiyo watampiga kwa mawe.

3 Mimi nitauelekeza uso wangu dhidi ya mtu huyo, nami nitamkatilia mbali na watu wake. Kwa maana kwa kumtoa mmoja wa watoto wake kwa mungu Moleki, amenajisi madhabahu yangu na kulinajisi Jina langu takatifu.

4 Ikiwa watu wa jumuiya watafumba macho wakati mtu huyo anapomtoa mmoja wa watoto wake kwa mungu Moleki, nao wakaacha kumwua,

5 mimi nitauelekeza uso wangu dhidi ya mtu huyo pamoja na jamaa yake, nami nitawakatilia mbali yeye na watu wote waliofanya ukahaba na Moleki.

6 “ ‘Mimi nitauelekeza uso wangu dhidi ya mtu anayewaendea waaguzi na wenye pepo kwa kujifanyia ukahaba kwa kuwafuata, nami nitamkatilia mbali na watu wake.

7 “ ‘Jitakaseni basi, nanyi iweni watakatifu, kwa sababu mimi ndimiBwanaMungu wenu.

8 Shikeni amri zangu na kuzifuata. Mimi ndimiBwana, niwafanyaye ninyi watakatifu.

9 “ ‘Ikiwa mtu ye yote atamlaani baba yake au mama yake, lazima auawe. Amemlaani baba yake au mama yake, nayo damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe.

10 “ ‘Ikiwa mtu atazini na mke wa mtu mwingine, yaani mke wa jirani yake, wazinzi hao wawili lazima wauawe.

11 “ ‘Kama mtu atakutana kimwili na mke wa baba yake, hakumheshimu baba yake. Mwanaume huyo na mwanamke huyo wote wauawe; damu yao itakuwa juu ya vichwa vyao wenyewe.

12 “ ‘Ikiwa mtu atakutana kimwili na mke wa mwanawe, lazima wote wawili wauawe. Walichokifanya ni upotovu; damu yao itakuwa juu ya vichwa vyao wenyewe.

13 “ ‘Kama mwanaume akikutana kimwili na mwanaume mwenzake kama vile mwanaume afanyavyo na mwanamke, wanaume hao wawili wamefanya lililo chukizo sana. Lazima wauawe; nayo damu yao itakuwa juu ya vichwa vyao wenyewe.

14 “ ‘Ikiwa mwanaume ataoa binti pamoja na mama yake, huo ni uovu. Wote watatu ni lazima wachomwe moto, ili kwamba pasiwepo na uovu katikati yenu.

15 “ ‘Kama mwanaume akikutana kimwili na mnyama, ni lazima auawe, na pia ni lazima mnyama huyo auawe.

16 “ ‘Kama mwanamke atamsogelea mnyama kukutana naye kimwili, mwueni mwanamke huyo pamoja na mnyama pia. Lazima wauawe; damu yao itakuwa juu ya vichwa vyao wenyewe.

17 “ ‘Ikiwa mtu anamwoa dada yake, binti aliyezaliwa na baba yake au mama yake, nao wakakutana kimwili, ni aibu. Lazima wakatiliwe mbali machoni pa watu wao. Huyo mwanaume amemwaibisha dada yake, hivyo atawajibika kwa ajili ya uovu huo.

18 “ ‘Ikiwa mwanaume atalala na mwanamke aliye katika hedhi yake na kukutana naye kimwili, amefunua mtiririko wa hedhi yake, naye huyo mwanamke amejifunua uchi wake. Wote wawili lazima wakatiliwe mbali na watu wao.

19 “ ‘Usikutane kimwili na dada wa mama yako wala wa baba yako, kwa maana hilo litamwaibisha jamaa wa karibu; ninyi wawili mtawajibika kwa ajili ya uovu huo.

20 “ ‘Ikiwa mwanaume atakutana kimwili na shangazi yake, huyo amemwaibisha mume wa huyo shangazi. Nao watawajibika kwa ajili ya uovu huo; watakufa bila kuzaa mtoto.

21 “ ‘Ikiwa mwanaume ataoa mke wa ndugu yake, hili ni tendo chafu; amemwaibisha ndugu yake. Nao hawatazaa mtoto.

22 “ ‘Shika amri na sheria zangu zote na kuzifuata, ili kwamba katika nchi ninayowaleta kuishi isiwatapike.

23 Kamwe msiishi kwa kufuata desturi za mataifa nitakayoyafukuza mbele yenu. Kwa sababu walifanya mambo haya yote, nami nikachukizwa sana nao.

24 Lakini niliwaambia, “Mtaimiliki nchi yao; nitawapa ninyi kuwa urithi, nchi inayotiririka maziwa na asali.” Mimi ndimiBwanaMungu wenu, ambaye amewatenga kutoka katika mataifa.

25 “ ‘Kwa hiyo, ninyi lazima mweze kutofautisha kati ya wanyama walio safi na wasio safi, pia kati ya ndege wasio safi na walio safi. Msijitie unajisi kutokana na mnyama ye yote, au ndege, wala kitu cho chote kitambaacho juu ya ardhi, vile ambavyo nimevitenga kuwa najisi kwa ajili yenu.

26 Mtakuwa watakatifu kwangu, kwa sababu Mimi,Bwana, ni mtakatifu, nami nimewatenga kutoka katika mataifa kuwa wangu mwenyewe.

27 “ ‘Mwanaume au mwanamke ambaye ni mchawi, mwaguzi au mwenye kupunga pepo miongoni mwenu lazima auawe. Mtawapiga kwa mawe; nayo damu yao itakuwa juu ya vichwa vyao wenyewe.’ ”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/LEV/20-3252b31f231e97062733bbc39f0a4c8d.mp3?version_id=1627—

Mambo ya Walawi 21

Sheria Kwa Ajili Ya Makuhani

1 Bwanaakamwambia Mose, “Sema na makuhani, wana wa Aroni, uwaambie: ‘Kwa utaratibu wa kiibada kamwe kuhani asijitie unajisi kwa ajili ya kugusa maiti ya mtu wake ye yote,

2 isipokuwa maiti ya jamaa yake wa karibu, kama vile mama yake au baba yake, mwanawe au binti yake, ndugu yake,

3 au dada yake asiyeolewa ambaye anamtegemea kwa kuwa hana mume, kwa ajili ya hao aweza kugusa maiti na kujitia unajisi.

4 Kamwe asijitie unajisi mwenyewe kutokana na wale watu ambao anahusiana nao kwa kuoana, na hivyo kujitia unajisi.

5 “ ‘Kamwe makuhani wasinyoe nywele za vichwa vyao wala wasinyoe pembeni mwa ndevu zao au kuweka chale kwenye miili yao.

6 Lazima wawe watakatifu kwa Mungu wao na kamwe wasilinajisi jina la Mungu wao. Kwa sababu ndio wanaotoa sadaka za kuteketezwa kwa moto, kwaBwana, chakula cha Mungu wao, hivyo lazima wawe watakatifu.

7 “ ‘Kamwe wasioe wanawake waliojinajisi kwa ukahaba au waliopewa talaka na waume wao, kwa sababu makuhani ni watakatifu kwa Mungu wao.

8 Waoneni kuwa watakatifu, kwa sababu ndio wanaotoa chakula cha Mungu wenu. Kumbukeni kuwa ni watakatifu, kwa sababu MimiBwanani mtakatifu, Mimi niwafanyaye ninyi watakatifu.

