Ezekieli 32

Maombolezo Kwa Ajili Ya Farao

1 Katika mwaka wa kumi na mbili, mwezi wa kumi na mbili, siku ya kwanza ya mwezi, neno la Mungu likanijia kusema:

2 “Mwanadamu, fanya maombolezo kwa ajili ya Farao mfalme wa Misri na umwambie:

“ ‘Wewe ni kama simba miongoni mwa mataifa,

wewe ni kama joka kubwa baharini,

unayevuruga maji kwa miguu yako

na kuchafua vijito.

3 “ ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo:

“ ‘Nikiwa pamoja na wingi mkubwa wa watu

nitautupa wavu wangu juu yako,

nao watakukokota katika wavu wangu.

4 Nitakutupa nchi kavu

na kukuvurumisha uwanjani.

Nitawafanya ndege wote wa angani watue juu yako

na wanyama wote wa nchi

watajishibisha nyama yako.

5 Nitatapanya nyama yako juu ya milima

na kujaza mabonde kwa mabaki yako.

6 Nitailowanisha nchi kwa damu yako inayotiririka

njia yote hadi milimani,

nayo mabonde yatajazwa na nyama yako.

7 Nitakapokuzimisha, nitafunika mbingu

na kuzitia nyota zake giza;

nitalifunika jua kwa wingu,

nao mwezi hautatoa nuru yake.

8 Mianga yote itoayo nuru angani

nitaitia giza juu yako;

nitaleta giza juu ya nchi yako,

asemaBwanaMwenyezi.

9 Nitaifadhaisha mioyo ya mataifa mengi

nitakapokuangamiza miongoni mwa mataifa,

nikikuleta uhamishoni miongoni mwa nchi

ambazo haujapata kuzijua.

10 Nitayafanya mataifa mengi wakustaajabie,

wafalme wao watatetemeka

kwa hofu kwa ajili yako

nitakapotikisa upanga wangu mbele yao.

Siku ya anguko lako

kila mmoja wao atatetemeka

kila dakika kwa ajili ya maisha yake.

11 “ ‘Kwa kuwa hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo:

“ ‘Upanga wa mfalme wa Babeli

utakuja dhidi yako.

12 Nitafanya makundi yako ya wajeuri kuanguka

kwa panga za watu mashujaa,

taifa katili kuliko mataifa yote.

Watakivunjavunja kiburi cha Misri,

nayo makundi yake yote

ya wajeuri yatashindwa.

13 Nitaangamiza mifugo yake yote

wanaojilisha kando ya maji mengi,

hayatavurugwa tena kwa mguu wa mwanadamu

wala kwato za mnyama

hazitayachafua tena.

14 Kisha nitafanya maji yake yatulie

na kufanya vijito vyake

vitiririke kama mafuta,

asemaBwanaMwenyezi.

15 Nitakapoifanya Misri kuwa ukiwa

na kuiondolea nchi kila kitu

kilichomo ndani yake,

nitakapowapiga wote waishio humo,

ndipo watakapojua kuwa

Mimi ndimiBwana.’

16 “Hili ndilo ombolezo watakalomwimbia. Binti za mataifa wataliimba, kwa kuwa Misri na makundi yake yote ya wajeuri wataliimba, asemaBwanaMwenyezi.”

17 Katika mwaka wa kumi na mbili, mwezi wa kwanza, siku ya kumi na tano ya mwezi, neno laBwanalikanijia kusema:

18 “Mwanadamu, omboleza kwa ajili ya makundi ya wajeuri wa Misri na uwatupe kuzimu yeye na binti za mataifa yenye nguvu, waende huko pamoja nao washukao shimoni.

19 Je, ninyi mnamzidi nani kwa uzuri? Shukeni chini! Nanyi mkalazwe pamoja na hao wasio tahiriwa!

20 Wataanguka miongoni mwa wale waliouawa kwa upanga. Upanga umefutwa, mwache aburutwe mbali pamoja na hao wajeuri wake wote.

21 Kutoka Kuzimu viongozi hodari watanena kuhusu Misri pamoja na wale walioungana nao, ‘Wameshuka chini nao wamelala kimya pamoja na hao wasiotahiriwa, pamoja na wale waliouawa kwa upanga.’

22 “Ashuru yuko huko pamoja na jeshi lake lote, amezungukwa na makaburi ya watu wake wote waliouawa, wale wote walioanguka kwa upanga.

23 Makaburi yao yako kwenye kina cha chini cha shimo na jeshi lake limelala kulizunguka kaburi lake. Wote waliokuwa wameeneza hofu kuu katika nchi ya walio hai wameuawa, wameanguka kwa upanga.

24 “Elamu yuko huko, pamoja na makundi yake yote ya wajeuri wakiwa wamelizunguka kaburi lake. Wote wameuawa, wameanguka kwa upanga. Wote waliokuwa wameeneza hofu katika nchi ya walio hai walishuka kuzimu bila kutahiriwa. Wanaichukua aibu yao pamoja na wale washukao shimoni.

25 Kitanda kimetandikwa kwa ajili yake miongoni mwa waliouawa, pamoja na makundi yake yote ya wajeuri wakiwa wamelizunguka kaburi lake. Wote ni watu wasiotahiriwa, wameuawa kwa upanga. Kwa sababu vitisho vyao vilienea katika nchi ya walio hai, wameichukua aibu yao pamoja na wale washukao shimoni, nao wamewekwa miongoni mwa waliouawa.

26 “Mesheki na Tubali wako humo, pamoja na makundi yao ya wajeuri wakiwa wameyazunguka makaburi yao. Wote hawakutahiriwa, wameuawa kwa upanga kwa sababu walieneza vitisho vyao katika nchi ya walio hai.

27 Je, hawakulala na mashujaa wengine wasiotahiriwa waliouawa, ambao wameshuka kaburini wakiwa na silaha zao za vita, ambao panga zao ziliwekwa chini ya vichwa vyao na uovu wao juu ya mifupa yao? Adhabu kwa ajili ya dhambi zao ilikuwa juu ya mifupa yao, ingawa vitisho vya mashujaa hawa vilikuwa vimeenea hadi kwenye nchi ya walio hai.

28 “Wewe pia, Ee Farao, utavunjwa nawe utalala miongoni mwa wasiotahiriwa, pamoja na wale waliouawa kwa upanga.

29 “Edomu yuko humo, wafalme wake wote na wakuu wake wote, ambao ijapokuwa wana nguvu, wamelazwa pamoja na wale waliouawa kwa upanga. Wamelala pamoja na wasiotahiriwa, pamoja na wale washukao shimoni.

30 “Wakuu wote wa kaskazini na Wasidoni wote wako huko, wameshuka chini pamoja na waliouawa kwa aibu ijapokuwa kuna vitisho vilivyosababishwa na nguvu zao. Wamelala bila kutahiriwa pamoja na wale waliouawa kwa upanga na kuchukua aibu yao pamoja na wale washukao chini shimoni.

31 “Farao, yeye pamoja na jeshi lake lote, atakapowaona atafarijiwa kwa ajili ya makundi yake yote ya wajeuri, wale waliouawa kwa upanga, asemaBwanaMwenyezi.

32 Ingawa nilimfanya Farao aeneze vitisho vyake katika nchi ya walio hai, Farao pamoja na makundi yake yote ya wajeuri watalazwa miongoni mwa wasiotahiriwa, pamoja na wale waliouawa kwa upanga, asemaBwanaMwenyezi.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EZK/32-f004430cd7113fc65cb6929eca50cbac.mp3?version_id=1627—

Ezekieli 33

Wajibu Wa Ezekieli Kuwa Mlinzi Kwa Watu Wake

1 Neno laBwanalikanijia kusema:

2 “Mwanadamu, sema na watu wako uwaambie, ‘Nitakapoleta upanga dhidi ya nchi, nao watu wa nchi wakamchagua mmoja wa watu wao na kumfanya awe mlinzi wao,

3 naye auonapo upanga unakuja dhidi ya nchi na kupiga tarumbeta kuonya watu,

4 kama mtu ye yote asikiapo sauti ya tarumbeta hakukubali kuonywa, basi upanga ujapo na kuutoa uhai wake, damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe.

5 Kwa kuwa alisikia sauti ya tarumbeta lakini hakukubali maonyo, damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe. Kama angekubali maonyo, angelijiokoa mwenyewe.

