Zekaria 7

Haki Na Rehema, Sio Kufunga

1 Katika mwaka wa nne wa utawala wa Mfalme Dario, neno laBwanalilimjia Zekaria siku ya nne ya mwezi wa tisa, mwezi wa Kisleu.

2 Watu wa Betheli walikuwa wamemtuma Shareza na Regam-Meleki pamoja na watu wao, kumsihiBwana

3 kwa kuwauliza makuhani wa nyumba yaBwanaMwenye Nguvu Zote na manabii, “Je, imempasa kuomboleza na kufunga katika mwezi wa tano, kama ambavyo nimekuwa nikifanya kwa miaka mingi?”

4 Kisha neno laBwanaMwenye Nguvu Zote likanijia kusema:

5 “Waulize watu wote wa nchi na makuhani, ‘Je, mlipofunga na kuomboleza katika mwezi wa tano na wa saba kwa miaka sabini iliyopita, mlifunga kweli kwa ajili yangu?

6 Na mlipokuwa mkila na kunywa, je, hamkuwa mnasheherekea kwa ajili ya nafsi zenu?

7 Je, haya sio maneno yaBwanaaliyosema kupitia manabii waliotangulia, wakati Yerusalemu pamoja na miji inayoizunguka ilipokuwa katika hali ya utulivu na ya mafanikio, wakati Negebu na Shefala zikiwa zimekaliwa na watu?’ ”

8 Neno laBwanalikamjia tena Zekaria:

9 “Hivi ndivyo asemavyoBwanaMwenye Nguvu Zote: ‘Fanyeni hukumu za haki, onyesheni rehema na huruma ninyi kwa ninyi.

10 Msimwonee mjane wala yatima, mgeni wala maskini. Msiwaziane mabaya mioyoni mwenu ninyi kwa ninyi.’

11 “Lakini wakakataa kusikiliza, wakanipa kisogo kwa ukaidi na kuziba masikio yao.

12 Wakaifanya mioyo yao migumu kama jiwe gumu na hawakuisikiliza sheria au maneno ambayoBwanaMwenye Nguvu Zote aliyatuma kwa njia ya Roho wake kupitia manabii waliotangulia. Kwa hiyoBwanaMwenye Nguvu Zote alikasirika sana.

13 “ ‘Wakati nilipoita, hawakusikiliza, kwa hiyo walipoita, sikusikiliza,’ asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

14 ‘Niliwatawanya kwa upepo wa kisulisuli miongoni mwa mataifa yote, mahali ambapo walikuwa wageni. Nchi ikaachwa ukiwa nyuma yao kiasi kwamba hakuna aliyeweza kuingia au kutoka. Hivi ndivyo walivyoifanya ile nchi iliyokuwa imependeza kuwa ukiwa.’ ”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ZEC/7-d996fd37dc78e47b0482ee31ac2e93e0.mp3?version_id=1627—

Zekaria 8

Bwana Anaahidi Kuibariki Yerusalemu

1 Neno laBwanaMwenye Nguvu Zote likanijia tena.

2 Hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote: “Nina wivu sana kwa ajili ya Sayuni, ninawaka wivu kwa ajili yake.”

3 Hili ndilo asemaloBwana: “Nitarudi Sayuni na kufanya makao Yerusalemu. Kisha Yerusalemu utaitwa mji wa kweli, mlima waBwanaMwenye Nguvu Zote utaitwa Mlima Mtakatifu.”

4 Hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote: “Kwa mara nyingine tena wazee wanaume kwa wanawake walioshiba umri wataketi katika barabara za Yerusalemu, kila mmoja akiwa na mkongojo wake mkononi kwa sababu ya umri wake.

5 Barabara za mji zitajaa wavulana na wasichana wanaocheza humo.”

6 Hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote: “Mambo haya yanaweza kuonekana ya ajabu kwa mabaki ya watu wakati huo, lakini yaweza kuwa ya ajabu kwangu?” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

7 Hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote: “Nitawaokoa watu wangu kutoka nchi za mashariki na magharibi.

8 Nitawarudisha waje kuishi Yerusalemu, watakuwa watu wangu nami nitakuwa mwaminifu na wa haki kwao kama Mungu wao.”

9 Hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote: “Ninyi ambao sasa mnasikia maneno haya yanayozungumzwa na manabii ambao walikuwepo wakati wa kuwekwa kwa msingi wa nyumba yaBwanaMwenye Nguvu Zote, mikono yenu na iwe na nguvu ili Hekalu liweze kujengwa.