9 “ ‘Ikiwa binti wa kuhani amejitia unajisi kwa kufanya ukahaba, anamwaibisha baba yake; lazima achomwe kwa moto.

10 “ ‘Kuhani mkuu, aliye miongoni mwa ndugu zake, ambaye amekwisha kutiwa mafuta kwa kumiminiwa juu ya kichwa chake na ambaye amewekwa wakfu kuvaa mavazi ya ukuhani, kamwe asiache nywele zake bila kufunikwa wala asirarue nguo zake.

11 Kamwe asiingie ndani mahali penye maiti. Kamwe asijitie unajisi, hata kwa ajili ya baba yake au mama yake,

12 wala asiondoke mahali patakatifu pa Mungu wake au kupanajisi, kwa sababu amewekwa wakfu kwa kupakwa mafuta ya Mungu wake. Mimi ndimiBwana.

13 “ ‘Mwanamke atakayemwoa ni lazima awe bikira.

14 Kamwe asimwoe mjane, au mwanamke aliyepewa talaka, wala mwanamke aliyejinajisi kwa ukahaba, bali atamwoa tu bikira kutoka miongoni mwa watu wake,

15 hivyo hatawatia unajisi watoto wake miongoni mwa watu wake. Mimi ndimiBwana, nimfanyaye mtakatifu.’ ”

16 Bwanaakamwambia Mose,

17 “Mwambie Aroni: ‘Kwa vizazi vijavyo hakuna mzao wako mwenye dosari atakayekaribia kutoa chakula cha Mungu wake.

18 Hakuna mtu mwenye dosari yo yote awezaye kukaribia: hakuna mtu aliye kipofu au kiwete, au aliyeharibika uso au asiye na viungo kamili,

19 hakuna mtu mwenye mguu au mkono uliolemaa,

20 au mwenye kibiongo au aliyedumaa, au aliye na tatizo la macho, au aliye na uvimbe wenye usaha au majipu, au aliyehasiwa.

21 Hakuna mzao wa kuhani Aroni mwenye kilema cho chote atakayekaribia kutoa sadaka kwaBwanaya kuteketezwa kwa moto. Kama ana kilema, kamwe asikaribie kutoa chakula cha Mungu wake.

22 Anaweza kula chakula kitakatifu sana cha Mungu wake, pia hata chakula kitakatifu;

23 lakini kwa sababu ya kilema chake, kamwe asikaribie karibu na pazia wala kukaribia madhabahu, asije akanajisi mahali patakatifu pangu. Mimi ndimiBwana, niwafanyaye watakatifu.’ ”

24 Basi Mose akamwambia Aroni jambo hili na wanawe pamoja na Waisraeli wote.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/LEV/21-0f25e6a1e915580ef462ca08f53b4909.mp3?version_id=1627—

Mambo ya Walawi 22

Matumizi Ya Sadaka Takatifu

1 Bwanaakamwambia Mose,

2 “Mwambie Aroni na wanawe kushughulikia kwa uangalifu sadaka takatifu Waisraeli wanazoziweka wakfu kwangu, ili wasilinajisi Jina langu takatifu. Mimi ndimiBwana.

3 “Waambie: ‘Katika vizazi vijavyo, ikiwa ye yote wa wazao wako ni najisi kwa taratibu za kiibada, naye akakaribia sadaka takatifu Waisraeli wanazoziweka wakfu kwaBwana, mtu huyo lazima akatiliwe mbali na uso wangu. Mimi ndimiBwana.

4 “ ‘Ikiwa mzao wa Aroni ana ugonjwa wa ngozi unaoambukiza au anatokwa na usaha mwilini, hawezi kula sadaka takatifu mpaka atakasike. Vile vile atakuwa najisi ikiwa atagusa kitu cho chote kilichotiwa unajisi kwa kugusa maiti au mtu aliyetokwa na shahawa,

5 au ikiwa atagusa kitu cho chote kitambaacho hicho kimfanyacho mtu najisi, au mtu ye yote awezaye kumtia unajisi, unajisi uwao wote.

6 Mtu anayegusa kitu cho chote cha aina hiyo atakuwa najisi mpaka jioni. Kamwe hatakula sadaka yo yote takatifu mpaka yeye mwenyewe awe ameoga kwa maji.

7 Wakati jua linapotua, atakuwa safi na baada ya hilo anaweza kula sadaka takatifu, kwa kuwa ni vyakula vyake.

8 Kamwe asile nyama ya mzoga wala iliyoraruliwa na wanyama pori, naye akatiwa unajisi kwa hilo. Mimi ndimiBwana.

9 “ ‘Makuhani lazima washike maagizo yangu ili wasiwe na hatia, wakafa kwa kuyadharau. Mimi ndimiBwananinayewafanya watakatifu.

10 “ ‘Hakuna mtu ye yote asiye wa jamaa ya kuhani anayeruhusiwa kula sadaka takatifu, wala mgeni wa kuhani au mfanyakazi wake haruhusiwi kuila.

11 Lakini ikiwa kuhani amenunua mtumwa kwa fedha, au mtumwa amezaliwa katika nyumba ya kuhani huyo, mtumwa huyo aweza kula chakula cha huyo kuhani.

12 Ikiwa binti wa kuhani ameolewa na mtu asiye kuhani, binti huyo haruhusiwi kula cho chote cha matoleo matakatifu.

13 Lakini ikiwa binti wa kuhani amekuwa mjane au amepewa talaka, naye hana watoto, naye akarudi kuishi na jamaa ya baba yake kama wakati wa usichana wake, binti huyo anaweza kula chakula cha baba yake. Hata hivyo, mtu asiyeruhusiwa hawezi kula cho chote katika chakula hiki.

14 “ ‘Ikiwa mtu ye yote amekula sadaka takatifu kwa makosa, lazima atoe malipo ya sadaka hiyo kwa kuhani na kuongeza sehemu ya tano ya thamani ya sadaka hiyo.

15 Kamwe makuhani wasiinajisi sadaka takatifu ambayo Waisraeli wameitoa kwaBwana

16 kwa kuwaruhusu kuzila sadaka hizo takatifu, na hivyo kuwaletea hatia ya kudaiwa malipo. Mimi ndimiBwananiwafanyaye watakatifu.’ ”

Dhabihu Zisizokubalika

17 Bwanaakamwambia Mose,

18 “Sema na Aroni, wanawe na Waisraeli wote na uwaambie: ‘Ikiwa mmoja wenu, aliye Mwisraeli au mgeni anayeishi katika nchi ya Israeli, atatoa matoleo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa kwa moto kwaBwana, iwe kutimiza nadhiri au kuwa sadaka ya hiari,

19 lazima mtoe mnyama dume asiye na dosari akiwa ng’ombe, mbuzi au kondoo ili kwamba aweze kukubalika kwa niaba yako.

20 Kamwe usitoe kitu cho chote chenye dosari kwa sababu hakitakubaliwa kwa niaba yako.

21 Mtu ye yote aletapo sadaka ya amani kwaBwanakutoka kundi la ng’ombe au mbuzi ili kutimiza nadhiri maalum au sadaka ya hiari, lazima sadaka hiyo isiwe na dosari au waa ili ikubalike.

