Kutoka 22

Ulinzi Wa Mali

1 “Kama mtu akiiba maksai au kondoo na kumchinja au kumwuza, ni lazima alipe ng’ombe watano badala ya maksai mmoja na kondoo wanne badala ya kondoo mmoja.

2 “Kama mwizi akishikwa anavunja nyumba akapigwa hata akafa, aliyemwua hana hatia ya kumwaga damu;

3 lakini jambo hilo likitokea wakati jua limechomoza, huyo mtu atakuwa na hatia ya kumwaga damu.

“Mwizi huyo sharti alipe, lakini kama hana kitu, lazima auzwe ili alipe kwa ajili ya wizi wake.

4 “Kama mnyama aliyeibwa akikutwa hai mikononi mwake, ikiwa ni maksai au punda au kondoo, lazima alipe mara mbili.

5 “Kama mtu akichunga mifugo yake katika shamba au shamba la mizabibu, na akawaachia wajilishe katika shamba la mtu mwingine, ni lazima alipe vitu bora kutoka kwenye shamba lake mwenyewe au kutoka katika shamba lake la mizabibu.

6 “Kama moto ukiwaka na kuenea kwenye vichaka vya miiba na kuteketeza miganda ya nafaka au nafaka ambayo haijavunwa, au kuteketeza shamba lote, mtu yule aliyewasha moto lazima alipe.

7 “Kama mtu akimpa jirani yake fedha au mali nyingine amtunzie, na kama vikiibwa kutoka katika nyumba ya huyo jirani, kama mwizi atashikwa, lazima alipe mara mbili.

8 Lakini mwizi asipopatikana, mwenye nyumba atafika mbele ya waamuzi ili kuthibitisha kuwa hakuchukua mali ya mwenzake.

9 Pakiwepo jambo lo lote la mali isiyo halali, ikiwa ni maksai, punda, kondoo, mavazi, ama mali yo yote iliyopotea ambayo fulani atasema, ‘Hii ni mali yangu,’ pande zote mbili wataleta mashauri yao mbele ya waamuzi. Yule ambaye waamuzi watamwona kuwa na hatia atamlipa jirani yake mara mbili.

10 “Kama mtu akimpa jirani yake punda, ng’ombe, kondoo au mnyama mwingine ye yote amtunzie, akifa au akijeruhiwa au akichukuliwa wakati haonekani na mtu ye yote,

11 jambo hili kati yao wawili litaamuliwa kwa kuapa kiapo mbele zaBwana, kwamba huyo jirani hakuhusika na wizi wa mali ya jirani yake. Mwenye mali itampasa akubali jambo hili, na hakuna malipo yatakayohitajika.

12 Lakini kama mnyama aliibwa kwa jirani, itampasa amlipe mwenye mnyama.

13 Kama ameraruliwa na mnyama pori, ataleta mabaki ya mnyama kama ushahidi, naye hatadaiwa kulipa mnyama aliyeraruliwa.

14 “Kama mtu akimwazima mnyama kutoka kwa jirani yake, na kama akiumia au akafa na mwenye mnyama hayupo, lazima amlipe huyo mnyama.

15 Lakini mwenye mnyama akiwa angalipo na mnyama wake, mwazimaji hatalazimika kumlipa. Kama mnyama alikuwa amekodishwa, fedha iliyolipwa kwa kukodisha inatosha kwa kufidia hasara.

Uwajibikaji Wa Kijamii

16 “Kama mtu akimshawishi bikira ambaye hajaposwa na akilala naye, lazima alipe mahari, kisha atamwoa msichana huyo.

17 Baba wa msichana akikataa katakata kumpa huyo mtu huyo msichana wake, bado ni lazima huyo mtu atalipa mahari kama inavyostahili malipo ya ubikira.

18 “Usiruhusu mwanamke mchawi aishi.

19 “Mtu ye yote aziniye na mnyama lazima auawe.

20 “Mtu awaye yote anayemtolea mungu mwingine dhabihu isipokuwaBwana, lazima aangamizwe.

21 “Usimtendee mgeni vibaya au kumwonea, kwa kuwa nanyi mlikuwa wageni huko Misri.

22 “Usimdhulumu mjane wala yatima.

23 Kama ukifanya hivyo nao wakinililia, hakika nitasikia kilio chao.

24 Hasira yangu itawaka, nami nitawaua kwa upanga, wake zenu watakuwa wajane na watoto wenu watakuwa yatima.

25 “Kama ukimkopesha mmojawapo wa watu wangu fedha ambaye ni mhitaji, usiwe kama mtu mkopesha fedha; usimtoze riba.

26 Kama ukichukua vazi la jirani kama rehani, ulirudishe kwake kabla jua kuzama,

27 kwa kuwa vazi lake ndilo pekee alilonalo la kumfunika mwili wake. Ni nini kingine atajifunika nacho? Atakaponililia, nitasikia, kwa kuwa nina huruma.

28 “Usimkufuru Mungu au kulaani mtawala wa watu wako.

29 “Usiache kutoa sadaka kutoka ghala zako au mapipa yako.

“Lazima unipe mzaliwa wa kwanza wa wana wako.

30 Ufanye vivyo hivyo kwa ng’ombe wako na kwa kondoo wako. Waache wakae na mama zao kwa siku saba, lakini siku ya nane unipe.

31 “Ninyi mtakuwa watu wangu watakatifu. Kwa hiyo msile nyama ya mnyama aliyeraruliwa na wanyama pori; mtupieni mbwa.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EXO/22-30949aeb20e271408a1e5ea50a10f4a5.mp3?version_id=1627—

Kutoka 23

Sheria Za Haki Na Rehema

1 “Usieneze habari za uongo. Usimsaidie mtu mwovu kwa kuwa shahidi mwenye nia ya kudhuru wengine.

2 “Usifuate umati wa watu katika kutenda mabaya. Unapotoa ushahidi kwenye mashtaka, usipotoshe haki ukijumuika na umati wa watu,

3 nawe usimpendelee mtu maskini katika mashtaka yake.

4 “Kama ukikutana na maksai au punda wa adui yako anapotea, hakikisha umemrudisha kwake.

5 Ukiona punda wa mtu anayekuchukia ameanguka na mzigo wake, usimwache hapo alipoangukia; hakikisha kuwa umemsaidia.

6 “Usiwanyime haki watu wako walio maskini katika mashtaka yao.

7 Ujiepushe na mashtaka ya uongo, wala usimwue mtu asiye na hatia au mtu mwaminifu, kwa maana sitamhesabia hana hatia yeye aliye na hatia.

8 “Usipokee rushwa, kwa kuwa rushwa hupofusha wale waonao, na kupinda maneno ya wenye haki.

9 “Usimwonee mgeni; ninyi wenyewe mnajua jinsi mgeni anavyojisikia, kwa sababu mlikuwa wageni Misri.

Sheria Za Sabato

10 “Kwa muda wa miaka sita mtapanda mashamba yenu na kuvuna mazao,

11 lakini katika mwaka wa saba usiilime ardhi wala kuitumia, ili watu walio maskini miongoni mwenu waweze kupata chakula kutoka kwenye hayo mashamba, nao wanyama pori wapate chakula kwa yale mabaki watakayobakiza. Utafanya hivyo katika shamba lako la mizabibu na la mizeituni.

