Malaki 1

1 Ujumbe: Neno laBwanakwa Israeli kupitia kwa Malaki.

Yakobo Alipendwa, Esau Alichukiwa

2 Bwanaasema, “Nimewapenda ninyi.”

“Lakini ninyi mnauliza, ‘Wewe umetupendaje?’ ”

Bwanaasema, “Je, Esau hakuwa ndugu yake Yakobo? Hata hivyo nimempenda Yakobo,

3 lakini nikamchukia Esau, nami nimeifanya milima yake kuwa ukiwa na urithi wake nimewapa mbweha wa jangwani.”

4 Edomu anaweza kusema, “Ingawa tumepondwapondwa, tutajenga upya magofu.”

Lakini hili ndiloBwanaMwenye Nguvu Zote asemalo: “Wanaweza kujenga, lakini nitabomoa. Wataitwa Nchi Ovu, watu ambao siku zote wapo chini ya ghadhabu yaBwana.

5 Mtayaona kwa macho yenu wenyewe na kusema, ‘Bwanani mkuu, hata nje ya mipaka ya Israeli!’

Dhabihu Zilizo Na Mawaa

6 “Mwana humheshimu baba yake, naye mtumishi humheshimu bwana wake. Kama mimi ni baba, iko wapi heshima ninayostahili? Kama mimi ni bwana, iko wapi heshima ninayostahili?” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote. “Ni ninyi, Enyi makuhani, mnaolidharau Jina langu.

“Lakini mnauliza, ‘Tumelidharau Jina lako kwa namna gani?’

7 “Mnatoa sadaka chakula kilichotiwa unajisi juu ya madhabahu yangu.

“Lakini ninyi mnauliza, ‘Tumekutia unajisi kwa namna gani?’

“Kwa kusema kuwa meza yaBwanani ya kudharauliwa.

8 Wakati mletapo dhabihu wanyama walio vipofu, je, hilo si kosa? Mnapoleta dhabihu zilizo vilema au wanyama wagonjwa, je, hilo si kosa? Jaribuni kuvitoa kwa mtawala wenu! Je, angefurahiwa nanyi? Je, atawakubalia?” AsemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

9 “Basi mwombeni Mungu awe na neema kwetu. Je, kwa sadaka kama hizo kutoka mikononi mwenu, atawapokea?” AsemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

10 “Laiti mmoja wenu angalifunga milango ya Hekalu, ili msije mkawasha moto usiokuwa na faida juu ya madhabahu yangu! Sina furaha nanyi,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote, “nami sitaikubali sadaka toka mikononi mwenu.

11 Jina langu litakuwa kuu miongoni mwa mataifa, kuanzia maawio ya jua hata machweo yake. Kila mahali uvumba na sadaka safi zitaletwa kwa Jina langu, kwa sababu Jina langu litakuwa kuu miongoni mwa mataifa,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

12 “Lakini mnalinajisi Jina langu kwa kusema kuhusu meza ya Bwana, ‘Imetiwa unajisi pamoja na chakula chake. Ni ya kudharauliwa.’

13 Nanyi mnasema, ‘Mzigo gani huu!’ Nanyi mnaidharau kwa kiburi,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

“Wakati mnapowaleta wanyama mliopokonya kwa nguvu, vilema au walio wagonjwa na kuwatoa kama dhabihu, je, niwakubali kutoka mikononi mwenu?” asemaBwana.

14 “Amelaaniwa yeye adanganyaye aliye na mnyama wa kiume anayekubalika katika kundi lake na kuweka nadhiri ya kumtoa, lakini akatoa dhabihu ya mnyama aliye na dosari kwaBwana. Kwa kuwa mimi ni Mfalme Mkuu, nalo Jina langu linapaswa kuogopwa miongoni mwa mataifa,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/MAL/1-2d81f459cdbe68056fa3c5106d0e3452.mp3?version_id=1627—

Malaki 2

Onyo Kwa Makuhani

1 “Sasa onyo hili ni kwa ajili yenu, Enyi makuhani.

2 Kama hamtasikiliza, na kama hamtaki kuielekeza mioyo yenu kuheshimu Jina langu, nitatuma laana juu yenu, nami nitalaani baraka zenu. Naam, nimekwisha kuzilaani, kwa sababu hamkuielekeza mioyo yenu kuniheshimu mimi,” AsemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

3 “Kwa sababu yenu nitawakatilia mbali wazao wenu. Nitazipaka nyuso zenu mavi, mavi ya dhabihu zenu. Nanyi mtafukuzwa pamoja nazo mtoke mbele zangu.

