Yeremia 19

Gudulia La Udongo Lililovunjika

1 Hili ndilo asemaloBwana: “Nenda ukanunue gudulia la udongo kutoka kwa mfinyanzi. Wachukue baadhi ya wazee wa watu na wa makuhani

2 na mtoke mwende mpaka kwenye Bonde la Ben-Hinomu, karibu na ingilio la Lango la Vigae. Huko tangaza maneno ninayokuambia,

3 nawe useme, ‘Sikieni neno laBwana, enyi wafalme wa Yuda na watu wa Yerusalemu. Hili ndiloBwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli asemalo: Sikilizeni! Nitaleta maafa mahali hapa ambayo yatafanya masikio ya kila mmoja atakayesikia habari zake yawashe.

4 Kwa kuwa wameniacha na kupafanya mahali hapa kuwa pa miungu ya kigeni, wameiteketezea sadaka miungu ambayo wao wala baba zao wala wafalme wa Yuda kamwe hawakuijua, nao wamelijaza eneo hili kwa damu isiyo na hatia.

5 Wamejenga mahali pa juu pa kuabudia miungu pa Baali ili kuteketeza wana wao katika moto kama sadaka kwa Baali, kitu ambacho sikukiamuru wala kukitaja, wala hakikuingia akilini mwangu.

6 Hivyo jihadharini, siku zinakuja, asemaBwana, wakati watu hawatapaita tena mahali hapa Tofethi ama Bonde la Ben-Hinomu, bali Bonde la Machinjo.

7 “ ‘Nitaiharibu mipango ya Yuda na Yerusalemu mahali hapa. Nitawafanya waanguke kwa upanga mbele ya adui zao, katika mikono ya wale watafutao uhai wao, nami nitaitoa mizoga yao kuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wa nchi.

8 Nitauharibu mji huu na kuufanya kitu cha kudharauliwa, wote wapitao karibu watashangaa na wataudhihaki kwa ajili ya majeraha yake yote.

9 Nitawafanya wao kula nyama ya wana wao na binti zao, kila mmoja atakula nyama ya mwenzake wakati wa dhiki ya kuzungukwa na jeshi lililowekwa juu yao na adui wanaotafuta uhai wao.’

10 “Kisha livunje lile gudulia wakati wale walio pamoja nawe wakiwa wanaangalia,

11 uwaambie, ‘Hili ndiloBwanaMwenye Nguvu Zote asemalo: Nitalivunja taifa hili na mji huu kama gudulia hili la mfinyanzi lilivyovunjwa, nalo haliwezi kutengenezeka tena. Watawazika waliokufa huko Tofethi hata isiwepo nafasi zaidi.

12 Hivi ndivyo nitakavyopafanya mahali hapa na kwa wale waishio ndani yake, asemaBwana. Nitaufanya mji huu kama Tofethi.

13 Nyumba zilizoko Yerusalemu na zile za wafalme wa Yuda zitatiwa unajisi kama mahali hapa, yaani, Tofethi. Nyumba zote ambazo walifukiza uvumba juu ya mapaa yake kwa jeshi lote la angani na kumimina dhabihu ya kinywaji kwa miungu mingine.’ ”

14 Kisha Yeremia akarudi kutoka Tofethi, mahali ambapoBwanaalikuwa amemtuma kutoa unabii, akasimama katika ua wa Hekalu laBwanana kuwaambia watu wote,

15 “Hili ndiloBwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: ‘Sikilizeni! Nitaleta juu ya mji huu pamoja na vijiji vinavyouzunguka kila maafa niliyosema dhidi yake, kwa sababu wamekuwa na shingo ngumu na hawakuyasikiliza maneno yangu.’ ”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JER/19-314cbf23476c1ea047aacb146d7dd69e.mp3?version_id=1627—

Yeremia 20

Yeremia Ateswa Na Pashuri

1 Ikawa kuhani Pashuri mwana wa Imeri, mkuu wa maafisa wa Hekalu laBwana, alipomsikia Yeremia akitoa unabii juu ya mambo haya,

2 akaamuru Yeremia nabii apigwe na kufungwa katika mkatale katika Lango la Juu la Benyamini katika Hekalu laBwana.

3 Siku ya pili Pashuri alipomwachia kutoka kwenye mkatale, Yeremia akamwambia, “Bwanahakukuita jina lako kuwa Pashuri bali Magor-Misabibu.

4 Kwa kuwa hili ndilo asemaloBwana: ‘Nitakufanya kuwa hofu kuu kwako wewe mwenyewe na rafiki zako wote, kwa macho yako mwenyewe utawaona wakianguka kwa upanga wa adui zao. Nitawatia Wayahudi wote mikononi mwa mfalme wa Babeli, ambaye atawachukua na kuwapeleka Babeli ama awaue kwa upanga.

5 Nitatia utajiri wote wa mji huu kwa adui zao, yaani, mazao yao yote, vitu vyao vyote vya thamani na hazina zote za wafalme wa Yuda. Watavitwaa kwa nyara na kuvipeleka Babeli.

6 Nawe Pashuri pamoja na wote waishio katika nyumba yako mtakwenda uhamishoni Babeli. Mtafia humo na kuzikwa, wewe na rafiki zako wote ambao umewatabiria uongo.’ ”

Malalamiko Ya Yeremia

7 EeBwana, umenidanganya,

nami nikadanganyika;

wewe una nguvu kuliko mimi,

nawe umenishinda.

Ninadharauliwa mchana kutwa,

kila mmoja ananidhihaki.

8 Kila ninenapo, ninapiga kelele

nikitangaza ukatili na uharibifu.

Kwa hiyo neno laBwanalimeniletea matukano

na mashutumu mchana kutwa.

9 Lakini kama nikisema, “Sitamtaja

wala kusema tena kwa jina lake,”

neno lake linawaka ndani ya moyo wangu kama moto,

moto uliofungwa ndani ya mifupa yangu.

Nimechoka sana kwa kulizuia ndani mwangu;

kweli, siwezi kujizuia.

10 Ninasikia minong’ono mingi,

“Hofu iko pande zote!

Mshitakini! Twendeni tumshitaki!”

Rafiki zangu wote wananisubiri niteleze,

wakisema,

“Labda atadanganyika;

kisha tutamshinda

na kulipiza kisasi juu yake.”