10 Kabla ya wakati huo, hapakuwepo na ujira kwa mtu wala mnyama. Hakuna mtu aliyeweza kufanya shughuli yake kwa usalama kwa sababu ya adui yake, kwa kuwa nilikuwa nimemfanya kila mtu adui wa jirani yake.

11 Lakini sasa sitawatendea mabaki ya watu hawa kama nilivyowatenda zamani,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

12 “Mbegu itakua vizuri, mzabibu utazaa matunda yake, ardhi itatoa mazao yake, na mbingu zitadondosha umande wake. Vitu hivi vyote nitawapa mabaki ya watu kama urithi wao.

13 Jinsi mlivyokuwa kitu cha laana katikati ya mataifa, Ee Yuda na Israeli, ndivyo nitakavyowaokoa, nanyi mtakuwa baraka. Msiogope, bali iacheni mikono yenu iwe na nguvu.”

14 Hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote: “Kama nilivyokuwa nimekusudia kuleta maangamizi juu yenu, wakati baba zenu waliponikasirisha na sikuonyesha huruma,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote,

15 “hivyo sasa nimeazimia kufanya mema tena kwa Yerusalemu na Yuda. Msiogope.

16 Haya ndiyo mtakayoyafanya: Semeni kweli kila mtu kwa mwenzake, mtoe hukumu ya kweli na haki kwenye mahakama zenu,

17 usipange mabaya dhidi ya jirani yako, msipende kuapa kwa uongo, nayachukia yote haya,” asemaBwana.

18 Neno laBwanaMwenye Nguvu Zote likanijia tena.

19 Hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote: “Saumu za miezi ya nne, tano, saba na kumi itakuwa sikukuu za furaha na za shangwe kwa Yuda. Kwa hiyo uipende kweli na amani.”

20 Hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote: “Mataifa mengi na wakazi wa miji mingi watakuja,

21 na wenyeji wa mji mmoja watakwenda kwenye mji mwingine na kusema, ‘Twende mara moja na tukamsihiBwana, na kumtafutaBwanaMwenye Nguvu Zote. Mimi mwenyewe ninakwenda.’

22 Pia watu wa kabila nyingi na mataifa yenye nguvu yatakuja Yerusalemu kumtafutaBwanaMwenye Nguvu Zote na kumsihi.”

23 Hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote: “Katika siku hizo watu kumi kutoka lugha zote na mataifa, watang’ang’ania upindo wa joho la Myahudi mmoja na kusema, ‘Twende pamoja nawe kwa sababu tumesikia kwamba Mungu yu pamoja nawe.’ ”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ZEC/8-2a05f3df0113be2add0cbb18079c346b.mp3?version_id=1627—

Zekaria 9

Hukumu Juu Ya Adui Za Israeli

Neno

1 Neno laBwanaliko kinyume na nchi ya Hadraki

na Dameski itakuwa mahali pa kupumzika,

kwa kuwa macho ya watu na ya kabila zote

za Israeli yako kwaBwana,

2 pia juu ya Hamathi inayopakana nayo,

juu ya Tiro na Sidoni,

ingawa wana ujuzi mwingi sana.

3 Tiro amejijengea ngome imara,

amelundika fedha kama mavumbi

na dhahabu kama taka za mitaani.

4 Lakini Bwana atamwondolea mali zake

na kuuangamiza uwezo wake wa baharini,

naye atateketezwa kwa moto.

5 Ashkeloni ataona hili na kuogopa;

Gaza atagaagaa kwa maumivu makali,

pia Ekroni, kwa sababu

matumaini yake yatanyauka.

Gaza atampoteza mfalme wake

na Ashkeloni ataachwa pweke.

6 Wageni watakalia mji wa Ashdodi,

nami nitakatilia mbali kiburi cha Wafilisti.

7 Nitaondoa damu vinywani mwao,

chakula kile walichokatazwa kati ya meno yao.

Mabaki yao yatakuwa mali ya Mungu wetu,

nao watakuwa viongozi katika Yuda,

naye Ekroni atakuwa kama Wayebusi.

8 Lakini nitailinda nyumba yangu

dhidi ya majeshi ya wanyang’anyi.

Kamwe mdhalimu hatashambulia watu wangu tena,

kwa maana sasa ninawachunga.

Kuja Kwa Mfalme Wa Sayuni

9 Shangilia sana, Ee Binti Sayuni!

Piga kelele, Binti Yerusalemu!

