Kutoka 2

Kuzaliwa Kwa Mose

1 Basi mtu mmoja wa nyumba ya Lawi akaoa mwanamke Mlawi,

2 naye mwanamke huyo akapata mimba, akazaa mtoto wa kiume. Alipoona mtoto huyo ni mzuri, akamficha kwa miezi mitatu.

3 Lakini alipoona hawezi kumficha zaidi, akamtengenezea kisafina cha matete, akakipaka lami. Kisha akamweka huyo mtoto ndani yake, akakificha katikati ya matete kando ya ukingo wa Mto Nile.

4 Dada wa huyo mtoto akasimama mbali ili kuona kitakachompata mtoto.

5 Ndipo binti Farao akatelemka mtoni Nile kuoga, nao wahudumu wake wakawa wanatembea ukingoni mwa mto. Binti mfalme akaona kisafina katikati ya manyasi, akamtuma mmoja wa mtumwa wake wa kike kukichukua.

6 Alifungua kisafina akaona mtoto ndani yake. Mtoto alikuwa akilia, akamhurumia. Akasema, “Huyu ni mmoja wa watoto wa Kiebrania.”

7 Ndipo dada wa huyo mtoto akamwuliza binti Farao, “Je, niende nikakutafutie mmoja wa wanawake wa Kiebrania akulelee huyu mtoto?”

8 Binti Farao akamjibu, “Ndiyo, nenda.” Yule msichana akaenda akamleta mama wa mtoto.

9 Binti Farao akamwambia, “Mchukue huyu mtoto unisaidie kumlea, nami nitakulipa.” Basi yule mwanamke akamchukua mtoto na kumlea.

10 Mtoto alipokua, akampeleka kwa binti Farao, naye akawa mwanawe. Akamwita jina lake Mose, akisema, “Nilimtoa kwenye maji.”

Mose Akimbilia Midiani

11 Siku moja, baada ya Mose kukua, akaondoka kwenda walikokuwa watu wake, na akachunguza jinsi walivyokuwa wakifanya kazi ngumu. Akamwona Mmisri akimpiga Mwebrania, mmojawapo wa watu wake.

12 Mose akatazama huku na huko asione mtu ye yote, akamwua yule Mmisri, akamficha mchangani.

13 Kesho yake akatoka, akaona Waebrania wawili wakipigana. Akamwuliza yule aliyekosa, “Mbona unampiga Mwebrania mwenzako?”

14 Yule mtu akamjibu, “Ni nani aliyekuweka wewe kuwa mtawala na mwamuzi juu yetu? Je, unataka kuniua kama ulivyomwua yule Mmisri?” Ndipo Mose akaogopa na kuwaza, “Jambo lile nililofanya lazima limefahamika.”

15 Farao aliposikia jambo hili, alijaribu kumwua Mose, lakini Mose akamkimbia Farao na kwenda kuishi katika nchi ya Midiani, akaketi kando ya kisima.

16 Kuhani wa Midiani alikuwa na binti saba, nao wakaja kisimani ili kuchota maji na kujaza hori kwa ajili ya kunyweshea mifugo ya baba yao.

17 Baadhi ya wachungaji wakaja wakawafukuza hao wasichana. Ndipo Mose akainuka, akawasaidia na kunywesha mifugo yao.

18 Hao wasichana waliporudi nyumbani kwa Reueli baba yao, akawauliza, “Imekuwaje leo mmerudi mapema hivyo?”

19 Wakamjibu, “Mmisri mmoja alituokoa kutoka mikononi mwa wachungaji. Pia mtu huyo alituchotea maji na kunywesha mifugo.”

20 Akawauliza binti zake, “Yuko wapi? Mbona mmemwacha? Mkaribisheni ale chakula.”

21 Mose akakubali kukaa kwa huyo mtu, ambaye alimpa Mose binti yake aliyeitwa Sipora amwoe.

22 Sipora alizaa mtoto wa kiume, naye Mose akamwita Gershoni, akisema, “Nimekuwa mgeni katika nchi ya kigeni.”

23 Baada ya muda mrefu, mfalme wa Misri akafa. Waisraeli wakalia kwa huzuni katika utumwa wao, walilia na kilio chao cha kutaka msaada kwa ajili ya utumwa kikamfikia Mungu.

24 Mungu akasikia kilio chao cha huzuni, akakumbuka Agano alilofanya na Abrahamu pamoja na Isaki na Yakobo.

25 Kwa hiyo Mungu akawaangalia Waisraeli na kuwahurumia.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EXO/2-a1b5f045bd1707b13e160ef279683ac6.mp3?version_id=1627—

Kutoka 3

Mose Na Kichaka Kinachowaka Moto

1 Basi Mose alikuwa anachunga mifugo ya Yethro mkwewe, kuhani wa Midiani. Mose akapeleka mifugo mbali nyuma ya jangwa, naye akafika Horebu, mlima wa Mungu.

2 Huko malaika waBwanaakamtokea Mose katika mwali wa moto kutoka katika kichaka. Mose akaona hilo, ingawa kile kichaka kilikuwa kinawaka moto, kilikuwa hakiteketei.

3 Ndipo Mose akawaza, “Nitageuka sasa nione kitu hiki cha ajabu, nami nione ni kwa nini kichaka hiki hakiteketei.”

4 Bwanaalipoona kuwa amegeuka ili aone, Mungu akamwita kutoka ndani ya kile kichaka, “Mose! Mose!”

Naye Mose akajibu, “Mimi hapa.”

5 Mungu akamwambia, “Usikaribie zaidi. Vua viatu vyako, kwa maana mahali unaposimama ni ardhi takatifu.”

6 Kisha akamwambia, “Mimi ni Mungu wa baba yako, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaki, na Mungu wa Yakobo.” Mose aliposikia hayo, akafunika uso wake kwa sababu aliogopa kumtazama Mungu.

7 Bwanaakamwambia, “Hakika nimeona mateso ya watu wangu katika Misri. Nimesikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao, nami naguswa na mateso yao.

8 Basi nimeshuka niwaokoe kutoka mkono wa Wamisri, niwatoe na kuwapandisha kutoka katika nchi hiyo, niwapeleke katika nchi nzuri na kubwa, nchi itiririkayo maziwa na asali, nchi ya Wakanaani, Wahiti, Waamori, Waperizi, Wahivi na Wayebusi.