4 Nanyi mtajua kuwa nimewapelekea onyo hili ili kwamba Agano langu na Lawi lipate kuendelea,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

5 “Agano langu lilikuwa pamoja naye, agano la uhai na amani, nami nilimpa yote, ili aniche na kuniheshimu, naye akaniheshimu na kusimama akilicha Jina langu.

6 Fundisho la kweli lilikuwa kinywani mwake, wala hakuna uongo wo wote uliopatikana katika midomo yake. Alitembea nami katika amani na unyofu, naye akawageuza wengi kutoka dhambini.

7 “Kwa maana yapasa midomo ya kuhani kuhifadhi maarifa. Tena kutoka kinywani mwake watu wangepaswa kutafuta mafundisho, kwa sababu yeye ni mjumbe waBwanaMwenye Nguvu Zote.

8 Lakini mmegeuka mkaiacha njia na kwa mafundisho yenu mmesababisha wengi kujikwaa, mmevunja agano na Lawi,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

9 “Kwa hiyo nimewasababisha ninyi kudharauliwa na kufedheheshwa mbele ya watu wote, kwa sababu hamkufuata njia zangu, bali mmeonyesha upendeleo katika mambo ya sheria.”

Yuda Si Mwaminifu

10 Je, sote hatuna Baba mmoja? Hatukuumbwa na Mungu mmoja? Kwa nini basi tunalinajisi Agano la baba zetu kwa kukosa uaminifu kila mmoja kwa mwenzake?

11 Yuda amevunja uaminifu. Jambo la kuchukiza limetendeka katika Israeli na katika Yerusalemu: Yuda amepanajisi mahali patakatifu apendapoBwana, kwa kuoa binti wa mungu mgeni.

12 Kwa maana kwa mtu awaye yote atendaye jambo hili,Bwanana amkatilie mbali kutoka hema za Yakobo, hata kama huwa anamleteaBwanaMwenye Nguvu Zote sadaka.

13 Kitu kingine mnachokifanya: Mnaifurikisha madhabahu yaBwanakwa machozi. Mnalia na kuugua kwa sababu yeye haziangalii tena sadaka zenu wala hazikubali kwa furaha kutoka mikononi mwenu.

14 Mnauliza, “Kwa nini?” Ni kwa sababuBwanani shahidi kati yako na mke wa ujana wako, kwa sababu umevunja uaminifu naye, ingawa yeye ni mwenzako, mke wa agano lako la ndoa.

15 Je,Bwanahakuwafanya wao kuwa mmoja? Katika mwili na katika roho wao ni wa Mungu. Kwa nini wawe mmoja? Kwa sababu Mungu alikuwa akitafuta mzao mwenye kumcha Mungu. Kwa hiyo jihadharini wenyewe katika roho zenu, mtu asivunje uaminifu kwa mke wa ujana wake.

16 “Ninachukia kuachana,” asemaBwana, Mungu wa Israeli, “pia nachukia mtu anayejivika jeuri kama vazi,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

Kwa hiyo jihadharini wenyewe katika roho zenu, wala msije mkavunja uaminifu.

Siku Ya Hukumu

17 MmemchoshaBwanakwa maneno yenu.

Nanyi mnauliza, “Tumemchosha kwa namna gani?”

Mmemchosha kwa kusema, “Wote watendao mabaya ni wema machoni paBwana, naye anapendezwa nao” au “Mungu wa haki yuko wapi?”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/MAL/2-c418f954b47c68ff590265794d4cdda5.mp3?version_id=1627—

Malaki 3

1 “Angalieni, nitamtuma mjumbe wangu, atakayeiandaa njia mbele yangu. Ndipo ghafula Bwana mnayemtafuta atakuja hekaluni mwake. Mjumbe wa Agano, ambaye mnamwonea shauku, atakuja,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

2 Lakini ni nani atakayeweza kustahimili hiyo siku ya kuja kwake? Ni nani awezaye kusimama atakapotokea? Kwa kuwa atakuwa kama moto wa mfua fedha au kama sabuni ya afuaye nguo.

