Mwanzo 2

1 Kwa hiyo mbingu na dunia zikakamilika, pamoja na vyote vilivyomo.

2 Katika siku ya saba Mungu alikuwa amekamilisha kazi aliyokuwa akiifanya, hivyo siku ya saba akapumzika kutoka kazi zake zote.

3 Mungu akaibariki siku ya saba akaifanya takatifu, kwa sababu katika siku hiyo alipumzika kutoka kazi zote za kuumba alizokuwa amefanya.

Adamu Na Eva

4 Haya ndiyo maelezo ya mbingu na dunia wakati zilipoumbwa.

BwanaMungu alipoziumba mbingu na dunia,

5 hapakuwepo na mche wa shambani uliokuwa umejitokeza ardhini, wala hapakuwepo na mmea wa shamba uliokuwa umeota, kwa kuwaBwanaMungu alikuwa hajanyeshea mvua juu ya nchi, na hapakuwepo mtu wa kuilima ardhi,

6 lakini umande ulitokeza kutoka ardhini na kunyesha uso wote wa nchi:

7 BwanaMungu alimuumba mtu kutoka mavumbiya ardhi, akampulizia pumzi ya uhai puani mwake, mtu akawa kiumbe hai.

8 BasiBwanaMungu alikuwa ameotesha bustani upande wa mashariki, katika Edeni, huko akamweka huyo mtu aliyemuumba.

9 BwanaMungu akafanya aina zote za miti ziote kutoka ardhini, miti yenye kupendeza macho na mizuri kwa chakula. Katikati ya bustani ulikuwepo mti wa uzima na mti wa ujuzi wa mema na mabaya.

10 Mto wa kunyeshea bustani ulitiririka toka Edeni, kuanzia hapa ukagawanyika kuwa mito minne.

11 Mto wa kwanza uliitwa Pishoni, nao huzunguka nchi yote ya Havila ambako kuna dhahabu.

12 (Dhahabu ya nchi hiyo ni nzuri, lulu na vito shohamu pia hupatikana huko.)

13 Jina la mto wa pili ni Gihoni, ambao huzunguka nchi yote ya Kushi.

14 Jina la mto wa tatu ni Tigrisi, unaopita mashariki ya Ashuru. Mto wa nne ni Eufrati.

15 BwanaMungu akamchukua huyo mtu, akamweka kwenye Bustani ya Edeni ailime na kuitunza.

16 BwanaMungu akamwagiza huyo mtu, akamwambia, “Uko huru kula matunda ya mti wo wote katika bustani,

17 lakini kamwe usile matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, kwa maana siku utakapokula matunda yake, hakika utakufa.”

18 BwanaMungu akasema, “Si vyema huyu mtu awe peke yake. Nitamfanyia msaidizi wa kumfaa.”

19 BasiBwanaMungu alikuwa amefanyiza kutoka katika ardhi wanyama wote wa porini na ndege wote wa angani. Akawaleta kwa huyu mtu aone atawaitaje, nalo jina lo lote alilokiita kila kiumbe hai, likawa ndilo jina lake.

20 Hivyo Adamu akawapa majina wanyama wote wa kufugwa, ndege wa angani, na wanyama wote wa porini.

Lakini kwa Adamu hakupatikana msaidizi wa kumfaa.

21 HivyoBwanaMungu akamfanya Adamu kulala usingizi mzito, naye alipokuwa amelala akachukua moja ya mbavu zake, akapafunika mahali pale kwa nyama.

22 KishaBwanaMungu akamfanya mwanamke kutoka kwenye ule ubavu aliouchukua kutoka kwa huyo mwanaume, akamleta huyo mwanamke kwa huyo mwanaume.

23 Huyo mwanaume akasema,

“Huyu sasa ni mfupa wa mifupa yangu

na nyama ya nyama yangu,

# ataitwa ‘mwanamke,’

kwa kuwa alitolewa katika mwanaume.”

24 Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.

25 Adamu na mkewe wote wawili walikuwa uchi, wala hawakuona aibu.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/GEN/2-2d1cbbd845aaad2395f2bf2bd55363d5.mp3?version_id=1627—

Mwanzo 3

Anguko La Mwanadamu

1 Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa porini ambaoBwanaMungu aliwafanya. Nyoka akamwambia mwanamke, “Ati kweli Mungu alisema, ‘Kamwe msile matunda ya mti wo wote wa bustanini’?”

2 Mwanamke akamjibu nyoka, “Tunaweza kula matunda ya miti iliyoko bustanini,

3 lakini Mungu alisema, ‘Kamwe msile tunda la mti ulio katikati ya bustani, wala msiguse kabisa, la sivyo mtakufa.’ ”

4 Lakini nyoka akamwambia mwanamke, “Hakika hamtakufa.

5 Kwa maana Mungu anajua ya kuwa wakati mtakapoyala macho yenu yatafumbuliwa, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.”

6 Mwanamke alipoona ya kuwa tunda la mti huo lilikuwa zuri kwa chakula na la kupendeza macho, tena linatamanika kwa kujipatia hekima, basi akachuma katika matunda yake, akala, pia akampa mumewe, aliyekuwa pamoja naye, naye akala.