9 Sasa kilio cha Waisraeli kimenifikia, nami nimeona jinsi Wamisri wanavyowatesa.

10 Basi, sasa nenda. Ninakutuma kwa Farao ili kuwatoa watu wangu Waisraeli kutoka Misri.”

11 Lakini Mose akamwambia Mungu, “Mimi ni nani hata niende kwa Farao kuwatoa Waisraeli nchini Misri?”

12 Naye Mungu akasema, “Mimi nitakuwa pamoja nawe. Hii itakuwa ishara kwako kwamba ni Mimi nimekutuma: Hapo utakapokuwa umewatoa watu Misri, mtamwabudu Mungu katika mlima huu.”

13 Mose akamwambia Mungu, “Ikiwa nitawaendea Waisraeli na kuwaambia, ‘Mungu wa baba zenu amenituma kwenu,’ nao wakiniuliza, ‘Jina lake ni nani?’ Nitawaambia nini?”

14 Mungu akamwambia Mose, “MIMI NIKO AMBAYE NIKO. Hivyo ndivyo utakavyowaambia Waisraeli: ‘MIMI NIKO amenituma kwenu.’ ”

15 Vile vile Mungu akamwambia Mose, “Waambie Waisraeli, ‘Bwana, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaki, na Mungu wa Yakobo amenituma kwenu.’ Hili ndilo Jina langu milele, Jina ambalo mtanikumbuka kwalo kutoka kizazi hadi kizazi.

16 “Nenda, ukawakusanye wazee wa Israeli, uwaambie, ‘Bwana, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Abrahamu, Isaki na Yakobo, alinitokea akaniambia: Nimewatazama, nami nimeona mliyofanyiwa katika Misri.

17 Nami nimeahidi kuwapandisha kutoka katika mateso yenu katika nchi ya Misri, niwapeleke nchi ya Wakanaani, Wahiti, Waamori, Waperizi, Wahivi na Wayebusi, nchi itiririkayo maziwa na asali.’

18 “Wazee wa Israeli watakusikiliza. Kisha wewe na wazee mtakwenda kwa mfalme wa Misri na kumwambia, ‘Bwana, Mungu wa Waebrania ametutokea. Turuhusu tuende safari ya siku tatu huko jangwani kutoa dhabihu kwaBwanaMungu wetu.’

19 Lakini nafahamu kwamba mfalme wa Misri hatawaruhusu kwenda, mpaka mkono wenye nguvu umlazimishe.

20 Kwa hiyo nitaunyosha mkono wangu na kuwapiga Wamisri kwa maajabu yote nitakayofanya miongoni mwao. Baada ya hayo, atawaruhusu mwondoke.

21 “Nami nitawapa hawa watu upendeleo mbele ya Wamisri, kwa hiyo mtakapoondoka nchini hamtaondoka mikono mitupu.

22 Kila mwanamke Mwisraeli atamwomba jirani yake Mmisri na mwanamke ye yote anayeishi nyumbani kwake ampe vyombo vya fedha, dhahabu na nguo, ambavyo mtawavika wana wenu na binti zenu. Hivyo mtawateka nyara Wamisri.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EXO/3-75afe32655ae4038c3055f705d8e66f2.mp3?version_id=1627—

Kutoka 4

Ishara Za Mose

1 Mose akamjibu, “Itakuwaje kama hawataniamini au kunisikiliza, waseme, ‘Bwanahakukutokea’?”

2 NdipoBwanaakamwambia, “Ni nini hicho kilicho mkononi mwako?”

Akajibu, “Fimbo.”

3 Bwanaakasema, “Itupe chini.”

Mose akaitupa chini hiyo fimbo nayo ikawa nyoka, naye akaikimbia.

4 KishaBwanaakamwambia, “Nyosha mkono wako uikamate mkiani.” Basi Mose akanyosha mkono akamkamata yule nyoka, nayo ikabadilika tena kuwa fimbo mkononi mwake.

5 Bwanaakasema, “Hivi ndivyo Waisraeli watakavyoamini kuwaBwana, Mungu wa baba zao, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaki, na Mungu wa Yakobo, amekutokea wewe.”

6 KishaBwanaakamwambia, “Weka mkono wako ndani ya joho lako.” Basi Mose akaweka mkono wake ndani ya joho lake, naye alipoutoa, ulikuwa na ukoma, mweupe kama theluji.

7 Mungu akamwambia, “Sasa urudishe tena huo mkono ndani ya joho lako.” Basi Mose akaurudisha mkono wake ndani ya joho lake na alipoutoa, ulikuwa mzima, kama sehemu zingine za mwili wake.

8 NdipoBwanaakamwambia, “Kama hawatakuamini wewe, au kutojali ishara ya kwanza, wataamini ishara ya pili.

9 Lakini kama hawataamini ishara hizi mbili au hawatawasikiliza ninyi, chukua kiasi cha maji kutoka Mto Nile uyamimine juu ya ardhi kavu. Maji mtakayotoa mtoni yatakuwa damu juu ya ardhi.”

10 Mose akamwambiaBwana, “Ee Bwana, kamwe sijapata kuwa msemaji kwa ufasaha wakati uliopita wala tangu ulipoanza kuzungumza na mtumishi wako. Ulimi wangu ni mzito kuzungumza.”

11 Bwanaakamwambia, “Ni nani aliyempa mwanadamu kinywa? Ni nani aliyemfanya mtu kuwa kiziwi au bubu? Ni nani anayempa mtu kuona au upofu? Je, si mimi,Bwana?

12 Sasa nenda, nitakusaidia kusema, nami nitakufundisha jambo la kusema.”

13 Lakini Mose akasema, “Ee Bwana, tafadhali mtume mtu mwingine kufanya kazi hiyo.”

14 Ndipo hasira yaBwanaikawaka dhidi ya Mose, akamwambia, “Vipi kuhusu ndugu yako, Aroni Mlawi? Ninajua yeye anaweza kuzungumza vizuri. Naye yuko tayari njiani kukulaki, na moyo wake utafurahi wakati atakapokuona.

15 Utazungumza naye na kuweka maneno kinywani mwake. Nitawasaidia ninyi wawili kusema, nami nitawafundisha jambo la kufanya.

16 Aroni ataongea na watu badala yako na itakuwa kwamba yeye amekuwa kinywa chako nawe utakuwa kama Mungu kwake.

17 Lakini chukua fimbo hii mkononi mwako ili uweze kuitumia kufanya ishara hizo za ajabu.”

Mose Anarudi Misri

18 Kisha Mose akarudi kwa Yethro mkwewe akamwambia, “Niruhusu nirudi kwa watu wangu Misri kuona kama yuko hata mmoja wao ambaye bado anaishi.”