6 Lakini kama mlinzi akiona upanga unakuja na asipige tarumbeta kuonya watu na upanga ukija na kutoa uhai wa mmoja wao, yule mtu ataondolewa kwa sababu ya dhambi yake, lakini damu yake nitaitaka mkononi mwa mlinzi huyo.’

7 “Mwanadamu, nimekufanya wewe kuwa mlinzi kwa ajili ya nyumba ya Israeli, kwa hiyo sikia neno nisemalo na uwape maonyo kutoka kwangu.

8 Nimwambiapo mtu mwovu, ‘Ewe mtu mwovu, hakika utakufa,’ nawe hukusema neno la kumwonya ili atoke katika njia zake, yule mtu mwovu atakufa kwa ajili ya dhambi yake, mimi nitaitaka damu yake mkononi mwako.

9 Lakini kama utamwonya huyo mtu mwovu aache njia zake mbaya naye hafanyi hivyo, atakufa kwa ajili ya dhambi yake, lakini utakuwa umejiokoa mwenyewe.

10 “Mwanadamu, sema na nyumba ya Israeli uwaambie, ‘Hili ndilo mnalosema: “Makosa yetu na dhambi zetu zimetulemea, nasi tunadhoofika kwa sababu ya hayo. Tutawezaje basi kuishi?” ’

11 Waambie, ‘Hakika kama mimi niishivyo, asemaBwanaMwenyezi, sifurahii kifo cha watu waovu, bali kwamba wageuke kutoka katika njia zao mbaya wapate kuishi. Geukeni! Geukeni kutoka katika njia zenu mbaya! Kwa nini mkafe Ee nyumba ya Israeli?’

12 “Kwa hiyo, mwanadamu, waambie watu wako, ‘Haki ya mtu mwenye haki haitamwokoa wakati anapoacha kutii, wala uovu wa mtu mwovu hautamsababisha yeye kuanguka anapotubu na kuacha uovu. Mtu mwenye haki, kama akitenda dhambi, hataishi kwa sababu ya uadilifu wake wa awali.’

13 Kama nikimwambia mtu mwenye haki kwamba hakika utaishi, lakini akategemea hiyo haki yake na kutenda uovu, hakuna tendo lo lote la haki alilotenda litakalokumbukwa, atakufa kwa ajili ya uovu alioutenda.

14 Nami kama nikimwambia mtu mwovu, ‘Hakika utakufa,’ kisha akageuka kutoka katika dhambi yake na kufanya lile lililo haki na sawa,

15 kama akirudisha kile alichochukuwa rehani kwa ajili ya deni, akarudisha alichoiba na kufuata amri zile ziletazo uzima, wala hafanyi uovu, hakika ataishi, hatakufa.

16 Hakuna dhambi yo yote aliyoitenda itakayokumbukwa juu yake. Ametenda lile lililo haki na sawa, hakika ataishi.

17 “Lakini watu wako wanasema, ‘Njia ya Bwana si sawa.’ Lakini ni njia zao ambazo si sawa.

18 Kama mtu mwenye haki akigeuka kutoka katika uadilifu wake na kufanya uovu, atakufa kwa ajili ya huo uovu.

19 Naye mtu mwovu kama akigeuka kutoka katika uovu wake na kufanya lile lililo haki na sawa, kwa kufanya hivyo ataishi.

20 Lakini, Ee nyumba ya Israeli, unasema, ‘Njia ya Bwana si sawa.’ Lakini nitamhukumu kila mmoja wenu sawasawa na njia zake mwenyewe.”

Anguko La Yerusalemu Laelezewa

21 Mwaka wa kumi na mbili wa uhamisho wetu, mwezi wa kumi, siku ya tano, mtu aliyekuwa ametoroka kutoka Yerusalemu akanijia na kusema, “Mji wa Yerusalemu umeanguka!”

22 Basi jioni kabla mtu huyo hajaja, mkono waBwana, ulikuwa juu yangu, naye alifungua kinywa changu kabla ya mtu yule aliyenijia asubuhi hajafika. Basi kinywa changu kilifunguliwa na sikuweza tena kunyamaza.

23 Ndipo neno laBwanalikanijia kusema:

24 “Mwanadamu, watu wanaoishi katika magofu hayo katika nchi ya Israeli wanasema hivi, ‘Abrahamu alikuwa mtu mmoja tu, hata hivyo akaimiliki nchi. Lakini sisi ni wengi, hakika tumepewa nchi kuwa milki yetu.’

25 Kwa hiyo waambie, ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Kwa kuwa mnakula nyama pamoja na damu na kuinulia sanamu zenu macho na kumwaga damu, je, mtaimiliki nchi?

26 Mnategemea panga zenu, mnafanya mambo ya machukizo na kila mmoja wenu humtia unajisi mke wa jirani yake. Je, mtaimiliki nchi?’

27 “Waambie hivi: ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Hakika kama niishivyo, wale waliobaki katika magofu wataanguka kwa upanga, wale walio nje mashambani nitawatoa wararuliwe na wanyama pori, nao wale walio katika ngome na kwenye mapango watakufa kwa tauni.

28 Nitaifanya nchi kuwa ukiwa na utupu na kiburi cha nguvu zake zitafikia mwisho, nayo milima ya Israeli itakuwa ukiwa ili mtu ye yote asipite huko.

29 Kisha watajua kuwa Mimi ndimiBwana, nitakapokuwa nimeifanya nchi kuwa ukiwa na utupu kwa sababu ya mambo yote ya machukizo waliyotenda.’

30 “Kwa habari yako wewe, mwanadamu, watu wako wanaongea habari zako wakiwa karibu na kuta na kwenye milango ya nyumba, wakiambiana kila mmoja na mwenzake, ‘Njoni msikie ujumbe ule utokao kwaBwana.’

31 Watu wangu wanakujia, kama wafanyavyo, nao wanaketi mbele yako kama watu wangu na kusikiliza maneno yako, lakini hawayatendi. Kwa maana udanganyifu u katika midomo yao, lakini mioyo yao ina tamaa ya faida isiyo halali.

32 Naam, mbele yao umekuwa tu kama yeye aimbaye nyimbo za mapenzi kwa sauti nzuri za kuvutia na kupiga vyombo kwa ustadi, kwa kuwa wanasikia maneno yako lakini hawayatendi.

33 “Wakati mambo haya yote yatakapotimia, kwa kuwa hakika yatatokea, ndipo watakapojua kwamba nabii amekuwapo miongoni mwao.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EZK/33-27a165227a9aa7e31b9ae8a128143a53.mp3?version_id=1627—

Ezekieli 34

Wachungaji Na Kondoo

1 Neno laBwanalikanijia kusema:

2 “Mwanadamu, tabiri juu ya wachungaji wa Israeli, tabiri na uwaambie: ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Ole wa wachungaji wa Israeli ambao hujitunza wenyewe tu! Je, haiwapasi wachungaji kutunza kundi la kondoo?

3 Mnakula mafuta ya wanyama, mnavaa mavazi ya sufu na kuchinja kondoo walionona, lakini hamlitunzi kundi.

4 Hamkuwatia nguvu walio dhaifu wala hamkuwaganga wenye maradhi wala kuwafunga waliojeruhiwa. Hamkuwarudisha waliotangatanga wala kuwatafuta wale waliopotea. Badala yake mmewatawala kwa ukali na kwa ukatili.

5 Hivyo walitawanyika kwa sababu hapakuwepo mchungaji, nao walipotawanyika, wakawa chakula cha wanyama wa mwitu wote.

6 Kondoo wangu walitawanyika, wakatangatanga kwenye milima yote na kwenye kila kilima kirefu. Kondoo wangu walitawanyika juu ya uso wa dunia yote bila kuwa na ye yote wa kuwaulizia wala wa kuwatafuta.

7 “ ‘Kwa hiyo, ninyi wachungaji, lisikieni neno laBwana:

8 Kwa hakika kama niishivyo, asemaBwanaMwenyezi, kwa sababu kondoo zangu wamekosa mchungaji na hivyo wametekwa nyara na kuwa chakula cha wanyama wote wa mwituni na kwa sababu wachungaji wangu, hawakuwatafuta kondoo zangu, bali wachungaji wamejitunza wenyewe, nao hawakuwalisha kondoo zangu,

9 kwa hiyo enyi wachungaji, sikieni neno laBwana:

10 Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Mimi ni kinyume na wachungaji nami nitawadai kondoo zangu mikononi mwao. Nitawafukuza kutoka kwenye kuchunga kundi langu, ili wachungaji wasiendelee kujitunza wenyewe. Nitaokoa kondoo zangu kutoka kwenye vinywa vyao, nao kondoo hawatakuwa tena chakula chao.