7 Ndipo macho yao wote wawili yakafumbuliwa, wakajiona kwamba walikuwa uchi; hivyo wakashona majani ya mtini, wakajifunika.

8 Ndipo yule mwanaume na mkewe, waliposikia sauti yaBwanaMungu alipokuwa akitembea bustanini wakati wa utulivu wa jioni, wakajificha kutoka mbele zaBwanaMungu katikati ya miti ya bustani.

9 LakiniBwanaMungu akamwita Adamu, “Uko wapi?”

10 Naye akajibu, “Nilikusikia katika bustani nikaogopa kwa sababu nilikuwa uchi, hivyo nikajificha.”

11 Mungu akamwuliza, “Ni nani aliyekuambia yakuwa ulikuwa uchi? Je, umekula matunda ya mti niliokuamuru usile?”

12 Adamu akasema, “Huyu mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa sehemu ya tunda kutoka kwenye huo mti, nami nikala.”

13 NdipoBwanaMungu akamwuliza mwanamke, “Ni nini hili ambalo umelifanya?” Mwanamke akajibu, “Nyoka alinidanganya, nami nikala.”

14 HivyoBwanaMungu akamwambia nyoka, “Kwa kuwa umefanya hili,

“Umelaaniwa kuliko wanyama wote

wa kufugwa na wa porini!

Utatambaa kwa tumbo lako

na kula mavumbi

siku zote za maisha yako.

15 Nami nitaweka uadui

kati yako na huyo mwanamke,

na kati ya uzao wako na wake,

huo atakuponda kichwa,

nawe utamgonga kisigino.”

16 Kwa mwanamke akasema,

“Nitakuzidishia sana utungu wakati wa kuzaa kwako;

kwa utungu utazaa watoto.

Tamaa yako itakuwa kwa mumeo

naye atakutawala.”

17 Kwa Adamu akasema, “Kwa sababu umemsikiliza mke wako na ukala kutoka kwenye mti niliokuamuru, ‘Msile tunda lake,’

“Ardhi imelaaniwa kwa sababu yako,

kwa kazi ngumu utakula chakula kitokacho humo

siku zote za maisha yako.

18 Itazaa miiba na mibaruti kwa ajili yako,

nawe utakula mimea ya shambani.

19 Kwa jasho la uso wako

utakula chakula chako

hadi utakaporudi ardhini,

kwa kuwa ulitwaliwa kutoka humo,

kwa kuwa wewe u mavumbi

na mavumbini wewe utarudi.”

20 Adamu akamwita mkewe Eva, kwa kuwa atakuwa mama wa wote walio hai.

21 BwanaMungu akawatengenezea Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika.

22 KishaBwanaMungu akasema, “Sasa mtu huyu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya. Sharti asiruhusiwe kunyosha mkono wake na kuchuma pia kutoka katika mti wa uzima akala, naye akaishi milele.”

23 HivyoBwanaMungu akamfukuzia mbali kutoka Bustani ya Edeni, akalime ardhi ambamo alitolewa.

24 Baada ya kumfukuzia mbali Adamu, Mungu akaweka makerubi mashariki ya Bustani ya Edeni, pamoja na upanga wa moto ukimulika huku na huko kulinda njia ya kuuendea mti wa uzima.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/GEN/3-d3efac989f195a73d84da1fe1f568963.mp3?version_id=1627—

Mwanzo 4

Kaini Na Abeli

1 Adamu akakutana kimwili na mkewe Eva, akapata mimba, akamzaa Kaini. Eva akasema, “Kwa msaada waBwananimemzaa mwanaume.”

2 Baadaye akamzaa Abeli ndugu yake.

Basi Abeli akawa mfugaji, na Kaini akawa mkulima.

3 Baada ya muda Kaini akaleta baadhi ya mazao ya shamba kama sadaka kwaBwana.

4 Lakini Abeli akaleta fungu nono kutoka katika baadhi ya wazaliwa wa kwanza wa mifugo yake.Bwanaakamkubali Abeli pamoja na sadaka yake,

5 lakini Mungu hakumkubali Kaini pamoja na sadaka yake. Kwa hiyo Kaini akakasirika sana, uso wake ukawa na huzuni.

6 KishaBwanaakamwambia Kaini, “Kwa nini umekasirika? Kwa nini uso wako una huzuni?

7 Ukifanya lililo sawa, hutakubalika? Lakini usipofanya lililo sawa, dhambi inakuvizia mlangoni mwako, inakutamani wewe, lakini inakupasa uishinde.”

8 Basi Kaini akamwambia ndugu yake Abeli, “Twende shambani.” Walipokuwa shambani, Kaini akamshambulia Abeli ndugu yake, akamwua.

9 KishaBwanaakamwuliza Kaini, “Ndugu yako Abeli yuko wapi?”

Akamjibu, “Sijui, je, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?”