12 “Kwa siku sita fanya kazi zako, lakini siku ya saba usifanye kazi, ili maksai wako na punda wako wapate kupumzika, naye mtumwa aliyezaliwa nyumbani mwako, pamoja na mgeni, wapate kustarehe.

13 “Uzingatie kutenda kila kitu nilichokuambia. Usiombe kwa majina ya miungu mingine, wala usiyaruhusu kusikika kinywani mwako.

Sikukuu Tatu Za Mwaka

14 “Mara tatu kwa mwaka utanifanyia sikukuu.

15 “Utaadhimisha Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu; kwa siku saba utakula mikate isiyotiwa chachu kama nilivyokuagiza. Fanya jambo hili kwa wakati uliopangwa katika mwezi wa Abibu, ndio mwezi wa nne, kwa sababu katika mwezi huo ulitoka Misri.

“Mtu ye yote asije mbele yangu mikono mitupu.

16 “Utaadhimisha Sikukuu ya Mavuno kwa malimbuko ya mazao yako uliyopanda katika shamba lako.

“Utaadhimisha Sikukuu ya Kukusanya mavuno mwishoni mwa mwaka, unapokusanya mavuno yako toka shambani.

17 “Mara tatu kwa mwaka wanaume wote watakuja mbele zaBwanaMwenyezi.

18 “Msitoe damu ya dhabihu kwangu pamoja na kitu cho chote kilicho na chachu.

“Mafuta ya mnyama wa sadaka ya sikukuu yangu yasibakizwe mpaka asubuhi.

19 “Utaleta malimbuko bora ya ardhi yako katika nyumba yaBwanaMungu wako.

“Usimchemshe mwana-mbuzi kwa kutumia maziwa ya mama yake.

Malaika Wa Mungu Kuandaa Njia

20 “Tazama, ninamtuma malaika akutangulie mbele yako akulinde njiani na kukuleta mpaka mahali nilipoandaa.

21 Mtamtii na kusikiliza kile anachokisema. Usiasi dhidi yake; hatakusamehe uasi wako, kwa maana Jina langu limo ndani yake.

22 Kama ukitii kweli kweli kile asemacho na kufanya yote nisemayo, nitakuwa adui wa adui zako, na nitawapinga wale wakupingao.

23 Malaika wangu atatangulia mbele yako na kukuleta katika nchi ya Waamori, Wahiti, Waperizi, Wakanaani, Wahivi na Wayebusi, nami nitawafutilia mbali.

24 Usiisujudie miungu yao, au kuiabudu, wala kufuata desturi yao. Utayabomoa kabisa na kuvunjavunja mawe yao ya ibada vipande vipande.

25 UtamwabuduBwanaMungu wako, na baraka zake zitakuwa juu ya vyakula vyako na maji yako. Nami nitaondoa maradhi miongoni mwako,

26 na hakuna atakayeharibu mimba wala atakayekuwa tasa katika nchi yako. Nami nitakupa maisha makamilifu.

27 “Nitapeleka utisho wangu mbele yako na kufadhaisha kila taifa utakalolifikia. Nitafanya adui zako wote wakupe kisogo na kukimbia.

28 Nitatanguliza manyigu mbele yako kuwafukuza Wahivi, Wakanaani na Wahiti waondoke njiani mwako.

29 Lakini sitawafukuza kwa mara moja, kwa sababu nchi itabaki ukiwa na wanyama pori watakuwa wengi mno kwako.

30 Nitawafukuza kidogo kidogo mbele yako, mpaka uwe umeongezeka kiasi cha kutosha kuimiliki nchi.

31 “Nitaweka mipaka ya nchi yako kuanzia Bahari ya Shamu hadi Bahari ya Wafilisti, na kuanzia jangwani hadi Mto Eufrati. Nitawatia watu wanaoishi katika nchi hizo mikononi mwako, nawe utawafukuza watoke mbele yako.

32 Usifanye agano lo lote nao wala na miungu yao.

33 Usiwaache waishi katika nchi yako, la sivyo watakusababisha utende dhambi dhidi yangu, kwa sababu ibada ya miungu yao hakika itakuwa mtego kwako.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EXO/23-ba4f1db97b8523ca33680e476c6b7fef.mp3?version_id=1627—

Kutoka 24

Agano Lathibitishwa

1 Kisha Mungu akamwambia Mose, “Njoni huku juu kwaBwana, wewe na Aroni, Nadabu na Abihu, pamoja na wazee sabini wa Israeli. Mniabudu kwa mbali,

2 lakini Mose peke yake ndiye atakayemkaribiaBwana; wengine wasije karibu. Nao watu wasije wakapanda pamoja naye.”

3 Mose alipokwenda na kuwaambia watu maneno yote na sheria zote zaBwana, wakaitikia kwa sauti moja, “Kila kitu alichosemaBwanatutakifanya.”

4 Ndipo Mose akaandika kila kituBwanaalichokuwa amesema.

Akaamka kesho yake asubuhi na mapema na kujenga madhabahu chini ya mlima na kusimamisha nguzo kumi na mbili za mawe kuwakilisha makabila kumi na mawili ya Israeli.

5 Kisha akawatuma vijana wanaume wa Kiisraeli, nao wakatoa sadaka za kuteketezwa na dhabihu za mafahali wachanga kuwa sadaka za amani kwaBwana.

6 Mose akachukua nusu ya damu ya wale wanyama na kuiweka kwenye mabakuli na nusu nyingine akainyunyiza juu ya madhabahu.

7 Kisha akachukua kile Kitabu cha Agano na kuwasomea watu. Nao wakajibu, “Tutafanya kila kitu alichosemaBwana, nasi tutatii.”

8 Ndipo Mose akachukua ile damu, akainyunyiza juu ya watu, akasema, “Hii ni damu ya Agano ambaloBwanaamefanya nanyi kufuatana na maneno haya yote.”

9 Mose na Aroni, Nadabu na Abihu, pamoja na wazee sabini wa Israeli wakapanda mlimani,

10 nao wakamwona Mungu wa Israeli. Chini ya miguu yake kulikuwa na kitu kama sakafu ya mawe ya yakuti samawi, iliyo safi kama anga angavu.

11 Lakini Mungu hakuinua mkono wake dhidi ya hawa viongozi wa Waisraeli; walimwona Mungu, nao wakala na kunywa.

12 Bwanaakamwambia Mose, “Panda uje kwangu huku mlimani na ukae hapa, nami nitakupa vibao vya mawe, vyenye sheria na amri ambazo nimeziandika ziwe mwongozo wao.”

13 Basi Mose akaondoka na Yoshua mtumishi wake, naye Mose akapanda juu kwenye mlima wa Mungu.

14 Mose akawaambia wazee wa Israeli, “Tungojeni hapa mpaka tutakapowarudia. Aroni na Huri wako pamoja nanyi, na kila aliye na neno aweza kuwaendea wao.”

