Mwanzo 12

Wito Wa Abramu

1 Bwanaakawa amemwambia Abramu, “Ondoka katika nchi yako, waache watu wako na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha.

2 “Mimi nitakufanya taifa kubwa

na nitakubariki,

Nitalikuza jina lako,

nawe utakuwa baraka.

3 Nitawabariki wale wanaokubariki,

na ye yote akulaaniye nitamlaani;

na kupitia kwako mataifa yote duniani

yatabarikiwa.”

4 Hivyo Abramu akaondoka kamaBwanaalivyokuwa amemwambia; naye Loti akaondoka pamoja naye. Wakati Abramu alipoitwa aondoke Harani, alikuwa na miaka sabini na mitano.

5 Abramu akamchukua Sarai mkewe pamoja na Loti mwana wa ndugu yake, mali zote walizokuwa nazo pamoja na watu aliokuwa amewapata huko Harani, wakasafiri mpaka nchi ya Kanaani, wakafika huko.

6 Abramu akasafiri katika nchi hiyo akafika huko Shekemu, mahali penye mti wa mwaloni ulioko More. Wakati huo Wakanaani walikuwa wanaishi katika nchi hiyo.

7 Bwanaakamtokea Abramu akamwambia, “Nitawapa uzao wako nchi hii.” Hivyo hapa Abramu akamjengeaBwanaaliyekuwa amemtokea madhabahu.

8 Kutoka huko Abramu akasafiri kuelekea kwenye vilima mashariki ya Betheli, naye akapiga hema huko, Betheli ikiwa upande wa magharibi na Ai upande wa mashariki. Huko alimjengeaBwanamadhabahu na akaliitia jina laBwana.

9 Kisha Abramu akasafiri kuelekea upande wa Negebu.

Abramu Katika Nchi Ya Misri

10 Basi kulikuwako na njaa katika nchi, naye Abramu akashuka kwenda Misri kukaa huko kwa muda, kwa maana njaa ilikuwa kali.

11 Alipokuwa karibu kuingia Misri, akamwambia Sarai mkewe, “Ninajua ya kwamba wewe ni mwanamke mzuri wa sura.

12 Wakati Wamisri watakapokuona, watasema, ‘Huyu ni mke wake.’ Ndipo wataniua, lakini wewe watakuacha hai.

13 Sema wewe ni dada yangu, ili nitendewe mema kwa ajili yako, na maisha yangu yatahifadhiwa kwa sababu yako.”

14 Abramu alipoingia Misri, Wamisri wakamwona Sarai kuwa ni mwanamke mzuri sana wa sura.

15 Maafisa wa Farao walipomwona, wakamsifia kwa Farao; ndipo Sarai akachukuliwa kwenda kwenye jumba lake la kifalme.

16 Kwa ajili ya Sarai, Farao akamtendea Abramu mema, akapata kondoo, ng’ombe, punda, ngamia na watumishi wa kiume na wa kike.

17 LakiniBwanaakamwadhibu Farao na nyumba yake kwa maradhi ya kufisha kwa sababu ya kumchukua Sarai, mke wa Abramu.

18 Ndipo Farao akamwita Abramu, akamwuliza, “Umenifanyia nini? Kwa nini hukuniambia ni mke wako?

19 Kwa nini ulisema, ‘Yeye ni dada yangu,’ hata nikamchukua kuwa mke wangu? Sasa basi, mke wako huyu hapa. Mchukue uende zako!”

20 Kisha Farao akawapa watu wake amri kuhusu Abramu, wakamsindikiza pamoja na mke wake na kila alichokuwa nacho.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/GEN/12-e048a7de7cef87af73314d799d493030.mp3?version_id=1627—

Mwanzo 13

Abramu Na Loti Watengana

1 Hivyo Abramu akakwea kutoka Misri kwenda Negebu, yeye na mkewe na kila kitu alichokuwa nacho, pia Loti akaenda pamoja naye.

2 Wakati huo Abramu alikuwa tajiri sana wa mifugo, fedha na dhahabu.

3 Kutoka Negebu, akapita mahali hadi mahali, hadi akafika Betheli, mahali hapo ambapo mwanzoni alipiga hema lake kati ya Betheli na Ai

4 hapo ambapo alikuwa amejenga madhabahu ya kwanza. Huko Abramu akaliitia jina laBwana.

5 Basi Loti, ambaye alikuwa anafuatana na Abramu, alikuwa pia na makundi ya mbuzi, kondoo, ng’ombe na mahema.

6 Lakini nchi haikuwatosha kukaa pamoja kwa ajili ya wingi wa mali zao.

7 Ukazuka ugomvi kati ya wachunga mifugo wa Abramu na wale wa Loti. Wakati huo, Wakanaani na Waperizi ndio waliokuwa wenyeji wa nchi hiyo.

8 Hivyo Abramu akamwambia Loti, “Pasiwe na ugomvi wo wote kati yangu na wewe, wala kati ya wachungaji wangu na wako, kwa kuwa sisi ni ndugu.

9 Je, nchi yote haiko mbele yako? Tutengane. Kama ukielekea kushoto, nitakwenda kulia; kama ukielekea kulia, mimi nitakwenda kushoto.”

10 Loti akatazama akaona lile bonde lote la Yordani kuwa lilikuwa na maji tele, kama bustani yaBwana, kama nchi ya Misri, kuelekea Soari. (Hii ilikuwa kablaBwanahajaharibu Sodoma na Gomora.)

11 Hivyo Loti akajichagulia bonde lote la Yordani, akaelekea upande wa mashariki. Watu hao wawili wakatengana:

12 Abramu akaishi katika nchi ya Kanaani, wakati Loti aliishi miongoni mwa miji ya lile bonde na kupiga mahema yake karibu na Sodoma.