22 Kamwe usimtoleeBwanamnyama aliye kipofu, aliyejeruhiwa wala aliye kilema, au cho chote kilicho na uvimbe, au chenye upele au vidonda vinavyotoka usaha. Kamwe cho chote cha aina hii kisiwekwe juu ya madhabahu kuwa sadaka iliyotolewa kwaBwanaya kuteketezwa kwa moto.

23 Pengine, waweza kuamua na ukatoa sadaka ya hiari ng’ombe au kondoo mwenye kilema au aliyedumaa, lakini hii haitakubalika ili kuwa sadaka ya kutimiza nadhiri.

24 Kamwe usimtoleeBwanamnyama ambaye mapumbu yake yamejeruhiwa, au aliyehasiwa, au yaliyoraruliwa au kukatwa. Kamwe usifanye katika nchi yako mwenyewe,

25 na kamwe usikubali wanyama wa aina hii kutoka katika mkono wa mgeni na kuwatoa wanyama hao kuwa chakula kwa Mungu wako. Wanyama hao hawatakubaliwa kwa niaba yako, kwa sababu wana vilema, nao wana dosari.’ ”

26 Bwanaakamwambia Mose,

27 “Wakati ndama, mwana-kondoo au mwana-mbuzi azaliwapo, atabaki na mama yake kwa siku saba. Kuanzia siku ya nane na kuendelea anaweza kukubaliwa kuwa sadaka iliyotolewa kwaBwanakwa kuteketezwa kwa moto.

28 Usimchinje ng’ombe na ndama wake, au kondoo na kitoto chake siku moja.

29 “UnapomtoleaBwanadhabihu ya shukrani, itoe kwa namna ambayo itakubalika kwa niaba yako.

30 Ni lazima iliwe siku iyo hiyo, pasipo kubakiza cho chote mpaka asubuhi. Mimi ndimiBwana.

31 “Shikeni maagizo yangu na kuyafuata. Mimi ndimiBwana.

32 Msilinajisi Jina langu takatifu. Lazima nikubalike kuwa mtakatifu kwa Waisraeli. Mimi ndimiBwananinayewafanya watakatifu

33 na niliyewatoa katika nchi ya Misri niwe Mungu wenu. Mimi ndimiBwana.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/LEV/22-cfb2ab300106a4582dcaa9f85ce6e717.mp3?version_id=1627—

Mambo ya Walawi 23

Sikukuu Zilizoamuriwa

1 Bwanaakamwambia Mose,

2 “Sema na Waisraeli na uwaambie: ‘Hizi ndizo sikukuu zangu zilizoamuriwa, sikukuu zilizoamuriwa zaBwana, ambazo mtazitangaza kuwa makusanyiko matakatifu.

Sabato

3 “ ‘Kuna siku sita mnazoweza kufanya kazi, lakini siku ya saba ni Sabato ya kupumzika, siku ya kusanyiko takatifu. Hamtafanya kazi yo yote, po pote mnapoishi, ni Sabato kwaBwana.

Pasaka Na Mikate Isiyotiwa Chachu

4 “ ‘Hizi ni sikukuu zaBwanazilizoamuriwa, makusanyiko matakatifu mtakayoyatangaza kwa nyakati zilizoamuriwa:

5 Pasaka yaBwanahuanza jioni ya siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza.

6 Siku ya kumi na tano ya mwezi huo wa kwanza Sikukuu yaBwanaya Mikate Isiyotiwa Chachu huanza; kwa siku saba mtakula mikate isiyotiwa chachu.

7 Katika siku ya kwanza mtafanya kusanyiko takatifu na msifanye kazi zenu za kawaida.

8 Kwa siku saba mtamleteaBwanasadaka ya kuteketezwa kwa moto. Kwenye siku hiyo ya saba mtafanya kusanyiko takatifu na msifanye kazi zenu za kawaida.’ ”

Malimbuko

9 Bwanaakamwambia Mose,

10 “Sema na Waisraeli na uwaambie: ‘Mtakapoingia katika nchi nitakayowapa na kuvuna mazao ya nchi hiyo, leteni kwa kuhani mganda wa mavuno ya kwanza ya nafaka.

11 Naye atauinua huo mganda mbele zaBwanaili ukubaliwe kwa niaba yenu; kuhani ataupunga siku inayofuata Sabato.

12 Siku hiyo mtakapoinua huo mganda, lazima mtoe kwaBwanadhabihu ya kuteketezwa kwa moto mwana-kondoo wa mwaka mmoja asiye na dosari,

13 pamoja na sadaka ya unga laini wa nafaka sehemu mbili za kumi za efauliochanganywa na mafuta, sadaka iliyotolewa kwaBwanakwa kuteketezwa kwa moto, harufu nzuri ya kupendeza, na sadaka ya kinywaji robo ya hiniya divai.

14 Kamwe msile mkate wo wote, au nafaka iliyokaangwa au nafaka mpya, mpaka siku ile mtakayomletea Mungu wako sadaka hii. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo po pote mnapoishi.

Sikukuu Za Majuma

15 “ ‘Tangu siku ile iliyofuata Sabato, siku mliyotoa sadaka ya mganda wa kuinuliwa, hesabuni majuma saba kamili.

16 Mtahesabu mpaka siku inayofuata Sabato ya saba, siku hamsini, ndipo mtatoa sadaka ya nafaka mpya kwaBwana.

17 Kutoka po pote mnapoishi, leteni mikate miwili iliyookwa kwa unga laini, sehemu mbili za kumi za efa uliookwa wenye chachu, kuwa sadaka ya kuinuliwa ya malimbuko kwaBwana.

18 Toeni pamoja na hiyo mikate wana-kondoo saba, kila mmoja wa mwaka mmoja asiye na dosari, fahali mchanga, na kondoo waume wawili. Watakuwa sadaka ya kuteketezwa kwa moto iliyotolewa kwaBwana, pamoja na sadaka za nafaka na sadaka za vinywaji, sadaka iliyotolewa kwa moto yenye harufu nzuri ya kumpendezaBwana.

19 Kisha toeni dhabihu mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na wana-kondoo wawili kila mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya amani.

20 Kuhani atawainua hao wana-kondoo wawili mbele zaBwanakuwa sadaka ya kuinuliwa, pamoja na mkate wa malimbuko. Ni sadaka takatifu kwaBwanakwa ajili ya kuhani.

21 Siku iyo hiyo mtatangaza kusanyiko takatifu, na msifanye kazi zenu za kawaida. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo po pote mnapoishi.

22 “ ‘Mnapovuna mavuno ya ardhi yenu, msivune hadi mpakani mwa shamba lenu au kukusanya masazo ya mavuno yenu. Hayo utayaacha kwa ajili ya maskini na mgeni. Mimi ndimiBwanaMungu wenu.’ ”

Sikukuu Ya Tarumbeta

23 Bwanaakamwambia Mose,

24 “Waambie Waisraeli: ‘Katika siku ya kwanza ya mwezi wa saba mtakuwa na siku ya mapumziko, kusanyiko takatifu kwa ukumbusho pamoja na kupigwa kwa tarumbeta.

25 Msifanye kazi zenu zo zote za kawaida, lakini toeni sadaka kwaBwanailiyoteketezwa kwa moto.’ ”

Siku Ya Upatanisho

26 Bwanaakamwambia Mose,

27 “Siku ya kumi ya mwezi huu wa saba ni Siku ya Upatanisho. Mtafanya kusanyiko takatifu, mfunge, nanyi mtoe sadaka kwaBwanaya kuteketezwa kwa moto.