15 Mose alipopanda juu mlimani, wingu liliufunika huo mlima,

16 nao utukufu waBwanaukatua juu ya Mlima Sinai. Kwa muda wa siku sita wingu lilifunika mlima, na siku ya sabaBwanaakamwita Mose kutoka katikati ya lile wingu.

17 Kwa Waisraeli utukufu waBwanaulionekana kama moto uteketezao juu ya mlima.

18 Kisha Mose akaingia ndani ya lile wingu alivyokuwa akipanda mlimani. Naye akakaa huko mlimani kwa muda wa siku arobaini, mchana na usiku.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EXO/24-95d63d427e1ace0eaddbdb937a15a7b9.mp3?version_id=1627—

Kutoka 25

Sadaka Kwa Ajili Ya Maskani Ya Mungu

1 Bwanaakamwambia Mose,

2 “Waambie Waisraeli waniletee sadaka. Utapokea sadaka kwa ajili yangu kutoka kwa kila mtu ambaye moyo wake wapenda kutoa.

3 Hizi ndizo sadaka utakazozipokea kutoka kwao: dhahabu, fedha na shaba;

4 nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu, pamoja na nguo za kitani safi; singa za mbuzi;

5 ngozi za kondoo waume zilizotiwa rangi nyekundu, na ngozi za mbuzi; mbao za mshita;

6 mafuta ya mzeituni kwa ajili ya taa; vikolezi kwa ajili ya mafuta ya kupaka, na kwa ajili ya uvumba wenye harufu nzuri;

7 na vito vya shohamu na vito vingine vya kutiwa kwenye kile kisibau na kifuko cha kifuani.

8 “Kisha amuru watengeneze mahali patakatifu kwa ajili yangu, nami nitakaa miongoni mwao.

9 Tengeneza hema hili na vyombo vyake vyote sawasawa na kielelezo nitakachokuonyesha.

Sanduku La Agano

10 “Nao watatengeneza Sanduku la mbao za mshita, lenye urefu wa dhiraa mbili na nusu, upana dhiraa moja na nusu, na kimo cha dhiraa moja na nusu.

11 Utalifunika hilo Sanduku kwa dhahabu safi ndani na nje, na kulifanyia ukingo wa dhahabu juu yake kulizunguka.

12 Utalitengenezea pete nne za dhahabu na kuzifunga kwenye miguu yake minne, pete mbili upande mmoja na pete mbili upande mwingine.

13 Kisha utatengeneza mipiko ya mti wa mshita na kuzifunika kwa dhahabu.

14 Utaiingiza hiyo mipiko kwenye hizo pete zilizo katika pande mbili za hilo Sanduku ili kulibeba.

15 Hiyo mipiko itabakia daima katika hizo pete za hilo Sanduku; haitaondolewa.

16 Kisha weka ndani ya hilo Sanduku ule Ushuhuda nitakaokupa.

17 “Tengeneza kiti cha rehema cha dhahabu safi, chenye urefu wa dhiraa mbili na nusu, na upana wa dhiraa moja na nusu.

18 Tengeneza makerubi wawili kwa dhahabu iliyofuliwa kwenye miisho miwili ya hicho kifuniko.

19 Tengeneza kerubi mmoja kwenye mwisho mmoja, na kerubi mwingine kwenye mwisho mwingine; yatengeneze makerubi yawe kitu kimoja na hicho kifuniko katika miisho hiyo miwili.

20 Makerubi hao watakuwa wametandaza mabawa kuelekea juu, yakitia kivuli hicho kifuniko. Makerubi hao wataelekeana, wakitazama hicho kifuniko.

21 Weka huo Ushuhuda nitakaokupa ndani ya hilo Sanduku la Agano, na uweke hicho kifuniko juu ya hilo Sanduku.

22 Hapo juu ya hicho kifuniko, kati ya hao makerubi wawili walioko juu ya hilo Sanduku la Ushuhuda, hapo ndipo nitakapokutana nawe na kukupa maagizo yangu kwa ajili ya Waisraeli.

Meza Ya Mikate Ya Wonyesho

23 “Tengeneza meza ya mti wa mshita yenye urefu wa dhiraa mbili, upana wa dhiraa moja na kimo cha dhiraa moja na nusu.

24 Ifunike hiyo meza kwa dhahabu safi kisha uifanyie ukingo wa dhahabu kuizunguka pande zote.

25 Kisha tengeneza upapi wenye upana wa nyanda nnena ufanyie ule upapi ukingo kuuzunguka pande zote.

26 Tengeneza pete nne za dhahabu kwa ajili ya meza hiyo, uzifungie kwenye pembe nne, kwenye miguu yake minne.

27 Pete hizo zitakuwa karibu na ukingo ule kushika ile mipiko ambayo ni ya kubebea hiyo meza.

28 Tengeneza mipiko ya mti wa mshita, uifunike dhahabu, hiyo mipiko itakuwa ya kuibebea hiyo meza.

29 Tengeneza sahani zake na masinia yake kwa dhahabu safi, pamoja na bilauri na bakuli zake kwa ajili ya kumiminia sadaka.

30 Utaweka mikate Mitakatifu juu ya meza hii iwe mbele yangu daima.

Kinara Cha Taa

31 “Tengeneza kinara cha taa cha dhahabu safi nacho kiwe cha kazi ya kufua, tako lake na ufito wake; vikombe vyake vinavyofanana na ua, matovu yake na maua yake, vitakuwa vya kitu kimoja.

32 Matawi sita yatatokeza kuanzia ule ufito wa katikati wa kinara cha taa: matawi matatu upande mmoja na matawi matatu upande mwingine.

33 Vikombe vitatu mfano wa maua ya mlozi yenye matovu na maua yawe katika tawi moja, matovu matatu katika tawi jingine, na vivyo hivyo kwa matawi yote sita yaliyoanzia kwenye kinara cha taa.

34 Juu ya kinara chenyewe vitakuwepo vikombe vinne mfano wa maua ya mlozi, pamoja na matovu yake na maua yake.

35 Tovu moja litakuwa chini ya jozi ya kwanza ya matawi yaliyoanzia kwenye kinara cha taa, tovu la pili chini ya jozi ya pili, nalo tovu la tatu chini ya jozi ya tatu, yaani matawi sita kwa jumla.

36 Matovu na matawi yote yatakuwa ya kitu kimoja na kile kinara cha taa vyote vitafuliwa kutoka dhahabu safi.

37 “Kisha tengeneza taa zake saba uziweke juu ya kinara hicho ili ziweze kuangaza mbele yake.

38 Vitu vya kusawazishia vya tambi na vyano, vitakuwa dhahabu safi.

39 Utatumia talanta mojaya dhahabu safi kutengeneza hicho kinara na hivi vifaa vyake vyote.

40 Hakikisha kuwa umevitengeneza sawasawa na kile kielelezo ulichoonyeshwa kule mlimani.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EXO/25-a7b6b835771db0a2f88ed1cd7fba41c3.mp3?version_id=1627—

Kutoka 26

Maskani Ya Mungu

1 “Tengeneza Hema kwa mapazia kumi ya kitani iliyosokotwa vizuri na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu, naye fundi stadi atatarizi makerubi kwenye mapazia hayo.