13 Basi watu wa Sodoma walikuwa waovu, wakifanya sana dhambi dhidi yaBwana.

14 Baada ya Loti kuondokaBwanaakamwambia Abramu, “Ukiwa hapo ulipo, inua macho yako utazame kaskazini na kusini, mashariki na magharibi.

15 Nchi yote unayoiona nitakupa wewe na uzao wako hata milele.

16 Nitaufanya uzao wako uwe mwingi kama mavumbi ya nchi, hivyo kama kuna ye yote awezaye kuhesabu mavumbi, basi uzao wako utahesabika.

17 Ondoka, tembea katika marefu na mapana ya nchi, kwa maana ninakupa wewe.”

18 Basi Abramu akaondoa mahema yake, akaenda kuishi karibu na mialoni ya Mamre huko Hebroni, huko akamjengeaBwanamadhabahu.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/GEN/13-fd8cd4fb66a854ea4852303c95ddb7e2.mp3?version_id=1627—

Mwanzo 14

Abramu Amwokoa Loti

1 Wakati huu Amrafeli mfalme wa Shinari, Arioko mfalme wa Elasari, Kedorlaoma mfalme wa Elamu, na Tidali mfalme wa Goimu

2 kwa pamoja walikwenda kupigana vita dhidi ya Bera mfalme wa Sodoma, Birsha mfalme wa Gomora, Shinabu mfalme wa Adma, Shemeberi mfalme wa Seboimu, na mfalme wa Bela (yaani Soari).

3 Hawa wote waliotajwa mwishoni waliunganisha majeshi yao kutoka Bonde la Sidimu (yaani Bahari ya Chumvi).

4 Walikuwa wametawaliwa na Mfalme Kedorlaoma kwa miaka kumi na miwili, lakini mwaka wa kumi na tatu waliasi.

5 Mnamo mwaka wa kumi na nne, Mfalme Kedorlaoma na wafalme waliojiunga naye walikwenda kupigana na kuwashinda Warefai katika Ashtaroth-kanaimu, Wazuzi katika Hamu, Waemi katika Shawe-Kiriathaimu,

6 na Wahori katika nchi ya kilima cha Seiri, hadi El-Parani karibu na jangwa.

7 Kisha wakarudi wakaenda En-Misfati (yaani Kadeshi), wakashinda nchi yote ya Waamaleki, pamoja na Waamori waliokuwa wakiishi Hasason-Tamari.

8 Ndipo mfalme wa Sodoma, mfalme wa Gomora, mfalme wa Adma, mfalme wa Seboimu, na mfalme wa Bela (yaani Soari) wakatoka kupanga majeshi yao kwenye Bonde la Sidimu

9 dhidi ya Kedorlaoma, mfalme wa Elamu, Tidali mfalme wa Goimu, Amrafeli mfalme wa Shinari, na Arioko mfalme wa Elasari, yaani wafalme wanne dhidi ya wafalme watano.

10 Basi Bonde la Sidimu lilikuwa limejaa mashimo ya lami, nao wafalme wa Sodoma na wa Gomora walipokimbia, baadhi ya watu walitumbukia huko na wengine wakakimbilia vilimani.

11 Wale wafalme wanne wakateka mali yote ya Sodoma na Gomora pamoja na vyakula vyao vyote, kisha wakaenda zao.

12 Pia walimteka Loti mwana wa ndugu yake Abramu pamoja na mali zake, kwa kuwa alikuwa akiishi Sodoma.

13 Mtu mmoja aliyekuwa ametoroka akaja kumpa Abramu Mwebrania taarifa. Wakati huu Abramu alikuwa anaishi karibu na mialoni ya Mamre Mwamori, aliyekuwa ndugu yake Eshkoli na Aneri, ambao wote walikuwa wameungana na Abramu.

14 Abramu alipopata habari kwamba jamaa yake amechukuliwa mateka, akawaita watu 318 wa nyumbani mwake waliokuwa wamefunzwa kupigana vita, wakawafuatilia hadi Dani.

15 Wakati wa usiku Abramu aliwagawa watu wake katika vikosi ili awashambulie, na akawafuatilia, akawafukuza hadi Hoba, kaskazini ya Dameski.

16 Akarudisha mali zote, na akamrudisha Loti jamaa yake na mali zake, pamoja na wanawake na watu wengine.

17 Abramu aliporudi baada ya kumshinda Mfalme Kedorlaoma na wale wafalme waliojiunga naye, mfalme wa Sodoma akatoka kwenda kumlaki katika Bonde la Shawe (yaani Bonde la Mfalme).

18 Ndipo Melkizedeki mfalme wa Salemu alipoleta mkate na divai. Alikuwa kuhani wa Mungu Aliye Juu Sana;

19 akambariki Abramu, akisema,

“Abarikiwe Abramu na Mungu Aliye Juu Sana,

Muumba wa mbingu na nchi.

20 Abarikiwe Mungu Aliye Juu Sana,

ambaye amewaweka adui zako mkononi mwako.”

Ndipo Abramu akampa Melkizedeki sehemu ya kumi ya kila kitu.

21 Mfalme wa Sodoma akamwambia Abramu, “Nipe hao watu na hizo mali uchukue wewe mwenyewe.”

22 Lakini Abramu akamwambia mfalme wa Sodoma, “Nimeinua mkono wangu kwaBwana, Mungu Aliye Juu Sana, Muumba wa mbingu na dunia, na nimeapa

23 kwamba sitapokea kitu cho chote kilicho chako, hata kama ni uzi au gidamu ya kiatu, ili kamwe usije ukasema, ‘Nimemtajirisha Abramu.’