10 Bwanaakasema, “Umefanya nini? Sikiliza! Damu ya ndugu yako inanililia mimi kutoka ardhini.

11 Sasa umelaaniwa na umehamishwa kutoka katika ardhi, ambayo imefungua kinywa chake na kupokea damu ya ndugu yako kutoka mkononi mwako.

12 Utakapoilima ardhi, haitakupa tena mazao yake. Utakuwa mtu wa kutangatanga duniani asiye na utulivu.”

13 Kaini akamwambiaBwana, “Adhabu yangu ni zaidi ya niwezavyo kustahimili.

14 Leo unanifukuza kutoka katika nchi, nami nitafichwa mbali na uwepo wako. Nitakuwa mtu wa kutangatanga asiyetulia duniani na ye yote anionaye ataniua.”

15 LakiniBwanaakamwambia, “La sivyo, ikiwa mtu ye yote atamwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba zaidi.” KishaBwanaakamwekea Kaini alama ili mtu ye yote ambaye angemwona asimwue.

16 Kwa hiyo Kaini akaondoka mbele zaBwanaakaenda kuishi katika nchi ya Nodi, iliyoko mashariki ya Edeni.

17 Kaini akakutana kimwili na mkewe, naye akapata mimba na akamzaa Enoki. Wakati huo Kaini alikuwa anajenga mji, akauita Enoki jina la mtoto wake.

18 Enoki akamzaa Iradi, Iradi akamzaa Mehuyaeli, Mehuyaeli akamzaa Methushaeli, na Methushaeli akamzaa Lameki.

19 Lameki alioa wanawake wawili, mmoja aliitwa Ada, na mwingine Sila.

20 Ada akamzaa Yabali ambaye ni baba wa wale walioishi katika mahema na kufuga wanyama.

21 Kaka yake aliitwa Yubali, aliyekuwa baba wa wote wapigao zeze na filimbi.

22 Pia Sila alikuwa na mtoto wa kiume aliyeitwa Tubali-Kaini ambaye alifua vifaa vya aina mbalimbali vya shaba na chuma. Naama alikuwa dada wa Tubali-Kaini.

23 Lameki akawaambia wake zake,

“Ada na Sila nisikilizeni mimi;

wake wa Lameki sikieni maneno yangu.

Nimemwua mtu kwa kunijeruhi,

kijana mdogo kwa kuniumiza.

24 Kama Kaini atalipizwa kisasi mara saba,

basi Lameki itakuwa mara sabini na saba.”

25 Adamu akakutana kimwili na mke wake tena, akamzaa mwana, akamwita Sethi, akisema, “Mungu amenijalia mwana mwingine badala ya Abeli, kwa kuwa Kaini alimwua.”

26 Pia Sethi akamzaa mwana, akamwita Enoshi.

Wakati huo watu wakaanza kuliitia jina laBwana.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/GEN/4-84fb547288756e1086109815d6509031.mp3?version_id=1627—

Mwanzo 5

Kutoka Adamu Hadi Noa

1 Hii ni orodha iliyoandikwa ya vizazi vya Adamu.

Wakati Mungu alipomuumba Adamu, alimfanya kwa sura ya Mungu.

2 Aliwaumba mwanaume na mwanamke, akawabariki. Walipokwisha kuumbwa akawaita “Mwanadamu.”

3 Adamu alipokuwa ameishi miaka 130, alikuwa na mwana aliyekuwa na sura yake, mwenye kufanana naye. Akamwita Sethi.

4 Baada ya Sethi kuzaliwa, Adamu aliishi miaka 800, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.

5 Adamu aliishi jumla ya miaka 930, ndipo akafa.

6 Sethi alipokuwa ameishi miaka 105, akamzaa Enoshi.

7 Baada ya kumzaa Enoshi, Sethi aliishi miaka 807, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.

8 Sethi aliishi jumla ya miaka 912, ndipo akafa.

9 Enoshi alipokuwa ameishi miaka tisini, akamzaa Kenani.

10 Baada ya kumzaa Kenani, Enoshi aliishi miaka 815, naye alikuwa na watoto wengine wa kiume na wa kike.

11 Enoshi aliishi jumla ya miaka 905, ndipo akafa.

12 Kenani alipokuwa ameishi miaka sabini, akamzaa Mahalaleli.

13 Baada ya kumzaa Mahalaleli, Kenani aliishi miaka 840, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.

14 Kenani aliishi jumla miaka 910, ndipo akafa.

15 Mahalaleli alipokuwa ameishi miaka sitini na mitano, akamzaa Yaredi.

16 Baada ya kumzaa Yaredi, Mahalaleli aliishi miaka 830, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.

17 Mahalaleli aliishi jumla ya miaka 895, ndipo akafa.

18 Yaredi alipokuwa ameishi miaka 162, akamzaa Enoki.

19 Baada ya kumzaa Enoki, Yaredi aliishi miaka 800, naye akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.

20 Yaredi aliishi jumla ya miaka 962, ndipo akafa.

21 Enoki alipokuwa ameishi miaka sitini na mitano, akamzaa Methusela.

22 Baada ya kumzaa Methusela, Enoki alitembea na Mungu miaka 300, na akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.