28 Msifanye kazi siku hiyo, kwa sababu ni Siku ya Upatanisho, upatanisho unapofanyika kwa ajili yenu mbele zaBwanaMungu wenu.

29 Mtu ye yote ambaye hatafunga siku hiyo ni lazima akatiliwe mbali na watu wake.

30 Mtu ye yote atakayefanya kazi siku hiyo nitamwangamiza kutoka miongoni mwa watu wake.

31 Hamtafanya kazi kamwe. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo po pote mnapoishi.

32 Ni Sabato ya mapumziko kwenu ninyi, ni lazima mfunge. Tangu jioni ya siku ya tisa ya mwezi hadi jioni inayofuata, mtaishika Sabato yenu.”

Sikukuu Ya Vibanda

33 Bwanaakamwambia Mose,

34 “Waambie Waisraeli: ‘Katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, Sikukuu yaBwanaya vibanda itaanza, nayo itaadhimishwa kwa siku saba.

35 Siku ya kwanza ni kusanyiko takatifu, msifanye kazi zenu za kawaida.

36 Kwa siku saba toeni sadaka kwaBwanaza kuteketezwa kwa moto, kwenye siku ya nane fanyeni kusanyiko takatifu na mtoe sadaka kwaBwanaya kuteketezwa kwa moto. Ni kusanyiko la mwisho, msifanye kazi zenu za kawaida.

37 (“ ‘Hizi ni sikukuu zaBwanazilizoamuriwa, ambazo mtazitangaza kuwa makusanyiko matakatifu kwa kuleta sadaka kwaBwanaza kuteketeza kwa moto: sadaka za kuteketezwa na sadaka za nafaka, dhabihu na sadaka za vinywaji zitahitajika kila siku.

38 Sadaka hizi ni nyongeza ya zile mnazozitoa katika Sabato zaBwana, na pia ni nyongeza ya matoleo yenu ya cho chote mlichoweka nadhiri, na sadaka zenu zote za hiari mnazozitoa kwaBwana.)

39 “ ‘Basi kuanzia siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, baada ya kuvuna mazao yote ya nchi, mtaadhimisha sikukuu kwaBwanakwa siku saba; siku ya kwanza ni mapumziko, pia siku ya nane ni mapumziko.

40 Kwenye siku ya kwanza mtachukua matunda mazuri ya miti, matawi ya mitende, matawi yenye majani mengi, na matawi ya mirebi, nanyi mtashangilia mbele zaBwanaMungu wenu kwa siku saba.

41 Mtaadhimisha siku hii kuwa sikukuu kwaBwanakwa siku saba kila mwaka. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo; iadhimisheni kwenye mwezi wa saba.

42 Mtaishi katika vibanda kwa siku saba: Wazawa wote wa Waisraeli wataishi katika vibanda,

43 ili wazao wenu wajue kuwa niliwafanya Waisraeli waishi kwenye vibanda nilipowatoa Misri. Mimi ndimiBwanaMungu wenu.’ ”

44 Kwa hiyo Mose akawatangazia Waisraeli sikukuu zilizoamuriwa naBwana.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/LEV/23-09161edba0f1f306b2a1c438e35cbfed.mp3?version_id=1627—

Mambo ya Walawi 24

Mafuta Na Mikate Mbele Za Bwana

1 Bwanaakamwambia Mose,

2 “Waagize Waisraeli wakuletee mafuta safi yaliyokamuliwa ya zeituni kwa ajili ya mwanga ili kwamba taa ziwe zinawaka mfululizo.

3 Nje ya pazia la Ushuhuda ndani ya Hema la Kukutania, Aroni ataziwasha taa mbele zaBwanakuanzia jioni hadi asubuhi kwa mfululizo. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo.

4 Taa zilizo juu ya kinara cha dhahabu safi mbele zaBwanalazima zihudumiwe mfululizo.

5 “Chukua unga laini na uoke mikate kumi na miwili, ukitumia sehemu mbili za kumi za efaza unga kwa kila mkate.

6 Iweke katika mistari miwili, kila mstari mikate sita, uiweke mbele zaBwanajuu ya meza iliyotengenezwa kwa dhahabu safi.

7 Kando ya kila mstari weka uvumba safi kama sehemu ya ukumbusho ili kuwakilisha mikate kuwa sadaka iliyotolewa kwaBwanakwa kuteketezwa kwa moto.

8 Mikate hii itawekwa mbele zaBwanakila wakati, Sabato baada ya Sabato, kwa niaba ya Waisraeli, kuwa Agano la kudumu.

9 Hii ni mali ya Aroni na wanawe, watakaoila katika mahali patakatifu, kwa sababu ni sehemu takatifu sana ya fungu lao la kawaida la sadaka iliyotolewa kwaBwanakwa kuteketezwa kwa moto.”

Mwenye Kukufuru Apigwa Mawe

10 Basi mwana wa mama wa Kiisraeli ambaye baba yake ni Mmisri alikwenda miongoni mwa Waisraeli na mapigano yakatokea ndani ya kambi kati yake na Mwisraeli.

11 Huyu mwana wa mwanamke wa Kiisraeli akalikufuru Jina laBwanana kulaani; kwa hiyo wakamleta kwa Mose. (Jina la mama yake aliitwa Shelomithi binti wa Dibri wa kabila la Dani.)

12 Nao wakamweka mahabusu mpaka mapenzi yaBwanayatakapokuwa wazi kwao.

13 NdipoBwanaakamwambia Mose:

14 “Mchukue huyo aliyekufuru nje ya kambi. Wale wote waliomsikia akikufuru wataweka mikono juu ya kichwa chake, kisha kusanyiko lote litampiga mawe.

15 Waambie Waisraeli: ‘Ikiwa mtu ye yote atamlaani Mungu wake, atakuwa na hatia kwa uovu wake;

16 ye yote atakayekufuru Jina laBwanani lazima auawe. Kusanyiko lote litampiga kwa mawe. Iwapo ni mgeni au mzawa, atakapolikufuru Jina laBwana, ni lazima auawe.

17 “ ‘Kama mtu ye yote atamwua mtu mwingine, ni lazima auawe.

18 Mtu ye yote auaye mnyama wa mtu mwingine lazima afidie, uhai kwa uhai.

19 Ikiwa mtu ye yote atamjeruhi jirani yake, cho chote alichomtenda naye atatendewa:

20 iwapo amemvunja mfupa atavunjwa mfupa, jicho kwa jicho, jino kwa jino. Kama alivyomjeruhi mwenzake, vivyo hivyo ndivyo atakavyojeruhiwa.

21 Ye yote auaye mnyama wa mtu lazima alipe fidia, lakini ye yote auaye mtu, lazima auawe.

22 Mtakuwa na sheria iyo hiyo kwa mgeni na kwa mzawa. Mimi ndimiBwanaMungu wenu.’ ”

23 Kisha Mose akasema na Waisraeli, nao wakamchukua yule aliyekufuru nje ya kambi na kumpiga mawe. Waisraeli wakafanya kamaBwanaalivyomwagiza Mose.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/LEV/24-f8b917f43fb3bf2f920307751a43acfa.mp3?version_id=1627—

Mambo ya Walawi 25

Mwaka Wa Sabato

1 Bwanaakamwambia Mose katika Mlima Sinai,

2 “Sema na Waisraeli na uwaambie: ‘Mtakapoingia katika nchi ninayowapa ninyi, nchi yenyewe ni lazima ishike Sabato kwa ajili yaBwana.