24 Sitapokea cho chote, ila kile tu watu wangu walichokula na sehemu ambayo ni fungu la watu waliokwenda pamoja nami, ambao ni Aneri, Eshkoli na Mamre. Wao na wapewe fungu lao.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/GEN/14-7ca36f7bdd2373513b15f3eeb88497d4.mp3?version_id=1627—

Mwanzo 15

Agano La Mungu Na Abramu

1 Baada ya jambo hili, neno laBwanalikamjia Abramu katika maono:

“Usiogope, Abramu.

Mimi ni ngao yako,

na thawabu yako kubwa sana.”

2 Lakini Abramu akasema, “EeBwanaMwenyezi, utanipa nini na mimi sina hata mtoto na atakayerithi nyumba yangu ni huyu Eliezeri Mdameski?”

3 Abramu akasema, “Hukunipa watoto, hivyo mtumishi katika nyumba yangu ndiye atakuwa mrithi wangu.”

4 Ndipo neno laBwanalilipomjia: “Mtu huyu hatakuwa mrithi wako, bali mwana atakayetoka katika viuno vyako mwenyewe ndiye atakayekuwa mrithi wako.”

5 Akamtoa nje na kusema, “Tazama juu kuelekea mbinguni na uhesabu nyota, kama hakika utaweza kuzihesabu.” Ndipo akamwambia, “Hivyo ndivyo uzao wako utakavyokuwa.”

6 Abramu akamwaminiBwana, naye kwake hili likahesabiwa kuwa haki.

7 Pia akamwambia, “Mimi ndimiBwana, niliyekutoa toka Uru ya Wakaldayo nikupe nchi hii uimiliki.”

8 Lakini Abramu akasema, “EeBwanaMwenyezi, nitawezaje kujua kwamba nitapata kuimiliki?”

9 NdipoBwanaakamwambia, “Niletee mtamba wa ng’ombe, mbuzi na kondoo dume, kila mmoja wa miaka mitatu, pamoja na hua na kinda la njiwa.”

10 Abramu akamletea hivi vyote, akampasua kila mnyama vipande viwili, akavipanga kila kimoja kuelekea mwenzake, lakini hata hivyo ndege, hakuwapasua vipande viwili.

11 Kisha ndege walao nyama wakatua juu ya mizoga, lakini Abramu akawafukuza.

12 Wakati jua lilipokuwa linatua, Abramu akashikwa na usingizi mzito, giza nene na la kutisha likaja juu yake.

13 KishaBwanaakamwambia, “Ujue hakika kwamba wazao wako watakuwa wageni kwenye nchi ambayo si yao wenyewe, nao watakuwa watumwa na watateswa kwa miaka mia nne.

14 Lakini nitaliadhibu taifa lile wanaolitumikia kama watumwa, hatimaye watatoka huko na mali nyingi.

15 Wewe, hata hivyo utakwenda kwa baba zako kwa amani na kuzikwa katika uzee mwema.

16 Katika kizazi cha nne wazao wako watarudi hapa, kwa maana dhambi ya Waamori bado haijafikia kipimo kilichojaa.”

17 Wakati jua lilipokuwa limezama na giza limeingia, tanuru la moshi na mwali wa moto unaowaka vikatokea na kupita kati ya vile vipande vya nyama.

18 Siku hiyoBwanaakafanya Agano na Abramu, na kumwambia, “Nitawapa wazao wako nchi hii, kuanzia mto wa Misrihadi mto ule mkubwa, Eufrati,

19 yaani nchi ya Wakeni, Wakenizi, Wakadmoni,

20 Wahiti, Waperizi, Warefai,

21 Waamori, Wakanaani, Wagirgashi na Wayebusi.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/GEN/15-460d102ba5d44f28ea511a1d317e181d.mp3?version_id=1627—

Mwanzo 16

Hagari Na Ishmaeli

1 Basi Sarai, mkewe Abramu, alikuwa hajamzalia watoto. Lakini alikuwa na mtumishi wa kike Mmisri jina lake Hagari,

2 hivyo Sarai akamwambia Abramu, “Bwanaamenizuilia kupata watoto. Nenda, ukakutane kimwili na mtumishi wangu wa kike, huenda nitaweza kupata watoto kupitia kwake.”

Abramu akakubaliana na lile Sarai alilosema.

3 Hivyo baada ya Abramu kuishi katika nchi ya Kanaani miaka kumi, Sarai akamchukua mtumishi wake wa kike wa Kimisri, Hagari na kumpa mumewe awe mke wake.

4 Akakutana kimwili na Hagari, naye akapata mimba.

Hagari alipojua kuwa ana mimba, alianza kumdharau Sarai.

5 Ndipo Sarai akamwambia Abramu, “Unawajibika na manyanyaso ninayoyapata. Nilimweka mtumishi wangu mikononi mwako, sasa kwa vile anajua kwamba ana mimba, ananidharau mimi.Bwanana aamue kati yako na mimi.”

6 Abramu akamwambia, “Mtumishi wako yuko mikononi mwako. Mtendee lo lote unalofikiri ni bora zaidi.” Ndipo Sarai akamtesa Hagari, hivyo akamtoroka.

7 Malaika waBwanaakamkuta Hagari karibu na chemchemi huko jangwani; ilikuwa chemchemi ile iliyokuwa kando ya barabara iendayo Shuri.

8 Malaika akamwambia, “Hagari, mtumishi wa Sarai, umetokea wapi, na unakwenda wapi?”

Akamjibu, “Ninamkimbia bibi yangu Sarai.”

9 Ndipo malaika waBwanaakamwambia, “Rudi kwa bibi yako ukajishushe chini yake.”

10 Malaika akaendelea akasema, “Nitazidisha wazao wako, hivi kwamba watakuwa wengi mno wasiohesabika.”

11 Pia malaika waBwanaakamwambia:

“Wewe sasa una mimba

nawe utamzaa mwana.