11 LakiniBwanayu pamoja nami

kama shujaa mwenye nguvu;

hivyo washitaki wangu watajikwaa

na kamwe hawatashinda.

Watashindwa, nao wataaibika kabisa;

kukosa adabu kwao hakutasahauliwa.

12 EeBwanaMwenye Nguvu Zote,

wewe umjaribuye mwenye haki

na kupima moyo na nia,

na nione ukilipiza kisasi juu yao,

kwa maana kwako

nimeliweka shauri langu.

13 MwimbieniBwana!

MpeniBwanasifa!

Huokoa uhai wa mhitaji

kutoka mikononi mwa waovu.

14 Ilaaniwe siku niliyozaliwa!

Nayo isibarikiwe ile siku

mama yangu aliyonizaa!

15 Alaaniwe mtu yule aliyemletea baba yangu habari,

yule aliyemfanya afurahi sana, akisema,

“Mtoto amezaliwa kwako,

tena mtoto wa kiume!”

16 Mtu huyo na awe kama miji ile

ambayoBwanaMungu

aliiangamiza bila huruma.

Yeye na asikie maombolezo asubuhi

na kilio cha vita wakati wa adhuhuri.

17 Kwa sababu hakuniua nikiwa tumboni,

hivyo mama yangu angekuwa kaburi langu,

nalo tumbo lake la uzazi

lingebaki kuwa kubwa daima.

18 Kwa nini basi nilitoka tumboni

ili kuona taabu na huzuni

na kuzimaliza siku zangu katika aibu?

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JER/20-cedf2c89bb12c3fc49c923a2d0582c7b.mp3?version_id=1627—

Yeremia 21

Mungu Anakataa Ombi La Sedekia

1 Neno lilimjia Yeremia kutoka kwaBwanawakati Mfalme Sedekia alipowatuma Pashuri mwana wa Malkiya na kuhani Sefania mwana wa Maaseya kwake kusema:

2 “Tuulizie sasa kwaBwanakwa sababu Nebukadneza mfalme wa Babeli anatushambulia. LabdaBwanaatatenda maajabu kwa ajili yetu kama nyakati zilizopita ili Nebukadneza atuondokee.”

3 Lakini Yeremia akawajibu, “Mwambieni Sedekia,

4 ‘Hili ndiloBwana, Mungu wa Israeli asemalo: Ninakaribia kuwageuzia silaha za vita zilizo mikononi mwenu, ambazo mnatumia kupigana na mfalme wa Babeli na Wakaldayo ambao wako nje ya ukuta wakiwazunguka kwa jeshi. Nami nitawakusanya ndani ya mji huu.

5 Mimi mwenyewe nitapigana dhidi yenu kwa mkono wangu ulionyooshwa na mkono wa nguvu kwa hasira na ghadhabu kali na ukali mwingi.

6 Nitawaangamiza waishio katika mji huu, watu na wanyama, nao watauawa kwa tauni ya kutisha.

7 Baada ya hayo, nitamtia Sedekia mfalme wa Yuda, maafisa wake na watu wa mji huu ambao walinusurika tauni, upanga na njaa mkononi mwa Nebukadneza mfalme wa Babeli na kwa adui zao wale wanaotafuta uhai wao. Atawaua kwa upanga, hatakuwa na rehema juu yao au huruma wala kuwasikitikia,’ asemaBwana.

8 “Zaidi ya hayo, waambie watu hawa, ‘Hili ndilo asemaloBwana: Tazama, naweka mbele yenu njia ya uzima na njia ya mauti.

9 Ye yote atakayekaa katika mji huu atakufa kwa upanga, njaa au tauni. Lakini ye yote atakayetoka na kujisalimisha kwa Wakaldayo ambao wameuzunguka mji huu kwa jeshi atanusurika, naye ataishi.

10 Nimekusudia kuufanyia mji huu jambo baya wala si jema. Utatiwa mikononi mwa mfalme wa Babeli naye atauteketeza kwa moto, asemaBwana.’

11 “Zaidi ya hayo, iambie nyumba ya kifalme ya Yuda, ‘Sikia neno laBwana,

12 Ewe nyumba ya Daudi, hili ndiloBwanaasemalo:

“ ‘Hukumuni kwa haki kila asubuhi,

Mwokoeni kutoka mikononi mwa mdhalimu

yeye aliyetekwa nyara,

la sivyo ghadhabu yangu italipuka

na kuwaka kama moto

kwa sababu ya uovu mlioufanya:

itawaka na hakuna wa kuizima.

13 Niko kinyume nawe, Ee Yerusalemu,

wewe uishiye juu ya bonde hili

kwenye uwanda wa juu wa miamba,

asemaBwana,

wewe usemaye, “Ni nani awezaye

kuja kinyume chetu?

Nani ataingia mahali pa kimbilio letu?”

14 Nitawaadhibu kama istahilivyo matendo yenu,

asemaBwana.

Nitawasha moto katika misitu yenu

ambao utateketeza kila kitu

kinachowazunguka ninyi.’ ”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JER/21-98eb96f08aac4f2dc1e604a1079c9c98.mp3?version_id=1627—

Yeremia 22

Hukumu Dhidi Ya Wafalme Waovu

1 Hili ndilo asemaloBwana: “Shuka kwenye jumba la kifalme la mfalme wa Yuda na utangaze ujumbe huu huko:

2 ‘Sikia neno laBwana, Ee mfalme wa Yuda, wewe uketiye kwenye kiti cha enzi cha Daudi, wewe, maafisa wako na watu wako mnaokuja kwa kupitia malango haya.

3 Hili ndiloBwanaasemalo: Tenda kwa haki na kwa adili. Mwokoe kutoka mkononi mwa mdhalimu yeye aliyetekwa nyara. Usimtendee mabaya wala ukatili mgeni, yatima au mjane wal a usimwage damu isiyo na hatia mahali hapa.

4 Kwa kuwa kama ukiwa mwangalifu kushika maagizo haya, ndipo wafalme watakaokalia kiti cha enzi cha Daudi watakapoingia kupitia malango ya jumba hili la kifalme, wakiwa wamepanda magari na farasi huku wakifuatana na maafisa wao na watu wao.

5 Lakini kama hukuyatii maagizo haya, asemaBwana, ninaapa kwa nafsi yangu kwamba jumba hili litakuwa gofu.’ ”

6 Kwa kuwa hili ndiloBwanaasemalo kuhusu jumba la kifalme la mfalme wa Yuda:

“Ingawa uko kama Gileadi kwangu,

kama kilele cha Lebanoni,

hakika nitakufanya uwe kama jangwa,

kama miji ambayo haijakaliwa na watu.