3 Ataketi kama mfuaji na asafishaye fedha, atawatakasa Walawi, naye atawasafisha kama dhahabu na fedha. KishaBwanaatakuwa na watu watakaoleta sadaka katika haki,

4 nazo sadaka za Yuda na Yerusalemu zitakubalika kwaBwana, kama katika siku zilizopita, kama katika miaka ya zamani.

5 “Basi nitakuja karibu nanyi ili kuhukumu. Nami nitakuwa mwepesi kushuhudia dhidi ya wachawi, wazinzi, waapao kwa uongo, wanaopunja vibarua malipo yao, wanaowaonea wajane na yatima, nao wanaowanyima wageni haki, lakini hawaniogopi mimi,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

Kumwibia Mungu

6 “MimiBwanasibadiliki. Kwa hiyo ninyi, Enyi uzao wa Yakobo, hamjaangamizwa.

7 Tangu wakati wa baba zenu mmegeukia mbali na amri zangu nanyi hamkuzishika. Nirudieni mimi, nami nitawarudia ninyi,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

“Lakini mnauliza, ‘Tutarudi kwa namna gani?’

8 “Je, mwanadamu atamwibia Mungu? Hata hivyo mnaniibia mimi.

“Lakini mnauliza, ‘Tunakuibia kwa namna gani?’

“Mnaniibia zaka na dhabihu.

9 Mko chini ya laana, ninyi taifa lote, kwa sababu mnaniibia mimi.

10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu. Nijaribuni katika hili,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote, “nanyi mwone kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni na kuwamwagieni baraka nyingi mpaka mkose nafasi ya kutosha au la.

11 Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu, wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

12 “Ndipo mataifa yote yatawaita mliobarikiwa, kwa maana nchi yenu itakuwa ya kupendeza sana,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

13 “Mmesema vitu vigumu dhidi yangu,” asemaBwana.

“Hata hivyo mnauliza, ‘Tumesema nini dhidi yako?’

14 “Mmesema, ‘Ni bure kumtumikia Mungu. Tumepata faida gani kwa kushika maagizo yake na kwenda kama waombolezaji mbele zaBwanaMwenye Nguvu Zote?

15 Lakini sasa wenye kiburi wanabarikiwa. Hakika watenda mabaya wanastawi, pia hata wale wanaoshindana na Mungu ndio wanaosalimika.’ ”

16 Ndipo wale waliomchaBwanawakasemezana wao kwa wao, nayeBwanaakasikiliza naye akasikia. Kitabu cha kumbukumbu kikaandikwa mbele yake kuhusu wale ambao walimchaBwanana kuliheshimu jina lake.

17 “Nao watakuwa watu wangu,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote, “katika siku ile nitakapowafanya watu kuwa hazina yangu. Nitawahurumia, kama vile kwa huruma mtu amhurumiavyo mwanawe anayemtumikia.

18 Kwa mara nyingine tena utaona tofauti kati ya wenye haki na waovu, kati ya wale wanaomtumikia Mungu na wale wasiomtumikia.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/MAL/3-e12e85093aad32613aefd604cc373f9f.mp3?version_id=1627—

Malaki 4

Siku Ya Bwana

1 “Hakika siku inakuja, itawaka kama tanuru. Wote wenye kiburi na kila mtenda mabaya watakuwa mabua makavu na siku ile inayokuja itawawasha moto,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote. “Hakuna mzizi wala tawi litakalosalia kwao.

2 Bali kwenu ninyi mnaoliheshimu Jina langu, jua la haki litawazukia, lenye kuponya katika mbawa zake. Nanyi mtatoka nje na kurukaruka kama ndama aliyeachiwa kutoka zizini.

3 Kisha ninyi mtawakanyaga waovu nao watakuwa majivu chini ya nyayo za miguu yenu siku ile nitakayofanya mambo haya,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

4 “Kumbukeni sheria ya mtumishi wangu Mose, amri na sheria nilizompa huko Horebu kwa ajili ya Israeli wote.

5 “Tazama, nitawapelekea nabii Eliya kabla ya kuja siku ile iliyo kuu na ya kutisha yaBwana.

6 Ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, la sivyo nitakuja na kuipiga nchi kwa laana.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/MAL/4-5240a62128de639eb6ba1d9251f8fc90.mp3?version_id=1627—

Zekaria 1

Wito Wa Kumrudia Bwana

1 Katika mwezi wa nane wa mwaka wa pili wa utawala wa Mfalme Dario, neno laBwanalilimjia nabii Zekaria mwana wa Berekia, mwana wa Ido, kusema:

2 “Bwanaaliwakasirikia sana baba zako wa zamani.