# Utamwita jina lake Ishmaeli,

kwa sababuBwanaamesikia juu ya huzuni yako.

12 Atakuwa punda-mwitu katikati ya wanadamu,

mkono wake utakuwa dhidi ya kila mtu

na mkono wa kila mtu dhidi yake,

naye ataishi kwa uhasama

na ndugu zake wote.”

13 AkampaBwanaaliyezungumza naye jina hili: “Wewe ndiwe Mungu unionaye mimi,” kwa maana alisema, “Sasa nimemwona yeye anayeniona mimi.”

14 Ndiyo sababu kisima kile kikaitwa Beer-Lahai-Roi,ambacho bado kipo huko hata leo kati ya Kadeshi na Beredi.

15 Hivyo Hagari akamzalia Abramu mwana, naye Abramu akamwita huyo mwana Hagari aliyemzalia, Ishmaeli.

16 Abramu alikuwa na umri wa miaka themanini na sita wakati Hagari alipomzalia Ishmaeli.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/GEN/16-e2e9a6d23dd9a353b7ca777736b89045.mp3?version_id=1627—

Mwanzo 17

Agano La Tohara

1 Abramu alipokuwa na miaka tisini na tisa,Bwanaakamtokea akamwambia, “Mimi ndimi Mungu Mwenyezi; enenda mbele zangu na uishi kwa unyofu.

2 Nami nitafanya Agano langu kati yangu na wewe, nami nitakuzidisha sana sana.”

3 Abramu akaanguka kifudifudi, naye Mungu akamwambia,

4 “Kwa upande wangu, hili ndilo Agano langu na wewe: Wewe utakuwa baba wa mataifa mengi.

5 Jina lako hutaitwa tena Abramu, bali jina lako litakuwa Abrahamu, kwa maana nimekufanya wewe baba wa mataifa mengi.

6 Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana, kwako yatatoka mataifa nao wafalme watatoka kwako.

7 Nitalithibitisha Agano langu kama Agano la milele kati yangu na wewe na wazao wako baada yako na vizazi vijavyo niwe Mungu wako na Mungu wa wazao wako.

8 Nchi yote ya Kanaani, unakoishi sasa kama mgeni, nitakupa kuwa milki yako milele, na uzao wako, nami nitakuwa Mungu wao.”

9 Ndipo Mungu akamwambia Abrahamu, “Kwa upande wako, lazima ushike Agano langu, wewe na wazao wako kwa ajili ya vizazi vijavyo.

10 Hili ni Agano langu na wewe pamoja na wazao wako baada yako, Agano mtakalolishika: Kila mwanaume miongoni mwenu atatahiriwa.

11 Mtafanyiwa tohara na hii itakuwa ni alama ya Agano kati yangu na ninyi.

12 Kwa vizazi vijavyo, kila mwanaume miongoni mwenu mwenye siku nane ni lazima atahiriwe, pamoja na watakaozaliwa nyumbani mwako au walionunuliwa kwa fedha kutoka kwa mgeni, wale ambao sio watoto wako.

13 Awe amezaliwa nyumbani mwako au amenunuliwa kwa fedha yako, ni lazima watahiriwe. Agano langu katika mwili wako litakuwa ni Agano la milele.

14 Kila mwanaume asiyetahiriwa, ambaye hajapata tohara ya mwilini, atatengwa na watu wake, amelivunja Agano langu.”

15 PiaBwanaakamwambia Abrahamu, “Kwa upande wa Sarai mkeo, hutamwita tena Sarai bali jina lake litakuwa Sara.

16 Nitambariki na hakika nitakupatia mwana kwake. Nitambariki na kwamba atakuwa mama wa mataifa, wafalme wa mataifa watatoka kwake.”

17 Abrahamu akaanguka kifudifudi, akacheka na kusema moyoni mwake, “Je, mtu wa miaka mia moja aweza kuzaa mwana? Je, Sara atazaa mtoto katika umri wa miaka tisini?”

18 Abrahamu akamwambia Mungu, “Laiti Ishmaeli naye angeshiriki baraka yako!”

19 Ndipo Mungu akasema, “Ndiyo, lakini mkeo Sara atakuzalia wewe mwana, nawe utamwita jina lake Isaki. Nitalithibitisha Agano langu naye kama Agano la milele kwa ajili yake na wazao wake baada yake.

20 Kwa upande wa Ishmaeli, nimekusikia: hakika nitambariki, nitamfanya awe na uzao mwingi na nitaongeza sana idadi yake. Atakuwa baba wa watawala kumi na wawili, nami nitamfanya awe taifa kubwa.

21 Lakini Agano langu nitalithibitisha kwa Isaki, ambaye Sara atakuzalia mwaka ujao majira kama haya.”

22 Wakati alipomaliza kuzungumza na Abrahamu, Mungu akapanda juu akaondoka kwa Abrahamu.

23 Siku ile ile, Abrahamu akamchukua Ishmaeli mwanawe na wote waliozaliwa nyumbani mwake pamoja na walionunuliwa kwa fedha zake, kila mwanaume wa nyumbani mwake, akawatahiri, kama Mungu alivyomwagiza.

24 Abrahamu alikuwa na umri wa miaka tisini na tisa alipotahiriwa,

25 naye Ishmaeli mwanawe alitahiriwa akiwa na umri wa miaka kumi na mitatu.

26 Abrahamu na Ishmaeli mwanawe walitahiriwa siku ile ile,

27 Kila mwanaume nyumbani mwa Abrahamu, pamoja na wote waliozaliwa nyumbani mwake au aliyenunuliwa kutoka kwa mgeni, alitahiriwa pamoja naye.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/GEN/17-f90ab5c026d7b25470117513550dffd8.mp3?version_id=1627—

Mwanzo 18

Wageni Watatu

1 Bwanaakamtokea Abrahamu karibu na mialoni ya Mamre wakati alipokuwa ameketi kwenye ingilio la hema lake wakati wa adhuhuri.

