Ezekieli 12

Kutekwa Kwa Yuda Kwaelezwa

1 Neno laBwanalikanijia kusema:

2 “Mwanadamu, unaishi miongoni mwa watu waasi. Wana macho ya kuona, lakini hawaoni na masikio ya kusikia lakini hawasikii, kwa kuwa ni watu waasi.

3 “Kwa hiyo, mwanadamu, funga mizigo yako kwa kwenda uhamishoni tena wakati wa mchana, wakiwa wanakutazama, toka nje na uende mahali pengine kutoka hapo ulipo. Labda wataelewa, ingawa wao ni nyumba ya kuasi.

4 Wakati wa mchana, wakiwa wanakutazama, toa nje mizigo yako iliyofungwa kwa ajili ya kwenda uhamishoni. Kisha wakati wa jioni, wakiwa wanakutazama toka nje kama wale waendao uhamishoni.

5 Wakiwa wanakutazama, toboa ukuta utolee mizigo yako hapo.

6 Beba mizigo hiyo begani mwako wakikuangalia uichukue nje wakati wa giza la jioni. Funika uso wako ili usione nchi, kwa maana nimekufanya ishara kwa nyumba ya Israeli.”

7 Basi nikafanya kama nilivyoamuriwa. Wakati wa mchana nilitoa vitu vyangu nje vilivyofungwa tayari kwa uhamishoni. Kisha wakati wa jioni nikatoboa ukuta kwa mikono yangu. Nikachukua mizigo yangu nje wakati wa giza la jioni, nikiwa nimeibeba mabegani mwangu huku wakinitazama.

8 Asubuhi neno laBwanalikanijia kusema:

9 “Mwanadamu, je, nyumba ile ya kuasi ya Israeli haikukuuliza, ‘Unafanya nini?’

10 “Waambie, ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Neno hili linamhusu mkuu aliye katika Yerusalemu na nyumba yote ya Israeli ambao wako huko.’

11 Waambie, ‘Mimi ndiye ishara kwenu.’

“Kama vile nilivyotenda, basi litatendeka vivyo hivyo kwao. Watakwenda uhamishoni kama mateka.

12 “Naye mkuu aliye miongoni mwao atabeba mizigo yake begani mwake kwenye giza la jioni na kuondoka na tundu litatobolewa ukutani kwa ajili yake ili kupitia hapo. Atafunika uso wake ili kwamba asiweze kuiona nchi.

13 Nitatandaza wavu wangu kwa ajili yake, naye atanaswa kwenye mtego wangu, nitamleta mpaka Babeli, nchi ya Wakaldayo, lakini hataiona, naye atafia huko.

14 Wote wanaomzunguka nitawatawanya pande zote, watumishi wake na majeshi yake yote, nami nitawafuatilia kwa upanga uliofutwa.

15 “Wao watajua kwamba Mimi ndimiBwana, nitakapowatawanya miongoni mwa mataifa na kuwafukuza huko na huko katika nchi zote.

16 Lakini nitawaacha wachache wao waokoke na upanga, njaa na tauni, ili kwamba katika mataifa watakakokwenda waweze kutambua matendo ya machukizo waliotenda. Ndipo watajua kuwa Mimi ndimiBwana.”

17 Neno laBwanalikanijia kusema:

18 “Mwanadamu, tetemeka wakati ulapo chakula chako, tetemeka kwa hofu wakati unywapo maji yako.

19 Waambie watu wa nchi: ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo kuhusu hao wanaoishi Yerusalemu na katika nchi ya Israeli: Watakula chakula chao kwa wasiwasi na kunywa maji yao kwa kufadhaika, kwa kuwa nchi yao itanyang’anywa kila kitu chake kwa sababu ya udhalimu wa wote wanaoishi humo.

20 Miji inayokaliwa na watu itaharibiwa na nchi itakuwa ukiwa. Ndipo mtakapojua kwamba Mimi ndimiBwana.’ ”

21 Neno laBwanalikanijia kusema:

22 “Mwanadamu, ni nini hii mithali mlio nayo katika nchi ya Israeli: ‘Siku zinapita na hakuna maono yo yote yanayotimia?’

23 Waambie, ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Nitaikomesha mithali hii, nao hawataitumia tena katika Israeli.’ Waambie, ‘Siku zimekaribia wakati kila maono yatakapotimizwa.

24 Kwa maana hapatakuwepo tena na maono ya uongo wala ubashiri wa udanganyifu miongoni mwa watu wa Israeli.

25 Lakini MimiBwananitasema neno nitakalo, nalo litatimizwa bila kuchelewa. Kwa maana katika siku zako, wewe nyumba ya kuasi, nitatimiza kila nisemalo, asemaBwanaMwenyezi.’ ”

26 Neno laBwanalikanijia kusema:

27 “Mwanadamu, nyumba ya Israeli inasema, ‘Maono yale anayoyaona ni kwa ajili ya miaka mingi ijayo, naye hutabiri kuhusu siku zijazo zilizo mbali.’

28 “Kwa hiyo, waambie, ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Hakuna maneno yangu yatakayocheleweshwa tena zaidi, lo lote nisemalo litatimizwa, asemaBwanaMwenyezi.’ ”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EZK/12-66366def2f29df73fac3567ce3465a02.mp3?version_id=1627—

Ezekieli 13

Manabii Wa Uongo Walaumiwa

1 Neno laBwanalikanijia kusema:

2 “Mwanadamu, tabiri dhidi ya manabii wa Israeli wanaotabiri sasa. Waambie hao ambao hutabiri kutokana na mawazo yao wenyewe: ‘Sikia neno laBwana!

3 Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Ole wao manabii wapumbavu wafuatao roho yao wenyewe na wala hawajaona cho chote!

4 Manabii wako, Ee Israeli ni kama mbweha katikati ya magofu.

5 Hamjakwea kwenda kuziba mahali palipobomoka katika ukuta ili kuukarabati kwa ajili ya nyumba ya Israeli, ili kwamba isimame imara kwenye vita katika siku yaBwana.

6 Maono yao ni ya uongo na ubashiri wao ni wa udanganyifu. Wao husema, “Bwanaamesema,” wakatiBwanahakuwatuma, bado wakitarajia maneno yao kutimizwa.

7 Je, hamjaona maono ya uongo na kusema ubashiri wa udanganyifu hapo msemapo, “Bwanaasema,” lakini Mimi sijasema?

8 “ ‘Kwa hiyo hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Kwa sababu ya uongo wa maneno yenu na kwa madanganyo ya maono yenu, Mimi ni kinyume na ninyi, asemaBwanaMwenyezi.

9 Mkono wangu utakuwa dhidi ya manabii ambao huona maono ya uongo na kusema ubashiri wa udanganyifu. Hawatakuwa katika baraza la watu wangu au kuandikwa katika kumbukumbu ya nyumba ya Israeli wala hawataingia katika nchi ya Israeli. Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimiBwanaMwenyezi.

10 “ ‘Kwa sababu ni kweli wanapotosha watu wangu, wakisema, “Amani,” wakati ambapo hakuna amani, pia kwa sababu, wakati ukuta dhaifu unapojengwa, wanaufunika kwa kupaka chokaa,

11 kwa hiyo waambie hao wanaoupaka chokaa isiyokorogwa vyema kwamba ukuta huo utaanguka. Mvua kubwa ya mafuriko itanyesha, nami nitaleta mvua ya mawe inyeshe kwa nguvu, nao upepo wa dhoruba utavuma juu yake.

12 Wakati ukuta utakapoanguka, je, watu hawatawauliza, “Iko wapi chokaa mliyopaka ukuta?”

13 “ ‘Kwa hiyo hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Katika ghadhabu yangu nitauachia upepo wa dhoruba, pia katika hasira yangu mvua ya mawe na mvua ya mafuriko itanyesha ikiwa na ghadhabu ya kuangamiza.