3 Kwa hiyo waambie watu: Hivi ndivyoBwanaMwenye Nguvu Zote asemavyo: ‘Nirudieni mimi,’ asemaBwanaMwenye Nguvu Zote, ‘nami nitawarudia ninyi,’ asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

4 Msiwe kama baba zenu, ambao manabii waliotangulia waliwatangazia: Hivi ndivyoBwanaMwenye Nguvu Zote asemavyo: ‘Geukeni, mziache njia zenu mbaya na matendo yenu maovu.’ Lakini hawakunisikiliza wala kufuata maelekezo yangu, asemaBwana.

5 Wako wapi baba zako sasa? Nao manabii, je, wanaishi milele?

6 Je, maneno yangu na amri zangu nilizowaagiza manabii watumishi wangu, hayakuwapata baba zenu?”

“Kisha walitubu na kusema, ‘BwanaMwenye Nguvu Zote ametutenda sawasawa na njia zetu na matendo yetu yalivyostahili, kama alivyokusudia kufanya.’ ”

Maono Ya Kwanza: Mtu Katikati Ya Miti Ya Mihadasi

7 Katika siku ya ishirini na nne ya mwezi wa kumi na moja, yaani mwezi uitwao Shebati, katika mwaka wa pili wa kutawala kwake Mfalme Dario, neno laBwanalilimjia nabii Zekaria mwana wa Berekia mwana wa Ido.

8 Wakati wa usiku nilipata maono, mbele yangu alikuwepo mtu akiendesha farasi mwekundu! Alikuwa amesimama katikati ya miti ya mihadasi kwenye bonde. Nyuma yake walikuwepo farasi wekundu, wa kikahawia na weupe.

9 Nikauliza, “Hivi ni vitu gani bwana wangu?”

Malaika aliyekuwa akizungumza na mimi akanijibu, “Nitakuonyesha kuwa ni nini.”

10 Kisha yule mtu aliyesimama katikati ya miti ya mihadasi akaeleza, “Ni wale ambaoBwanaamewatuma waende duniani kote.”

11 Nao wakatoa taarifa kwa yule malaika waBwana, aliyekuwa amesimama katikati ya miti ya mihadasi, “Tumepita duniani kote na kukuta ulimwengu wote umepumzika kwa amani.”

12 Kisha malaika waBwanaakasema, “BwanaMwenye Nguvu Zote, utazuia mpaka lini rehema kutoka Yerusalemu na miji ya Yuda, ambayo umeikasirikia kwa miaka hii sabini?”

13 Kwa hiyoBwanaakazungumza maneno ya upole na ya kufariji kwa malaika aliyezungumza nami.

14 Kisha malaika yule aliyekuwa akizungumza nami akasema, “Tangaza neno hili: Hili ndiloBwanaMwenye Nguvu Zote asemalo: ‘Nina wivu sana kwa ajili ya Yerusalemu na Sayuni,

15 lakini nimeyakasirikia sana mataifa yanayojisikia kuwa yako salama. Nilikuwa nimewakasirikia Israeli kidogo tu, lakini mataifa hayo yaliwazidishia maafa.’

16 “Kwa hiyo, hivi ndivyo asemavyoBwana: ‘Nitairudia Yerusalemu kwa rehema na huko nyumba yangu itajengwa tena. Nayo kamba ya kupimia itanyoshwa Yerusalemu,’ asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

17 “Endelea kutangaza zaidi kwamba: Hivi ndivyo asemavyoBwanaMwenye Nguvu Zote: ‘Miji yangu itafurika tena ustawi naBwanaatamfariji tena Sayuni na kumchagua Yerusalemu.’ ”

Maono Ya Pili: Pembe Nne Na Mafundi Wanne

18 Kisha nikatazama juu, na pale mbele yangu nikaona pembe nne!

19 Nikamwuliza yule malaika aliyekuwa akizungumza nami, “Ni nini hivi?”

Akanijibu, “Hizi ni zile pembe zilizowatawanya Yuda, Israeli na Yerusalemu.”