Tazama, Mfalme wako anakuja kwako,

ni mwenye haki naye ana wokovu,

mpole naye amepanda punda,

mwana punda, mtoto wa punda.

10 Nitaondoa magari ya vita kutoka Efraimu

na farasi wa vita kutoka Yerusalemu,

nao upinde wa vita utavunjwa.

Atatangaza amani kwa mataifa.

Utawala wake utaenea kutoka bahari hadi bahari,

na kutoka Mto Eufrati hadi mwisho wa dunia.

11 Kwako wewe, kwa sababu ya damu ya Agano langu nawe,

nitawaacha huru wafungwa wako

watoke kwenye shimo lisilo na maji.

12 Rudieni ngome yenu, Enyi wafungwa wa tumaini;

hata sasa ninatangaza kwamba

nitawarejesheeni maradufu.

13 Nitampinda Yuda kama nipindavyo upinde wangu,

nitamfanya Efraimu mshale wangu.

Nitawainua wana wako, Ee Sayuni,

dhidi ya wana wako, Ee Uyunani,

na kukufanya kama upanga wa shujaa wa vita.

Bwana Atatokea

14 KishaBwanaatawatokea;

mshale wake utamulika

kama umeme wa radi.

BwanaMwenyezi atapiga tarumbeta,

naye atatembea katika tufani za kusini,

15 naBwanaMwenye Nguvu Zote atawalinda.

Wataangamiza na kushinda

kwa mawe ya kutupa kwa kombeo.

Watakunywa na kunguruma kama waliolewa mvinyo;

watajaa kama bakuli linalotumika kunyunyizia

kwenye pembe za madhabahu.

16 BwanaMungu wao atawaokoa siku hiyo

kama kundi la watu wake.

Watang’ara katika nchi yake

kama vito vya thamani kwenye taji.

17 Jinsi gani watavutia na kuwa wazuri!

Nafaka itawastawisha vijana wanaume,

nayo divai mpya vijana wanawake.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ZEC/9-08089358769e121f8d7a1cfb11bd5758.mp3?version_id=1627—

Zekaria 10

Bwana Ataitunza Yuda

1 MwombeniBwanamvua wakati wa vuli;

ndiyeBwanaatengenezaye mawingu ya tufani.

Huwapa watu manyunyu ya mvua,

pia mimea ya shambani kwa ajili ya kila mtu.

2 Sanamu huzungumza udanganyifu,

waaguzi huona maono ya uongo;

husimulia ndoto ambazo si za kweli,

wanatoa faraja batili.

Kwa hiyo watu wanatangatanga kama kondoo

walioonewa kwa kukosa mchungaji.

3 “Hasira yangu inawaka dhidi ya wachungaji,

nami nitawaadhibu viongozi;

kwa kuwaBwanaMwenye Nguvu Zote

atalichunga kundi lake,

nyumba ya Yuda,

naye atawafanya kuwa kama farasi

mwenye kiburi akiwa vitani.

4 Kutoka Yuda litatokea Jiwe la pembeni,

kutoka kwake vitatoka vigingi vya hema,

kutoka kwake utatoka upinde wa vita,

kutoka kwake atatoka kila mtawala.

5 Kwa pamoja watakuwa kama mashujaa

wanaokanyaga barabara za matope

wakati wa vita.

Kwa sababuBwanayu pamoja nao,

watapigana na kuwashinda wapanda farasi.

6 “Nitaiimarisha nyumba ya Yuda

na kuiokoa nyumba ya Yosefu.

Nitawarejesha kwa sababu

nina huruma juu yao.

Watakuwa kama watu ambao

sijawahi kuwakataa

kwa sababu mimi ndimiBwanaMungu wao,

nami nitawajibu.

7 Waefraimu watakuwa kama mashujaa,

mioyo yao itafurahi kana kwamba ni kwa divai.

Watoto wao wataona na kufurahi,

mioyo yao itashangilia katikaBwana.

8 Nitawaashiria na kuwakusanya ndani.

Hakika nitawakomboa,

nao watakuwa wengi

kama walivyokuwa mwanzoni.

9 Ijapokuwa niliwatawanya miongoni mwa mataifa,

hata hivyo wakiwa katika nchi za mbali

watanikumbuka mimi.

Wao na watoto wao watanusurika katika hatari

nao watarudi.

10 Nitawarudisha kutoka Misri

na kuwakusanya toka Ashuru.

Nitawaleta katika nchi ya Gileadi na Lebanoni,

na hapo hapatakuwa na nafasi ya kuwatosha.