14 Nitaubomoa ukuta mlioupaka chokaa na kuuangusha chini ili msingi wake uachwe wazi. Utakapoanguka, mtaangamizwa ndani yake, nanyi mtajua kuwa Mimi ndimiBwana.

15 Hivyo ndivyo nitakavyoitimiza ghadhabu yangu dhidi ya huo ukuta na dhidi yao walioupaka chokaa. Nitawaambia ninyi, “Ukuta umebomoka na vivyo hivyo wale walioupaka chokaa,

16 wale manabii wa Israeli waliotabiri juu ya Yerusalemu na kuona maono ya amani kwa ajili yake wakati kulipokuwa hakuna amani, asemaBwanaMwenyezi.” ’

17 “Sasa, mwanadamu, kaza uso wako dhidi ya binti za watu wako wanaotabiri mambo kutoka katika mawazo yao wenyewe. Tabiri dhidi yao

18 na useme, ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Ole wao wanawake washonao hirizi za uchawi juu ya viwiko vyao vyote na kutengeneza shela za urefu wa aina mbalimbali kwa ajili ya kufunika vichwa vyao kwa makusudi ya kuwanasa watu. Je, mtatega uhai wa watu wangu lakini ninyi mponye wa kwenu?

19 Ninyi mmeninajisi miongoni mwa watu wangu kwa ajili ya konzi chache za shayiri na chembe za mkate. Kwa kuwaambia uongo watu wangu, wale ambao husikiliza uongo, mmewaua wale watu ambao wasingekufa na kuwaacha hai wale ambao wasingeishi.

20 “ ‘Kwa hiyo hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Mimi niko kinyume na hizo hirizi zenu za uchawi ambazo kwa hizo mnawatega watu kama ndege, nami nitazirarua kutoka mikononi mwenu, nitawaweka huru watu wale mliowatega kama ndege.

21 Nitazirarua shela zenu na kuwaokoa watu wangu kutoka mikononi mwenu, nao hawatakuwa tena mawindo ya nguvu zenu. Ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimiBwana.

22 Kwa sababu mliwavunja moyo wenye haki kwa uongo wenu, wakati mimi sikuwaletea huzuni na kwa kuwa mliwatia moyo waovu ili wasiziache njia zao mbaya na hivyo kuokoa maisha yao,

23 kwa hiyo hamtaona tena maono ya uongo wala kufanya ubashiri. Nitawaokoa watu wangu kutoka mikononi mwenu. Nanyi ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimiBwana.’ ”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EZK/13-33d8c953fa347a115444578671fc149c.mp3?version_id=1627—

Ezekieli 14

Waabudu Sanamu Walaumiwa

1 Baadhi ya wazee wa Israeli walinijia na kuketi mbele yangu.

2 Ndipo neno laBwanalikanijia kusema:

3 “Mwanadamu, watu hawa wameweka sanamu katika mioyo yao na kuweka vitu viovu vya kukwaza mbele ya macho yao. Je, kweli niwaruhusu waniulize jambo lo lote?

4 Kwa hiyo sema nao uwaambie, ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Wakati Mwisraeli ye yote anapoweka sanamu moyoni mwake na kuweka kitu kiovu cha kukwaza mbele ya macho yake na kisha akaenda kwa nabii, MimiBwananitamjibu peke yangu sawasawa na ukubwa wa ibada yake ya sanamu.

5 Nitafanya jambo hili ili kukamata tena mioyo ya watu wa Israeli, ambao wote wameniacha kwa ajili ya sanamu zao.

6 “Kwa hiyo iambie nyumba ya Israeli, ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Tubuni! Geukeni kutoka kwenye sanamu zenu na mkatae matendo yenu yote ya machukizo!

7 “ ‘Mwisraeli ye yote au mgeni ye yote anayeishi katika Israeli anapojitenga nami na kujiwekea sanamu katika moyo wake na kwa hivyo kuweka kitu kiovu cha kukwaza mbele ya macho yake na kisha akamwendea nabii kuuliza shauri kwangu, mimiBwananitamjibu mwenyewe.

8 Nitaukaza uso wangu dhidi ya mtu huyo na kumwadibisha ili wengine waonywe na kumfanya kitu cha kudharauliwa na watu. Nitamkatilia mbali kutoka katika watu wangu. Ndipo mtakapojua Mimi ndimiBwana.

9 “ ‘Naye nabii kama atakuwa ameshawishika kutoa unabii, MimiBwananitakuwa nimemshawishi nabii huyo, nami nitaunyosha mkono wangu dhidi yake na kumwangamiza kutoka miongoni mwa watu wangu Israeli.

10 Watachukua hatia yao, nabii atakuwa na hatia sawa na yule mtu aliyekuja kuuliza neno kwake.

11 “ ‘Ndipo watu wa Israeli hawataniacha tena, wala kujitia unajisi tena kwa dhambi zao zote. Ndipo watakuwa watu wangu nami nitakuwa Mungu wao, asemaBwanaMwenyezi.’ ”

Hukumu Isiyoepukika

12 Neno laBwanalikanijia kusema,

13 “Mwanadamu, kama nchi itanitenda dhambi kwa kutokuwa waaminifu nami nikinyoosha mkono wangu dhidi yake kukatilia mbali upatikanaji wake wa chakula na kuipelekea njaa na kuua watu wake na wanyama wao,

14 hata kama watu hawa watatu: Noa, Danieli na Yobu wangekuwa ndani ya nchi hiyo, ndio hao tu wangeweza kujiokoa wenyewe kwa uadilifu wao, asemaBwanaMwenyezi.

15 “Au kama nikipeleka wanyama pori katika nchi hiyo yote na kuifanya isiwe na watoto, nayo ikawa ukiwa kwamba hakuna mtu apitaye katika nchi hiyo kwa sababu ya wanyama pori,

16 hakika kama niishivyo, asemaBwanaMwenyezi, hata kama watu hawa watatu wangekuwa humo ndani yake, wasingeweza kuokoa wana wao wala binti zao. Wao peke yao wangeokolewa, lakini nchi ingekuwa ukiwa.

17 “Au kama nikileta upanga dhidi ya nchi hiyo na kusema, ‘Upanga na upite katika nchi yote,’ nami nikiua watu wake na wanyama wao,

18 hakika kama niishivyo, asemaBwanaMwenyezi, hata kama watu hawa watatu wangekuwa humo ndani yake, wasingeweza kuokoa wana wao wala binti zao. Wao wenyewe tu wangeokolewa.

19 “Au kama nikipeleka tauni katika nchi hiyo na kumwaga ghadhabu yangu juu yake kwa njia ya kumwaga damu, kuua watu wake na wanyama wao,

20 hakika kama niishivyo, asemaBwanaMwenyezi, hata kama Noa, Danieli na Yobu wangekuwa humo ndani yake, wasingeweza kumwokoa mwana wala binti. Wao wangeweza kujiokoa wenyewe tu kwa uadilifu wao.

21 “Kwa maana hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Itakuwa vibaya kiasi gani nitakapopeleka dhidi ya Yerusalemu hukumu zangu nne za kutisha, yaani, upanga, njaa, wanyama pori na tauni, ili kuua watu wake na wanyama wao!

22 Lakini watakuwepo wenye kuokoka, wana na binti wataletwa kutoka nje ya nchi hiyo. Watawajia ninyi, nanyi mtakapoona mwenendo wao na matendo yao, mtafarijika kuhusu maafa niliyoleta juu ya Yerusalemu, kwa ajili ya yale yote niliyoleta juu yake.