20 KishaBwanaakanionyesha mafundi wanne.

21 Nikauliza, “Hawa wanakuja kufanya nini?”

Akanijibu, “Hizi ndizo pembe zilizowatawanya Yuda ili asiwepo atakayeweza kuinua kichwa chake, lakini mafundi wamekuja kuzitia hofu na kuzitupa chini hizi pembe za mataifa ambayo yaliinua pembe zao dhidi ya nchi ya Yuda na kuwatawanya watu wake.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ZEC/1-820ed10f4b850a2f4b472d51dc147d9d.mp3?version_id=1627—

Zekaria 2

Maono Ya Tatu: Mtu Mwenye Kamba Ya Kupimia

1 Kisha nikatazama juu: pale mbele yangu alikuwepo mtu mwenye kamba ya kupimia mkononi mwake!

2 Nikamwuliza, “Unakwenda wapi?”

Akanijibu, “Kupima Yerusalemu, kupata urefu na upana wake.”

3 Kisha malaika aliyekuwa akizungumza nami akaondoka, malaika mwingine akaja kukutana naye

4 na kumwambia: “Kimbia, umwambie yule kijana, ‘Yerusalemu utakuwa mji usio na kuta kwa sababu ya wingi wa watu na mifugo iliyomo.

5 Mimi mwenyewe nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka,’ asemaBwana, ‘nami nitakuwa utukufu wake ndani yake.’

6 “Njoni! Njoni! Kimbieni mtoke katika nchi ya kaskazini,” asemaBwana, “Kwa kuwa nimewatawanya kwenye pande nne za mbingu,” asemaBwana.

7 “Njoo, Ee Sayuni! Kimbia, wewe ukaaye ndani ya Binti Babeli!”

8 Kwa kuwa hivi ndivyo asemavyoBwanaMwenye Nguvu Zote: “Baada ya yeye kuniheshimu na kunituma mimi dhidi ya mataifa yaliyokuteka wewe nyara, kwa kuwa ye yote awagusaye ninyi, anaigusa mboni ya jicho lake,

9 hakika nitauinua mkono wangu dhidi yao ili watumwa wao wawateke nyara. Ndipo mtakapojua ya kwambaBwanaMwenye Nguvu Zote amenituma.

10 “Piga kelele na ufurahie, Ee Binti Sayuni, kwa maana ninakuja, nami nitaishi miongoni mwenu,” asemaBwana.

11 “Mataifa mengi yataunganishwa naBwanasiku hiyo, nao watakuwa watu wangu. Nitaishi miongoni mwenu nanyi mtajua kwambaBwanaMwenye Nguvu Zote amenituma kwenu.

12 Bwanaatairithi Yuda kama fungu lake katika nchi takatifu na atachagua tena Yerusalemu.

13 Tulieni mbele zaBwana, enyi watu wote, kwa sababu ameinuka kutoka makao yake matakatifu.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ZEC/2-06be10e5a99c4aa4dc8c4b6f42a72993.mp3?version_id=1627—

Zekaria 3

Maono Ya Nne: Mavazi Safi Kwa Ajili Ya Kuhani Mkuu

1 Kisha akanionyesha Yoshua, Kuhani Mkuu akiwa amesimama mbele ya malaika waBwana, naye Shetani amesimama upande wake wa kuume ili amshitaki.

2 Bwanaakamwambia Shetani, “Bwanaakukemee Shetani!Bwana, ambaye ameichagua Yerusalemu, akukemee! Je, mtu huyu siyo kijinga kinachowaka kilichonyakuliwa kwenye moto?”

3 Wakati huu, Yoshua alikuwa amevaa nguo chafu alipokuwa amesimama mbele ya malaika.

4 Malaika akawaambia wale waliokuwa wamesimama mbele yake, “Mvueni hizo nguo zake chafu.”

Kisha akamwambia Yoshua, “Tazama, nimeiondoa dhambi yako, nami nitakuvika mavazi ya kitajiri.”

5 Kisha nikasema, “Mvike kilemba kilicho safi kichwani mwake.” Kwa hiyo wakamvika kilemba safi kichwani na kumvika yale mavazi mengine, wakati malaika waBwanaakiwa amesimama karibu.

6 Malaika waBwanaakamwamuru Yoshua:

7 “Hivi ndivyo asemavyoBwanaMwenye Nguvu Zote: ‘Ikiwa utakwenda katika njia zangu na kushika masharti yangu, basi utaitawala nyumba yangu na kuwa na amri juu ya nyua zangu, nami nitakupa nafasi miongoni mwa hawa wasimamao hapa.