Yethro akamwambia, “Nenda, nami nakutakia mema.”

19 BasiBwanaalikuwa amemwambia Mose huko Midiani, “Rudi Misri kwa maana watu wote waliotaka kukuua wamekufa.”

20 Basi Mose akamchukua mkewe na wanawe, akawapandisha juu ya punda na kuanza safari kurudi Misri. Naye akaichukua ile fimbo ya Mungu mkononi mwake.

21 Bwanaakamwambia Mose, “Utakaporudi Misri, hakikisha kwamba utafanya mbele ya Farao maajabu yote niliyokupa uwezo wa kuyafanya. Lakini nitafanya moyo wake kuwa mgumu ili kwamba asiwaruhusu watu waende.

22 Kisha mwambie Farao, ‘Hili ndilo asemaloBwana: Israeli ni mwanangu mzaliwa wa kwanza,

23 nami nilikuambia, “Ruhusu mwanangu aondoke, ili aweze kuniabudu mimi.” Lakini ukakataa kumruhusu kwenda, basi nitaua mwana wako mzaliwa wa kwanza.’ ”

24 Mose alipokuwa mahali pa kulala wageni akiwa njiani kurudi Misri,Bwanaakakutana naye, akataka kumwua.

25 Lakini Sipora akachukua jiwe gumu, akakata govi la mwanawe na kugusa nalo miguu ya Mose. Sipora akasema, “Hakika wewe ni bwana arusi wa damu kwangu.”

26 Sipora alipomwita Mose, “Bwana arusi wa damu,” alikuwa anamaanisha ile tohara. Baada ya hayoBwanaakamwacha.

27 Bwanaakamwambia Aroni, “Nenda jangwani ukamlaki Mose.” Basi akakutana na Mose kwenye mlima wa Mungu, akambusu.

28 Kisha Mose akamwambia Aroni kila kituBwanaalichomtuma kusema, vile vile habari za ishara na maajabu alizokuwa amemwamuru kufanya.

29 Mose na Aroni wakawakusanya wazee wote wa Waisraeli,

30 naye Aroni akawaambia kila kituBwanaalichokuwa amemwambia Mose. Pia akafanya ishara mbele ya watu,

31 nao wakaamini. Nao waliposikia kuwaBwanaanajishughulisha nao na kwamba ameona mateso yao, walisujudu na kuabudu.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EXO/4-9c9aad99928c8d70ca28de3effe7430c.mp3?version_id=1627—

Kutoka 5

Matofali Bila Nyasi

1 Baadaye Mose na Aroni wakaenda kwa Farao, wakamwambia, “Hili ndilo asemaloBwana, Mungu wa Israeli: ‘Waruhusu watu wangu waende, ili waweze kunifanyia sikukuu huko jangwani.’ ”

2 Farao akasema, “HuyoBwanani nani, hata nimtii na kuruhusu Israeli uende? Simjui huyoBwanawala sitawaruhusu Israeli waende.”

3 Ndipo Mose na Aroni wakasema, “Mungu wa Waebrania amekutana nasi. Sasa turuhusu tuwe na safari ya siku tatu ya jangwani ili tukamtoleeBwanaMungu wetu dhabihu, la sivyo aweza kutupiga sisi kwa tauni au kwa upanga.”

4 Lakini mfalme wa Misri akasema, “Mbona ninyi Mose na Aroni mnawachukua watu waache kazi zao? Rudini kwenye kazi zenu!”

5 Kisha Farao akasema, “Tazama, sasa watu hawa ni wengi, nanyi mnawazuia kufanya kazi.”

6 Siku iyo hiyo Farao akatoa amri hii kwa viongozi wa watumwa na wasimamizi wa watu akawaambia:

7 “Tangu sasa msiwape hawa watu nyasi za kutengenezea matofali. Wao wakusanye nyasi zao wenyewe.

8 Lakini watakeni kutengeneza matofali kiasi kile kile cha mwanzo, kiwango kisipunguzwe. Wao ni wavivu, ndiyo sababu wanalia, wakisema, ‘Turuhusiwe twende kumtolea Mungu wetu dhabihu.’

9 Fanyeni kazi kuwa ngumu zaidi kwa watu hao ili kwamba wakazane na kazi na kuacha kusikiliza uongo.”

10 Basi viongozi wa watumwa na wasimamizi wakaenda kuwaambia watu, “Hivi ndivyo Farao asemavyo: ‘Sitawapa tena nyasi.

11 Nendeni mkatafute nyasi wenyewe po pote mnapoweza kuzipata, lakini kazi yenu haitapunguzwa hata kidogo.’ ”

12 Basi watu wakatawanyika kote nchini Misri kukusanya mabua ya kutumia badala ya nyasi.

13 Viongozi wa watumwa wakasisitiza, wakisema, “Timizeni kazi mnayotakiwa kwa kila siku, kama wakati ule mlipokuwa mkipewa nyasi.”

14 Wasimamizi wa Kiisraeli waliochaguliwa na viongozi wa watumwa wa Farao walipigwa na kuulizwa, “Kwa nini hamkutimiza kiwango chenu cha kutengeneza matofali jana na leo, kama mwanzoni?”

15 Ndipo wasimamizi wa Kiisraeli wakaenda kumlilia Farao, wakisema: “Mbona umewatendea watumishi wako hivi?

16 Watumishi wako hawapewi nyasi, hata hivyo tumeambiwa, ‘Tengenezeni matofali!’ Watumishi wako wanapigwa, lakini kosa ni la watu wako wenyewe.”

17 Farao akasema, “Ninyi ni wavivu ndiyo sababu mnasema, ‘Turuhusu twende tukamtoleeBwanadhabihu.’

18 Sasa nendeni kazini. Hamtapewa nyasi zo zote, nanyi ni lazima mtengeneze matofali.”

19 Wasimamizi wa Kiisraeli walitambua kuwa wako taabuni walipoambiwa, “Hamtakiwi kupunguza idadi ya matofali mliotakiwa kutengeneza kila siku.”

20 Walipoondoka kwa Farao, wakawakuta Mose na Aroni wakingojea kukutana nao,

21 wakawaambia Mose na Aroni, “Bwanana awaangalie awahukumu ninyi! Mmetufanya tunuke kwa Farao na maafisa wake, nanyi mmeweka upanga mikononi mwao ili kutuua sisi.”