3 Kwa miaka sita mtapanda mazao katika mashamba yenu, nanyi kwa miaka sita mtaikata mizabibu yenu matawi na kuvuna mazao yake.

4 Lakini mwaka wa saba nchi lazima iwe na Sabato ya mapumziko, ni Sabato kwaBwana. Msipande mbegu katika mashamba yenu, wala msikate mizabibu yenu matawi.

5 Msivune na kuweka akiba kinachoota chenyewe, wala kuvuna na kusindika zabibu ambayo hamkuhudumia mashamba yake. Nchi lazima iwe na mwaka wa mapumziko.

6 Cho chote nchi itoacho katika mwaka wa Sabato kitakuwa chakula chenu wenyewe, watumishi wenu wa kiume na wa kike, mfanyakazi aliyeajiriwa, na mkazi wa muda anayeishi miongoni mwenu,

7 vile vile malisho ya mifugo yenu na wanyama pori katika nchi yenu. Cho chote nchi itakachozalisha kinaweza kuliwa.

Mwaka Wa Yubile

8 “ ‘Hesabu Sabato saba za miaka, yaani miaka saba mara saba, ili kwamba Sabato saba za miaka utakuwa muda wa miaka arobaini na tisa.

9 Ndipo tarumbeta itapigwa kila mahali katika siku ya kumi ya mwezi wa saba; katika Siku ya Upatanisho piga tarumbeta katika nchi yako yote.

10 Mwaka wa hamsini mtauweka wakfu na kutangaza uhuru katika nchi kwa wakazi wake wote. Itakuwa ni yubilekwenu; kila mmoja wenu atairudia mali ya jamaa yake, na kila mmoja kurudi kwenye ukoo wake.

11 Mwaka wa hamsini utakuwa yubile kwenu, msipande wala msivune kile kiotacho chenyewe, au kuvuna zabibu zisizohudumiwa.

12 Kwa kuwa ni yubile, nayo itakuwa takatifu kwenu; mtakula tu kile kilichotoka moja kwa moja mashambani.

13 “ ‘Katika Mwaka huu wa Yubile kila mmoja atarudi kwenye mali yake mwenyewe.

14 “ ‘Ikiwa utauza ardhi kwa mmoja wa wazawa wa nchi yako, au ukinunua ardhi kutoka kwake, mmoja asimpunje mwingine.

15 Utanunua ardhi kwa mzawa wa nchi yako kwa misingi ya hesabu ya miaka baada ya Yubile. Naye ataiuza kwako kwa misingi ya hesabu ya miaka iliyobaki kwa kuvuna mavuno.

16 Miaka inapokuwa mingi, utaongeza bei, nayo miaka ikiwa michache, utapunguza bei, kwa sababu kile anachokuuzia kwa hakika ni hesabu ya mazao.

17 Mmoja asimpunje mwingine, bali utamcha Mungu wako. Mimi ndimiBwanaMungu wako.

18 “ ‘Fuateni amri zangu, mwe waangalifu kutii amri zangu, nanyi mtaishi salama katika nchi.

19 Kisha nchi itazaa matunda yake, nanyi mtakula na kushiba na kuishi humo kwa salama.

20 Mwaweza kuuliza, “Tutakula nini katika mwaka wa saba ikiwa hatutapanda wala kuvuna mazao yetu?”

21 Nitawapelekeeni baraka ya pekee katika mwaka wa sita, kwamba nchi itazalisha mazao ya kutosha kwa miaka mitatu.

22 Iwapo mtapanda mwaka wa nane mtakula mavuno ya miaka iliyopita, pia mtaendelea kuyala mazao hayo mpaka yajapo mavuno ya mwaka wa tisa.

23 “ ‘Kamwe ardhi isiuzwe kwa mkataba wa kudumu, kwa sababu nchi ni mali yangu, nanyi ni wageni na wapangaji wangu.

24 Katika nchi yote mtakayoshika kuwa milki yenu, ni lazima mtoe ukombozi wa ardhi.

25 “ ‘Ikiwa mmoja wa wazawa wa nchi yako amekuwa maskini na akauza baadhi ya mali yake, ndugu yake wa karibu atakuja na kukomboa kile ndugu yako alichokiuza.

26 Iwapo mtu huyo hana jamaa wa karibu wa kukomboa mali hiyo kwa ajili yake, lakini yeye mwenyewe akafanikiwa na kupata njia itoshayo kuikomboa,

27 ataamua tena thamani yake kwa miaka tangu alipoiuza, na kurudisha kiasi kilichobaki cha thamani kwa mtu ambaye alikuwa amemwuzia mali hiyo, naye ataweza kuirudia mali yake.

28 Lakini kama hatapata njia ya kumlipa mnunuzi, ile mali aliyouza itabaki kumilikiwa na mnunuzi mpaka Mwaka wa Yubile. Mali hiyo itarudishwa mwaka wa Yubile, naye anaweza kuirudia mali yake.

29 “ ‘Ikiwa mtu atauza nyumba iliyo ndani ya mji uliozungukwa kwa ukuta, yeye anayo haki ya kuikomboa mwaka mmoja baada ya mauzo ya hiyo nyumba. Wakati huo anaweza kuikomboa.

30 Ikiwa haikukombolewa kabla ya mwaka mmoja kamili kupita, nyumba iliyo ndani ya mji uliozungukwa kwa ukuta itakuwa mali ya kudumu ya mnunuzi na wazao wake. Haitarudishwa mwaka wa Yubile.

31 Lakini nyumba zilizo vijijini bila ya kuwa na kuta zilizozizunguka zitahesabiwa kama mashamba. Zinaweza kukombolewa, nazo zirudishwe katika mwaka wa Yubile.

32 “ ‘Walawi siku zote wana haki ya kukomboa nyumba zao katika miji ya Walawi wanayoimiliki.

33 Kwa hiyo mali ya Mlawi inaweza kukombolewa, yaani nyumba iliyouzwa katika mji wo wote wanaoushikilia itarudishwa mwaka wa Yubile, kwa sababu nyumba zilizo katika miji ya Walawi ni mali yao miongoni mwa Waisraeli.

34 Lakini nchi ya malisho iliyo mali ya miji yao kamwe isiuzwe, ni milki yao ya kudumu.

35 “ ‘Ikiwa mmoja wa wazawa wa nchi yako amekuwa maskini naye akashindwa kujitegemeza mwenyewe katikati yako, msaidie kama vile ambavyo ungelimsaidia mgeni au kama mkazi wa muda, ili aweze kuendelea kuishi katikati yako.

36 Usichukue riba wala faida yo yote kutoka kwake, bali utamwogopa Mungu wako, ili kwamba mzawa wa nchi yako aweze kuendelea kuishi katikati yako.

37 Usimkopeshe fedha ili alipe na riba, wala usimwuzie chakula kwa faida.

38 Mimi ndimiBwanaMungu wako, niliyekuleta kutoka nchi ya Misri nikupe nchi ya Kanaani nami niwe Mungu wako.

39 “ ‘Ikiwa mmoja wa wazawa wa nchi yako amekuwa maskini katikati yako naye akajiuza kwako, usimfanye atumike kama mtumwa.