23 Mtafarijika wakati mtakapoona mwenendo wao na matendo yao, kwa kuwa mtajua kwamba sikufanya lo lote ndani yake bila sababu, asemaBwanaMwenyezi.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EZK/14-2d309217ba3a2dfec287a73d3c9427ee.mp3?version_id=1627—

Ezekieli 15

Yerusalemu Mzabibu Usiofaa

1 Neno laBwanalikanijia kusema:

2 “Mwanadamu, je, ni vipi mti wa mzabibu unaweza kuwa bora zaidi kuliko tawi la mti mwingine wo wote ndani ya msitu?

3 Je, mti wake kamwe huchukuliwa na kutengeneza cho chote cha manufaa? Je, watu hutengeneza vigingi vya kuning’inizia vitu kutokana na huo mti wake?

4 Nao baada ya kutiwa motoni kama nishati na moto ukateketeza ncha zote mbili na kuunguza sehemu ya kati, je, unafaa kwa lo lote?

5 Kama haukufaa kitu cho chote ulipokuwa mzima, je, si zaidi sana sasa ambapo hauwezekani kufanyishwa cho chote cha kufaa baada ya moto kuuchoma na kuuunguza?

6 “Kwa hiyo hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Kama nilivyoutoa mti wa mzabibu miongoni mwa miti ya msituni kuwa nishati kwa ajili ya moto, hivyo ndivyo nitakavyowatendea watu waishio Yerusalemu.

7 Nitaukaza uso wangu dhidi yao. Ingawa watakuwa wameokoka kwenye moto, bado moto utawateketeza. Nami nitakapoukaza uso wangu dhidi yao, ninyi mtajua kwamba Mimi ndimiBwana.

8 Nitaifanya nchi kuwa ukiwa kwa sababu wamekuwa si waaminifu, asemaBwanaMwenyezi.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EZK/15-e257daa6618d40e316467667473c16fb.mp3?version_id=1627—

Ezekieli 16

Yerusalemu, Mwanamke Asiye Mwaminifu

1 Neno laBwanalikanijia kusema:

2 “Mwanadamu, ijulishe Yerusalemu kuhusu mwenendo wake wa machukizo

3 na useme, ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi, analomwambia Yerusalemu: Wewe asili yako na kuzaliwa kwako ni katika nchi ya Kanaani, baba yako alikuwa Mwamori, naye mama yako alikuwa Mhiti.

4 Siku uliyozaliwa kitovu chako hakikukatwa, wala hukuogeshwa kwa maji ili kukufanya safi, wala hukusuguliwa kwa chumvi wala kufunikwa kwa nguo.

5 Hakuna ye yote aliyekuonea huruma au kukusikitikia kiasi cha kukutendea mojawapo ya mambo haya. Badala yake, ulipozaliwa ulitupwa nje penye uwanja, kwa kuwa katika siku uliyozaliwa ulidharauliwa.

6 “ ‘Ndipo nilipopita karibu nawe nikakuona ukigaagaa kwenye damu yako, nawe ulipokuwa umelala hapo penye hiyo damu nikakuambia, “Ishi!”

7 Nilikufanya uote kama mmea wa shambani. Ukakua na kuongezeka sana, ukawa kito cha thamani kuliko vyote. Matiti yako yakatokeza na nywele zako zikaota, wewe uliyekuwa uchi na bila kitu cho chote.

8 “ ‘Baadaye nikapita karibu nawe, nilipokutazama na kukuona kuwa umefikia umri wa kupendwa, nililitandaza vazi langu juu yako na kuufunika uchi wako. Nikakuapia na kuingia kwenye Agano na wewe, asemaBwanaMwenyezi, nawe ukawa wangu.

9 “ ‘Nilikuogesha kwa maji, nikakuosha ile damu na kukupaka mafuta.

10 Nikakuvika vazi lililotariziwa na kukuvalisha viatu vya kamba vya ngozi. Nikakuvika nguo za kitani safi na kukufunika kwa mavazi ya thamani kubwa.

11 Nikakupamba kwa vito: nikakuvika bangili mikononi mwako na mkufu shingoni mwako,

12 nikaweka hazama puani mwako, vipuli masikioni mwako na taji nzuri sana kichwani mwako.

13 Kwa hiyo ulipambwa kwa dhahabu na fedha, nguo zako zilikuwa za kitani safi, hariri na nguo iliyokuwa imetariziwa. Chakula chako kilikuwa unga laini, asali na mafuta ya zeituni. Ukawa mzuri sana ukainuka kuwa malkia.

14 Umaarufu wako ulifahamika miongoni mwa mataifa kwa ajili ya uzuri wako, kwani ulikuwa mkamilifu kwa ajili ya utukufu wangu niliokuwa nimeuweka juu yako, asemaBwanaMwenyezi.

15 “ ‘Lakini ulitumainia uzuri wako na kutumia umaarufu wako kuwa kahaba. Ulifanya uzinzi kwa kila mtu aliyepita, uzuri wako ukawa kwa ajili yake.

16 Ulichukua baadhi ya mavazi yako ukayatumia kupamba mahali pako pa juu pa kuabudia miungu, mahali ambapo ulifanyia ukahaba wako. Mambo ya namna hiyo hayastahili kutendeka wala kamwe kutokea.

17 Pia ulichukua vito vizuri nilivyokupa, vito vilivyotengenezwa kwa dhahabu yangu na fedha yangu, ukajitengenezea navyo sanamu za kiume na ukafanya ukahaba nazo.

18 Ukayachukua mavazi yako niliyokupa yaliyotariziwa na ukazivalisha hizo sanamu, ukatoa mbele ya hizo sanamu mafuta yangu na uvumba wangu.

19 Pia chakula changu nilichokupa ili ule: unga laini, mafuta ya zeituni na asali, ulivitoa mbele yao kuwa uvumba wa harufu nzuri. Hayo ndiyo yaliyotokea, asemaBwanaMwenyezi.

20 “ ‘Nawe uliwachukua wanao na binti zako ulionizalia mimi na kuwatoa kafara kuwa chakula kwa sanamu. Je, ukahaba wako haukukutosha?

21 Uliwachinja watoto wangu na kuwatoa kafara kwa sanamu.

22 Katika matendo yako yote ya machukizo, pamoja na ukahaba wako hukukumbuka siku za ujana wako, wakati ulipokuwa uchi kabisa bila kitu cho chote, ulipokuwa ukigaagaa kwenye damu yako.

23 “ ‘Ole! Ole wako! AsemaBwanaMwenyezi. Pamoja na maovu yako yote mengine,

24 Ukajijengea jukwaa na kujifanyia mahali pa fahari pa ibada za miungu kwenye kila uwanja wa mikutano.

25 Katika kila mwanzo wa barabara ulijenga mahali pa fahari pa ibada za miungu na kuaibisha uzuri wako, ukiutoa mwili wako kwa kuzidisha uzinzi kwa kila apitaye.

26 Ulifanya ukahaba wako na Wamisri, jirani zako waliojaa tamaa, ukaichochea hasira yangu kwa kuongezeka kwa uzinzi wako.

27 Hivyo nilinyoosha mkono wangu dhidi yako na kuipunguza nchi yako, nikakutia kwenye ulafi wa adui zako, binti za Wafilisti, walioshtushwa na tabia yako ya uasherati.

28 Ulifanya ukahaba na Waashuru pia, kwa kuwa hukuridhika, hata baada ya hayo, ukawa bado hukutosheleka.

29 Ndipo ukaongeza uzinzi wako kwa Wakaldayo nchi ya wafanyabiashara, hata katika hili hukutosheka.

30 “ ‘Tazama jinsi ulivyo na dhamiri dhaifu, asemaBwanaMwenyezi, unapofanya mambo haya yote, ukifanya kama kahaba asiyekuwa na aibu!

31 Unapojenga jukwaa lako kila mwanzo wa barabara na kufanyiza mahali pa fahari pa ibada za miungu katika kila kiwanja cha wazi, lakini hukuwa kama kahaba, kwa sababu ulidharau malipo.