Mungu Anaahidi Ukombozi

22 Mose akarudi kwaBwanana kumwambia, “Ee Bwana, mbona umewaletea watu hawa taabu? Kwa nini basi ukanituma mimi?

23 Tangu nilipomwendea Farao kuzungumza naye kwa jina lako, amewapatisha taabu watu hawa, nawe kamwe hujawakomboa watu wako.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EXO/5-b44f7ad909c8d3ed672171230554e2c6.mp3?version_id=1627—

Kutoka 6

1 KishaBwanaakamwambia Mose, “Sasa utaona kitu nitakachomfanyia Farao: Kwa sababu ya mkono wangu wenye nguvu atawaachia watu waende; kwa sababu ya mkono wangu wenye nguvu atawafukuza waondoke nchini mwake.”

2 Pia Mungu akamwambia Mose, “Mimi ndimiBwana.

3 Nilimtokea Abrahamu, Isaki na Yakobo kama Mungu Mwenyezi, ingawa sikuwajulisha Jina langu, Yehova, Mimi mwenyewe sikujitambulisha kwao.

4 Pia niliweka Agano langu nao kuwapa nchi ya Kanaani, ambako waliishi kama wageni.

5 Zaidi ya hayo, nimesikia kilio cha huzuni cha Waisraeli ambao Wamisri wamewatia utumwani, nami nimelikumbuka Agano langu.

6 “Kwa hiyo, waambie Waisraeli: ‘Mimi ndimiBwana, nami nitawatoa mtoke katika kongwa la Wamisri. Nitawaweka huru mtoke katika kuwa watumwa wao, nami nitawakomboa kwa mkono ulionyooshwa pamoja na matendo makuu ya hukumu.

7 Nitawatwaa mwe watu wangu mwenyewe, nami nitakuwa Mungu wenu. Ndipo mtajua kuwa mimi ndimiBwanaMungu wenu, niliyewatoa chini ya kongwa la Wamisri.

8 Nami nitawaleta mpaka nchi niliyoapa kwa mkono ulioinuliwa kumpa Abrahamu, Isaki na Yakobo. Nitawapa iwe milki yenu. Mimi ndimiBwana.’ ”

9 Mose akawaarifu Waisraeli jambo hili, lakini hawakumsikiliza kwa sababu ya maumivu makuu ya moyoni na utumwa wa kikatili.

10 NdipoBwanaakamwambia Mose,

11 “Nenda, mwambie Farao mfalme wa Misri awaachie Waisraeli waondoke nchini mwake.”

12 Lakini Mose akamwambiaBwana, “Ikiwa Waisraeli hawatanisikiliza, kwa nini yeye Farao anisikilize mimi, ambaye huzungumza kwa kigugumizi?”

Orodha Ya Jamaa Ya Mose Na Aroni

13 NdipoBwanaakanena na Mose na Aroni kuhusu Waisraeli na Farao mfalme wa Misri, naye akawaamuru wawatoe Waisraeli kutoka Misri.

14 Hawa walikuwa wakuu wa jamaa zao:

Wana wa Reubeni mzaliwa wa kwanza wa kiume wa Israeli walikuwa Hanoki, Palu, Hesroni na Karmi. Hawa walikuwa ndio koo za Reubeni.

15 Wana wa Simeoni walikuwa Yemueli, Yamini, Ohadi, Yakini, Sohari na Shauli mwana wa mwanamke Mkanaani. Hawa walikuwa ndio koo za Simeoni.

16 Haya yalikuwa ndiyo majina ya wana wa Lawi kufuatana na orodha zao: Gershoni, Kohathi na Merari. Lawi aliishi miaka 137.

17 Wana wa Gershoni kwa koo, walikuwa Libni na Shimei.

18 Wana wa Kohathi walikuwa Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli. Kohathi aliishi miaka 133.

19 Wana wa Merari walikuwa Mahli na Mushi.

Hizi ndizo zilizokuwa koo za Lawi kufuatana na orodha zao.

20 Amramu akamwoa Yokobedi, shangazi yake, ambaye alimzalia Aroni na Mose. Amramu aliishi miaka 137.

21 Wana wa Ishari walikuwa Kora, Nefegi na Zikri.

22 Wana wa Uzieli walikuwa Mishaeli, Elisafani na Sithri.

23 Aroni akamwoa Elisheba binti wa Aminadabu ndugu yake Nashoni, naye akamzalia Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.

24 Wana wa Kora walikuwa Asiri, Elikana na Abiasafu. Hawa walikuwa ndio koo za Kora.

25 Eleazari mwana wa Aroni akamwoa mmoja wa binti za Putieli, naye akamzalia Finehasi.

Hawa walikuwa ndio wakuu wa jamaa za Walawi, ukoo kwa ukoo.

26 Hawa walikuwa Aroni na Mose wale wale ambaoBwanaaliwaambia, “Watoeni Waisraeli katika nchi ya Misri kwa vikosi vyao.”

27 Ndio hao hao waliozungumza na Farao mfalme wa Misri kuhusu kuwatoa Waisraeli Misri. Ilikuwa ni huyo Mose na huyo Aroni.

Aroni Kuzungumza Badala Ya Mose

28 Bwanaaliponena na Mose huko Misri,

29 akamwambia, “Mimi ndimiBwana. Mwambie Farao mfalme wa Misri kila kitu nikuambiacho.”

30 Lakini Mose akamwambiaBwana, “Kwa kuwa mimi huzungumza kwa kigugumizi, Farao atanisikiliza mimi?”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EXO/6-ed29fb24e95e530bc5efe363168d265a.mp3?version_id=1627—

Kutoka 7

1 KishaBwanaakamwambia Mose, “Tazama, nimekufanya kuwa kama Mungu kwa Farao, naye Aroni, huyo ndugu yako, atakuwa nabii wako.

2 Utasema kila kitu nitakachokuagiza, naye Aroni ndugu yako atamwambia Farao awaachie Waisraeli watoke katika nchi yake.

3 Lakini nitaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, hata ingawa nitazidisha ishara na maajabu katika Misri,

4 hatawasikiliza. Kisha nitaupeleka mkono wangu juu ya Misri, na kwa matendo makuu ya hukumu nitavitoa vikundi vyangu, watu wangu Waisraeli.