23 Enoki aliishi jumla ya miaka 365.

24 Enoki akatembea na Mungu, kisha akatoweka, kwa sababu Mungu alimchukua.

25 Mathusela alipokuwa ameishi miaka 187, akamzaa Lameki.

26 Baada ya kumzaa Lameki, Methusela aliishi miaka 782, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.

27 Methusela aliishi jumla ya miaka 969, ndipo akafa.

28 Lameki alipokuwa ameishi miaka 182, alimzaa mwana.

29 Akamwita jina lake Noa, akasema, “Yeye ndiye atakayetufariji katika kazi na maumivu makali ya mikono yetu yaliyosababishwa na ardhi iliyolaaniwa naBwana.”

30 Baada ya Noa kuzaliwa, Lameki aliishi miaka 595, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.

31 Aliishi jumla ya miaka 777, ndipo akafa.

32 Baada ya Noa kuishi miaka 500, aliwazaa Shemu, Hamu na Yafethi.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/GEN/5-1a026391c0a934a9d29f79ed31e98036.mp3?version_id=1627—

Mwanzo 6

Sababu Za Gharika

1 Watu walipoanza kuongezeka idadi katika uso wa dunia na watoto wa kike wakazaliwa kwao,

2 wana wa Mungu wakawaona kuwa hao binti za wanadamu walikuwa wazuri wa sura, wakaoa ye yote miongoni mwao waliyemchagua.

3 NdipoBwanaakasema, “Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye ni wa kufa, siku zake zitakuwa miaka 120.”

4 Wanefili walikuwako duniani siku hizo, na baadaye, hao wana wa Mungu walipoingia kwa hao binti za wanadamu na kuzaa nao. Wanefili walikuwa mashujaa na watu waliojulikana wa zamani hizo.

5 Bwanaakaona jinsi ambavyo uovu wa mwanadamu umekuwa mkubwa duniani na ya kuwa kila mwelekeo wa mawazo ya moyo wake wakati wote ulikuwa mbaya tu.

6 Bwanaakasikitika kwamba alimuumba mwanadamu duniani, moyo wa Mungu ukajaa masikitiko.

7 Kwa hiyoBwanaakasema, “Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba kutoka kwenye uso wa dunia, wanadamu na wanyama, pamoja na viumbe vitambaavyo na ndege wa angani. Kwa maana nasikitika kwa kuwaumba.”

8 Lakini Noa akapata kibali machoni paBwana.

9 Hivi ndivyo vizazi vya Noa.

Noa alikuwa mtu wa haki, asiye na lawama miongoni mwa watu wa wakati wake, tena alitembea na Mungu.

10 Noa alikuwa na wana watatu: Shemu, Hamu na Yafethi.

11 Wakati huu dunia ilikuwa imejaa uharibifu na jeuri machoni pa Mungu.

12 Mungu akaona jinsi dunia ilivyoharibika, kwa maana watu wote duniani walikuwa wameharibu njia zao.

13 Kwa hiyo Mungu akamwambia Noa, “Nitawaangamiza watu wote, kwa kuwa dunia imejaa jeuri kwa sababu yao. Hakika mimi nitaangamiza watu pamoja na dunia.

14 Kwa hiyo jitengenezee safina kubwa kwa mbao za mvinje, tengeneza vyumba ndani yake na uipake lami ndani na nje.

15 Hivi ndivyo utakavyoitengeneza: Safina iwe na urefu wa dhiraa 300, upana wake dhiraa hamsini, na kimo chake dhiraa thelathini.

16 Itengenezee paa na umalizie safina kwa kuacha nafasi ya dhiraa mojajuu. Weka mlango ubavuni mwa safina, na uifanye ya ghorofa ya chini, ya kati na ya juu.

17 Nitaleta gharika ya maji juu ya nchi ili kuangamiza uhai wote chini ya mbingu, kila kiumbe chenye pumzi ya uhai ndani yake. Kila kitu juu ya nchi kitaangamia.

18 Lakini Mimi nitaweka Agano langu na wewe, nawe utaingia ndani ya Safina, wewe pamoja na mke wako, wanao na wake zao.

19 Utaingiza ndani ya Safina kila aina ya kiumbe hai wawili wawili, wa kiume na wa kike, ili kuwahifadhi hai pamoja na wewe.

20 Wawili wa kila aina ya ndege, wa kila aina ya mnyama na wa kila aina ya kitambaacho ardhini watakuja kwako ili wahifadhiwe hai.

21 Utachukua kila aina ya chakula kitakacholiwa, na ukiweke akiba kama chakula kwa ajili yako na yao.”

22 Noa akafanya kila kitu sawasawa kama vile Mungu alivyomwamuru.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/GEN/6-611272bc888c83c0befacf24bb734d95.mp3?version_id=1627—

Mwanzo 7

Gharika

1 NdipoBwanaakamwambia Noa, “Ingia katika safina wewe na jamaa yako yote, kwa sababu katika kizazi hiki nimeona ya kuwa wewe ni mwenye haki.