11 Watapita katika bahari ya mateso;

bahari iliyochafuka itatulizwa

na vilindi vyote vya Mto Nile vitakauka.

Kiburi cha Ashuru kitashushwa,

nayo fimbo ya utawala ya Misri itatoweka.

12 Nitawaimarisha katikaBwana,

na katika jina lake watatembea,”

asemaBwana.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ZEC/10-7ec337ae9edf5ebc6d71d1068febb350.mp3?version_id=1627—

Zekaria 11

1 Fungua milango yako, Ee Lebanoni,

ili moto uteketeze mierezi yako!

2 Piga yowe, Ee mti wa msunobari,

kwa kuwa mwerezi umeanguka;

miti ya fahari imeharibiwa!

Piga yowe, enyi mialoni ya Bashani,

msitu mnene umefyekwa!

3 Sikiliza yowe ya wachungaji;

malisho yao manono yameangamizwa!

Sikia ngurumo za simba;

kichaka kilichostawi sana

cha Yordani kimeharibiwa!

Wachungaji Wawili Wa Kondoo

4 Hili ndilo asemaloBwanaMungu wangu: “Lilishe kundi lililokusudiwa kuchinjwa.

5 Wanunuzi wake huwachinja na kuondoka pasipo kuadhibiwa. Wale wanaowauza husema, ‘Bwanaasifiwe, mimi ni tajiri!’ Wachungaji wao wenyewe hawawahurumii.

6 Kwa kuwa sitawahurumia tena watu wa nchi,” asemaBwana. “Nitawakabidhi kila mtu mkononi mwa jirani yake na mfalme wake. Wataitenda jeuri nchi, nami sitawaokoa kutoka mikononi mwao.”

7 Kwa hiyo nikalilisha kundi lililotiwa alama kwa kuchinjwa, hasa kundi lililoonewa sana. Kisha nikachukua fimbo mbili, moja nikaiita Fadhili na nyingine Umoja, nami nikalilisha kundi.

8 Katika mwezi mmoja nikawaondoa wachungaji watatu.

Kundi la kondoo likanichukia, nami nikachoshwa nao,

9 nikasema, “Sitakuwa mchungaji wenu. Waache wanaokufa wafe na wanaoangamia waangamie. Wale waliobakia kila mmoja na ale nyama ya mwenzake.”

10 Kisha nikachukua fimbo yangu inayoitwa Fadhili nikaivunja, kutangua Agano nililofanya na mataifa yote.

11 Likatanguka siku hiyo, kwa hiyo wale waliodhurika katika kundi, waliokuwa wakiniangalia wakajua kuwa hilo lilikuwa neno laBwana.

12 Nikawaambia, “Mkiona kuwa ni vyema, nipeni ujira wangu, la sivyo, basi msinipe.” Kwa hiyo wakanilipa vipande thelathini vya fedha.

13 NayeBwanaakaniambia, “Mtupie mfinyanzi”: hiyo bei nzuri waliyonithaminia! Kwa hiyo nikachukua hivyo vipande thelathini vya fedha na kumtupia huyo mfinyanzi katika nyumba yaBwana.

14 Kisha nikaivunja fimbo yangu ya pili iitwayo Umoja, kuvunja udugu kati ya Yuda na Israeli!

15 KishaBwanaakaniambia, “Vitwae tena vifaa vya mchungaji mpumbavu.

16 Kwa maana ninakwenda kumwinua mchungaji juu ya nchi ambaye hatamjali aliyepotea, wala kuwatafuta wale wachanga au kuwaponya waliojeruhiwa, wala kuwalisha wenye afya, lakini atakula nyama ya kondoo wanono na kuzirarua kwato zao.

17 “Ole wa mchungaji asiyefaa,

anayeliacha kundi!

Upanga na uupige mkono wake na jicho lake la kuume!

Mkono wake na unyauke kabisa,

jicho lake la kuume lipofuke kabisa!”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ZEC/11-0b5e697f06c9d0abe484dd4a4beb0ab5.mp3?version_id=1627—

Zekaria 12

Maadui Wa Yerusalemu Kuangamizwa

1 Hili ni neno laBwanakuhusu Israeli.Bwana, yeye azitandaye mbingu, awekaye misingi ya dunia na aiumbaye roho ya mwanadamu ndani yake, asema:

2 “Nitakwenda kufanya Yerusalemu kuwa kikombe cha kulewalewa kwa mataifa yote yanayoizunguka. Yuda utazingirwa kwa vita na Yerusalemu pia.