5 Nao Wamisri watajua kuwa Mimi ndimiBwananitakapounyosha mkono wangu dhidi ya Misri na kuwatoa Waisraeli watoke humo.”

6 Mose na Aroni wakafanya sawasawa kama vileBwanaalivyowaagiza.

7 Mose alikuwa na umri wa miaka themanini na Aroni alikuwa na umri wa miaka themanini na mitatu walipozungumza na Farao.

Fimbo Ya Aroni Yawa Nyoka

8 Bwanaakamwambia Mose na Aroni,

9 “Farao atakapowaambia, ‘Fanyeni mwujiza,’ basi mwambie Aroni, ‘Chukua fimbo yako na uitupe chini mbele ya Farao,’ nayo fimbo itakuwa nyoka.”

10 Ndipo Mose na Aroni wakaenda kwa Farao wakafanya sawasawa kama vileBwanaalivyoagiza. Aroni akaitupa ile fimbo yake chini mbele ya Farao na maafisa wake, nayo ikawa nyoka.

11 Farao naye akawaita watu wenye maarifa na wachawi na waganga wa Kimisri, nao wakafanya vivyo hivyo kwa siri ya uganga wao.

12 Kila mmoja alitupa fimbo yake chini, nayo ikawa nyoka. Lakini fimbo ya Aroni ikazimeza zile fimbo zao.

13 Hata hivyo moyo wa Farao ukawa mgumu, naye hakuwasikiliza Mose na Aroni, sawasawa kama vileBwanaalivyokuwa amesema.

Pigo La Kwanza: Damu

14 KishaBwanaakamwambia Mose, “Moyo wa Farao ni mgumu, anakataa kuwaachia watu kuondoka.

15 Nenda kwa Farao asubuhi wakati anapokwenda mtoni. Ungoje ukingoni mwa Nile ili kuonana naye, nawe uchukue mkononi mwako fimbo ile iliyobadilishwa kuwa nyoka.

16 Kisha umwambie, ‘Bwana, Mungu wa Waebrania, amenituma nikuambie: Uwaachie watu wangu waende, ili wapate kuniabudu jangwani. Lakini hadi sasa hujasikiliza.

17 Hili ndiloBwanaasemalo: Kwa hili utajua kuwa Mimi ndimiBwana: Fimbo iliyo mkononi mwangu nitapiga nayo maji ya Nile nayo yatabadilika kuwa damu.

18 Samaki waliomo katika Mto Nile watakufa, nao mto utanuka vibaya, Wamisri hawataweza kunywa hayo maji yake.’ ”

19 Bwanaakamwambia Mose, “Mwambie Aroni, ‘Chukua ile fimbo yako unyoshe mkono wako juu ya maji ya Misri, juu ya chemchemi na mifereji, juu ya madimbwi na mabwawa yote,’ navyo vitabadilika kuwa damu. Damu itakuwa kila mahali katika Misri, hata kwenye vyombo vya miti na vya mawe.”

20 Mose na Aroni wakafanya kama vileBwanaalivyokuwa amewaagiza. Akainua fimbo yake machoni pa Farao na maafisa wake na kuyapiga maji ya Mto Nile, na maji yote yakabadilika kuwa damu.

21 Samaki katika Mto Nile wakafa, nao mto ukanuka vibaya sana kiasi kwamba Wamisri hawakuweza kunywa maji yake. Damu ilikuwa kila mahali katika nchi ya Misri.

22 Lakini waganga wa Misri kwa kutumia siri ya uganga wao wakafanya vivyo hivyo, nao moyo wa Farao ukawa mgumu, hakuwasikiliza Mose na Aroni, kama vileBwanaalivyokuwa amesema.

23 Badala yake, akageuka akaenda kwenye jumba lake la kifalme, wala hakulitia hili moyoni.

24 Nao Wamisri wote wakachimba kandokando ya Mto Nile kupata maji ya kunywa, kwa sababu hawakuweza kunywa maji ya mto.

Pigo La Pili: Vyura

25 Zilipita siku saba baada yaBwanakuyapiga maji ya Mto Nile.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EXO/7-9fb9d369450f2de775bc9c295e7f62b9.mp3?version_id=1627—

Kutoka 8

1 NdipoBwanaakamwambia Mose, “Nenda kwa Farao ukamwambie, ‘Hili ndilo asemaloBwana: Waachie watu wangu waende, ili wapate kuniabudu.

2 Kama ukikataa kuwaruhusu kuondoka, basi nitaipiga nchi yako yote kwa kuwaletea vyura.

3 Mto Nile utafurika vyura. Watakuja kwenye jumba lako la kifalme na katika chumba chako cha kulala na kitandani mwako, katika nyumba za maafisa wako na kwa watu wako, vyura hao wataingia katika meko yenu na kwenye vyombo vya kukandia unga.

4 Vyura watapanda juu yako, juu ya watu wako na maafisa wako wote.’ ”

5 NdipoBwanaakamwambia Mose, “Mwambie Aroni, ‘Nyosha mkono wako ukiwa na ile fimbo yako juu ya vijito, mifereji na madimbwi, fanya vyura waje juu ya nchi ya Misri.’ ”

6 Ndipo Aroni akaunyosha mkono wake juu ya maji ya Misri, nao vyura wakatokea na kuifunika nchi.

7 Lakini waganga wakafanya vivyo hivyo kwa siri ya uganga wao, nao pia wakafanya vyura kuja juu ya nchi ya Misri.

8 Ndipo Farao akamwita Mose na Aroni na kusema, “MwombeniBwanaawaondoe vyura kutoka kwangu na kwa watu wangu, nami nitawaachia watu wenu waende kumtoleaBwanadhabihu.”

9 Mose akamwambia Farao, “Ninakupa heshima ya kuamua ni wakati gani wa kukuombea wewe, maafisa wako na watu wako ili kwamba vyura watoke kwenu na kwenye nyumba zenu. Isipokuwa wale walio katika Mto Nile.”

10 Farao akasema, “Kesho.”

Mose akamjibu, “Itakuwa kama unavyosema, ili upate kujua kwamba hakuna ye yote kamaBwanaMungu wetu.

11 Vyura wataondoka kwako na katika nyumba zako, kwa maafisa wako na kwa watu wako, ila watabakia katika Mto Nile tu.”

12 Baada ya Mose na Aroni kuondoka kwa Farao, Mose akamliliaBwanakuhusu vyura aliokuwa amewaleta kwa Farao.

13 NayeBwanaakafanya lile Mose alilomwomba. Vyura wafia ndani ya nyumba, viwanjani na mashambani.

14 Wakayakusanya malundo, nchi nzima ikanuka.

15 Lakini Farao alipoona pametokea nafuu, akaushupaza moyo wake na hakuwasikiliza Mose na Aroni, kama vileBwanaalivyokuwa amesema.