32 “ ‘Wewe mke mzinzi! Unapenda wageni, kuliko mume wako mwenyewe.

33 Kila kahaba hupokea malipo, lakini wewe hutoa zawadi kwa wapenzi wako wote, ukiwahonga ili waje kwako kutoka kila mahali kwa ajili ya ukahaba wako.

34 Kwa hiyo wewe ulikuwa tofauti na wanawake wengine kwenye ukahaba wako, hakuna aliyekutongoza ili kuzini naye, wewe ndiye uliyelipa wakati hakuna malipo uliyolipwa wewe. Wewe ulikuwa tofauti.

35 “ ‘Kwa hiyo, wewe kahaba, sikia neno laBwana!

36 Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Kwa kuwa umemwaga tamaa zako na kuonyesha uchi wako katika uzinzi wako kwa wapenzi wako na kwa sababu ya sanamu zako zote za machukizo na kwa sababu uliwapa damu ya watoto wako,

37 kwa hiyo nitawakusanya wapenzi wako wote, wale ambao ulijifurahisha nao, wale uliowapenda na wale uliowachukia pia. Nitawakusanya wote dhidi yako kutoka pande zote na nitakuvua nguo mbele yao, nao wataona uchi wako wote.

38 Nitakuhukumia adhabu wanayopewa wanawake wafanyao uasherati na hao wamwagao damu, nitaleta juu yenu kisasi cha damu cha ghadhabu yangu na wivu wa hasira yangu.

39 Kisha nitakutia mikononi mwa wapenzi wako, nao watabomoa majukwaa yako na kuharibu mahali pako pa fahari pa ibada ya miungu. Watakuvua nguo zako na kuchukua vito vyako vya thamani na kukuacha uchi na bila kitu.

40 Wataleta kundi la watu dhidi yako, watakaokupiga kwa mawe na kukukatakata vipande vipande kwa panga zao.

41 Watachoma nyumba zako na kutekeleza adhabu juu yako machoni pa wanawake wengi. Nitakomesha ukahaba wako, nawe hutawalipa tena wapenzi wako.

42 Ndipo ghadhabu yangu dhidi yako itakapopungua na wivu wa hasira yangu utaondoka kwako. Nitatulia wala sitakasirika tena.

43 “ ‘Kwa sababu hukuzikumbuka siku za ujana wako, lakini ulinikasirisha kwa mambo haya yote, hakika nitaleta juu ya kichwa chako yale uliyotenda, asemaBwanaMwenyezi. Je hukuongeza uasherati juu ya matendo yako yote ya kuchukiza?

44 “ ‘Kila mtu atumiaye maneno ya mithali hii, atayatumia juu yako: “Alivyo mama, ndivyo alivyo bintiye.”

45 Wewe ni binti halisi wa mama yako, ambaye alimchukia kabisa mume wake na watoto wake, tena wewe ni dada halisi wa dada zako, waliowachukia kabisa waume zao na watoto wao. Mama yako alikuwa Mhiti na baba yako alikuwa Mwamori.

46 Dada yako mkubwa alikuwa Samaria, aliyeishi upande wako wa kaskazini na binti zake, pamoja na dada yake, naye dada yako mdogo, aliyeishi kusini yako pamoja na binti zake, alikuwa Sodoma.

47 Hukuziendea njia zao tu na kuiga matendo yao ya kuchukiza, bali kwa muda mfupi katika njia zako zote uliharibika tabia zaidi kuliko wao.

48 Hakika kama niishivyo, asemaBwanaMwenyezi, dada yako Sodoma pamoja na binti zake, kamwe hawakufanya yale ambayo wewe na binti zako mmefanya.

49 “ ‘Sasa hii ilikuwa ndiyo dhambi ya dada yako Sodoma: yeye na binti zake walikuwa na majivuno, walafi na wazembe, hawakuwasaidia maskini na wahitaji.

50 Walijivuna na kufanya mambo ya machukizo sana mbele zangu. Kwa hiyo niliwakatilia mbali nami kama mlivyoona.

51 Samaria hakufanya hata nusu ya dhambi ulizofanya. Wewe umefanya mambo mengi sana ya kuchukiza kuliko wao, nawe umewafanya dada zako waonekane kama wenye haki kwa ajili ya mambo haya yote uliyofanya.

52 Chukua aibu yako, kwa kuwa umefanya uovu wa dada zako uwe si kitu, nao waonekane kama wenye haki. Kwa kuwa dhambi zako zilikuwa mbaya zaidi kuliko zao, wameonekana wenye haki zaidi kuliko wewe. Kwa hiyo basi, chukua aibu yako, kwa kuwa umewafanya dada zako waonekane wenye haki.

53 “ ‘Lakini nitarudisha baraka za Sodoma na binti zake na za Samaria na binti zake, nami nitarudisha baraka zako pamoja na zao,

54 ili upate kuchukua aibu yako na kufedheheka kwa ajili ya yote uliyotenda ambayo yamekuwa faraja kwao wakijilinganisha na wewe.

55 Nao dada zako, Sodoma na binti zake na Samaria na binti zake, watarudishwa kama vile walivyokuwa mwanzoni, nawe pamoja na binti zako mtarudishwa kama mlivyokuwa hapo awali.

56 Hukuweza hata kumtaja dada yako Sodoma kwa sababu ya dharau yako katika siku za kiburi chako,

57 kabla uovu wako haujafunuliwa. Hata hivyo, sasa unadhihakiwa na binti za Edomu na jirani zake wote na binti za Wafilisti, wale wote wanaokuzunguka wanakudharau.

58 Utachukua matokeo ya uasherati wako na matendo yako ya kuchukiza, asemaBwana.

59 “ ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Nitakushughulikia kama unavyostahili, kwa kuwa umedharau kiapo changu kwa kuvunja Agano.

60 Lakini nitakumbuka Agano nililolifanya nawe wakati wa ujana wako, nami nitaweka nawe Agano imara la milele.

61 Ndipo utakapozikumbuka njia zako na kuona aibu utakapowapokea dada zako, wale walio wakubwa wako na wadogo wako. Nitakupa hao wawe binti zako, lakini si katika msingi wa Agano langu na wewe.

62 Hivyo nitalifanya imara Agano langu na wewe, nawe utajua kuwa Mimi ndimiBwana.

63 Basi, nitakapofanya upatanisho kwa ajili yako, kwa yale yote uliyoyatenda, utakumbuka na kuaibika, nawe kamwe hutafumbua tena kinywa chako kwa sababu ya aibu yako, asemaBwanaMwenyezi.’ ”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EZK/16-ea8dbb2fdb782373f72162c85d044c9e.mp3?version_id=1627—

Ezekieli 17

Tai Wawili Na Mizabibu

1 Neno laBwanalikanijia kusema:

2 “Mwanadamu, tega kitendawili, ukawaambie nyumba ya Israeli fumbo.

3 Waambie hivi, ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Tai mkubwa mwenye mabawa yenye nguvu, yaliyojaa manyoya marefu ya rangi mbalimbali, alikuja Lebanoni. Akatua kwenye kilele cha mwerezi,

4 akakwanyua ncha yake na kuichukua mpaka nchi ya wafanyabiashara, akaipanda huko katika mji wa wachuuzi.

5 “ ‘Akachukua baadhi ya mbegu za nchi yako na kuziweka katika udongo wenye rutuba. Akazipanda kama mti umeao kando ya maji mengi,

6 nazo zikaota na kuwa mzabibu mfupi, unaoeneza matawi yake. Matawi yake yakamwelekea huyo tai, mizizi yake ikabaki chini ya huo mzabibu. Kwa hiyo ukawa mzabibu na kutoa matawi na vitawi vyenye majani mengi.