3 Katika siku hiyo, wakati mataifa yote ya dunia yatakapokusanyika dhidi yake, nitaufanya Yerusalemu kuwa jabali lisilosogezwa kwa mataifa yote. Wote watakaojaribu kulisogeza watajiumiza wenyewe.

4 Katika siku hiyo nitampiga kila farasi kwa hofu ya ghafula, naye ampandaye nitampiga kwa uwazimu,” asemaBwana. “Nitalielekeza jicho langu la ulinzi juu ya nyumba ya Yuda, nami nitawapofusha farasi wote wa mataifa.

5 Kisha viongozi wa Yuda watasema mioyoni mwao, ‘Watu wa Yerusalemu wana nguvu kwa sababuBwanaMwenye Nguvu Zote ni Mungu wao.’

6 “Katika siku hiyo nitawafanya viongozi wa Yuda kuwa kama kigae cha moto ndani ya lundo la kuni, kama mwenge uwakao kati ya miganda. Watateketeza kulia na kushoto mataifa yote yanayowazunguka, lakini Yerusalemu utabaki salama mahali pake.

7 “Bwanaatayaokoa makao ya Yuda kwanza, ili heshima ya nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu isiwe kubwa zaidi kuliko ile ya Yuda.

8 Katika siku hiyo,Bwanaatawakinga wale waishio Yerusalemu, ili kwamba aliye dhaifu kupita wote miongoni mwao awe kama Daudi, nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama Malaika waBwanaakiwatangulia.

9 Katika siku hiyo nitatoka kuangamiza mataifa yote yatakayoushambulia Yerusalemu.

Kumwombolezea Yule Aliyechomwa Mkuki

10 “Nami nitamiminia nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu roho ya neemana maombi. Watanitazama mimi, yule waliyemchoma, nao watamwombolezea kama mtu anayemwombolezea mwanawe wa pekee na kusikitika kwa uchungu kama anayemsikitikia mzaliwa wake wa kwanza wa kiume.

11 Katika siku hiyo kilio kitakuwa kikubwa Yerusalemu, kama kilio cha Hadad-Rimoni katika tambarare ya Megido.

12 Nchi itaomboleza, kila ukoo peke yake, nao wake zao peke yao. Ukoo wa nyumba ya Daudi na wake zao, ukoo wa nyumba ya Nathani na wake zao,

13 ukoo wa nyumba ya Lawi na wake zao, ukoo wa Shimei na wake zao,

14 na koo zote zilizobaki na wake zao.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ZEC/12-45113d9771af5d9b045bd9d1bcff06e4.mp3?version_id=1627—

Zekaria 13

Kutakaswa Dhambi

1 “Katika siku hiyo, chemchemi itafunguliwa kwa nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu, kuwatakasa dhambi na unajisi.

2 “Katika siku hiyo, nitayakatilia mbali majina ya sanamu kutoka nchi, nayo hayatakumbukwa tena,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote. “Nitaondoa manabii wao pamoja na roho ya uchafu katika nchi.

3 Ikiwa yupo ye yote atakayeendelea kutabiri, baba yake na mama yake waliomzaa watamwambia, ‘Ni lazima ufe, kwa sababu umesema uongo kwa jina laBwana.’ Atakapotabiri, wazazi wake mwenyewe watampasua tumbo.

4 “Katika siku hiyo, kila nabii ataaibika kwa maono ya unabii wake. Hatavaa vazi la kinabii la nywele ili apate kudanganya watu.

5 Atasema, ‘Mimi sio nabii. Mimi ni mkulima; ardhi imekuwa kazi yangu tangu ujana wangu.’

6 Ikiwa mtu atamwuliza, ‘Majeraha haya yaliyo mwilini mwako ni ya nini?’ Atajibu, ‘Ni majeraha niliyoyapata katika nyumba ya rafiki zangu.’

Mchungaji Apigwa, Nao Kondoo Watawanyika

7 “Amka, Ee upanga, dhidi ya mchungaji wangu,

dhidi ya mtu aliye karibu nami!”

asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

“Mpige mchungaji,

nao kondoo watatawanyika,

nami nitageuza mkono wangu

dhidi ya walio wadogo,

8 katika nchi yote,” asemaBwana,

“theluthi mbili watapigwa na kuangamia;

hata hivyo theluthi moja watabakia ndani yake.

9 Hii theluthi moja nitaileta katika moto;

nitawasafisha kama fedha isafishwavyo

na kuwajaribu kama dhahabu.