2 Abrahamu akainua macho akaona watu watatu wamesimama karibu naye. Alipowaona, aliharakisha kutoka kwenye ingilio la hema lake kuwalaki na kuwasujudia hadi nchi.

3 Akasema, “Kama nimepata kibali machoni penu, ee bwana wangu, usimpite mtumishi wako.

4 Acha yaletwe maji kidogo, kisha ninyi nyote mnawe miguu yenu na mpumzike chini ya mti huu.

5 Niruhusuni niwapatie chakula kidogo mle, ili mpate nguvu mwendelee na safari yenu, kwa kuwa mmekuja kwa mtumishi wenu.”

Nao wakamjibu, “Vema sana, fanya kama unavyosema.”

6 Hivyo Abrahamu akaharakisha akaingia hemani kwa Sara. Akasema, “Chukua vipimo vitatu vya unga laini haraka, ukande na uoke mikate.”

7 Kisha akakimbia kwenda kwenye kundi akachagua ndama mzuri, laini na akampa mtumishi, ambaye aliharakisha kumtayarisha.

8 Kisha akaleta jibini, maziwa na nyama ya yule ndama iliyoandaliwa, akaviweka mbele ya wageni. Walipokuwa wakila, alisimama karibu nao chini ya mti.

9 Wakamwuliza, “Yuko wapi Sara mkeo?”

Akasema, “Yuko huko, ndani ya hema.”

10 KishaBwanaakasema, “Hakika nitakurudia tena majira kama haya mwakani na Sara mkeo atakuwa ana mwana.”

Sara alikuwa akiwasikiliza kwenye ingilio la hema, lililokuwa nyuma yake.

11 Abrahamu na Sara walikuwa wazee tena waliosogea miaka, naye Sara alikwishakoma katika desturi ya wanawake.

12 Hivyo Sara akacheka kimoyomoyo alipokuwa akiwaza, “Baada ya mimi kuwa mkongwe hivi na bwana wangu amezeeka, je, nitaweza kufurahia jambo hili?”

13 NdipoBwanaakamwambia Abrahamu, “Kwa nini Sara amecheka na kusema, ‘Kweli nitazaa mtoto nami sasa ni mzee?’

14 Je, kuna jambo lo lote gumu lisilowezekana kwaBwana? Nitakurudia mwakani majira kama haya, naye Sara atakuwa na mwana.”

15 Sara akaogopa kwa kuwa alidanganya na kusema, “Mimi sikucheka.”

Lakini Bwana akasema, “Ndiyo, ulicheka!”

Abrahamu Aiombea Sodoma

16 Wakati watu hao waliposimama ili waondoke, walielekeza nyuso zao Sodoma, Abrahamu akawatoa kitambo kidogo ili awasindikize.

17 NdipoBwanaakasema, “Je, nimfiche Abrahamu jambo ninalokusudia kufanya?

18 Hakika Abrahamu atakuwa taifa kubwa na lenye nguvu, kupitia kwake mataifa yote ya dunia yatabarikiwa.

19 Kwa maana nimemchagua yeye, ili kwamba aongoze watoto wake na jamaa yake kumtiiBwana, wawe waadilifu na kutenda haki, iliBwanaatimize ahadi yake kwa Abrahamu.”

20 BasiBwanaakasema, “Kilio dhidi ya Sodoma na Gomora ni kikubwa sana na dhambi yao inasikitisha sana,

21 kwamba nitashuka nione kama waliyoyatenda ni mabaya kiasi cha kilio kilichonifikia. Kama sivyo, nitajua.”

22 Basi wale watu wakageuka wakaenda kuelekea Sodoma, lakini Abrahamu akabaki amesimama mbele zaBwana.

23 Ndipo Abrahamu akamsogelea akasema: “Je, utawaangamiza wenye haki na waovu?

24 Je, ikiwa watakuwepo watu wenye haki hamsini katika mji huo, hivi kweli utauangamiza na wala hutauacha kwa ajili ya hao watu hamsini wenye haki waliomo ndani yake?

25 Hilo na liwe mbali nawe, kufanya jambo kama hilo, kuwaua wenye haki pamoja na waovu, kuwatendea wenye haki sawasawa na waovu. Iwe mbali nawe! Je, Mwamuzi wa dunia yote hatafanya lililo sawa?”

26 Bwanaakasema, “Kama nikipata watu hamsini wenye haki katika mji wa Sodoma, nitausamehe huo mji wote kwa ajili yao.”

27 Kisha Abrahamu akasema tena: “Sasa kwa kuwa nimekuwa na ujasiri wa kuzungumza na Bwana, ingawa mimi si kitu bali ni mavumbi na majivu;

28 je, kama hesabu ya wenye haki imepungua watano katika hamsini, utauangamiza huo mji wote kwa ajili ya hao watano waliopungua?”

Bwana akamwambia, “Kama nikiwakuta huko watu arobaini na watano, sitauangamiza.”

29 Abrahamu akazungumza naye kwa mara nyingine, “Je, kama huko watapatikana watu arobaini tu?”

Akamjibu, “Kwa ajili ya hao arobaini, sitauangamiza.”

30 Ndipo akasema, “Bwana na asikasirike, lakini niruhusu nizungumze. Je, kama huko watakuwepo thelathini tu?”

Akajibu, “Sitapaangamiza ikiwa nitawakuta huko watu thelathini.”

31 Abrahamu akasema, “Sasa kwa kuwa nimekuwa na ujasiri sana kuzungumza na Bwana, je, kama wakipatikana huko watu ishirini tu?”