Pigo La Tatu: Viroboto

16 NdipoBwanaakamwambia Mose, “Mwambie Aroni, ‘Nyosha fimbo yako uyapige mavumbi ya ardhi,’ nayo nchi yote ya Misri mavumbi yatakuwa viroboto.”

17 Wakafanya hivyo, Aroni aliponyosha mkono wake wenye fimbo na kuyapiga mavumbi ya nchi, viroboto wakawajia watu na wanyama. Mavumbi yote katika nchi ya Misri yakawa viroboto.

18 Lakini waganga walipojaribu kutengeneza viroboto kwa siri ya uganga wao, hawakuweza. Nao viroboto walikuwa juu ya watu na wanyama.

19 Waganga wale wakamwambia Farao, “Hiki ni kidole cha Mungu.” Lakini moyo wa Farao ukawa mgumu naye hakuwasikiliza, kama vileBwanaalivyosema.

Pigo La Nne: Mainzi

20 KishaBwanaakamwambia Mose, “Amka mapema asubuhi na usimame mbele ya Farao wakati anapokwenda mtoni nawe umwambie, ‘Hili ndiloBwanaasemalo: Waachie watu wangu waende, ili wapate kuniabudu.

21 Kama hutawaachia watu wangu waondoke nitakupelekea makundi ya mainzi juu yako, kwa maafisa wako, kwa watu wako na kwenye nyumba zenu. Nyumba za Wamisri zitajazwa mainzi, hata na ardhi yote ya Misri.

22 “ ‘Lakini siku ile nitafanya kitu tofauti katika nchi ya Gosheni, ambapo watu wangu wanaishi, hapatakuwepo na makundi ya mainzi, ili mpate kujua kwamba Mimi,Bwana, niko katika nchi hii.

23 Nitaweka tofauti kati ya watu wangu na watu wenu. Ishara hii ya ajabu itatokea kesho.’ ”

24 NayeBwanaakafanya hivyo. Makundi makubwa ya mainzi yalimiminika katika jumba la kifalme la Farao na katika nyumba za maafisa wake, pia nchi yote ya Misri ikaharibiwa na mainzi.

25 Ndipo Farao akamwita Mose na Aroni na kuwaambia, “Nendeni mkamtolee Mungu wenu dhabihu katika nchi hii.”

26 Lakini Mose akamwambia, “Hilo halitakuwa sawa. Dhabihu tutakazomtoleaBwanaMungu wetu zitakuwa chukizo kwa Wamisri. Kama tukitoa dhabihu ambazo ni chukizo mbele yao, je, hawatatupiga mawe?

27 Ni lazima twende mwendo wa siku tatu mpaka tufike jangwani ili tumtoleeBwanaMungu wetu dhabihu, kama alivyotuagiza.”

28 Farao akamwambia, “Nitawaruhusu mwende kumtoleaBwanaMungu wenu dhabihu huko jangwani, lakini hamna ruhusa kwenda mbali sana. Sasa mniombee.”

29 Mose akajibu, “Mara tu nitakapoondoka, nitamwombaBwanana kesho mainzi yataondoka kwa Farao, kwa maafisa wake na kwa watu wake. Hakikisha tu kwamba Farao hatatenda kwa udanganyifu tena kwa kutokuwaachia watu waende kumtoleaBwanadhabihu.”

30 Ndipo Mose akamwacha Farao na kumwombaBwana,

31 nayeBwanaakafanya lile Mose alilomwomba. Mainzi yakaondoka kwa Farao, kwa maafisa wake na kwa watu wake, wala hakuna hata inzi aliyebakia.

32 Lakini wakati huu pia Farao akaushupaza moyo wake, wala hakuwaruhusu Waisraeli waondoke.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EXO/8-86110830b3f7cdf00a4f586f39abd3d4.mp3?version_id=1627—

Kutoka 9

Pigo La Tano: Vifo Vya Mifugo

1 NdipoBwanaakamwambia Mose, “Nenda kwa Farao ukamwambie, ‘Hili ndiloBwana, Mungu wa Waebrania asemalo: “Waachie watu wangu waende ili wapate kuniabudu.”

2 Kama ukikataa kuwaachia waende, nawe ukiendelea kuwashikilia,

3 mkono waBwanautaleta pigo baya kwa mifugo yako, juu ya farasi wako, punda, ngamia, ng’ombe wako, kondoo na mbuzi.

4 LakiniBwanaataweka tofauti kati ya mifugo ya Israeli na ile ya Misri, kwamba hakuna mnyama wa Mwisraeli atakayekufa.’ ”

5 Bwanaakaweka wakati na kusema, “KeshoBwanaatalitenda hili katika nchi.”

6 Siku iliyofuataBwanaakalitenda: Mifugo yote ya Wamisri ikafa, lakini hakuna hata mnyama mmoja wa wana wa Israeli iliyekufa.

7 Farao akatuma watu kuchunguza, nao wakakuta kuwa hakuna hata mnyama mmoja wa Waisraeli aliyekufa. Lakini moyo wa Farao haukukubali kuwaachia watu waende.

Pigo La Sita: Majipu

8 KishaBwanaakamwambia Mose na Aroni, “Chukueni majivu ya tanuru, naye Mose ayarushe angani mbele ya Farao.

9 Yatakuwa vumbi jepesi juu ya nchi yote ya Misri, pia yatatokea majipu yenye kufura juu ya watu na wanyama katika nchi yote.”

10 Basi wakachukua majivu kwenye tanuru na kusimama mbele ya Farao. Mose akayarusha hewani, nayo majipu yenye kufura yakatokea miilini mwa watu na wanyama.

11 Waganga hawakuweza kusimama mbele ya Mose kwa sababu ya majipu yale yaliyokuwa miilini mwao na juu ya miili ya Wamisri wote.

12 LakiniBwanaakaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, naye hakuwasikiliza Mose na Aroni, sawasawa kama vileBwanaalivyokuwa amemwambia Mose.

Pigo La Saba: Mvua Ya Mawe

13 KishaBwanaakamwambia Mose, “Amka mapema asubuhi, usimame mbele ya Farao, umwambie, ‘Hili ndilo asemaloBwana, Mungu wa Waebrania: Waachie watu wangu waende, ili kwamba waweze kuniabudu,

14 au wakati huu nitaleta mapigo yangu yenye nguvu dhidi yako, maafisa wako na watu wako, ili upate kujua kuwa hakuna mwingine kama Mimi katika dunia yote.