11 “ ‘Kwa kuwa hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Mimi mwenyewe nitawaulizia kondoo zangu na kuwatafuta.

12 Kama vile mchungaji atafutavyo kundi lake lililotawanyika wakati akiwa pamoja nalo, hivyo ndivyo nitakavyowatafuta kondoo wangu. Nitawaokoa kutoka mahali pote walipokuwa wametawanyikia katika siku ya mawingu na giza nene.

13 Nitawatoa katika mataifa na kuwakusanya kutoka nchi mbalimbali, nami nitawaleta katika nchi yao wenyewe. Nitawalisha kwenye milima ya Israeli, katika mabonde na mahali pote panapokalika katika nchi.

14 Nitawachunga kwenye malisho mazuri na miinuko ya mlima wa Israeli patakuwa mahali pao pa malisho. Huko watajipumzisha kwa amani katika nchi ya malisho mazuri, nao watajilisha huko katika malisho tele katika milima ya Israeli.

15 Mimi mwenyewe nitawachunga kondoo zangu na kuwafanya wapumzike, asemaBwanaMwenyezi.

16 Nitawaulizia kondoo waliopotea na kuwaleta walio tangatanga. Nitawafunga waliojeruhiwa na kuwatia nguvu waliodhaifu lakini wale waliojikinai na wenye nguvu nitawaangamiza. Nitalichunga kundi kwa haki.

17 “ ‘Kwa habari yenu, enyi kundi langu, hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Nitahukumu kati ya kondoo na kondoo, kati ya kondoo waume na mbuzi.

18 Je, haiwatoshi ninyi kujilisha kwenye malisho mazuri? Je, ni lazima ninyi kuyakanyaga pia malisho yenu yaliyobaki kwa miguu yenu? Je, haiwatoshi ninyi kunywa maji safi? Je, ni lazima kuyachafua maji mengine kwa miguu yenu?

19 Je, ni lazima kundi langu wajilishe kwa yale mliyoyakanyaga na kunywa maji mliyoyachafua kwa miguu yenu?

20 “ ‘Kwa hiyo, hili ndiloBwanaMwenyezi awaambialo: Tazama, mimi mwenyewe nitahukumu kati ya kondoo wanono na waliokonda.

21 Kwa sababu mmewapiga kikumbo na kuwapiga kwa pembe zenu kondoo wote walio dhaifu mpaka wakawafukuza,

22 nitaliokoa kundi langu na hawatatekwa nyara tena. Nitahukumu kati ya kondoo na kondoo.

23 Nitaweka juu yao mchungaji mmoja, mtumishi wangu Daudi, naye atawachunga, atawachunga na kuwa mchungaji wao.

24 MimiBwananitakuwa Mungu wao, naye mtumishi wangu Daudi atakuwa mkuu miongoni mwao. MimiBwananimenena.

25 “ ‘Nitafanya nao Agano la amani na kuwaondoa wanyama wa mwitu kutoka katika nchi yao ili kondoo wangu waweze kupumzika nyikani na msituni kwa salama.

26 Nitawabariki wao pamoja na maeneo yanayozunguka kilima changu. Nitawanyeshea mvua kwa majira yake, kutakuwepo mvua za baraka.

27 Miti ya shambani itatoa matunda yake na ardhi itatoa mazao yake, watu watakaa salama katika nchi yao. Watajua kuwa Mimi ndimiBwana, nitakapovunja vifungo vya nira zao na kuwaokoa kutoka katika mikono ya wale waliowafanya watumwa.

28 Hawatatekwa tena nyara na mataifa, wala wanyama pori hawatawala tena. Wataishi kwa salama, wala hakuna ye yote atakayewatia hofu.

29 Nitawapa nchi yenye sifa kutokana na mazao yake, hawatapatwa na njaa katika nchi tena wala hawatadharauliwa na mataifa.

30 Ndipo watakapojua kuwa Mimi,Bwana, Mungu wao, niko pamoja nao na ya kuwa wao, nyumba ya Israeli, ni watu wangu, asemaBwanaMwenyezi.

31 Ninyi ni kondoo wangu, kondoo wa malisho yangu, ninyi ni watu wangu, nami ni Mungu wenu, asemaBwanaMwenyezi.’ ”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EZK/34-a98c9cb75bb1932db4fb679e55fc9d16.mp3?version_id=1627—

Ezekieli 35

Unabii Dhidi Ya Edomu

1 Neno laBwanalikanijia kusema:

2 “Mwanadamu, elekeza uso wako juu ya mlima Seiri, utabiri dhidi yake

3 na useme: ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Mimi ni kinyume nawe, Ee mlima Seiri, nami nitanyosha mkono wangu dhidi yako na kukufanya ukiwa na usiyekaliwa na watu wala kulimika.

4 Nitaifanya miji yako kuwa magofu nawe utakuwa ukiwa. Ndipo utakapojua kuwa Mimi ndimiBwana.

5 “ ‘Kwa sababu ulificha moyoni uadui wa siku nyingi nawe ukawatoa Waisraeli wauawe kwa upanga wakati wa maafa yao, wakati adhabu yake ilipofikia kilele chake,

6 kwa hiyo hakika kama niishivyo, asemaBwanaMwenyezi, nitakutia katika umwagaji damu nao utakufuatia. Kwa kuwa hakuchukia kumwaga damu, kumwaga damu kutakufuatia.

7 Nitaufanya Mlima Seiri ukiwa na usiokaliwa na watu wala kulimika na kuukatilia mbali na wote wanaokuja na wanaokwenda.

8 Nitaijaza milima yenu kwa watu wake waliouawa, wale waliouawa kwa upanga wataanguka juu ya vilima vyako na katika mabonde yako na katika makorongo yako yote.

9 Nitakufanya ukiwa milele, watu hawataishi katika miji yako. Ndipo utakapojua kuwa Mimi ndimiBwana.

10 “ ‘Kwa sababu umesema, “Mataifa haya mawili na nchi hizi zitakuwa zetu nasi tutazimiliki,” ingawa hata mimiBwananilikuwa huko,

11 kwa hiyo hakika kama niishivyo, asemaBwanaMwenyezi, nitakutenda kwa kadiri ya hasira na wivu uliouonyesha katika chuki yako juu yao nami nitafanya nijulikane miongoni mwao wakati nitakapokuhukumu.

12 Ndipo utakapojua kuwa MimiBwananimesikia mambo yote ya dharau uliyosema dhidi ya milima ya Israeli. Ulisema, “Wamefanyika ukiwa na kutiwa mikononi mwetu tuwararue.”

13 Ulijigamba dhidi yangu na kusema maneno dhidi yangu bila kujizuia, nami nikayasikia.

14 Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Wakati dunia yote inashangilia nitakufanya ukiwa.

15 Kwa sababu ulishangilia wakati urithi wa nyumba ya Israeli ulipofanyika ukiwa, hivyo ndivyo nitakavyokutendea. Utakuwa ukiwa, Ee mlima Seiri, wewe na Edomu yote. Kisha ndipo watajua kuwa Mimi ndimiBwana.’ ”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EZK/35-2c943a2013a3831088f73f89b74d7af3.mp3?version_id=1627—

Ezekieli 36

Unabii Kwa Milima Ya Israeli

1 “Mwanadamu, itabirie milima ya Israeli na useme, ‘Ee milima ya Israeli, sikieni neno laBwana.

2 Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Kwa sababu adui wanasema juu yako, “Aha! Mahali palipoinuka pa zamani pamekuwa milki yetu.” ’

3 Kwa hiyo tabiri na useme, ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Kwa sababu wamewafanya ukiwa na kuwagandamiza kila upande ili mpate kuwa milki ya mataifa mengine na kuwa kitu cha kusimangwa na kudhihakiwa miongoni mwa watu,

4 kwa hiyo, Ee milima ya Israeli, sikieni neno laBwanaMwenyezi: Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo kwa milima na vilima, kwa makorongo na mabonde, kwa mahame yaliyo ukiwa, miji iliyoachwa ambayo imetekwa nyara na kudharauliwa na mataifa mengine yanayowazunguka,

5 hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Katika wivu wangu uwakao nimenena dhidi ya mataifa mengine na dhidi ya Edomu yote, kwa maana kwa furaha na hila katika mioyo yao waliifanya nchi yangu kuwa milki yao ili wapate kuteka nyara sehemu yake ya malisho.’