Wataliitia Jina langu

nami nitawajibu;

nitasema, ‘Hawa ni watu wangu,’

nao watasema, ‘Bwanani Mungu wetu.’ ”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ZEC/13-e23899078fb1e45117b740bf03ba066c.mp3?version_id=1627—

Zekaria 14

Bwana Yuaja Kutawala

1 Siku yaBwanainakuja ambayo nyara zilizotekwa kwenu zitagawanywa miongoni mwenu.

2 Nitayakusanya mataifa yote huko Yerusalemu kupigana dhidi yake, mji utatekwa, nyumba zitavamiwa na kuporwa na wanawake watanajisiwa. Nusu ya mji watakwenda uhamishoni, lakini watakaobaki hawataondolewa kutoka mjini.

3 KishaBwanaatatoka na kupigana dhidi ya watu wa yale mataifa, kama apiganavyo siku ya vita.

4 Siku hiyo miguu yake itasimama juu ya Mlima wa Mizeituni, mashariki mwa Yerusalemu, nao Mlima wa Mizeituni utagawanyika mara mbili kuanzia mashariki hadi magharibi, ukifanya bonde kubwa, nusu ya mlima ukisogea kuelekea kaskazini na nusu kuelekea kusini.

5 Nanyi mtakimbia kupitia katika bonde hilo la mlima wangu kwa kuwa litaenea hadi Aseli. Mtakimbia kama mlivyokimbia tetemeko la ardhi katika siku za Uzia mfalme wa Yuda. KishaBwanaMungu wangu atakuja na watakatifu wote pamoja naye.

6 Siku hiyo hakutakuwepo nuru, baridi wala theluji.

7 Itakuwa siku ya kipekee, isiyo na mchana wala usiku, siku ijulikanayo naBwana. Jioni inapofika nuru itakuwepo.

8 Siku hiyo, maji yaliyo hai yatatiririka kutoka Yerusalemu, nusu kwenda kwenye bahari ya masharikina nusu kwenda kwenye bahari ya magharibi, wakati wa kiangazi na wakati wa masika.

9 Bwanaatakuwa mfalme juu ya dunia yote. Katika siku hiyo atakuwepoBwanammoja na jina lake litakuwa jina pekee.

10 Nchi yote kuanzia Geba, kaskazini mwa Yuda, hadi Rimoni, kusini mwa Yerusalemu, itakuwa kama Araba. Lakini Yerusalemu utainuliwa juu na kubaki mahali pake, toka Lango la Benyamini hadi mahali pa Lango la Kwanza, mpaka kwenye Lango la Pembeni na kutoka Mnara wa Hananeli hadi kwenye mashinikizo ya divai ya mfalme.

11 Utakaliwa na watu, kamwe hautaharibiwa tena, Yerusalemu utakaa salama.

12 Hii ndiyo tauni ambayoBwanaatapiga nayo mataifa yote ambayo yalipigana dhidi ya Yerusalemu: Nyama ya miili yao itaoza wangali wamesimama kwa miguu yao, macho yao yataoza kwenye matundu yake na ndimi zao zitaoza vinywani mwao.

13 Katika siku hiyoBwanaatawatia wanaume hofu kuu. Kila mwanaume atakamata mkono wa mwenzake nao watashambuliana.

14 Yuda pia atapigana katika Yerusalemu. Utajiri wa mataifa yote yanayoizunguka Yerusalemu utakusanywa, wingi wa dhahabu, fedha na nguo.

15 Tauni ya aina iyo hiyo itapiga farasi na nyumbu, ngamia na punda, nao wanyama wote walioko kwenye kambi za adui.

16 Kisha walionusurika katika mataifa yote ambayo yaliushambulia Yerusalemu watakuwa wakipanda Yerusalemu kila mwaka kumwabudu Mfalme,BwanaMwenye Nguvu Zote na kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda.

17 Ikiwa taifa lo lote la dunia hawatakwenda Yerusalemu kumwabudu Mfalme,BwanaMwenye Nguvu Zote, mvua haitanyesha kwao.

18 Ikiwa watu wa Misri nao hawatakwenda kushiriki, hawatapata mvua.Bwanaataleta juu yao tauni ile ambayo itawapiga mataifa yale ambayo hayatakwenda kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda.

19 Hii itakuwa adhabu ya Misri na adhabu ya mataifa yote yale ambayo hayatakwenda Yerusalemu kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda.

20 Katika siku hiyo, kengele zilizofungwa kwenye farasi zitaandikwa maneno haya: TAKATIFU KWABwana, navyo vyungu vya kupikia katika nyumba yaBwanavitakuwa kama bakuli takatifu mbele ya madhabahu.