2 Uchukue wanyama saba walio safi wa kila aina, wa kiume na wa kike na wanyama wawili wawili wa kila aina walio najisi wa kiume na wa kike.

3 Pia uchukue ndege saba walio safi wa kila aina, wa kiume na wa kike, ili kuhifadhi aina zao mbalimbali katika dunia yote.

4 Siku saba tangu sasa nitaleta mvua juu ya nchi kwa siku arobaini mchana na usiku, nami nitafutilia mbali kutoka katika uso wa nchi kila kiumbe hai nilichokiumba.”

5 Noa akafanya yote kamaBwanaalivyomwamuru.

6 Noa alikuwa na miaka 600 gharika ilipokuja juu ya dunia.

7 Noa na mkewe na wanawe na wake zao wakaingia katika safina ili waepuke ile gharika.

8 Jozi ya wanyama wasio najisi na walio najisi, ndege na viumbe vita ambaavyo,

9 wa kiume na wa kike, walikuja kwa Noa wakaingia katika safina kama Mungu alivyomwamuru Noa.

10 Baada ya siku zile saba maji ya gharika yakaja juu ya dunia.

11 Katika siku ya kumi na saba ya mwezi wa pili mwaka wa 600 wa kuishi kwake Noa, siku hiyo ndipo chemchemi zote hata zilizo chini sana ya ardhi zilibubujika kwa nguvu, na malango ya mafuriko ya mbinguni yakafunguliwa.

12 Mvua ikanyesha juu ya nchi siku arobaini mchana na usiku.

13 Siku hiyo Noa, na mkewe, na wanawe Shemu, Hamu na Yafethi pamoja na wake zao wakaingia katika ile safina.

14 Nao walikuwa pamoja na kila mnyama wa mwituni kufuatana na aina yake, wanyama wote wafugwao kufuatana na aina zao, kila kiumbe kitambaacho juu ya ardhi kwa aina yake, kila ndege kufuatana na aina yake kila kiumbe chenye mabawa.

15 Viumbe vyote vyenye pumzi ya uhai ndani yake vikaja kwa Noa viwili viwili, vikaingia katika safina.

16 Wanyama walioingia katika safina walikuwa wa kiume na wa kike, wa kila kiumbe chenye uhai kama Mungu alivyomwamuru Noa, ndipoBwanaakamfungia ndani.

17 Kwa siku arobaini mafuriko yaliendelea kujaa duniani na maji yalivyozidi kuongezeka, yaliinua safina juu sana kutoka kwenye uso wa nchi.

18 Maji yakajaa na kuongezeka sana juu ya nchi, na safina ikaelea juu ya uso wa maji.

19 Maji yakazidi kujaa juu ya nchi, yakaifunika milima yote mirefu chini ya mbingu yote.

20 Maji yakaendelea kujaa yakaifunika milima kwa kina cha zaidi ya dhiraa kumi na tano.

21 Kila kiumbe hai kitambaacho juu ya nchi kikaangamia: Ndege, wanyama wa kufugwa, wanyama pori, viumbe vyote juu ya nchi na wanadamu wote.

22 Kila kiumbe juu ya nchi kavu chenye pumzi ya uhai kikafa.

23 Kila kitu chenye uhai juu ya uso wa nchi kilifutiliwa mbali, watu, wanyama, viumbe vitambaavyo na ndege warukao angani wakafutiliwa mbali toka duniani. Waliobaki ni Noa peke yake na wale waliokuwa pamoja naye ndani ya safina.

24 Maji yakaifunika dunia kwa siku 150.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/GEN/7-874c521a5d2bae9b59e933adf27e40cb.mp3?version_id=1627—

Mwanzo 8

Mwisho Wa Gharika

1 Mungu akamkumbuka Noa na wanyama wote wa porini na wa kufugwa waliokuwa naye ndani ya safina, akatuma upepo ukavuma katika dunia, nayo maji yakaondoka.

2 Zile chemchemi zilizo chini sana ya ardhi pamoja na malango ya mafuriko ya mbinguni yakawa yamefungwa nayo mvua ikawa imekoma kunyesha kutoka angani.

3 Maji yakaendelea kupungua taratibu katika nchi. Kunako mwisho wa siku ya 150, maji yalikuwa yamepungua,

4 katika siku ya kumi na saba ya mwezi wa saba, safina ikatua katika milima ya Ararati.

5 Maji yakaendelea kupungua hadi mwezi wa kumi, na siku ya kwanza ya mwezi wa kumi, vilele vya milima vikaonekana.

6 Baada ya siku arobaini Noa akafungua dirisha alilokuwa amelifanya katika safina

7 na akamtoa kunguru, akawa akiruka kwenda na kurudi mpaka maji yalipokwisha kukauka juu ya nchi.

8 Kisha akamtoa hua ili aone kama maji yameondoka juu ya uso wa ardhi.

9 Lakini hua hakupata mahali pa kutua kwa kuwa maji yalienea juu ya uso wa dunia yote, kwa hiyo akarudi kwa Noa ndani ya safina. Noa akanyoosha mkono akamchukua yule hua akamrudisha ndani ya safina.