6 Kwa hiyo tabiri kuhusu nchi ya Israeli na uiambie milima na vilima, makorongo na vijito na mabonde: ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Ninanena katika wivu wa ghadhabu yangu kwa sababu mmedharauliwa na mataifa.

7 Kwa hiyo hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Ninaapa kwa mkono wangu ulioinuliwa kwamba mataifa wanaowazunguka nao pia watadharauliwa.

8 “ ‘Lakini ninyi, Ee milima ya Israeli, mtatoa matawi na matunda kwa ajili ya watu wangu Israeli, kwa sababu hivi karibuni watakuja nyumbani.

9 Mimi ninawajibika nanyi na nitawaangalia kwa upendeleo, mtalimwa na kupandwa mbegu,

10 nami nitaizidisha idadi ya watu kwenu, naam, nyumba yote ya Israeli. Miji itakaliwa na watu na magofu yatajengwa upya.

11 Nitaongeza idadi ya watu na wanyama juu yenu, nao watazaana sana na kuwa wengi mno. Nitawakalisha watu ndani yenu kama ilivyokuwa wakati uliopita, nami nitawafanya mfanikiwe kuliko hapo kwanza. Ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimiBwana.

12 Nitawafanya watu, watu wangu Israeli, kutembea juu yenu. Watawamiliki ninyi, nanyi mtakuwa urithi wao, kamwe hamtawaondolea tena watoto wao.

13 “ ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Kwa sababu watu wanakuambia, “Unawala watu na kuliondolea taifa lako watoto wake,”

14 kwa hiyo hutakula tena watu wala kulifanya tena taifa lako lisiwe na watoto, asemaBwanaMwenyezi.

15 Sitakufanya tena usikie dhihaka za mataifa, wala kudharauliwa na kabila za watu, wala kulifanya taifa lako lianguke, asemaBwanaMwenyezi.’ ”

16 Neno la Mungu likanijia tena, kusema:

17 “Mwanadamu, nyumba ya Israeli walipokuwa wakiishi katika nchi yao wenyewe, waliinajisi kwa mwenendo wao na matendo yao. Mwenendo wao mbele zangu ulikuwa kama mwanamke aliye katika hedhi.

18 Hivyo nilimwaga ghadhabu yangu juu yao kwa sababu walikuwa wamemwaga damu katika nchi na kwa sababu walikuwa wameitia nchi unajisi kwa sanamu zao.

19 Nikawatawanya miongoni mwa mataifa, nao wakaenda huko na huko katika nchi mbalimbali, nikawahukumu sawasawa na mwenendo wao na matendo yao.

20 Tena po pote walipokwenda miongoni mwa mataifa walilitia unajisi Jina langu takatifu, kwa kuwa watu walisema kuhusu wao, ‘Hawa ndio watu waBwana, lakini imewapasa kuondoka katika nchi yake.’

21 Lakini niliwahurumia kwa ajili ya Jina langu takatifu, ambalo nyumba ya Israeli imelitia unajisi miongoni mwa mataifa huko walikokwenda.

22 “Kwa hiyo iambie nyumba ya Israeli, ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Si kwa ajili yako, Ee nyumba ya Israeli, kwamba ninafanya mambo haya, bali ni kwa ajili ya Jina langu takatifu, ambalo mmelitia unajisi miongoni mwa mataifa mliyoyaendea.

23 Nitauonyesha utakatifu wa Jina langu kuu, ambalo limetiwa unajisi miongoni mwa mataifa, jina ambalo limetiwa unajisi miongoni mwao. Ndipo mataifa watakapojua kuwa Mimi ndimiBwana, asemaBwanaMwenyezi, nitakapojionyesha mwenyewe kuwa mtakatifu kwa kuwapitia ninyi mbele ya macho yao.

24 “ ‘Kwa kuwa nitawaondoa ninyi toka katika mataifa, nitawakusanya kutoka katika nchi zote na kuwarudisha kwenye nchi yenu wenyewe.

25 Nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi, nitawatakasa kutoka katika uchafu wenu wote na kutoka katika sanamu zenu zote.

26 Nitawapa moyo mpya na kuweka roho mpya ndani yenu, nitaondoa ndani yenu moyo wenu wa jiwe na kuwapa moyo wa nyama.

27 Nami nitaweka Roho yangu ndani yenu na kuwafanya ninyi mfuate amri zangu na kuwafanya kuwa waangalifu kuzishika sheria zangu.

28 Mtaishi katika nchi niliyowapa baba zenu, ninyi mtakuwa watu wangu nami nitakuwa Mungu wenu.

29 Nitawaokoa ninyi kutoka katika unajisi wenu wote. Nitaiita nafaka na kuiongeza iwe nyingi sana nami sitaleta njaa juu yenu.

30 Nitaongeza matunda ya miti na mazao ya mashamba, ili kwamba msipate tena aibu miongoni mwa mataifa kwa ajili ya njaa.

31 Ndipo mtakapozikumbuka njia zenu za uovu na matendo yenu maovu, nanyi mtajichukia wenyewe kwa ajili ya dhambi zote na matendo yenu ya kuchukiza.

32 Ninataka ninyi mjue kwamba sifanyi hili kwa ajili yenu, asemaBwanaMwenyezi. Oneni aibu na mkatahayari kwa ajili ya mwenendo wenu, Ee nyumba ya Israeli!

33 “ ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Siku ile nitakapowasafisha kutoka katika dhambi zenu zote, nitarudisha watu waishi katika miji yenu na magofu yatajengwa upya.

34 Nchi iliyokuwa ukiwa italimwa badala ya kukaa ukiwa machoni mwa wale wote wanaopita ndani yake.

35 Watasema, “Hii nchi iliyokuwa imeachwa ukiwa sasa imekuwa kama bustani ya Edeni, miji ile iliyokuwa magofu, ukiwa na kuangamizwa, sasa imejengewa ngome na kukaliwa na watu.”

36 Ndipo mataifa yanayowazunguka yaliyobakia watakapojua kuwa MimiBwananimejenga tena kile kilichoharibiwa na nimepanda tena kile kilichokuwa ukiwa. MimiBwananimenena, nami nitalifanya.’

37 “Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Mara nyingine tena nitasikia maombi ya nyumba ya Israeli na kuwatendea jambo hili: Nitawafanya watu wake kuwa wengi kama kondoo,

38 kuwa wengi kama kundi la kondoo kwa ajili ya dhabihu huko Yerusalemu wakati wa sikukuu zao za wakati ulioamriwa. Hivyo ndivyo miji iliyokuwa magofu itajazwa na makundi ya watu. Ndipo watakapojua kuwa Mimi ndimiBwana.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EZK/36-f2bbfde741697b3c05db37b4b8908a58.mp3?version_id=1627—

Ezekieli 37

Bonde La Mifupa Mikavu

1 Mkono waBwanaulikuwa juu yangu, naye akanitoa nje kwa Roho waBwanana kuniweka katikati ya bonde lililokuwa limejaa mifupa tele.

2 Akanipitisha pande zote kwenye hiyo mifupa, nami nikaona mifupa mingi sana ndani ya lile bonde, mifupa iliyokuwa imekauka sana.

3 Akaniuliza, “Mwanadamu, mifupa hii yaweza kuishi?”

Nikajibu, “EeBwanaMwenyezi, wewe peke yako wajua.”

4 Ndipo akaniambia, “Itabirie mifupa hii na uiambie, ‘Enyi mifupa mikavu, sikieni neno laBwana!

5 Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo kwa hii mifupa: Nitatia pumzindani yenu, nanyi mtaishi.

6 Nitawawekea mishipa, nami nitaifanya nyama ije juu yenu na kuwafunika kwa ngozi. Nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtakuwa hai. Ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimiBwana.’ ”

7 Basi nikatabiri kama nilivyoamriwa. Wakati nilipokuwa ninatabiri, kukawa na sauti, sauti ya kugongana, nayo mifupa ikasogeleana, mfupa kwa mfupa mwenziwe.