8 “ ‘Sikiliza, Ee Yoshua Kuhani Mkuu, pamoja na wenzako walioketi mbele yako, ambao ni watu walio ishara ya mambo yatakayokuja: Ninakwenda kumleta mtumishi wangu, Tawi.

9 Tazama, jiwe nililoliweka mbele ya Yoshua! Kuna macho saba juu ya jiwe lile moja, nami nitachora maandishi juu yake,’ asemaBwanaMwenye Nguvu Zote, ‘nami nitaiondoa dhambi ya nchi hii kwa siku moja.

10 “ ‘Katika siku hiyo kila mmoja wenu atamwalika jirani yake akae chini ya mzabibu wake na mtini wake,’ asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ZEC/3-c64274bd8a3b66d89d3b97fa83c4bb8b.mp3?version_id=1627—

Zekaria 4

Maono Ya Tano: Kinara Cha Taa Cha Dhahabu Na Mizeituni Miwili

1 Kisha malaika aliyezungumza nami akarudi na kuniamsha, kama mtu aamshwavyo kutoka katika usingizi wake.

2 Akaniuliza, “Unaona nini?”

Nikajibu, “Ninaona kinara cha taa cha dhahabu tupu, nacho kina bakuli juu yake na taa zake saba juu yake, tena iko mirija saba ya kuleta mafuta, kwenye taa zote zilizo juu yake.

3 Pia kuna mizeituni miwili karibu yake, mmoja upande wa kuume wa bakuli na mwingine upande wa kushoto.”

4 Nikamuuliza malaika aliyezungumza nami, “Hivi ni vitu gani, bwana wangu?”

5 Akanijibu, “Hujui kuwa hivi ni vitu gani?”

Nikajibu, “Hapana, bwana wangu.”

6 Kisha akaniambia, “Hili ni neno laBwanakwa Zerubabeli: ‘Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa Roho yangu,’ asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

7 “Wewe ni kitu gani, Ee mlima mkubwa sana? Mbele ya Zerubabeli wewe utakuwa ardhi tambarare. Kisha ataweka jiwe la juu kabisa la mwisho na watu wakipiga kelele wakisema, ‘Mungu libariki! Mungu libariki!’ ”

8 Kisha neno laBwanalikanijia:

9 “Mikono ya Zerubabeli iliweka msingi wa Hekalu hili, mikono yake pia italimalizia. Kisha mtajua ya kuwaBwanaMwenye Nguvu Zote amenituma mimi kwenu.

10 “Ni nani anayeidharau siku ya mambo madogo? Watu watashangilia watakapoona timazi mkononi mwa Zerubabeli.

“(Hizi saba ni macho yaBwanaambayo huzunguka duniani kote.)”

11 Kisha nikamwuliza yule malaika, “Hii mizeituni miwili iliyoko upande wa kuume na wa kushoto wa kinara cha taa ni nini?”

12 Tena nikamwuliza, “Haya matawi mawili ya mizeituni karibu na hiyo mirija miwili ya dhahabu inayomimina mafuta ya dhahabu ni nini?”

13 Akajibu, “Hujui kuwa haya ni nini?”

Nikamjibu, “Hapana, bwana wangu.”

14 Kwa hiyo akasema, “Hawa ni wawili ambao wamepakwa mafuta ili kumtumikia Bwana wa dunia yote.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ZEC/4-51d0f1bc6012e8fa94020756f8a1cb5a.mp3?version_id=1627—

Zekaria 5

Maono Ya Sita: Kitabu Kinachoruka

1 Nikatazama tena: na hapo mbele yangu kulikuwa na kitabu kilichoruka!

2 Akaniuliza, “Unaona nini?”

# Nikamjibu, “Naona kitabu kinachoruka chenye, urefu wa dhiraa ishirinina upana wa dhiraa kumi.”

3 Akaniambia, “Hii ni laana inayotoka kwenda juu ya nchi yote, kwa kuwa kufuatana na yale yaliyoandikwa katika upande mmoja, kila mwizi atafukuziwa mbali, pia kufuatana na yaliyo upande wa pili, kila aapaye kwa uongo atafukuziwa mbali.