10 Noa akangojea siku saba zaidi kisha akamtoa tena hua kutoka katika safina.

11 Wakati hua aliporejea kwa Noa jioni, alikuwa amechukua katika mdomo wake jani bichi la mzeituni, lililochumwa wakati ule ule! Ndipo Noa akajua ya kuwa maji yameondoka juu ya uso wa dunia.

12 Akangojea siku saba zaidi na akamtuma tena hua, lakini wakati huu hua hakurudi tena kwa Noa.

13 Katika siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza ya mwaka 601, wa kuishi kwake Noa, maji yalikuwa yamekauka duniani. Kisha Noa akafungua mlango wa safina akaona ya kuwa uso wa ardhi ulikuwa umekauka.

14 Katika siku ya ishirini na saba ya mwezi wa pili dunia ilikuwa imekauka kabisa.

15 Ndipo Mungu akamwambia Noa,

16 “Toka ndani ya safina, wewe na mkeo na wanao na wake zao.

17 Utoe nje kila aina ya kiumbe hai aliye pamoja nawe: Ndege, wanyama na viumbe vyote vitambaavyo juu ya ardhi, ili wakazae, na kuongezeka na kuijaza tena dunia.”

18 Kwa hiyo Noa akatoka nje pamoja na mkewe, wanawe na wake zao.

19 Wanyama wote na viumbe vyote vitambaavyo juu ya ardhi na ndege wote, kila kitu kiendacho juu ya nchi, aina moja baada ya nyingine vikatoka katika safina, kila aina ya kiumbe, kimoja baada ya kingine.

Noa Atoa Dhabihu

20 Kisha Noa akamjengeaBwanamadhabahu, akachukua baadhi ya wale wanyama wote wasio najisi na ndege wasio najisi, akatoa sadaka ya kuteketezwa juu ya madhabahu.

21 Bwanaakasikia harufu nzuri ya kupendeza, naye akasema moyoni mwake, “Kamwe sitailaani tena ardhi kwa sababu ya mwanadamu, hata ingawaje kila mwelekeo wa moyo wake ni mbaya tangu ujana. Kamwe sitaangamiza tena viumbe hai vyote kama nilivyofanya.”

22 “Kwa muda dunia idumupo,

wakati wa kupanda na wa kuvuna,

wakati wa baridi na wa joto,

wakati wa kiangazi na wa masika,

mchana na usiku

kamwe havitakoma.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/GEN/8-2be6a936c3a1ee174d8e9adcb5e4b86b.mp3?version_id=1627—

Mwanzo 9

Mungu Aweka Agano Na Noa

1 Ndipo Mungu akambariki Noa na wanawe, akiwaambia, “Zaeni mkaongezeke kwa idadi na mkaijaze tena dunia.

2 Wanyama wote wa duniani, ndege wote wa angani, kila kiumbe kitambaacho juu ya ardhi, na samaki wote wa baharini wamekabidhiwa mikononi mwenu, nao watawaogopa na kuwahofu.

3 Kila kitu chenye uhai kiendacho kitakuwa chakula chenu. Kama vile nilivyowapa mimea mbalimbali, sasa nawapa kila kitu.

4 “Lakini kamwe msile nyama ambayo bado ina damu ya uhai wake, kwa maana damu ni uhai.

5 Hakika damu ya uhai wenu nitaidai. Nitaidai kutoka kwa kila mnyama. Kutoka kwa kila mwanadamu pia nitaidai kwa ajili ya uhai wa mtu mwenzake.

6 “Ye yote amwagaye damu ya mwanadamu,

damu yake itamwagwa na mwanadamu,

kwa kuwa katika mfano wa Mungu,

Mungu alimuumba mwanadamu.

7 Kuhusu ninyi, zaeni mwongezeke kwa wingi, mzidi katika dunia na kuijaza.”

8 Ndipo Mungu akamwambia Noa na wanawe pamoja naye:

9 “Sasa mimi ninaweka Agano langu nanyi, pamoja na uzao wenu baada yenu,

10 pia na kila kiumbe hai kilichokuwa pamoja nanyi: Ndege, wanyama wa kufugwa na wanyama wote wa porini, wale wote waliotoka katika safina pamoja nanyi, kila kiumbe hai duniani.

11 Ninaweka Agano nanyi: Kamwe uhai hautafutwa tena kwa gharika, kamwe haitakuwepo tena gharika ya kuangamiza dunia.”

12 Mungu akasema, “Hii ni ishara ya Agano ninalofanya kati yangu na ninyi na kila kiumbe hai kilicho pamoja nanyi, Agano kwa vizazi vyote vijavyo:

13 Nimeweka upinde wangu wa mvua mawinguni, nao utakuwa ishara ya Agano nifanyalo kati yangu na dunia.

14 Wakati wo wote ninapotanda mawingu juu ya dunia na upinde wa mvua ukijitokeza mawinguni,

15 nitakumbuka Agano langu kati yangu na ninyi na viumbe vyote vilivyo hai vya kila aina. Kamwe maji hayatakuwa tena gharika ya kuangamiza uhai wote.