7 “ ‘Lakini kulikuwapo na tai mwingine mkubwa, mwenye mabawa yenye nguvu yaliyojaa manyoya. Tazama! Huu mzabibu ukatoa mizizi yake kumwelekea huyo tai kutoka mle kwenye shamba lile ulikopandwa na kutanda matawi yake kumwelekea kwa ajili ya kupata maji.

8 Ulikuwa umepandwa katika udongo mzuri wenye maji mengi ili uweze kutoa matawi, kuzaa matunda na uweze kuwa mzabibu mzuri sana.

9 “Waambie, ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Je, utastawi? Je, hautang’olewa na kuondolewa matunda yake, ili uweze kunyauka? Majani yake mapya yanayochipua yote yatanyauka. Hautahitaji mkono wenye nguvu au watu wengi kuung’oa na mizizi yake.

10 Hata kama utapandwa pengine, Je, utastawi? Je, hautanyauka kabisa wakati upepo wa mashariki utakapoupiga, yaani, hautanyauka kabisa katika udongo mzuri ambamo ulikuwa umestawi vizuri?’ ”

11 Ndipo neno laBwanalikanijia kusema:

12 “Waambie nyumba hii ya kuasi, ‘Je, mnajua hii ina maana gani?’ Waambie: ‘Mfalme wa Babeli alikwenda Yerusalemu na kumchukua mfalme na watu maarufu, akarudi nao na kuwaleta mpaka Babeli.

13 Ndipo akamchukua mmoja wa jamaa ya kifalme na kufanya mapatano naye, akamfanya aape. Akawachukua pia viongozi wa nchi,

14 ili kuudhoofisha ufalme huo, usiweze kuinuka tena, ila uweze kuendelea tu chini ya mapatano yake.

15 Lakini mfalme aliasi dhidi yake kwa kutuma wajumbe wake kwenda Misri ili kupatiwa farasi na jeshi kubwa. Je, atashinda? Je, atafanikiwa? Je, mtu afanyaye mambo kama hayo ataokoka? Je, atavunja mapatano na bado aokoke?

16 “ ‘Hakika kama niishivyo, asemaBwanaMwenyezi, atafia huko Babeli, katika nchi ya mfalme aliyemketisha katika kiti cha enzi, ambaye alidharau kiapo chake na kuvunja mapatano yake.

17 Farao na jeshi lake kubwa, na wingi wake wa watu hawataweza kusaidia cho chote katika vita, wakati watakapozungukwa na jeshi ili kukatilia mbali maisha ya watu wengi.

18 Alidharau kiapo kwa kuvunja Agano. Kwa sababu aliahidi kwa mkono wake mwenyewe na bado akafanya mambo haya yote, hataokoka.

19 “ ‘Kwa hiyo hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Hakika kama niishivyo, nitaleta juu ya kichwa chake kiapo changu, alichokidharau na Agano langu lile alilolivunja.

20 Nitautandaza wavu wangu kwa ajili yake, naye atanaswa katika mtego wangu. Nitamleta mpaka Babeli na kutekeleza hukumu juu yake huko kwa kuwa hakuwa mwaminifu kwangu.

21 Askari wake wote wanaotoroka wataanguka kwa upanga, nao watakaonusurika watatawanyika katika pande zote za dunia. Ndipo utakapojua kuwa MimiBwananimesema.

Hatimaye Israeli Kutukuzwa

22 “ ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Mimi mwenyewe nitachukua chipukizi kutoka kwenye kilele cha juu sana cha mwerezi na kukipanda, nitavunja kitawi kichanga kutoka matawi yake ya juu kabisa na kukipanda juu ya mlima mrefu ulioinuka sana.

23 Katika vilele vya mlima mrefu wa Israeli nitakipanda, kitatoa matawi na kuzaa matunda na kuwa mwerezi mzuri sana. Ndege wa kila aina wataweka viota vyao ndani yake, nao watapata makazi katika kivuli cha matawi yake.

24 Miti yote ya kondeni itajua kuwa MimiBwananinaishusha miti mirefu na kuikuza miti mifupi kuwa miti mirefu. Mimi naikausha miti mibichi na kuifanya miti mikavu istawi.

“ ‘MimiBwananimesema, nami nitatenda.’ ”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EZK/17-1743a85857e4b5b29a3371abf17845e5.mp3?version_id=1627—

Ezekieli 18

Roho Itendayo Dhambi Itakufa

1 Neno laBwanalikanijia kusema:

2 “Je, ninyi watu mna maana gani kutumia mithali hii inayohusu nchi ya Israeli:

“ ‘Baba wamekula zabibu zenye chachu,

nayo meno ya watoto yametiwa ganzi’?

3 “Hakika kama niishivyo, asemaBwanaMwenyezi, hamtatumia tena mithali hii katika Israeli.

4 Kwa kuwa kila roho ni mali yangu, kama vile ilivyo roho ya baba, vivyo hivyo roho ya mtoto ni mali yangu. Roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa.

5 “Mtu aweza kuwa ni mwenye haki

atendaye yaliyo haki na sawa.

6 Hakula katika mahali pa ibada za miungu

kwenye milima

wala hakuziinulia macho sanamu

za nyumba ya Israeli.

Hakumtia unajisi mke wa jirani yake,

wala hakukutana kimwili na mwanamke

wakati wa siku zake za hedhi.

7 Hamwonei mtu ye yote,

bali hurudisha kilichowekwa rehani kwake.

Hanyang’anyi, bali huwapa wenye njaa chakula chake

na huwapa nguo walio uchi.

8 Hakopeshi kwa riba

wala hajipatii faida ya ziada.

Huuzuia mkono wake usifanye mabaya,

naye huhukumu kwa haki kati ya mtu na mtu.

9 Huzifuata amri zangu

na kuzishika sheria zangu kwa uaminifu.

Huyo mtu ni mwenye haki;

hakika ataishi,

asemaBwanaMwenyezi.

10 “Aweza kuwa ana mwana jeuri, amwagaye damu au atendaye mojawapo ya mambo haya

11 (ingawa baba yake hakufanya mojawapo ya haya):

“Hula katika mahali pa ibada za miungu kwenye milima.

Humtia unajisi mke wa jirani yake.

12 Huwaonea maskini na wahitaji.

Hunyang’anyana.

Harudishi kile kilichowekwa rehani kwake.

Huziinulia sanamu macho.

Hufanya mambo ya machukizo.

13 Hukopesha kwa riba na kutafuta faida ya ziada.

Je, mtu wa namna hii ataishi? Hapana, hataishi! Kwa sababu amefanya mambo haya yote ya machukizo, hakika atauawa na damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe.

14 “Lakini yawezekana mwana huyo ana mwana aonaye dhambi hizi zote anazofanya baba yake, naye ingawa anaziona, yeye hafanyi mabaya kama haya:

15 “Hakula katika mahali pa ibada za miungu

kwenye milima,

wala hainulii macho sanamu

za nyumba ya Israeli.

Hakumtia unajisi

mke wa jirani yake.

16 Hakumwonea mtu ye yote

wala hakutaka rehani kwa ajili ya mkopo.

Hanyang’anyi,

bali huwapa wenye njaa chakula chake

na huwapa nguo walio uchi.

17 Huuzuia mkono wake usitende dhambi,

hakopeshi kwa riba

wala hajipatii faida ya ziada.

Huzishika amri zangu

na kuzifuata sheria zangu.

Hatakufa kwa ajili ya dhambi za baba yake; hakika ataishi.

18 Lakini baba yake atakufa kwa ajili ya dhambi yake mwenyewe, kwa sababu alitoza bei isiyo halali kwa nguvu, akamnyang’anya ndugu yake na kufanya yaliyo mabaya miongoni mwa watu wake.

19 “Lakini mnauliza, ‘Kwa nini mwana asiadhibiwe kwa uovu wa baba yake?’ Kwa vile mwana ametenda yaliyo haki na sawa na amekuwa mwangalifu kuzishika amri zangu zote, hakika ataishi.