2 Mapazia yote yatakuwa na ukubwa mmoja: kila moja litakuwa na urefu wa dhiraa ishirini na nanena upana wa dhiraa nne.

3 Unganisha mapazia matano kuwa kipande kimoja; fanya vivyo hivyo kwa hayo mengine matano.

4 Tengeneza vitanzi vya kitambaa cha buluu kwenye ukingo wa pazia la mwisho la kipande cha kwanza, pia kipande cha mwisho cha pazia la pili ufanye vivyo hivyo.

5 Fanya vitanzi hamsini katika pazia la mwisho la kipande cha kwanza na vitanzi hamsini vingine kwenye pazia la mwisho la kipande cha pili, vitanzi vyote vielekeane.

6 Kisha tengeneza kulabu hamsini za dhahabu ili kukaza mapazia pamoja kufanya Hema liwe moja.

7 “Tengeneza mapazia kumi na moja ya singa za mbuzi kwa ajili ya kufunika Hema.

8 Mapazia hayo kumi na moja yatakuwa na kipimo cha aina moja. Kila pazia litakuwa na urefu wa dhiraa thelathini na tatuna upana wa dhiraa nne.

9 Unganisha hayo mapazia matano pamoja na hayo mengine sita pamoja. Kunja hilo pazia la sita mara mbili mbele ya Hema.

10 Tengeneza vitanzi hamsini ukingoni mwa pazia la mwisho la kipande cha kwanza, na vitanzi hamsini ukingoni mwa pazia la mwisho la kipande cha pili.

11 Kisha tengeneza kulabu hamsini za shaba, uziingize katika vile vitanzi hamsini ili kukaza Hema kuwa kitu kimoja.

12 Kuhusu kile kipande cha ziada cha pazia la Hema, nusu ya hilo pazia lililobaki litaning’inizwa upande wa nyuma wa Hema.

13 Mapazia ya hema yatakuwa na urefu wa dhiraa moja zaidi pande zote, sehemu itakayobaki itaning’inia pande zote za Hema ili kuifunika.

14 Tengeneza kifuniko cha Hema kwa ngozi za kondoo waume zilizotiwa rangi nyekundu, juu ya kifuniko hicho ufunike ngozi laini za wanyama.

15 “Tengeneza mihimili ya mti wa mshita kwa ajili ya Hema.

16 Kila mhimili uwe na urefu wa dhiraa kumina upana wake dhiraa moja na nusu,

17 ikiwa na ndimi mbili zilizo sambamba. Tengeneza mihimili yote ya Hema jinsi hii.

18 Tengeneza mihimili ishirini ya upande wa kusini wa Hema,

19 kisha tengeneza vitako arobaini vya fedha vya kuweka chini ya hiyo mihimili, vitako viwili kwa kila mhimili, moja chini ya kila ulimi.

20 Kuhusu upande mwingine, yaani upande wa kaskazini wa Hema, tengeneza mihimili ishirini

21 na vitako arobaini vya fedha, viwili chini ya kila mhimili.

22 Kisha tengeneza mihimili sita kwa kila mwisho, yaani, upande wa magharibi wa Hema,

23 pia utengeneze mihimili miwili ya pembe za mwishoni.

24 Katika pembe hizi mbili ni lazima mihimili iwe miwili kuanzia chini mpaka juu na kushikizwa kwenye pete moja, yote miwili itafanana.

25 Kwa hiyo itakuwepo mihimili minane na vitako kumi na sita vya fedha, viwili chini ya kila mhimili.

26 “Pia tengeneza fito za mti wa mshita: tano kwa ajili ya mihimili ya upande mmoja wa Hema,

27 tano kwa ajili ya mihimili ya upande mwingine, na tano kwa ajili ya mihimili ya upande wa magharibi, mwishoni kabisa mwa Hema.

28 Ufito wa katikati utapenya toka mwisho huu hadi mwisho mwingine katikati ya mihimili.

29 Funika hiyo mihimili kwa dhahabu, kisha tengeneza pete za dhahabu ambazo zitashikilia hizo fito. Pia funika fito hizo kwa dhahabu.

30 “Simamisha Hema sawasawa na ramani uliyoonyeshwa kule juu mlimani.

31 “Tengeneza pazia la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu na kitani safi iliyosokotwa vizuri, naye fundi stadi atarizi makerubi kwenye hayo mapazia.

32 Litundike kwa kulabu za dhahabu kwenye nguzo nne za mti wa mshita ambazo zimefunikwa kwa dhahabu, zikiwa zimesimamishwa kwenye vitako vinne vya fedha.

33 Ning’iniza pazia hilo kwenye vifungo, kisha weka Sanduku la Ushuhuda nyuma ya pazia. Pazia litatenganisha Patakatifu na Patakatifu pa Patakatifu.

34 Weka kifuniko cha kiti cha rehema juu ya Sanduku la Ushuhuda ndani ya mahali Patakatifu pa Patakatifu.

35 Weka meza nje ya pazia upande wa kaskazini wa Hema, kisha weka kinara cha taa upande wa kusini wa Hema.

36 “Kwa ajili ya lango la hema, tengeneza pazia la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu na kitani safi iliyosokotwa vizuri, ambayo ni kazi ya mtarizi.

37 Tengeneza kulabu za dhahabu kwa ajili ya hilo pazia na nguzo tano za mshita zilizofunikwa kwa dhahabu. Kisha mimina vitako vitano vya shaba kwa ajili yake.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EXO/26-1d653225be8f1117d25d057a148ca0a9.mp3?version_id=1627—

Kutoka 27

Madhabahu Ya Sadaka Ya Kuteketezwa

1 “Jenga madhabahu ya mbao za mti wa mshita, kimo chake ni dhiraa tatu;itakuwa mraba, urefu wake dhiraa tanona upana wake dhiraa tano.

2 Tengeneza upembe kwenye kila pembe ya hizo pembe nne, ili kwamba zile pembe na madhabahu ziwe zimeungana na uifunike madhabahu kwa shaba.

3 Tengeneza vyombo vyake vyote kwa shaba: vyungu vyake vya kuondolea majivu, sepeto zake, mabakuli ya kunyunyizia, nyuma za nyama, na vyombo vya kuchukulia moto.

4 Kisha itengenezee hiyo madhabahu wavu wa shaba, na utengeneze pete za shaba kwenye kila pembe nne za huo wavu.

5 Weka wavu huo chini ya ukingo wa madhabahu ili ufike nusu ya kimo cha madhabahu.

6 Tengeneza mipiko ya mti wa mshita kwa ajili ya madhabahu, ifunike kwa shaba.

7 Hiyo mipiko itaingizwa kwenye zile pete ili iwe katika pande mbili za madhabahu, wakati inapobebwa.

8 Tengeneza madhabahu iwe na uvungu ndani yake, ukitumia mbao. Utaitengeneza sawasawa na vile ulivyoonyeshwa mlimani.

Ua Wa Kukutania

9 “Tengeneza ua kwa ajili ya Hema la Kukutania. Upande wa kusini utakuwa na urefu wa dhiraa mia moja,na itakuwa na mapazia ya kitani iliyosokotwa vizuri,

10 pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini. Pia kutakuwa na kulabu za fedha na tepe za fedha juu ya hizo nguzo.