15 Kwa kuwa mpaka sasa ningelikuwa nimenyosha mkono wangu na kukupiga wewe na watu wako kwa pigo ambalo lingekufutilia mbali juu ya nchi.

16 Lakini nimekuacha wewe uwepo kwa kusudi hili hasa, ili nipate kukuonyesha uwezo wangu na ili Jina langu lipate kutangazwa katika dunia yote.

17 Bado unaendelea kujiinua juu ya watu wangu, wala hutaki kuwaachia waende.

18 Kwa hiyo, kesho wakati kama huu nitaleta mvua mbaya sana ya mawe ambayo haijapata kunyesha katika nchi ya Misri, tangu siku ilipoumbwa mpaka leo.

19 Sasa toa amri urudishe wanyama wote watoke malishoni na cho chote ambacho kipo mashambani waje mpaka mahali pa usalama, kwa sababu mvua ya mawe itanyesha juu ya kila mtu na kila mnyama ambaye hajaletwa ndani ambao bado wako nje mashambani, nao watakufa.’ ”

20 Wale maafisa wa Farao ambao waliliogopa neno laBwanawakafanya haraka kuwaleta watumwa wao na mifugo yao ndani.

21 Lakini wale waliopuuza neno laBwanawakawaacha watumwa wao na mifugo yao shambani.

22 NdipoBwanaakamwambia Mose, “Nyosha mkono wako kuelekea angani ili kwamba mvua ya mawe inyeshe juu ya Misri yote, juu ya watu, wanyama na juu ya kila kitu kiotacho katika mashamba ya Misri.”

23 Mose alipoinyosha fimbo yake kuelekea angani,Bwanaakatuma ngurumo na mvua ya mawe, umeme wa radi ulimulika hadi nchi. Kwa hiyoBwanaakanyesha mvua ya mawe juu ya nchi ya Misri,

24 mvua ya mawe ikanyesha na radi ikamulika pote. Ikawa dhoruba ya kutisha ambayo haijakuwako katika nchi ya Misri, tangu nchi hiyo iwe taifa.

25 Mvua ya mawe ikaharibu kila kitu katika nchi ya Misri kilichokuwa katika mashamba, watu na wanyama, ikaharibu kila kitu kinachoota mashambani na kuvunja kila mti.

26 Mahali pekee ambapo mvua ya mawe haikunyesha ni nchi ya Gosheni, ambako Waisraeli waliishi.

27 Ndipo Farao akawaita Mose na Aroni akawaambia, “Wakati huu nimetenda dhambi.Bwanani mwenye haki, mimi na watu wangu ni wakosaji.

28 MwombeniBwana, kwa kuwa tumepata ngurumo na mvua za mawe za kututosha. Nitawaachia mwondoke; hamtahitaji kungoja zaidi.”

29 Mose akamjibu, “Nitakapokuwa nimetoka nje ya mji, nitanyosha mikono yangu juu kumwombaBwana. Ngurumo zitakoma na hapatakuwepo mvua ya mawe tena, ili upate kujua kuwa, nchi ni mali yaBwana.

30 Lakini ninajua kuwa wewe na maafisa wako bado hamumwogopiBwanaMungu.”

31 (Kitani na shayiri viliharibiwa, kwa kuwa shayiri ilikuwa na masuke, na kitani ilikuwa katika kutoa maua.

32 Hata hivyo, ngano na jamii nyingine ya ngano hazikuharibiwa kwa sababu zilikuwa hazijakomaa bado.)

33 Kisha Mose akaondoka kwa Farao akaenda nje ya mji. Mose akanyosha mikono yake kuelekea kwaBwana, ngurumo na mvua ya mawe vikakoma, mvua haikuendelea tena kunyesha nchini.

34 Farao alipoona kwamba mvua ya mawe na ngurumo zimekoma, akafanya dhambi tena. Yeye na maafisa wake wakafanya mioyo yao kuwa migumu.

35 Kwa hiyo moyo wa Farao ukawa mgumu, wala hakuwaachia Waisraeli waende, kama vileBwanaalivyokuwa amesema kupitia Mose.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EXO/9-60cf000dea5816567e8e847290354ff7.mp3?version_id=1627—

Kutoka 10

Pigo La Nane: Nzige

1 NdipoBwanaakamwambia Mose, “Nenda kwa Farao, kwa kuwa nimeufanya moyo wake kuwa mgumu na mioyo ya maafisa wake ili kwamba nipate kutenda ishara hizi zangu za ajabu miongoni mwao

2 ili upate kuwaeleza watoto wako na wajukuu wako jinsi nilivyowatendea Wamisri kwa ukali na jinsi nilivyofanya ishara zangu miongoni mwao, nanyi mpate kujua kuwa Mimi ndimiBwana.”

3 Kwa hiyo Mose na Aroni wakaenda kwa Farao na kumwambia, “Hili ndiloBwana, Mungu wa Waebrania, asemalo: ‘Utaendelea hata lini kukataa kunyenyekea mbele yangu? Waachie watu wangu waende, ili wapate kuniabudu.

4 Kama ukikataa kuwaachia waende, kesho nitaleta nzige katika nchi yako.

5 Nao watafunika uso wa ardhi hata usionekana. Watatafuna mabaki machache yaliyobakizwa baada ya ile mvua ya mawe, yaani pamoja na kila mti unaoota katika mashamba yenu.

6 Nzige hao watajaza nyumba zako, za maafisa wako wote na za Wamisri wote. Jambo ambalo baba zenu wala babu zenu hawajapata kuona tangu siku ile walipoanza kuishi katika nchi hii mpaka leo hii.’ ” Ndipo Mose akageuka na kumwacha Farao.

7 Maafisa wa Farao wakamwambia, “Mpaka lini huyu mtu atakuwa tanzi kwetu? Waachie hao watu waende zao, ili wapate kumwabuduBwanaMungu wao. Je, bado hutambui kuwa Misri imeangamia?”

8 Ndipo Mose na Aroni wakaletwa kwa Farao. Farao akawaambia, “Nendeni, mkamwabuduBwanaMungu wenu. Lakini ni nani hasa watakaokwenda?”

9 Mose akajibu, “Tutakwenda na vijana wetu na wazee, pamoja na wana wetu na binti zetu, pia pamoja na kondoo zetu, ng’ombe, mbuzi, farasi na punda kwa sababu tutaadhimisha sikukuu kwaBwana.”