16 Wakati wo wote upinde wa mvua unapotokea mawinguni, nitauona na kukumbuka Agano la milele kati ya Mungu na viumbe vyote vilivyo hai vya kila aina duniani.”

17 Hivyo Mungu akamwambia Noa, “Hii ndiyo ishara ya Agano ambalo nimelifanya kati yangu na viumbe vyote vilivyo hai duniani.”

Wana Wa Noa

18 Wana wa Noa waliotoka ndani ya safina ni: Shemu, Hamu na Yafethi. (Hamu ndiye aliyekuwa baba wa Kanaani.)

19 Hawa ndio waliokuwa wana watatu wa Noa, kutokana nao watu walienea katika dunia.

20 Noa akawa mkulima, akawa mtu wa kwanza kupanda mizabibu.

21 Alipokunywa huo mvinyo wake akalewa na akalala uchi kwenye hema lake.

22 Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake na kuwaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje.

23 Lakini Shemu na Yafethi wakachukua nguo wakaitanda mabegani mwao wote wawili, kisha wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao. Nyuso zao zilielekea upande mwingine ili wasiuone uchi wa baba yao.

24 Noa alipolevuka kutoka kwenye mvinyo wake na kujua lile ambalo mwanawe mdogo kuliko wote alilokuwa amemtendea,

25 akasema,

“Alaaniwe Kanaani!

Atakuwa mtumwa wa chini sana

kuliko watumwa wote kwa ndugu zake.”

26 Pia akasema,

“AbarikiweBwana, Mungu wa Shemu!

Kanaani na awe mtumwa wa Shemu.

27 Mungu na apanue mipaka ya Yafethi;

Yafethi na aishi katika mahema ya Shemu,

na Kanaani na awe mtumwa wake.”

28 Baada ya gharika Noa aliishi miaka 350.

29 Noa alikuwa na jumla ya miaka 950, ndipo akafa.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/GEN/9-aeeaed3f28c8c0a6df85c2bc1ed1ad83.mp3?version_id=1627—

Mwanzo 10

Mataifa Yaliyotokana Na Noa

1 Hawa ndio wazao wa Noa: Shemu, Hamu na Yafethi, ambao walizaa wana baada ya gharika.

Wazao Wa Yafethi

2 Wana wa Yafethi walikuwa:

Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi.

3 Wana wa Gomeri walikuwa:

Ashkenazi, Rifathi na Togarma.

4 Wana wa Yavani walikuwa:

Elisha, Tarshishi, Kitimu na Rodanimu.

5 (Kutokana na hawa mataifa ya Pwani yalienea katika nchi zao, kwa koo zao katika mataifa yao, kila moja kwa lugha yake lenyewe.)

Wazao Wa Hamu

6 Wana wa Hamu walikuwa:

Kushi, Misraimu, Putu na Kanaani.

7 Wana wa Kushi walikuwa:

Seba, Havila Sabta, Raama na Sabteka.

Wana wa Raama walikuwa:

Sheba na Dedani.

8 Kushi alikuwa baba yake Nimrodi, ambaye alikua akawa mtu shujaa mwenye nguvu duniani.

9 Alikuwa mwindaji hodari mbele zaBwana. Ndiyo sababu watu husema, “Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda mbele zaBwana.”

10 Vituo vyake vya kwanza katika ufalme wake vilikuwa Babeli, Ereki, Akadi na Kalne katika Shinari.

11 Kutoka katika nchi ile alikwenda Ashuru, ambako alijenga Ninawi, Rehobothiri, Kala

12 na Reseni, iliyo kati ya Ninawi na Kala; huo ndio mji mkubwa.

13 Misraimu alikuwa baba wa:

Waludi, Wanami, Walehabi, Wanaftuhi,

14 Wapathrusi, Wakasluhi (ambao Wafilisti walitokana nao) na Wakaftori.

15 Kanaani alikuwa baba wa:

Sidoni mzaliwa wake wa kwanza, Hethi,

16 Wayebusi, Waamori, Wagirgashi,

17 Wahivi, Waariki, Wasini,

18 Waarvadi, Wasemari na Wahamathi.

Baadaye koo za Wakanaani zilitawanyika,

19 na mipaka ya Kanaani ilienea kutoka Sidoni kuelekea Gerari hadi Gaza, kisha kuelekea Sodoma, Gomora, Adma na Seboimu, hadi kufikia Lasha.

20 Hawa ni wana wa Hamu kwa koo zao na lugha zao, katika nchi zao na mataifa yao.

Wazao Wa Shemu

21 Shemu ambaye ni ndugu mkubwa wa Yafethi, kwake kulizaliwa wana pia. Shemu alikuwa baba wa wana wote wa Eberi.

22 Wana wa Shemu walikuwa:

Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu.

23 Wana wa Aramu walikuwa:

Usi, Huli, Getheri na Mashi.

24 Arfaksadi alikuwa baba wa Sela,

naye Sela akamzaa Eberi.