Bwana akajibu, “Kwa ajili ya hao ishirini, sitauangamiza.”

32 Abrahamu akasema, “Bwana na asikasirike, lakini niruhusu nizungumze tena mara moja tu. Itakuwaje kama watapatikana huko watu kumi tu?”

Bwana akajibu, “Kwa ajili ya hao kumi, sitauangamiza.”

33 Bwanaalipomaliza kuzungumza na Abrahamu, akaondoka, naye Abrahamu akarudi nyumbani kwake.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/GEN/18-355456cda864f19775493e3544700c3c.mp3?version_id=1627—

Mwanzo 19

Kuangamizwa Kwa Sodoma Na Gomora

1 Malaika wale wawili wakafika Sodoma wakati wa jioni, naye Loti alikuwa ameketi kwenye lango la mji. Wakati alipowaona, aliondoka kwenda kuwalaki na kuwasujudia hadi chini.

2 Akasema, “Bwana zangu, tafadhali karibuni kwenye nyumba ya mtumishi wenu. Mnaweza kunawa miguu na kulala hapa kisha asubuhi na mapema mwendelee na safari yenu.”

Wakamjibu, “La hasha, tutalala hapa nje uwanjani.”

3 Lakini akasisitiza kwa nguvu kwamba waingie pamoja naye nyumbani kwake. Akawaandalia chakula, mikate isiyotiwa chachu, nao wakala.

4 Kabla hawajaenda kulala, watu wote kutoka kila sehemu ya mji wa Sodoma, vijana kwa wazee, waliizunguka nyumba.

5 Wakamwita Loti wakisema, “Wako wapi wale watu ambao walikuja kwako jioni hii? Watoe nje kwetu ili tuweze kuwalawiti.”

6 Loti akatoka nje kuonana nao, akaufunga mlango nyuma yake,

7 akasema, “La hasha, rafiki zangu. Msifanye jambo hili ovu.

8 Tazama, ninao binti wawili ambao kamwe hawajakutana kimwili na mwanaume. Acha niwatoe nje kwenu, nanyi mnaweza kuwafanyia lo lote mnalotaka. Lakini msiwafanyie cho chote watu hawa, kwa sababu wako kwenye ulinzi chini ya dari langu.”

9 Wakamjibu, “Tuondokee mbali.” Wakaendelea kusema, “Huyu mtu alikuja hapa kama mgeni na sasa anataka kuwa mwamuzi wetu! Tutakutenda vibaya kuliko wao.” Waliendelea kumlazimisha Loti na kusonga mbele ili kuvunja mlango.

10 Lakini watu wale waliokuwa ndani wakanyoosha mkono wakamvuta Loti ndani ya nyumba na kufunga mlango.

11 Kisha wakawapiga kwa upofu wale watu waliokuwa mlangoni mwa ile nyumba, vijana kwa wazee, hivyo hawakuweza kuupata mlango.

12 Wale watu wawili wakamwambia Loti, “Una mtu mwingine ye yote hapa, wakwe zako, wana au binti, ama ye yote mwingine aliye wako katika mji huu? Waondoe hapa,

13 kwa sababu tunapaangamiza mahali hapa. Kilio kwaBwanadhidi ya watu wa hapa, ni kikubwa kiasi kwamba ametutuma kupaangamiza.”

14 Kwa hiyo Loti alitoka ili kuzungumza na wakwe zake, waliokuwa wamewaposa binti zake. Akawaambia, “Fanyeni haraka kuondoka mahali hapa, kwa kuwaBwanayu karibu kuangamiza mji huu!” Lakini wakwe zake walifikiri kwamba alikuwa akitania.

15 Kunako mapambazuko, malaika wakawahimiza Loti, wakamwambia, “Fanya haraka! Mchukue mke wako na binti zako wawili walioko hapa, la sivyo utaangamizwa wakati mji utakapoadhibiwa.”

16 Alipositasita, wale watu wakamshika mkono wake na mikono ya mke wake na binti zake wawili na kuwaongoza salama nje ya mji, kwa kuwaBwanaalikuwa na huruma kwao.

17 Mara walipokwisha kuwatoa nje, mmoja wao akawaambia, “Mkimbie kwa usalama wenu! Msitazame nyuma, wala msisimame po pote katika tambarare! Kimbilieni milimani, ama sivyo mtaangamizwa!”

18 Lakini Loti akawajibu, “La hasha, bwana zangu, tafadhalini!

19 Mtumishi wenu amepata kibali mbele ya macho yenu, nanyi mmeonyesha wema mkubwa kwangu kwa kuokoa maisha yangu. Lakini siwezi kukimbilia milimani, janga hili litanikumba, nami nitakufa.

20 Tazama, hapa kuna mji karibu wa kukimbilia, nao ni mdogo. Niruhusuni nikimbilie humo, ni mdogo sana, ama sivyo? Ndipo maisha yangu yatasalimika.”

21 Akamwambia, “Vema sana, nitalikubali hili ombi pia, sitauangamiza mji ulioutaja.

22 Lakini ukimbilie huko haraka, kwa sababu sitaweza kufanya lo lote mpaka ufike huko.” (Ndiyo maana mji huo ukaitwa Soari.)

23 Wakati Loti alipofika Soari, jua lilikuwa limechomoza katika nchi.

24 NdipoBwanaakanyesha moto wa kiberiti juu ya Sodoma na Gomora, uliotoka mbinguni kwaBwana.

25 Hivyo akaiteketeza miji ile na eneo lote la tambarare, pamoja na wote waliokuwa wanaishi katika miji, hata pia mimea yote katika nchi.