7 Nitawatuma waharabu dhidi yako,

kila mtu akiwa na silaha zake,

nao watazikata boriti zako nzuri za mierezi

na kuzitupa motoni.

8 “Watu kutoka mataifa mengi watapitia karibu na mji huu na kuulizana, ‘Kwa niniBwanaamefanya jambo la namna hii juu ya mji huu mkubwa?’

9 Nalo jibu litakuwa: ‘Kwa sababu wameliacha Agano laBwana, Mungu wao na wameabudu na kuitumikia miungu mingine.’ ”

10 Usimlilie yeye aliyekufa wala usimwombolezee;

badala yake, afadhali umlilie kwa uchungu

yule aliyepelekwa uhamishoni,

kwa sababu kamwe hatairudia

wala kuiona tena nchi yake alikozaliwa.

11 Kwa kuwa hili ndilo asemaloBwanakuhusu Shalumumwana wa Yosia, aliyeingia mahali pa baba yake kuwa mfalme wa Yuda, lakini ameondoka mahali hapa: “yeye kamwe hatarudi tena.

12 Atafia huko mahali walipompeleka kuwa mateka, hataiona tena nchi hii.”

13 “Ole wake yeye ajengaye jumba lake la kifalme

kwa njia ya dhuluma,

vyumba vyake vya juu kwa udhalimu,

akiwatumikisha watu wa nchi yake pasipo malipo,

bila kuwalipa kwa utumushi wao.

14 Asemaye, ‘Nitajijengea jumba kubwa la kifalme

na vyumba vya juu vyenye nafasi kubwa.’

Hivyo anaweka ndani yake madirisha makubwa,

huweka mbao za mierezi

na kuipamba kwa rangi nyekundu.

15 “Je, inakufanya kuwa mfalme

kwa kuongeza idadi ya mierezi?

Je, baba yako hakuwa na chakula na kinywaji?

Alifanya yaliyo sawa na haki,

hivyo yeye akafanikiwa katika yote.

16 Aliwatetea maskini na wahitaji,

hivyo yeye akafanikiwa katika yote,

Je, hiyo si ndiyo maana ya kunijua mimi?”

asemaBwana.

17 “Lakini macho yako na moyo wako vimeelekezwa tu

katika mapato ya udhalimu,

kwa kumwaga damu isiyo na hatia,

kwa uonevu na ukatili.”

18 Kwa hiyo hili ndilo asemaloBwanakuhusu Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda:

“Hawatamwombolezea wakisema:

‘Ole, ndugu yangu! Ole umbu langu!’

Hawatamwombolezea wakisema:

‘Ole, bwana wangu! Ole, fahari yake!’

19 Atazikwa maziko ya punda:

ataburutwa na kutupwa

nje ya malango ya Yerusalemu.”

20 “Panda Lebanoni ukapige kelele,

sauti yako na isikike huko Bashani,

piga kelele toka Abarimu, kwa kuwa

wale wote waliojiunga nawe

wameangamizwa.

21 Nilikuonya wakati ulipojisikia kwamba uko salama,

lakini ulisema, ‘Mimi sitasikiliza!’

Hii imekuwa ndiyo kawaida yako tangu ujana wako;

hujanitii mimi.

22 Upepo utawaondoa wachungaji wako wote,

wale ulioungana nao

watakwenda uhamishoni.

Kisha utaaibika na kufedheheka kwa sababu

ya uovu wako wote.

23 Wewe uishiye Lebanoni,

wewe uliyetulia

kwenye majengo ya mierezi,

tazama jinsi utakavyoomboleza

maumivu makali yatakapokupata,

maumivu kama yale ya mwanamke

mwenye utungu wa kuzaa!

24 “Hakika kama niishivyo,” asemaBwana, “hata kama wewe, Yekoniamwana wa Yehoyakimumfalme wa Yuda, ungekuwa pete yangu ya muhuri katika mkono wangu wa kuume, bado ningekung’oa utoke hapo.

25 Nitakutia mikononi mwa wale wanaotafuta uhai wako, wale unaowaogopa, yaani Nebukadneza mfalme wa Babeli na kwa Wakaldayo.

26 Nitakutupa mbali wewe na mama aliyekuzaa mwende katika nchi nyingine, ambayo hakuna hata mmoja wenu aliyezaliwa huko, nanyi mtafia huko.

27 Kamwe hamtarudi katika nchi mliyotamani kuirudia.”

28 Je, huyu Yekonia ni mtu aliyedharauliwa,

chungu kilichovunjika,

tena chombo kisichotakiwa na mtu ye yote?

Kwa nini yeye na watoto wake watupwe nje kwa nguvu,

na kutupwa kwenye nchi wasioijua?

29 Ee nchi, nchi, nchi,

sikia neno laBwana!

30 Hili ndiloBwanaasemalo:

“Mwandike huyu mtu kama asiye na mtoto,

mtu ambaye hatafanikiwa maisha yake yote,

kwa maana hakuna mtoto wake atakayefanikiwa,

kukaa kwenye kiti cha enzi cha Daudi

wala kuendelea kutawala katika Yuda.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JER/22-44564e86e85d800cc764660656ea5d8f.mp3?version_id=1627—

Yeremia 23

Tawi La Haki

1 “Ole wa wachungaji wanaoharibu na kutawanya kondoo wa malisho yangu!” AsemaBwana.

2 Kwa hiyo hili ndiloBwana, Mungu wa Israeli, analowaambia wachungaji wanaowachunga watu wangu: “Kwa sababu mmelitawanya kundi langu, na kuwafukuzia mbali wala hamkuwatunza, basi mimi nitawaadhibu kwa ajili ya uovu mliofanya,” asemaBwana.

3 “Mimi mwenyewe nitayakusanya mabaki ya kundi langu kutoka nchi zote ambazo nimewafukuzia nami nitawarudisha katika malisho yao, mahali ambapo watazaa na kuongezeka idadi yao.

4 Nitaweka wachungaji juu yao ambao watawachunga, nao hawataogopa tena au kutishwa, wala hatapotea hata mmoja,” asemaBwana.