40 Atatendewa kama mfanyakazi aliyeajiriwa, au kama mkazi wa muda katikati yako, naye atatumika mpaka Mwaka wa Yubile.

41 Ndipo yeye na watoto wake wataachiwa, naye atarudi kwa watu wa ukoo wake na kwenye mali ya baba zake.

42 Kwa sababu Waisraeli ni watumishi wangu niliowaleta kutoka nchi ya Misri, kamwe wasiuzwe kama watumwa.

43 Usiwatawale kwa ukatili, lakini utamcha Mungu wako.

44 “ ‘Watumwa wako wa kiume na wa kike watatoka katika mataifa yanayokuzunguka; kutoka kwao waweza kununua watumwa.

45 Pia waweza kununua baadhi ya wakazi wa muda wanaoishi katikati yako na jamaa ya koo zao waliozaliwa katika nchi yako, nao watakuwa mali yako.

46 Hao waweza kuwarithisha watoto wako kuwa urithi wao na wanaweza kuwafanya watumwa maisha yao yote, lakini usiwatawale ndugu zako Waisraeli kwa ukatili.

47 “ ‘Ikiwa mgeni au mkazi wa muda katikati yako atakuwa tajiri na mmoja wa wazawa wa nchi yako akawa maskini, naye akajiuza kwa yule mgeni anayeishi katikati yako au kwa mmoja wa jamaa wa koo za wageni,

48 anayo haki ya kukombolewa baada ya kujiuza. Mmoja wa jamaa zake aweza kumkomboa:

49 Mjomba wake, au binamu yake, au ye yote aliye ndugu wa damu katika ukoo wake aweza kumkomboa. Au ikiwa atafanikiwa, anaweza kujikomboa mwenyewe.

50 Yeye na huyo aliyemnunua watahesabu muda kuanzia mwaka aliojiuza hadi Mwaka wa Yubile. Mahali pa kuanzia bei ya kuachiwa kwake itakadiriwa na kilicholipwa kwa mfanyakazi aliyeajiriwa kwa idadi ya hiyo miaka.

51 Ikiwa imebaki miaka mingi, ni lazima atalipia ukombozi wake fungu kubwa la bei iliyolipwa kumnunua yeye.

52 Ikiwa miaka iliyobaki ni michache kufikia Mwaka wa Yubile, atafanya hesabu yake naye atalipa malipo yanayostahili kwa ajili ya ukombozi wake.

53 Atatendewa kama mtu wa kuajiriwa mwaka hadi mwaka; lazima uone kwamba yule aliyemnunua hamtawali kwa ukatili.

54 “ ‘Hata ikiwa hakukombolewa kwa njia mojawapo ya hizi, yeye na watoto wake wataachiwa katika Mwaka wa Yubile,

55 kwa maana Waisraeli ni mali yangu kama watumishi. Wao ni watumishi wangu, niliowatoa kutoka nchi ya Misri. Mimi ndimiBwanaMungu wako.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/LEV/25-a6eaa14c9edca4cbf232df3093ea569b.mp3?version_id=1627—

Mambo ya Walawi 26

Thawabu Ya Utii

1 “ ‘Msijitengenezee sanamu au kusimamisha kinyago cha kuchonga, mnara, wala jiwe la kuabudia, pia msijiwekee jiwe lililochongwa katika nchi yenu na kusujudu mbele yake. Mimi ndimiBwanaMungu wenu.

2 “ ‘Zishikeni Sabato zangu na kuheshimu mahali patakatifu pangu. Mimi ndimiBwana.

3 “ ‘Ikiwa mtafuata amri zangu na kuwa waangalifu kutii maagizo yangu,

4 nitawanyeshea mvua katika majira yake, nayo ardhi itatoa mazao yake na miti ya mashambani itazaa matunda yake.

5 Kupura nafaka kwenu kutaendelea mpaka wakati wa kuvuna zabibu, pia kuvuna zabibu kutaendelea mpaka wakati wa kupanda mbegu, nanyi mtakula na kushiba, na mtaishi salama katika nchi yenu.

6 “ ‘Nitawapa amani katika nchi, mpate kulala pasipo kutiwa hofu na ye yote. Nitawaondoa wanyama wakali watoke kwenye nchi, nao upanga hautapita katika nchi yenu.

7 Mtawafukuza adui zenu, nanyi mtawaua kwa upanga mbele yenu.

8 Watu wenu watano watafukuza adui mia, watu wenu mia watafukuza adui 10,000, nao adui zenu wataanguka kwa upanga mbele yenu.

9 “ ‘Nitawaangalia kwa upendeleo na kuwafanya mzae na kuzidisha idadi yenu, nami nitalishika Agano langu na ninyi.

10 Wakati wa kuvuna mtakuwa bado mnakula mavuno yaliyohifadhiwa muda mrefu, ndipo itawalazimu kuyaondoa ghalani ili mpate nafasi ya mavuno mapya.

11 Nitafanya makao yangu miongoni mwenu, nami sitawachukia.

12 Nitatembea katikati yenu niwe Mungu wenu, nanyi mtakuwa watu wangu.

13 Mimi ndimiBwanaMungu wenu, niliyewatoa katika nchi ya Misri ili msiendelee kuwa watumwa wa Wamisri, nikavunja kongwa lenu na kuwawezesha kutembea mkiwa mmeinua vichwa vyenu juu.

Adhabu Ya Kutokutii

14 “ ‘Lakini kama hamtanisikiliza na kutimiza maagizo haya yote,

15 nanyi kama mtazikataa amri zangu na kuzichukia sheria zangu, tena mkishindwa kutimiza amri zangu na hivyo mkavunja Agano langu,

16 ndipo nitakapowafanyia hili: Nitawaletea juu yenu hofu ya ghafula, magonjwa ya kufisha na homa itakayopofusha macho yenu na kuwaondolea uhai wenu. Mtapanda mbegu bila ya mafanikio, kwa sababu adui zenu wataila.

17 Nitauelekeza uso wangu dhidi yenu ili kwamba mshindwe na adui zenu; wale wanaowachukia watawatawala, nanyi mtakimbia ingawa hakuna mtu anayewafukuza.

18 “ ‘Kama baada ya haya yote hamtanisikiliza, nitawaadhibu mara saba zaidi kwa ajili ya dhambi zenu.

19 Nitakivunja kiburi chenu cha ukaidi na kuifanya anga lililo juu yenu liwe kama chuma na ardhi yenu kama shaba.

20 Nguvu zenu zitatumika bila ya mafanikio, kwa sababu ardhi yenu haitawazalia mazao yake, wala miti ya nchi yenu haitazaa matunda yake.

21 “ ‘Kama mtaendelea kuwa na uadui nami na kukataa kunisikiliza, nitawazidishia mateso yenu mara saba zaidi, kama dhambi zenu zinavyostahili.

22 Nitawatuma wanyama mwitu dhidi yenu, nao watawaibieni watoto wenu, watawaangamiza ng’ombe wenu na kuifanya idadi yenu kuwa ndogo hivi kwamba barabara zenu zitakuwa hazina watu.

23 “ ‘Ikiwa pamoja na mambo haya hamtakubali maonyo yangu lakini mkaendelea kuweka uadui nami,

24 mimi mwenyewe nitaweka uadui nanyi na kuwatesa kwa ajili ya dhambi zenu mara saba zaidi.