8 Nikatazama, mishipa na nyama vikatokea juu ya mifupa na ngozi ikaifunika, lakini hapakuwepo pumzi ndani yake.

9 Ndipo aliponiambia, “Utabirie upepo, tabiri, mwanadamu na uuambie, ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Njoo kutoka pande nne, Ee pumzi, nawe upulizie pumzi ndani ya hawa waliouawa, ili wapate kuishi.’ ”

10 Hivyo nikatabiri kama alivyoniamuru, nayo pumzi ikawaingia, wakawa hai na wakasimama kwa miguu yao, jeshi kubwa mno.

11 Ndipo akaniambia: “Mwanadamu, mifupa hii ni nyumba yote ya Israeli. Nao wanasema, ‘Mifupa yetu imekauka na tumaini letu limetoweka, tumekatiliwa mbali.’

12 Hivyo watabirie na uwaambie: ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Enyi watu wangu, nitayafunua makaburi yenu na kuwatoa ndani yake, nami nitawarudisha tena katika nchi ya Israeli.

13 Ndipo ninyi watu wangu, mtakapojua kuwa Mimi ndimiBwana, nitakapoyafunua makaburi yenu na kuwatoa humo.

14 Nitatia Roho yangu ndani yenu nanyi mtaishi, nami nitawakalisha katika nchi yenu wenyewe. Ndipo mtakapojua kwamba MimiBwananimenena, nami nitalitenda, asemaBwana!’ ”

Taifa Moja Chini Ya Mfalme Mmoja

15 Neno laBwanalikanijia kusema:

16 “Mwanadamu, chukua fimbo na uandike juu yake, ‘Hii ni kwa ajili ya Yuda na Waisraeli waliofungamana naye.’ Kisha chukua fimbo nyingine, uandike juu yake, ‘Fimbo ya Efraimu, ni kwa ajili ya Yosefu na nyumba yote ya Israeli wanaofungamana naye.’

17 Ziunganishe pamoja kuwa fimbo moja ili kwamba ziwe fimbo moja katika mkono wako.

18 “Watu wako watakapokuuliza, ‘Je, hutatuambia ni nini maana ya jambo hili?’

19 Waambie, ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Nitaichukua fimbo ya Yosefu, iliyoko mikononi mwa Efraimu na ya makabila ya Israeli yanayofungamana naye na kuiunganisha na fimbo ya Yuda, nikizifanya kuwa fimbo moja, nao watakuwa wamoja katika mkono wangu.’

20 Inua mbele ya macho yao zile fimbo ulizoziandika

21 kisha waambie, ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Nitawatoa Waisraeli katika mataifa walikokuwa wamekwenda. Nitawakusanya po pote walipo na kuwarudisha katika nchi yao wenyewe.

22 Nitawafanya kuwa taifa moja katika nchi, katika milima ya Israeli. Patakuwa na mfalme mmoja juu yao wote na kamwe hawatagawanyika tena kuwa mataifa mawili au kugawanyika katika falme mbili.

23 Hawatajitia tena unajisi kwa sanamu zao na vinyago vyao visivyo na maana wala kwa makosa yao yo yote, kwa maana nitawaokoa kutoka katika dhambi zao zote zilizowarudisha nyuma, nami nitawatakasa. Wao watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao.

24 “ ‘Mtumishi wangu Daudi atakuwa mfalme juu yao, nao wote watakuwa na mchungaji mmoja. Watafuata sheria zangu na kuzishika amri zangu kwa uangalifu.

25 Wataishi katika nchi niliyompa mtumishi wangu Yakobo, nchi ambamo baba zenu waliishi. Wao na watoto wao na watoto wa watoto wao wataishi humo milele, naye Daudi mtumishi wangu atakuwa mkuu wao milele.

26 Nitafanya nao Agano la amani, litakuwa Agano la milele. Nitawafanya imara na kuongeza idadi yao, nami nitaweka mahali patakatifu pangu miongoni mwao milele.

27 Maskani yangu yatakuwa pamoja nao, nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.

28 Ndipo mataifa watakapojua kwamba MimiBwanandiye ninayeifanya Israeli kuwa takatifu, wakati mahali patakatifu pangu patakapokuwa miongoni mwao milele.’ ”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EZK/37-777a713afed8989a30f0fb84e36039ab.mp3?version_id=1627—

Ezekieli 38

Unabii Dhidi Ya Gogu

1 Neno laBwanalikanijia kusema:

2 “Mwanadamu, kaza uso wako dhidi ya Gogu, katika nchi ya Magogu, mkuu wa Roshi, Mesheki na Tubali, tabiri dhidi yake

3 na useme: ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Ee Gogu, mimi ni kinyume nawe, mtawala mkuu wa Roshi, Mesheki na Tubali.

4 Nitakugeuza kuelekea ulikotoka na kukutia ndoana kwenye mataya yako na kukutoa nje wewe pamoja na jeshi lako lote, yaani, farasi wako, wapanda farasi wako waliojiandaa tayari kwa vita, pamoja na kundi kubwa la wajeuri wakiwa na ngao na vigao, wote wakipunga panga zao.

5 Uajemi, Kushina Putu watakuwa pamoja nao, wote wakiwa na ngao na kofia za chuma,

6 pia Gomeri pamoja na vikosi vyake vyote na nyumba ya Beth-Togarma kutoka kaskazini ya mbali pamoja na vikosi vyake vyote, mataifa mengi wakiwa pamoja nawe.

7 “ ‘Jiandae, uwe tayari, wewe na makundi yako yote ya wajeuri yaliyokusanyika pamoja nawe, nawe waamrishe.

8 Baada ya siku nyingi utaitwa vitani. Katika miaka ijayo utaivamia nchi ile ambayo imepona kutoka katika vita, ambayo watu wake walikusanywa kutoka katika mataifa mengi ili kuja katika milima ya Israeli, ambayo kwa muda mrefu ilikuwa imeachwa ukiwa. Wameletwa kutoka katika mataifa na sasa wote wanaishi katika hali ya salama.

9 Wewe na vikosi vyako vyote na mataifa mengi yaliyo pamoja nawe mtapanda juu, mtawazoa kama tufani na kuifunika nchi kama wingu.

10 “ ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Katika siku ile mawazo yataingia moyoni mwako nawe utapanga mipango mibaya.

11 Utasema, “Nitapigana vita na nchi ambayo vijiji vyake havina maboma, nitawashambulia watu wanaoishi kwa amani na wasiotarajia vita, wote wanaishi bila maboma na bila malango na makomeo.

12 Nitateka mateka na kuchukua nyara mali za wale waliorudi kuishi katika mahame na wale watu waliokusanywa kutoka kwa mataifa, ambao sasa wana mifugo na mali nyingi, wanaoishi katikati ya nchi.”

13 Sheba na Dedani pamoja na wafanyabiashara wa Tarshishi na vijiji vyake vyote watakuambia, “Je, umekuja kuteka mateka? Je, umekusanya makundi yako ya wajeuri ili kuchukua nyara mali, kutwaa fedha na dhahabu, kutunyang’anya mifugo na mali na kuteka nyara nyingi zaidi?” ’

14 “Kwa hiyo, mwanadamu, tabiri na umwambie Gogu: ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Katika siku ile, watu wangu Israeli watakapokuwa wanaishi salama, Je, wewe mwenyewe hutalijua hilo?

15 Utakuja kutoka kwako huko kaskazini ya mbali, ukiwa pamoja na mataifa mengi, wote wakiwa wamepanda farasi, kundi kubwa, jeshi kuu.

16 Utakuja dhidi ya watu wangu Israeli kama wingu lifunikavyo nchi. Siku zijazo, Ee Gogu, nitakuleta wewe dhidi ya nchi yangu, ili kwamba mataifa wapate kunijua Mimi nitakapojionyesha mtakatifu kwa kukupitia wewe mbele ya macho yao.

17 “ ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Je, wewe si yule niliyenena juu yako katika siku za zamani kwa kupitia kwa watumishi wangu manabii wa Israeli? Wakati ule walitabiri kwa miaka mingi kwamba ningekuleta upigane nao.

18 Hili ndilo litakalotokea katika siku ile: Gogu atakaposhambulia nchi ya Israeli, hasira yangu kali itaamka, asemaBwanaMwenyezi.

19 Katika wivu wangu na ghadhabu yangu kali ninasema kuwa wakati ule patakuwepo tetemeko kuu katika nchi ya Israeli.

20 Samaki wa baharini, ndege wa angani, wanyama wa kondeni, kila kiumbe kitambaacho ardhini, na watu wote walio juu ya uso wa nchi watatetemeka mbele zangu. Milima itapinduka, majabali yatapasuka na kila ukuta utaanguka chini.