11 Upande wa kaskazini itakuwa na urefu wa dhiraa mia moja, nao utakuwa na mapazia na nguzo zake ishirini, na vitako ishirini vya shaba, pamoja na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo.

12 “Upande wa magharibi wa ua wa kukutania utakuwa na upana wa dhiraa hamsini,nao utakuwa na mapazia na nguzo zake kumi na vitako vyake kumi.

13 Upande wa mwisho wa mashariki jua linakotokea, ua wa mkutano utakuwa na upana wa dhiraa hamsini.

14 Mapazia yenye urefu wa dhiraa kumi na tano ambayo yatakuwa upande mmoja wa lango, pamoja na nguzo tatu na vitako vitatu,

15 Kutakuwepo tena na mapazia ya dhiraa kumi na tanokwa upande mwingine wa mlango, pamoja na nguzo tatu na vitako vitatu.

16 “Kuhusu lango la kuingilia kwenye ua wa kukutania, weka pazia lenye urefu wa dhiraa ishirini, la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu pamoja na kitani iliyosokotwa vizuri kazi ya mtarizi. Pazia hilo litashikiliwa na nguzo nne na vitako vinne.

17 Nguzo zote zinazozunguka ua wa kukutania zitakuwa na tepe na kulabu za fedha, na vitako vya shaba.

18 Ua wa kukutania utakuwa na urefu wa dhiraa mia moja na upana wa dhiraa hamsini, ukiwa na mapazia ya kitani yaliyosokotwa vizuri yenye urefu wa dhiraa tano kwenda juu na vitako vya shaba.

19 Vyombo vingine vyote vinavyotumika katika Maskani kwa shughuli yo yote, pamoja na vigingi vyote, na hata vile vya ua wa kukutania vitakuwa vya shaba.

Mafuta Ya Kinara Cha Taa

20 “Utawaamuru Waisraeli wakuletee mafuta safi ya zeituni yaliyokamuliwa kwa ajili ya mwanga ili zile taa ziwake daima.

21 Katika Hema la Kukutania, nje ya pazia lililo mbele ya Sanduku la Ushuhuda, Aroni na wanawe watahakikisha kuwa taa hizo zinawaka kuanzia jioni mpaka asubuhi mbele zaBwana. Hili litakuwa agizo la milele miongoni mwa Waisraeli kwa vizazi vyote vijavyo.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EXO/27-1a7f7488fcb35d2931e7edc419f53690.mp3?version_id=1627—

Kutoka 28

Mavazi Ya Kikuhani

1 “Mtwae Aroni ndugu yako aliyeletwa kwako kutoka miongoni mwa Waisraeli, pamoja na wanawe Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari, ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani.

2 Mshonee Aroni ndugu yako mavazi matakatifu ili yampe ukuu na heshima.

3 Waambie mafundi stadi wote niliowapa hekima katika shughuli hiyo wamtengenezee Aroni mavazi hayo, ili awekwe wakfu, anitumikie katika kazi ya ukuhani.

4 Haya ndiyo mavazi watakayoshona: kifuko cha kifuani, kisibau, kanzu, joho lililorembwa, kilemba na mshipi. Mavazi haya yatashonwa kwa ajili ya ndugu yako Aroni na wanawe ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani.

5 Waambie watumie dhahabu na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu pamoja na kitani safi.

Kisibau

6 “Tengeneza kisibau cha nyuzi za rangi ya dhahabu, za buluu, za zambarau, za rangi nyekundu na kitani safi iliyosokotwa, kazi ya fundi stadi.

7 Kitakuwa na vipande viwili vya mabegani vilivyoshikizwa kwenye pembe zake mbili ili kufungia kisibau.

8 Mshipi wa kiunoni uliotengenezwa kwa ustadi ambao ni kitu kimoja na kisibau utatengenezwa kwa nyuzi za rangi ya dhahabu, za buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu, kitani safi iliyosokotwa vizuri.

9 “Chukua mawe mawili ya shohamu na uchore juu yake majina ya wana wa Israeli

10 kufuatana na walivyozaliwa, majina sita katika jiwe moja na mengine sita katika jiwe jingine.

11 Yachore majina ya wana wa Israeli juu ya hayo mawe mawili kama vile sonara anavyochonga muhuri. Kisha uyatie hayo mawe katika vijalizo vya dhahabu

12 na uvifungie juu ya vipande vya mabega ya kisibau yawe kama mawe ya kumbukumbu ya wana wa Israeli. Aroni atavaa majina hayo mabegani mwake kama kumbukumbu mbele zaBwana.

13 Tengeneza vijalizo vya dhahabu

14 na mikufu miwili ya dhahabu safi, iliyosokotwa kama kamba, na uifunge mikufu hiyo kwenye vijalizo.

Kifuko Cha Kifuani

15 “Fanyiza kifuko cha kifuani kwa ajili ya kufanya maamuzi, kazi ya fundi stadi. Kitengeneze kama kile kisibau: cha nyuzi za rangi ya dhahabu, buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu, cha kitani safi iliyosokotwa.

16 Kitakuwa cha mraba, nusu dhiraakila upande, na kikunjwe mara mbili.

17 Kisha weka safu nne za vito vya thamani juu yake. Safu ya kwanza itakuwa ya akiki, yakuti manjano na zabarajadi;

18 katika safu ya pili kitakuwa na almasi, yakuti samawi na zumaridi;

19 safu ya tatu itakuwa na hiakintho, akiki nyekundu na amethisto;

20 na safu ya nne itakuwa ya krisolitho, shohamu na yaspi. Yote yatiwe kwenye vijalizo vya dhahabu.

21 Patakuwa na mawe kumi na mawili, moja kwa kila jina la wana wa Israeli, kila moja lichorwe kama muhuri likiwa na jina la moja ya makabila kumi na mawili ya Israeli.

22 “Kwa ajili ya kifuko cha kifuani, tengeneza mikufu ya dhahabu safi, iliyosokotwa kama kamba.

23 Tengeneza pete mbili za dhahabu kwa ajili yake uzifungie kwenye pembe mbili za kifuko cha kifuani.

24 Funga ile mikufu miwili ya dhahabu kwenye zile pete zilizo katika pembe za kifuko cha kifuani,

25 zile ncha nyingine mbili za mkufu wa dhahabu zishikamanishe kwenye vijalizo viwili vya kisibau upande wa mbele.

26 Tengeneza pete mbili za dhahabu uzifunge kwenye ncha mbili za chini upande wa ndani wa kifuko cha kifuani karibu na kisibau.

27 Tengeneza pete mbili zaidi za dhahabu na uzishikize mbele katika ncha za chini za vipande vya kisibau, mahali kinapoungana juu ya mshipi wa kiunoni wa kisibau.

28 Pete za kifuko cha kifuani zitafungwa pamoja na zile za kisibau kwa kamba ya buluu, ili kiunganishwe na ule mshipi wa kiunoni ili kifuko cha kifuani kisitoke na kuachana na kisibau.