5 Bwanaasema, “Siku zinakuja,

nitakapomwinulia Daudi Tawi lenye haki,

Mfalme atakayetawala kwa hekima

na kutenda lililo haki na sawa katika nchi.

6 Katika siku zake, Yuda ataokolewa

na Israeli ataishi salama.

Hili ndilo jina atakaloitwa kwalo:

BwanaHaki Yetu.

7 “Hivyo basi, siku zinakuja, wakati ambapo watu hawatasema tena, ‘Hakika kamaBwanaaishivyo, aliyewapandisha Waisraeli kutoka nchi ya Misri,’

8 bali watasema, ‘Hakika kama aishivyoBwana, aliyewatoa wazao wa Israeli katika nchi ya kaskazini na katika nchi zote alizokuwa amewafukuzia,’ asemaBwana. Ndipo wataishi katika nchi yao wenyewe.”

Manabii Wasemao Uongo

9 Kuhusu manabii:

Moyo wangu umevunjika ndani yangu;

mifupa yangu yote inatetemeka.

Nimekuwa kama mtu aliyelewa,

kama mtu aliyelemewa na divai,

kwa sababu yaBwana

na maneno yake matakatifu.

10 Nchi imejaa wazinzi;

kwa sababu ya laana nchi imekauka

na malisho yaliyoko nyikani yamekauka.

Mwenendo wa manabii ni mbaya

na mamlaka yao si ya haki.

11 “Nabii na kuhani wote si wacha Mungu;

hata hekaluni mwangu ninaona uovu wao,”

asemaBwana.

12 “Kwa hiyo mapito yao yatakuwa utelezi,

watafukuziwa mbali gizani

na huko wataanguka.

Nitaleta maafa juu yao

katika mwaka wa kuadhibiwa kwao,”

asemaBwana.

13 “Miongoni mwa manabii wa Samaria

nililiona jambo la kuchukiza:

Walitabiri kwa Baali

na kuwapotosha Israeli watu wangu.

14 Nako miongoni mwa manabii wa Yerusalemu

nimeona jambo baya sana:

Wanafanya uzinzi

na kuenenda katika uongo.

Wanatia nguvu mikono ya watenda mabaya,

kwa ajili hiyo hakuna ye yote

anayeachana na uovu wake.

Wote wako kama Sodoma kwangu;

watu na Yerusalemu wako kama Gomora.”

15 Kwa hiyo, hili ndiloBwanaMwenye Nguvu Zote asemalo kuhusu manabii:

“Nitawafanya wale chakula kichungu

na kunywa maji yaliyotiwa sumu,

kwa sababu kutokana na manabii wa Yerusalemu

kutokumcha Mungu kumeenea katika nchi yote.”

16 Hili ndiloBwanaMwenye Nguvu Zote asemalo:

“Msisikilize wanachowatabiria manabii,

wanawajaza matumaini ya uongo.

Wanasema maono kutoka katika akili zao wenyewe,

hayatoki katika kinywa chaBwana.

17 Huendelea kuwaambia wale wanaonidharau mimi kwamba,

Bwanaasema: ‘Mtakuwa na amani.’

Kwa wale wote wafuatao ugumu wa mioyo yao

husema, ‘Hakuna dhara litakalowapata.’

18 Lakini ni yupi miongoni mwao aliyesimama

katika baraza laBwana

ili kuona au kusikia neno lake?

Ni nani aliyesikiliza

na kusikia neno lake?

19 Tazama, dhoruba yaBwana

itapasuka kwa ghadhabu,

kisulisuli kitazunguka zunguka

juu ya vichwa vya waovu.

20 Hasira yaBwanahaitageuka

mpaka amelitimiza kusudi la moyo wake.

Siku zijazo mtalifahamu kwa wazi.

21 Mimi sikuwatuma manabii hawa,

lakini bado wamekimbia

wakitangaza ujumbe wao.

Mimi sikusema nao,

lakini wametabiri.

22 Lakini kama wangesimama barazani mwangu,

wangetangaza maneno yangu kwa watu wangu,

nao wangewageuza kutoka katika njia zao mbaya

na kutoka katika matendo yao maovu.”

23 “Je, mimi ni Mungu aliyeko hapa karibu tu,”

Bwanaasema,

“wala si Mungu aliyeko pia mbali?

24 Je, mtu ye yote aweza kujificha

mahali pa siri ili nisiweze kumwona?”

Bwanaasema.

“Je, mimi sikuijaza mbingu na nchi?”

Bwanaasema.

25 “Nimesikia wanayoyasema manabii, hao wanaotabiri uongo kwa Jina langu. Wanasema, ‘Nimeota ndoto! Nimeota ndoto!’

26 Mambo haya yataendelea mpaka lini ndani ya mioyo ya hawa manabii wa uongo, ambao hutabiri maono ya uongo ya akili zao wenyewe?

27 Wanadhani ndoto wanazoambiana wao kwa wao zitawafanya watu wangu walisahau Jina langu, kama baba zao walivyolisahau Jina langu kwa kumwabudu Baali.

28 Mwache nabii aliye na ndoto aseme ndoto yake, lakini yule aliye na neno langu na aliseme kwa uaminifu. Kwa maana jani kavu lina uhusiano gani na ngano?” asemaBwana.

29 “Je, neno langu si kama moto,” asemaBwana, “na kama nyundo ivunjayo mwamba vipande vipande?

30 “Kwa hiyo, niko kinyume na manabii wanaoibiana maneno kana kwamba ni yangu,” asemaBwana.

31 “Naam, mimi niko kinyume na manabii wanaotikisa ndimi zao wenyewe na kusema, ‘Bwanaasema.’

32 Kweli, niko kinyume na hao wanaotabiri ndoto za uongo,” asemaBwana. “Wanazisimulia na kuwapotosha watu wangu kwa uongo wao bila kujali, lakini sikuwatuma wala sikuwaweka. Hawawafaidii watu hawa hata kidogo,” asemaBwana.

Maneno Ya Uongo Na Manabii Wa Uongo

33 “Watu hawa, au nabii, au kuhani watakapokuuliza, ‘Mzigo waBwanani nini?’ Wewe utawaambia, ‘Ninyi ndio mzigo. Nami nitawavua kama vazi, asemaBwana.’