21 Nitaita upanga vita dhidi ya Gogu juu ya milima yangu yote, asemaBwanaMwenyezi. Upanga wa kila mtu utakuwa dhidi ya ndugu yake.

22 Nitatekeleza hukumu juu yake kwa tauni na kwa umwagaji wa damu. Nitanyesha mvua ya mafuriko, mvua ya mawe na moto wa kiberiti juu yake na juu ya vikosi vyake na juu ya mataifa mengi walio pamoja naye.

23 Nami hivyo ndivyo nitakavyoonyesha ukuu wangu na utakatifu wangu, nami nitajijulisha mbele ya macho ya mataifa mengi. Ndipo watakapojua kuwa Mimi ndimiBwana.’

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EZK/38-fc3385726f85b950cab532550c9ec505.mp3?version_id=1627—

Ezekieli 39

Majeshi Ya Gogu Yataangamizwa

1 “Mwanadamu, tabiri dhidi ya Gogu useme: ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Ee Gogu mimi ni kinyume nawe, mtawala mkuu wa Roshi, Mesheki na Tubali.

2 Nitakugeuza kuelekea ulikotoka na kukuburuta. Nitakuleta kutoka kaskazini ya mbali na kukupeleka wewe dhidi ya milima ya Israeli.

3 Kisha nitaupiga upindi wako kutoka mkono wako wa kushoto na kuifanya mishale ianguke kutoka mkono wako wa kuume.

4 Utaanguka kwenye milima ya Israeli, wewe pamoja na vikosi vyako vyote na yale mataifa yaliyo pamoja nawe. Nitakutoa uwe chakula cha ndege wa aina zote walao nyama na cha wanyama wa mwituni.

5 Utaanguka katika uwanja, kwa kuwa nimenena, asemaBwanaMwenyezi.

6 Nitatuma moto juu ya Magogu na kwa wale wanaoishi kwa salama huko pwani, nao watajua kwamba Mimi ndimiBwana.

7 “ ‘Nitalifanya Jina langu takatifu lijulikane miongoni mwa watu wangu Israeli. Sitaliacha tena Jina langu takatifu litiwe unajisi, nayo mataifa watajua kuwa MimiBwanandimi niliye Mtakatifu wa Israeli.

8 Hili jambo linakuja! Hakika litatokea, asemaBwanaMwenyezi. Hii ndiyo siku ile niliyosema habari zake.

9 “ ‘Ndipo wale wanaoishi katika miji ya Israeli watakapotoka na kutumia hizo silaha kuwashia moto na kuziteketeza, yaani, kigao na ngao, pinde na mishale, rungu za vita na mikuki. Kwa miaka saba watavitumia kama kuni.

10 Hawatahitaji kukusanya kuni kutoka mashambani wala kukata kuni kutoka kwenye misitu, kwa sababu watatumia silaha kuwa kuni. Nao watawateka mateka wale waliowateka na kuchukua nyara mali za wale waliochukua mali zao nyara, asemaBwanaMwenyezi.

11 “ ‘Siku ile nitampa Gogu mahali pa kuzikia katika Israeli, katika bonde la wale wasafirio upande wa mashariki kuelekea baharini. Jambo hili litazuia njia ya wasafiri kwa sababu Gogu na makundi yake yote ya wajeuri watazikwa huko. Kwa hiyo litaitwa Bonde la Hamon-Gogu.

12 “ ‘Kwa miezi saba nyumba ya Israeli itakuwa ikiwazika ili kuisafisha nchi.

13 Watu wote wa nchi watawazika, nayo siku nitakayotukuzwa itakuwa siku ya kumbukumbu kwa ajili yao, asemaBwanaMwenyezi.

14 “ ‘Watu wataajiriwa mara kwa mara kuisafisha nchi. Baadhi yao watapita nchini kote na zaidi yao hao wengine, watawazika wale waliosalia juu ya uso wa nchi. Mwisho wa hiyo miezi saba wataanza upekuzi wao.

15 Wakati wanapopita nchini kote na mmoja wao akaona mfupa wa mwanadamu, ataweka alama kando yake mpaka wachimba kaburi wawe wameuzika katika Bonde la Hamon-Gogu.

16 (Pia mji uitwao Hamonautakuwa humo.) Hivyo ndivyo watakavyoisafisha nchi.’

17 “Mwanadamu, hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Ita kila aina ya ndege na wanyama wote wa mwituni, waambie: ‘Kusanyikeni mje pamoja kutoka pande zote kwa ajili ya dhabihu ninayowaandalia, dhabihu kuu katika milima ya Israeli. Huko mtakula nyama na kunywa damu.

18 Mtakula nyama za watu mashujaa na kunywa damu za wakuu wa dunia kana kwamba ni za kondoo waume na kondoo wake, mbuzi na mafahali, wote walionona kutoka Bashani.

19 Katika dhabihu ninayoandaa kwa ajili yenu, mtakula mafuta mpaka mkinai na kunywa damu mpaka mlewe.

20 Kwenye meza yangu watajishibisha kwa farasi na wapanda farasi, watu mashujaa na maaskari wa kila aina,’ asemaBwanaMwenyezi.

21 “Nitauonyesha utukufu wangu miongoni mwa mataifa, nayo mataifa yote wataiona adhabu nitakayotoa na mkono wangu nitakaouweka juu yao.

22 Kuanzia siku ile na kuendelea nyumba ya Israeli itajua kuwa Mimi ndimiBwana, Mungu wao.

23 Na mataifa watajua kuwa nyumba ya Israeli walikwenda utumwani kwa ajili ya dhambi yao, kwa sababu hawakuwa waaminifu kwangu. Hivyo niliwaficha uso wangu na kuwatia mikononi mwa adui zao, nao wote wakaanguka kwa upanga.

24 Niliwatendea sawasawa na uchafu wao na makosa yao, nami nikawaficha uso wangu.

25 “Kwa hiyo hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Sasa nitamrudisha Yakobo kutoka utumwani, nami nitawahurumia watu wote wa Israeli, nami nitakuwa na wivu kwa ajili ya Jina langu takatifu.

26 Wataisahau aibu yao na jinsi walivyoonyesha kutokuwa waaminifu kwangu wakati walipoishi kwa salama katika nchi yao, bila kuwa na mtu ye yote wa kuwatia hofu.

27 Nitakapokuwa nimewarudisha kutoka katika mataifa na kuwakusanya kutoka katika nchi za adui zao, mimi nitajionyesha kuwa mtakatifu kwa kupitia kwao machoni mwa mataifa mengi.

28 Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimiBwana, Mungu wao, ingawa niliwapeleka uhamishoni miongoni mwa mataifa, nitawakusanya tena katika nchi yao wenyewe, bila kumwacha ye yote nyuma.

29 Sitawaficha tena uso wangu, kwa maana nitamimina Roho wangu juu ya nyumba ya Israeli, asemaBwanaMwenyezi.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EZK/39-3cfd7071071499b75c0e88a3f4b42451.mp3?version_id=1627—

Ezekieli 40

Eneo La Hekalu Jipya

1 Katika mwaka wa ishirini na tano wa uhamisho wetu, mwanzoni mwa huo mwaka, siku ya kumi ya mwezi, katika mwaka wa kumi na nne baada ya kuanguka kwa mji, siku hiyo hiyo mkono waBwanaulikuwa juu yangu, naye akanipeleka huko.

2 Nikiwa katika maono ya Mungu alinichukua mpaka nchi ya Israeli, naye akaniweka kwenye mlima mrefu sana, ambako upande wa kusini kulikuwepo baadhi ya majengo ambayo yalionekana kama mji.

3 Akanipeleka huko, nami nikamwona mtu ambaye kuonekana kwake kulikuwa kama kuonekana kwa shaba. Alikuwa amesimama kwenye lango akiwa na kamba ya kitani na ufito wa kupimia mkononi mwake.

4 Mtu huyo akaniambia, “Mwanadamu, angalia kwa macho yako na usikie kwa masikio yako nawe uzingatie kitu nitakachokuonyesha, kwa kuwa ndiyo sababu umeletwa hapa. Iambie nyumba ya Israeli kila kitu utakachoona.”