21 Kila chungu kilichoko Yerusalemu na Yuda kitakuwa kitakatifu kwaBwanaMwenye Nguvu Zote na wote wanaokuja kutoa dhabihu watachukua baadhi ya vyungu hivyo na kupikia. Katika siku hiyo hatakuwepo tena mfanyabiashara katika nyumba yaBwanaMwenye Nguvu Zote.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ZEC/14-698a795a95f1f16342cf6326c69ea23d.mp3?version_id=1627—

Hagai 1

Wito Wa Kuijenga Nyumba Ya Bwana

1 Katika mwaka wa pili wa utawala wa Mfalme Dario wa Uajemi, katika siku ya kwanza ya mwezi wa sita, neno laBwanalilikuja kupitia kwa nabii Hagai kwenda kwa Zerubabeli mwana wa Shealtieli, mtawala wa Yuda na kwa Kuhani Mkuu Yoshuamwana wa Yehosadaki:

2 Hivi ndivyo asemavyoBwanaMwenye Nguvu Zote: “Hawa watu husema, ‘Wakati haujawadia wa kujenga nyumba yaBwana.’ ”

3 Kisha neno laBwanalikaja kupitia kwa nabii Hagai:

4 “Je, ni wakati wenu ninyi wa kuishi katika nyumba zenu zilizojengwa vizuri, wakati hii nyumba ikibaki, gofu?”

5 Sasa hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote: “Zitafakarini vyema njia zenu.

6 Mmepanda vingi, lakini mmevuna haba. Mnakula lakini hamshibi, mnakunywa, lakini hamtosheki. Mnavaa nguo, lakini hamsikii joto. Mnapata mishahara, lakini inatoweka kama imewekwa kwenye mfuko uliotobokatoboka.”

7 Hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote: “Zitafakarini vyema njia zenu.

8 Pandeni milimani mkalete miti na kujenga nyumba, ili nipate kuifurahia nitukuzwe.”

9 “Mlitarajia mengi, kumbe, yametokea kidogo. Ulichokileta nyumbani nilikipeperusha. Kwa nini?” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote. “Ni kwa sababu ya nyumba yangu, inayobaki katika hali ya magofu, wakati kila mmoja wenu anajishughulisha na nyumba yake mwenyewe.

10 Kwa hiyo, kwa sababu yenu mbingu zimezuia umande wake na ardhi mavuno yake.

11 Niliita ukame mashambani na milimani, kwenye nafaka, mvinyo mpya, mafuta pamoja na cho chote kinachozalishwa na ardhi, juu ya watu na ng’ombe, pamoja na kazi za mikono yenu.”

12 Kisha Zerubabeli mwana wa Shealtieli, Yoshua Kuhani Mkuu mwana wa Yehosadaki, pamoja na mabaki yote ya watu wakaitii sauti yaBwanaMungu wao pamoja na ujumbe wa nabii Hagai, kwa sababu alikuwa ametumwa naBwanaMungu wao. Watu walimwogopaBwana.

13 Kisha Hagai, mjumbe waBwana, akawapa watu ujumbe huu waBwana, “Mimi niko pamoja nanyi,” asemaBwana.

14 Kwa hiyoBwanaakachochea roho ya Zerubabeli mwana wa Shealtieli, mtawala wa Yuda, na roho ya Kuhani Mkuu Yoshua mwana wa Yehosadaki, pamoja na roho ya mabaki yote ya watu. Walikuja wakaanza kufanya kazi katika nyumba yaBwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wao,

15 katika siku ya ishirini na nne mwezi wa sita katika mwaka wa pili wa utawala wa Mfalme Dario.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/HAG/1-69a75d53ced7552db5a3c2fe4a8597fc.mp3?version_id=1627—

Hagai 2

Utukufu Ulioahidiwa Wa Nyumba Mpya

1 Katika siku ya ishirini na moja ya mwezi wa saba, neno laBwanalilikuja kupitia nabii Hagai, kusema,

2 “Sema na Zerubabeli mwana wa Shealtieli, mtawala wa Yuda, Kuhani Mkuu Yoshua mwana wa Yehosadaki na mabaki ya watu. Uwaulize,

3 ‘Ni nani miongoni mwenu aliyebaki ambaye aliiona hii nyumba katika utukufu wake wa mwanzo? Sasa inaonekanaje kwenu? Je, haionekani kwenu kama si kitu?