34 Kwa habari ya nabii, kuhani, au wale watu wasemao, ‘Mzigo waBwana,’ nitawaadhibu wao na nyumba zao.

35 Hivyo mtaambiana kila mmoja na mwenzake, miongoni mwenu: ‘Bwanaamejibu nini?’ au ‘Bwanaamesema nini?’

36 Lakini kamwe msiseme tena, ‘Nina mzigo waBwana,’ kwa sababu kila neno la mtu binafsi linakuwa mzigo wake mwenyewe na hivyo kupotosha maneno ya Mungu aliye hai,BwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wetu.

37 Hivi ndivyo utakavyoendelea kumwuliza nabii: ‘Bwanaamekujibu nini?’ Au ‘Je,Bwanaamesema nini?’

38 Ingawa unadai, ‘Huu ni mzigo waBwana,’ hili ndiloBwanaasemalo: Ulitumia maneno, ‘Huu ndio mzigo waBwana,’ hata ingawa nilikuambia kuwa kamwe usiseme, ‘Huu ni mzigo waBwana.’

39 Kwa hiyo, hakika nitakusahau na kukutupa mbali na uso wangu pamoja na mji niliowapa ninyi na baba zenu.

40 Nitaleta juu yako fedheha ya kudumu na aibu ya kudumu ambayo haitasahaulika.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JER/23-7ce7ca3828ff1e73e6bddcedf17d0968.mp3?version_id=1627—

Yeremia 24

Vikapu Viwili Vya Tini

1 Baada ya Yekoniamwana wa Yehoyakimumfalme wa Yuda pamoja na maafisa, mafundi stadi na wahunzi wa Yuda kuchukuliwa kutoka Yerusalemu kwenda Babeli na Nebukadneza mfalme wa Babeli kwenda uhamishoni huko Babeli,Bwanaakanionyesha vikapu viwili vya tini vilivyowekwa mbele ya Hekalu laBwana.

2 Kikapu kimoja kilikuwa na tini nzuri sana, kama zile za mavuno ya kwanza, kikapu cha pili kilikuwa na tini dhaifu sana, mbaya mno zisizofaa kuliwa.

3 KishaBwanaakaniuliza, “Je, Yeremia unaona nini?”

Nikamjibu, “Ninaona tini zile zilizo nzuri, ni nzuri sana, lakini zilizo dhaifu, ni mbaya mno zisizofaa kuliwa.”

4 Kisha neno laBwanalikanijia:

5 “Hili ndiloBwana, Mungu wa Israeli asemalo: ‘Kama zilivyo hizi tini nzuri, ndivyo ninavyowaona kuwa bora watu wa uhamisho kutoka Yuda, niliowaondoa kutoka mahali hapa kwenda katika nchi ya Wakaldayo.

6 Macho yangu yatakuwa juu yao kwa ajili ya kuwapatia mema, nami nitawarudisha tena katika nchi hii. Nitawajenga wala sitawabomoa, nitawapanda wala sitawang’oa,

7 nitawapa moyo wa kunifahamu mimi, kwamba mimi ndimiBwana. Watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao, kwa maana watanirudia kwa moyo wao wote.

8 “ ‘Lakini kama zilivyo zile tini dhaifu, ambazo ni mbaya mno zisizofaa kuliwa,’ asemaBwana, ‘ndivyo nitakavyomtendea Sedekia mfalme wa Yuda, maafisa wake na mabaki wengine kutoka Yerusalemu, kwamba wamebaki katika nchi hii au wanaishi Misri.

9 Nitawafanya kuwa chukizo kabisa na kitu cha kulaumiwa katika mataifa yote ya dunia, watakuwa aibu na kitu cha kudharauliwa, chombo cha dhihaka na kulaaniwa, po pote nitakakowafukuzia.

10 Nitautuma upanga, njaa na tauni dhidi yao mpaka wawe wameangamia kutoka nchi niliyowapa wao na baba zao.’ ”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JER/24-470e55bc0d3f7a0e53c096330bff09fb.mp3?version_id=1627—

Yeremia 25

Miaka Sabini Ya Kuwa Mateka

1 Neno likamjia Yeremia kuhusu watu wote wa Yuda katika mwaka wa nne wa kutawala kwake Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, ambao ulikuwa mwaka wa kwanza wa utawala wa Nebukadneza mfalme wa Babeli.

2 Hivyo nabii Yeremia akawaambia watu wote wa Yuda na wale wote waishio Yerusalemu:

3 Kwa miaka ishirini na mitatu, kuanzia mwaka wa kumi na tatu wa utawala wa Yosia mwana wa Amoni mfalme wa Yuda mpaka siku hii ya leo, neno laBwanalimekuwa likinijia nami nimesema nanyi mara kwa mara lakini hamkusikiliza.

4 IngawaBwanaamewatuma watumishi wake wote hao manabii kwenu mara kwa mara, hamkusikiliza wala hamkujali.

5 Wakasema, “Geukeni sasa, kila mmoja wenu kutoka katika njia yake mbaya na matendo yake maovu ndipo mtaweza kukaa katika nchi ambayoBwanaaliwapa ninyi na baba zenu milele.

6 Msiifuate miungu mingine ili kuitumikia na kuiabudu, msinikasirishe kwa vitu ambavyo mmevitengeneza kwa mikono yenu.”

7 “Lakini ninyi hamkunisikiliza mimi, tena mkanikasirisha kwa vitu mlivyovitengeneza kwa mikono yenu, nanyi mmejiletea madhara juu yenu wenyewe,” asemaBwana.

8 Kwa hiyoBwanaMwenye Nguvu Zote asema hivi: “Kwa sababu hamkuyasikiliza maneno yangu,

9 nitayaita mataifa yote ya kaskazini na mtumishi wangu Nebukadneza mfalme wa Babeli,” asemaBwana, “nitawaleta waishambulie nchi hii na wakazi wake wote na dhidi ya mataifa yote yanayowazunguka. Nitawaangamiza kabisa na kuwafanya kitu cha kuchukiwa na kudharauliwa na kuwa magofu daima.

10 Nitawaondolea sauti ya shangwe na furaha, sauti ya bibi na bwana arusi, sauti ya mawe ya kusagia na mwanga wa taa.

11 Nchi hii yote itakuwa ukiwa na isiyofaa kitu, nayo mataifa haya yatamtumikia mfalme wa Babeli kwa miaka sabini.”

12 “Lakini miaka sabini itakapotimia, nitamwadhibu mfalme wa Babeli na taifa lake na nchi ya Wakaldayo kwa ajili ya hatia yao,” asemaBwana. “Nitaifanya kuwa ukiwa milele.