29 “Wakati wo wote Aroni aingiapo Mahali Patakatifu, atakuwa na yale majina ya wana wa Israeli moyoni mwake juu ya kile kifuko cha kifuani cha uamuzi kama kumbukumbu ya kudumu mbele zaBwana.

30 Pia weka Urimu na Thumimundani ya kifuko cha kifuani, yawe juu ya moyo wa Aroni kila mara aingiapo mbele zaBwana. Kwa hiyo siku zote Aroni atakuwa na uwezo kufanya maamuzi kwa ajili ya wana wa Israeli mbele zaBwana.

Mavazi Mengine Ya Kikuhani

31 “Shona kanzu ya kuvalia kisibau kwa kitambaa cha buluu tupu,

32 katikati weka nafasi ya kuingizia kichwa. Kutakuwa na utepe unaofanana na ukosi uliozungushwa kwenye nafasi hiyo ya shingo, ili isichanike.

33 Tengeneza makomamanga ya nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu kuzunguka pindo la hilo joho, weka pia vikengele vya dhahabu kati ya hayo makomamanga.

34 Hivyo vikengele vya dhahabu na makomamanga vitapishana kuzunguka pindo la kanzu.

35 Ni lazima Aroni alivae anapofanya huduma. Sauti ya hivyo vikengele itasikika anapoingia na kutoka katika mahali patakatifu mbele zaBwana, ili asije akafa.

36 “Tengeneza bamba la dhahabu safi na uchore kama muhuri juu yake maneno haya: MTAKATIFU KWABwana.

37 Lifunge hilo bamba kwa kamba ya buluu kwenye kilemba, nalo ni lazima liwe mbele ya kilemba.

38 Aroni alivae bamba hilo kwenye paji la uso wake, naye atachukua hatia kuhusu sadaka takatifu za Waisraeli wanazoweka wakfu, sadaka za aina yo yote. Litakuwa kwenye paji la uso wa Aroni daima ili zikubalike kwaBwana.

39 “Fuma koti la kitani safi na ufanye kilemba cha kitani safi. Mshipi uwe ni kazi ya mtarizi.

40 Watengenezee wana wa Aroni makoti, mishipi na kofia, ili kuwapa ukuu na heshima.

41 Baada ya kumvika Aroni ndugu yako pamoja na wanawe nguo hizi, watie mafuta na kuwabariki. Waweke wakfu ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani.

42 “Watengenezee nguo za ndani za kitani zitakazofunika mwili, kutoka kiunoni hadi mapajani.

43 Aroni na wanawe ni lazima wavae haya kila wanapoingia katika Hema la Kukutania au wanaposogelea madhabahu wakati wa kutoa huduma mahali patakatifu, ili wasije wakafanya kosa wakafa.

“Haya yawe maagizo ya kudumu kwa Aroni na vizazi vyake.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EXO/28-5675bc9f94b2fe42a79412f3816bc21a.mp3?version_id=1627—

Kutoka 29

Kuweka Wakfu Makuhani

1 “Hili ndilo utakalofanya ili kuwaweka wakfu makuhani ili wanitumikie mimi katika kazi ya ukuhani: Chukua fahali mchanga mmoja na kondoo waume wawili wasio na dosari.

2 Kutokana na unga laini wa ngano usiotiwa chachu, tengeneza mikate na maandazi yaliyokandwa kwa mafuta, pamoja na mikate midogo myembamba.

3 Viwekwe vyote ndani ya kikapu na kuvitoa pamoja na yule fahali na wale kondoo waume wawili.

4 Kisha mlete Aroni na wanawe kwenye lango la Hema la Kukutania na uwaoshe kwa maji.

5 Chukua yale mavazi na umvike Aroni koti, joho la kisibau na kisibau chenyewe pamoja na kile kifuko cha kifuani. Mfungie hicho kisibau kwa ule mshipi wa kiunoni uliosukwa kwa ustadi.

6 Weka kilemba kichwani mwake na kuweka taji takatifu ishikamane na hicho kilemba.

7 Chukua yale mafuta ya upako umimine juu ya kichwa chake.

8 Walete wanawe na uwavike makoti,

9 pia uwavike zile tepe za kichwani. Ndipo uwafunge Aroni na wanawe mishipi. Ukuhani ni wao kwa agizo la kudumu. Kwa njia hii utamsimika Aroni na wanawe.

10 “Mlete yule fahali mbele ya Hema la Kukutania, naye Aroni na wanawe wataweka mikono yao juu ya kichwa chake.

11 Mchinje huyo fahali mbele zaBwanakwenye mlango wa Hema la Kukutania.

12 Chukua sehemu ya damu ya huyo fahali na kuipaka kwenye pembe za hiyo madhabahu kwa kidole chako, na damu iliyobaki uimwage sehemu ya chini ya madhabahu.

13 Kisha chukua mafuta yote ya huyo mnyama ya sehemu za ndani, yale yanayofunika ini na figo zote mbili pamoja na mafuta yake, uvichome juu ya madhabahu.

14 Lakini nyama ya huyo fahali na ngozi yake na matumbo yake utavichoma nje ya kambi. Hii ni sadaka ya dhambi.

15 “Chukua mmoja wa wale kondoo dume, naye Aroni na wanawe wataweka mikono yao juu ya kichwa chake.

16 Mchinje huyo kondoo dume, chukua damu yake na uinyunyizie pande zote za hiyo madhabahu.

17 Mkate huyo kondoo dume vipande vipande na usafishe sehemu za ndani pamoja na miguu, ukiviweka pamoja na kichwa na vipande vingine.

18 Kisha mteketeze huyo kondoo mzima juu ya madhabahu. Hii ni sadaka ya kuteketezwa kwaBwana, harufu ya kupendeza, sadaka iliyotolewa kwaBwanakwa moto.

19 “Mchukue yule kondoo dume mwingine, naye Aroni na wanawe waweke mikono yao juu ya kichwa chake.

20 Mchinje, uchukue sehemu ya damu yake na kuipaka kwenye masikio ya Aroni na wanawe, kwenye vidole gumba vya mikono yao ya kuume, pia kwenye vidole gumba vya miguu yao ya kuume. Kisha nyunyiza hiyo damu pande zote za madhabahu.

21 Pia chukua sehemu ya damu iliyo juu ya madhabahu na sehemu ya mafuta ya upako, umnyunyizie Aroni na mavazi yake, pia wanawe na mavazi yao. Ndipo Aroni na wanawe pamoja na mavazi yao watakuwa wamewekwa wakfu.

22 “Chukua mafuta ya huyu kondoo dume, mafuta ya mkia, mafuta ya sehemu za ndani yale yanayofunika ini, figo zote mbili na mafuta yake, pamoja na paja la kulia. (Huyo ndiye kondoo dume kwa ajili ya kuwasimika.)

23 Kutoka kwenye kile kikapu chenye mikate isiyotiwa chachu, kilichoko mbele zaBwana, chukua mkate, andazi lililokandwa kwa mafuta na mkate mdogo mwembamba.