4 Lakini sasa uwe imara, Ee Zerubabeli,’ asemaBwana. ‘Kuwa imara, Ee Kuhani Mkuu Yoshua mwana wa Yehosadaki. Muwe imara, enyi watu wote wa nchi,’ asemaBwana, ‘na mfanye kazi. Kwa kuwa mimi nipo pamoja nanyi,’ asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

5 ‘Hili ndilo nililoagana nanyi mlipotoka katika nchi ya Misri. Pia Roho wangu anadumu katikati yenu. Msiogope.’

6 “Hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote, ‘Baada ya muda kidogo kwa mara nyingine nitazitingisha mbingu na nchi, bahari na nchi kavu.

7 Nitatikisa mataifa yote, nacho kile kinachotamaniwa na mataifa yote kitakuja, nami nitaujaza utukufu katika nyumba hii,’ asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

8 ‘Fedha ni mali yangu na dhahabu ni mali yangu,’ asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

9 ‘Utukufu wa nyumba hii ya sasa utakuwa mkubwa kuliko utukufu wa ile nyumba ya mwanzoni,’ asemaBwanaMwenye Nguvu Zote. ‘Na mahali hapa nitawapa amani,’ asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.”

Baraka Kwa Watu Waliotiwa Unajisi

10 Katika siku ya ishirini na nne ya mwezi wa tisa, katika mwaka wa pili wa utawala Mfalme Dario, neno laBwanalilikuja kwa nabii Hagai:

11 “Hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote: ‘Ulizeni makuhani jinsi sheria inavyosema:

12 Kama mtu akibeba nyama iliyowekwa wakfu katika pindo la vazi lake, kisha lile pindo likagusa mkate au mchuzi, divai, mafuta au chakula kingine, je, kitu hicho kitakuwa kimewekwa wakfu?’ ”

Makuhani wakajibu, “La hasha.”

13 Kisha Hagai akasema, “Je, kama mtu aliyetiwa unajisi kwa kugusa maiti akigusa mojawapo ya vitu hivi, kitu hicho kitakuwa kimetiwa unajisi?”

Makuhani wakajibu, “Ndiyo, huwa kimenajisiwa.”

14 Kisha Hagai akasema, “ ‘Basi ndivyo walivyo machoni pangu hawa watu na taifa hili,’ asemaBwana. ‘Lo lote wafanyalo na cho chote watoacho hapo ni najisi.

15 “ ‘Sasa fikirini kwa uangalifu kuanzia leo na kuendelea, pia tafakarini jinsi mambo yalivyokuwa kabla halijawekwa jiwe moja juu ya lingine katika Hekalu laBwana.

16 Wakati mtu alipoendea lundo la nafaka la vipimo ishirini, kulikuwa na vipimo kumi tu. Wakati mtu alipoendea pipa la mvinyo ili kuchota vipimo hamsini, kulikuwa na vipimo ishirini tu.

17 Kazi zenu zote za mikono nilizipiga kwa ukame, ukungu na mvua ya mawe, lakini hata hivyo, hamkunigeukia mimi,’ asemaBwana.

18 ‘Tangu leo na kuendelea, kuanzia siku hii ya ishirini na nne ya mwezi wa tisa, tafakarini siku ambayo msingi wa Hekalu laBwanauliwekwa. Tafakarini.

19 Je, bado kuna mbegu iliyobakia ghalani? Mpaka sasa, hakuna mzabibu au mtini, mkomamanga wala mzeituni uliozaa tunda.

“ ‘Kuanzia leo na kuendelea, nitawabariki.’ ”

Zerubabeli Pete Ya Muhuri Ya Bwana

20 Neno laBwanalikamjia Hagai kwa mara ya pili katika siku ya ishirini na nne ya mwezi kusema,

21 “Mwambie Zerubabeli mtawala wa Yuda kwamba nitazitikisa mbingu na nchi.

22 Nitapindua viti vya enzi vya kifalme na kuziharibu kabisa nguvu za falme za kigeni. Nitapindua magari ya vita pamoja na waendeshaji wake; farasi na wapanda farasi wataanguka, kila mmoja kwa upanga wa ndugu yake.

23 “ ‘Katika siku ile,’ asemaBwanaMwenye Nguvu Zote, ‘nitakuchukua wewe, mtumishi wangu Zerubabeli, mwana wa Shealtieli,’ asemaBwana. ‘Nitakufanya kama pete yangu ya muhuri, kwa kuwa nimekuchagua,’ asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/HAG/2-26cce82c34d9eebd11892eb101f1a27b.mp3?version_id=1627—