13 Nitaleta juu ya nchi hiyo mambo yote niliyosema dhidi yake, yote yaliyoandikwa katika kitabu hiki na kutolewa unabii na Yeremia dhidi ya mataifa yote.

14 Wao wenyewe watakuwa watumwa wa mataifa mengi na wafalme wakuu, nitawalipizia sawa sawa na matendo yao na kazi ya mikono yao.”

Kikombe Cha Ghadhabu Ya Mungu

15 Hili ndiloBwana, Mungu wa Israeli, aliloniambia: “Chukua kutoka mkononi mwangu kikombe hiki kilichojaa mvinyo ya ghadhabu yangu na kuyanywesha mataifa yote ambayo ninakutuma kwao.

16 Watakapoinywa watapepesuka na kukasirika sana kwa sababu ya upanga nitakaoupeleka katikati yao.”

17 Hivyo nikakichukua kikombe kutoka mkononi mwaBwanana kuyafanya mataifa yote aliyonituma kwao kukinywa:

18 Yaani Yerusalemu na miji ya Yuda, wafalme wake na maafisa wake, kuwafanya magofu na kuwa kitu cha kuchukiza, cha dhihaka na laana, kama walivyo leo,

19 Farao mfalme wa Misri, watumishi wake, maafisa wake na watu wake wote,

20 pia wageni wote walioko huko, wafalme wote wa nchi ya Uzi, wafalme wote wa Wafilisti (wale wa Ashkeloni, Gaza, Ekroni na watu walioachwa huko Ashdodi),

21 Edomu, Moabu na Amoni,

22 wafalme wote wa Tiro na Sidoni, wafalme wa nchi za pwani ng’ambo ya bahari,

23 Dedani, Tema, Buzi na wote walio maeneo ya mbali,

24 wafalme wote wa Arabuni na wafalme wote wa watu wageni wanaoishi katika jangwa,

25 wafalme wote wa Zimri, Elamu na Umedi,

26 wafalme wote wa pande za kaskazini, wa karibu na wa mbali mmoja baada ya mwingine, yaani, falme zote juu ya uso wa dunia. Baada ya hao wote, mfalme wa Sheshakiatakunywa pia.

27 “Kisha uwaambie, ‘Hili ndiloBwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli asemalo: Kunyweni, mlewe na mtapike, angukeni wala msiinuke tena kwa sababu ya upanga nitakaotuma miongoni mwenu.’

28 Lakini kama wakikataa kupokea kikombe kutoka mikononi mwako na kunywa, waambie, ‘Hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote: Ni lazima mnywe!

29 Tazama, nimeanza kuleta maafa juu ya mji ulio na Jina langu, je, kweli ninyi mtaepuka kuadhibiwa? Hamwezi kuepuka kuadhibiwa kwa maana nitaleta vita juu ya wote waishio duniani, asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.’

30 “Basi sasa toa unabii kwa maneno haya yote dhidi yao, uwaambie:

“ ‘Bwanaatanguruma kutoka juu;

atatoa sauti ya ngurumo

kutoka makao yake matakatifu

na kunguruma kwa nguvu sana

dhidi ya nchi yake.

Atapiga kelele kama wao wakanyagao mizabibu,

atapiga kelele dhidi ya wote waishio duniani.

31 Ghasia zitasikika hadi miisho ya dunia,

kwa maanaBwanaataleta mashtaka

dhidi ya mataifa;

ataleta hukumu juu ya wanadamu wote

na kuwaua waovu wote,’ ”

asemaBwana.

32 Hili ndiloBwanaMwenye Nguvu Zote asemalo:

“Tazama! Maafa yanaenea

kutoka taifa moja hadi jingine;

tufani kubwa inainuka

kutoka miisho ya dunia.”

33 Wakati huo, hao waliouawa naBwanawatatapakaa kila mahali, kuanzia mwisho mmoja wa dunia hadi mwisho mwingine. Hawataombolezewa wala kukusanywa au kuzikwa lakini watakuwa kama mavi yaliyoenea juu ya ardhi.

34 Lieni na kuomboleza, enyi wachungaji,

mgaegae mavumbini,

ninyi viongozi wa kundi.

Kwa maana wakati wenu wa kuchinjwa umewadia;

mtaanguka na kuvunjwavunjwa

kama vyombo vizuri vya udongo.

35 Wachungaji hawatakuwa na mahali pa kukimbilia,

viongozi wa kundi hawatapata

mahali pa kutorokea.

36 Sikia kilio cha wachungaji,

maombolezo ya viongozi wa kundi,

kwa maanaBwanaanayaharibu malisho yao.

37 Makao yao ya amani yataharibiwa

kwa sababu ya hasira kali yaBwana.

38 Kama simba ataacha pango lake,

nchi yao itakuwa ukiwa

kwa sababu ya upanga wa mdhalimu

na kwa sababu ya hasira kali

yaBwanaMungu.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JER/25-5c30d2d0c9b69be6b39f63c913312dd4.mp3?version_id=1627—

Yeremia 26

Yeremia

1 Mwanzoni mwa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, neno hili lilikuja kutoka kwaBwana:

2 “Hili ndiloBwanaasemalo: Simama katika ua wa nyumba yaBwanana useme na watu wote wa miji ya Yuda wanaokuja kuabudu katika nyumba yaBwana. Waambie kila kitu nitakachokuamuru, usipunguze neno.

3 Huenda watasikiliza na kila mmoja akageuka kutoka katika njia yake mbaya. Kisha nitawahurumia na kuacha kuwaletea maafa niliyokuwa ninapanga kwa sababu ya maovu waliyofanya.

4 Waambie, ‘Hili ndilo asemaloBwana: Ikiwa hamtanisikiliza na kuifuata sheria yangu ambayo nimeiweka mbele yenu,

5 nanyi ikiwa hamtayasikiliza maneno ya watumishi wangu manabii, ambao nimewatuma kwenu tena na tena (ijapokuwa hamkuwasikiliza),

6 ndipo nitaifanya nyumba hii kama Shilo na mji huu kuwa kitu cha kulaaniwa na mataifa yote ya dunia.’ ”

7 Makuhani, manabii na watu wote wakamsikia Yeremia akiyasema maneno haya ndani ya nyumba yaBwana.

8 Lakini mara tu Yeremia alipomaliza kuwaambia watu kila kituBwanaalichomwamuru kukisema, makuhani, manabii na watu wote walimkamata wakisema, “Ni lazima ufe!