20 Roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa. Mwana hataadhibiwa kwa ajili ya makosa ya baba yake, wala baba hataadhibiwa kwa ajili ya makosa ya mwanawe. Haki ya mtu mwenye haki itahesabiwa juu yake na uovu wa mtu mwovu utalipizwa juu yake.

21 “Lakini mtu mwovu akiacha dhambi zake zote alizozitenda na kushika amri zangu zote na kufanya lililo haki na sawa, hakika ataishi, hatakufa.

22 Hakuna kosa lo lote alilotenda litakalokumbukwa juu yake. Kwa ajili ya mambo ya haki aliyoyatenda, ataishi.

23 Je, mimi ninafurahia kifo cha mtu mwovu? AsemaBwanaMwenyezi. Je, si mimi ninafurahi wanapogeuka kutoka katika njia zao mbaya na kuishi?

24 “Lakini kama mtu mwenye haki akiacha haki yake na kutenda dhambi na kufanya mambo ya machukizo ambayo mtu mwovu hufanya, Je, ataishi? Hakuna hata mojawapo ya matendo ya haki aliyotenda litakalokumbukwa. Kwa sababu ya kukosa uaminifu kwake anayo hatia na kwa sababu ya dhambi alizozitenda, atakufa.

25 “Lakini mnasema, ‘Njia ya Bwana si ya haki.’ Sikia, Ee nyumba ya Israeli: Njia yangu siyo iliyo ya haki? Je, si njia zenu ndizo ambazo si za haki?

26 Kama mtu mwenye haki akiacha haki yake na kutenda dhambi, atakufa kwa ajili ya dhambi yake, kwa sababu ya dhambi alizotenda, atakufa.

27 Lakini mtu mwovu akigeuka kutoka katika maovu aliyoyatenda na kufanya yaliyo haki na sawa, ataokoa maisha yake.

28 Kwa kuwa anayafikiria na kugeuka kutoka makosa yake yote aliyoyatenda na kuyaacha, hakika ataishi, hatakufa.

29 Lakini nyumba ya Israeli inasema, ‘Njia za Bwana si haki.’ Je, njia zangu si za haki, Ee nyumba ya Israeli? Je, si njia zenu ndizo ambazo si za haki?”

30 “Kwa hiyo, Ee nyumba ya Israeli, nitawahukumu, kila mmoja sawasawa na njia zake, asemaBwanaMwenyezi. Tubuni! Geukeni kutoka katika makosa yenu yote, ndipo dhambi haitakuwa anguko lenu.

31 Tupilieni mbali makosa yenu yote mliyoyatenda, nanyi mpate moyo mpya na roho mpya. Kwa nini mfe, Ee nyumba ya Israeli?

32 Kwa maana sifurahii kifo cha mtu awaye yote afaye katika uovu, asemaBwanaMwenyezi. Tubuni basi, mkaishi!

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EZK/18-a01e3034636fd4059d631e32fae63d58.mp3?version_id=1627—

Ezekieli 19

Maombolezo Kwa Ajili Ya Wakuu Wa Israeli

1 “Wewe fanya maombolezo kuhusu wakuu wa Israeli

2 na useme:

“ ‘Tazama jinsi gani mama yako alivyokuwa simba jike

miongoni mwa simba!

Alilala katikati ya wana simba

na kulisha watoto wake.

3 Alimlea mmoja wa watoto wake,

naye akawa simba mwenye nguvu.

Akajifunza kurarua mawindo

naye akala watu.

4 Mataifa wakasikia habari zake,

naye akanaswa katika shimo lao.

Wakamwongoza kwa ndoana

mpaka nchi ya Misri.

5 “ ‘Mama yake alipongoja na kuona tumaini lake halitimiziki,

nayo matarajio yake yametoweka,

akamchukua mwanawe mwingine

na kumfanya simba mwenye nguvu.

6 Alizungukazunguka miongoni mwa simba,

kwa kuwa sasa alikuwa simba mwenye nguvu.

Akajifunza kurarua mawindo

naye akala watu.

7 Akabomoa ngome zao

na kuiharibu miji yao.

Nchi na wote waliokuwa ndani yake

wakatiwa hofu kwa kunguruma kwake.

8 Kisha mataifa wakaja dhidi yake

kutoka sehemu zilizomzunguka.

Wakatanda nyavu zao kwa ajili yake,

naye akanaswa katika shimo lao.

9 Kwa kutumia ndoana wakamvutia kwenye tundu

na kumleta mpaka kwa mfalme wa Babeli.

Wakamtia gerezani, hivyo kunguruma kwake

hakukusikika tena

katika milima ya Israeli.

10 “ ‘Mama yako alikuwa kama mzabibu

katika shamba lako la mizabibu

uliopandwa kando ya maji,

ukiwa unazaa sana na wenye matawi mengi

kwa sababu ya wingi wa maji.

11 Matawi yake yalikuwa na nguvu,

yaliyofaa kuwa fimbo ya enzi ya mtawala.

Ulikuwa mrefu kupita miti mingine

katikati ya matawi manene;

ulionekana kwa urahisi

kwa ajili ya urefu wake

na wingi wa matawi yake.

12 Lakini uling’olewa kwa hasira kali

na kutupwa chini.

Upepo wa mashariki uliufanya usinyae,

matunda yake yakapukutika,

matawi yake yenye nguvu yakanyauka

na moto ukayateketeza.

13 Sasa umepandwa jangwani

katika nchi kame na ya kiu.

14 Moto ulienea kuanzia katika mmojawapo ya matawi yake makubwa

na kuteketeza matunda yake.

Hakuna tawi lenye nguvu lililobaki juu yake

lifaalo kuwa fimbo ya enzi ya mtawala.’

Hili ndilo ombolezo, na litumike kama ombolezo.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EZK/19-89ac9b9aa938911dd35fc7da69f4da6e.mp3?version_id=1627—

Ezekieli 20

Israeli Waasi

1 Katika mwaka wa saba, mwezi wa tano siku ya kumi, baadhi ya wazee wa Israeli wakaja ili kutaka ushauri kwaBwana, wakaketi mbele yangu.

2 Ndipo neno laBwanalikanijia kusema:

3 “Mwanadamu, sema na wazee wa Israeli uwaambie, ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Kwa nini mmekuja? Je, ni kutaka ushauri kwangu? Hakika kama niishivyo, sitawaruhusu mtake ushauri toka kwangu, asemaBwanaMwenyezi.’

4 “Je, utawahukumu? Je, mwanadamu, utawahukumu? Basi uwakabili kwa ajili ya machukizo ya baba zao

5 na uwaambie: ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Siku ile nilipochagua Israeli, niliwaapia wazao wa nyumba ya Yakobo kwa mkono ulioinuliwa nami nikajidhihirisha kwao huko Misri. Kwa mkono ulioinuliwa niliwaambia, “Mimi ndimiBwana, Mungu wenu.”

6 Siku ile niliwaapia wao kwamba nitawatoa katika nchi ya Misri na kuwaleta katika nchi niliyowachagulia, nchi itiririkayo maziwa na asali, nchi nzuri kupita zote.

7 Nami nikawaambia, “Kila mmoja wenu aondolee mbali sanamu za chukizo ambazo mmekazia macho, nanyi msijitie unajisi kwa sanamu za Misri. Mimi ndimiBwana, Mungu wenu.”

8 “ ‘Lakini waliniasi na hawakunisikiliza, hawakuondolea mbali sanamu za machukizo ambazo walikuwa wamezikazia macho, wala kuondolea mbali sanamu za Misri. Ndipo nikasema, nitawamwagia ghadhabu yangu na kutimiza hasira yangu dhidi yao huko Misri.