25 Nitawaletea upanga juu yenu ili kuwapatiliza kwa kuvunja Agano langu. Mtakapokimbilia mijini mwenu, nitatuma tauni katikati yenu, nanyi mtatiwa mikononi mwa adui zenu.

26 Nitakatilia mbali upatikanaji wa mkate wenu, wanawake kumi wataoka mkate wenu katika tanuru moja, nao wataugawa mkate kidogo kwa kupima. Mtakula, lakini hamtashiba.

27 “ ‘Kama hata baada ya haya bado hamtanisikiliza lakini mkaendelea kuweka uadui nami,

28 ndipo katika hasira yangu nitaweka uadui nanyi, nami mwenyewe nitawaadhibu mara saba kwa ajili ya dhambi zenu.

29 Mtakula nyama ya wana wenu na nyama ya binti zenu.

30 Nitapaharibu mahali penu pa juu pa kuabudia miungu, nitabomoa madhabahu zenu za kufukizia uvumba na kuzilundika maiti zenu juu ya sanamu zenu zisizo na uhai, nami nitawachukia ninyi sana.

31 Nitaifanya miji yenu kuwa magofu na kuharibu mahali patakatifu penu pa kuabudia, nami sitapendezwa na harufu nzuri ya sadaka zenu.

32 Nitaiharibu nchi, ili kwamba adui zenu watakaokuja kuishi humo washangae.

33 Nitawatawanya ninyi miongoni mwa mataifa na kuufuta upanga wangu na kuwafuatia. Nchi yenu itaharibiwa, nayo miji yenu itakuwa magofu.

34 Ndipo nchi itafurahia Sabato zake muda wote ule itakapokuwa ukiwa, nanyi mkiwa katika nchi ya adui zenu, ndipo nchi itapumzika na kufurahia Sabato zake.

35 Wakati wote nchi itakapobaki ukiwa, itapumzika na kufurahia Sabato zake ambazo haikuzipata mlipokuwa mnaishi humo.

36 “ ‘Kwa habari ya wenzenu wale watakaobaki, nitaifanya mioyo yao kuwa na hofu kuu katika nchi za adui zao kiasi kwamba sauti ya jani linalopeperushwa na upepo itawafanya wakimbie. Watakimbia kana kwamba wanakimbia upanga, nao wataanguka, ingawa hakuna anayewafukuza.

37 Watajikwaa mmoja juu ya mwingine kama wakimbiao upanga, hata ingawa hakuna anayewafuatia. Hivyo hamtaweza kusimama mbele ya adui zenu.

38 Mtaangamia katikati ya mataifa; nchi ya adui zenu itawala.

39 Wengine wenu watakaobaki wataangamia katika nchi za adui zao kwa sababu ya dhambi zao; pia kwa sababu ya dhambi za baba zao wataangamia.

40 “ ‘Lakini kama watatubu dhambi zao na dhambi za baba zao, udanganyifu wao dhidi yangu na uadui wao kwangu,

41 ambao ulinifanya niwe na uadui nao hata nikawapeleka katika nchi ya adui zao, kisha mioyo yao isiyotahiriwa ikanyenyekea na kutubu dhambi yao,

42 nitakumbuka Agano langu na Yakobo, na Agano langu na Isaki, na Agano langu na Abrahamu, nami nitaikumbuka nchi.

43 Kwa kuwa wataiacha nchi ukiwa, nayo itafurahia Sabato zake wakati ikiwa ukiwa pasipo wao kuwepo. Watalipizwa kwa ajili ya dhambi zao, kwa sababu walizikataa sheria zangu na kuzichukia amri zangu.

44 Lakini pamoja na hili, wakati wakiwa katika nchi ya adui zao, sitawakataa wala kuwachukia kiasi cha kuwaharibu kabisa na kuvunja Agano langu nao. Mimi ndimiBwanaMungu wao.

45 Lakini kwa ajili yao nitalikumbuka Agano langu na baba zao ambao niliwatoa Misri mbele ya mataifa ili niwe Mungu wao. Mimi ndimiBwana.’ ”

46 Hizi ndizo amri, sheria na pia masharti ambazoBwanaalifanya kati yake mwenyewe na Waisraeli katika Mlima Sinai kwa kupitia Mose.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/LEV/26-3e5216a88d61c051bc518e8e9ace7c59.mp3?version_id=1627—

Mambo ya Walawi 27

Kukomboa Kile Kilicho Cha Bwana

1 Bwanaakamwambia Mose,

2 “Sema na Waisraeli na uwaambie: ‘Kama mtu ye yote ataweka nadhiri maalum ili kuweka watu wakfu kwaBwana, kwa kutoa kiasi cha thamani inayolingana,

3 thamani ya mwanaume mwenye kati ya umri wa miaka ishirini na miaka sitini atakombolewa kwa shekeli hamsiniza fedha, kulingana na shekeli ya mahali patakatifu;

4 ikiwa ni mwanamke, weka thamani yake kwa shekeli thelathini.

5 Kama ni mwenye umri wa miaka kati ya mitano na ishirini, weka thamani ya mwanaume kuwa shekeli ishirini, na mwanamke shekeli kumi.

6 Kama ni mtu mwenye umri kati ya mwezi mmoja na miaka mitano, weka thamani ya mwanaume kuwa shekeli tano za fedha, na ile ya mwanamke kuwa shekeli tatuza fedha.

7 Kama ni mtu mwenye miaka sitini na zaidi, weka thamani ya mwanaume kuwa shekeli kumi na tanona mwanamke shekeli kumi.

8 Kama mtu ye yote anayeweka nadhiri ni maskini mno kulipa kiasi kilichowekwa, atampeleka huyo mtu kwa kuhani, ambaye ataweka thamani yake kulingana na kile mweka nadhiri anachoweza kulipa.

9 “ ‘Kama kile mtu alichokiwekea nadhiri ni mnyama anayekubalika kama sadaka kwaBwana, mnyama wa namna hiyo aliyetolewa kwaBwanaanakuwa mtakatifu.

10 Mtu haruhusiwi kumbadilisha au kutoa mnyama mzuri kwa mbaya, au mnyama mbaya kwa mzuri; kama atatoa mnyama badala ya mwingine, wanyama wote wawili, yaani yule aliyetolewa na yule aliyebadiliwa, huwa watakatifu.

11 Kama alichokiwekea nadhiri ni mnyama aliye najisi kiibada, yaani yule asiye kubalika kuwa sadaka kwaBwana, huyo mnyama lazima aletwe kwa kuhani,

12 ambaye ataamua ubora wa mnyama huyo kama ni mzuri au mbaya. Thamani yo yote atakayoweka kuhani, hivyo ndivyo itakavyokuwa.

13 Kama mwenye mnyama atapenda kumkomboa mnyama huyo, lazima aongeze sehemu ya tano ya thamani yake.

14 “ ‘Kama mtu ataweka nyumba yake wakfu kama kitu kitakatifu kwaBwana, kuhani ataamua ubora wa nyumba hiyo kama ni nzuri au mbaya. Thamani yo yote kuhani atakayoweka, basi hivyo ndivyo itakavyokuwa.

15 Kama mtu aliyeweka nyumba yake wakfu ataikomboa, lazima aongeze sehemu ya tano ya thamani yake, nayo nyumba itakuwa tena yake.