26 Lakini mke wa Loti akatazama nyuma, hivyo akawa nguzo ya chumvi.

27 Asubuhi na mapema siku iliyofuata, Abrahamu akaamka na kurudi mahali pale aliposimama mbele zaBwana.

28 Akatazama upande wa Sodoma na Gomora, kuelekea nchi yote ya tambarare, akaona moshi mzito ukipanda kutoka kwenye nchi, kama moshi utokao kwenye tanuru.

29 Kwa hiyo Mungu alipoiangamiza miji ya tambarare alimkumbuka Abrahamu, akamtoa Loti kutoka kwenye lile janga lililoharibu miji ile ambamo Loti alikuwa ameishi.

Loti Na Binti Zake

30 Loti na binti zake wawili waliondoka Soari na kufanya makao yao kule milimani, kwa maana aliogopa kukaa Soari. Yeye na binti zake wawili waliishi katika pango.

31 Siku moja binti mkubwa akamwambia yule mdogo, “Baba yetu ni mzee na hakuna mwanaume mahali hapa atakayekutana na sisi kimwili, kama ilivyo desturi ya mahali pote duniani.

32 Tumnyweshe baba yetu mvinyo kisha tukutane naye kimwili ili tuhifadhi uzao wetu kupitia baba yetu.”

33 Usiku ule walimnywesha baba yao mvinyo, alipolewa binti yake mkubwa akaingia na kukutana naye kimwili. Baba yao hakujua wakati binti yake alipoingia kulala naye wala alipotoka.

34 Siku iliyofuata binti mkubwa akamwambia yule mdogo, “Usiku uliopita mimi nilikutana kimwili na baba yangu. Tumnyweshe divai tena, usiku huu nawe ukutane naye kimwili ili tuweze kuhifadhi uzao wetu kupitia baba yetu.”

35 Kwa hiyo wakamnywesha baba yao mvinyo tena usiku ule, naye binti yake mdogo akaingia, akakutana naye kimwili. Kwa mara nyingine baba yao hakujua binti yake alipolala naye wala alipoondoka.

36 Hivyo binti wawili wa Loti wakapata mimba kwa baba yao.

37 Binti mkubwa akamzaa mwana, akamwita jina lake Moabu; ndio baba wa Wamoabu hata leo.

38 Binti mdogo naye pia akamzaa mwana, naye akamwita Benami; ndiye baba wa Waamoni hata leo.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/GEN/19-c3bec4e378369614e1d5d7fa08ebda07.mp3?version_id=1627—

Mwanzo 20

Abrahamu Na Abimeleki

1 Basi Abrahamu akaendelea mbele kutoka huko hadi nchi ya Negebu na akaishi kati ya Kadeshi na Shuri. Kwa muda mfupi alikaa Gerari kama mgeni,

2 huko Abrahamu akasema kuhusu Sara mkewe, “Huyu ni dada yangu.” Kisha Abimeleki mfalme wa Gerari akatuma Sara aletwe, naye akamchukua.

3 Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto wakati wa usiku na kumwambia, “Wewe ni kama mfu kwa sababu ya huyu mwanamke uliyemchukua; yeye ni mke wa mtu.”

4 Wakati huo Abimeleki alikuwa bado hajamsogelea, kwa hiyo akasema, “Je, Bwana utaliharibu taifa lisilo na hatia?

5 Hakusema kwangu, ‘Huyu ni dada yangu,’ naye Sara pia hakusema, ‘Huyu ni kaka yangu’? Nimefanya haya kwa dhamiri njema na mikono safi.”

6 Kisha Mungu akamwambia katika ndoto, “Ndiyo, najua ya kwamba umefanya haya kwa dhamiri safi, kwa hiyo nimekuzuia usinitende dhambi. Ndiyo sababu sikukuacha umguse.

7 Sasa umrudishe huyo mke wa mtu, kwa maana ni nabii, naye atakuombea nawe utaishi. Lakini kama hukumrudisha, ujue kwa hakika kuwa wewe na watu wako wote mtakufa.”

8 Kesho yake asubuhi na mapema Abimeleki akawaita maafisa wake wote, na baada ya kuwaambia yote yaliyotokea, waliogopa sana.

9 Kisha Abimeleki akamwita Abrahamu na kumwambia, “Wewe umetufanyia nini? Nimekukosea nini hata ukaleta hatia kubwa namna hii juu yangu na ufalme wangu? Umenifanyia mambo ambayo hayakupasa kufanyika.”

10 Abimeleki akamwuliza Abrahamu, “Ulikuwa na kusudi gani kufanya hivi?”

11 Abrahamu akajibu, “Niliwaza kwamba, ‘Hakika hakuna hofu ya Mungu mahali hapa, nao wataniua kwa sababu ya mke wangu.’

12 Pamoja na hayo, ni kweli kwamba yeye ni dada yangu, binti wa baba yangu ingawa si mtoto wa mama yangu; basi akawa mke wangu.

13 WakatiBwanaaliponifanya nisafiri mbali na nyumbani mwa baba yangu, nilimwambia, ‘Hivi ndivyo utakavyoonyesha pendo lako kwangu: Kila mahali tutakapokwenda, kuhusu mimi sema, “Huyu ni kaka yangu.” ’ ”

14 Kisha Abimeleki akatwaa kondoo na ng’ombe, na watumwa wa kiume na wa kike akampa Abrahamu, akamrudisha Sara kwa mumewe.

15 Abimeleki akasema, “Nchi yangu iko mbele yako, ishi po pote unapotaka.”

16 Akamwambia Sara, “Ninampa kaka yako shekeli elfu moja za fedha. Hii ni kufidia kosa lililofanyika dhidi yako mbele ya wote walio pamoja nawe; haki yako imethibitishwa kabisa.”