9 Lakini kwa ajili ya Jina langu nilifanya kile ambacho kingelifanya lisitiwe unajisi machoni mwa mataifa waliyoishi miongoni mwao na ambao machoni pao nilikuwa nimejifunua kwa Waisraeli kwa kuwatoa katika nchi ya Misri.

10 Kwa hiyo nikawaongoza watoke Misri na kuwaleta jangwani.

11 Nikawapa amri zangu na kuwajulisha sheria zangu, kwa kuwa mtu anayezitii ataishi kwa hizo.

12 Pia niliwapa Sabato zangu kama ishara kati yangu nao, ili wapate kujua kuwa MimiBwananiliwafanya kuwa watakatifu.

13 “ ‘Lakini watu wa Israeli waliniasi Mimi jangwani. Hawakufuata amri zangu, bali walikataa sheria zangu, ingawa mtu yule anayezitii ataishi kwa hizo, nao walizinajisi Sabato zangu kabisa. Hivyo nilisema ningemwaga ghadhabu yangu juu yao na kuwaangamiza huko jangwani.

14 Lakini kwa ajili ya Jina langu nikafanya kile ambacho kitalifanya Jina langu lisitiwe unajisi machoni mwa mataifa ambao mbele yao nilikuwa nimewatoa Waisraeli.

15 Tena kwa mkono ulioinuliwa nikawaapia huko jangwani kwamba nisingewaingiza katika nchi niliyokuwa nimewapa, yaani, nchi itiririkayo maziwa na asali, nchi nzuri kuliko zote,

16 kwa sababu walikataa sheria zangu na hawakufuata amri zangu na wakazinajisi Sabato zangu. Kwa kuwa mioyo yao iliandama sanamu zao.

17 Lakini niliwahurumia wala sikuwaangamiza wala hakuwafuta kabisa jangwani.

18 Niliwaambia watoto wao kule jangwani, “Msifuate amri za baba zenu wala kushika sheria zao au kujinajisi kwa sanamu zao.

19 Mimi ndimiBwana, Mungu wenu, fuateni amri zangu tena iweni waangalifu kushika sheria zangu.

20 Zitakaseni Sabato zangu ili ziwe ishara kati yangu nanyi. Ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimiBwana, Mungu wenu.”

21 “ ‘Lakini watoto hao wakaniasi: Hawakufuata amri zangu, wala hawakuwa waangalifu kushika sheria zangu, ingawa mtu anayezitii anaishi kwa hizo, nao wakazinajisi Sabato zangu. Hivyo nikasema ningemwaga ghadhabu yangu juu yao na kutimiza hasira yangu dhidi yao huko jangwani.

22 Lakini nikauzuia mkono wangu na kwa ajili ya Jina langu nikafanya kile ambacho kingelifanya Jina langu lisitiwe unajisi machoni mwa mataifa ambao mbele yao nilikuwa nimewatoa Waisraeli.

23 Tena kwa mkono ulioinuliwa nikawaapia huko jangwani kwamba ningewatawanya miongoni mwa mataifa na kuwatawanya katika nchi mbalimbali,

24 kwa sababu hawakutii sheria zangu lakini walikuwa wamekataa amri zangu na kuzinajisi Sabato zangu, nayo macho yao yakatamani sanamu za baba zao.

25 Pia niliwaacha wafuate amri ambazo hazikuwa nzuri na sheria ambazo mtu hawezi kuishi kwa hizo.

26 Nikawaacha wanajisiwe kwa matoleo yao, kuwatoa wazaliwa wao wa kwanza kafara kwa sanamu, yaani, kule kuwapitisha wazaliwa wao wa kwanza kwenye moto, nipate kuwajaza na hofu ili wajue kwamba Mimi ndimiBwana.’

27 “Kwa hiyo, mwanadamu, sema na watu wa Israeli na uwaambie, ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Katika hili pia, baba zenu walinikufuru kwa kuniacha mimi:

28 Nilipowaleta katika nchi ile ambayo nilikuwa nimeapa kuwapa na kuona kilima cho chote kirefu au mti wo wote wenye majani mengi, huko walitoa dhabihu zao, wakatoa sadaka ambazo zilichochea hasira yangu, wakafukiza uvumba wenye harufu nzuri na kumimina sadaka zao za kinywaji.

29 Ndipo nikawaambia: Ni nini maana yake hapa mahali pa juu pa kuabudia miungu mnapopaendea?’ ” (Basi jina la mahali pale panaitwa Bamahata hivi leo.)

Hukumu Na Kurudishwa

30 “Kwa hiyo iambie nyumba ya Israeli: ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Je, mtajinajisi kama vile baba zenu walivyofanya na kutamani vinyago vyao vya machukizo?

31 Mnapotoa matoleo yenu, yaani, wana wenu kafara katika moto, mnaendelea kujinajisi na sanamu zenu zote hadi siku hii ya leo. Je, niulizwe neno na ninyi, Ee nyumba ya Israeli? Hakika kama niishivyo, asemaBwanaMwenyezi, mimi sitaulizwa neno na ninyi.

32 “ ‘Lile lililoko mioyoni mwenu kamwe halitatokea, mnaposema, “Tunataka tuwe kama mataifa mengine, kama watu wengine wa dunia, wanaotumikia miti na mawe.”

33 Hakika kama niishivyo asemaBwanaMwenyezi, nitatawala juu yenu kwa mkono wa nguvu na kwa mkono ulionyooshwa na kwa ghadhabu iliyomwagwa.

34 Nitawatoa toka katika mataifa na kuwakusanya kutoka katika nchi mlikotawanywa, kwa mkono wa nguvu na kwa mkono ulionyooshwa na kwa ghadhabu iliyomwagwa.

35 Nitawaleta katika jangwa la mataifa na huko nitatekeleza hukumu juu yenu uso kwa uso.

36 Kama nilivyowahukumu baba zenu katika jangwa la nchi ya Misri, ndivyo nitakavyowahukumu ninyi, asemaBwanaMwenyezi.

37 Nitawafanya mpite chini ya fimbo yangu, nami nitawaleta katika mkataba wa Agano.

38 Nitawaondoa miongoni mwenu wale wanaohalifu na wale wanaoasi dhidi yangu. Ingawa nitawatoa katika nchi wanazoishi, hawataingia katika nchi ya Israeli. Ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimiBwana.

39 “ ‘Kwa habari zenu ninyi, Ee nyumba ya Israeli, hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Nendeni mkatumikie sanamu zenu, kila mmoja wenu! Lakini baadaye hakika mtanisikiliza mimi nanyi hamtalinajisi tena Jina langu takatifu, kwa matoleo yenu na sanamu zenu.

40 Kwa kuwa katika mlima wangu mtakatifu, mlima mrefu wa Israeli, asemaBwanaMwenyezi, hapo katika nchi nyumba yote ya Israeli itanitumikia mimi, nami huko nitawakubali. Huko nitataka sadaka zenu na matoleo ya malimbuko yenu, pamoja na dhabihu zenu takatifu zote.

41 Nitawakubali ninyi kama uvumba wenye harufu nzuri wakati nitakapowatoa katika mataifa na kuwakusanya kutoka katika nchi mlipokuwa mmetawanyika, nami nitajionyesha kuwa mtakatifu miongoni mwenu na machoni mwa mataifa.

42 Ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimiBwana, nitakapowaleta katika nchi ya Israeli, nchi niliyokuwa nimeapa kwa mkono ulioinuliwa kuwapa baba zenu.

43 Hapo ndipo nitakapokumbuka mwenendo wenu na matendo yenu yote ambayo kwayo mlijitia unajisi, nanyi mtajichukia wenyewe kwa ajili ya maovu yote mliyokuwa mmetenda.