24 Viweke vitu hivi vyote mikononi mwa Aroni na wanawe na uviinue mbele zaBwanakuwa sadaka ya kuinuliwa.

25 Kisha vichukue vitu hivyo kutoka mikononi mwao, uviteketeze juu ya madhabahu pamoja na sadaka ya kuteketezwa kuwa harufu nzuri ya kupendeza kwaBwana, sadaka iliyotolewa kwaBwanakwa moto.

26 Baada ya wewe kuchukua kidari cha huyo kondoo dume wa kusimikwa kwa Aroni, kiinue mbele zaBwanakuwa sadaka ya kuinuliwa, nayo itakuwa fungu lako.

27 “Weka wakfu zile sehemu za kondoo dume aliyetumika kwa kumsimika Aroni na wanawe: kidari kile kilichoinuliwa na lile paja lililotolewa.

28 Siku zote hili litakuwa fungu la kawaida kutoka kwa Waisraeli kwa ajili ya Aroni na wanawe. Hili ni toleo la Waisraeli watakalotoa kwaBwanakutoka katika sadaka zao za amani.

29 “Mavazi matakatifu ya Aroni yatakuwa ya wazao wake ili kwamba waweze kutiwa mafuta na kusimikwa wakiwa wameyavaa.

30 Mwana atakayeingia mahali pake kuwa kuhani na kuja kwenye Hema la Kukutania kuhudumu katika Mahali Patakatifu atayavaa kwa siku saba.

31 “Chukua nyama ya huyo kondoo dume wa kuwasimika uipike katika Mahali Patakatifu.

32 Kwenye ingilio la Hema la Kukutania, Aroni na wanawe wataila ile nyama ya huyo kondoo dume pamoja na ile mikate iliyo kwenye hicho kikapu.

33 Watakula sadaka hizi ambazo kwa hizo upatanisho ulifanywa kwa ajili ya kusimikwa kwao na kuwekwa kwao wakfu. Lakini hakuna mtu mwingine ye yote anayeruhusiwa kuvila, kwa sababu ni vitakatifu.

34 Ikiwa nyama yo yote ya huyo kondoo dume iliyotumika kwa kuwasimika au mkate wo wote umebaki mpaka asubuhi, vichomwe. Kamwe visiliwe, kwa sababu ni vitakatifu.

35 “Hivyo utamfanyia Aroni na wanawe kila kitu kama vile nilivyokuamuru: Utachukua muda wa siku saba kuwaweka wakfu.

36 Utatoa dhabihu ya fahali kila siku kuwa sadaka ya dhambi ili kufanya upatanisho. Takasa madhabahu kwa kufanya upatanisho kwa ajili yake, nayo uitie mafuta na kuiweka wakfu.

37 Kwa muda wa siku saba fanya upatanisho kwa ajili ya madhabahu na kuiweka wakfu. Ndipo madhabahu itakuwa takatifu sana na cho chote kitakachoigusa kitakuwa kitakatifu.

38 “Kwa kawaida hiki ndicho utakachotoa juu ya madhabahu kila siku: wana-kondoo wawili wenye umri wa mwaka mmoja.

39 Utamtoa mmoja asubuhi na huyo mwingine wakati wa machweo.

40 Pamoja na mwana-kondoo wa kwanza utatoa efa mojaya unga wa ngano laini uliochanganywa na robo ya hiniya mafuta yaliyokamuliwa ya zeituni pamoja na robo ya hini ya divai kuwa sadaka ya kinywaji.

41 Huyo mwana-kondoo mwingine mtoe dhabihu wakati wa machweo pamoja na sadaka za unga na za kinywaji kama vile ulivyofanya asubuhi, kuwa harufu ya kupendeza, sadaka iliyotolewa kwaBwanakwa moto.

42 “Kwa vizazi vijavyo itakuwa kawaida kutoa sadaka hii ya kuteketezwa kila mara kwenye ingilio la Hema la Kukutania mbele zaBwana. Hapo ndipo nitakapokutana na ninyi na kusema nanyi,

43 Huko ndipo nitakapokutana na Waisraeli, nalo Hema la Kukutania litatakaswa na utukufu wangu.

44 “Kwa hiyo nitaliweka wakfu Hema la Kukutania pamoja na madhabahu, nami nitamweka wakfu Aroni na wanawe ili wanitumikie mimi katika kazi ya ukuhani.

45 Ndipo nitakapofanya makao miongoni mwa Waisraeli na kuwa Mungu wao.

46 Nao watajua kuwa Mimi NdimiBwanaMungu wao, aliyewatoa Misri ili nipate kufanya makao miongoni mwao. Mimi NdimiBwanaMungu wao.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EXO/29-4937014ebc00925ce8cb4a1c8c12d420.mp3?version_id=1627—

Kutoka 30

Madhabahu Ya Kufukizia Uvumba

1 “Tengeneza madhabahu ya mti wa mshita kwa ajili ya kufukizia uvumba.

2 Madhabahu iwe mraba, urefu na upana wa dhiraa mojana kimo cha dhiraa mbili, pembe zake zitakuwa za kitu kimoja nayo.

3 Funika juu ya hiyo madhabahu, na pande zote na pembe zake kwa dhahabu safi, na ufanyize ukingo wa dhahabu kuizunguka.

4 Tengeneza pete mbili za dhahabu kwa ajili ya madhabahu chini ya huo ukingo, nyingine mbili upande wa pili ili kushika hiyo mipiko itumikayo wakati wa kuibeba.

5 Tengeneza mipiko ya mti wa mshita na uifunike kwa dhahabu.

6 Weka hiyo madhabahu mbele ya lile pazia lililo mbele ya Sanduku la Ushuhuda, lililo mbele ya kiti cha rehema kilicho juu ya Sanduku la Ushuhuda, mahali ambapo nitakutana nawe.

7 “Itampasa Aroni kufukiza uvumba wenye harufu nzuri juu ya madhabahu kila siku asubuhi wakati anapowasha zile taa.

8 Itampasa afukize uvumba tena wakati anapowasha taa wakati wa machweo ili uvumba ufukizwe daima mbele zaBwanakwa vizazi vijavyo.

9 Usifukize uvumba mwingine wo wote juu ya madhabahu hii au sadaka nyingine yo yote ya kuteketezwa wala sadaka ya nafaka, wala usimimine sadaka ya kinywaji juu yake.

10 Mara moja kwa mwaka Aroni atafanya upatanisho juu ya pembe za hiyo madhabahu. Upatanisho huu wa mwaka lazima ufanywe kwa damu ya sadaka ya upatanisho kwa ajili ya dhambi kwa vizazi vijavyo. Ni takatifu sana kwaBwana.”

Fedha Ya Upatanisho

11 NayeBwanaakamwambia Mose,

12 “Utakapowahesabu Waisraeli, kila mmoja lazima alipe kwaBwanafidia kwa ajili ya nafsi yake wakati wa kuhesabiwa kwake. Ndipo hakutakuwa na pigo juu yao unapowahesabu.

13 Kila mmoja anayekwenda upande wa wale waliokwisha hesabiwa atatoa nusu shekeli, kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, ambayo ina uzito wa gera ishirini. Hii nusu shekeli ni sadaka kwaBwana.