17 Kisha Abrahamu akamwomba Mungu, naye Mungu akamponya Abimeleki, mke wake, na watumwa wake wa kike kwamba waweze kupata watoto tena,

18 kwa kuwaBwanaalikuwa ameyafunga matumbo ya wote katika nyumba ya Abimeleki kwa sababu ya mke wa Abrahamu.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/GEN/20-e60b3ec0343050cc0c82305af3bde6a0.mp3?version_id=1627—

Mwanzo 21

Kuzaliwa Kwa Isaki

1 Wakati huuBwanaakamrehemu Sara kama alivyokuwa amesema, nayeBwanaakamtendea Sara kile alichokuwa ameahidi.

2 Sara akapata mimba, akamzalia Abrahamu mwana katika uzee wake, majira yale ya Mungu aliomwahidi.

3 Abrahamu akamwita Isaki yule mwana ambaye Sara alimzalia.

4 Isaki alipokuwa na umri wa siku nane, Abrahamu akamtahiri, kama Mungu alivyomwamuru.

5 Abrahamu alikuwa na miaka 100 wakati Isaki mwanawe alipozaliwa.

6 Sara akasema, “Mungu ameniletea kicheko, kila mmoja atakayesikia jambo hili atacheka pamoja nami.”

7 Akaongeza kusema, “Nani angemwambia Abrahamu kuwa Sara angenyonyesha watoto? Tena nimemzalia mwana katika uzee wake.”

Hagari Na Ishmaeli Wafukuzwa

8 Mtoto akakua akaachishwa kunyonya na siku hiyo Abrahamu alifanya sherehe kubwa.

9 Lakini Sara aliona kuwa mwana ambaye Hagari, Mmisri, aliyemzalia Abrahamu alikuwa anadhihaki,

10 Sara akamwambia Abrahamu, “Mwondoe mwanamke huyu mtumwa na mwanawe, kwa kuwa mwana wa mwanamke mtumwa kamwe hatashiriki urithi pamoja na mwanangu Isaki.”

11 Jambo hili lilimhuzunisha sana Abrahamu kwa sababu lilimhusu mwanawe.

12 Lakini Mungu akamwambia, “Usihuzunike hivyo kwa sababu ya kijana na mtumishi wako wa kike. Sikiliza lo lote Sara analokuambia, kwa sababu uzao wako utahesabiwa kupitia Isaki.

13 Nitamfanya huyu mwana wa mtumishi wako wa kike kuwa taifa pia, kwa sababu naye ni uzao wako.”

14 Kesho yake asubuhi na mapema, Abrahamu akachukua chakula na kiriba cha maji, akampa Hagari. Akaviweka mabegani mwa Hagari, akamwondoa pamoja na kijana. Akashika njia, akatangatanga katika jangwa la Beer-Sheba.

15 Maji yalipokwisha kwenye kiriba, akamwacha kijana chini ya mojawapo ya vichaka.

16 Kisha akajiendea zake akaketi karibu, umbali wa kutupa mshale, akawaza, “Siwezi kumwangalia kijana akifa.” Ikawa alipokuwa ameketi pale karibu, akaanza kulia kwa huzuni.

17 Mungu akamsikia kijana akilia, malaika wa Mungu akamwita Hagari kutoka mbinguni na kumwambia, “Kuna nini Hagari? Usiogope, Mungu amesikia kijana analia akiwa amelala pale.

18 Mwinue kijana na umshike mkono, kwa maana nitamfanya kuwa taifa kubwa.”

19 Ndipo Mungu akamfumbua Hagari macho yake naye akaona kisima cha maji. Hivyo akaenda akajaza kiriba maji na kumpa kijana anywe.

20 Mungu akawa pamoja na huyu kijana alipokuwa akiendelea kukua. Aliishi jangwani na akawa mpiga upindi.

21 Alipokuwa akiishi katika Jangwa la Parani, mama yake akampatia mke kutoka Misri.

Mapatano Katika Beer-Sheba

22 Wakati huo Abimeleki na Fikoli mkuu wa majeshi yake wakamwambia Abrahamu, “Mungu yu pamoja nawe katika kila kitu unachofanya.

23 Sasa niapie hapa mbele za Mungu kwamba hutanitenda hila mimi, watoto wangu wala wazao wangu. Nitendee mimi na nchi ambayo unaishi kama mgeni wema ule ule ambao nimekutendea.”

24 Abrahamu akasema, “Ninaapa hivyo.”

25 Ndipo Abrahamu akalalamika kwa Abimeleki kuhusu kisima cha maji ambacho watumishi wa Abimeleki walikuwa wamekinyang’anya.

26 Lakini Abimeleki akasema, “Sijui ni nani ambaye amefanya hili. Hukuniambia, leo tu ndipo ninasikia habari zake.”

27 Hivyo Abrahamu akaleta kondoo na ng’ombe akampa Abimeleki, nao watu hawa wawili wakafanya mapatano.

28 Abrahamu akatenga kondoo wake saba kutoka kwenye kundi,

29 Abimeleki akamwuliza Abrahamu, “Ni nini maana ya hawa kondoo wa kike saba uliowatenga peke yao?”

30 Abrahamu akamjibu, “Upokee hawa kondoo wa kike saba kutoka mkononi mwangu kama ushahidi kuwa nilichimba kisima hiki.”

31 Hivyo mahali pale pakaitwa Beer-Sheba, kwa sababu watu wawili waliapiana hapo.

32 Baada ya mapatano kufanyika huko Beer-Sheba, Abimeleki na Fikoli mkuu wa majeshi yake wakarudi katika nchi ya Wafilisti.

33 Abrahamu akapanda mti wa mkwaju huko Beer-Sheba, na hapo akaliitia jina laBwana, Mungu wa milele.

34 Naye Abrahamu akakaa katika nchi ya Wafilisti kwa muda mrefu.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/GEN/21-4146966073bce336b0fbeac084cd1f2a.mp3?version_id=1627—