44 Nanyi mtajua kuwa mimi ndimiBwana, nitakaposhughulika nanyi kwa ajili ya Jina langu na wala si sawasawa na njia zenu mbaya na matendo yenu maovu, Ee nyumba ya Israeli, asemaBwanaMwenyezi.’ ”

Unabii Dhidi Ya Kusini

45 Neno laBwanalikanijia kusema:

46 “Mwanadamu, uelekeze uso wako upande wa kusini, hubiri juu ya upande wa kusini na utoe unabii juu ya msitu wa Negebu.

47 Waambie watu wa Negebu: ‘Sikieni neno laBwana. Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Ninakaribia kukutia moto, nao utateketeza miti yako yote, mibichi na iliyokauka. Miali ya moto haitaweza kuzimwa na kila uso kutoka kusini mpaka kaskazini utakaushwa kwa moto huo.

48 Kila mmoja ataona kuwa mimiBwanandiye niliyeuwasha huo moto, nao hautazimwa.’ ”

49 Ndipo niliposema, “Aa,BwanaMwenyezi! Wao hunisema, ‘Huyu si huzungumza mafumbo tu?’ ”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EZK/20-3a1401bbe967adbbfce971d7593ecd82.mp3?version_id=1627—

Ezekieli 21

Babeli, Upanga Wa Mungu Wa Hukumu

1 Neno laBwanalikanijia kusema:

2 “Mwanadamu, uelekeze uso wako juu ya Yerusalemu na uhubiri dhidi ya mahali patakatifu. Tabiri dhidi ya nchi ya Israeli

3 uiambie: ‘Hili ndiloBwanaasemalo: Mimi niko kinyume nawe. Nitautoa upanga wangu kwenye ala yake na kumkatilia mbali mwenye haki na mwovu.

4 Kwa sababu nitamkatilia mbali mwenye haki na mwovu, upanga wangu utakuwa wazi dhidi ya kila mmoja kuanzia kusini mpaka kaskazini.

5 Ndipo watu wote watajua ya kuwa MimiBwananimeutoa upanga wangu kwenye ala yake, nao hautarudi humo tena.’

6 “Kwa hiyo lia kwa uchungu, mwanadamu! Lia kwa uchungu mbele yao kwa moyo uliopondeka na kwa huzuni nyingi.

7 Nao watakapokuuliza, ‘Kwa nini unalia kwa uchungu?’ Utasema hivi, ‘Kwa sababu ya habari zinazokuja. Kila moyo utayeyuka na kila mkono utalegea, kila roho itazimia na kila goti litalegea kama maji.’ Habari hizo zinakuja! Hakika zitatokea, asemaBwanaMwenyezi.”

8 Neno laBwanalikanijia, kusema:

9 “Mwanadamu, tabiri na useme, ‘Hili ndilo Bwana asemalo:

“ ‘Upanga, upanga,

ulionolewa na kusuguliwa:

10 umenolewa kwa ajili ya mauaji,

umesuguliwa ili ung’ae

kama umeme wa radi!

“ ‘Je, tuifurahie fimbo ya utawala ya mwanangu Yuda? Upanga unaidharau kila fimbo ya namna hiyo.

11 “ ‘Upanga umewekwa tayari ili kusuguliwa,

ili upate kushikwa mkononi,

umenolewa na kusuguliwa,

umewekwa tayari kwa mkono wa mwuaji.

12 Piga kelele na uomboleze, Ee mwanadamu,

kwa kuwa upanga u dhidi ya watu wangu;

u dhidi ya wakuu wote wa Israeli.

Wametolewa wauawe kwa upanga

pamoja na watu wangu.

Kwa hiyo pigapiga kifua chako.

13 “ ‘Kwa maana upanga huu umejaribiwa na kuhakikishwa, itakuwaje basi fimbo ya ufalme ya Yuda inayoudharau kama haitakuwapo tena, bali itakuwa imeondolewa kabisa? asemaBwanaMwenyezi.’

14 “Hivyo basi, mwanadamu, tabiri

na ukapige makofi.

Upanga wako na upige mara mbili,

naam, hata mara tatu.

Ni upanga wa kuchinja,

upanga wa mauaji makuu,

ukiwashambulia kutoka kila upande.

15 Ili mioyo ipate kuyeyuka

na wanaouawa wawe wengi,

nimeweka upanga wa kuchinja

kwenye malango yao yote.

Lo! Umetengenezwa

umetemete kama umeme wa radi,

umeshikwa kwa ajili ya kuua.

16 Ee upanga, kata upande wa kuume,

kisha upande wa kushoto,

mahali po pote makali yako

yatakapoelekezwa.

17 Mimi nami nitapiga makofi,

nayo ghadhabu yangu itapungua.

MimiBwananimesema.”

18 Neno laBwanalikanijia kusema:

19 “Mwanadamu, weka alama njia mbili ambazo upanga wa mfalme wa Babeli utapitia, njia hizo zikianzia katika nchi hiyo hiyo. Weka kibao pale ambapo njia zinagawanyika kuelekea mjini.

20 Weka alama njia moja kwa ajili ya upanga upate kuja dhidi ya Raba ya Waamori na nyingine upate kuja dhidi ya Yuda na Yerusalemu iliyozungushiwa ngome.

21 Kwa kuwa mfalme wa Babeli sasa amesimama katika njia panda, katika makutano ya njia mbili, akipiga ramli: anapiga kura kwa kutumia mishale, anataka shauri kwa sanamu zake, anachunguza maini ya wanyama.

22 Upande wake wa kuume inakuja kura ya Yerusalemu, ambapo ataweka vyombo vya kuvunjia boma, ili kuamrisha mauaji, kupiga ukelele wa vita, kuweka vyombo vya kuvunjia boma kwenye malango, kuweka jeshi kuzunguka na kufanya uzingiraji.

23 Itakuwa kama kupiga ramli kwa uongo kwa wale watu ambao wameapa kumtii yeye. Lakini mfalme wa Babeli atawakumbusha juu ya uovu wao na kuwachukua mateka.

24 “Kwa hiyo hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: ‘Kwa sababu enyi watu mmekumbusha uovu wenu kwa kuasi waziwazi, mkidhihirisha dhambi zenu katika yale yote mfanyayo, kwa kuwa mmefanya jambo hili, mtachukuliwa mateka.

25 “ ‘Ee mtawala kafiri na mwovu wa Israeli, ambaye siku yako imewadia, ambaye wakati wako wa adhabu umefikia kilele chake,

26 hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Vua kilemba, ondoa taji. Kwa kuwa mambo hayatakuwa kama yalivyokuwa. Aliye mnyonge atakwezwa na aliyekwezwa atashushwa.

27 Mahame! Mahame! Nitaufanya mji kuwa mahame! Hautajengwa upya mpaka aje yule ambaye ndiye mwenye haki nao; yeye ndiye nitakayempa.’

28 “Nawe, mwanadamu, tabiri na useme, ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo kuhusu Waamoni na matukano yao.

“ ‘Upanga, upanga,

umefutwa kwa ajili ya kuua,

umesuguliwa ili kuangamiza

na unametameta kama umeme wa radi!

29 Wakati wakitoa maono ya uongo kwa ajili yako,

wanapobashiri uongo kwa ajili yako,

wanakuweka wewe kwenye shingo za watu wapotovu,

wale walio waovu,

wale ambao siku yao imewadia,

wakati wa adhabu yao ya mwisho.

30 Urudishe upanga kwenye ala yake!

Katika mahali ulipoumbiwa,

katika nchi ya baba zako,

huko nitakuhukumu.

31 Nitamwaga ghadhabu yangu juu yako

na kupuliza moto wa hasira yangu dhidi yako;

nitakutia mikononi mwa watu wakatili,

watu stadi katika kuangamiza.

32 Mtakuwa kuni za kuwashia moto,

damu yenu itamwagwa katika nchi yenu,

wala hamtakumbukwa tena;

kwa maana MimiBwananimesema.’ ”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EZK/21-d97fe0927b9befe7076fc228bcfe3ea8.mp3?version_id=1627—