Lango La Mashariki Kuelekea Ukumbi Wa Nje

5 Nikaona ukuta uliozunguka eneo lote la Hekalu. Ule ufito wa kupimia uliokuwa mkononi mwa yule mtu ulikuwa na urefu wa dhiraa ndefu sita, yaani, dhiraa ndefu ni sawa na dhiraa na nyanda nne, akapima ule ukuta. Ukuta huo ulikuwa na unene wa dhiraa ndefu sita na kimo cha dhiraa ndefu sita.

6 Kisha akaenda kwenye lango linaloelekea mashariki. Akapanda ngazi zake akapima kizingiti cha lango, nacho kilikuwa na kina cha huo ufito.

7 Vyumba vya kupumzikia vya walinzi vilikuwa na urefu wa huo ufito mmoja na upana wa huo ufito, kuta zilizogawa vyumba hivyo vya mapumziko zilikuwa na unene wa dhiraa tano. Nacho kizingiti cha lango lililokuwa karibu na ukumbi unaoelekea hekaluni ulikuwa na kina cha huo ufito.

8 Kisha akapima baraza ya njia ya lango,

9 ambayo ilikuwa na kina cha dhiraa nanena miimo yake ilikuwa na unene wa dhiraa mbili. Baraza ya lango ilielekea Hekalu.

10 Ndani ya lango la mashariki kulikuwepo vyumba vitatu vya kupumzikia kila upande, vyote vitatu vilikuwa na vipimo vilivyo sawa, nazo nyuso za kuta zilizotenganisha kila upande zilikuwa na vipimo vilivyo sawa.

11 Kisha akapima upana wa ingilio la lango, ilikuwa dhiraa kumi na urefu wake ulikuwa dhiraa kumi na tatu.

12 Mbele ya kila chumba cha kupumzikia kulikuwepo ukuta uliokuwa na kimo cha dhiraa mojakwenda juu, navyo hivyo vyumba vilikuwa dhiraa sita mraba.

13 Kisha akapima njia ya lango kuanzia juu ya ukuta wa nyuma wa chumba kimoja cha kupumzikia hadi juu ya ukuta wa nyuma wa chumba upande wa pili kukawa na nafasi ya dhiraa ishirini na tano, kuanzia ukuta mmoja hadi mwingine.

14 Akapima pia ukumbi, urefu wa dhiraa ishirinina lango linalofuatia hiyo nguzo kila upande wa huo ukumbi.

15 Umbali kuanzia ingilio la njia ya lango hadi mwisho kabisa wa baraza yake ulikuwa dhiraa hamsini.

16 Kulikuwa na vidirisha kwenye hivyo vyumba vya walinzi na nguzo za hivyo vyumba zilikuwa kwenye mzunguko wa hilo lango, vivyo hivyo kulikuwa na madirisha yaliyozunguka kuelekeana na ua na juu ya kila nguzo kulikuwa na mapambo ya miti ya mitende.

Ukumbi Wa Nje

17 Kisha akanileta katika ukumbi wa nje. Huko nikaona vyumba vingine pamoja na njia iliyokuwa imejengwa kuzunguka ukumbi wote, kulikuwa na vyumba thelathini vimepangana kando ya hiyo njia.

18 Njia hii iliyojengwa iliambaa na lango, ikiwa na urefu sawa na lango, hii ilikuwa ni njia ya chini.

19 Kisha akapima umbali kutoka ndani ya lango la chini mpaka nje ya ukumbi wa ndani, nao ulikuwa dhiraa mia mojaupande wa mashariki na dhiraa mia moja upande wa kaskazini.

Lango La Kaskazini

20 Kisha akapima urefu na upana wa lango linaloelekea kaskazini, kukabili ukumbi wa nje.

21 Vyumba vyake vilikuwa vitatu kila upande, kuta zilizogawanya vyumba na baraza ilikuwa na vipimo sawa na zile kuta za lango la kwanza. Zilikuwa na urefu wa dhiraa hamsini na upana wa dhiraa ishirini na tano.

22 Madirisha yake, baraza yake na nakshi yake ya miti ya mitende vilikuwa na vipimo sawasawa na vile vya lango linaloelekea mashariki. Kulikuwa na ngazi saba za kupandia huko, pamoja na baraza yake mkabala nazo.

23 Kulikuwa na lango kwenye ukumbi wa ndani lililoelekea lile lango la kaskazini, kama vile ilivyokuwa ule upande wa mashariki. Akapima kutoka lango moja hadi lile lililo mkabala nalo, lilikuwa dhiraa mia moja.

Lango La Kusini

24 Ndipo akaniongoza mpaka upande wa kusini, nami nikaona lango linaloelekea kusini. Akaipima miimo yake na baraza yake, navyo vilikuwa na vipimo sawa kama hivyo vingine.

25 Lango na baraza yake vilikuwa na madirisha membamba pande zote, kama madirisha ya huko kwingine. Ilikuwa na urefu wa dhiraa hamsini na upana wake dhiraa ishirini na tano.

26 Kulikuwa na ngazi saba za kupandia huko, pamoja na baraza yake mkabala nazo, ilikuwa na nakshi ya miti ya mitende kwenye kuta zinazogawanya vyumba kila upande.

27 Ukumbi wa ndani pia ulikuwa na lango linaloelekea kusini, naye akapima kutoka lango hili mpaka kwenye lango la nje upande wa kusini, ilikuwa dhiraa mia moja.

Malango Ya Kuelekea Ukumbi Wa Ndani

28 Kisha akanileta mpaka ukumbi wa ndani kwa kupitia lango la kusini, naye akapima lango la kusini, ambalo lilikuwa na vipimo sawa na yale mengine.

29 Vyumba vyake, kuta zilizogawanya vyumba na ukumbi wake zilikuwa na vipimo sawasawa na zile nyingine. Hilo lango na baraza yake vilikuwa na madirisha pande zote. Navyo vilikuwa na urefu wa dhiraa hamsini na upana wa dhiraa ishirini na tano.

30 (Baraza za malango zilizozunguka ukumbi wa ndani zilikuwa na upana wa dhiraa ishirini na tano na kina cha dhiraa tano.)

31 Baraza yake ilielekeana na ukumbi wa nje, miimo yake ilinakshiwa miti ya mitende, kulikuwa na ngazi nane za kupandia huko.

32 Kisha akanileta mpaka kwenye ukumbi wa ndani ulioko upande wa mashariki, naye akalipima lango hilo, lilikuwa na vipimo vilivyo sawasawa na yale mengine.

33 Vyumba vyake, kuta zake na baraza yake vilikuwa na vipimo vilivyo sawa na vile vingine. Lile lango pamoja na baraza yake vilikuwa na madirisha pande zote. Urefu wake ulikuwa dhiraa hamsini na upana wake dhiraa ishirini na tano.

34 Baraza yake ilielekea ukumbi wa nje, miimo yake ilinakshiwa miti ya mitende pande zote. Kulikuwa na ngazi nane za kupandia huko.

35 Kisha akanileta mpaka kwenye lango la kaskazini na kulipima. Lilikuwa na vipimo sawa na yale mengine,

36 kama vile ilivyokuwa kwa vyumba, kuta zake na baraza yake, tena kulikuwa na madirisha pande zote. Ilikuwa na urefu wa dhiraa hamsini na upana wake dhiraa ishirini na tano.

37 Baraza yake ilielekeana na ukumbi wa nje, miimo yake ilinakshiwa miti ya mitende pande zote, kulikuwa na ngazi nane za kupandia huko.

Vyumba Vya Kutayarishia Dhabihu

38 Kulikuwa na chumba na mlango karibu na baraza katika kila njia ya ndani ya lango ambamo sadaka za kuteketezwa zilioshwa.

39 Kwenye baraza ya lile lango kulikuwepo meza mbili kila upande, ambako sadaka za kuteketezwa, sadaka za dhambi na sadaka za hatia zilichinjiwa.

40 Karibu na ukuta wa nje wa baraza ya lile lango karibu na ngazi kwenye ingilio kuelekea kaskazini kulikuwa na meza mbili, nako upande mwingine wa ngazi kulikuwepo na meza mbili.

41 Kwa hiyo kulikuwa na meza nne upande mmoja wa lango na nyingine nne upande mwingine, zote zilikuwa meza nane, ambapo dhabihu zilichinjiwa.