16 “ ‘Kama mtu anaweka sehemu ya ardhi ya jamaa yake wakfu kwaBwana, thamani yake itawekwa kulingana na kiasi cha mbegu inayohitajiwa kupandwa katika ardhi hiyo, yaani homerimoja ya mbegu za shayiri kwa shekeli hamsini za fedha.

17 Kama akiweka shamba lake wakfu katika Mwaka wa Yubile, ile thamani iliyokwisha wekwa itakuwa iyo hiyo.

18 Lakini kama akiweka shamba lake wakfu baada ya Yubile, kuhani ataweka thamani kulingana na idadi ya miaka iliyobaki kufikia Mwaka unaofuata wa Yubile, na thamani yake iliyoamuliwa itapunguzwa.

19 Kama mtu anayeweka wakfu shamba anataka kulikomboa, lazima aongeze sehemu ya tano ya thamani yake, nalo shamba litakuwa lake tena.

20 Kama pengine halikomboi shamba, au kama ameliuza kwa mtu mwingine, kamwe haliwezi kukombolewa.

21 Shamba litakapoachiwa mwaka wa Yubile, litakuwa takatifu, kama shamba lililotolewa kwaBwana, nalo litakuwa mali ya makuhani.

22 “ ‘Kama mtu ameweka wakfu kwaBwanashamba alilonunua, ambalo si sehemu ya ardhi ya jamaa yake,

23 kuhani ataamua thamani yake hadi Mwaka wa Yubile, naye huyo mtu atalazimika kulipa thamani yake siku hiyo kama kitu kitakatifu kwaBwana.

24 Katika Mwaka wa Yubile, shamba litarudishwa kwa mtu yule ambaye lilinunuliwa kutoka kwake, yule ambaye ardhi ilikuwa mali yake.

25 Kila thamani lazima iwekwe kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, geraishirini kwa shekeli.

26 “ ‘Kwa vyo vyote, hakuna mtu atakayeweka wakfu mzaliwa wa kwanza wa mnyama, kwa kuwa mzaliwa wa kwanza tayari ni mali yaBwana; awe maksai au kondoo, ni waBwana.

27 Kama ni mmoja wa wanyama walio najisi, aweza kumnunua kwa bei iliyowekwa, akiongeza sehemu ya tano ya thamani yake. Kama hatamkomboa, mnyama huyo atauzwa kwa bei iliyowekwa.

28 “ ‘Lakini cho chote kile mtu alichonacho na kukitoa kwaBwana, ikiwa ni binadamu, au mnyama, au ardhi ya jamaa, chaweza kuuzwa au kukombolewa; cho chote kilichotolewa ni kitakatifu sana kwaBwana.

29 “ ‘Mtu ye yote aliyetolewa ili kuangamizwa, hawezi kukombolewa. Mtu kama huyo lazima auawe.

30 “ ‘Zaka ya kila kitu kutoka shambani, ikiwa ni nafaka kutoka kwenye ardhi, au tunda kwenye miti, ni mali yaBwana; ni takatifu kwaBwana.

31 Kama mtu akikomboa cho chote cha zaka yake, lazima aongeze sehemu ya tano ya thamani yake.

32 Zaka yote ya kundi la ng’ombe au la kondoo na mbuzi, kila mnyama wa kumi apitaye chini ya fimbo ya yule awachungaye, atakuwa mtakatifu kwaBwana.

33 Yule mnyama wa kumi hatachaguliwa kwa kigezo cha uzuri au ubaya, naye haruhusiwi kubadiliwa. Ikiwa atabadiliwa, basi mnyama yule wa kwanza na huyo aliyebadiliwa wote watahesabiwa kuwa watakatifu, na haiwezekani kuwakomboa.’ ”

34 Haya ndiyo maagizoBwanaaliyompa Mose juu ya Mlima Sinai kwa ajili ya Waisraeli.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/LEV/27-2fcd77b31e64f84b296a0b3543b0ef72.mp3?version_id=1627—

Kutoka 1

Waisraeli Waonewa

1 Haya ndiyo majina ya wana wa Israeli ambao walikwenda Misri na Yakobo, kila mmoja akiwa pamoja na jamaa yake:

2 Reubeni, Simeoni, Lawi na Yuda;

3 Isakari, Zabuloni na Benyamini;

4 Dani na Naftali; Gadi na Asheri.

5 Wazao wote wa Yakobo walikuwa watu sabini; Yosefu alikuwa tayari yuko Misri.

6 Basi Yosefu na kaka zake wote na kizazi kile chote walikufa,

7 lakini Waisraeli walikuwa wamezaana na kuongezeka sana, idadi yao ikawa kubwa mno, kwa hiyo wakaijaza nchi.

8 Kisha mfalme mpya, ambaye hakufahamu habari za Yosefu, aliitawala Misri.

9 Akawaambia watu wake, “Tazameni, Waisraeli wamekuwa wengi mno kwa idadi kuliko sisi.

10 Njoni, ni lazima tuwashughulikie kwa uangalifu, la sivyo watazidi kuwa wengi zaidi, na ikiwa patatokea vita, watajiunga na adui zetu kupigana dhidi yetu na kuondoka katika nchi hii.”

11 Basi Wamisri wakaweka wasimamizi wa kuwasimamia na kuwatesa Waisraeli kwa kazi ngumu, nao wakajenga miji ya Pithomu na Ramesesi ya kuweka akiba ya Farao.

12 Lakini walivyozidi kuteswa ndivyo walivyozidi kuongezeka na kuenea katika nchi; Wamisri wakawaogopa Waisraeli,

13 kwa hiyo wakawatumikisha kwa ukatili.

14 Wakafanya maisha ya Waisraeli kuwa machungu kwa kufanya kazi ngumu ya kutengeneza lami na kufyatua matofali, na kazi zote za mashambani; katika kazi zao zote ngumu, Wamisri waliwatumia Waisraeli kwa ukatili.

15 Mfalme wa Misri akawaambia wakunga wa Kimisri waliowazalisha wanawake wa Kiebrania, ambao majina yao ni Shifra na Pua,

16 “Mtakapowazalisha wanawake wa Kiebrania wanapojifungua, chunguzeni; ikiwa ni mtoto wa kiume, mwueni; lakini ikiwa ni msichana, mwacheni aishi.”

17 Lakini hao wakunga walimcha Mungu na hawakufanya kile mfalme wa Misri alichowaambia kufanya, bali wakawaacha watoto wa kiume waishi.

18 Ndipo mfalme wa Misri akawaita hao wakunga, akawauliza, “Kwa nini mmefanya hivi? Mbona mmeacha watoto wa kiume waishi?”

19 Wakunga wakamjibu Farao, “Wanawake wa Kiebrania ni tofauti na wanawake wa Kimisri; wao wana nguvu, nao hujifungua watoto kabla wakunga hawajafika.”

20 Kwa hiyo Mungu akawatendea mema wakunga hao. Waisraeli wakaongezeka na kuendelea kuwa wengi zaidi.

21 Kwa vile hao wakunga walimcha Mungu, Mungu akawajalia kuwa na jamaa zao wenyewe.

22 Kisha Farao akatoa agizo hili kwa watu wake wote: “Kila mtoto wa kiume atakayezaliwa kwa Waebrania lazima atupwe katika Mto Nile, bali kila mtoto wa kike aachwe aishi.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EXO/1-47bcea5e8836c872fafc0b455f09e8fd.mp3?version_id=1627—