25 Eberi akazaa wana wawili:

Mmoja aliitwa Pelegi, kwa kuwa katika wakati wake ndipo dunia ilipogawanyika; nduguye aliitwa Yoktani.

26 Yoktani alikuwa baba wa:

Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera,

27 Hadoramu, Uzali, Dikla,

28 Obali, Abimaeli, Seba,

29 Ofiri, Havila na Yobabi. Hawa wote walikuwa wana wa Yoktani.

30 Nchi waliyoishi ilienea toka Mesha kuelekea Sefari kwenye nchi ya vilima iliyoko mashariki.

31 Hao ndio wana wa Shemu kwa koo zao na lugha zao, katika nchi zao na mataifa yao.

32 Hizi ndizo koo za wana wa Noa, kufuatana na vizazi vyao, katika mataifa yao. Kutokana na hawa mataifa yalienea duniani kote baada ya gharika.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/GEN/10-1fd99e32014be110f3e0dad531912a2c.mp3?version_id=1627—

Mwanzo 11

Mnara Wa Babeli

1 Wakati huo dunia yote ilikuwa na lugha moja na msemo mmoja.

2 Watu walipoelekea upande wa mashariki, wakafika kwenye tambarare katika nchi ya Shinarinao wakaishi huko.

3 Wakasemezana wao kwa wao, “Njoni, tufyatue matofali na tuyachome vizuri kwa moto.” Walitumia matofali badala ya mawe, na lami kwa ajili ya kushikamanishia hayo matofali.

4 Ndipo wakasema, “Njoni, tujijengee mji wenye mnara ambao utafika hadi mbinguni, ili tujipatie jina tusije tukatawanyika usoni pa dunia yote.”

5 LakiniBwanaakashuka ili auone mji na mnara wanadamu waliokuwa wanaujenga.

6 Bwanaakasema, “Kama taifa moja wanaozungumza lugha moja wameanza kufanya hili, basi hakuna lo lote watakalopanga kufanya ambalo halitawezekana kwao.

7 Njoni, tushuke tuvuruge lugha yao ili wasielewane wao kwa wao.”

8 HivyoBwanaakawatawanya kutoka mahali pale kwenda katika dunia yote, nao wakaacha kuujenga huo mji.

9 Ndiyo maana pakaitwa Babeli, kwa sababu hapo ndipoBwanaalipoivuruga lugha ya dunia nzima. Kutoka hapoBwanaakawatawanya katika uso wa dunia yote.

Shemu Hadi Abramu

10 Hivi ndivyo vizazi vya Shemu.

Miaka miwili baada ya gharika, Shemu alipokuwa na miaka 100, akamzaa Arfaksadi.

11 Baada ya kumzaa Arfaksadi, Shemu aliishi miaka 500, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike.

12 Wakati Arfaksadi alipokuwa na miaka thelathini na mitano, akamzaa Sela.

13 Baada ya Arfaksadi kumzaa Sela, aliishi miaka 403, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike.

14 Sela alipokuwa na miaka thelathini, akamzaa Eberi.

15 Sela baada ya kumzaa Eberi, aliishi miaka 403, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike.

16 Eberi alipokuwa na miaka thelathini na minne, akamzaa Pelegi.

17 Baada ya Eberi kumzaa Pelegi, aliishi miaka 430, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike.

18 Pelegi alipokuwa na miaka thelathini, akamzaa Reu.

19 Baada ya Pelegi kumzaa Reu, aliishi miaka 209, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike.

20 Reu alipokuwa na miaka thelathini na miwili, akamzaa Serugi.

21 Baada ya Reu kumzaa Serugi, aliishi miaka 207, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike.

22 Serugi alipokuwa na miaka thelathini, akamzaa Nahori.

23 Baada ya Serugi kumzaa Nahori, aliishi miaka 200, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike.

24 Nahori alipokuwa na miaka ishirini na tisa, akamzaa Tera.

25 Baada ya Nahori kumzaa Tera, aliishi miaka 119, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike.

26 Tera alipokuwa na miaka sabini, akamzaa Abramu, Nahori na Harani.

Wazao Wa Tera

27 Hawa ndio wazao wa Tera.

Tera aliwazaa Abramu, Nahori na Harani. Harani akamzaa Loti.

28 Tera alipokuwa bado hai, Harani akafa huko Uru ya Wakaldayo, nchi alimozaliwa.

29 Abramu na Nahori walioa. Mke wa Abramu aliitwa Sarai, na mke wa Nahori aliitwa Milka; Milka na Iska walikuwa watoto wa Harani.

30 Sarai alikuwa tasa, hakuwa na watoto.

31 Tera akamchukua Abramu mwanawe, Loti mwana wa Harani mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka kwa pamoja katika Uru ya Wakaldayo kwenda nchi ya Kanaani. Lakini walipofika Harani, wakaishi huko.

32 Tera alikufa huko Harani akiwa na miaka 205.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/GEN/11-1db10e635fab98889cf22bfc2234ffd2.mp3?version_id=1627—