10 Farao akasema, “Bwanaawe pamoja nanyi, kama nikiwaruhusu mwondoke pamoja na wanawake wenu na watoto wenu! Ni wazi kwamba mna makusudi mabaya.

11 La hasha! Wanaume peke yao na waende, wakamwabuduBwana, kwa kuwa hilo ndilo mmekuwa mkiomba.” Kwa hiyo Mose na Aroni wakaondolewa mbele ya Farao.

12 BasiBwanaakamwambia Mose, “Nyosha mkono wako juu ya Misri ili kundi la nzige liweze kuingia juu ya nchi na kutafuna kila kitu kiotacho katika mashamba na kila kitu kilichosazwa na ile mvua ya mawe.”

13 Kwa hiyo Mose akanyosha fimbo yake juu ya Misri,Bwanaakauleta upepo wa mashariki ukavuma katika nchi yote mchana wote na usiku kucha, kufikia asubuhi upepo ukawa umeleta nzige.

14 Wakaivamia Misri yote na kukaa kila eneo la nchi kwa wingi. Kamwe hapajapata kuwepo pigo la nzige kama hilo, wala halitakuwepo tena.

15 Wakafunika ardhi yote mpaka ardhi ikawa nyeusi. Wakatafuna kile chote kilichokuwa kimebakizwa na ile mvua ya mawe, kila kitu kiotacho mashambani pamoja na matunda kwenye miti. Hakuna kitu cho chote cha kijani kilichosalia katika miti au mmea katika nchi yote ya Misri.

16 Farao akawaita Mose na Aroni kwa haraka na kuwaambia, “Nimetenda dhambi dhidi yaBwanaMungu wenu na dhidi yenu pia.

17 Sasa unisamehe dhambi yangu mara moja tena na umwombeBwanaMungu wako aondoe pigo hili baya kwangu.”

18 Kisha Mose akaondoka kwa Farao akamwombaBwana.

19 NayeBwanaakaugeuza upepo ukavuma kutoka magharibi, wenye nguvu nyingi, ambao uliwaondoa wale nzige na kuwapeleka kwenye Bahari ya Shamu. Hakuna nzige hata mmoja aliyebaki po pote katika nchi ya Misri.

20 LakiniBwanaakaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, wala hakuwaachia Waisraeli waondoke.

Pigo La Tisa: Giza

21 KishaBwanaakamwambia Mose, “Nyosha mkono wako kuelekea angani ili giza litande katika nchi ya Misri, giza ambalo watu wanaweza kulipapasa na kulihisi.”

22 Kwa hiyo Mose akaunyosha mkono wake kuelekea angani, na giza nene likafunika pote katika nchi ya Misri kwa muda wa siku tatu.

23 Hakuna mtu ye yote aliyeweza kumwona mwenzake, wala kuondoka mahali alipokuwa kwa muda wa siku tatu. Lakini Waisraeli wote walikuwa na mwanga katika maeneo yao waliyokuwa wanaishi.

24 Ndipo Farao akamwita Mose na kusema, “Nendeni, mkamwabuduBwana. Hata wanawake na watoto wenu mwaweza kwenda nao pia, lakini kondoo, mbuzi na ng’ombe wenu waacheni.”

25 Lakini Mose akasema, “Huna budi kuturuhusu tuwe na dhabihu na sadaka za kuteketezwa za kutoa mbele zaBwanaMungu wetu.

26 Sisi ni lazima tuondoke na mifugo yetu pia, wala hakuna ukwato utakaoachwa nyuma. Inatupasa kutumia baadhi ya hiyo mifugo katika kumwabuduBwanaMungu wetu, kwa kuwa mpaka tutakapofika huko hatutakuwa tumefahamu ni nini tutakachotumia katika kumwabuduBwana.”

27 LakiniBwanaakaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, hakuwa radhi kuwaachia waondoke.

28 Farao akamwambia Mose, “Ondoka mbele yangu! Hakikisha kuwa hutakuja mbele yangu tena! Siku ile utakapouona uso wangu utakufa.”

29 Mose akamjibu, “Iwe kama ulivyosema! Kamwe sitauona uso wako tena.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EXO/10-0dabd0dca1915061e7c3b6f2a9e996a9.mp3?version_id=1627—

Kutoka 11

Pigo La Kumi: Kuuawa Wazaliwa Wa Kwanza

1 BasiBwanaalikuwa amemwambia Mose, “Nitaleta pigo moja zaidi kwa Farao na katika nchi ya Misri. Baada ya hilo, atawaacha mwondoke hapa na atakapofanya hivyo, atawafukuza mtoke kabisa.

2 Waambie watu wote waume kwa wake wawaombe majirani zao vitu vya fedha na vya dhahabu.”

3 (Bwanaakawafanya Wamisri wawe na moyo wa ukarimu kwa Waisraeli, naye Mose mwenyewe akaheshimiwa sana na maafisa wa Farao na watu wote katika nchi ya Misri.)

4 Kwa hiyo Mose akasema, “Hili ndiloBwanaasemalo: ‘Panapo usiku wa manane Mimi nitapita katika nchi yote ya Misri.

5 Kila mwanaume kifungua mimba katika Misri atakufa, kuanzia mzaliwa wa kwanza wa kiume wa Farao, aketiye penye kiti cha ufalme, hadi mzaliwa wa kwanza wa kiume wa mtumwa wa kike, anayesaga nafaka kwa jiwe, pamoja na kila mzaliwa wa kwanza wa mifugo.

6 Patakuwepo kilio kikubwa katika nchi yote ya Misri, kilio kibaya ambacho hakijakuwepo wala kamwe hakitakuwepo tena.

7 Lakini miongoni mwa Waisraeli hakuna hata mbwa atakayembwekea mwanadamu wala mnyama ye yote.’ Ndipo mtakapojua kuwaBwanahuweka tofauti kati ya Misri na Israeli.

8 Maafisa hawa wako wote watanijia, wakisujudu mbele yangu, wakisema, ‘Ondoka, wewe pamoja na watu wako wote wanaokufuata!’ Baada ya haya nitaondoka.” Kisha Mose, huku akiwa amewaka hasira, akamwacha Farao.

9 Bwanaalikuwa amemwambia Mose, “Farao atakataa kukusikiliza, ili maajabu yangu yapate kuongezeka katika nchi ya Misri.”

10 Mose na Aroni wakafanya maajabu haya yote mbele ya Farao, lakiniBwanaakaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, wala hakuwaachia Waisraeli waondoke katika nchi yake.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EXO/11-36b1a91016d5978725053312a164e683.mp3?version_id=1627—