9 Kwa nini unatoa unabii katika jina laBwanakwamba nyumba hii itakuwa kama Shilo na mji huu utakuwa ukiwa na kuachwa tupu?” Nao watu wote wakamkusanyikia na kumzunguka Yeremia ndani ya nyumba yaBwana.

10 Maafisa wa Yuda waliposikia kuhusu mambo haya, wakapanda kutoka katika jumba la kifalme wakaenda katika nyumba yaBwanana kushika nafasi zao kwenye ingilio la Lango Jipya la nyumba yaBwana.

11 Kisha makuhani na manabii wakawaambia maafisa pamoja na watu wote, “Mtu huyu anastahili ahukumiwe kifo kwa sababu ametoa unabii mabaya dhidi ya mji huu. Mmesikia kwa masikio yenu wenyewe!”

12 Kisha Yeremia akawaambia maafisa wote na watu wote: “Bwanaamenituma kutoa unabii dhidi ya nyumba hii na mji huu mambo yote mliyoyasikia.

13 Sasa tengenezeni njia zenu na matendo yenu na kumtiiBwanaMungu wenu. NdipoBwanaatawahurumia na kuacha kuleta maafa aliyokuwa ameyatamka dhidi yenu.

14 Lakini kwa habari yangu mimi, niko mikononi mwenu, nifanyieni lo lote mnaloona kuwa ni jema na la haki.

15 Hata hivyo, jueni kwa hakika, ikiwa mtaniua, mtakuwa mmejipatia dhambi kwa damu isiyo na hatia juu yenu wenyewe na juu ya mji huu na wote wanaoishi ndani yake, kwa maana ni kweliBwanaamenituma kwenu ili niseme maneno haya yote masikioni mwenu.”

16 Kisha maafisa na watu wote wakawaambia makuhani na manabii, “Mtu huyu asihukumiwe kifo! Amesema nasi katika jina laBwana, Mungu wetu.”

17 Baadhi ya wazee wa nchi wakasogea mbele wakaliambia kusanyiko lote la watu,

18 “Mika wa Moreshethi alitoa unabii katika siku za Hezekia mfalme wa Yuda. Akawaambia watu wote wa Yuda, ‘Hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote:

“ ‘Mji wa Sayuni utalimwa kama shamba,

Yerusalemu utakuwa lundo

la kifusi cha changarawe,

kilima cha Hekalu kitakuwa kichuguu

kilichoota vichaka.’

19 Je, Hezekia mfalme wa Yuda au mtu mwingine ye yote katika Yuda alimhukumu Mika kufa? Je, Hezekia hakumchaBwanana kuhitaji msaada wake? Je,Bwanahakuwahurumia na akaacha kuleta maafa aliyokuwa ametamka dhidi yao? Tunakaribia sana kujiletea maangamizo ya kutisha sisi wenyewe!”

20 (Wakati huu, Uria mwana wa Shemaya kutoka mji wa Kiriath-Yearimu alikuwa mtu mwingine aliyetoa unabii kwa jina laBwana; alitoa unabii juu ya mambo yaliyofanana na haya dhidi ya mji huu na nchi hii kama alivyofanya Yeremia.

21 Mfalme Yehoyakimu na wakuu wake wote na maafisa waliposikia maneno yake, mfalme alitafuta kumwua. Lakini Uria alipata habari na kwa kuogopa akakimbilia Misri.

22 Hata hivyo, Mfalme Yehoyakimu alimtuma Elnathani mwana wa Akbori huko Misri, pamoja na watu wengine ili kwenda kumkamata Uria.

23 Wakamrudisha Uria kutoka Misri na kumpeleka kwa Mfalme Yehoyakimu, ambaye alimwua kwa upanga na mwili wake kutupwa kwenye eneo la makaburi ya watu wasio na cheo.)

24 Zaidi ya hayo, Ahikamu mwana wa Shefani akamuunga mkono Yeremia, kwa hiyo hakutiwa tena mikononi mwa watu ili auawe.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JER/26-460b47dc5c6b23ac701f6aafbae52496.mp3?version_id=1627—

Yeremia 27

Yuda Kumtumikia Nebukadneza

1 Mwanzoni mwa utawala wa Sedekia mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, neno hili lilimjia Yeremia kutoka kwaBwana:

2 Hili ndiloBwanaaliloniambia: “Tengeneza nira, ujivike shingoni mwako uifunge kwa kamba za ngozi.

3 Kisha utume ujumbe kwa wafalme wa Edomu, Moabu, Amoni, Tiro na Sidoni kupitia wajumbe ambao wamekuja Yerusalemu kwa Sedekia mfalme wa Yuda.

4 Wape ujumbe kwa ajili ya mabwana zao na uwaambie, ‘Hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: “Waambieni hivi mabwana zenu:

5 Kwa uwezo wangu mkuu na kwa mkono wangu ulionyooshwa nimeumba dunia na watu wake na wanyama walioko ndani yake, nami humpa ye yote inipendezavyo.

6 Sasa nitazitia nchi zenu zote mkononi mwa mtumishi wangu Nebukadneza mfalme wa Babeli, nitawafanya hata wanyama wa mwituni wamtumikie.

7 Mataifa yote yatamtumikia yeye pamoja na mwanawe na mwana wa mwanawe hadi wakati wa nchi yake utakapowadia, kisha mataifa mengi na wafalme wenye nguvu nyingi watamshinda.

8 “ ‘ “Lakini kama kukiwa na taifa lo lote au ufalme ambao hautamtumikia Nebukadneza mfalme wa Babeli ama kuinamisha shingo yake chini ya nira yake, nitaliadhibu taifa hilo kwa upanga, njaa na tauni, asemaBwana, mpaka nitakapoliangamiza taifa hilo kwa mkono wake.

9 Kwa hiyo msiwasikilize manabii wenu, waaguzi wenu, waota ndoto wenu, watabiri na wachawi wanaowaambia ninyi, ‘Hamtamtumikia mfalme wa Babeli.’

10 Wanawatabiria ninyi uongo ambako kutawafanya ninyi mhamishwe mbali kutoka kwenye nchi yenu, nitawafukuzia mbali nanyi mtaangamia.