4 BwanaMwenye Nguvu Zote asema, ‘Nitaituma hiyo laana, nayo itaingia katika nyumba ya mwizi na nyumba ya huyo aapaye kwa uongo kwa Jina langu. Itabaki katika nyumba yake na kuiharibu, pamoja na mbao zake na mawe yake.’ ”

Maono Ya Saba: Mwanamke Ndani Ya Kikapu

5 Kisha yule malaika aliyekuwa akizungumza nami akanijia na kuniambia, “Tazama juu uone ni nini kile kinachojitokeza.”

6 Nikamwuliza, “Ni kitu gani?”

Akanijibu, “Ni kikapu cha kupimia.” Kisha akaongeza kusema, “Huu ni uovu wa watu katika nchi nzima.”

7 Kisha kifuniko kilichotengenezwa kwa madini ya risasi kilichokuwa kimefunika kile kikapu, kiliinuliwa na ndani ya kile kikapu alikuweko mwanamke ameketi!

8 Akasema, “Huu ni uovu,” tena akamsukumia ndani ya kikapu na kushindilia kifuniko juu ya mdomo wa kikapu.

9 Kisha nikatazama juu: na pale mbele yangu, walikuwepo wanawake wawili, wakiwa na upepo katika mabawa yao! Walikuwa na mabawa kama ya korongo, nao wakainua kile kikapu na kuruka nacho kati ya mbingu na nchi.

10 Nikamwuliza yule malaika aliyekuwa akizungumza nami, “Wanakipeleka wapi hicho kikapu?”

11 Akanijibu, “Wanakipeleka katika nchi ya Babeli na kujenga nyumba kwa ajili yake. Itakapokuwa tayari, kikapu kitawekwa pale mahali pake.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ZEC/5-031fb2a0523b1a93f0ac97c4c8da5cd7.mp3?version_id=1627—

Zekaria 6

Maono Ya Nane: Magari Manne Ya Vita

1 Nikatazama juu tena: nikaona mbele yangu magari manne ya vita yakija kutoka kati ya milima miwili, milima ya shaba!

2 Gari la kwanza lilivutwa na farasi wekundu, la pili lilivutwa na farasi weusi,

3 la tatu lilivutwa na farasi weupe na gari la nne lilivutwa na farasi wa madoadoa ya kijivu, wote wenye nguvu.

4 Nikamwuliza malaika aliyekuwa akizungumza nami, “Hawa ni nani bwana wangu?”

5 Malaika akanijibu, “Hizi ni roho nne za mbinguni zisimamazo mbele ya uwepo wa Bwana wa dunia yote, zinatoka kwenda kufanya kazi yake.

6 Gari linalovutwa na farasi weusi linaelekea katika nchi ya kaskazini, la farasi weupe linaelekea magharibi na la farasi wa madoadoa ya kijivu linaelekea kusini.”

7 Wakati hao farasi wenye nguvu walipokuwa wakitoka, walikuwa wakijitahidi kwenda duniani kote. Akasema, “Nenda duniani kote!” Kwa hiyo wakaenda duniani kote.

8 Kisha akaniita, “Tazama, wale wanaokwenda kuelekea nchi ya kaskazini wamepumzisha Roho yangu katika nchi ya kaskazini.”

Taji Kwa Ajili Ya Yoshua

9 Neno laBwanalikanijia kusema:

10 “Chukua fedha na dhahabu kutoka kwa watu waliohamishwa, yaani Heldai, Tobia na Yedaya ambao wamefika kutoka Babeli. Siku iyo hiyo nenda nyumbani kwa Yosia mwana wa Sefania.

11 Chukua fedha na dhahabu utengeneze taji, nawe uiweke kichwani mwa Kuhani Mkuu Yoshua, mwana wa Yehosadaki.

12 Umwambie, hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote: ‘Huyu ndiye mtu ambaye jina lake ni Tawi, naye atachipua kutoka mahali pake na kujenga Hekalu laBwana.

13 Ni yeye atakayejenga Hekalu laBwana, naye atavikwa utukufu na ataketi kumiliki katika kiti cha enzi naye atakuwa kuhani katika kiti chake cha enzi. Hapo patakuwa amani kati ya hao wawili.’

14 Taji itatolewa kwa Heldai, Tobia, Yedaya na Heni mwana wa Sefania kama kumbukumbu ndani ya Hekalu laBwana.

15 Wale walio mbali sana watakuja na kusaidia kulijenga Hekalu laBwana, nanyi mtajua ya kwambaBwanaMwenye Nguvu Zote amenituma kwenu. Hili litatokea ikiwa mtamtiiBwanaMungu wenu kwa bidii.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ZEC/6-37bf2cdc07051c6c342943793dc898da.mp3?version_id=1627—