14 Wote wale wanaovuka, wenye umri wa miaka ishirini au zaidi, watatoa sadaka kwaBwana.

15 Matajiri hawatalipa zaidi ya nusu shekeli, nao maskini hawatatoa pungufu wakati mnatoa sadaka kwaBwanakwa kufanya upatanisho wa nafsi zenu.

16 Utapokea fedha ya upatanisho kutoka kwa Waisraeli na uzitumie kwa ajili ya huduma ya Hema la Kukutania. Itakuwa ni ukumbusho kwa Waisraeli mbele zaBwanakufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu.”

Sinia La Kunawia

17 KishaBwanaakamwambia Mose,

18 “Tengeneza sinia la shaba, lenye kishikilio cha shaba kwa ajili ya kunawia. Liweke kati ya Hema la Kukutania na madhabahu, kisha weka maji ndani yake.

19 Aroni na wanawe watanawa mikono na miguu yao kwa maji yatokayo katika hilo sinia.

20 Wakati wo wote wanapoingia katika Hema la Kukutania, watanawa kwa maji ili kwamba wasije wakafa. Pia, wanapokaribia madhabahu ili kuhudumu kwa kuleta sadaka zilizotolewa kwaBwanakwa moto,

21 watanawa mikono na miguu yao ili kwamba wasije wakafa. Hii itakuwa ni amri ya kudumu kwa ajili ya Aroni na wazao wake kwa vizazi vijavyo.”

Mafuta Ya Upako

22 KishaBwanaakamwambia Mose,

23 “Chukua vikolezi bora vifuatavyo: shekeli 500za manemane ya maji, shekeli 250za mdalasini wenye harufu nzuri, shekeli 250 za miwa yenye harufu nzuri,

24 shekeli 500 za aina nyingine ya mdalasini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, pia hiniya mafuta ya zeituni.

25 Vikolezi hivi vitengeneze kuwa mafuta matakatifu ya upako yenye harufu nzuri, kazi ya mtengeneza manukato. Yatakuwa mafuta matakatifu ya upako.

26 Kisha yatumie kupaka hilo Hema la Kukutania, Sanduku la Ushuhuda,

27 meza na vifaa vyake vyote, kinara cha taa na vifaa vyake vyote, madhabahu ya kufukizia uvumba,

28 madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na vyombo vyake vyote na sinia pamoja na kitako chake.

29 Utaviweka wakfu ili viwe vitakatifu sana na kila kitakachoigusa kitakuwa kitakatifu.

30 “Mtie Aroni na wanawe mafuta na uwaweke wakfu ili waweze kunitumikia katika kazi ya ukuhani.

31 Waambie Waisraeli, ‘Haya yatakuwa mafuta matakatifu yangu ya upako kwa vizazi vijavyo.

32 Usiyamimine juu ya miili ya wanadamu wala usitengeneze mafuta ya aina nyingine kwa utaratibu huu. Ni mafuta matakatifu na ni lazima myaone kuwa ni matakatifu.

33 Mtu ye yote atakayetengeneza manukato kama hayo na ye yote atakayeyamimina juu ya mtu ye yote ambaye si kuhani atakatiliwa mbali na watu wake.’ ”

Uvumba

34 KishaBwanaakamwambia Mose, “Chukua vikolezi vyenye harufu nzuri vifuatavyo: natafi, shekelethi, kelbena na uvumba safi vyote vikiwa na vipimo sawa,

35 pia tengeneza mchanganyiko wa uvumba wenye harufu nzuri, kazi ya mtengeneza manukato. Utiwe chumvi ili upate kuwa safi na mtakatifu.

36 Saga baadhi yake kuwa unga na uweke mbele ya Sanduku la Ushuhuda ndani ya Hema la Kukutania, mahali ambapo nitakutana nawe. Itakuwa takatifu sana kwenu.

37 Msitengeneze uvumba mwingine wo wote wa namna hii kwa ajili yenu wenyewe; uoneni kuwa ni mtakatifu kwaBwana.

38 Ye yote atakayetengeneza uvumba kama huu ili kufurahia harufu yake nzuri lazima akatiliwe mbali na watu wake.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EXO/30-f855ef22ca0022d537eab1870226f7ba.mp3?version_id=1627—

Kutoka 31

Bezaleli Na Oholiabu

1 NdipoBwanaakamwambia Mose,

2 “Tazama, nimemchagua Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda,

3 nami nimemjaza Roho wa Mungu, pamoja na ustadi, uwezo na maarifa katika aina zote za ufundi,

4 ili kubuni kazi za ustadi katika ufundi wa dhahabu, fedha na shaba,

5 kuchonga vito vya kutia mahali, kufanya kazi kwa mbao na kujishughulisha na aina zote za ufundi.

6 Tena nimemweka Oholiabu mwana wa Ahisamaki, wa kabila la Dani, ili kumsaidia. Pia mafundi wote nimewapa ustadi wa kufanya kila kitu nilichokuamuru wewe:

7 Hema la Kukutania, Sanduku la Ushuhuda pamoja na kiti cha rehema juu yake, pia na vifaa vyote vya kwenye hema,

8 meza na vifaa vyake, kinara cha taa cha dhahabu safi na vifaa vyake vyote, madhabahu ya kufukizia uvumba,

9 madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na vyombo vyake vyote, sinia na kinara chake,

10 pamoja na mavazi matakatifu yaliyofumwa ya kuhani Aroni, na mavazi kwa ajili ya wanawe wakati wanahudumu katika kazi ya ukuhani,

11 pia mafuta ya upako na uvumba wenye harufu nzuri kwa ajili ya Mahali Patakatifu. Watavitengeneza sawasawa kama vile nilivyokuagiza wewe.”

Sabato

12 KishaBwanaakamwambia Mose,

13 “Waambie Waisraeli, ‘Ninyi ni lazima mzishike Sabato zangu. Hii itakuwa ni ishara kati yangu na ninyi kwa ajili ya vizazi vijavyo, ili mpate kujua kwamba Mimi NdimiBwana, niwafanyaye ninyi watakatifu.

14 “ ‘Mtaishika Sabato, kwa sababu ni takatifu kwenu. Ye yote atakayeinajisi lazima auawe, ye yote atakayefanya kazi siku hiyo lazima akafie mbali na watu wake.

15 Kwa siku sita, mtafanya kazi, lakini siku ya saba ni Sabato ya kupumzika, takatifu kwaBwana. Ye yote afanyaye kazi yo yote siku ya Sabato ni lazima auawe.

16 Waisraeli wataishika Sabato, kuiadhimisha kwa vizazi vijavyo kuwa Agano la milele.

17 Itakuwa ishara kati yangu na Waisraeli milele, kwa kuwa kwa muda wa siku sitaBwanaaliumba mbingu na dunia, na siku ya saba akaacha kufanya kazi, akapumzika.’ ”

18 Bwanaalipomaliza kusema na Mose juu ya Mlima Sinai, Mungu akampa vile vibao viwili vya Ushuhuda, vibao vya mawe vilivyoandikwa kwa kidole cha Mungu.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EXO/31-8f2f95bdae8eb4a879dd1078b469e814.mp3?version_id=1627—