11 Lakini ikiwa taifa lo lote litainama na kuweka shingo yake katika nira ya mfalme wa Babeli na kumtumikia, nitaliacha taifa hilo katika nchi yake yenyewe ili wailime na kuishi humo, asemaBwana.” ’ ”

12 Nilitoa ujumbe huo huo kwa Sedekia mfalme wa Yuda. Nilisema, “Ingiza shingo yako katika nira ya mfalme wa Babeli, mtumikie yeye na watu wake, nawe utaishi.

13 Kwa nini wewe na watu wako mfe kwa upanga, njaa na tauni ambayoBwanaameonya juu ya taifa lo lote ambalo halitamtumikia mfalme wa Babeli?

14 Msiyasikilize maneno ya manabii wanaowaambia kwamba, ‘Hamtamtumikia mfalme wa Babeli,’ kwa sababu wanawatabiria uongo.

15 ‘Sikuwatuma hao,’ asemaBwana. ‘Wanatabiri uongo kwa Jina langu. Kwa hiyo, nitawafukuzia mbali nanyi mtaangamia, ninyi pamoja na manabii wanaowatabiria.’ ”

16 Kisha nikawaambia makuhani na watu wote hawa, “Hili ndilo asemaloBwana: Msiwasikilize manabii wanaosema, ‘Hivi karibuni sana vyombo vya nyumba yaBwanavitarudishwa kutoka Babeli.’ Wanawatabiria ninyi uongo.

17 Ninyi msiwasikilize. Mtumikieni mfalme wa Babeli nanyi mtaishi. Kwa nini mji huu uwe magofu?

18 Kama wao ni manabii na wanalo neno laBwana, basi na wamsihiBwanaMwenye Nguvu Zote kwamba vyombo vilivyobaki katika nyumba yaBwanana katika jumba la kifalme la mfalme wa Yuda na katika Yerusalemu visipelekwe Babeli.

19 Kwa maana hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote kuhusu zile nguzo, ile Bahari, vile vishikizo viwezavyo kuhamishika, vinara na vyombo vingine vilivyoachwa katika mji huu,

20 ambavyo Nebukadneza mfalme wa Babeli hakuvichukua wakati alipomchukua Yekoniamwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda kwenda uhamishoni huko Babeli kutoka Yerusalemu, pamoja na wakuu wote wa Yuda na Yerusalemu.

21 Naam, hili ndiloBwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo kuhusu vitu ambavyo vimebaki ndani ya nyumba yaBwanana ndani ya jumba la kifalme la mfalme wa Yuda na katika Yerusalemu:

22 ‘Vitachukuliwa kupelekwa Babeli, nako huko vitabaki mpaka siku nitakayovijilia,’ asemaBwana. ‘Kisha nitavirudisha na kuvirejesha tena mahali hapa.’ ”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JER/27-22fef31aa57262e873068fe74e6163b2.mp3?version_id=1627—

Yeremia 28

Hanania Nabii Wa Uongo

1 Katika mwezi wa tano wa mwaka ule ule, yaani mwaka wa nne, mwanzoni mwa utawala wa Sedekia mfalme wa Yuda, nabii Hanania mwana wa Azuri, ambaye alitoka Gibeoni, akaniambia katika nyumba yaBwanambele ya makuhani na watu wote:

2 “Hili ndiloBwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli asemalo: ‘Nitaivunja nira ya mfalme wa Babeli.

3 Katika muda wa miaka miwili nitavirudisha mahali hapa vyombo vyote vya nyumba yaBwanaambavyo Nebukadneza mfalme wa Babeli aliviondoa kutoka hapa na kuvipeleka Babeli.

4 Pia nitamrudisha mahali hapa Yekoniamwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda pamoja na wote waliohamishwa kutoka Yuda ambao walikwenda Babeli,’ asemaBwana, ‘kwa kuwa nitaivunja nira ya mfalme wa Babeli.’ ”

5 Ndipo nabii Yeremia akamjibu nabii Hanania mbele ya makuhani na watu wote waliokuwa wamesimama ndani ya nyumba yaBwana.

6 Akasema, “Amen!Bwanana afanye hivyo!Bwanana ayatimize maneno uliyotoa unabii kwa kuvirudisha mahali hapa kutoka Babeli vyombo vya nyumba yaBwanapamoja na wote waliohamishwa.

7 Hata hivyo, nisikilize nikuambie yale nitakayoyasema masikioni mwako na masikioni mwa watu hawa wote:

8 Tangu mwanzo, manabii waliokutangulia wewe na mimi walitabiri vita, maafa na tauni dhidi ya nchi nyingi na falme kubwa.

9 Lakini nabii atakayetabiri amani atatambuliwa kuwa kweli ametumwa naBwanaikiwa unabii wake utatimia.”

10 Kisha nabii Hanania akaiondoa nira iliyokuwa shingoni mwa Yeremia na kuivunja,

11 naye akasema mbele ya watu wote, “Hili ndilo asemaloBwana: ‘Vivi hivi ndivyo nitakavyoivunja nira ya Nebukadneza mfalme wa Babeli kutoka kwenye shingo za mataifa katika muda huu wa miaka miwili.’ ” Kwa jambo hili, nabii Yeremia akaondoka zake.

12 Kitambo kidogo baada nabii Hanania kuivunja nira kutoka katika shingo ya nabii Yeremia, neno laBwanalikamjia Yeremia:

13 “Nenda ukamwambie Hanania, ‘Hili ndilo asemaloBwana: Umevunja nira ya mti, lakini badala yake utapata nira ya chuma.

14 Hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: Nitaweka nira ya chuma kwenye shingo za mataifa haya yote ili kufanya yamtumikie Nebukadneza mfalme wa Babeli, nao watamtumikia. Nitampa kutawala hata wanyama wa mwituni.’ ”

15 Kisha nabii Yeremia akamwambia nabii Hanania, “Sikiliza Hanania!Bwanahajakutuma, lakini wewe umelishawishi taifa hili kuamini uongo.

16 Kwa hiyo, hili ndilo asemaloBwana: ‘Hivi karibuni nitakuondoa kutoka juu ya uso wa dunia. Mwaka huu utakufa, kwa sababu umetangaza uasi dhidi yaBwana.’ ”

17 Katika mwezi wa saba wa mwaka ule ule, nabii Hanania akafa.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JER/28-3413058eee3e7851ec5f1108be449b17.mp3?version_id=1627—