42 Pia kulikuwa na meza nne za mawe yaliyochongwa kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, kila meza ilikuwa na urefu wa dhiraa moja na nusu, upana wake dhiraa moja na nusu na kimo cha dhiraa moja. Juu ya meza hizo viliwekwa vyombo vya kuchinjia sadaka za kuteketezwa na dhabihu nyingine mbalimbali.

43 Kulikuwa na kulabu, urefu wake nyanda nne, zilikuwa zimeshikizwa ukutani pande zote. Meza zilikuwa kwa ajili ya nyama za sadaka.

Vyumba Kwa Ajili Ya Makuhani

44 Nje ya lango la ndani, kwenye ukumbi wa ndani, kulikuwa na vyumba viwili, kimoja upande wa lango la kaskazini nacho kilielekea kusini, kingine upande wa lango la kusini nacho kilielekea kaskazini.

45 Akaniambia, “Chumba kinachoelekea upande wa kusini ni kwa ajili ya makuhani ambao wana usimamizi wa hekaluni,

46 nacho chumba kinachoelekea upande wa kaskazini ni kwa ajili ya makuhani wenye usimamizi wa madhabahuni. Hawa ni wana wa Sadoki, ambao ndio Walawi pekee wanaoweza kumkaribiaBwanaili kuhudumu mbele zake.”

47 Ndipo alipopima ukumbi: nao ulikuwa mraba wa dhiraa mia moja urefu na upana. Madhabahu ilikuwa mbele ya Hekalu.

Hekalu

48 Akanileta mpaka kwenye baraza ya Hekalu naye akaipima miimo ya hiyo baraza, nayo ilikuwa na upana wa dhiraa tatukila upande. Upana wa ingilio ulikuwa dhiraa kumi na nnena kuta zake zilikuwa na upana wa dhiraa tatu kila upande.

49 Baraza ilikuwa na dhiraa ishirini kwenda juu na dhiraa kumi na mbilikuanzia mbele hadi nyuma. Kulikuwa na ngazi kumi za kupandia huko, pia kulikuwa na nguzo kwa kila upande wa miimo.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EZK/40-90dfbba3fe1ad386d0ec90589fe487f2.mp3?version_id=1627—

Ezekieli 41

1 Kisha yule mtu akanileta katika sehemu ya nje ya patakatifu naye akaipima miimo, upana wake ulikuwa dhiraa sitakila upande.

2 Ingilio lilikuwa la upana wa dhiraa kumi na kuta zilizojitokeza kila upande zilikuwa na upana wa dhiraa tano. Pia akapima sehemu ya nje ya patakatifu, nayo ilikuwa na urefu wa dhiraa arobainina upana wa dhiraa ishirini.

3 Kisha akaingia sehemu ya ndani ya patakatifu na kupima miimo ya ingilio, kila mmoja ulikuwa na upana wa dhiraa mbili. Ingilio lilikuwa na upana wa dhiraa sita, na kuta zilizotokeza kila upande zilikuwa na upana wa dhiraa saba.

4 Naye akapima urefu wa ndani ya patakatifu nao ulikuwa dhiraa ishirini na upana wake ulikuwa dhiraa ishirini hadi mwisho wa sehemu ya nje ya patakatifu. Akaniambia, “Hapa ndipo Patakatifu pa Patakatifu.”

5 Kisha akapima ukuta wa Hekalu, nao ulikuwa na unene wa dhiraa sita, na kila chumba cha pembeni kuzunguka Hekalu kilikuwa na upana wa dhiraa nne.

6 Vyumba vya pembeni vilikuwa na ghorofa tatu, kimoja juu ya kingine, kila ghorofa ilikuwa na vyumba thelathini. Kulikuwa na boriti katika ukuta wote wa Hekalu ili kuimarisha vyumba vya pembeni, kwa hiyo boriti hizo hazikushikamanishwa kwenye ukuta wa Hekalu.

7 Vyumba vya pembeni vilivyozunguka Hekalu vilizidi kupanuka kulingana na sakafu zilivyokwenda juu. Ujenzi uliozunguka Hekalu ulijengwa kukwea juu, kwa hiyo vyumba vilipanuka kwa kadiri ya kila kimoja kilivyokwenda juu. Ngazi za kupandia zilianzia sakafu ya chini hadi sakafu ya juu kabisa kwa kupitia sakafu ya kati.

8 Nikaona pia kuwa Hekalu lilikuwa na kitako kilichoinuliwa pande zote, huu ulikuwa ndio msingi wa vile vyumba vya pembeni ambao ulikuwa na urefu wa ule ufito mmoja wa kupimia, yaani, dhiraa ndefu sita.

9 Ukuta wa nje wa vyumba vya pembeni ulikuwa na unene wa dhiraa tano. Eneo la wazi katikati ya vyumba vya pembeni vya Hekalu

10 na vyumba vya makuhani lilikuwa na upana wa dhiraa ishirini kuzunguka Hekalu pande zote.

11 Kulikuwa na maingilio kwenye vyumba vya pembeni kutokea eneo lililo wazi, moja upande wa kaskazini na lingine upande wa kusini, nao msingi uliounganisha lile eneo la wazi ulikuwa na upana wa dhiraa tano ukilizunguka lote.

12 Jengo lililoelekeana na ua wa Hekalu upande wa magharibi lilikuwa na upana wa dhiraa sabini. Ukuta wa jengo hilo ulikuwa na unene wa dhiraa tano, kulizunguka lote, urefu ulikuwa wa dhiraa tisini.

13 Kisha akapima Hekalu, lilikuwa na urefu wa dhiraa mia moja na ua wa Hekalu na jengo pamoja na kuta zake vilikuwa na urefu wa dhiraa mia moja pia.

14 Upana wa ua wa Hekalu upande wa mashariki, pamoja na upande wa mbele wa Hekalu ulikuwa dhiraa mia moja.

15 Kisha akapima urefu wa jengo linaloelekeana na ua upande wa nyuma wa Hekalu, pamoja na vyumba vyake kila upande, ilikuwa dhiraa mia moja.

Mahali Patakatifu pa nje, mahali Patakatifu pa ndani, pamoja na baraza inayoelekeana na ukumbi,

16 pamoja na vizingiti, madirisha membamba na vyumba vyote vitatu, kila kimoja pamoja na kizingiti vilifunikwa kwa mbao. Sakafu, ukuta mpaka kwenye madirisha na madirisha yenyewe vilifunikwa kwa mbao.

17 Katika nafasi iliyokuwa juu upande wa nje wa ingilio la mahali Patakatifu pa ndani na juu ya kuta zilizozunguka Patakatifu pa ndani na Patakatifu pa nje kwa nafasi zilizo sawa

18 kulinakshiwa makerubi na miti ya mitende. Miti ya mitende ilikuwa kati ya kerubi na kerubi. Kila kerubi alikuwa na nyuso mbili:

19 upande mmoja uso wa mwanadamu kuelekea mti wa mtende na upande mwingine uso wa simba ukielekea mti mwingine wa mtende. Ilinakshiwa kuzunguka Hekalu lote.

20 Kuanzia sakafu mpaka eneo lililo juu ya ingilio, palinakshiwa makerubi na miti ya mitende pamoja na kwenye ukuta wa nje wa patakatifu.

21 Mahali patakatifu pa nje palikuwa na miimo ya mlango uliokuwa mraba na ule uliokuwa katika Patakatifu Pa Patakatifu ulikuwa unafanana na huo mwingine.

22 Kulikuwa na madhabahu ya mbao kimo chake dhiraa tatu na ilikuwa dhiraa mbili mraba pande zote, tako lake na pande zake zilikuwa za mbao. Yule mtu akaniambia, “Hii ni meza ambayo iko mbele zaBwana.”

23 Mahali patakatifu pa nje na Patakatifu Pa Patakatifu zilikuwa na milango miwili.

24 Kila mlango ulikuwa na vipande viwili, vipande viwili vilivyoshikwa na bawaba vyenye kufunguka kwa kila mlango.

25 Juu ya hiyo milango ya Patakatifu palinakshiwa makerubi na miti ya mitende kama yale yaliyonakshiwa kwenye kuta na kulikuwa na ubao ulioning’inia mbele ya baraza kwa nje.

26 Katika kuta za pembeni za ukumbi kulikuwa na madirisha membamba yaliyonakshiwa miti ya mitende kila upande. Vyumba vya pembeni vya Hekalu pia vilikuwa vimefunikwa kwa mbao.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EZK/41-80e6aeb20c415ab3db57fd246c32c901.mp3?version_id=1627—